Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Responsive Advertisement

PENZI LA MCHORA TATTOO-1





PENZI LA MCHORA TATTOO-1
LATIFA NTANGA
0719618409

"Romeo, inatosha basii nimeshindwa mimi siwezi. Niache niondoke niacheee" Alisema Lisa kwa uchungu sana huku machozi yakimtoka.
"Baby please nielewe mama'ngu nimekosa nisamehe sana mke wangu nakuomba nielewe nakupenda sana Lisa usiniache" alisema Romeo huku akipiga magoti chini na kumuomba msamaha mpenzi wake.
"Sitaki imetosha kila siku wewe wakufanya umalaya halafu unakuja kuomba msamaha kwa sababu unajua nakupenda ndio maana unanitesa kwanini Romeo kw.a.n.i..niiiii" Alisema Lisa na kuangua kilio kikubwa zaidi, alilia sana Romeo alijiona mkosaji sana alisimama na kumkumbatia Lisa na kuanza kumbembeleza.
"Sorry mkewangu.. I promise sitokuumiza tena.. Nisamehe mama yangu." Alisema Romeo huku akimbembeleza Lisa ambaye alikuwa anazidi kulia tu.
"Romeo mara ya ngapi hii..kila siku nakufumania na wanawake wengine i mean mimi sikufai? Basi niache baki na hao wanawake zako" alisema Lisa kwa hasira.
"Hapana mke wangu usiseme hivyo, ni shetani tu mama. Nakuahidi sitorudia nisamehe mke wangu mzuri tafadhari" alisema Romeo na alijua udhaifu mkubwa wa Lisa ni kuambiwa maneno matamu na kumbembeleza, Lisa alikuwa kama mtoto alipenda sana kubembelezwa na kudekezwa sana, na Romeo alijua udhaifu wake basi akaanza kumbembeleza sana.
"Nakupenda sana Lisa wangu, mwanamke wa maisha yangu nitaishije bila wewe mama? Please don't leave me alone mom, ilove you ni tamaa tu na shetani ananipitia ila for real nakupenda sana mke wangu na hakuna wa kufanana na wewe.. Baby wangu wewe mzuri sana ona macho yako mazuri matamu baby lips zako oopss mie hoi" alisema Romeo na kumsogelea Lisa mdomoni akambusu.
"Sitaki huko niache kawafuate malaya zako" alisema Lisa.
"Mmh mama usiseme hivyo bwana wewe ndio mke wangu, naanzaje kukuacha mke wangu hivi sikumbuki tumetoka wapi kweli?" Alisema Romeo na kumfanya Lisa machozi yamtoke.
"Don't cry love please" alisema Romeo na kumkumbatia kwa nguvu mpenzi wake huyo.
"Romeo naumia sana. Ndio maana nilikataa usiwe mchora Tattoo yote kwa sababu nilijua utabadirika ile sio kazi kabisa" alisema Lisa.
"Hapana mke wangu nisamehe nakuahidi sitofanya ujinga tena nielewe mama yangu" alisema Romeo na kuzidi kumbembeleza sana Lisa.
"Siwezi kukuamini kila siku maneno yako ni hayo tu kwanini mimi jamani?" Alisema Lisa na kuzidi kulia, kutoka ndani ya moyo wake Lisa alimpenda sana Romeo na kumuona ni mwanaume wa maisha yake, aliwahi kuwa na mwanaume kabla ya Romeo ila aliachana naye ndipo akakutana na Romeo ambaye alikuwa ni house boy wao. Kipindi hiko Romeo alikuwa ndio ametoka mkoani kwao, alikuwa bado mshamba hajui kuoga wala kuvaa ni Lisa ambaye alimpenda sana Romeo na kuamua kumbadilisha, pesa alizokuwa akilipwa mshahara pamoja na pesa nyingine Lisa alimpatia baada ya hapo. Romeo akaacha kazi nyumbani kwao na Lisa akaenda kupanga chumba maeneo ya mbali, Lisa akawa mara kwa mara anaenda kwa Romeo na mapenzi yao yakazidi kushamiri siku hadi siku. Walipendana sana, Romeo alikuwa anajishughulisha na biashara mbalimbali ambapo siku moja alikutana na mtoto wa mjini Cruz ambaye alikuwa ni mchora Tattoo akaongea na Romeo na kumuomba asaidiane naye kwenye kazi yake. Romeo akamueleza Lisa ambaye alimgomea kufanya hiyo kazi.
"Kwanini lakini hutaki?" Aliuliza Romeo.
"Ile sio kazi Romeo kuna wanawake washenzi watakuja wavue nguo uwachore Tattoo za makalio. Wengine hadi kwenye utupu wao wanataka Tattoo kazi gani hiyo lakini?" Aliuliza Lisa kwa hasira.
"Baby jamani tatizo wewe sio muelewa, mbona wapo watu na familia zao wanafanya kazi hiyo bila tatizo" alisema Romeo.
"Ok fine, mimi sio muelewa poa, kwaheri" alisema Lisa akafungua mlango na kutoka kwa hasira.
"Baby mke wangu njoo bwana usiondoke" ilibidi Romeo amkimbilie Lisa ambapo alimkuta tayari kaingia kwenye gari lake na kuondoka kwa hasira, kwa sababu Lisa kwao walikuwa wamezaliwa wawili yeye na mdogo wake wa kiume Ayan. Familia yao ilikuwa inajiweza sana kifedha, Lisa alilelewa kama yai wazazi wake walikuwa wakimpenda sana. Kila alichohitaji alipewa, alikuwa bado binti mdogo mwenye miaka kumi na tisa na ndio alikuwa mwaka wa kwanza chuo.
Lisa alikuwa msichana mdogo mzuri sana, rangi yake ilikuwa nzuri si mweupe wala mweusi, zaidi alijaaliwa umbo kubwa makalio makubwa sana na miguu ya bia kwa makusudi alipenda kuvaa sketi fupi au gauni fupi. Wanaume wengi walikuwa walichanganyikiwa kila walipomuona. Hatimaye bahati ikamuangukia Romeo tena house boy ambaye hakuwa na pesa wala chochote kile.
Lisa aliendesha gari kwa hasira sana huku akitukana na kuongea mwenyewe. Romeo alibakia akiwa na mawazo sana akili moja ikimtuma akubali kufanya kazi na Cruz huku nyingine ikimkataza asifanye.
"Nifanye lipi sasa?" Alijiuliza Romeo. Ghafla simu yake ikaingia meseji.
"Penzi la mchora Tattoo siliwezi, ukiamua kufanya hiyo kazi ndio mwisho wa mapenzi yetu"

Itaendelea.
Lipia 250 usome kipande kinachofuata, 0719618409 lisa ntanga. 

See less

Post a Comment

0 Comments