PENZI LA MCHORA TATTOO
MTUNZI-LATIFA
Sehemu ya Nne
Lisa alikuwa ameuchapa usingizi wa maana juu ya kitanda tano kwa sita! Kilikuwa chumba kikubwa kiasi kwani ndani kulikuwa na kitanda futi tano, pembeni kulikuwa na sofa la watu wawili, pamoja na meza ndogo ya kioo. TV kubwa ya flat, pamoja na friji dogo la kishkaji. Chumba kilikuwa na kilakitu ndani ukiingia hupati shida kutambua kuna uwepo wa mwanamke yani wanaoishi humo ndani ni mume na mke.
Lisa alikuwa ni mke kwa Romeo yeye ndio alimshauri vitu vingi mwanaume wake, na ata hiko chumba kodi ya mwanzo aliyelipa ni Lisa pamoja na vitu vya ndani walisaidiana kununua pamoja. Hakika walipendana sana.
Romeo alikuwa bafuni ambapo choo kilikuwa cha ndani, hiyo nyumba ilikuwa na wapangaji watano na kila mmoja na maisha yake haikuwa nyumba ya kushinda watu nyumbani kukaa kuchunguzana. Umbea hakuna kabisa, kila mtu anaondoka asubuhi kurudi usiku mara chache sana siku za wikiendi ndio walikuwa nakionekana wapangaji wengine wakifua. Romeo alioga baada ya hapo alitoka nakurudi chumbani akajifuta maji mwilini, akavaa nguo nakutoka zake hadi nje. Alienda buchani akanunua nyama, baada ya hapo akaongoza hadi gengeni nakununua nyanya, vitunguu na viungo vingine. Baada ya hapo akanunua unga nakurudi zake hadi ndani akabandika nyama kwenye jiko la gesi.
Romeo alilelewa kwenye maisha ya chini sana, mamayake alimfundisha kazi zote ndani pamoja na kupika, hakuna chakula ambacho hajui kupika, tena alikuwa msafi sana chumbani kwake kuzuri kwenye hali yakuvutia sio kama wanaume wengine ukiingia ndani kama dampo vile hakufai. Basi mbona iliiva akaunga losti la nguvu pilipili kibao, akasonga na ugali laini sio ule wa geto ugali mgumu. Baada ya hapo akatenga mezani nakumuamsha Lisa.
"Baby wake up" alimuamsha Lisa ambaye alikuwa anakoroma kwa usingizi mkali uliomjaa.
"Mkewangu amka tule bwana" alisema Romeo na Lisa akafumbua macho kwa uchovu.
"Baby..nimechoka!" Alisema kwa sauti ya chini Lisa.
"Pole mkewangu twende akajimwagie maji utoe uchovu" Romeo alisema nakumsaidia Lisa kuinuka akiwa mtupu bila nguo moja kwa moja hadi bafuni akamfungulia maji na Lisa akaanza kuoga. Baada ya hapo akarudi chumbani Romeo akamfuta maji, Lisa akachukua kanga yake nyepesi nakuivaa.
"Njoo ukae mapajani kwangu nikulishe" alisema Romeo nakumfanya Lisa atabasamu basi akaenda kumkalia Romeo na wakaanza kulishana kama ndege, hadi Walipomaliza.
"Yani mumewangu unajua sana kupika najivunia kuwa nawewe" alisema Lisa.
"Mpe zawadi mamamkwe wako yeye ndio kanifundisha" alisema Romeo nakumfanya Lisa acheke sana.
"Siku moja inabidi twende tukamuone jamani nikampe zawadi yake!" Alisema Lisa.
"Usijali mpenzi tutaenda tu wewe ndio mkewangu lazima mama akujue"
"Nashukuru mumewangu"
Lisa akainuka nakuosha vyombo baada ya hapo wakalaliana kwenye sofa huku wakitizama muvi nzuri ya mapenzi.
Siku hiyo Lisa alishinda hapo hadi jioni akaondoka nakurudi nyumbani kwao huku akiwa na furaha sana.
"Nakuahidi ukimaliza masomo yako nakuja kwenu kujitambulisha ili nikuoe uwe mkewangu kihalali" Lisa alikuwa akikumbuka maneno ya Romeo akajikuta anatabasamu pekeyake.
**
"Oya mwamba nambie" akiwa amejilaza kitandani Romeo akapigiwa simu na Cruz.
"Fresh babu"
"Oya pande zipi?"
"Nipo gheto huku"
"Vipi chakudeka hayupo nini?"
"Ha-ha unautani na mkewangu wewe, amesharudi kwao"
"Dah mtoto anakupenda sana huyo usimzingue bwana yani fanya makeke yako ila huyo ndio mke mwanangu"
"Najua sana yani ndio roho yangu huyu"
"Hamna shida ila fanya mpango tukutane maisha club leo"
"Dah hakuna shida mida gani sasa?"
"Kwenye saa nne hivi"
"Poa hakuna shida" Waliongea nakuagana. Romeo aliendelea kuangalia muvi huku akinywa juisi taratibu.
"Baby..nimefika home mwenzio" meseji iliingia kwenye simu ya Romeo kutoka kwa Lisa ambaye alimsave baby wife.
"Ok mom, nafurahi kusikia umefika salama"
"Aya love badae, I love you"
"Thanx baby"
Ghafla simu ikaita tena kuchek jina likasomeka.
Muuza sindano kwanza alicheka sana Romeo halafu akapokea simu.
"Baby mambo" ilisikika sauti upande wa pili.
"Safi nambie"
"Nimekumisi sana uko wapi tuonane?"
"Nipo tu home"
"Romeo jamani nimekumisi mwenzio nikikufikiria tu najichafua"
"Mmh jamani kweli?"
"Kweli mpenzi wangu, naomba leo nikuone jamani unitoe zimejaa mwenzio"
"OK usijali ila hatulali sawa?"
"Sawa hamna shida"
"Poa chukua chumba basi mimi sipo vizuri"
"Hilo si tatizo mpenzi"
"Poa utanishtua"
"Aya mume" alisema nakukata simu.
"Hahhaa wanawake bana eti nishakuwa mume wake" alicheka Romeo nakukumbuka jinsi alivyokutana na huyo msichana ilikuwa hivi..
Inaaendelea. baadaye
OFA.. OFA KWA SHILINGI 250/- UTAWEZA KUSOMA KIPANDE CHA HADITHI WHATSAPP NA FB inbox.
Namba ya malipo.
0763361677 jina Lisa Ntanga.
0 Comments