Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Responsive Advertisement

CHOMBEZO: * *DADA BINAMU**




 SIMULIZI YA KUSISIMUA..


* *DADA BINAMU**

Mtunzi: mejah plan maker.
Mtindo: mtindo wa moja kwa moja/mtindo rejea..
Mahali: dar-es-salaam.
WhatsApp: 0712563243.

TAHADHALI.
ISOSIMWE NA WENYE UMRI CHINI YA MIAKA🔞

ILIVYOJIRI..
"Asante mtoto bado ananyonya ni mdogo sana hivyo nashukuru" alijibu yule Dada na kuondoka huku nyuma alimuachia sule maswali mengii mno "huyu Dada mbona simuelewi au ananipenda nini? Lakini amezaa na nani au ananidanganya??"

Aliwaza mpaka akapitiwa na usingizi alikuja kushtuka amechelewa "Leo mhindi atanitukana mmh, hapa hata kuoga siogi" alibeba beg lake na kuondoka kuelekea kunako kazi.

EPISODE O6...
Sule alifanya kazi ya juhudi sana, huku akiweka imani kuwa iko siku nae atakuwa na sehemu yake, changamoto ni sehemu ya maisha na ukiweka juhudi lazima utafanikiwa maana penye nia pana njia na ndivyo alivyoamini sule. Ilipotimu saa kumi sule na vijana wengine walijiandaa kwaajiri ya kuelekea majumban mwao kitu pekee ambacho kiliumiza kichwa cha sule ni juu ya yule mwanamke aliyekuja nyumbani jana usiku "inawezekana ananipenda lakini je?? Mpenzi wangu jesmina akirejea itakuwaje??" Alijiuliza maswali mengi sana..

Kiza kilitanda angani kuashilia usiku ulishaingia kila mtu alikuwa nyumbani kwake na wengine ndio walikuwa wanarudi makazini ikiwemo sule pia. Alishtushwa alipoingia ndani alisikia harufu nzuri ya manukato "oooh huyu mwanamke amenipenda nini(alijiuliza)" huku anafunua hotpots mezani ikatoka harufu nzuri saaana naam kilikuwa chakula kizuri pia, ndizi zilizochanganywa na nyama na viungo mbalimbali ikiwepo nazi pia "ewaaaaa mwanamke huyu amejidhatiti kuchukua huu mjengo" alijiwazia sule huku akichukua kijiko na kuchota chakula kuweka kwenye sahani.
Baada ya kula aliweka cd ya kikorea na kuangalia movie iliyokwenda kwa jina la destiny to love you, iliyokuwa na kisa kizuri cha mapenzi na matukio ya kuhuzunisha, sule macho aliyakodoa kwenye runinga hakutka kupoteza hata pointi moja.
Ghafla alisikia anaitwa kwa dirishani "sule! Sule! Sule(sauti ya kike) sule ilibidi asimamishe cd ili apate kusikia vizuri " mmh nani wewe usiku huu" aliuliza kwa woga kidogo "mimi zawadi nifungulie" ilijibu ile sauti nje, sule bado akulizika "kwema lakini uko??
" wee nifungulie tutaongea" hapo mwisho ile sauti ilionekana yenye kulia hivyo sule akutaka kuuliza tena alifungua mlango na kusubiri kidogo ili kumuona huyo mwanamke alikuwa ni nani. Mara akatokea zawadi akiwa na mtoto mkononi. Sule alishangaa kumuona ni yule binti mwenye mazoea ya kuja kwake hivi karibuni. Aliketi kwenye miguu ya sule na kuendelea kulia.. "Kuna nini tena jamani mbona sikuelewi" aliuliza sule bila kupata majibu yeyote..

Usiku walipolala bado sule aliendelea kuuliza swali lilelile "zawadi kimekufika nini" ndipo zawadi akaamua kumweleza kilichotokea.

FLASHBACK(TUNARUDI NYUMA)..

Zawadi alitazama chini akimwangalia dada yake miriamu ambaye nae alikuwa ni mwenye majonzi. Ndugu walikuwa wamejipanga kudhurumu mali zote kwa sababu moja alisikika baba yao mkubwa "hatuwez kuwaachia mali watoto wa kike, hawa wataenda kuolewa mali watazikuta kwa waume zao" alipata ushirikiano kutoka kwa ndugu wengine ambao walishikilia kidete mali ziuzwe kila mtu afe na chake. Alisimama miriamu(dada yake zawadi) "kusema ukweli hatuwez kukubaliana na maamuzi ya kikao hiki angalau mngesema mnatugawia asilimia sitini ya mali za wazazi wetu ila kutopewa kabisa hawezekani tutaenda hata mahakamani" aliongea kwa kujiamini miriamu

"Unaona unaona sasa nilikuwa namaanisha kipindi chote kile masalu aliwalea hawa watoto kizungu hata mila na desturi awazijui kweli mtoto wa kike anaweza kunipandishia hivi?? Hata mke wangu awezi kufanya hivi" kulitokea vurugu pale na kikao kikavurugika..
********

Maisha yalienda vizuri baada ya mahakama kuhidhinisha kuwa mali zitaenda kwa watoto wa marehemi yani miriamu na zawadi. Walitoka wakiwa wenye furaha na kila mtu aliamini anaweza kutimiza malengo yake.
Baada ya muda kwenda sana miriamu alianza kubadilika akawa na marafiki walevi wanaopenda starehe alianza kuuza vitu kidogokidogo bila kumshirikisha ndugu yake. Zawadi akuwa na namna kwakuwa alimuheshimu dada yake aliendelea kuvumilia akijisomea bahati mbaya dada yake (miriamu) akaanza kuleta wanaume pale ndani mara huyu na kesho huyu siku zikasogea. Siku moja dada yake akiwa ayupo yupo yeye na shemeji yake yani mtu wa dada yake alishangaa anamvamia bafuni akamvuta kwa nguvu na kuanza kumbaka.

Hakuwahi kushiriki mapenzi na mwanaume katika maisha yake ivyo alijisikia vibaya na maumivu makali sanaa, sehemu za siri na chini ya kitovu/tumboni. Dada yake akutaka kumuamin zawadi wakaanza kumnyanyasa wakati mwingine walimnyima hata chakula hivyo maisha yake yalikuwa ni ya hivyo hivyo na kipindi hicho alikuwa mjamzito..
********

Hatimaye zawadi alijifungua mtoto wa kike ambaye hakutaka kumpa yule mwanaume maana ingekuwa ni aibu kuzaa na shemeji yake hivyo alisingizia baba wa mtoto yupo nje ya nchi kimasomo.
Aliamua kujenga urafiki na majirani na kwakuwa alikuwa na fani ya ususi alikuwa akisuka vichwa winne vitano anapata pesa ya kujikimu kimaisha.
"Dada naomba nisaidie mtaji nifanye biashara" aliomba zawadi baada kuona atakufa asipokuwaa makini
"Mtaji muombe huyo aliyekuzalisha huyo mtoto tusisumbuane" alijibu miriamu kwa dharau

"Kwanza dada kumbuka mali hizi ni za kwetu wote naomba basi tugawane kila mtu aendelee na maisha yake" aliposema hivyo ndipo ulipotokea ugomvi dada yake na bwana yake walimshangia na kumpiga sana kisha kumfukuza na mtoto wake usiku usiku.

TUENDELEE NA SULE..
"Aiseeee kumbe ndivyo alivyokufanyia" alihamaki sule

"Hapa sijui nitaishike na huyu mtoto" aliongea zawadi huku anabubujikwa na machozi

"Hapana mimi nipo utaishi tu ila inabidi uende mahakamani uombe mahakama igawe ile mirathi" aliongea sule huku anamkumbatia zawadi hapo ndipo ulikuwa mwanzo wa mapenzi baina ya hawa watu wawili na yule mtoto sule akamuita angela.

TUREJEE LEO..
Baada ya simulizi yote ile. Angela alishangaa sana na kujikuta ana maswali mengi ya kumuuliza baba yake, ila kabla hajafanya hivyo alisikia anaitwa na mama yake, akanyanyuka kuelekea ndani "angela, kesho nitakupigia simu saa sita tuonane" aliongea mzee sule wakati angela anaingia ndani..

Angela alikuwa ni mwenye maswali sana usiku huo alitamani kumuuliza mama yake lakini nafsi ikakataa akawaza juu ya masara na ule mpango wa kumuoa akapata nguvu "kumbe hata hivyo mimi na masara hatuna undugu wowote sasa ole wao wapinge masara asinioe" alijisemea angela huku anakumbatia mto wake.
Kulipokucha angela aliendelea na shughuli zake za siku. Upande wa pili masara aliwaza sana kauli ya mama yake kuwa hatukuwa na radhi kama mtoto wake atamuoa binamu yake hilo likamuuzima kichwa mno masara ukizingatia alishakulea mno kwa binamu yake angela.

Baba angela alimtazama mwanae kisha akameza fundo la mate akatabasamu "yani mama yake mtupu enzi za usichana wake" alijisemea mzee huyu mwenye tamaa ya damu changa.
Waliagiza vinywaji na kuendelea kupiga soga mbili tatu kabla angela ajauliza swali "baba unataka kusema mimi sio mtoto wako wa kumzaa"
Mzee alijibu kwa kukurupa bila kufikiria "exactly/sahihi" na alifanya hivyo ili kupalilia swala lake la penzi juu ya angela.
"Unasema kweli???" Alidadisi angela

"Mimi sijawahi kuwa na mtoto kwenye maisha yangu ilikuwa hivi"

TURUDI NYUMA (FLASH BACK)
Niliendelea na shughuli zangu kama kawaida kule kwa mhindi. Mhindi alianza kuniamini na kunipeleka chuo cha udereva na baadae nikapata leseni nikatoka kubeba mizigo nikawa dereva wa kupeleka watoto shule na familia kwa ujumla kwenye mitoko ya kila siku. Japo kwa wakati huo pesa ilikuwa kiduchu sana lakini kuliko kutokuwa na kitu ni heri nipate hiko kiduchu maana kilinifaa kwa familia yangu. Tulisonga na maisha na upendo wa familia yetu ukazidi maradufu. Mtoto(angela) alikuwa na kuanza shule ambapo alisifiwa sana kwa kuwa na kichwa chepesi kwani alijua kusoma akiwa bado chekechea.

Mke wangu aliweza kushinda kesi ya mirathi na mahakama ikagawa mirathi ambapo kulikuwa na nyumba mabibo na kimara mbezi. Hapo rasmi tukaamia kimara na maisha yakaendelea.
Siku moja nikiwa nipo barabarani kwa bahati mbaya nilipata ajali ya pikipiki na kuumia sehemu za kiuno. Daktari aliniambia kuwa sitakuwa na uwezo wa kuzaa tena nililia sanaa sana. Ila mke wangu akanifariji na kuniambia "mtoto huyu hapa angela ni mtoto wako, Mungu amekupa zawadi upaswi kujilaumu kwa yaliyotokea ni mitihani" toka siku hiyo nilimpenda sana huyo mtoto (angela) na nilifanya kila kitu ili apate kusoma.

Juma rafik yangu wa muda mrefu alinipa wazo ambalo lilinifumbua macho "twaweza kutoka katika umaskini rafiki yangu""

JE NI WAZO GANI HILO USIKOSE SEHEMU IJAYO.


Post a Comment

0 Comments