LATIFA NTANGA
0719618409
Penzi jipya likachanua kati ya Romeo na Editha ambaye alikufa nakuoza kwa Romeo. Hatimaye waandishi wa habari wakazipata tetesi za Editha kutoka na Romeo. Ilikuwa bonge la habari kwao wakaingia kazini na kufuatilia kwa kina ili watakapoandika kwenye magazeti yao basi habari iwe ya uhakika.
Hatimaye Romeo na Editha wakafumwa kwenye onyesho la Malaika band chini ya kiongozi wake Christian Bella. Siku hiyo wapenzi hao walikuwa pamoja kama ndege, mapaparazi wakawafuma na kuwaphotoa picha za kutosha kwenye mahaba tofauti.
"Editha habari yako?" Paparazi mmoja alimfuta Editha baada ya kupata picha za kutosha.
"Safi, Derick vipi?" Alisema Editha.
"Nakuona mrembo, huyo ndio shemeji nini?" Aliuliza huyo mwandishi wa magazeti ya udaku.
"Yeah huyu ndio mume wangu mtarajiwa nampenda sana anaitwa Romeo" Alisema Editha.
"Ok kwahiyo tusubiri harusi hivi karibuni?" Aliuliza huyo mwandishi.
"Ndio kwanini isiwe ni hivi soon nitawapa kadi za mualiko msijali" Alisema Editha na akamkumbatia Romeo na kumbusu. Baada ya kujitosheleza na maswali mwandishi wa udaku aliondoka zake akiwa na habari motomoto. Siku hiyo Romeo na Editha, walikula bata sana hadi usiku sana wakaondoka na moja kwa moja wakaenda nyumbani kwa Editha kulala. Walikuwa wakiishi kama mume na mke japo kuwa Romeo alikuwa na kwake.
***
"MREMBO WA BONGO MUVI EDITHA AZAMA KWENYE PENZI ZITO LA MCHORA TATTOO" Asubuhi siku iliyofuata magazeti ya udaku yalipambwa na picha za Editha pamoja na Romeo wakiwa kwenye mahaba mazito sana. Kila aliyeona alishangaa kwa sababu hapo mwanzo hawakuwahi kuona mahusiano ya Editha ambaye alikuwa msiri sana lakini sasa mambo yote hadharani. Editha alipagawa na penzi la Romeo alikuwa haoni wala asikii juu yake.
Mara kwa mara Editha alipokuwa akienda kwenye sherehe au hata mikutano na wasanii wenzake alikuwa akienda na Romeo na hilo likawa kosa kubwa sana kwani kupitia sherehe hizo Romeo alipata mawasiliano ya msanii na mwanamziki wa bongo fleva, Livia ambaye alikuwa akivuma sana kwa kipindi hiko. Livia alikuwa msichana wa kichaga, alikuwa mfupi kiasi mweupe mwenye uzuri wa asili alikuwa mrembo haswa! Nyimbo zake nyingi zilikuwa za mapenzi alikuwa na sauti tamu ya kumtoa nyoka pangoni huku umbo lake likimtuliza nyoka na kumfanya apagawe haswa! Livia alijua kutumia kiuno chake alikuwa na kiuno laini bila mfupa hiko, alikuwa anakizungusha haswa na kufanya wanaume wachanganyikiwe kila alipopanda stejini alifanya shangwe ziwe kubwa kwaajili yake, alipenda sana kuvaa nguo za ajabu na kufanya wanaume wengi watokwe na udenda wakimuona.
"Siamini kama nimepata namba yako!" Ilisikika sauti ya Romeo kwenye simu alipompigia Livia.
"Why Shem? Unajua namuheshimu sana Editha ni rafiki yangu mkubwa yule yani siwezi kukunyima mawasiliano yangu shemeji" Alisema Livia. Nakumfanya Romeo atabasamu huku moyoni akisema
"Umekwisha wewe! Hakunaga ushemeji tunakulaga!!"
Itaendelea.
0 Comments