Alinishawishi Diana basi nikakubali tukaondoka nakupanda gari la msasani, tulishuka macho tukachukua bodaboda adi coco.
Ilikuwa bado mapema shule tulitoka saa sita hakukuwa na foreni saa saba na nusu tukawa coco tayari.
Basi wezangu walikuwa na pesa tukakodisha nguo zakuogelea apo kila mmoja akachagua yake tukavaa nakuvua nguo za shule tukaogelea adi tulipochoka tukaanza kukimbizana kwenye michanga tulifurahi siku iyo adi saa kumi jioni tukaanza kujiandaa kuondoka. Mara nikasikia naitwa na mwanaume nikageuka nimsikilize ni mbaba mkubwa
"Ujambo Mrembo?"
"Sijambo shikamoo"
"Asante"
Alijibu uku anatabasamu alinichefua sana nikataka nianze kumchamba maana sicheleweshangi gafla wakaja mashoga zangu nakumsalimia kwa furaha yule mbaba.
Kumbe wenzangu walikuwa na mabwana tayari mie ndo nilikuwa mgeni sina mpenzi na mwanaume akinitokea nampa matusi adi anakoma
"Sisi tunaelekea ubungo tupeleke basi"
Salma akamwambia yule baba akakubali basi tukajiandaa nakuvaa nguo zetu za shule tukapanda gari lake nakuanza kutupeleka
"Nimempenda sana Lisa natamani awe mpenzi wangu"
Alisema uyo mwanaume ambae alitwambia anaitwa Mr Antony
"Lisa muoga uyu ila usijali utampata tu"
Diana alidakia kusema nikataka kuongea akaniwahi kuniziba mdomo maana ananijua nipoje.
Basi alipitia njia ya shekilango akakatiza makaburi ya ufi nakutokea shungashunga ndo maeneo ya kwetu walianza kunipeleka mimi kwanza lakini hatukifika nyumbani ila tulipo nyumba yetu inaonekana basi nikaagana nao nakutelemka ile nashuka tu kwenye gari naona gari la baba limesimama pembeni ameteremka nakuja nilipo ata kabla lile gari alijaondoka akanifikia
Baba alipofika akaninasa kofi moja bila kuongea akasogea adi kwenye gari nakugonga kioo
"Fungua mlango toka nje"
Alimwambia yule mwanaume aliekuwa ndani ya gari, ambae alifungua kioo kumsikiliza baba aliekuwa amevaa magwanda yake yakiwanajeshi nilijua muda huo ndo alikuwa anatoka uko kambini kwake Lugalo.
"Habari yako muheshimiwa?"
Alianza kusalimia Mr Antony,
"Salama, samahani nimeona binti yangu akishuka kwenye gari lako unaweza kunambia umemtoa wapi leo ijumaa shuleni wanatoka saa sita mchana na sasa ivi ni saa kumi na moja niambie umetoka nae wapi"
Aliongea baba akiwa siriazi zaidi alikuwa anakunja mikono ya nguo yake yakijeshi nakuifanya iwe fupi mikononi akionyesha hana masihara anaweza kumpiga uyo mwanaume anaeongea nae nilipomuangalia alionyesha anauoga kwa mbali ila alijitahidi kujikaza.
"Oh kumbe ni binti yako mimi nilimkuta coco beach akiwa na rafiki zake wawili wapo humu kwenye gari ngoja niwaite"
Akawaita wale mashoga zangu ambao waliteremka watoka nje nakumuona baba alivyo uoga uliwajaa walitetemeka ovyo.
"Ndo hawa marafiki zake niliwaona coco nikawachukulia kama watoto wangu nikaamua kuwasaidia niwapeleke majumbani kwao ndio nimeanza na uyo ulosema binti yako bado ninasafari yakuwapeleka hawa weninge majumbani kwao"
Alijitetea Mr Antony nakumfanya baba awageukie wale wenzangu Diana na Salma
"Aliyosema uyu baba ni kweli au?"
Aliwauliza akiwakazia macho wote wakatingisha kichwa kukubali,
"Mlipoenda uko coco mlitoa ruhusa majumbani kwenu na wewe Lisa unaanzaje kwenda bila kuaga nyumbani mlifata wanaume uko eeh?"
Baba aliwauliza akawashushia makofi wezangu wote waliobaki wanalia kisha akamwambia yule mwanaume awapeleke kwao kesi ikabaki kwangu sasa alinibutua adi tunafika nyumbani
"Ole wako siku nyingine utoke bila kuaga shenzi wewe"
Yani nilikuwa napigwa sana ila sikomi nikaingia chumbani nikalia nakumlaani baba bora afe kabisa.
Mama aliporudi akaambiwa ata hakuniuliza yeye alishachoka kuongea.
Basi siku zikazidi kusonga adi nikaingia kidato cha tatu bado niliendelea kuwa mtukutu baba ananipiga tu adi nikamaliza kidato cha nne nilishukuru mungu apo nikajiona nishamaliza masomo tena nilizidi kutanuka nakuwa mkubwa nilifikisha miaka kumi na nane basi nilijiona mtu mzima kabisa, sifai kupigwa sikutaka ata kungojea majibu nikaomba nipelekwe kwa bibiyangu Songea nikakae nimkimbie baba maana shule nimemaliza ningekuwa nazurura kilasiku ningedundwa na baba muhimu kuondoka kwake.
Siku moja usiku tunakula nikaanza maongezi.
"Nimemkumbuka bibi yangu mimi nataka nikamuone tena nikake uko adi majibu yakitoka"
Niliongea kiunyonge mwenyewe
"Ila bora ukakae kijijini labda utajua kazi umelegea kama mlenda vile"
Mama alisema baba akaniangalia Alisema
"Najua unanikimbia sawa nenda kule kuna babayako mdogo nitamwambia akulinde ukitoka tu akupige"
Nilichukia maisha gani yakupigwa kilasiku nikajikuta namchukia babayangu kuliko shetani nilimuangalia nikatamani nimuwekee sumu afe.
"Sawa anipige tu nishazoea si mnanifanya mie ngoma"
Nilimjibu baba
"Katulie mwanangu hatokupiga babayako mdogo usijali"
Mama alisema sikumjibu nayeye nikainuka nakuelekea chumbani kwangu.
"Jiandae kesho safari Asubuh na mapema"
Baba alisema nikaondoka zangu nimenuna.
Basi nilifika nikapanga nguo zangu vizuri nakuweka nikaingia kulala.
*****
Asubuh kulikucha nikajiandaa nakutoka baba nikawaaga wote baba ndie alinipeleka adi stand ya mkoa ubungo akaniacha nimepanga gari nayeye kuondoka.
Basi saa mbili Asubuh safari ikaanza nilikuwa na simu apo tayari mama alininunulia, nikaanza kuchat na mashoga zangu nikiwaaga naenda kijijini
"Loh shosti umeishiwa na urembo wote ukaishi kijijini aibu"
Alinambia Nasra
"Mwezangu babayangu kazidi kunipiga nimeona niondoke tu"
Nikachat adi saa nane sijui tumefika wapi pale nilichoka nakulala zangu kwenye kiti.
Nikaja kushtuka imefika saa kumi na mbili giza limeanza kuingia.
Ghafla tukatokea porini barabara haionekani kila mtu akashangaa
"Tumefikaje uku wewe dereva vipi?"
Watu wote walishangaa tukamsogelea dereva tumuulize tukamkuta amelala uku damu zinamtoka na kondakta ajulikani wapi alipo apo wote tulijawa uoga kila mtu akatoka kwenye gari nakukimbia ovyo mie begi lilikuwa zito nilitupa uko nakutoka mbio nisijue wapi naelekea, kila mmoja alikimbia njia yake gari likabaki na dereva aliekufa tu.
Usiku ulishaingia, nilikimbia nikiwa pekeyangu nikatokea porini zaidi kunatisha uku milio ya wadudu inasikika
"Mama wee nakufa mimi uuuhh"
Nikaanza kulia giza limetanda sioni mbele wala nyuma natetemeka kwa uoga nikasogea kwenye mti mkubwa nakukaa chini nimejikunyata apo hofu imenijaa sina tumaini lolote
"Mungu ipokee roho yangu"
Apo ndo nilikumbuka kuna mungu kumbe wakati mama alipokuwa ananiambia niende kanisani nilikuwa nagoma leo yamenikuta sasa nilijuta bora ningebaki tu nyumbani safari yakijijini imekuwa ndo mwisho wangu.
"Nakufa mimi leo"
Nilizidi kutetemeka mara kwa mbali nikaona miale ya moto watu wanaimba nakuja kule nilipo nikatamani nikimbie ila nguvu nilikuwa sina hatimae wakanisogelea wakinishangaa sana walikuwa wanatisha niliisi wachawi walivaa kaniki chini juu vifua wazi ni wanaume watatu
Walizidi kunishangaa uku wakinimulika na ile miale ya moto usoni, hatimae mmoja akaongea nakuniuliza
"Unaitwa nani?"
"Naitwa Lisa"
"Umetoka wapi umefata nini uku kwenye ufalme wa Odinya?"
Aliuliza lakini sikumuelewa
"Mimi nimetoka Dar es salaam nilikuwa naelekea Songea kwa bibi yangu kuna sehemu tulifika ni porini akuna aliejua tupo wapi tukamsogelea dereva tumuulize tumemkuta amekufa wote kwenye gari tukatoka nakukimbia ndio mimi nimefika apa"
Nilijielezea nakuangua kilio kikubwa wale wanaume wakaangaliana nakusema wanisaidie
"Tumpeleke kwa Mfalme uyu"
Wakasema nilishtuka nikajua napelekwa kuzimu sasa.
"Kwani nyie ni wachawi au?"
Nikawauliza nakuwafanya wacheke alafu mmoja akanijibu
"Sisi ni watu kawaida ila tunaishi kiutamaduni yani kiasili pia tunamilikiwa na mfalme usiogope sisi watu wema twende tukusaidie"
Basi waliposema ivyo kidogo uoga ukanipungua nikainuka nakuongozana nao, walikuwa wanaimba nyimbo zao zakushangilia sijui ata sikuwaelewa.
Tulipita maporini humo uku ile miale ya moto ikitusaidia kuona mbele hatimae nikaanza kuona kwa mbali nyumba baadhi uku moto umewashwa kwa nje. Tulizidi kusonga adi tulipofika kwenye iko kijiji chao moja kwa moja nikapelekwa kwenye nyumba kubwa nje wamesimama walinzi walioshika mikuki mikononi mwao tukawasogelea.
Basi wakasalimiana nakuomba waingie ndani kuonana na mfalme ambapo walikubaliwa tukaingia wote.
Alitwa kijakazi mmoja akatumwa amwambie Mfalme kuna wageni wake nje ambapo baada ya muda mfupi alitoka nikamuona mwanaume wa makamo tu si mtu mzima sana alikuwa amevaa nguo za kijadi kama mganga vile
"Uishi miaka mingi ewe mfalme wetu"
Walisema uku wameinamisha vichwa vyao chini namimi nikawageza nikainama.
"Karibuni"
Alisema uyo mwanaume ambae ni Mfalme kisha akasogea kwenye kiti cha ngozi nakukaa.
"Ewe Mfalme wetu mtukufu uyu binti tumemkuta porini usiku huu amesema kapotezana na wenzake tumeona kuliko kumuacha msituni auliwe na wanyama tukaamua kumleta mbele zako ili umsaidie"
Aliongea mwanaume mmoja kati ya wale walionikuta porini kule.
"Kwasasa ningependa apumzike adi kesho ndio niamue nini kifanyike juu yake! Somoiyeee njo haraka"
Aliisema Mfalme nakumuita kijakazi mmoja jina lake Somoiye ambae alikuja nakuinamisha kichwa kwa adabu zote.
"Naam mtukufu Mfalme"
Alisema akiwa ameinama bado.
"Mchukue uyu msichana kampeleke chumba cha wageni mpe chakula ashibe na maji aoge kisha mbadirishe nguo izo"
Alisema Mfalme
"Sawa mtukufu Mfalme"
Aliitia uyo binti Somoiye akanishika mkono tukaondoka apo nakunipeleka kwenye nyumba moja iliyokuwa ya udongo imezungushwa na nyasi.
Tukaingia ndani ambapo kulikuwa na mkeka chini uku pembeni kuna kitanda cha kamba na shuka juu.
"Unaitwa nani?"
Aliniuliza
"Naitwa Lisa"
"Ooh Lisa liene"
"Sio ivyo ni Lisa tu"
"Yani nimeongeza maana yake umekuja mwenyewe"
Alisema ila sikumuelewa
"Ngoja nikakuletee chakula kwanza"
Alisema akainuka nakutoka umo ndani kulikuwa na kibatari kinawaka ndo mara ya kwanza naingia nyumba ya nyasi kwani ata kwa bibiyangu sio kijinini ni songea mjini nyumba yake ya tofari na kuna kilakitu ndani adi maji yapo, sasa uku nilipokuja leo ndo mara ya kwanza kilakitu kigeni kwangu.
Baada ya muda mfupi Somoiye akaja na sinia limefunikwa juu
"Karibu Lisa liene"
Alisema nikamshukuru nilifunua nakukuta ugali na nyama yakuchoma nilikuwa na njaa nikaufakamia wote adi nilipotosheka alinipa maji ya kunywa matamu ayo kama ya mvua
"Kuishi uku adi raha jaman"
Nilijisemea kimoyomoyo.
"Asante Somoiye"
"Usijal mrembo wangu"
Alikuwa mcheshi uyo mdada ambae kiumri yeye mkubwa kwangu basi akatoka na vyombo aliporudi alishika vitenge viwili na tait fupi moja akanipatia
"Njo nikuonyeshe bafu uoge kisha ukapumzike"
Alinambia nikatoka nakuingia kuoga adi nilipomaliza akanisaidia jinsi yakujifunga izo nguo
Kitenge kikubwa nilijifunga chini kiunoni na kingine kidogo kama kitop nikajifunga juu nikafanana na mavazi aliyovaa yeye sasa.
Baada ya apo nikarudi kulala ndani.
"Usiku mwema kesho asubuhi nitakuja kukuona sawa eeh"
Alinambia akaondoka nakuniacha nimejawa na mawazo siamini maisha yangu yamekuwaje.
Kulala kwenye kitanda cha kamba niliogopa nikalala kwenye mkeka chini, usingizi haukuja mapema nilikuwa na mawazo sana ata sijui muda gani nilipitiwa nikaja kushtuka asubuhi kumekucha
"Lisa liene amka"
Ni Somoiye ndie alikuja kuniamsha nikashtuka nakutoka nae nje ambapo alinipeleka kwa Mfalme aliniitaji.
Sasa niliweza kuona iki kijiji kilivyo madhari yake ilivutia kulikaa kiasili sana nakupendeza.
Nyumba nyingi za udongo na kuezekwa kwa nyasi zilienea maeneo mengi uku kukiwa na miti ya matunda mbalimbali na mboga za majani walizopanda nilizidi kushangaa sababu sikuwahi kufika vijijini nakujionea zaidi hii ni milki ya kifalme ambayo wanaishi kiutamaduni nilipenda sana kulivyo nikawa naangaza macho sehemu nyingi nakuangalia.
Basi nikafikishwa kwa Mfalme nakumsalimia ambapo nilimkuta na mkewake Malkia Tamara alikuwa mwanamke mzuri sana mwenye haiba ya upole.
"Unaitwa nani binti?"
Aliuliza uyo Malkia
"Naitwa Lisa"
"Ooh basi tutakuita Lisa liene maana yake umekuja mwenyewe"
Alisema akitabasamu nikamkubalia sawa.
Baada ya apo wakaanza kunihoji nimefikaje kijijini kwao, nikawaelezea ilivyokuwa wakanipa pole nakuahidi watanisaidia jinsi yakuondoka kurudi nyumbani
"Ila nimepapenda sana uku kwenu kuzuri naomba nikae ata mwezi mmoja"
Nikawaomba ili niendelee kujifunza mengi basi walikubali nakusema nitaishi nao apo kwao nilifurahi sana.
"Inabidi lipigwe baragumu nakuwaitwa wanakijiji watambue uwepo wa mgeni apa kijijini"
Alisema Mfalme na mkewe akakubali.
"Mashable kapige ngoma wanakijiji wakusanyike"
Aliamliwa kijana mmoja ambae aliondoka mbio nakwenda kupiga ngoma.
Mara vijakazi wakaja na kifungua kinywa wakaweka kwenye meza moja iliyokuwa humo ndani tulipokaa ambapo Malkia akanikaribisha chai, Mara ghafla akaja kijana wa kiume umri wake kama miaka ishirini na tano ivi alikuwa amevaa mavazi yakifalme pia
"Muishi miaka mingi Mfalme na Malkia"
Alisalimia baada ya apo akakaa nakujumuika nasi
"Lisa uyu ni kijana wangu nina watoto wawili wakike ambae ametoka yupo kwa shangazi yake na wakiume ndo huyu "
Alisema Malkia
"Muthan uyu anaitwa Lisa ni mgeni wetu apa kijijini"
Alimuelezea mtoto wake ambae alimuelewa utamburisho ukaisha apo tukaanza kula pamoja, nilipata bahati sana yakukaa na kula na Mfalme na familia yake.
Uko nje wanakijiji walikusanyika wengi uwanjani ambapo ni mbele ya nyumba ya Mfalme basi tulipomaliza kula tukatoka wote pamoja nakuelekea uko kwenye uwanja ambapo kulikuwa na mikeka imetandikwa mingi watu wamekaa apo kwa mbele kulikuwa na viti anavyokaa Mfalme na familia yake.
Ilikuwa sehemu maalumu kwa mikutano hakikuwa na jua walijenga kama ukumbi ivi ambapo likitokea tatizo wote wanakusanyika apo.
Watu walikuwa wengi zaidi wamevaa nguo za kitamaduni walipendeza machoni mwangu.
Wakubwa kwa watoto walijaa apo,
"Mdumu miaka mingi Mfalme na Malkia"
Walisema wote nakuinama kwa heshima.
Mfalme alisogea akaka kwenye kiti chake cha ngozi sijui ya mdudu gani yule na malia pia akakaa kwake na mtoto wao akakaa pamoja na mie uku pembeni walikuja walinzi kama sita na mikuki yao wakasimama pembeni yetu kutulinda.
Mfalme akakooa nakuanza kuongea na wananchi wake
Kabla ajaanza akatokea msichana mmoja kavaa nguo zake fupi sana anatembea kwa maringo uyo akasogea sehemu nakukaa uku akijipepea kama anasikia joto.
"Uyo binti aliefika sasa aje uku mbele"
Aliongea Mfalme akiwa amechukia
ITAENDELEA
0 Comments