Nilistaajabu maneno aliyonambia nikamgeukia mamayake mzazi Harvey
"Mama mbona sielewi jamani?"
Nilimuuliza kwa upole jibu alilonipa machozi yalinitoka bila kupenda
"Usichokielewa kipi apo? Au ulitaka kuolewa na mwanangu mwisho umuue urithi mali mwaka mzima uzai unachotegemea nini nyumba itakushinda hii nataka wajukuu mimi"
Sikuamini maneno ya uyu mama ambae alikuwa akionyesha kunipenda nikifurahi nakufarijika nimepata mkwe mzuri kumbe ni tofauti mara wifi nae akaingilia
"Machozi yako kayatoe Leba wakati unazaa sio apa unasikia? Unajitawala unaona umefika eeh kakayangu utaki kumzalia kazi kujinenepea unamkosesha ata raha ya ndoa"
Walinichangia kwa maneno wote ata sikupata wakunisaidia nilibaki nalia machozi yauchungu yakinitoka nakufanya ile furaha yangu itoweke moyo wangu uliuma sana.
"Jamani ata mimi natamani mtoto ila mungu ajanijaalia bado"
Nilijaribu kujitetea
"Ivi ujawahi kutoa mimba wewe sema kweli?"
Neema mchina akaniuliza
"Apana mama sijawahi"
Nilimjibu
"Aah koma wee usiniite mama sijazaa mie tusizeeshane"
Alisema nakunifanya nitamani ata kucheka kwa maneno yake.
"Ila kama kweli unataka mtoto twende kwa mganga upate dawa sio kusema mungu ajakujaalia utakufa bila kuzaa"
Alisema nikaogopa maneno yake.
"Wewe Lisa unataka mtoto au utaki na kama utaki kwenda kwa mganga hii nyumba utaondoka tulete mwanamke anaezaa"
Alisema mamamkwe nikaona nikubali tu kwenda kwa mganga.
Basi apo wakafurahi tena wakaondoka uku wakicheka nakuniacha mnyonge ata hamu yakula sina.
***
Usiku alirudi mumewangu nikamuelezea yote alisikitika sana lakini akaniomba nikubali kwenda sababu anatamani sana mtoto.
"Mkewangu nakuomba kubali kwenda natamani sana kuitwa baba najua sisi ni wasomi hatupaswi kuamini waganga ila tambua tunashida inabidi tuwaamini labda tutafanikiwa"
Alisema Harvey sikuwa na jinsi nikamuelewa japo moyowangu uliniuma sana nilijua atakataa lakini amweungana na ndugu zake sikuweza kujizuia kilio cha kwikwi kikanishika nakumfanya aanze kunibembeleza.
"Nyamaza mamangu usilie nakuomba"
Alinisii akiwa kanikumbatia mwisho nikapitiwa na usingizi adi kulipokucha ilikuwa ni wikiendi asubuhi tu alikuja Mamamkwe na Neema mchina ambapo hawakuwa na maongezi mengi sana
"Tumekuja kumfata uyu bibie twende uko kwa mtaalamu"
Alisema Neema
"Aah mamdogo ebu tumia ustaarabu basi apa ni kwangu na uyu ni mkewangu pia naweza kukubali au kukataa asiende ustaarabu muhimu"
Harvey alichukia sababu kufika tu bila salamu Neema akaanza kuropoka.
"Ooh umekuwa siku izi sasa unaweza kunijibu ivyo mimi mamayako? Au kisa uyu kinyago ndo anakupa jeuri ushalishwa limbwata eeh?"
Alizidi kusema na kwa mara ya kwanza nikamshuhudia Harvey amechukia niliogopa sana.
"Mama nakuomba umwambie ndugu yako naweza kumpiga ata risasi za miguu na asinipeleke kokote ujinga nyumbani kwangu sitaki uyu mke nimemuoa mimi hamjaoa nyie mnajuaje kama mimi labda nina matatizo kwanini mumlaumu yeye eti azai kwani alipenda kuwa ivi au hamjui kama ata sisi tunaumia kukosa mtoto pia jana tulikubaliana aende uko kwa mganga atibiwe lakini wewe Neema uliekosa adabu ambae ata ndoa ujui ni nini kizazi huna unakuja kumwambiaje mkewangu we umezaa au?"
Alifoka Harvey nakunifanya nitetemeke adi nikaamini msemo unaosema muogope mtu mpole akichukia anakuwa mkorofi sana leo nilijionea kwa Harvey yule ambae muda mwingi alikuwa anacheka tabasamu alitoki usoni mwake leo amekuwa mkali adi nitamani kukimbilia chumbani.
Maneno yake yalimgusa sana Neema nakumfanya awe mpole mamamkwe nae akaingilia nakumuomba mwanae apunguze hasira.
haikuwa kazi rahisi ilichukuwa muda sana mwisho wakaelewana mie nilikuwa kimya nasikiliza tu baada ya maelewano wakapanga iwe lini siku yakwenda kwa mtaalamu au waniletee dawa nitumie bila kwenda.
"Apana uyu inabidi aende kwanza"
Alishauri Neema
"Sawa ila sitaki alale uko mnaenda nae na mumrudishe mkewangu"
Alisema Harvey wakamkubalia baada ya apo nikaingia chumbani kujiandaa na mumewangu akaja pia
Nilikuwa namuogopa alijua ilo akanisogelea nakunikumbatia kisha akanikiss mdomoni.
"Nakupenda mkewangu"
Alisema akiniangalia usoni uku anatabasamu.
"Nakupenda pia mumewangu"
"Naomba usiniogope sawa alafu akikusema lolote uyu Neema niambie"
Alisema ila nikamuitikia tu lakini sikuwa tayari kusema kitu nisije kuvunja undugu wao.
Basi nilijiandaa nilipomaliza nikatoka nakuungana na hao wamama tukatoka nje nakupanda gari walilokuja nalo safari ikaanza.
Ilituchukua masaa matatu tufakifa ni bagamoyo kunaitwa Mlingotini.
Tulifika tukashuka kwenye gari nakuanza kutembea Neema ndie alikuwa mwenyeji wetu akituonyesha njia kwenye mapori ndani ndani adi tulipofika sehemu moja tukaona kijumba kidogo cha nyasi mbele kuna pembe kubwa limefungwa vitambaa vyekundu na vyeusi.
Mara tukasikia sauti kutoka ndani ikisema
"Karibuni karibuni sana ingieni kinyumenyume"
Sauti ilitokea ndani ikasema ivyo niiliogopa nakuanza kutetemeka uku nikijiuliza
"mtu yupo ndani amejuaje nje kuna watu?"
Sikupata jibu, basi akaanza Neema kuingia kinyume akafatia mama mkwe wa mwisho nilikuwa mimi.
Humo ndani kulijaaa tunguri nyingi zilizozungushiwa mahirizi makubwa uku ngozi za wanyama zimetandikwa chini nakuwa kama zuria uyo mganga alijifunga kaniki nyeusi chini juu kifua wazi anamahirizi shingoni yananin'ginia kama cheni, jicho moja kajichora na unga mweupe alikuwa anatisha kama mchawi.
Akaanza kupiga manyanga uku anaimba nyimbo zisizoeleweka
"Najua shida yenu ni mtoto hesabuni mshafanikiwa mimi mchepe wa mchepule ndio kiboko ya matatizo"
Alisema
"Tawile mganga"
Neema akaitia kidogo nikapata faraja nitafanikiwa kupata mtoto nakuona uyu mganga ni mkweli.
"Sogea apa mbele we binti"
Aliniita nikakaa kwenye ngozi iliyokuwa mbele yake akachukua tunguri moja nakuniweka kichwani akaanza kuimba uku anafanya kama anatwanga na kifimbo kidogo baada ya apo akatoa ile fimbo iliyokuwa na rangi nyeusi akanipa mdomoni nilambe ilikuwa kama mkaa vile, baada ya apo akafungua kibuyu nakutoa unga mweupe akamimina kwenye karatasi nakunipa
"Hii dawa utaoga siku saba"
Akatoa mzizi mmoja nakunipa nichemshe nakunywa siku saba pia alafu akanipa na mafuta akinambia nijipake sehemu za siri kabla yakukutana na mumewangu.
"Baada ya mwezi majibu mtayaona"
Alisema mganga kwa kujiamini sana.
Basi Neema alitoa pesa akaweka tukaanza safari yakurudi nyumbani uku akimsifia yule mganga.
"Namuamini sana yule babu noma Lisa we jiandae kupata mtoto"
Alisema akiwa anafurahi sana, japo sikupenda kwenda kwa mganga lakini nilitamani nipate tu uyo mtoto.
Basi tulifika nyumbani usiku wakaniacha nakuondoka zao.
"Pole mke wangu"
Alinambia mumewangu nikamshukuru nilikuta ameandaa chakula tukajumuika pamoja kula baada ya apo tukaingia kulala.
Asubuhi ilifika nikaanza kutumia dawa adi zilipotimia siku saba nikamaliza dawa zote.
Hatimae mwezi mmoja ukafika sina dalili yoyote ya kuwa na ujauzito.
Mamamkwe alipopata habari akamwambia na Neema ambae alienda kwa waganga zaidi ya watano akaja na furushi la dawa nikaanza kutumia miezi sita ikapita akuna mimba wala ujauzito.
Nilikonda raha ya ndoa sikuipata kilasiku nikawa mtumwa wa madawa na mimba sipati ndugu wa mumewangu walinichoka nakuniita mgumba sizai mara tasa amani ya moyo wangu ilitoweka nikawa mtu wakulia kilasiku mumewangu akawa mfariji wangu ila mwisho nayeye alichoka nakuwa mlevi kilasiku anarudi amelewa nikaamua kuwashirikisha wazazi wangu juu ya ndoa yangu.
"Mwanangu ndoa zina mitihani mingi inahitaji uvumilivu mkabidhi mungu ndoa yako atakusimamia kwa kilakitu"
Mamayangu alinambia tangu apo nikaanza kwenda kanisani nikuhudhuria ibada zote nikisikia sehemu kuna mkutano wa injili naenda naomba sana nafunga lakini akuna matokeo yoyote
"Eeh mungu si unipe uyo mtoto jamani kwanini ulinipa mume nakunifanya nisizae naitwa mgumba naitwa tasa mie mungu wangu nihurumie"
Moyowangu unauma unachoma sana naumia wakunifariji sina, wazazi na ndugu wa mumewangu walinichoka nakuniona kama kinyago thamani yangu ilitoweka sikuwa yule Lisa nilesifika kwa urembo na umbo lakuwapagawisha wanaume nilifujika nilikonda macho yote yalipoteza nuru nakuwa mekundu adi natisha.
Mwaka mwengine ukafika bila mtoto shetani alitawala ndoa yangu Harvey akaanza kulala nje, nilipokuwa nikimuuliza kwanini arudi nyumbani anasingizia kazi nyingi ofisini.
Ikanibidi nimshatie mamayake ambae alinijibu
"Mwache alale nje ata mwezi kuliko kulala ndani na mwanamke mgumba usiezaa tena kuanzia leo ukome kuniambia upuuzi mfyuu"
Alisema uyo mama nilijuta kuingia kwenye familia hii kukosa mtoto kulininyima raha ya dunia kuna muda nilitamani nijiue kabisa.
Mumewangu akuonyesha kunijali kwa lolote ata ikitokea siku analala nyumbani anakuja amelewa nakuingia chumba cha wageni kulala.
****
Dunia yote niliona imenielemea ndoa ilikuwa chungu Harvey alibadirika mapenzi juu yetu hayakuwepo tena alinionyesha wazi amenichoka akunipenda tena.
Niliamua kurudi nyumbani kwetu ambapo baba alinikatalia kubaki nirudi kwa mumewangu
"Wewe ni mke wa mtu unaanzaje kurudi nyumbani bila mumeo au talaka? aya rudi ukamalizane na mumewako sitaki kukuona"
"Baba mumewangu amebadirika analewa alali nyumbani ata siku mbili arudi"
Nilisema uku nikilia
"Ayo ni kawaida kwenye ndoa muhimu uvumilivu tu rudi kwa mumeo"
Sikuwa na jinsi niliondoka uku nalia nilipofika nje mama akaja
"Lisa mwanangu kavumilie yakikuzidia rudi nyumbani mamayako sijafa ni mzima achana na uyu babayako mimi nipo"
Alisema mama nikamshukuru nakuondoka kurudi nyumbani kwangu nilishangaa kukuta mlango umefunguliwa nilipoingia ndani nikamkuta Harvey amekaa sebuleni uku glass ya wine ipo mkononi.
Aliponiona naingia akuuliza akanirushia ile glass usoni nakunipasua
"Unatoka wapi malaya wewe yani kuzaa huzai unaona bora kufanya umalaya eeh?"
Aliongea uku akivua mkanda wake nakuanza kunitandika nao mwilini nilijaribu kujitetea nikimwambia
"Nisamehe mumewangu nimetoka kuwasalimia wazazi wangu"
"Iko ndo umeona kisingizio uwasalimie unafaida gani wewe bora ungewapelekea mjukuu unaenda mwenyewe ili iweje tena unatoka bila kuaga shenzi kabisa"
Alisema akizidi kunipiga sikuweza kujitetea tena alinipiga adi alipotosheka akaniacha
"Subiri si unajiona umefika nyumba utaiona chungu hii utatoka bila kufukuzwa"
Alisema ivyo nakutoka nje nikasikia mlio wa gari nakujua ameondoka kabisa, maumivu niliyokuwa nayasikia ayana mfano sikulia kwa ajiri ya kipigo bali kwa jinsi Harvey alivyobadirika nilijikuta namlaumu mungu kwanini ameamua kuchukua furaha yangu yule mwanaume mpole mwenye kunipenda nakunithamini leo amekuwa kama shetani iliniuma maumivu yalinijaa nililia bila kupata wakunibembeleza.
Nikainuka nakuingia bafuni kuona usoni nilipasuka kwenye paji nilioga nilipomaliza nikaingia chumbani nakumpigia simu mama kumueleza sababu kwenda hospital niliogopa.
Usiku huo huo mama alikuja na dawa akanipaka nakunipa zakumeza kupunguza maumivu.
"Pole mwanangu"
Alisema uku akionyesha hudhuni
"Mama nampenda sana mumewangu naamini mungu atambadirisha"
Nilisema kama kujifariji
"Najua maumivu unayopata nakuomba yakikuzidia rudi nyumbani"
Alisema mama hakukaa sana aliondoka zake.
Nilibaki mnyonge siku mbili Harvey akurudi nyumbani adi siku ya tatu akaja usiku na mwanamke akiwa amelewa sana akanifukuza chumbani nakuingia yeye na mwanamke wake maumivu niliyoyasikia hayaelezeki
Sikutegemea kama mumewangu angefikia hatua yakuleta mwanamke ndani ya nyumba namimi nikiwepo iliniuma sana.
"Harvey mumewangu nimekukosea nini mimi?"
"Koma mimi sio mumeo wewe ni housegirl humu ndani beba takataka zako zote humu utoke iki chumba hakikuhusu ni changu kuanzia leol utalala chumba cha wageni"
Alisema nakunifukuza ndani nguo zangu zote akatoa kabatin nakunirushia nje ya mlango baada ya apo akaingia chumbani na uyo mwanamke wake nakujifungia.
Nililia sana nakumlaumu mungu kwanini ameruhusu aya yote yatokee sikuweza kulala nilikesha nalia adi asubuhi sikuweza kutoka nje nilisikia mlio wa gari nakujua Harvey ameondoka.
Huo ukawa mwanzo kilasiku alikuja na wanawake wapya nililia mwisho nilizoea nakukaa kimya nikiangalia nini mwisho wake.
Aliona sifa leo kaleta mwanamke mnene kesho mwembamba, Mara mweusi Mara mweupe warefu kwa wafupi wakawa wanapishana ndani wenye maumbo na wasiokuwa na maumbo kila aina nyumba iligeuka gesti sasa adi nilimpuuza nakumuona ni mjinga baada ya mtoto atapata magonjwa sikutaka kumsemesha lolote asije akajirudi akutane namimi aniambukize magonjwa yake bora afe mwenyewe.
Siku moja nilikaa nakuwaza naishi kwenye hii nyumba ili iweje ikiwa mwanaume mwenyewe ndo uyo cha wote nikaamua kumshirikisha mamayangu anipe ushauri nifanyaje
"Sasa kama mwanaume kafikia hatua yakuleta wanawake ndani unachosubiri apo nini?"
"Sasa mama nifanyeje maana sielewi"
"Akuna chakufanya zaidi ludi nyumbani muache na uhuni wake"
Alisema nikamuelewa
Baada ya apo nikamsubiri Harvey arudi usiku ambapo sikujali amelewa wala mzima siku iyo nilijiandaa sababu nilishamchoka tabia zake nilikuwa mpole lakini kwa dharura nikaamua niwe mrembo mcharuko yule Lisa alievurugwa alirudi sasa.
****
Ilikuwa usiku saa tano nimekaa sebuleni nacheki tv na si kawaida yangu muda huo nakuwa chumbani nimejifungia Harvey alikuja akashangaa kunikuta nipo sebuleni,
"Wewe malaya unafanya nini apo yani unajiachia kuangalia Television unajua nilinunua bei gani?"
Alianza kufoka uku akiwa na mwanamke pembeni.
Siku iyo nilijiandaa kabisa nilivaa kipensi kufupi kama naenda club juu nina t-shirt ambayo haiwezi kuchanika haraka, sikumjibu ila nilisimama nakumgeukia yule mwanamke kwanza
"Umewezaje kuingia kwenye nyumba yangu ukiwa na mumewangu unajiamini kitu gani haswa?"
Nilimuuliza
"Mimi amenambia hana mke anaishi pekeyake"
Alisema uyo msichana ambae alikuwa mnene kiasi amejazia.
"Sasa sikiliza kama yeye ajasema mie ndo nakwambia uyu ni mumewangu wa ndoa kwa usalama wako ondoka kabla sijakuvuruga"
Nilisema uku nimekaza sura nikionyesha sina masihara
"Lisa Lisa nitakupasua naomba ukome kuniingilia mambo yangu mwanamke tasa wewe uzai nani akutake?"
Harvey aliingilia kusema
"Sawa mimi tasa sizai tangu uanze umalaya wako ushatia mimba wanawake wangapi zaidi naisi wamekupa maradhi tu mwanaume malaya wewe kilasiku kuleta wanawake wapya humu ndani alafu we binti utakuwa wa mia mbili umalaya wako kuokota wanaume ovyo utakufa na ukimwi"
Niliongea kwa hasira maneno yalimchoma Harvey akanivamia anipige sikukubali nilikumbuka enzi nipo shuleni nilikuwa napigana adi na wanaume nikaona nipambane nae na vile amelewa ndo kabisa.
Tulivaana ngumi zikaanza apo yule mwanamke alipoona ivyo alitoka mbio nakutuacha.
"Lisa nakuua leo"
"Sema tutauana uwezi kuniua mimi pekeyangu"
Nilikuwa chini yeye juu akinipiga japo nilijaribu kujitetea alipoona haitoshi akasimama akiyumba nakuvua mkanda anipige nao sikukubali nilikuwa na glass mezani nikachukua nakumpiga nayo ya usoni ikampasua.
"Aaah Lisa umeniumiza"
"Kufa kabisa shetani we"
Nilimjibu nikamuacha anatokwa na damu nikaingia ndani nilishafungasha mizigo yangu nikabeba nakutoka nje nilipoenda adi barabarani nikapata bajaji iliyonipeleka adi nyumbani.
Saa sita usiku walishangaa wazazi wangu imekuwaje uku nina damu jicho moja limevimba na kipensi nilichovaa.
"Aya imekuwaje tena?"
Baba akauliza
"Nimemchoka yule mwanaume malaya kilasiku kuleta wanawake ndani leo nimepigana nae video hii apa"
Muda ambao Harvey aliingia niliweka simu yangu sehemu ya rekodi sababu nilijiandaa kwailo nilijua ugomvi lazima utokee na ushahidi niwe nao nilitaka niende mahakamani kudai talaka, basi nikawaonyesha video baba alicheka sana
"Kumbe ujaacha ucharuko wako ila umekusaidia bila ivyo uyu mwanaume angekuumiza"
Alisema baba
"Wewe baba Lisa nawe sasa unacheka nini ebu tulaleni jamani kesho tuongee iweje"
Mama alisema
"Sio kuongea nataka kwenda mahakamani nikadai talaka yangu"
Niliwaambia
"Sawa kesho tutapanga iweje kapumzike mwanangu"
Alisema baba nikaingiza ndani mabegi yangu nakuoga nikalala kwa amani bila kumuwaza Harvey.
Asubuhi kulikucha tukaweka kikao baada ya apo nikaongozana na wazazi wangu adi mahakamani nakufungua kesi yakupigwa na Harvey pia nikitaka anipe talaka yangu basi tuachane barua ya wito ikaandikwa nakupelekwa kwa Harvey ambae alishtuka sana alipoipata akawaambia ndugu zake tarehe 20/4/2015 akaja mahakamani kesi ikasikilizwa apo hakukuwa na mjadala akaandika talaka nakunipatia sikutaka chochote kutoka kwake wasijekusema sijazaa sijui mali sijachuma nae nilichoshukuru roho yangu ipo salama.
Basi kesi ikaisha nakurudi nyumbani japokuwa niliachana na Harvey bado moyowangu haukutaka kumsahau nilimkumbuka kilasiku nikikesha nalia nakutamani siku zirudi nyuma niwe nae moyo wangu ulikuwa na kidonda kikubwa sikujua lini kitaisha, furaha ilitoweka nakuwa mnyonge muda wote mfariji pekee alikuwa ni mamayangu adi siku moja akaja chumbani nakusema anamazungumzo namimi
ITAENDELEA
0 Comments