"Wee Lisa iyo kanga ndani umevaa nini?"
Bibi aliniuliza
"Bibi naniliu bwana si unaona joto?"
"Ujue wazazi wako wametoka kuangalia mashamba yao uko Mpitimbi muda wowote wanarudi pia kakayako yupo ndani sasa aje kukuona na iyo kanga moja jamani itakuwaje?"
"Bibi uyo Gedion anamademu kabisa kwaiyo kuniona mie ata si ajabu"
Basi nikamwambia nakwenda jikoni nimamkuta msichana anapika
"We mambo"
Nilimsalimia nikimshangaa maana sio ndugu yetu
"Poa ujambo mdogo angu?"
Loh eti mie mdogo wake alinichefua katika kitu sipendi mtu anidharau eti mie mdogo
"Mfyuuuuu mdogo wako nani yani nimekustahi tu kukupa salamu ukajiona bonge la mjanja mie ukaniona boya eeh eti mdogo wangu loh huna haya wala ujui vibaya mja mtoka pabaya na bichwa lako kama tikiti maji"
Nilimporomoshea kichambo mdada wa watu adi akaangua kilio kilichomshtua bibi akaja jikoni, Mara nasikia honi inalia wazazi wangu wanarudi nao
"Kunanini uku jikoni we Suzy unalia nini?"
Bibi akauliza
"Amna bibi amejikata na kisu"
Nikamjibu mie apo
"Ooh pole basi ngoja niangalie hao waliokuja"
Alisema nakutoka nje nikamsogelea Suzy sasa
"Nisamehe dadangu usiseme nimekuchamba babangu mkorofi uyo kama kazaliwa porini usiseme nitakupa pesa ila unizoee mimi ndio nilivyoumbwa"
Nilimwambia nikimbembeleza akanielewa mwenyewe basi tukaanza kupiga story apo uku nikijishaua kumsaidia kazi eti
Mara mama nae akaja jikoni nakunishangaa
"Hee Mrembo mcharuko leo unasaidia kazi makubwa"
Alisema akicheka
"Mama nawe sasa umefata nini uku?"
"We mtoto koma nisiingie jikoni kisa nini?"
Alienda kwenye friji akachukua matunda nakutoka zake, basi Suzy akapika apo adi alipomaliza nikamsaidi kutenga mezani wakaanza kula.
Siku iyo walishinda apo apo adi usiku nikaitwa na baba kikao niliwekewa.
"Lisa kesho tunaondoka nakuomba ukae vizuri na bibi yako umapepe wako uache ole wako nisikie umemsumbua nitakuja kukukata maskio ayo"
Baba akaanza mikwala yake,
"Mwanangu utulie usimsumbue bibi yako"
Mama nae akasema mara Gedion akadakia
"Ndio Lisa umsikilize bibi"
Nilimkata jicho baya ilo maana anajifanya mwema mbele ya wazazi kumbe ovyo adi wanawake anao.
Basi wakaongea apo adi walipotosheka wenyewe mimi nikawaaga nakuingia chumbani kulala.
"Yani mimi ilikuwa nizaliwe marekani uku bongo bahati mbaya tu uyu baba kama apate ajari afe sijui lipoje kwanza naisi alizaliwa vita kuu ya dunia ananikera ningejua anapoishi Izraeli mtoa roho ningempelekea pesa aje achukue roho yake"
Nilikuwa naisi naonewa sana nilimchukia baba kuliko shetani.
Basi nililala adi asubuhi niliposhtuka mlango unagongwa nikaamka kufungua ni mama
"Mwanangu sisi ndio tunaondoka ubaki salama shika hii pesa utakusaidia"
Alinipa elfu hamsini nikamshukuru mamangu mara baba nae akaja
"Kwaheri ndo tunaondoka ivyo"
"Sawa safari njema"
"Aya"
Akasema nakuondoka
"Hee baba ndo unipi pesa?"
"Wewe oesa yanini kilakitu kipo apa?"
"Kwaiyo nikiwa na tatizo nitoe wapi pesa?"
"Tatizo gani mtoto mdogo wewe?"
"Nikiwa kwa siku zangu je chu..
Kabla sijaendelea mama akaniziba mdomo.
"Aibu mwanangu kumwambia babayako ivyo loh jaman Lisa utakuwa mkubwa lini mungu wangu mie"
Mama nae akaanza kulalamika
"Ameyataka mwenyewe mi namuomba pesa ataki adi ajue nataka za nini sindo nimemwambia"
Baba alijua kosa lake hakusema kitu akaingia mfukoni nakutoa wallet yake akanipa elfu therathini, basi tukaagana apo kisha wakapanda gari nakuondoka.
Nilishukuru walivyoenda nipumzike kipigo sasa, ilikuwa bado mapema saa kumi na mbili asubuhi nikarudi tena kulala adi saa tatu ndo niliamka.
"Shikamo bibi"
"Marahaba ujambo?"
"Sijambo mbona umependeza asubuhi yote hii safari ya wapi?"
Nilimkuta anakunywa chai kapendeza na gauni lake la kitenge alafu bibi yangu nae kajaaliwa anamshepu wa nguvu adi raha.
"Kanisani kwani ujui leo jumapili?"
Aliposema ivyo nikazusha ugonjwa apo apo
"Mama weeee kiuno kinauma uuuuhh bibiiii"
Nikaanza kulia nakumshtua
"Wewe lisa nini tatizo?"
Bibi akanikokota adi chumbani nikafikia kulala nikijifanya kweli naumwa.
Akatoka nakwenda kumuita Suzy
"Baki umuangalie Lisa mie naenda kanisani"
Alimwambia nakuondoka nililaa kama nusu saa nikaamka
"Unaenda wapi?"
Akaniuliza Suzy
"Naenda kunywa chai njaa inaniuma"
"We si mngonjwa lakini?"
"Kwaiyo kama mgonjwa nisile nife eeh ata kuuguza ujui baada uniletee chakula umekaa tu apo"
Nilimjibu nikatoka nakwenda jikoni kuchukua chai nikanywa.
"Suzy ivi wapi wanakodisha cd za movie?"
Nilipomaliza kula nikamuuliza
"Kule juu barabarani"
"Sawa ngoja nichukue pesa twende tukakodi tuje kuangalia"
Basi niliinuka nakuingia chumbani nikachukua elfu tano tukatoka nakuelekea uko wanapokodisha izo cd.
Nilikuwa naangalia mazingira ya iyo mitaa sijui kunaitwaje mi bado mgeni sikujua bado.
Basi tukafika kwenye fremu moja tukaingia apo tulikuta wakaka watatu wamekaa wanacheki movie kwenye Laptop
"Mambo zenu"
Suzy aliwasalimia mi ndo ata muda wakusalimia nilikuwa sina.
"Aah poa warembo karibuni"
"Asante"
Alijibu, basi nikawa bize kuchagua zangu cd nilipenda sana zakiindi
"We mkaka ile cd aliyoekti Sonil sheti ipo wapi?"
"Inaitwaje iyo?"
"Bwana sijui jina we tafuta nipe"
Basi akainuka mmoja nakunisaidia kutafuta
"Mmmh we mdada umebarikiwa jamani"
Alisema uyo mkaka sikumjibu na wenzake pia wakaniangalia vizuri kumbe mwanzo hawakuniona walikuwa bize kucheki movie
"Ee bwana dah mtoto mbona kajazia sana kama mlima kitonga duh"
Basi wakaanza kunisifia apo wote wakainuka kanisadia kutafuta izo cd
Suzy alibaki anawatizama tu hao wakaka walivyopagawa na umbo langu tena kama kawaida nina kanga moja tu na juu nilivaa kitop kilinibana.
"Naomba namba yako ya simu"
Mmoja akasema
"Sina ata simu mie"
"Dah basi poa badae jioni njoo nina zawadi yako oya nyie shemeji yenu huyu sitaki shobo"
Aliwapiga mkwara wenzake nikamjua uyo ndo mwenye iyo library sijui yakukodisha izo cd basi nikamuitikia.
"Yani nimekupenda ata pesa sikudai"
Alisema nilifurahi nikashukuru pesa yangu imepona nikachagua movie karibu cd kumi bure kabisa baada ya apo tukaondoka zetu nakuacha gumzo uku nyuma wakiniongelea.
"Twende dukani tukanunue soda"
Nilimwambia Suzy
"Mmmh ila Lisa wewe noma cd zote bure ningekuwa mimi ningeogopa"
"Kwani nimeiba si mwenyewe amenipa atanibaka au si adi nikubali kulala nae"
Nilimjibu tukizidi kutembea, njiani wanaume wakware hawakuacha kuniangalia maana iyo vibration nyuma si mchezo.
Basi tulifika tukanunua soda nakurudi nyumbani tukaweka cd nakuangalia adi jioni tulikesha tunaangalia cd tu Suzy akaingia kupika mie habari sina aliivisha tukala nakuzidi kutizama adi bibi aliporudi.
"Hee makubwa aya izo cd mmezipata wapi?"
"Nilikuja nazo bibi"
"Ooh sawa"
Akaingia ndani Suzy wacha acheke
"Yani Lisa wewe"
Basi siku iyo ikapita kesho yake ikafika bibi akasema babangu mdogo aliekuwa chuo mbeya anarudi tujiandae tukampokee na uyo baba atasikuwahi kumuona mie.
Basi ilipofika muda tukaenda stand nakumpokea nilijua mkubwa kumbe mkaka tu miaka ishirini na tano sijui, basi tukarudi nyumbani.
Siku zikazidi kusonga nilipata mashoga mitaani nikawa naenda kuzurura uko adi jioni narudi.
Basi ikafika December sikukuu ya Christmas nikatoka na marafiki zangu Nora na Maureen tukaenda club kwa mara ya kwanza nikaingia club wezangu wakaagiza pombe wakanishawishi namimi ninywe marafiki wabaya jamani wanapotosha.
Basi nikanywa adi nililewa wenzangu wakapata mabwana nakunikimbia nikabaki pekeyangu ata sijielewi nimelewa hatari akatokea mwanaume mmoja akanichukua nakunipandisha kwenye gari tukaondoka adi lodge alipochukua chumba tukalala humo yote yalitokea sijielewi nimelewa vibaya ndo mara ya kwanza kunywa pombe.
Asubuhi sasa kulipokucha nikaamka pombe apo zimeisha nikajishangaa nipo wapi mara sijakaa vizuri namuona mwanaume kajifunga taulo anatoka chooni nilishtuka kumuangalia usoni ni babayangu mdogo Dominic
"Haaaaa baba"
ITAENDELEA
0 Comments