"We nae vipi unavunja vyombo?"
Aliuliza Gedion akicheka sikumjibu nikainama kuokota nakuingia jikoni niliweka kwenye sehemu yakutupa taka, nilipotoka nikaongoza adi chumbani kwangu
"Lisa njo tule unaenda wapi?"
Gedion akaniita sikumsikiliza nikaingia chumbani, mara mlango ukafunguliwa akaingia Harvey
"Wewe nani kakutuma uingie chumbani kwangu?"
Nilitahamaki nikamuuliza.
"Sorry mamy naomba twende tukale pamoja pia nimekuletea zawadi hii"
Alitoa mfuko nakunikabidhi
"Harvey..
Niliita kabla sijaendelea kuongea alinikatisha maneno yangu
"Shiii nakuomba pokea alafu inuka chakula kinapoa"
Alisema akanishika mkono nakuniinua tukatoka nakungana na Gedion mezani tulipoanza kula pamoja.
Japokuwa niliongea kwa ukali Harvey hakujali ilo aliniongelesha kwa upole na sauti yake iliyokuwa nzuri, basi tulikula tulipomaliza nikaingia jikoni kuosha vyombo.
Harvey na Gedion waliingia chumbani kwao namimi nilipomaliza nikaenda ndani kwangu.
Cha kwanza ilikuwa kuangalia zawadi gani aliyoniletea nikafungua mfuko nakukuta pafyumu nzuri ambayo napenda kuitumia nilitabasamu nakujua ni Gedion ndio atakuwa amemwambia sababu yeye hawezi kujua, pia nikaona chocolate nikajikuta nacheka nakuanza kuila, sababu napenda sana chocolate.
Basi nilijilaza kitandani nakupitiwa usingizi nilikuja kushtuka nilipoisi mtu ananigusa mwili wangu nilipofumbua macho nikamuona Harvey
"Wee..umefata nini?"
Nilikurupuka nakumuuliza
"Nimekuja kukuaga naondoka"
"Mmmh aya safari njema"
"Nashukuru mtoto mzuri"
Alitabasamu nakufanya dimpoz zake zionekane basi alitoka Gedion akamsindikiza adi nje alipoondoka zake.
***
Siku zikazidi kusonga uku Harvey akizidi kujenga ukaribu namimi kipindi chote iko hakuwahi kunitamkia ananipenda zaidi ya urafiki wa kawaida japo dalili zote zilionyesha ananitaka kimapenzi ila hakuwahi kunambia nikajua Gedion amemueleza nina mpenzi tayari.
Ilikuwa kawaida yake usiku kabla yakulala lazima aniage nakunitakia njozi njema pia Asubuhi akiamka tu lazima anisalimie nakunitakia siku njema.
Sikuweza kumkwepa Harvey tukazidi kuwasiliana adi siku moja akaniomba nitoke kuna sehemu anaitaji kwenda namimi.
"Naanzaje kutoka baba nitamwambiaje?"
"Lisa nimeongea na Gedion utatoka nae yeye ndie atakae muaga baba usijali"
"Mh sawa"
Nilibaki kuguna tu.
Hatimae wikiendi ikafika ni jumamosi kaka Gedion akamuomba ruhusa baba anataka kutoka namimi tukatembee beach
"Ni vizuri umtoe dadayako siku izi amekuwa mtu wakushinda ndani tu"
Baba akamwambia
"Ndio nataka kumchangamsha"
Alijibu Gedion basi akaenda kujiandaa namimi pia nikawa chumbani kwangu najiandaa japo sikuipenda ile safari.
"Lisa naomba uvae nguo nzuri itayokubana umbo lako sawa eeh"
Gedion akatuma iyo meseji kwa simu nikabaki nacheka tu.
Basi nikatafuta gauni langu fupi kiasi linaishia juu ya magoti nikavaa linabana ni la mpira lilinichora umbo adi nikajikuta najitamani.
Basi nikajipulizia marashi mazuri yale aliyoniletea Harvey baada yakuwa tayari tukatoka Gedion alichukua gari ya baba tukapanda humo.
Safari yetu ilienda adi masaki sijui sehemu gani pale kuna hotel kubwa yakifahari akaweka gari packing nakushuka akaongoza njia yani humo ni wazungu tupu na watu wachache walioonekna wanapesa zao hotel nzuri upepo tu unavuma uku watu wachache wapo kwenye swimming pool wanaogelea na vichupi vyao basi tukaongoza adi sehemu kwenye viti tukamkuta Harvey amekaa apo aliponiona alitabasamu akainuka nakunikumbatia
"Wow you are beautiful and unanukia vizuri"
Alipenda kila neno lake kuchanganya kizungu pia basi akaniachia nakunikaribisha nikae ambapo nilipigwa butwaa Gedion simuoni ikabidi nimuulize yupo wapi
"Kwani ajakwambia amekuleta apa kwaajiri yangu?"
Nilishtuka aliposema ivyo sababu nilijua tutakuwa pamoja.
"Apana hakunambia"
"Ok usijali lakini maybe yupo na girl wake but ukitaka kuondoka atakuja kukuchukua so ondoa hofu"
Alinambia
"Mh sawa"
Nilimkubalia, mara akaja muhudumu nikaagiza kinywaji sababu Harvey nilimkuta anakunywa wine sijui whisky ile tena inaonyesha ya bei sana.
Nilipoletewa kinywaji Harvey akaagiza na chakula.
Basi tukapiga story kidogo chakula kikaja tulikula pamoja baada ya apo akaanzisha maongezi.
"Lisa nikwambie kitu?"
Aliniuliza
"Nambie Harvey"
"Ivi unajijua kama wewe ni Mrembo sana?"
"Jamani sasa unanambia au unaniuliza?"
"Yote ni sawa tu ila sikufichi Lisa wewe ni mzuri sana unaweza kumvutia mwanaume yoyote lijari"
Alisema kwa sauti ya utulivu ambayo haichoshi nilichokuja kugundua kwake alikuwa anajua kucheza na ulimi wake nakutoa maneno matamu hakuwa kama wanaume wengine
wanaobwatuka, Harvey alijua kutumia sauti yake kumfanya mwanamke asichoke kuisikia.
"Stop joking Harvey"
(Acha utani Harvey)
"Lisa serious not joking"
(Lisa nipo makini sio utani)
Alisema akiniangalia tulipokutanisha macho yetu akanikonyeza nakunifanya nijisikie aibu nikatizama pembeni.
Harvey alisogeza kiti karibu yangu akanishika mikono yangu nakuniangalia
"Lisa naomba tizama macho yangu kuna kipi unakiona"
Alisema nikamuangalia nakugundua yupo kwenye mapenzi mazito juu yangu, niliogopa sana nikamkumbuka james.
"Lisa nakupenda sana natamani siku moja uwe mkewangu"
"Apana Harvey haiwezekani nina mpenzi tayari"
Nilijaribu kuitoa mikono yangu lakini nilishindwa alinishika kwa nguvu.
"Najua msichana mrembo uwezi kukosa mwanaume ila naomba nifikilie ombi langu nakuhitaji sana"
"Lakini Harvey wewe si unae mpenzi?"
Nikamuuliza nakumfanya haiachie mikono yangu nakukaa vizuri kwenye kiti chake.
"Nilikuwa nae ila kwasasa sina, sitaki nikufiche Lisa nakueleza ukweli, nilimpenda sana Clara nikampa kila alichohijati zaidi adi familia yake niliihudumia nilipanga aje kuwa mke wangu,mama wa watoto wangu lakini ikawa tofauti Clara hakuwa anaridhika alinichanganya na wanaume wengine, mara kwa mara nilimfumania iliniuma sana akihitaji kiasi chochote cha pesa nilimpa adi gari nilimnunulia sikutaka asumbuke kupanda daladala, hali ya kwao ni ngumu waliishi nyumba ya kupanga na mamayake nikawaonea huruma nilimwibia pesa baba nakuwajengea nyumba, baba alichukia sana nilipochukua pesa zake lakini sikujali, nilichotaka ni kumpa furaha msichana wangu na familia yake, Lisa maumivu kilasiku yalinijaa Clara sijui alitaka roho yangu nimpe mimi nife au nini sababu kilakitu nilimpatia lakini bado akutosheka sitosahau siku moja nilimfumania na mwanaume aliniponza nikapigwa na yule mwanaume akisema namchukulia mwanamke wake, amna siku nilikuwa na hasira kama iyo najuana na polisi wengi tu nilichokifanya ni kupiga simu nakuwaambia Clara na mwanaume wake wamenifanyia fujo kwaiyo wakawekwe ndani adi nitapoamua mwenyewe kwenda kuwatoa adi sasa miezi miwili imepita bado wapo ndani yani nina hasira na Clara lakini kamwe siwezi kuchukia wanawake wote sababu najua hamfanani kila mwanamke na akili zake na sijaogopa kuanzisha uhusiano mwengine kisa kuna mmoja alinitenda vibaya najua mungu hakupanga awe mke wangu"
Alimaliza kusema Harvey uku macho yamekuwa mekundu kuonyesha jinsi gani alikuwa na hasira.
"Naenda toilet nakuja mamy"
Alinambia nakuinuka nikabaki namtizama Harvey alikuwa msafi mwenye kujipenda kimavazi alivutia kumuangalia.
Baada ya muda kidogo alirudi nakukaa
"Pole nimekuacha pekeyako"
Alisema akitabasamu
"Amna bwana usijali"
Mara muhudumu akaja na vinywaji nakuweka akaondoka.
"Harvey tumbo litapasuka jamani mimi nimetosheka"
"Mmmh Lisa jamani yani iyo red bull moja tu ikupasue tumbo ebu kunywa uko"
Alisema sikuwa na jinsi nikaendelea kunywa na giza lilishaanza kuingia
"Usiku umeingia mwambie Gedion aje tuondoke"
Nilimwambia
"Kwani umeshachoka kukaa namimi?"
"Apana sio ivyo"
"Mbona unataka kuondoka nyumbani unawahi nini?"
Aliniuliza nikakosa lakumjibu Harvey akasogea karibu yangu zaidi nakuniambia nisimame
"Kunanini tena?"
Nilimuuliza
"Simama mara moja nikwambie"
Basi nikasimama nayeye pia akasimama nilikuwa mfupi kwake kichwa changu kilishia maeneo ya kifuani kwake.
"Mmmh Harvey we mrefu"
Nilimwambia nakumfanya acheke alafu akanikumbatia
"Nakupenda Lisa"
Aliongea kwa sauti ndogo sikioni kwangu adi mwili ukanisisimka zaidi harufu ya marashi aliyopuliza yalikuwa yananukia vizuri sana bila kutarajia namimi nikamkumbatia.
Harvey alifarijika sana akuniachia haraka alizidi kunikumbatia sana mwisho akanikisi kwenye paji la uso.
"Nakuhitaji Lisa plz nikubali niwe mwanaume wa maisha yako"
Alisema nikamkumbuka James
"Apana Harvey haiwezekani siwezi kuwa nawe"
Nilimwambia nikajitoa mwilini mwake, maneno yangu yalimuumiza sana moyo wake alijisikia vibaya lakini sikuweza kubadirisha msimamo wangu nilimpenda sana james.
"Ok mama siwezi kulazimisha sababu mapenzi ni maridhiano ila muda wowote ukitaka kuwa namimi nakukaribisha milango ipo wazi"
Alisema nakutoa simu yake kumpigia Gedion aje kunichukua.
Basi nilikaa kimya nikimsubiri baada ya nusu saa alikuja wakaongea kidogo mwisho wakaagana.
"Lisa jaman naomba nikuage"
Alinambia Gedion akatangulia mbele kidogo nakumpa nafasi Harvey alienisogelea kanikumbatia na kunibusu shingoni.
"Ufike salama mrembo wangu"
Alisema akaniachia nikaondoka.
Tulifika nyumbani saa mbili usiku sikutaka kukaa sebuleni nilikuwa nimechoka nikaingia chumbani kulala.
Mara simu yangu ikaitwa jina ni Harvey nikapokea
"Lala salama malkia wangu but ilove you mwaah"
Alisema nakukata simu.
Nilijikuta natabasamu tu nakujilaza kitandani adi usingizi uliponipitia.
****
Siku zilizidi kusonga adi ilipofika mwezi wa kumi na moja nikaomba wazazi niende kijijini kwa bibi ata Christmas nikale uko nia yangu muda huo nikautumie kuwa na mpenzi wangu James nilimkumbuka sana.
Basi hawakuwa na tatizo nikakusanyiwa zawadi zakumpeleka bibi lakini mimi pia nikanunua zawadi ya James na mamayake nikawape.
Ila nilitaka kupanda gari la abiria sikutaka kupelekwa na baba au mama, wakanielewa siku ikafika nikajiandaa nakuvaa suluali yangu nzuri ya bluu iliyoikaa vyema juu nikapiga top nyeupe.
Gedion alitoka nakunisindikiza stand ya mkoa ubungo japo si mbali lakini tulitoka na gari, tulipofika ubungo mataa akasimamisha gari pembeni nakuongea na simu kama anamuelekeza mtu aje.
Basi baada ya nusu saa nikaona gari limekuja nakupaki pembeni yetu akashuka Harvey mara Gedion nae akatelemka nakuniomba namimi nishuke.
"Kuanini kwani unajua nachelewa na tiketi sijakata bado?"
"Usijali bwana Harvey anakupeleka adi kwa bibi teremka upande humo kwenye gari"
Alinambia nakunifanya nishangae sana, mara Harvey nae akasogea kwenye gari letu
ITAENDELEA
0 Comments