MEANDIKWA NA : JACK MAMBO
*********************************************************************************
"Profesa!Profesa!",alisikika kijana mmoja akimuita mzee mmoja aliyekuwa anapita njiani!
Mavazi yake yalichakaa Sana,ndala zake zilikuwa zimetoboka na kujaa viraka vingi!!
Nywele zake zilitoa tafsiri halisi,kuwa huyu Profesa ana muda mrefu hajayaona maji au haogi kabisa!kwa lugha ya mtaani tungesema Profesa ana ugomvi na maji!
Lilikuwa ni jambo la kushangaza kumuita Profesa mtu ambaye mavazi na muonekano wake vilibeba uhalisia wa maisha yake!
Kwa kumuangalia tu ungejua ni mtu wa shida nyingi maskini na mlala hoi,mtu ambaye kupitisha kwake ni kawaida!Mtu ambaye akibahatika kupata milo miwili anamshukuru Mungu mara sabini!
Kijana yule alipoona anamuita Profesa hageuki ndiyo kwanza ameinamisha kichwa chake chini mikono yake ikiwa nyuma,anatembea taratibu hana haraka!
Aliamua kumkimbilia,alipomfikia alimshika mkono akiwa anahema kwa kasi!
"Profesa!Profesa!",alimuita mzee yule akasimama akimtazama,moyoni Profesa aliskitika sana kuona kijana akiwa anahema kwa kasi kama kakimbia mbio za mita mia tano,kumbe ni umbali wa hatua ishirini tu au kumi na tano kwa makisio ya haraka!!
"Profesa nina shida nisaidie!"
Aliongea kijana yule akionekana ni wazi kuna jambo linalomsumbua!
Profesa alikuwa kimya anamuangalia tu kama hamsikii!
Kwa watu waliomzoea wanajua Profesa ili aweze kuongea na kutoa ushauri wa jambo lolote lile kuna namna ya kufanya!!
"Profesa kuna jambo linanitatiza sana!"
Yule kijana aliongea lakini bado Profesa alikuwa kimya anamsikiliza tu!
Kijana yule alijua ni nini anatakiwa kufanya ili Profesa aongee!
Alimshika mkono wakaongozana mpaka mpaka kwenye gari lake,akamfungulia mlango Profesa akapanda na yeye akapanda akawasha gari ili ampeleke Profesa sehemu ambayo itamfanya aongee!!
Safari iliishia katika hoteli moja nzuri ya kifahari!
Alipaki gari kisha akamfungulia mlango Profesa naye akashuka!
Mavazi aliyokuwa kavaa yalimtia hofu mlinzi akataka kumzuia akiamini kama sio chizi basi ni omba omba anaenda kusumbua wateja!
"Muache niko naye!",alisema yule kijana ndiyo mlinzi akamruhusu Profesa kuingia ndani!!
Walifika wakakaa kwenye meza ya peke yao!Watu waliwashangaa sana,hasa yule kijana kuingia na mtu ambaye si hadhi yake!Lakini yule kijana hakujali!Alichotaka ni suluhisho la tatizo lake na aliamini hakuna mwingine wa kumsaidia zaidi ya Profesa!
Sifa zake alizosikia kwa watu wakimhadithia zilimfanya amuamini Profesa moja kwa moja!
Mhudumu alikuja akawauliza ni chakula gani wangependa kutumia!!
"Niletee chipsi kuku,msikilize na Profesa",aliagiza yule kijana,kauli yake ilimuacha na maswali yule mhudumu,aliangaza macho huku na kule akitegemea atamuona Profesa maana kwa mtu anayemuona mbele yake ni kama kichaa kama siyo kichaa kabisa!
"Samahani kaka umesema nimsikilize Nani?"
"Profesa!"
"Yuko wapi?"
"Kwani nimekaa na nani?"
"Samahani!",alisema yule mhudumu akimsogelea Profesa,moyoni alijisemea Profesa mwenyewe ndiyo huyu!
"Samahani unatumia chakula gani?"
"Ugali wa dona na samaki ambaye hajaugwa kama yupo,chukuchuku!"
"Mchemsho!"
"Huo huo!"
Alisema Profesa akiongea kwa mara ya kwanza,sauti yake ilionekana ni ya mtu aliyechoka sana na kama hajachoka basi hajala siku kadhaa!!
Kijana yule alionyesha matumaini kwani kupata ushauri wa Profesa ni habari nyingine lakini pia kumfanya aongee ni habari nyingine!
Mhudumu aliondoka na punde alirejea akiwa na vyakula alivyoagizwa akaweka mezani!
"Karibuni!",aliwakaribisha kwa ukarimu.
"Ahsante tuletee na juisi tafadhali!"
Profesa baada ya kunawa tu hakusubiri hata juisi,alianza kula chakula chake akionyesha ni wazi kuwa alikuwa mtu mwenye njaa sana,kula yake ilitoa tafsiri ya njaa aliyokuwa nayo!!
Kijana naye alikula chipsi zake kibishoo taratibu!
Baada ya dakika kumi na tano Profesa alimaliza kula chakula chake!
Akainua macho yake kumtazama kijana ambaye alikula chipsi zake kibishoo!
Alibakiza chakula karibu chote akanawa mikono yake akawa anakunywa juisi yake taratibu!
Profesa bila kuuliza aliivuta sahani ya yule kijana akala chakula chote kilichobaki alipomaliza akashushia na maji glasi nzima akacheua kuonyesha sasa yuko sawa!!!
Akaishika glasi ya juisi akaanza kunywa taratibu.
Sura yake sasa ilichangamka hakuwa Profesa wa dakika chache zilizopita!
Kijana akaona huo sasa ndiyo muda wa kueleza dukuduku lake kwa Profesa ambaye anaamini angemsaidia sana!!
"Profesa nina shida!",aliongea yule kijana huku anameza funda moja la juisi kisha akaiweka glasi mezani!
"Unaonekana una shida kubwa eeh!Mpaka unasahau kujitambulisha!",aliongea Profesa huku anashusha glasi yake ya juisi mezani!
"Ooh!Samahani naitwa Derrick nimeelekezwa kwako na rafiki yangu!"
"Lakini tumekutana njiani kijana siyo kwangu!"
"Aaahhh!ndiyo nilikuwa nakuja kwako kama bahati nikakuona njiani!"
Hivi ndivyo alivyo Profesa ana hoja nyingi,ni mtu wa kuzua hoja katika kila swali na sentensi!
"Sawa una shida gani kijana!"
"Mimi shida yang....yani shida....shida yangu niiiiiiii....!"
"Kijana kuwa mwanaume bhana!unajivikaje ngozi ya swala wakati wewe ni chui.(maana yake yani unaongeaje kama mwanamke wakati wewe ni mwanaume).
Kijana yule aliinamisha kichwa chini kwa aibu!
"Jikaze sema nikusaidie shida nini?"
kijana aliamua kujikaza aeleze shida iliyomfanya amtafute Profesa!
"Shida yangu ni mke wangu Profesa!"
"Mke wako au mpenzi wako,maana vijana wa sasa hamjaoana tayari mnajivika vyeo mnaitana mume na mke sijui mkioana mtaitana nani,mke ni cheo umeoa!"
"Mkewangu kabisa Profesa nimeoa kwa ndoa ya kanisani kabisa!"
"Shida yake nini?",aliuliza Profesa!
"Mkewangu kabadilika sana,hayuko kama zamani!
Hanipokei tena nikitoka kazini nahisi simvutii tena!Anakuwa mkali hata chumbani hataki nimguse anasema eti namchafua,simfikishi na hafurahii kufanya mapenzi na mimi!"
"Ukifanya naye mapenzi huwa unatumia muda gani kumaliza?",aliuliza Profesa!
"Profesa huwa situmii muda mrefu nakuwa nimechoka sana,kazi zangu zinanichosha sana Profesa!"
"Huwa unabeba zege?",alisema Profesa!
"Hapana Profesa mi nakaa tu ofisini!"
"Ulishaskia mke wa mbeba zege analalamika hafikishwi?kazi yako ni ngumu kuliko kubeba zege?"
"Hapana zege ni ngumu!",alijibu yule kijana!
"Una miaka mingapi kwenye ndoa!"
"Miaka miwili Profesa!"
"Wakati unamuoa huyo binti ulikuwa na kitambi?"
"Hapana nilikuwa na six pack kabisa!"
"Unaamka sangapi kwenda kazini?"
"Huwa naamka saa mbili kazini naingia saa nne?"
"Wakati unaoa si ulikuwa na michepuko pia?na je ulikuwa unatumia muda gani kufanya mapenzi?
"Nilikuwa vizuri Profesa,tena nilikuwa kiboko mpaka wanawake walikuwa wananikimbilia,nilikuwa jabali na hata wakati namuoa mkewangu nilikuwa nasimamia ukucha haswa!",alisema kijana akijisifu kwa matokea ya kidato cha nne akasahau amefeli kidato cha sita!
"Hahahahaaa!Derrick unanifurahisha Sana!Sasa tatizo nini saivi unashindwa kusimamia kucha?"
"Sielewi Profesa!"
"Tatizo ni wewe Derrick!"
"Mimi tena jamani?Profesa siyo kweli!!
Alishangaa Derrick kuambiwa kuwa tatzo ni yeye,alikataa kabisa!
Tulipoishia.....Derrick amefika kwa Profesa kueleza shida yake lakini anashangaa baada Profesa kumwambia kuwa shida ni yeye na siyo mkewe!
Songa nayo..
"Tatizo ni wewe Derrick!", alisema Profesa.
"Mimi tena jamani?Profesa siyo kweli!
"Derrick,acha ubishi!Umeacha zamani kuishi kama mwanaume!"
"Unamaanisha nini Profesa?"
"Umekuwa mwanaume wa dar,tena mshukuru mkeo anayekuambia ukweli kuwa humvutii na humfikishi,wengine huwa hawasemi wanavumilia wakishindwa wanaamua kuchepuka!"
Derrick aliinama chini kwa aibu,maneno ya Profesa yalimchoma!
"Umeoa una six pack miaka miwili tu una kitambi,baada ya miaka mitano utakuwaje Derrick!
Nimekuona hata pale uliponikimbilia,ni hatua chache lakini jasho limekutoka,umezoea kutembelea matako Derrick!
Mwanaume unaagiza chipsi kuku hahahaha Derrick!tena unakula vichips vyenyewe unabakisha hahahaaa unajikaanga kwa mafuta yako Derrick!"
Derrick alikaa kimya,macho yake yalitazama chini kwa aibu!
Maneno ya Profesa yalikuwa msumari wenye ncha kali alihisi yanamchoma moyoni!Siyo msumari tu bali moto uliomuunguza moyoni!!
Profesa yeye alikuwa anacheka tu huku anakunywa juisi yake taratibu!
Derrick alinyanyua kichwa chake akamuangalia Profesa!Kisha akasema!
"Profesa nisaidie, nampenda mkewangu!"
Profesa alimuangalia Derrick Kisha akakohoa kurekebisha sauti take!
"Derrick!"
"Naam Profesa!"
"Unamuonaje mkeo?kabadilika?au na yeye anajizeesha mapema kabla ya muda wake kama unavyofanya wewe?"
"Profesa!mke wangu ni mrembo sana na kila siku anazidi kuwa mpya machoni mwangu!",alijibu Derrick.
"Inabidi huendane na kasi yake,jipende Derrick rudisha mwili wako,pengine alikupendea six pack Ila wewe sasa umefuga kitambi?pengine alikupendea utamu wa chumbani,pengine ulikuwa ukimshika mpaka anasema mume wangu ni kidume!
Derrick wanawake wanasimuliana,unamnyima mkeo stori ya kutambia kwa mashoga zake!Akisema mume wangu ni handsome wanamuuliza na kile kitambi je?
Derrick badilika sasa,amka mapema fanya mazoezi kula vizuri achana na vichips hivi na kuku hizi za kizungu!
Kula ugali Derrick,kula vyakula vyenye tija mwilini!Hakuna haja ya alkasusu,fanya mazoezi heshima yako itarudi!"
Machozi yalimtoka Derrick,alianza kulia kama mtoto!
"Profesa!nimemkosea mkewangu!"
Profesa alikuwa kimya anakunywa zake juisi tu taratibu!
Derrick alichukua leso akajifuta machozi!
"Profesa!umenipa funzo na hakika ntaenda kutoa elimu kwa wengine!Nilimuona mkewangu ni tatizo kumbe tatizo ni mimi!
Nakuahidi naenda kuyafanyia kazi yote yale ambayo umenimbia".
"Hahahahaaaa!",profesa alicheka huku anamalizia funda la mwisho la juisi!
"Unajua profesa kuna kitu unaweza ukawa unakosea bila kujua!Ahsante sana Profesa umenishika mkono ukanitoa kwenye bahari ya upumbavu!"
"Usijali kijana nipo kwa ajili yenu!"
"Sasa Profesa nikupe lift basi nikushushe hapo mbele!"
"Hahahahaaa!hapana kijana,kwa ulipofikia natamani hata ungekuwa na uwezo upae ukaokoe ndoa yako!"
"Hapana Profesa naomba nikushushe hapo mbele!"
"Derrick!unachelewa omba mkeo hasiwe amekata tamaa,kuirudisha imani ya mwanamke au upendo wake ukipotea ni sawa na kuzoa maji yaliyomwagika chini sakafuni!Hata ukiyazoa utazoa tope!"
"Usijali kuhusu mimi,mimi miguu yangu ilishalambwa na mbwa!situlii kama bahari leo Niko huku kesho kule!"
"Sawa Profesa nashukuru,ngoja niwahi"
"Wahi kijana,vita yako ni kubwa ni bora upambane na Simba aliyekasirika kuliko penzi linalochechemea!"
Derrick alikuna kichwa chake,mkononi mwake alishika funguo akainuka ili aondoke,akasahau kumalizia juisi!
"Hahahaha!Derick bado unafanya ubishoo kwenye kula,malizia juisi bhana!"
Derrick alipanda gari lake akaliondoa kwa kasi sana!
Profesa naye alishika njia yake akiwa anaelekea kusikojulikana!
Mara nyingi akitembea alikuwa anasimama anaangalia juu!
Profesa amepitia visa vingi vyenye kusikitisha,hivyo anasema anavyoangalia juu huwa anamuuliza Mungu!
"Mungu ni kweli nastahili aya?kwanini Mimi?kosa langu nini?ivi kweli nastahili aya????
Kuna hadithi nzuri ya mapenzi nyuma ya Profesa!
Ila hadithi ile inasimama kwenye upande wa pili wa huzuni!
Kama unavyojua mapenzi yalivyo yamekatika katika pande kuu mbili,UTAMU na UCHUNGU!
Hadithi ya Profesa ni nzuri ila imesimama kwenye uchungu tu,hakuwahi kuionja asali ile wanayosema wahenga!
Katika maisha yake ameishi kumpenda mwanamke mmoja tu,na hajawahi kiwa na mwanamke mwingine!
Profesa hajawahi kusaliti ila alisalitiwa sana!
Naitwa Profesa Masumbuko kama ambavyo wananiita,Ila majina yangu halisi niliyopewa na Mama yangu ni Masumbuko Charles!
Mama yangu anasema aliniita jina hili baada ya kupitia mateso mengi kipindi cha ujauzito wangu!
Alikiri kwa kinywa chake kuwa alijaribu kuniua mara kadhaa ila ikashindikana,Masumbuko niligoma kufa tumboni mwa mama yangu!
Licha ya dawa nyingi za kizungu na za hospitali bado Masumbuko niligoma kufa!
Kuna muda huwa natamani bora ningekufa kuliko maumivu haya ninayoyapitia duniani!
Mama yangu alishindwa kuniua,lakini huwezi amini hata mimi nilishindwa kujiua!
Nilishajaribu mara kadhaa kunywa sumu,kujichoma kisu na kujinyonga lakini nikizinduka najikuta hospitali nikiwa mzima!
Huwa nasema pengine huwa nakufa halafu nafufuka, haiwezekani kila nikijiua nikifumbua macho najikuta mzima wa afya!
Mateso niliyopitia duniani na maumivu makali ya mapenzi yalinifanya niyajue mapenzi kwa hali ambayo huwezi nidanganya!
Ukinisimulia kisa chako cha mapenzi kwa sentensi zako mbili tu nakuwa nimeshajua unapendwa au unapoteza muda!
Nilijikuta naangukia kuwa mshauri wa mapenzi mitaani,nikitoa ushauri kwa watu mbalimbali ambao uliwasaidia sana!
Unadhani nimesoma sana?hapana mi nimeishia Kidato cha sita tu!
Nadhani utakuwa una maswali mengi juu ya hili jina la Profesa!
Mimi sikusoma sana,nilisoma nikajua kizungu basi nikaacha shule baada ya kukosa mkopo utaoniwezesha kulipa ada na matumizi mengine ya chuo!
Jina la Profesa walinipa hawa walimwengu,wanaopitia maumivu mengi ya mapenzi!
Ushauri wangu umekuwa chachu kwenye mahusiano mengi!
Nilianza kutoa ushauri kwa marafiki zangu,wakaongezeka jirani zangu wakafata watu kutoka sehemu mbalimbali!
Sasa jina langu limeshakuwa Profesa,Profesa Masumbuko!
Je unajua ni nani aliyenifanya nipate ujuzi wa kuyajua mapenzi nje ndani!
Hahahahaaa!usiulize ni nani,ni mwanamke!Ndiyo mwanamke tena sio jini ni bindamu tu!
Ni kama wanawake wengine ila tofauti yake ni kuwa ,yeye alikuwa mwanamke mrembo zaidi machoni mwangu!
Nimeshaona warembo ila macho yangu yaliniambia kuwa yeye ndiyo mwanamke mrembo kushinda wanawake wote niliowahi kuwaona!
Akili na moyo vikanisaliti,nikamkumbatia na kumganda kama luba!
Nakiri tangu nimuone alizifunika mboni zangu!Sijawahi kutamani kuwa na mwanamke yoyote zaidi yake!
Nimekua chizi kwake sielewi,mtumwa wa mapenzi yake!
Nilikuwa bendera tu nayeye akawa upepo,napepea upande wowote anaonipeleka!
Hakuna jema ambalo sijawahi kufanya kwake,hakuna baya ambalo nilishatenda kwake!
Kwake hakuna jema alilowahi kutenda kwangu hata kwa bahati mbaya!Pia hakuna baya ambalo hajawahi kutenda kwangu!
Hahahhahahhaa!mapenzi bhana,mapenzi ni nini??
Kama ni utamu ukoje?kwani utamu wa mapenzi ni kukojoa basi ntakuwa na mimi nilishawahi kuonja utamu wa mapenzi!
Ila kama utamu wa mapenzi ni kujali,kupendwa,kuheshimiwa na kuthaminiwa...basi mimi sijawahi onja utamu wake hata kidogo!!!
Kama mapenzi shubir basi nimekula Sana!
Nimepitia maumivu mengi,nilishalia sana mimi,laiti ningekuwa nayakinga machozi yangu na kuyahifadhi kama kumbukumbu basi ningeshajaza mapipa kadhaa!!!
Sisemi kuwa wanawake wote ni wabaya,hapana!
Au wanaume wote tunaonewa,hapana!
Kuna wanawake wanajua kupenda na wanaume pia!
Ila wapo mashetani pia wanajua kutenda haswa!!!
Usjali najua nakuweka njia panda,ngoja nikupe story yangu!
Na wewe ukawasimulie wenzio huko!
Naamini utajifunza kitu kupitia hadithi hii ya Profesa Masumbuko!
Usipojifunza basi utajifunza siku yakikukuta,nami sitaki ufikie huko!
Nipe sikio lako!!
Nakumbuka siku hiyo kulikuwa na upepo mkali sana kijijini kwetu,kiasi kwamba unaweza kuhisi paa linaondoka muda si mrefu!
Wingu zito lilitanda,ghafla mvua kali ikanyesha.
Mvua iliyoambatana na radi kali na miungurumo yenye kutisha!
Mama alikuwa nje anakinga maji masafi ya mvua!Maana safari ya kwenda kisimani ilikuwa sawa na umbali wa kutoka Uhasibu mpaka mbagala!
Hivyo mvua ikinyesha ni kama inatupunguzia safari ndefu ya kisimani!
Wakati huo mimi nilikuwa ndani najaribu kupitia pitia mdaftari yangu.
Nakumbuka nilikuwa kidato cha pili kipindi hicho!!
Ghafla nikiwa ndani niliskia mama akiwa anaongea na mtu nje!!!
"Karibu ingia ndani ujikinge ikiisha utaendelea na safari zako!"
"Ahsante!"
Aliingia msichana mrembo,nikikuambia mrembo elewa alikuwa mrembo sana!
Nguo zake zilikuwa zimelowana na kushika mwilini mwake!
Umbo lake lilijichora kwa herufi namba nane ya chuo kikuu!!
Si unajua kuna nane ya chekechea na ya chuo kikuu!hahahaaa hujanielewa bado!Namaanisha nane inayoandikwa na mtoto wa chekechea haiwezi kufanana na ya mwanafunzi wa chuo kikuu!!
Alifika akasimama mbele yangu,macho yangu yalinisaliti yakaachana na madaftari yakabaki kumshangaa malikia huyu mrembo!
Sijui nilitumia dakika ngapi kumshangaa wala sikumbuki alinisalimia mara ngapi sikumskia!
"We Masu hata humkaribishi mwenzio jamani!",sauti ya mama ndiyo iliyonishtua nikazinduka kutoka kwenye mshangao ule wa ajabu!
"Ka..ka..karibu,Karibu ukae!",nilijibu nikibabaika sana,malikia yule alinichanganya haswa!!!
Alikaa binti yule ambaye alikuwa anatetemeka kwa baridi, nadhani sababu mvua ilimnyeshea sana,na angepata wapi pakujikinga ilihali kijijini kwetu nyumba no chache tena ziko mbali mbali haswa,kiasi kwamba hata kuazima chumvi kwa mwenzio mpaka ufunge safari!!
Sijui nilipatwa na nini?macho yangu yalikosa ujasiri sikuweza kumtazama yena binti yule aliyepambwa kwa nywele ndefu kichwani huku ngozi yake ikifunikwa kwa rangi nzuri ya mtume!
Rangi ambayo ukiwa nayo usukumani basi wazazi wako watakuozesha kwa ng'ombe nyingi sana!
Niliinama nikajifanya nasoma madaftari yangu,lakini kusema kweli kwa muda wote ule hakuna kilichoingia zaidi hata vile nilivyosoma vilipeperuka !!
Nilipojaribu kuinua macho yangu,nilimkuta na yeye ananiangalia!
Tulipokutanisha macho alitabasamu nikaviona vishimo kwenye mashavu yake!
Mwili wangu ulisisimka kwa hisia kali sana,sikuwa nimewahi kusisimka vile.
Nahisi ni kwa sababu nilikuwa sijayajua mapenzi kipindi kile,nilikuwa bado simjui mwanamke!
"Unaitwa nani binti!",mama ndiye aliyemuuliza baada ya kutoka chumbani!"
"Nani mimi?",aliuliza yule binti!
"Ndio!"
"Mimi naitwa Scolastika Robert!",aliposema tu jina lake nilichukua kalamu nikaliandika nyuma ya daftari langu!"
"Unatokea wapi na mvua hii?"
"Mi naishi kijiji cha pili,nilitumwa kwa shangazi,mvua imenikuta wakati narudi!"
"Aya sawa pole sogeza jiko uote moto!"
Alisema mama Kisha akaendelea kuchota maji!
Mvua ilikata baada ya dakika kama arobaini!Ndipo mama akaniambia.
"We Masu chukua baskeli umsimdikize mwenzio Ila usikawie!"
"Sawa mama!",moyoni nilifurahi kupewa hii nafasi lakini mpaka hapo sikujua nitaenda kuongea nini?"
Nilichukua baskeli nikampakiza Scola,safari ikaanza!
Nilikuwa kimya,sikujua ntaanzia wapi kumuongelesha Scola,ujanja huo sikuwa nao!
"Unaitwa nani?"
Hatimaye Scola alivunja ukimya,sauti yake ilikuwa nzuri sana ilipenya maskioni mwangu nikahisi kama naskiliza nyimbo nzuri za mapenzi kutoka mwanamuziki mashuhuri wa Marekani maarufu kama Cellin dion!
"Na...nani...mimi?"
"Ndiyo wewe!"
"Naitwa Masumbuko au niite Masu tu jina langu refu sana!"
"Hahahahaaa una jina baya!"
Kitu ambacho ulikuwa hukijui ni kuwa Scola hajawahi nisifia hata kwa bahati mbaya!
"Sio sanaaa!",nilimjibu ila moyoni nilikiri jina langu baya kweli,sijui kwanini mama alinipa jina hili lililobeba tafsiri halisi ya maisha yangu,Masumbuko na nimesumbuka kweli!
Baada ya safari ndefu tuliingia kijijini kwao!
"Nishushe hapa!",aliniambia nikasimamisha baskeli yangu!
"Umefika!"
"Hapana napitia sehemu kwanza nahisi baridi nikaote moto!"
"Kwani kwenu hamna jiko?"
"Kwani we tatizo lako ni nini Masumbuko,sumbukia yako bhana kwanza unaonekana mshamba mshamba hata nikisema unipe hutoweza!"
Alisema Scola muda huo anaishia porini kuota moto!
Maneno yake yalikuwa fumbo kwangu!sikuelewa alimaanisha nini,nikabaki najiuliza porini kule kuna moto gani?
Macho yangu yalimtazama Scola akiwa anapotelea porini!
Japo bado alikuwa binti mdogo lakini alikuwa si haba!
Scola alijaliwa msambwanda wa maana!
Niligeuza baskeli yangu kinyonge nikaanza safari ya kurudi nyumbani,
Niliskitika sababu Scola hakuonionyesha kwao,Ila tumaini nilikuwa nalo baada ya kujua anakaa Kijiji jirani!
Maisha yangu yalibadilika tangu nimuone malaika yule,chakula hakikulika,masomo hayakusomeka!
Tangu siku ile namuacha anapotelea porini akisema anaenda kuota moto,ni kama aliondoka na akili yangu!!!
"We Masu una nini siku hizi",aliniuliza mama siku moja!
"Kwanini mama!"
"Hueleweki si kutoa si kujumlisha Mambo yako zigizaga tu umekuwaje mwanangu!"
"Hapana mama niko sawa!"
"Mwanangu mwenyewe,nimekuzaa mwenyewe na nimekulea mwenyewe leo unaniambia uko sawa?"
Mama yangu ndiyo baba yangu,Masumbuko nilishakataliwa na baba yangu tangu nikiwa tumboni!Naskia aliondoka zake kwenda mjini huku nyuma akiacha maneno yenye kuumiza!
Alimwambia mama mimba siyo yake, akamwambia amtafutie baba yake siyo yeye!
Kwa shida alizopitia mama yangu kuilea mimba mpaka kunizaa na kunilea hadi nilipofikia kwa biashara yake ya genge unadhani kwanini asinitupie hili jina la "Masumbuko?"
Mpaka kipindi hicho nilikuwa bado sijajihusisha na mapenzi,nilitaka kusoma,nikiamini elimu ndiyo mkombozi wa maisha yangu!!!
Ila kama unavyojua mapenzi hayana kiapo, unaweza ukaumizwa ukasema sitopenda tena lakini baada ya siku kadhaa unajikuta umeanguka penzini tena umependa kweli.
Kwa hiyo mapenzi jamani hayana kiapo amini usiamini!
Scola ni alivunja kiapo changu,akaingia ndani ya moyo wangu!Akatembea kwenye misuli ya damu mwilini mwangu!
Sikuweza kuvumilia,siku moja baada ya kutoka shule niliamua kwenda kwenye Kijiji cha pili,niende nikamtafute Scola!!
Nilizungusha pedeli za baskeli yangu nikiwa na shauku kubwa ya kumuona malikia Scola!
Bahati mbaya ilikuwa kwangu,kwani kabla sijafika nusu ya safari yangu baskeli yangu ilipata pancha!
Nilipopatia pancha ni karibu kwa kurudi nyumbani kuliko kwenda kwenye kijiji anachokaa Scola!
Sikuwa na jinsi niliikokota baiskeli yangu kurudi nyumbani nikiwa mnyonge sana!
Mama aliponiona alishtuka maana sikumuaga,sababu ningemuaga hasingeniruhusu!
"We mwana wee!unatoka wapi?",alinipokea na swali ambalo tayari nilishaliandalia jibu!
"Nilikuwa naenda kwa kina Said mama kuchukua kitabu,lakini baiskeli imeniharibikia njiani!"
"Mwanangu Masu,umeanza lini kutoka bila kuniaga?"
"Samahani nilipitiwa mama!"
"Aya katengeneze hiyo baiskeli!"
Mama alinipa pesa nikaenda nikaenda sokoni kutengeneza baiskeli ikatengemaa.
Lakini jua tayari lilishaanza kuzama,haikuwezekana tena kwenda kumtafuta Scola siku ile!
Nilijipa moyo sababu kesho yake ilikuwa wikiendi hivyo ntakuwepo nyumbani!
Lakini wikiendi huwa naenda gengeni kwa mama kumsaidia saidia na yeye hupata muda mwingi wa kupumzika nyumbani pamoja na kufanya shughuli nyingi za usafi kama kufua na kadhalika!
Siku hiyo nilimtafuta Said nikamuomba kesho aje tukauze wote sokoni,nikiwa na maana yangu!
Kesho yake Said alikuja tukaenda wote sokoni,ndipo nikamuacha Said akiuza mimi nikapanda baiskeli kwenda Kijiji cha jirani kumtafuta Scola!
Siku hiyo nilifika salama ila tabu ikaja kumtafuta Scola wangu!
Nilikuwa mgeni katika Kijiji kile sikuwa namfahamu mtu zaidi ya Scola!
Kitu nilichogundua ni kuwa,Kijiji cha kina Scola kilikuwa kimechangamka kuliko Kijiji chetu!
Kilikuwa na watu wengi na pilika pilika nyingi za kutosha!
Niliamua kubahatisha nikaanza kumuulizia Scola!
Ila ili iwe rahisi kumpata niliamua kuwaulizia mabinti ambao niliona rika lao ni kama lake!
"Samahani dada!"
"Bila samahani!"
"Kwema?"
"Kwema!"
"Namuulizia Scola kama unamfahamu!"
"Nani huyu Scola Mapepe?"
"Mmhh!sijui ndiyo yeye maana hata sielewi maana yeye alisema anaitwa Scola iyo mapepe naiskia kwako!"
Hilo jina lilinichanganya,moyoni nikajiuliza Scola huyu?Scolastika ndiyo leo kawa Scola mapepe haiwezekani!
"Atakuwa huyo huyo,hapa kijijini hakuna mtu anaitwa Scola labda kilichokuchanganya ni hiyo Mapepe!"
"Samahani unaweza kujua halipo?"
"Scola leo wikiendi huwa anazurura hatari labda kama kubahatisha!"
"Nipeleke tafadhali!"
Binti yule alianza kunitembeza sehemu mbalimbali ambako Scola hupenda kutembelea Sana!
Tulizunguka kama nusu saa bila mafanikio!
"Kaka mi nimechoka kwanza nachelewa nyumbani Scola huyu kumpata sidhani!"
"Dada tafadhali nisaidie nina shida ya mhimu!"
"Nakupeleka sehemu moja hiyo tukimkosa hapo basi!"
"Sawa dada nashukuru!"
Nilimbeba binti yule ili anipeleke kwenye iyo sehemu ya mwisho!
Lakini cha kushangaza alifika hadi maeneo yale ambayo niliachana na Scola akisema anaenda kuota moto!
"Mmmhh!ndiyo huku?"
"Ndiyo kwani unapafahamu?"
"Hapana!"
Tulikatiza njia ile aliyopitia scola kuelekea kule porini!
Kwa mbali tuliona nyumba ya udongo iliyoezekwa kwa nyasi!
"Simama kwanza!",alisema yule binti Kisha akashuka kwenye baiskeli!
"Scola atakuwa paleeee kwenye ile nyumba Ila kama ni mpenzi wako usiende Ila kama kweli una shida naye nyingine nenda,mi naondoka kwaheri!"
Alisema binti yule akiniacha njia panda,nilibaki najiuliza huyu binti ana maana gani kuniambia maneno yale!
"Kama ni mpenzi wako usiende Ila kama kweli una shida naye nyingine nenda!"
Maneno yale yalipita kichwani nikabaki njia panda!
Ila kwa jinsi nilivyokuwa natamani kumuona Scola unahisi nini kingenizuia hata malaika hasingeweza!
Nilisogea karibu nikapaki baiskeli yangu nikaanza kutembea kuelekea kwenye ile nyumba!!!
Ni nyumba iliyojitenga sana,haijachangamana na nyumba zingine!!
Nilifika kwa nje hakukuwa na mtu,ila kuna sauti zilisikika.
Japo sikuwa najua lolote kuhusu mapenzi nilijua zile sauti ni za watu wanafanya mapenzi!
INAENDELEA....

0 Comments