“Oooops!!! Makosa”, nilisema kwa nguvu mara baada ya yule msichana kuondoka. “Makosa gani”? aliuliza Sabrina. “Hawakutakiwa kujibu sisi ndo ilitakiwa tuwe tunawahi tu”. “Mimi hata sikuelewi mbinu zako leo ni ngeni kabisa”. “Utanielewa tu kazi nzuri ni baada ya kulewa na tutaanza kufanya utumbo hapa mpaka watadata”.
“Siunajuaa mimi nikiamua kucheza nacheza sehemu yoyote”. Mara niliamua ninyanyuka pale tulipokaa na kuelekea kaunta huku nikitembea kwa madaha na kutingisha tako moja la kushoto.Nilitaka kuwachanganya maana niliamini safari hii watakuwa makini kunifuatilia.
Nilinda mpaka pale kaunta nikauliza kama wanachai ya ipad yangu.Nilijua kabisa watakuwa hawana. Nikiwa hapo kaunta ikapigwa nyimbo moja hivi ya Rihana hapo nilishindwa kujizuia nilicheza kidogo kuashiria kuwa wimbo huo nilikuwa naupenda sana.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Basi niliamua kurudi ile sehemu ambayo nilikuwa nimekaa na niliowapita wale vijana walishindwa kuvumilia waliniita.“Mambo mrembo inaelekea unajua sana kucheza hasa miziki ya nje”. “Kawaida jamani leo nipo na raha na huwa siwezi kujizuia”. “Raha ya nini tena jamani”.
“Raha ya kuja Tanzania ujue Marekani na penyewe panachosha sana”. “Alafu mbona mpo wenyewe mda mrefu tunaweza kujinga pamoja?”.Alichomekea kuoma kampani kijanja. “Tena itakuwa vizuri karibuni”, niliwajibu na kaunza kuondoka kwa mwendo wangu ule wa kuwaamsha waliolala.
Niliondoka kwa madaha yote jambo ambao nilijua huko nyuma lazima watu watadindisha tu wenyewe. Nilimkuta Sabriana akiwa ameshika mdomo hasiamini kile ambacho nilikifanya kwa mda huo mfupi maana ilikuwa ni kitendo cha kijasiri sana. “Wewe ni kiboko weka mbali na watoto”Sabrina aliatamka maneno hayo mara baada ya kuona wale vijana wakiomba muhudu anyanyue vivywaji vyao ili waje waburudike nao.
Walikuja pale kwa mbwembe huku wakioneka ni wazi walianza kulewa. Kweli mjini ni shule maana nilishaenda kozi ya kiingereza hivyo nilikuwa na swaga za kizungu.Maneno mawili ya Kiswahili maneno mawili ya kiingereza utanitaka sasa. Kampani ikawa kubwa na walianza wenyewe kujitambulisha na kueleza kuwa wao ni wafanyabiashara wa madini.
Mimi sikutaka mbwembwe niliwaeleza kuwa ni mwanafunzi lakini nasoma Marekani hapo nimekuja tu kwa sababu nipo likizo fupi. “Eeeeeh mpaka likizo fupi wewe unakuja huku alidakia kijana mwingine”. “Yeeah nikiwamiss marafiki zangu kama hawa lazima nije.
Na huwezi amini nimekuja kisiri hata Dady hajui”.Yaani akijua nipo Tanzania kinyemela anaweza hata kuniua”.Tukagonga cheers na kuendelea kupiga story za hapa na pale na Sabrina nilimtambulisha kama rafiki yangu naye ni mwanafunzi wa chuo kikuu Dar es Salaam.Basi tuliendelea kunywa huku sasa tukianz akulewa na kufanya story zinoge.
Baadaye mimi nilikuwa nakata mauno hapo hapo kwa chini nakuwafanya wapagawe.Mara kuna mda nilisimama na kaunza kucheza huku nikipiga nduru kuonesha kuwa nilikuwa napenda sana mziki. Alafu nlivyokuwa mjanja nilikuwa nategeategea zile nyimbo za nje ya nchi ndo nilicheza.
Baadaye Sabrina alitoa wazo kuwa kwa nini tusiingie club maana aliona kuwa nilikuwa na nyege za mziki. Wale jamaa walikuwa hawana kipingamizi hivyo tuliingia club. Haya ndo makoso makumbwa waliyoyafanya maana waliruhsu kuonesha ubora wangu na maana halisi ya kutengeza hips na malaio yangu.
Yale mazoezi hayakuwa ya bue jamani. Yani nilikuwa nanyambulikanyambulika mtoto kiuno kama hakina mfupa nyonga zinajizungusha kama feni walidata wakadatika. Yule bwana ambaye ndo alikwua ni target nilihakikisha kuwa nambana vizuri mpaka aombe mwenye kwenda kulala na mimi.
“Ulisema kuwa umechukua chumba kwenye ile hoteli ya…. nilihitaja sehemu ambayo walipofikia.Alishaingia laini huyu nikamwambia ndio tena itabid tukalale na rafiki yangu huyo maana mimi naogopa kulula mwenyewe. “Yule jamaa akapima maji kwa kuuliza kwa nini nisiende kulala naye na rafki yake akalala na rafii yangu.
SikujIbu swali hilo nilipotezea na kumtia hofu.
Wakati tukiendelea kucheza nilipata wazo kuwa nitumie mbinu ya kuondoka naye. Hpo tayari zile dawa za kulevya nilishakabidhiwa na Sabrina na nliziweka kwenye mkoba wangu.
Hakutaka kupoteza mda sana nilitegea mtu fulani hivi ambaye hata simjui alipoingia tu Club nilikimbia na kwenda kujificha mahali.Jamaa alinifata na kuuliza mbona nimekimbia ghafla. Nilimjibu kuwa kuna mtu aliyeingia amechafua hali ya hewa. Nilmiwammbia kuwa huyo aliyeingia ni kaka yangu hivyo tafadhali anisaidie hilo koti lake nijifunike alafu niondoke eneo hilo.
“Tafadhali nisaidie hilo koti maana akijua nipo hapa ni hatari sana ni mkorofi sana kaka yangu huyu”. Jamaa akaingia upepo akatoa koti na kunifunika. Ila kabla hajanipa lile koti kuna vitu alivitoa kwenye hilo koti na kuviweka kwenye mfuko wake wa suruali.
Hapo nikajua tu ndo hayo madini aliyokuwa akisema Sabrina. Basi nilimshika mkono na nilianza kupiga hatua ili tutoke nje. Pale mlangoni ilibidi watupishe tu maana ilionekana kuwa kama kuna tatizo limetokea. Tulivyofika nje niliita tax jambo lilofanya anizuie na kusema ngoja atanipeleka.
Tukasogea sehemu ambayo alikuwa amepaki gari yake tukaingia na safari ikaanza. Sasa nikawa nawasiliana na Sabrina kwa njia ya sms kumwambia kuwa nikifika pale nitajifanya nimesahu funguo hivyo tutaingia kwenye hicho chumba cha huyo mwanaume.
Kweli tulivyofika kwenye ile hotel tayari dada wa reception alipewa maelekezo na jinsi mimi nitakavyokuwa. Swali la kwanza kumuliza ni chumba namba ngapi dada akanjibu namba sita kwani si uliondoka na funguo.Hapo nikajifanya kuanza kujisachi kwenye pochi yangu.
“Ooh My God itakuwa nimemwachia yule rafiki yangu”. Nilianza kupigapiga miguu kuonesha kama nimechanganyikiwa vile. “Dada usipaniki twende chumbani kwangu alafu wakija wewe utarudi” alitoa wazo la busara kaka huyo. Kimoyo moyo nilisema tayari kashaingia King.
Basi tulipandisha ngazi na kwenda kwenye hicho chumba chao. Nilivyofika tu nilivua viatu vyangu huku nikilalamika kuwa ni joto sana. “Yaani ukikaa ulaya siku ukija Bongo unaweza hata kutamani kukaa uchi jinsi kulivyokuwa na joto” nilisema huku nikitafuta mbinu ya kuchojoa nguo zangu.
Nikafanya kama nakivua kile kinguo changu. Nikasimama na kumwambia joto limenishinda nataka kuoga. “Kuwa na amani wewe ingia kuoga tu au unaniogopa mimi”. “Sikuogopi kwani unang’ata nikampa ishara kuwa anisadie kufungua zipu huko mgongoni.
INAENDELEA
0 Comments