Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Responsive Advertisement

Simulizi: Uchawi wa mama mkwe sehemu ya pili (02)

 


Usione nipo hivi, nimechukia sana kuona unafahamu siri yetu rejareja, jaribu kumuambia mumeo uone. Umesikia?" Sikumjibu neno badala yake nilikuwa namuangalia kwa kumshangaa mama kwa kuendekeza uchawi.

Akaendelea. "Nilikuwa nakusikiliza kwa makini sana ulipokuwa chumbani na mume wangu lakini nilifurahi kuona kuwa hukumuambia mumeo ambaye ni mwanangu yale mambo ya usiku. Endelea kuficha siri." 


"UNAJUA mume wangu kichwa ambacho kimeniuma asubuhi kilikuwa cha ajabu sana. Nilikuwa nahisi kama kuna mtu ana nyundo ananigonga kichwani, nikajikuta nikilia," nilimdanganya.


"Pole sana, unajua wakati mwingine uwe unajikaza kulialia namna ile kama mwenzako ana presha anaweza kuanguka, ukampoteza."

"Pole sana, sikuwa na nia ya kukushitua ni maumivu tu ya mwili yalinifanya niwe vile."


Kimya kilipita huku wote tukiwa kitandani na baada ya dakika kama kumi na tano hivi nilimsikia mume wangu akikoroma.

Niliinuka kitandani hadi kwenye mlango na kuhakikisha kuwa umefungwa kwa ufunguo. Nilifanya hivyo ili kudhibiti wale waliokuja jana usiku bila taarifa.


Mimi nilichelewa sana kupata usingizi kutokana na kuwaza hili na lile kuhusiana na tabia mbaya ya uchawi ya mama mkwe.

Hata hivyo, usingizi hauna adabu, nilijishitukia nikiwa nimelala fofofo na baada ya hapo sikujua kilichoendelea hadi saa tisa usiku niliposhituka baada ya kuona mtu kanishika kichwani.


Nilipofumbua macho nilimuona mama mkwe akiwa chumbani kwetu akiwa mbele yangu. Nilitamani kupiga yowe lakini nilishindwa. Ni kwamba mwili ulikuwa unataka kufanya hivyo lakini nikawa sina nguvu hata ile ya kujitikisa.


Nilipigwa na butwaa na kujiuliza maswali mengi bila majibu. Huyu mama kaingiaje? Mbona mlango nilikuwa nimefunga kwa funguo?'

Yeye alikuwa akiniangalia huku akiwa ameweka kidole kimoja mdomoni ishara ya kuniambia kuwa nisiseme kitu nibaki nimetulia. Lakini haraka sana nilifumba mambo na akawa ananipigapiga kofi kwenye mashavu yangu ili kuthibitisha kama nimelala kweli usingizi au nilikuwa macho.


Niliamua kujifanya nimelala usingizi ili nione alichotaka kufanya. Alipanda kitandani na akawa anatutambuka mmoja baada ya mwingine. Kati ya mimi na mume wangu, alitutenganisha kwa kuweka nafasi katikati yetu kwa kuwa kitanda chetu kilikuwa kipana sana cha sita kwa sita.


Baadaye alipuliza tunguri yake na mara nje nikasikia upepo mkali ukivuma lakini ukaishia juu ya mabati ya nyumba yetu. Nilikosa amani kabisa. Nilifumba macho kwa nguvu sana kwa sababu mama mkwe alikuwa anashuka kitandani kupitia kichwani kwetu.


Nilimsikia akiimba nyimbo ambazo sikujua maana yake kwa sababu hazikuwa nyimbo za Kiswahili nadhani zilikuwa ni za kijini au kichawi. Kwa kuwa chumbani kulikuwa na mwanga hafifu kutokana na ukweli kwamba nilikuwa nimezima hata ile taa ya mwanga mdogo, sikujua kuwa mama mkwe alikuja chumbani mwetu akiwa na kijimfuko.


Nilikiona hicho kijimfuko baada ya yeye kuchuka chini na kukiinua na akawa anachakuachakua ndani. Alitoa kitu kirefu kama mkia wa taa, sikujua anataka kuufanyia nini na mwanga wa taa za nje ulinisaidia kuona kila alichokuwa akikifanya.

Nilihisi kuwa inawezekana ule siyo mkia wa taa bali ni kamba na hakuna ajabu kama ataamua kuitumia kuninyonga nayo.


Nilikuwa na hofu hiyo kwa sababu aliahidi mchana mara mbili kuwa kama mambo yake ya uchawi nitamjulisha mume wangu ambaye ndiye mwanaye, ataniua na mwili wangu kuufanya nyama ambayo ataila!


Mbaya zaidi ni kwamba sikuwa na uwezo wa kupiga yowe au kutumia nguvu ili asinifunge shingoni na kitu kile kama mkia wa taa. Hata hivyo, tofauti na mawazo yangu, aliinua ule mkia na kunitandika nao makalioni pwaa. Dakika hiyohiyo nikawa nakosa nguvu hata ya kufumbua macho.

Niliyalazimisha kuona nikafanikiwa japokuwa yalikuwa yamefunguka kidogo sana kutokana na kichapo cha mkia ule.


SOMA HAPA 👉KANUNI 365 ZA KUFANIKIWA KIMAISHA 


ITAENDELEA

Post a Comment

0 Comments