IMEANDIKWA NA : EDGAR MBOGO
*********************************************************************************
Kijana Prosper alikuwa amejilaza kwenye mkeka, akipunga upepo wa na kufaidi kimvuri cha mti wa mwembe dodo mkubwa sana, uliopo pembeni ya kibanda kidogo cha bati,( full suit), ambao kwa kipindi hiki cha mwezi wa kumi na mbili, uwa unadosha sana maembe, hivyo kumfanya awe na tahadhari nyingi sana pale chini ya mwembe dodo, huku ana waza mambo mengi sana juu ya maisha yake ya sasa na ya baadae, “ukweli ujinga siyo kipaji, ujinga nitaaluma ambayo mtu ujivunza kwa juhudi kubwa sana” aliwaza Prosper au Pross kama wenzake walivyo penda kumwita, asa wakati yupo shule, “hakika usiyo yafanya utotoni utakuja kuya fanya ukubwani” aliendelea kuwaza Prosper, huku akitazama juu kwenye mti huu uliostawi na kuzaa maembe mengi sana, ukiwa ni mmoja kati ya miembe kadhaa iliyopo kwenye eneo ili la shamba kubwa sana, lenye mazao mengi sana, ikiwepo minazi ambayo ilikuwa nusu ya shamba, ndizi michungwa mipapai na matunda mengine, pamoja na viazi vitamu na mihogo ambayo Pross aliipanda mwenyewe nje na maataba wa mwenye shamba, yeye akiwa kama mlinzi na mfanyakazi wa shamba ili, ambae nikama aliuzwa au alikabidhiwa kwa mmiliki mpya wa shamba ili ambae ni bwana Shinyangwe, toka kwa mmiliki wa zamani wa shamba ili, alie linunua mwezi mmoja uliopita.
Huyu mmili mpya alikuwa ni bwana Vitus Kipanta, mzee wa miaka hamsini na nane, askari mstaafu wa Jeshi la ulinzi, alie staafu akiwa na cheo cha nyota tatu, ukweli bwana Vitus Kipanta alimkumbusha machungu makubwa sana Prosper, mwenye miaka 22, machungu ambayo yalisababishwa na aba yake ambae alikuwa ni askari mstaafu wa jeshi la polisi, ambae mala baada ya kustaafu, na kulipwa mafao yake akaondoka na kuwaacha wakina Pross, kwenye nyumba ya serikali, (quarters) za polisi maeneo ya Mivinjeni, kipindi Pross akiwa amebakiza miezi mtatu kumaliza kidato cha sita, na bahati mbaya au nzuri, Pross alikuwa anaishi na mama wa kambo, yani wa kufikia, kwahiyo mke alie telekezwa na bwana Feruz, siyo mama mzazi wa Pross,
Na ukweli toka baba yao bwana wana Vitus Feruz aiache familia yake ya mke ambae na watoto watatu yani Pross ambae ndie mkubwa, na wadogo zake wawili aliochangia baba, yani watoto wa wili, wa mama huyu, alie mlea Pross, toka Pross akiwa na miaka kumi na tano, yani kidato cha pili, ambo ni wawili tu! mmoja akiwa wakike ambae alikuwa mdogo kabisa, na kwa sasa alikuwa darasa la sita, na kaka yake ambae sasa alikuwa kidato cha tatu, ukiachia watoto wa bwana Feruzi walio telekezwa, pia kulikuwa na mdogo wa mke wa bwana Feruzi, ambae wakina Pross umwita mama mdogo, huyu nae alikuwa na miezi michache hapa nyumbani kwa Feruzi, akitokea kijijini kwao Iringa.
Pross akiwa katika kumbukumbu ya machungu, anakumbuka kuwa baba yake ambae alimtoa kijijini kwa mama yake, alie wai kuwa mpenzi wake, na kumpatia ujauzito ambao alizaliwa yeye, kwa ahadi ya ndoa, iliyo potea, baada ya kukutana na mama huyu mwingine, Pross alikumbuka siku ambayo alikuwa likizo yake ya mwisho kabla ya kwenda kwenye mitihani, ambapo baba yao aliondoka nyumbani akisema anaenda kuangalia kama fedha zake zamafao zimeingia kwenye account yake, na kurudi siku ya pili mida ya saa sita mchana, akionekana wazi kuwa alikuwa amechoka kwa pombe na starehe, lakini Pross na wadogo zake, walifurahi sana, kumwona baba yao, wakijuwa kuwa, ata kuwa amekuja na mambo mazuri, lakini aikuwa hivyo maana baba na mama yao wakajifungia chumbani na kuanza kulumbana, hapo ndipo Pross ambae alikuwa ana umri wa miaka kumi na tisa, ambayo ilitosha kuelewa kinacho endelea, aka ng’amua mapema sana kuwa kulikuwa na ugomvi mkubwa sana, kati ya baba yake na mama yake wakambo, na akaja kuli thibitisha ilo, jioni ambapo baba yake aliondoka kama vile anaenda kutembea, na akurudi tena, ata wiki ilikatika, huku maisha yao yakianza kuwa magumu, maana awakuwa na kipato kingine zaidi ya kumtegemea baba yao, na walikuwa awakopesheki , sababu kila mwenye duka aliamini kuwa aadda ya kulipwa mafao yake bwana Feruzi, angeondoka muda wowote toka pale kwenye nyumba za Polisi, za Mivinjeni, na kupisha askari wengine katika nyumba ile, ya serikali, lakini mwokozi wao akawa mama mdogo, ambae alikuwa ana pewa ela na mwanaume mmoja ambae alikuwa ni askari pale line polisi, lakini pia alikuwa mume wa mtu.
Maisha yakazidi kuwa magumu kwa upande wa familia hii, huku wakimsikia mama yao akilalamika kuwa, kuna habari nyingi mtaani, kuwa baba yao anaonekana mitaa ya Kigamomboni huko Tuamoyo, akishinda na kura raha na mschana mmoja, ambae mwanzo mama yake akuwa anamjuwa, lakini japo akuwa na wasi wasi juu ya mama huyu wakambo ambae alimwonyesha upendo kama vile mwanae, ila Pross akaamua kwenda kigamboni kumtafuta baba yake, alitoka asubuhi na mapema, na kuanza kumsaka baba yake.
Kwa hakiri za kitoto, Pross alisaka kwenye mitaa akizunguka Tuamoyo nzima, mpaka uwanja wa swala kiiukia PCOL, na kufwata barabara ya mikadi, na alipoona ame kosea akarudi tena uwanja wa maputok akinyoosha mpaka karibu na kambi ya Jeshi, kisha akarudi tena Tuamoyo kwa kutumia chochoro za mitaa, huku akinunu amaji, na vitafunwa kama karanga, na vinginevyo, kiasi kwamba mpaka saa kumi jioni, Prosper alikuwa amejikuta maeneo ya CCM, ajuwi la kufanya na akuwa ata na nauri ya kurudia kwao Mivinjeni, “nitafanya nini” alijiuliza Pross, huku akitazama maduka na bar ndogo ndogo, zilizopo pembezoni mwa ukumbi wa CCM, ungesema anatazama kama ange mwona mtu ambae anaweza kuwa anamfahamu akamwombe nauri.
Kwahakika kama unge mwona Prosper kwa wakati huo, unge gundua mala moja kuwa kijana huyu alikuwa amechoka sana, kwa mwendo wa kutwa nzima, tena kwenye juwa kali, maana uso ulimpauka huyu kijana ambae urefu wake wa wastani, na mpata kidogo, alionekana kubonyea mgongo, kama vile anakibiongo, kwa jinsi alivyochoka, na miguu yake ambayo alikuwa amevaa viatu vya chini, vya mikanda, yani sendo, ilikuwa imechafuka vumi, kama ingekuwa kule kusini kwa wamwela, tungesema ametoka kucheza ngoma za wakati wa unyago.
Kijana akuwa na lakufanya, akaamua kuanza kutembea taratibu, kuelekea kivukoni, huku akiwaza atatoa wapi shilingi mia ya kuvukia, kwenye pantone, maana aliamini kitu ambacho akiwezi ni kuogelea tena kwa umbali mrefu kama ule wa kutoka kigamboni mpaka magogoni, lakini kama atafanikiwa kuvuka, anauwezo wa kutembea kwa mguu mpaka Mivinjeni, ata kama akifika kesho hiyo isinge sumbua, cha msingi ni kwamba avuke kwanza.
Bahati ilikuwa upande wa Prosper, nasema Bahati sababu alifanikisha lengo la safari yake, maana wakati Pross ana maliza kulivuka jengo la ukimbi wa CCM, akaiona bar moja ndogo, ambayo ilikuwa na watu wachache sana, na watu hao kwa mtazamo wa haraka walikuwa katika meza mbili, kama wateja, na ukiondoa wahudumu na mchoma chips, kulikuwa na mwanaume mmoja na wanawake sita, waliokaa kwenye meza mbili zilizo ungwa pamoja, na kuonekana kama meza moja ndefu, wakiwa wamevalia vinguo ambazo ziliwatamulisha kuwa ni wanawake wa aina gani, maana kama siyo fupi, basin i nyepesi na iliyo ana, na kuchora maungo yao.
Meza zile zilikuwa zime tapakaa vinywaji, navyo vikiwa ni pombe tupu, ambazo kwa haraka Pross akujuwa gharama ya pombe zile, lakini kwa mimi kama mwandishi na kwa maelezo ya Pross kichwa cha bei ya chini ilikuwa ni win flani ya box, iliyo kuwa inauzwa shilingi elfu saba kwa mwaka ule wa 2009, vingine vilionekana kuwa vya gharama ya juu zaidi, pamoja na sahani zilizo nona kwa vyakula tena akukuwa na nyama ya ng’ombe, ni ndizi choma kwa nyama ya kuku.
Mwanzo Prosper akumwona kwa sura yule mwanaume, sababu alikuwa amemgeuzia mgongo, kwa ukaaji wake, lakini aliweza kuziona sura za wanawake walio mzunguka, ambao walikuwa wana kunywa na kula, wakicheka kwa furaha, huku mmoja wa wachana wale, muda wote akimfanyia michezo ya kimahaba, bila kujari kuwa ilikuwa saa kumi jioni, na ile sehemu ni barabarani, ukweli Prosper alihisi kengere ya tahadhari ikigonga kichwani mwake asa baada ya kugundua kuwa wale waschana anao waona mbele yake anawafahamu, tena walikuwa wanatoka maeneo ya karibu na makazi ya askari wa jeshi la polisi, ni wadada flani ambao sifa zao siyo nzuri sana, pale mtaani, ni wadada ambao mala nyingi akiwa anarudi toka shule uwa anawaona kwenye vibar vya mtaani kwao wakiwa wanakunywa pombe na wanaume tofauti tofauti, sijuwi kwanini aliingiwa na wasi wasi mkuwa kwa kuwaona wale wanawake, lakini akapata wazo la kwenda kuwaomba wamsaidie nauri ya kufikia Mivinjeni, maana akuwa na njia nyingine, na aliamini kuwa uwepo wa wanawake wale ambao kwamwonekano siyo wanawake wa mchezo mchezo, ambao wakikutia mkononi, lazima uuze mpaka nguo ya ndani.
Prosper alipiga moyo konde na kusogea pale kwenye bar, “shikamo” alisalimia Prosper, mala baada ya kuifikia sehemu lengwa, wote saba wakamtazama Prosper ambae alikuwa amemkazia macho mmoja wa wanawake wale, lakini alishangaa kuona sura za wana wake awa zikibadirika toka kwenye vicheko na kukunja midomo kama vile wamemwona hasidi, au fisadi, “we! Pross, ume fwata nini huku?” alikuwa ni sauti ya kiume iliyo jaa mshangao wa kilevi, Prosper alie itambua ile sauti mala moja kuwa, akamtazama yule mzee, na alipo hakikisha kuwa ni baba yake kweli, kama alivyo isikia ile sauti yake, Pross akatabasamu,………
Akijuwa kuwa amesha mpata baba yake na safari ya nyumbani itaanza, ikiwa ni mwanzo wa kumaliza shida zao, “inamaana mama yako amekutuma uni fwatilie?” aliuliza mzee Feruz, kwa sauti ile ile ya mshangao wakilevi, “hapana baba, mimi mwenyewe ndio nilikuwa na kutafuta” alisema Prosper, kwa sauti ya furaha, “ulikuwa unanitafuta, kwani mimi nime potea, aya rudi nyumbani nitakuja huko huko” alisema bwana Vitus Feruz, yani baba yake Pross, huku wale waschana wakiwa wametulia kimya wakimkazia macho Pross, na kumkunjia midomo, kwa kum’beza.
Licha ya kuambiwa hivyo lakini Pross akaonekana kuganda pale pale, huku akimtazama baba yake kama vile anatamani kumweleza kitu, “wewe si umeamiwa uende, kwani umeona hii ndio sehemu ya kuongea na baba yako?” alisema yule mschana alie kaa karibu na bwana Feruzi, ambae Pross mwenyewe alishawai kummwona mala nyingi akiwa na wanaume tofauti, kule mivinjeni, “sina nauri” alisema Pross kwa sauti ya chini iliyo jaa aibu flani, “hooo! kumbe, sasa usinge niona unge rudije nyumbani?” aliuliza bwana Feruzi, huku anaingiza mkono kwenye mfuko wa nyuma wa suruali yake, na kutoa noti ya shirini elfu kumi, kisha akanyoosha mkono kumpatia Pross, lakini yule mschana alie kaa karibu na Feruzi akaidaka, “yani beby una wafundisha watoto vibaya, ela yote hii ya nauri?” alsema yule mschana kwa sauti ya kudeka, huku anachukuwa pochi yake na kuifungua, kisha akaiweka ile noti ya elfu kumi, na kuanza kuchambua chambua kwenye ile pochi, huku zikisikika sauti za cheke cheke zikigongana, “yani baby ukiendelea hivi, sijuwi kama utatamalizia kununua vifaa vya saloon” alisema yule mwanamke, ambae kiukweli ni kama wenzake tu! walionekana wazi kuwa ni wanawake ambao, awakuwa na huruma na fedha yay a mzee Feruzi yani baba yake Pross, kutokana na vitu vilivyo agizwa palemezani, mwisho yule mwanamke, akaibuka na chekecheke (coin) nne, tatu zikiwa za mia mbili mia mbili, na moja ya shilingi mia, kisha akampatia Pross,jumla yake zikiwa ni mia saba, “aya tangulia nyumbani, baba atakuja” alisema yule mwanamke mala baada ya kumpatia Pross shilingi mia saba mkononi mwake, “usimwambie mama yako ulicho kiona huku” alisisitiza bwana Vitus Feruz, kwa sauti ya kilevi, hapo Pross akaondoka zake kinyonge huku anazitazama zile fedha kwa uzuni kubwa, kwa mbali akisikia wale wanawake wakimsimanga baba yake, “yani we shemeji unavyo mwogopa huyo mkeo, kwani akiskia kuna nini, Didah siyupo” inamaana walimaanisha kuwa Didah ndio huyu alie mpatia Pross shilingi mia saba, “nani amwogope yeye mwenyewe ananijuwa, akizingiwa tu ndio kama hivi, anioni tena” Pross aliweza kumsikia vizuri baba yake, lakini yeye akujari akaendelea kutembea huku akiitazama ile mia saba, kwa uzuni.
Siyo kwamba zile ela azikutosha nauri, ya kufika Mivinjeni, hapana, zile fedha zilitosha nauri na chenji ingebakia kana mia tatu, lakini kilicho mfanya akose raha, ni kile anacho kifanya baba yake, maana wakati wao kule nyumbani wanateseka, yeye anaweza kukaa bar na kuwa nunulia wanawake wale, pombe na kuku, huku akisikia kuwa kuna saloon inafunguliwa, wanawake ambao walisha poteza thamani yao katika mtaa waliokuwa wanakaa, lakini kilicho mpa moyo ni kwamba baba yake alisema kuwa ata rudi nyumbani, kitu ambacho Pross alijaribu kujiuliza, ni kwamba kama wale wote ambao anafahamu fika kuwa wame toka kule Mvinjeni na kuja huku kigamboni, sasa mida kama hii ya jioni bado wanakunywa pombe nyingi kiasi kile, je watarudi Mivinjeni au watalala huko huko.
Saa mbili usiku ndio mida ambayo Pross alifika nyumbani kwao, na kukuta wenzake wamesha maliza kula, japo chakula aliwekewa ila kilikuwa ni kidogo, siyo kwamba walimfanyia makusudi, ila ukweli ni kwamba ata wenzake walikuwala moja tu, asubhi ilipita kavu, mchana ikapita kavu, usiku walikuwala tena chakula kidogo cha kunyang’anyana, kilicho mfanya Pross ajuwe kuwa wadogo zake awakushiba, ni pale alipowekewa chakula chake, akawaona wadogo zake bado wana kimendea, “vipi mwanangu baba yako umekutana nae, “aliuliza mama yake wakambo Pross, ambae kikawaida aliishi na Pross kama mwanae wa kumzaa, hapo Pross akawaza na kuwazua, kwamba akimficha na ikaja kugundulika kuwa alikutana nae, itamfanya atengeneze uadui na mama yake huyu, ambae amemlea kwa upendo mkubwa sana kuliko ata mama yake mzazi kule kijijini, “nime kutana nae, amesema nitangulie nyumbani atakuja” alisema Pross, ambae baada ya kuona wadogo zake wanamendea sahani yake, akawakaribisha wale kwapamoja, japo ilikuwa ni mikono miwili sahani nyeupe, “umemkuta anafanya nini?” aliuliza mama Pross, “nime mkuta anakunywa pombe, ila amesema atakuja” ilo Pross akujiuliza kabla ya kujibu, alilifyetua kama lilivyo, “mh! hapa tujipange, maana sidhani kama atarudi” alisema mama huyu ambae sasa alizidi kuwa mnyonge, na kupungua mwili kwamateso ya maisha, maana alivumilia kipindi mumewake anasubiri mfao yake, lakini ameyapata ndio kwanza yana mkuta aya yakukikimbiwa.
Nikweli ilikuwa kukimbiwa, maana ilikatika week nyingine bila bwana Vitus Feruz kurudi nyumbani kwake, ambako aliacha mke na watoto wa tatu, na shemeji yake wa kike, huku akijuwa fika kuwa muda wowote familia yake itatolewa pale balax, na wasinge kuwa na sehemu ya kwenda, maana akuwa amejenga nyumba yoyote, katika kipindi chake cha utumishi wamiaka zaidi ya therasini, akiwa ndani ya jeshi la polisi.
Ikaongezeka week ya pili, huku familia ya bwana Feruz ikiishi kwa kumtegemea mama mdogo, ambae sasa alilazimika kuongeza idadi ya wanaume, ili familia ya dada yake iweze kuishi na yeye kupata maitajio yake muhimu, pamoja na nauri za wakina Pross wakati wa kwenda shule, mana tayari shule zilifunguliwa na bwana Feruz akuwa ameonekana tena, ata simu yake aikupatikana tena hewani, maana alisha izima, akutaka mazowea na familia yake.
Naam siku chache kabla uongozi wa jeshi la polisi, auja wataka kuhama kwenye ile nyumba, na kupisha askari wengine, ilikuwa jumamoss siku ambayo Pross uwa anaitumia kujisomea kwaajili ya mihatini yake ya mwisho, mama akamwambia Pross aende tena Kigamboni, kumsaka baba yake, maana alisha anza kusikia tetesi za kuondolewa pale kwenye makazi ya askari, sababu mume wake akuwa tena askari wa jeshi la polisi, hivyo waliitaji msaada wake.
Ukweli ni kwamba siku hiyo Pross aliangaika kigamboni nzima, safari hii akiulizia kwenye mabar na gorocer mana alikumbuka siku ya mwisho alimwona kwenye Bar, tena alianzia pale pale alipo mkuta, mala ya mwisho, ukweli nikwmaba kwa muda mfupi tu! baba yake alifahamika sana pale Kigamboni, maana kuna wakati ilibidi auliziae kwa wahudumu, wa bar, “yule mzee tupa tupa, ana kunywa na mademu flani hivi, mala ya mwisho alikuwa bar ya pale, kwenye kona” ndivyo alivyo jibiwa Prosper, mala kwa mala, na akila alipoenda sehemu aliyo elekezwa, aliambiwa, “huyu jamaa sija mwona kwa siku kadhaa” yani mpaka mida ya saa mbili Pross akuwa amemwona baba yake, hivyo akaamua kuondoka zake kurudi nyumbani, ambako alifika saa nne usiku, na kutoa report kwa mama yake, juu ya kukosekana kwa baba yake.
Na siku yapili Pross akaenda mtaa wa karibu, ambako mala nyingi alikuwa anamwona sana yule mwanamke anae itwa Didah, ambae ndie kama mpenzi wa baba yake, lakini licha ya kusaka kila kona na kuulizia kwa baaadhi ya watu akaambiwa kuwa mwanamke huyu na wenzake awakuwepo hapo mtaani kwa siku kadhaa, mala moja moja uonekana akileta vifaa vya saloon yake na kuondoka tena , “wale mademu inaonekana wameliotea jamaa wanalikamua kinoma” kuna mmoja aliongea kauri hiyo ambayo ilimuumiza sana Propss, sababu huyo jamaa anae kamuliwa ni baba yake, na wakati wao wanateseka.
Jumatatu ndio siku ambayo wakina Pross walitakiwa kuhama pale nyumbani, sababu jioni wakati wanatoka shule na kufika pale nyumbani, wakakuta tayari vitu vyao vipo nje, na wanatakiwa waondoke, wakina Pross awakumkuta mama yao mdogo, ambapo mama yao aliwaambia kuwa wanamsubiri yeye ili wajuwe wanaenda kuishi wapi, maana yeye ndie alikuwa kama mkombozi wao kwa siku hizi za karibu.
Saa tatu usiku ndio muda ambao mama mdogo wao alipokuja na gari dogo la mizigo, wengi wanaita kilikoou, tukaanza kupakiza mizigo, ambayo ilienea kwenye gari lile, na tukapata nafasi ya kukaa na sisi, hakika usinge weza kuamini, kwa mtu alie fanya kazi kwa mika therathini , vyombo vyake vya ndani yani feniture zake zote, zikae kwenye kigari kidogo kama hiki, na zinatosha vizuri, na nafasi nyingine ibakia.
Safar ikaanza kuelekea sehemu ambayo mwanzo awakuwa wanaielewa zaidi ya mama yao mdogo pekee, walikamata barabara ya mandela kabla ya kukata kushoto baada ya kufika tazara kiisha wakaelekea ukonga, na hapa majumba sita wakakata kulia kueleka tabata, mpaka kinyelezi, alafu waka ifwata ile barabara ya maealamba mawili, na kwenda kutokea mbezi, alafu wakaifwata barabara ya morogoro, mwisho wake wakaishia Kibamba hospital, na kuingia upande wa kushoto, ambako walienda kama kilomita nne hivi, ndipo safari yao ikaishia mbele ya kijumba kimoja cha mabati, kilicho jengwa pembezoni mwa eneo la Hospital ya muhimbili (MUHAS) ikiwa ni kwenye mpaka baina ya makazi ya wananchi na eneo la serikali. …
“dada nazani wakati unamtafuta shemeji tuishi kwanza hapa” alisema mama mdogo, na hapo ndipo wakina Pross walipoanza kuelewa nini kinaendelea, katika maisha yao mapya, nadani ya kijumba hiki ambacho mama yao mdogo alikabidhwa na mtu mmoja, alie hama baada ya kupata sehemu nyingine.*******
Iliwalazimu wakina Pross kuzowea maisha yale, maana awakuwa na jinsi, kijumba kile ambacho kilikuwa na chumba kimoja na kijiukumbi kidogo, ikiwalazimu mama na mama mdogo kulala chumbani, huku Pross na wadogo zake wakilala pale sebuleni, huku akitumia siku za week end kulima lima nje ya kile kibanda chao, na kufanikiwa kupanda mboga mboga, ambazo mwanzo zilianza kuwasaidia wao wenyewe, na baadae wakawa wanakuja watu wengine kununua, na kuwa saidia wao kupata fedha ndogo ndogo za kununua chumvi sukari na mafuta ya kupikia, pia sabauni na nauri ya kuendea shuleni ambako kwa sasa nikama walikuwa wanasoma mbali sana, japo miezi michache baadae wakahama, na kuhamia shule za karibu.
Kwa upande wa Pross alifanikiwa kumaliza shule, yani kidato cha sita, huku matokeo yake yakija mabaya sana, maana yake alifeli, na kushindwa kuendelea, na masomo zaidi, sasa alishinda nyumbani, akianza kufanya kazi ndogo ndogo za kusaidia kwenye ujenzi, maana mtaa ule mpya ulikuwa na kazi nyingi za ujenzi, ukweli alisaidia sana pale nyummbani, sasa yeye na mama mdogo walikuwa wanategemewa, wote wawili, pia licha ya kujiusisha na kusaidia mafundi, lakini akuacha kulima mboga mboga, ambazo zilimpa ajira mama yake wakambo, ambae alikuwa anatembeza kwenye baadhi ya nyumba za wakazi wapale, ambao wengi wao walikuwa ni watu wenye uwezo kifedha, maana ata ukiyaona majumba yao unge juwa tu, kuwa watu wa huku siyo wa mchezo mchezo, majumba makubwa, nje magari kama siyo mawili basi matatu na kuendelea.******
INAENDELEA
INAENDELEA
0 Comments