" Naomba tuongee mambo kiume, sitotaka unidanganye kwa lolote"
"Sawa kaka"
"Kwanini umemlala mke wangu?"
"Ha.. ha .. hapana sio yeye kaka"
Dr mgweno alishtukia ngumi nzito ya kichwa na kuachia ukelele.
"Tulielewana tusidanganyane, niambie kwanini unatembea na mke wangu "
" Kaka mkeo amenitaka mwenyewe, angalia ni yeye mwenyewe amenipigia simu lelo"
"Una uhakika?"
" ndio kaka sidanganyi"
"Umemlala mara ngapi"
"Ni leo tu kaka"
"Una uhakika?"
"Sidanganyi kaka"
"Kwanini alikuwa anapiga sana makelele"
"Kaka mimi sijui ila wanawake wote niliolala nao huwa wanapiga makelele sana wanadai wanaumia"
"Kwanini wanaumia, huwa unawafanyaje"
"Wanasema eti nina naniliu kubwa"
Ansbert alitupa jicho lake kwenye sehemu za siri za Dr Mgweno na kuzitathmini.
"Hebu funua hilo taulo lako".
Dr mgweno alilifunua taulo lake na kumuonyesha Ansbert, Ansbert alishtuka na kushika mdomo.
"Haa yani hapo ndio imelala?"
"Ndio kaka"
"Sasa ikisimama inakuwaje?"
"Inakuwa kubwa zaidi"
"Mshenzi wewe paaaaa(kofi la uso) sitaki unijibu"
"Ina maana hilo dude lako lote umemuingizia mke wangu? Mungu wangu eeee"
Ansbert alishtuka sana kwani kusema ukweli Dr Mgweno alikuwa mlemavu wa maumbile, alikuwa na uume mkubwa mno na ndio maana wanawake wengi akishatembea nao mara moja hawarudi tena na mpaka wakati huo hajafanikiwa kupata mke wa kumuoa.
Ansbert alinyanyuka na kutoka taratibu ndani ya chumba huku akiwa na maumivu mengi moyoni mwake.
Aliingia kwenye chumba chake na kuchukua begi lake kwa ajili ya kuondoka, hasira zilikuwa zinamkaba sana kila alipokuwa anaondoka pale chumbani kwake.
Alipokuwa anakipita Chumba alichokuwa analalwa mkewe alijikuta hasira zikipanda mara dufu, aliamua kuingia tena lakini kabla hajaingia alitia mkono mfukoni na kutoa kitu flani.
Alikishika vizuri kisha akasukuma mlango na kuingia ndani. Wakti anaingia Dr Mgweno alikuwa bafuni anaoga.
Ansbert alikaa kitandani akimsubiri Dr Mgweno aje, Dr mgweno bila kujua lolote alitoka akiwa anajifuta maji usoni na taulo.
paa, paaa....Milio ya Risasi ilisikika huku Dr Mgweno akianguka chini kama mzigo.
Ansbert aliweka bunduki yake na kuondoka eneo la hii hoteli.
..................................
Rozina alikuwa chini ya dirisha kwa nje akisikiliza kila kitu kilichokuwa kinaendelea kule ndani.
Alitamani akimbie lakini hakuwa na namna kwani mazingira ya hii hoteli yalikuwa hayaruhusu, hakukuwa na njia ya kupitia kwa nyuma.
Alishtuka sana aliposikia milio ya Risasi akajua tayari Ansbert ameua.
Aliposikia hatua za mtu kuondoka akajua huyo ni Ansbert anaondoka.
Alichungulia Dirishani na kukuta mwili wa Dr mgweno ukiwa chini na unavuja damu.
Alichokifanya aliingia tena kupitia dirishani kisha akachukua vitu vyake na kuondoka huku akiwa na wasiwasi mwingi.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Roho ilimuuma sana kumuacha Dr Mgweno kwenye hali ile, alichokifanya alitafuta mtu mwenye simu kisha akaomba apige.
Alipopewa alipiga simu polisi na kuwajulisha kuwa kuna mtu amepigwa Risasi kwenye gesti fulani chumba fulani. kisha akamkabizi mwenye simu na kuondoka huku mwenye simu akiwa hajui kwamba simu ilipigwa wapi na kwa ajili gani.
............................................
Ansbert alikuwa kwenye gari yake akielekea Tanga Mkinga kwa akina Amina.
Alikuwa amechukua pesa nyingi sana kwenye akaunti yake na alidhamiria kukimbia kabisa jiji la Dar es salaa kwa kuhofia mkono wa dola.
Alifika kijiji cha Duga usiku na kumkuta Amina akiwa anasukwa na mwanamama mmoja.
Amina alishtuka sana baada ya kumuona Ansbert, alijikuta akiamka haraka na kumkimbilia kisha akamkumbatia.
Wakiwa wamekumbatiana alitokea Mama mmoja akiwa ameshika chupa yenye maji ndani ambayo yalionekana kama juisi ya ukwaju.
Amina dawa hii hapa, ukinywa leo tu kesho kila kitu kinakuwa kimeisha.
"Dawa ya nini hiyo Amina"
"Ya Kutoa Mimba, nina Mimba yako na nataka kuitoa."
"Haa usiitoe Amina, nataka kukuoa na nimekuja kukuchukua tuishi wote"
"Namkeo umemuachia nani"
"Ni stori ndefu ila nataka tuhamie Mombasa tukafanye bishara huko"
Njia nzima Rozina alikiwa analia chini chini, moyo wake ulikuwa kwenye maumivu makali sana ya kujutia.
Alijuta kufanya yale ambayo yamemfikisha hapo alipo, dhambi ya zinaa ilikuwa imesababisha mauti.
Alitamani siku zirudi nyuma ili asifanye kile alichokifanya lakini siku zote waswahili wanasema neno "Ninge" huja baada ya kukosea na "majuto siku zote ni mjukuu."
Kila alipokuwa anapita alikuwa amejaa hofu ya kukamatwa na polisi. Alikuwa na uhakika kuwa watu wa ile hoteli wanamfahamu sura yake kwani yeye ndie alienda kukodi chumba.
Japo jina aliandika la uongo kwenye daftari la mapokezi lakini sura yake ilionekana vyema.
Alikiwa anahaha, mara apande bajaji ya kuelekea kwake na kushuka njiani, alikuwa anaingia baa hii anatoka na kwenda nyingine alikosa kabisa amani ya moyo.
Kuna wakati lilimjia wazo la kujiua lakini aliogopa sana kufa ,kingine aliogopa kuhusu mwanae kuwa atapata shida.
Wazo la kwenda kwake alilipinga kwa asilimia zote akijua kuwa endapo atatafutwa basi watafutaji wataanzia kwake.
Alichokifanya alienda kwenye super market yake na kukutana na mhasibu ili ampe hela.
"Hans hebu nipe hela za mauzo ya wiki hii"
"Jamani bosi hata salam "
"Ah we nipe kwanza ninachotaka"
"Mbona baba kesha chukua kasema anaenda kuweka benki"
"Nini?"
Rozina hakuamini masikio yake, alienda moja kwa moja nyumbani huku akiingia kwa machale.
Alipofika alifungua kwenye kabati na kufungua droo ambayo Ansbert huwa anaweka fedha na nyaraka mbalimbali za benki.
Aliishia tu kushika kichwa kwani kulikuwa kweupe kabisa.
pona yake ni kwasababu alikuwa na akaunti yake binafsi japo haikuwa na hela nyingi sana.
Alichukua kadi yake akatoka mkuku mkuku huku akiwa amebeba vidani mbalimbali alivyokuwa ananunuliwa na mme wake kama zawadi kwa lengo la kwenda kuviuza.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Harakati zake zilifanikiwa na ndani ya muda mfupi tayari alikuwa na fedha ya kutosha mkononi.
………………
Polisi aliyekuwa mapokezi alipokea simu iliyomjulisha kitendo cha mauaji kilichofanyika kwenye moja ya hoteli zilizokuwepo pembeni kidogo ya mji.
Hoteli hii polisi waliifahamu sana kwani ilikuwa inamilikiwa na bosi wao wa mkoa kitengo cha uhasibu.
Wasingeweza kwenda kufanya upekuzi bila ya kumtaarifu kwanza mmiliki ambaye ni bosi wao.
"Bosi shkamoo"
"Marahaba Afande vipi"
"Safi, kuna taarifa ya mauaji imetufikia hapa kwamba kuna mtu ameuawa pale hotelini kwako"
"Taarifa ya lini hiyo"
"Imetufikia mda huu huu"
"Basi msifanye chochote, naenda mwenyewe huko"
Alichohofia Afande huyu ni kwamba endapo tukio lile litatangazwa litasababisha hoteli yake ikose soko kwani wateja wangebaini sio Sehemu salama.
Aliamua kulimaliza jambo hilo kimya kimya.
Kwakuwa alikiuwa na cheo kikubwa ,aliita askari kadhaa anaowaamini akawashikisha kitita kila mmoja kisha akawatuma kule hotelini.
Wahudumu wa hoteli walikuwa hawajui chochote kuhusu mauaji hadi pale walipoona askari wakitoka na mwili wa mtu anayevuja damu.
"Bosi wenu amesema taarifa hizi msiziseme kokote"
(Wahudumu walichimbwa mkwala)
Wakiwa kwenye gari walibaini kuwa yule jamaa aliyepigwa risasi hajafa ila amezimia tu kwasababu ya kuvuja damu sana.
Walimkimbiza Hospitali wakadai kuwa ni askari mwenzao amejeruhiwa wakati wanafanya mazoezi.
Dr Mgweno alitibiwa haraka haraka na kwa umakini mkubwa na ndani ya siku mbili akawa amepata fahamu na mkono wake ukiwa umefungwa P.O.P.O kubwa baada ya kufanyiwa upasuaji wa kutoa risasi chini ya bega.
Alipopona vyema na kupata uwezo wa kutembea aliomba kutuhusiwa ili arudi kwake lakini alikataliwa kwa madai kuwa bosi wake amesema asiondoke kwanza.
Aliwaza sana kuwa ni bosi gani aliyetoa amri bila kujua kuwa pale ametambulishwa kama yeye ni afande.
"Afande unajisikiaje?"
Dr Mgweno alishangaa sana kuitwa afande akabaki ametoa macho tu.
"Afande unajisikiaje?"
""Unaongea na mimi?""
"ndio kwani kuna Afande mwingine hapa?"
"Mbona mimi sio afande"
"Mimi ni Dokta"
Madakatari walishangaa yale majibu na kunongo'nezana kuwa mgonjwa wao atakuwa amepata tatizo la akili.
Ndani ya muda mfupi waliingia ma askari watatu wakiongozana na yule Askari Mkuu ambapo waliwaomba madaktari wawapishe kidogo.
Walianza kumhoji Dr Mgweno kuhusu jina lake mpaka kazi yake.
Walimhoji pia kuwa ni nini kilisababosha apigwe Risasi na hakusita kueleza ukweli wote.
"Sasa sikiliza, swala hili liwe siri yenu na kamwe usije ukadiriki kwenda na wake za watu kwenye hoteli yangu sawa?"
"Sawa afande"
"Kingine nataka unilipe gharama zangu za matibabu yako, sawa?"
"Sawa afande naomba unipeleke ofisini kwangu nikakulipe"
Waliingizana kwenye gari mpaka dukani kwa Dr Mgweno, walipofika walishuka na kuingia ndani.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Wale askari walishangaa kumuona Dr Mgweno akisalimiwa kwa adabu mno huku wakimuita bosi.
"Hii ni ofisi yako mwenyewe?"
"Ndio afande"
"Kwahiyo wewe ndio Dr Mgweno"
"Ndio mimi"
Wale askari walishangaa sana, hawakutarajia kuwa kwa muonekano wa Dr Mgweno anaweza akawa anamiliki duka kubwa la dawa kama lile ambalo ni maarufu mji mzima huku yeye mwenyewe akiwa daktari bingwa.
Muonekano wa Dr Mgweno ulikuwa ukimhukumu mara kwa mara, alikuwa haendani na Sifa yake.
Mara nyingi amekuwa akiishia kupewa siti za nyuma mpaka anapotokea mtu anayemfahamu ndio anahamishiwa mbele.
Tangu siku hiyo Askari wale waligeuka marafiki wakubwa kwa Dr Mgweno, hata kazi zao za siri wakawa wanashirikiana.
………………
""Namshukuru Mungu kuwa niko hai na nimenusurika kufa kwa mara ya pili baada ya kujuana na wewe. ""
""Nakuomba usinijue na mimi sitakujua kwa lolote, tufanye kama hatujawahi kuonana hata siku moja. ""
"Nayapenda maisha yangu na sitotaka uyakatishe. Nitakachofanya nitamtafuta mme wako ili kwa hali na mali nimuombe msamaha ili niishi kwa amani. "
……Rozina akiwa hotelini huku akisubiria kusikia taarifa za msiba wa Dr mgweno alishangaa kupokea ujumbe ambao ulionekana umetoka kwa Dr Mgweno.
Hakuamini macho yake kuwa Dr Mgweno alikuwa hai.
Alijikuta akilipuka kwa furaha asiamini kuwa hajasababisha mauaji.
…Oooh Ahsante Mungu! (Alijisemea Rozina)
…………
Ansbert na Amina walikuwa kwenye mji wa Mombasa ambapo tayari alikuwa ameshapata nyumba ya kuishi na sasa walikuwa wanashughulikia kufungua biashara.
Alishtuka siku moja alipofungua e-mail yake na kukutana na ujumbe mzito na mrefu kutoka kwa Dr Mgweno akiomba msamaha wa yote aliyoyafanya.
Alistaajabu sana kwani ilikuwa sio rahisi kuamini kuwa kwa Risasi zile bado mtu anaweza akabaki hai.
Ndani ya moyo wake alijiskia amani sana kwa kuondokewa na mzigo wa kuua na tayari alishatangaza msamaha kwa Dr Mgweno.
Jambo ambalo lilifwatia kwenye akili yake ni mali zake alizoacha Tanzania.
Alipiga mahesabu ya nyumba zake nne, gari tatu, supermarket aliyomfungulia Rozina, mashamba manne ya ekari mia kila moja na kiasi cha fedha alizokopesha watu.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Kikubwa zaidi Ni Mwanae Maro ambaye alikuwa anasoma boarding. Alikuwa amemmisi sana na hakutaka hata siku moja mwanae aishi kwa shida.
"Nitamfwata nimchukue na kumhamishia huku, nitauza mali zangu zote na nitahamishia makazi yangu huku"
Baada ya wiki moja Ansbert alikuwa amefungua baa kubwa Mombasa kwa kununua nyumba nzuri kisha akaikarabati na kuitengeneza kuwa baa.
ITAENDELEA
0 Comments