"Mtumeee"
nilipiga kelele mikono nikaweka kichwani nilianza kulia kwa sauti, Rajabu
alikuja na kuniuliza vipi alijua nimezidiwa
"Lameck
jamanii Lameck, uwiiiii Lameck wangu umepatwa na nini wewe" aisee
asikwambie mtu nilikuwa kama chizi niliinuka nikafungua kabati la nguo na
kuanza kutoa natupa chini
"Wewe vipi
umechanganyikiwa au?" Rajabu aliniuliza
Sikumjibu nilikuwa
nikitafuta nguo gauni la heshima niweze kuvaa nitoke, nilipolipata nilivaa na
kutaka kutoka, Rajabu akaniwahi
"Embu niambie
kuna nin?"
"Lameck kafa!
kafa! kafa jamani ameniacha" nilijikuta naongea tu hapo nikaanza kuona
umuhimu wa Lameck nikatamani hata nimuone ili nimwambie yaishe nibaki nae
asife,
"Sasa unataka
kwenda wapi? Kwanza una uhakika gani kama kafa?"
"Nimeona
status niache niende kwao" nilifanya fujo, nilihisi kuchanganyikiwa kwa
wakati ule
"Nimeona
status niache niende kwao" nilifanya fujo hizo, nikachomoka na kuondoka
Nilifika hadi
alipokuwa akiishi Lameck nilikuta watu wamesharudi kuzika, yaani jamani usiombe
yakukute niliishiwa nguvu hata za kutembea, nilipiga magoti na kuanza kulia,
nilitamani kila kilichotokea kiwe ndoto niamke tu mwenzenu, kufiwa kunauma
kiukweli japo nilimkosea Lameck lakini kilio changu kilitoka moyoni, watu
walisogea na kunishika huku na huko, wakaniingiza ndani
Niliwaona wazazi
wake Lameck nao walinitambua kwani tulikuwa tukijuana kupitia picha, nilivyolia
ndo nilimfanya mama Lameck nae alie upya, nilimsogelea akanikumbatia
"Mwanangu
ajali imemchukua, alinipigia simu akaniambia mama njoeni Tanzania na baba
nataka kuoa kwa haraka msichelewe, kumbe ndo alikuwa anatuita ili tuje
kushuhudia kifo chake, ungetulia nyumbani basi mwanangu labda yasingekukuta,
Aisha yupo hapa umemuacha mwenyewe mke wako" yule mama aliongea kwa
masikitiko huku akilia, hapo nikatambua kuwa Lameck kafa kwa ajali hapo nami
nikazidi kulia
Basi
tulibembelezwa tukanyamaza, nilikuwa mpole sina hata raha nikajiinamia, mara
nilihisi mtu kanishika mkono niliinua uso na kumuona rafiki yake Lameck,
aliniinua tukaenda nje pembeni kabisa
"Pole kwa
msiba lakini hutakiwi kulia tena, Lameck ameshaenda ila tambua haya ni makosa
yako Aisha, nilionana na lameck mara ya mwisho baada ya kutoka kwako na
kuniambia yote uliyomfanyia, wewe sio wa kumfanyia vile ndugu yangu kiukweli
umemuumiza sana, aliniomba nikupigie simu nimsaidie kukubembereza lakini
hukupokea, akasema basi muache kama hataki, kisha akaniaga, saa saba usiku
napokea simu na kuambiwa Lameck amepata ajali mbaya, ni kwasababu yako"
Alinilaumu
nikaanza kulia na kurudi ndani kiukweli niliumia nikajiona nina hatia, sasa
nitafanya nini maji yamesha mwagika
Siku hiyo nililala
hapo hapo matanga yakaisha watu wakaondoka, nami niliwaaga wazazi wa Lameck
kuwa nae
"Sawa ila
tuna maongezi na wewe lakini ngoja kwanza tukae kikao cha familia kisha
nitakupigia simu uje" alisema baba Lameck basi niliaga walinipa na pesa
kidogo ambazo zilikuwa za rambirambi nikaondoka,
*******
Nilirudi nyumbani
nikiwa sipo sawa kivile, Rajabu alininunia baada ya kukaa kule msibani
"Ushatoka
kumzika bwana ako ukaona ukae wee mpaka mmalize 40 kabisa" alisema hivyo
kwa kunikejeli kwani nililala siku mbili tu, hivyo hata 40 haijajulikana
itakuwa lini
Sikumjibu kitu
niliingia bafuni nikaoga kisha nikachukua nguo nyingine na kuvaa, mara simu
yangu ikaita alikuwa mama Lameck nilipokea haraka na kumsikiliza
"Mwanangu
itabidi kesho uje tuongee, Lameck aliwahi kutuambia kuwa wewe ni mjamzito sasa
tushakaa kikao itabidi tuzungumze"
"Sawa mama
kesho nitakuja" nilimkubalia na nikapangiwa muda wa kwenda
Ilipofika siku ya
pili sikwenda kwani sikuona umuhimu ikiwa mimba nilishatoa kwanza niliwaza
nitaenda kusema nini, basi nilipigiwa simu sikupokea, nikamwambia Rajab kuwa
wazazi wa lameck wanataka waongee na mimi kuhusu mimba akasema hakuna kwenda
watumie msg waambie huna mimba, kiukweli sikutuma msg niliogopa
Zilipita siku
mbili nikabadilisha na laini ili kukwepa usumbufu wao, nikiwa nimekaa sebuleni mlango
uligongwa nilifungua na kumuona rafiki wa Lameck na wazazi wa Lameck nilishtuka
Zilipita siku
mbili nikabadilisha na laini ili kukwepa usumbufu wao, nikiwa nimekaa sebuleni
mlango uligongwa nilifungua na kumuona rafiki wa Lameck na wazazi wa Lameck
nilishtuka
Sikutaka kujua
wamepajuaje kwani yule shemeji yangu alipajua vizuri, niliwakaribisha na
kuwasalimia
"Aisha upo
sawa wewe?" Baba Lameck aliniuliza
"Ndio
baba"
"Tumepata
wasiwasi kwenye kikao hatujakuona, pia simu yako haipatikani, tukamuomba Denis
atulete kwako tulihisi una matatizo" mama Lameck aliongea kwa upole
"Simu yangu
imeharibika pia nilikuwa sipo sawa" nilijibu, wakati huo Rajabu alikuwa
chumbani anasikiliza kwani niliweza kuona kitasa cha mlango kikicheza lakini
baadae kikatulia, nilijua fika alitaka kutoka lakini katulia
"Sasa
mwanangu kama tulivyokwambia ile majuzi, taarifa kuhusu kuwa na mimba tunazo,
kwasasa wewe ndo faraja yetu pamoja na mtoto aliyekuwa tumboni, tumeona
tukuchukue ili twende wote London ukaishi huko, uangalie hali yako mpaka
utakapo jifungua" waliniambia hivyo, nilishtuka maana sikujua niwaambie
nini, nilitamani siku moja kwenda nchi kama hiyo lakini naona ndoto zimefifia
"Mbona kimya
kwani una hofu ya nini mkwe?" Aliuliza baba Lameck,
Mara Rajabu
alitoka na kusalimia
"Nimesikia
kila kitu mlichoongea huyu haendi popote ni mke wangu, alishachana muda na
mtoto wenu pia hiyo mimba ilishatoka kwahiyo muacheni" aliongea na
kuwafanya washtuke mimi nilihisi ganzi mwili mzima
"Anachokisema
ni kweli?" Mama aliuliza
"Wee mama
kwani huamini au? Haya nenda kampime kama utakuta mimba nendeni, kwanza inukeni
muondoke huyu mke wangu sitaki muongee nae" alisema na kunitaka mimi
niingie chumbani
Nilimuomba
asiwafokee watu wazima lakini hakuelewa, basi ikabidi wale waondoke na kuomba
samahani kwa usumbufu, walisema hawajajua kama mimi nimeolewa, walikuwa ni watu
wastaarabu na wapole nilijikuta nikiona aibu na makosa yote niliyabeba mimi,
walivyoondoka tu nikamsogelea Rajabu
"Kwa nini
huna adabu wewe, huoni kama umenidhalilisha? Unataka mimi niishi maisha gani,
kila mtu unataka anichukie?" Niliongea kwa hasira, basi hiyo siku
tuligombana sana,
Ulipita mwezi
mmoja tukiwa watupatani kivile, pale kodi iliisha akakataa kulipa nikatoa akiba
zangu na kulipia,
Siku moja nikiwa
napika, mara nilisikia, simu ya Rajabu ikiita nilishangaa kwanini haipokelewi
kumbe hakuwepo ila aliweka chaji, nilitoka na kwenda kupokea nikakuta
ilishakata, niliangalia na kukuta msg, jina habiba nikalikumbuka lile jina ni
mwanamke wake wa muda mrefu alitakaga kumuoa aliandika hivi
"Hupokei simu
kwanini mimi Nina shida na pesa nataka niende hospital"
Basi nikaingia na
shauku ya kusoma na msg za nyuma
"Mpaka sasa
mimba inaingia miezi sita hutaki kuja hata kuniona"
"Najua pia
natamani kukuona lakini huku namalizia nyumba yetu nikuchukue tukae wote usione
kama mimi sikujali" Rajabu alijibu hivyo
Huwezi amini
nilianza kutetemeka mikono, sikutaka kuendelea tena kusoma msg nyingine,
nilirudisha simu pale pale
Basi niliacha
kusoma ile msg na kukaa kwenye sofa, nilisikia harufu kama mboga inaungua
lakini sikuweza kwenda kuishughulikia nilikasirika haswa
"Wee Aisha
usikii kama mboga inaungua au?" Alisema Rajabu baada ya kuingia ndani
Nilikaa kimya
akanifuata na kuniuliza tena, nikampa bonge la Kofi
"Kwani kama
unasikia Mboga inaungua kwanini usiende kuiokoa, au mpaka niende mimi? Wewe
huwezi au umezoea kusumbua wenzio?" Nilimwambia kwa hasira huku nikimtolea
macho,
"Yaani
kukwambia mboga inaungua ndo unipige kofi?" Alijikuta nae akiniuliza kwa
hasira huku akiwa ameshika shavu ujue kofi la kushtukiza linauma jamani
"Sikia wee
Malaya wa kiume, nishajua kama umempa mimba huyo kenge wako, nimeona msg zote
unanifanya mimi mjinga eh? Hivi wewe unasahau nimekufanyia mangapi mimi? Mbona
huna fadhila wewe? Kukupenda kote nikakupa kila kitu alafu unanifanyia
ujinga" nilizidi kupandisha hasira
"Haya tufanye
ushajua ukweli kwahiyo unaamuaje tunaachana au?" Aliniukiza kwa dharau
nilikasirika nikataka kumpiga kofi tena akanidaka mkono
"Nitakupiga
usinione mimi fala nitakuvunja nalwambia" alisema na kunisukumiza kwenye
kiti
"Nataka
kuonana na huyo kahaba wako anatoa hiyo mimba?" Nilisema kwa hasira
akaanza kunicheka
"Wewe
umechanganyikiwa eeh mimi nimtoe mwanamke wangu mimba? Utanitafutia mtoto wewe?
Kwanza huna kizazi utanizaliaje?" Aliniambia
"Na ile mimba
uliyonitoa iliingiaje kama sina kizazi labda wewe ndo huna kizazi kwasababu
sikuwahi kubeba mimba yako hata siku moja" nilimwambia na mimi kwa
kumkashifu ili ajisikie vibaya, akacheka
"Pole sana
yaani wewe kuzaa sahau kabisa ushatoa mimba na kizazi ushatolewa chote kama
ulikuwa ujui ndo nakwambia na nilikuwa nakufichia siri ila leo ndo nakupa
ukweli maana jeuli" alivyosema hivyo nilishtuka sana nilipiga kelele na
kulia, nilianza kumtukana Rajabu akawa ananipiga alinipiga mpaka nilihisi
kuchanganyikiwa nilianza kupiga kelele nakufa mara nyingi, nguvu ziliniishia
kabisa sikujielewa tena
Jioni niliamka na
kujikuta nipo hospital pembeni yangu kulikuwa na wanawake wawili wamekaa na
mwanaume mmoja, nilipowaangalia nikagundua ni majirani zangu pale nilipopanga,
waliniambia kuwa walisikia kelele walipokuja ndo wakanikuta tayari nimezimia
Rajabu alitoka nje na beg lake la mgongoni akakimbia, mimi wakanipeleka
hospital
ITAENDELEA
CHOMBEZO-
NINGEFANYA NINI?
SEHEMU YA 31
Jioni niliamka na
kujikuta nipo hospital pembeni yangu kulikuwa na wanawake wawili wamekaa na
mwanaume mmoja, nilipowaangalia nikagundua ni majirani zangu pale nilipopanga,
waliniambia kuwa walisikia kelele walipokuja ndo wakanikuta tayari nimezimia
Rajabu alitoka nje na beg lake la mgongoni akakimbia, mimi wakanipeleka
hospital
"Asante kwa
msaada wenu" niliwashukuru
"Kwani
ilikuwaje?" Mmoja aliniuliza hapo nilianza kutoka na machozi
"Wanaume
wabaya sana jamani" niliwahusisha wanaume wote wakati aliyenitenda haswa
alikuwa ni Rajabu
Walinimbembeleza
nikatulia, basi kwa kuwa yule jirani yangu alikuwa polisi aliniambia
atanisaidia kufungua kesi,
Tangu siku hiyo
sikuwa sawa, nilikuwa nawaza kila siku, kilio ndo ilikuwa sehemu kubwa ya
maisha yangu, kuweza kula vizuri nilianza kukonda, homa zilikuwa haziishi,
nikaenda hospital na kupima nikagundulika nina virusi vya ukimwi, nilijua
kabisa lazima niliambukizwa na Rajabu maana alikuwa hajatulia, nililia sana
siku hiyo, dokta akanishauri na kunitia moyo, alinitaka niishi kwa matumaini
pia nianze dozi
Nilitoka pale
hospital na kusimama nje, nikimkumbuka Lameck nikaanza kujuta kwa kila jambo
nililomfanyia, nilitamani nimuombe msamaha lakini nitamuombea wapi, Lameck
ameshafariki tena bila kunisamehe, nilianza kupiga kelele huku nakimbia ovyo
kama mtu aliyechanganyikiwa watu walinishangaa nikaanza kuwatukana tu,
"Mnaniangalia
hamnijui? Waone kwanza misura mibaya kama ng'ombe" niliwaambia na
kuendelea kukimbia tena,
Basi nilikuja
kupata akili ya kumtafufa Rajabu, niliamua kwenda kule tulipokuwa tunajenga
majohe, ilikuwa ni nyumba ya vyumba vitatu, sebule, dining na jiko, choo
kilikuwa cha ndani, nilikuta nyumba ilishaisha kila kitu, ilibaki rangi tu nje,
lakini ilionyesha tayari kuna watu wamehamia, nilishangaa na kujiuliza nani
anaishi pale
Niligonga akatoka
msichana mwenye mtoto mdogo, sikuweza kumjua hata nilipomuangalia
"Wewe ni nani
hapa?" Nilimuuliza
"Mimi ndo
mwenye hii nyumba" alinijibu
"Umeinunua
hii nyumba au? maana sikuelewi hii nyumba ni ya kwangu alafu ilikuwa haijaisha
vizuri nashanga nakuja nakuta mtu anaishi" niliongea nikiwa nishaanza
kuhamaki
"Jamani hii
nyumba ya mume wangu, yeye alinunua kiwanja na kuanza kujenga, sasa unavyosema
yako sikuelewi"
"Huyo mume
wako yupo wapi, nataka kumuuliza nani kamuuzia hapa" nilisema
"Ngoja
nimuite" aliita akiwa pale pale mlangoni, punde mwanaume akatoka,
sikuamini macho yangu alikuwa ni Rajabu
Yaani kama Mungu
amenisaidia kunipa ile akili ya kwenda kule majohe
"Baby huyu
mdada kaja hapa alikuwa ana shida na wewe anasema hapa ni kwake" alianza
kumuelezea nilivyomwambia
"Habiba nenda
ndani" alisema Rajabu
Hapo ndo
nikagundua kumbe yule ndo habiba mwenyewe niliyewahi kukuta msg zake, yule
msichana akatuacha
"Habiba nenda
ndani" alisema Rajabu
hapo ndo
nikagundua kumbe yule ndo habiba mwenyewe niliyewahi kukuta msg zake, yule
msichana akatuacha
"Enhee
ulikuwa unasemaje?" Aliniuliza
"Unaniuliza
nilikuwa nasemaje?" Niliuliza na mimi
"Ndio maana
umekuja kwangu sasa sijui shida yako nini?"
"Hapa ni
kwako wewe? Umesahau hiki kiwanja kanunua nani na pesa za kujengea katoa nani?
Unajisahaulisha, kwanza kwanini umehamia kwenye nyumba yangu?" Nilimuuliza
kwa hasira
"Wewe
usiniletee upuuzi wako hapa, pesa si ulinipa mwenyewe kwani uliniambia
nikununulie kiwanja? Ulinipa pesa nami nikaamua kununua kiwanja ili nikijenga
niishi na wewe lakini imeshindikana, sasa nini tena unachonitafutia?"
"Rajabu
usinitanie nakwambia, siwezi kukubali uniharibie maisha yangu kiasi hicho,
nataka nyumba yangu? Ona umenifanyia mambo mengi machafu, umeniambukiza
maradhi, wewe sio binadam" nilimwambia kwa hasira
"Sasa kama
mimi sio binadam kwanini unaniongelesha na hapa unasubiri nini? Ondoka mimi
sina shida na wewe tena tushamalizana" aliniambia mara yule mwanamke wake
akatoka
"Kuna nini
mbona sielewi nasikia mnagombana tu?" Aliuliza
"Huyu
mwanamke amechanganyikiwa achana nae" Rajabu alimjibu
"Mimi
nimechanganyikiwa? Mwambie ukweli mwanamke wako mimi nani?"
"Wewe si mbwa
tu, ulitaka uwe nani?" Rajabu alisema kwa dharau nikapata hasira
"Sawa mimi
mbwa ila leo ndo utajua kama mbwa koko au kichaa" nami nilijibu kwa
kujiamini
"Jamani embu
wee dada ungeenda tu nyumbani kwako" habiba alisema
"Niende
nyumbani kwangu wapi wakati ndo hapa" nilijibu
"Kwahiyo wewe
unatembea na mume wangu na unataka ukae hapa si ndio?"
"Sina shida
na mwanaume wako, labda nikukumbushe tu, tuliwahi kuongea kwenye simu zamani
sana siku uliyopiga simu ya rajabu nikaipokea mimi, ukasema wewe ni mchumba
wake, sasa tangu wakati ule nilikuwa na Rajabu akanifanyia mabaya mengi huku
akikutuchanganya na kama alivyotoka Moro alikwambia anakuja kutafuta maisha
basi alikuwa amekudanganya aliishi kwangu na hata hii nyumba ni yangu amejenga
kwa pesa yangu, hivyo lazima aondoke na kuniachia kila kitu" nilisema
"Anhaa kumbe
basi mimi siwezi kukutetea wewe uliniibia mwanaume wangu, hivyo kama ukimpa
pesa huo ni ujinga wako mwenyewe, acha kutupigia kelele kwanza hii nyumba imeandikishwa
jina la mwanangu hivyo siwezi kukubali kutoka hapa, wewe nenda popote"
alisema habiba wakawa wameungana
"Tena ondoka
hapa kabla sijakupiga makofi nikuumize" Rajabu alisema
"Haya nipige,
nipige nasema, siwezi kukubali unidhurumu" niliongea kwa hasira
"Basi nenda
unapotaka" alisema habiba nikataka kumzibua kofi Rajabu akawahi wakaanza
kunichangia walinipiga mpaka nguo zikachanika, watu wakaja na kutugombelezea,
wakanitoa mimi, basi nilistiliwa nguo nyingine na kuondoka
Nilitafuta sehemu
na kukaa pekee yangu na kuanza kulia,
Yote ni makosa
yangu, sikutakiwa kumuamini Rajabu ile siku ya kwanza tu niliyokutana nae,
niliona msg akimwambia rafiki yake kuhusu mimi kuwa amenitamani lakini
sikufanya lolote, ilitosha kabisa kumuona sio mwanaume sahihi,
Haikuishia hapo
bado Mungu hakuacha kunionyesha ushetani wa huyu mwanaume pale nilipoenda kwao
Moro na kunipeleka gest ikiwa ana kwake alafu nikagundua anataka kuoa, kumbe
mimi alinichezea nilipaswa kumpotezea pale pale, lakini kwa ujinga wangu
nikampa nafasi nyingine wakati tayari nilishakuwa kwenye mahusiano na
nilipendwa sana,
Tamaa zangu za
ngono na kutokuridhika kwa Lameck kumenifanya niwe msaliti, hatimae nikaanza
kufanya mapenzi kinyume na maumbile bila kufikiria madhara yake, sikutakiwa
kurudiana na Rajabu kabisa ikiwa niliachana nae kwa tabia zake chafu,
nilimsaliti mtu ambae aliweza kunisaidia nilipokamatwa pia akanitoa kwenye
maisha ya mateso na kunipa furaha, pamoja na yote sikumlipa hata jema moja
badala yake nikasababisha kifo, kiukweli najutia kila kitu kilichotokea lakini
maji yameshamwagika
Haikuishia hapo
bado Mungu hakuacha kunionyesha ushetani wa huyu mwanaume pale nilipoenda kwao
Moro na kunipeleka gest ikiwa ana kwake alafu nikagundua anataka kuoa, kumbe
mimi alinichezea nilipaswa kumpotezea pale pale, lakini kwa ujinga wangu
nikampa nafasi nyingine wakati tayari nilishakuwa kwenye mahusiano na
nilipendwa sana, tamaa zangu za ngono na kutokuridhika kumenifanya niwe
msaliti,
Hatimae nikaanza
kufanya mapenzi kinyume na maumbile bila kufikiria madhara yake, sikutakiwa
kuwa nae kabisa, nilimsaliti mtu ambae aliweza kunisaidia nilipokamatwa pia
akanitoa kwenye maisha ya mateso na kunipa furaha, pamoja na yote sikumlipa
hata jema moja badala yake nikasababisha kifo,
Hatimae leo
nimeachwa nikiwa sina thamani, sio Aisha yule wa zamani hakuna aliyekuwa
akitamani hata kunisalimia, nililia na kuomba Lameck kama ananisikia anisamehe
nilianza kuona umuhimu wake sikuacha kumkumbuka, NINGEFANYA NINI?
Akili yangu
ilikuwa ishabadilika, niliwaza kufanya jambo moja kubwa na zito,
"Lazima wote
wafe nitaua tu Mungu atanisamehe, siwezi kukubali maisha yangu yaharibike kisha
nikae kimya, nitaua kisha nami nitajiua tu" nilisema na kuanza kutembea
nilienda nilipokuwa naishi na kuchukua pesa ilikuwa elfu 30 tu, nilienda
kununua petrol, kisha ilipofika usiku kama saa 3 nilitafuta boda boda
ikanipeleka majohe hapo nilitafuta sehemu nikakaa mpaka saa Saba usiku nilianza
kumwaga ile petrol dirishani mlangoni na iliyobaki nikazungusha kwenye nyumba,
kisha nikachukua mjiti nikawasha moto na kuurusha, moto ulianza kupamba
nilisikia wakipiga kelele na kutaka msaada nikaanza kuwajibu
"Kufeni
washenzi nyinyi mnajifanya dhuruma eeh sasa mufe tu, tutakutana huko
mbinguni" nilisema kiukweli sikutaka kufanya jambo baya kama hilo lakini
moyo wangu uliuma yule habiba alikuwa na majibu mabaya kwangu yalinifanya
nipanic, unafikiri kwa maumivu na mateso yote aliyonipa Rajabu NINGEFANYA NINI?
kuua ndo niliona maamuzi sahihi tu ili kuufanya moyo wangu utulie, wangenipa
mali yangu basi tungemalizana ningekubali kuendelea na maisha yangu lakini wote
walijitia majeuli,
Nilianza kusikia
sauti ya mtoto nikamuonea huruma sana, kwani hakuwa na hatia, nililia na kaunza
kupiga mikelele kama mwehu, watu walijaa na kuanza kuzima ule moto, wengine
wakanikamata, nikawa nawapiga na kuwatukana, nikasikia sauti za watu wakisema
"Hawa
wamekufa jamani hawaongei tena"
Basi nilikuwa
nikitukana ovyo na kuwapiga wale watu wasinishike nilianza kuongea ovyo tu
**********
Nikiwa nimeamka
usingizini nilikuwa nimechoka sana, nilijiangalia na kujiona nimekonda mikono
membamba nguo nilizovaa ni chafu mno, nilishangaa imekuwaje, nilipoangalia
vizuri palikuwa ni hospital
Mara akaingia
msichana mmoja nilianza kukumbuka alikuwa ni rafiki yangu jesca niliyekuwa
nikikaa nae jirani kule Lumo kwa mama zangu, alikuwa ambadilika sana na kuwa
mzuri haswa
"Aisha
unanikumbuka mimi?" Aliniuliza
"Ndio wewe si
jesca" nilimwambia
"Asante Mungu
hakika umepona rafiki yangu" alisema
Nilihisi nimepona
ukimwi maana ndo ugonjwa niliokuwa nao
"Kwahiyo sina
virusi tena nimepona kabisa?" Nilimuuliza kwa mshangao
"Mmhh hata
nikikwambia huwezi kuelewa, ila kwa kifupi ulikuwa chizi Aisha" aliniambia
hivyo nikashangaa akaanza kunihadithia kila kitu
Kumbe ile siku
niliyomuua Rajabu na familia yake nikapata uchizi kabisa, lakini nilikumbuka
kuwa ile siku nilikuwa nikifanya fujo na kutukana watu sikujielewa tena, Kumbe
nilichukuliwa na kupelekwa polisi nikikaa miezi sita na baadae sikupewa hukumu
yoyote baada ya kuuwa kwani nilipimwa na kuonekana chizi, nilitolewa na kuanza
kuhangaika mitaani nikila ovyo na kulala ovyo,
Akaniambia pia
siku moja akiwa anatoka mini aliweza kuniona k koo nikiwa natembea peku na nguo
zikiwa chafu tena zimechanika, aliingiwa na huruma na kupanga kunisaidia, baada
ya mwezi alifanikiwa kunikamata na kunifunga mikamba akanipeleka hospital,
Nilishangaa kwani
nilihisi ni jana tu ndo nimeua ila jesca aliniambia ndani ya miaka miwili
nilikuwa chizi na leo ndo nimeweza kupata akili zangu baada ya kutibiwa kwa
muda mrefu na kubadilisha mahospita
Nilianza kulia
upya moyo uliniuma, hakika nilidhalilika sana, tamaa zangu zimeniponza nimekuja
kusababisha mtu aliyenipenda kafa, pia nikajikuta nakuwa muuaji bila kutarajia
na kuua kiumbe kisichokuwa na hatia yule mtoto mdogo, nilitoa mimba na mwisho
nikapoteza uwezo wa kuzaa, nimepata maradhi makubwa kutokana na kuingiliwa
kinyume na maumbile sasa navakishwa pempas kama mtoto mdogo, uzuri wangu wote
umekwisha, hakuna mwanaume atakayenitaka tena sina thamani,
Mpaka sasa jesca
ndo mtu pekee aliyenipa msaada, nipo kitandani siwezi kufanya chochote kile,
niliweza kumuomba jesca aniitie mtunzi anayeitwa Lissa wa mariam ili niweze
kumpa historia ya maisha yangu na aweze kuipost watu wajifunze wasiwe na tamaa
kama mimi, ningetulia na Lameck pengine leo ningekuwa mama mzuri na wa kuigwa
ila nimekuwa mbaya sifai kuigwa na jamnii
Kwasasa nasubiri
siku yangu ya kufa tu ikaribie maana hali yangu ishakuwa mbaya
*****MWISHO****

0 Comments