Mama Suzi
alichukua usafiri uliomfikisha mpaka hospital ya Mount Meru,mbio mbio
hakukumbuka hata kumlipa yule mwenye usafiri.
"Daktari
naomba unifanyie vipimo haraka"aliongea mama Suzi huku akihema kwa kasi.
"Vipimo gani
hivyo mbona una kasi hivyo?Aliuliza yule Daktari.
"Nifanyie
vipimo vya HIV"Aliongea mama Suzi huku akitoa mkono ili Daktari atoe damu.
"Sawa
subiri"aliongea dakitari.Baada ya kutoa ile damu aliiweka kwenye
vipimo,majibu yalitoka baada ya dakika tano kwamba mama Suzi ni
mwathirika.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Pole sana
mama,kuna mtu unaishi naye basi ndo huyo aliyekuua"aliongea Daktari.
"What!!(nini)
inamaana nimeathirika?aliuliza mama Suzi huku akimkumbuka Daudi.
"Ndio
mama,kula vizuri,fanya mazoezi,pumzisha mwili wako utaishi kwa amani kama
wengine harafu punguza mawazo"alisema kwa kirefu yule dakitari.Mama Suzi
hakutaka kuendelea kukaa pale alitoka kichwa kikiwa chini kwa mawazo.
"Pesa
zimetuua,hii dhambi hata mungu hawezi kuisamehe,nimemuua mwanangu kwa tamaa za
pesa"aliongea mama Suzi huku akipanda kwenye usafiri kurejea nyumbani
kwake.huko nyumbani kwa mama suzi,suzi alikuwa tayari kile kitanzi ameshakiweka
kwenye shingo yake taratibu alikivuta kuona kama kimekaa vyema.
"Mungu naomba
upokee roho yangu"alisema Suzi huku akianza kuhesabu.
"Moja"
"Mbili"
"Tat..."hakuimalizia,alisukuma
kiti kwa miguu kisha kitanzi kikamkaza shingoni kwake,hazikupita hata dakika
tano Suzi aliaga dunia.
Wakati huo mama
yake ndo alikuwa anafika nyumbani,aliita Suzi lakini hakumuona ndipo
alipokufungua mlango na kukuta umefungwa kwa ndani,alisukuma kwa nguvu mpaka
ukafunguka.
"Mungu
wangu!!!!alitastuka mama Suzi alipomuona mwanaye akitoka mapovu mdomoni.
"Ashaaga
dunia tayari"alijisemea mama Suzi huku akipanda kwenye kitu kusikiliza
mapigo ya moyo ya Suzi alikuta yamesimama.
"Siwezi
kupiga kelele,namimi namfuata mda si mrefu"alijisemea mama Suzi huku
akitoka na kuchukua bodaboda.
"Kaka
nipeleke stend"aliongea mama Suzi huku akitoa noti ya elfu kumi na kumpa
yule dereva bodaboda.
"Dada sasa
sina chenji labda ngoja nikaombe"alisema yule kijana.
"Hapana
twende tu"alisema mama Suzi. Baada ya kuingia kwenye barabara kuu kuna
wazo lilimjia mama Suzi.
"Hapa hapa
panatosha"alijisemea mama Suzi baada ya kuona basi kubwa likija
maenhttp://deusdeditmahunda.blogspot.com/eo yale kwa sipidi Kali.
"Mungu pokea
roho yangu najua utanikutanisha na mwanangu"kwisha kujisemea hayo mama
Suzi aliruka na kujitupa katikati ya barabara,lile basi lilikuwa na mwendo
mkali lilimkanyanga na kumsaga saga kabisa,kila mtu alistaajabu kitendo
kile.Haraka lililetwa gari la mchanga na kufukia eneo hilo,hakuna kilichobaki
zaidi ya damu.
"Kweli watu
washachoka na maisha"alijisemea kijana mmoja aliyeona tukio lile.Hata
Askari police walishindwa kuelewa sababu ya mama suzi kufanya vile,yule kijana
mwenye bodaboda alikamatwa kwa mahojiano lakini badae aliachiwa huru.
Glory alizidi
kufanya biashara yake ile ya kuuza genge,miezi ya kujifungua ilikaribia.
"Ngoja niende
mjini nikanunue vyombo kwa ajili ya mwanangu"alijisemea Glory huku
akichukua pesa yote na kwenda mjini.
Issa kila siku
hakuchoka kumfikiria Glory,maneno ya mama yake hayakuacha kujirudia kichwani
mwake.
"Wiki ijayo
niende nikamwambie ukweli"alijisemea Issa.
"Glory kodi
ya nyumba imeisha,hivyo jitahidi ulipe ndani ya wiki hii"ilikuwa sauti ya
mama mwenye nyumba akimwambia Glory.
"Haya mama
usjali"alijibu Glory japo hakujua ile pesa ya haraka ataipata wapi,pesa
alikuwa anaipata lakini alihakikisha ananua vifaa kwa ajili ya mwanaye.
Wiki moja
iliisha,hapo mama mwenye nyumba alirudi tena.
"Glory
usitake kunizungusha,leo ndo mwisho nataka hera yangu vinginevyo chukua mizigo
yako uondoke"aliongea mama mwenye nyumba.Glory alichanganyikiwa hakujua
pesa itatoka wapi.
"Lakini mama
ngoja niunganishe ntakupa"aliongea Glory.
"Nimechoka
ngonjera zako,ngoja nikuonyoshe"aliongea mwenye nyumba huku akiingia
chumbani kwa Glory.Alianza kutoa nguo za Glory pamoja na vifaa vyote alivirusha
nje.
"Chukua
takataka zako uondoke humu"alifoka kwa hasira mama mwenye nyumba,Glory
machozi yalianza kumtoka,alijitahidi kumuomba amvumilie lakini yule mama mwenye
nyumba alikuwa mgumu.Ghafla tumbo la Glory likaanza kumuuma,alikaa chini huku
akianza kuhisi uchungu wa kujifungua.
"Mamaaaa
nisaiiiidiiee"aliongea Glory kwa shida.
"Acha mikwala
mtoto wa kike nyanyuka hapa uondoke"bado mama mwenye nyumba alijua Glory
anafanya masihara.
"Nakufaaaaa"alipiga
kelele Glory hapo ndipo mama mwenye nyumba aligundua kuwa kweli Glory alitaka
kijifungua baada ya kuona damu iliyokuwa inamtoka Glory.
"Siwezi kubeba
mzigo usio wangu"alijisemea yule mama kisha akaondoka nyumbani
kwake,hakutaka kumsaidia Glory aliyekuwa hawezi hata kutembea.Wapangaji wote
waliishia kumtazama Glory aliyekuwa anapiga kelele.
"Leo ndo siku
ya kumwambia ukweli,hivyo lazima niende na vizawadi vitakavyomfanya
aniamini"alijisemea Issa huku akichagua nguo kwa ajili ya Glory. Alichukua
usafiri uliomfikisha nyumbani pale,alishangaa kumuona Glory akiwa analia kwa
sauti,alitupa ule mfuko uliokuwa na zawadi.
"Nini
shida"aliuliza Issa huku akimuinua Glory.
"Tumbo
linauma"alijibu Glory hakutaka kumwambia ukweli kwa kuogopa kuukosa msaada
wa Issa.Issa aliita bajaji na kumchua Glory mpaka hospital ya Mount Meru.Glory
alipokelewa na baadhi ya madaktari walionekana kuwa fasta sana.
"Habari yako
kijana"alisalimia mwanaume mmoja aliyekuwa amevalia mavazi ya kidaktari.
"Salama
kabisa"alijibu Issa.
"Hongera
kijana umepata mtoto wa kiume,mtoto yuko vizuri labda mama yake ndo
hajazinduka,ila tunaamini mda si mrefu atapataa nafuu"aliongea yule daktari.
"Waoooh,asanteni
kwa msaada wenu"alijibu Issa kwa tabasamu la kutengeneza.Baada ya masaa
matatu Glory alipata fahamu.
"Niitieni
yule kijana niongee naye"alisema Glory.
"Kijana
unaitwa"ilikuwa sauti ikimuita Issa aliyekuwa nje.Issa baada ya kuingia
ndani ya wodi alimkuta Glory akiwa amelala.
"Asante sana
kwa msaada wako bila wewe nilikuwa napoteza maisha"aliongea Glory.
"Usjali
kawaida tu msaada mhimu,sijui unajisikia kula nini"aliongea Issa.
"Kwa sasa
hapana,labda matunda"aliongea Glory.
"Basi ngoja
nikakuletee"aliongea Issa huku akinyanyuka.
"Kwa dunia ya
sasa hivi ni vijana wachache wenye moyo kama wa huyu mkaka,anaonekana ana
upendo wa dhati"alijisemea Glory.Yaani yule mama mwenye nyumba sijui ana
moyo gani ya kashindwa hata kunisaidia,msaada nimepewa na mtu mwingine ambaye
nilikuwa simtegemei kabsa?sijui huyu mkaka nitamlipa nini"alijisemea Glory
huku akimwangalia mwanaye.Issa alienda mpaka walipokuwa wanauza matunda
alichagua mtunda mazuri,hakujali gharama yeye alijitoa kwa kila kitu.
"Ila
nikimwambia ukweli ukakataa naamini nitaongeza swahabu kwa mungu,kama akikubali
nataka niuvunje ule mwiko waliouweka vijana wa sasa kuwa hawaoi mwanamke
aliyezaa kabla ya ndoa"alijisemea Issa.
"Aliyeleta
hii mitandao ya kijamii ndo katuharibu kabisa yaani vijana wameshindwa hata
kufanya kazi kutwa nzima kwenye hii mitandao na mada zao zile za
kipuuzi"bado aliendelea kujisemea Issa wakati huo akiyasubiri yale
matunda.
"Msaada wote
huu ninao utoa lazima nifanye kitu"alijisemea Issa wakati anayapokea yale
matunda.
Issa alirejea
akiwa na matunda ya kutosha,bado Glory alijiuliza atamlipa nini huyu kijana
aliyeonekana mkarimu mda wote.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Yataka moyo
kulea mtoto ambaye si damu yangu"alijisemea Issa,lakini bado aliyakumbuka
maneno ya mama yake.
"Ntahakikisha
anapata malezi bora najua mungu ataniongezea baraka"alijisemea Issa.
"Sasa jioni
mtaruhusiwa,hivyo kuna gharama kidogo hapa itabidi mzikamirishe"aliongea
daktari mmoja akimwambia Issa aliyekuwa ameketi karibu Glory.
"Haina shida
wewe tuambie ni shilingi ngapi inahitajika"alisema Issa.
"Sijui
ntamlipa nini mkaka wawatu"alijisemea Glory baada ya kumuona Issa akilipa
gharama zilizokuwa zinahitajika.
Baada ya
kuruhusiwa walienda moja kwa moja mpaka alipokuwa anaishi Glory,Issa alilipa
kodi iliyokuwa inahitajika pamoja na kuongezea miezi mingine sita.
Issa alihakikisha
kila kitu kilichokuwa kinahitajika kinakuwepo.
"Mwenda pole
hajikwai"alijisemea Issa kila alipokuwa anataka kumwambia Glory aliamini
akienda haraka anaweza kuharibu.
Baada ya wiki moja
Issa aliamua kuuvunja ukimya alienda kwanza mjini akanunua vyombo vya ndani
vyote pamoja na nguo za mtoto.
"Mwanangu
ntamuita jina la Bahati au unasemaje kaka"ilikuwa sauti ya Glory
akimuuliza Issa.
"Sina neno
juu ya hilo,jina zuri sana hilo"alisema Issa huku akiwaza jinsi ya
kumwambia.
"Glory"aliita
Issa.
"Abeee
kaka"
"Kwanza
kabisa nikuulize swali"
"Eee
niulize"
"Sawa
natambua wewe hapo ulipo tayari ushaitwa mama,je waweza kuniambia baba mwenye
mtoto ninani?aliuliza Issa.
"Kwa ufupi ni
hivi,Glory alifuta machozi kisha akaendelea.Mimi ni mtoto wa mzee mmoja anaitwa
Gozbert,pia wazazi wangu wote hao walijitahidi kunilea kwenye maadili mema
kabisa,hadi nahitimu shule ya msingi nilikuwa siwajui wanaume.Ndani ya kijiji
chetu alikuja mwanaume mmoja aliyekuwa anaitwa Peter,Peter alikuwa mwanaume
mpole sana.Siku moja naenda kisimani kuchota maji nilikutana naye,aliniangalia
sana mpaka nikajihisi labda nina kasoro,siku hiyo ilipita.Ilikuwa siku ya
jumapili siku hiyo nilikuwa nikitoka kanisani,nilikutana hapo aliita jina
niligeuka kumwangalia kisha akaniita kwa mkono baada ya kumfikia akitoa noti ya
elfu tano akanikabidhi mkononi,nilijaribu kuikataa lakini alilazimisha.
"Nenda katoe
sadaka kanisani"aliniambia hivyo.
"Mimi natoka
kanisani sasa hiyo sadaka nikaitoe kanisa gani?nilimuuliza.
"Hapana Glory
hata jumapili ijayo utatoa pia"alinijibu,niliipokea ile pesa kisha
tukaagana nikarudi nyumbani.Siku zilisogea,jumapili tena niliweza kuonana naye
alifanya vile vile mpaka nikamzoea,siku moja aliniita na kuniambia yote
yaliyokuwa moyoni mwake,nilitafakari huku nikimhaidi kumpa jibu wiki
ijayo.Alikuwa mvumilivu sana.Hatimae nilimkabaria,nakumbuka siku nampa jibu
alipiga magoti mbele yangu nakuhaidi kuwa hata nisaliti atakuwa nami kila
sehemu,nilifurahi kuona upendo wake,mpaka ilifikia hatua akaramba damu yangu
nakusema kuwa kila sehemu atakayokwenda nitakuwa kwenye damu yake,nilimuamini
kupita kiasi,lakini siku alipogundua kuwa nina ujauzito uliokuwa wake asilimia
mia alitoroka pale kijiji bila kuniaga,na sikujua alikoelekea.Namlaumu kwa
kuniharibia maisha yangu.Wazazi wangu walipogendua kuwa nina ujauzito
walinifukuza nyumbani na ndo maana mpaka sasa Niko hapa,hakika wanaume ni watu
wabaya sana"alimaliza kusimulia Glory huku machozi yakimtoka.
"Pole sana
Glory lakini usiseme kuwa wanaume wote ni waongo,wapo waaminifu pia japo ni
ngumu kuwapata kwa hii dunia ya sasa"aliongea Issa.
"Ni kweli
lakini toka siku ile wanaume nawachukia sana"aliongea Glory.
"Sasa mimi
niko hapa nilikuwa naomba nikufute machozi hayo,pia sahau yaliyopita naomba
tuanze maisha mapya"aliongea Issa,bila kusubiri jibu aliondoka eneo lile
akimuacha Glory akiyatafakari yale maneno.Ilikuwa ni ngumu kwa Glory kuyakataa
yale maneno,kila alipokuwa anakumbuka wema wote aliomfanyia Issa alishindwa
kabisa kukataa.
"Ngoja akija
lazima tupange maisha"alijisemea Glory ndani ya hizo siku alikuwa hajapata
nguvu ya kwenda gengeni kwake.Yeye alikuwa anakaa ndani huduma zote alikuwa
akizitoa Issa,Jioni ya siku ile Issa alikuja na zawadi mbali mbali kama
ilivyokuwa kawaida yake,hata alipofika hakumuuliza tena Glory zile habari yeye
alimpa zile zawadi kisha akaondoka.
"Mbona hana
haraka kama vijana wa sasa,atakuwa na upendo wa dhati huyu"alijisemea
Glory.
Baada ya wiki moja
tayari Glory alikuwa anaishi na Issa,Glory furaha yake ilianza kurejea
taratibu,maisha yao yalikuwa ya furaha kila siku waliishi kwa furaha,genge lao
waliliendeleza huku kila mtu akiwa wa kutabasamu mda wote.Siku zilisogea huku
Bahati mtoto wa akizidi kukua.Bado Issa hakufikiria sana kuhusu kulea mtoto
ambaye si damu yake wengi walimsema lakini hakutaka kusikiliza la mtu.
"Yaani na
unadhifu wako huo leo hii umeoa mwanamke aliyekimbiwa?hahaha.
"Sijawahi
kufikiria kuoa mwanamke aliyezaa kabla ya ndoa"
"Binafsi
siwezi hicho kitu,ila kaka jaribu kufuatiria sana mitandao ya kijamii huko
kidogo utaweza kupata uelewa,mwanamke aliyekimbiwa sio wa kuoa
kabisa"Yalikuwa maneno ya vijana wa kijiweni walipomuona Issa,kila kijana
alisema lake.Issa aliishia kuwasikiliza tu hakutaka kuwajibu lolote.Hata
alishindwa kutembea sehemu kutokana na kupata matusi kila sehemu aliyokuwa
anapita,marafiki zake wote aliwatenga waliokuwa wanataka kumtenganisha na
Glory.
"Maneno ya
binadamu hayawezi kunifanya chochote,lazima nisimame mimi mwenyewe na Glory
mpaka mwisho watu wanaosema hayo maneno ipo siku watanyamaza
wenyewe"alijisemea Issa.
"Habari yako
bwana Issa"alikuwa mwanaume mmoja akimsalimia Issa.
"Salama kwema
huko"Issa alijibu.
Kabla hajajibu
yule mwanaume alicheka kwanza.
"Huku
kwema,nasikia unalea damu ya mtu mwingine,labda nikufungue akili,huyo mtoto
unayemulea akija baba yake atamchukua na wewe utaishia kushika kichwa tu,na
akija kumchukua huwezi kukataa wakati sio wako,bado najiuliza kijana mtanashati
kama wewe umefikiria nini mpaka ukaoa mwanamke mwenye mimba?harafu mimba
yenyewe sio yako hahahahaha kijana sijui umekwama wapi,ila bado nafasi unayo
yakuweza kumuacha huyo mwanamke ukatafuta mabinti wengine mbona wanawake wengi
sana hapa?,tafakari kijana"alisema yule mwanaume kisha akaondoka.Issa
aliinamisha kichwa chini huku akitafakari yale maneno.
"Anayosema ni
yakweli kabisa,lakini siwezi kumtenga Glory,wahenga walisema ukipenda boga
penda na ua lake,mtasema mpaka mtachoka wenyewe"alijisemea Issa.
Fikiri rafiki yake
Issa alizipata zile taarifa kuwa Issa tayari anaishi na Glory,toka mwanzo
Fikiri alikuwa akimpenda Glory.alianza kumfuatiria Glory.
"Naam lazima
nifanye mapinduzi"alijisemea Fikiri.
Upendo wa Glory na
Issa ulizidi kukua,japo Issa aliambiwa maneno mengi na marafiki zake lakini
hakuwa tayari kusikia la mtu,kila alichokuwa anaambiwa hakusita kumwambia
Glory,naye Glory alizidi kumsihi Issa asisikie la mtu.Issa aliendelea kufanya
kazi kwa bidii lengo amtunze Glory na mwanaye.
"Ngoja nipone
ili nimpe penzi langu mwanaume huyu"alijisemea Glory,kila alipokuwa
anamwangalia Issa alijikuta akiwaza mambo mengi
sana.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Hapa ndo
nimeamini baadhi ya maneno ya watu kuwa wanaume waaminifu wapo japo ni
wachache"alijisemea Glory.Maisha yao yalisogea,ndani ya kipindi hicho
hawakukutana kimwili,kila mtu alilala peke yake,Issa alikuwa analala
chini,Glory alilala kitandani.
"Namsubiri
apone ili nianze kurudisha gharama zangu"alijisemea Issa.Bado marafiki
zake walizidi kumshauri aachane na Glory lakini yeye hakuwa tayari.
"Watazidi
kusema lakini ndo hivyo nishampenda siwezi kumuacha"alijisemea Issa,kule
mgodini kazi yake iliendelea.
"Yaani wewe
mzee baba huna akili kabisa,hivi kweli umedhamilia kuishi na mwanamke
aliyebebeshwa mimba?huoni aibu kijana mzuri kama wewe?yalikuwa maneno ya kijana
mmoja akimwambia Issa.
"Nasema
niacheni na maisha yangu,sitaki mtu yeyote anifatirie"alijibu Issa kwa
hasira.
"Hapo umebugi
mzee baba,ni sawa na kufuga nyoka atakung'ata mda wowote"bado yule kijana
aliyekuwa anaitwa Yasin alizidi kumkebehi Issa.
"Yasin nasema
tena niache,we fanya yako usisababisha tuharibiane siku"alisema Issa kwa
upole.
"Hahahahaa,huna
jipya wewe akili yako ndo itendelea kuwa chini"alisema kijana Yasin,maneno
yale yalimkera Issa,ghafla lilitokea tafarani kati ya Issa na yule kijana
Yasin,lakini fatarani hilo halikudumu baada ya wafanyakazi wengine kuingilia
kati ugomvi ule.Issa alianza kujitenga na marafiki zake.Fikiri licha ya kuwa
rafiki wa Issa lakini aliendelea kuwaza jinsi ya kumpata Glory.
"Siku hizi
hakuna mwanamke mgumu,ngoja nisubiri mtoto wake akue"alijisemea
Fikiri.Issa bado aliendelea kutoa huduma kama kawaida yake.Baada ya mwezi mmoja
Glory alianza kutembea tembea,genge lake alilianza upya,bado Issa hakuchoka
aliendelea kutoa matumizi.
"Sasa ni
wakati wangu kwenda kumtembelea Glory,najua mda huu Issa yupo
kazini"alijisemea Fikiri,alifunga safari mpaka nyumbani kwa Glory lakini hakumkuta,hakujua
kuwa kwa wakati huo Glory alikuwa gengeni kwake.
"Ngoja
nitarudi siku nyingine"alijisemea Fikiri,ila kabla hajatoka alifika
Issa,Fikiri alionesha kustuka kwakuwa hawakuwa na uelewano mzuri kwa wakati
ule.
"Karibu"alisema
Issa.
"Ahaa asante,nilipita
kukusalimia"alisema Fikiri.
"Sawa,karibu
tena"alijibu Issa kisha akaingia ndani.Fikiri alisimama kwa dakika kadhaa
akionekana kutafakari kitu.
"Naona Issa
ameshaanza uadui na mimi,sasa namkaribisha kwenye uwanja wa
vita"alijisemea Fikiri.Baada ya wiki moja Fikiri alirudi tena lakini bado
alipakuta kimya,Glory aliendelea kumwomba mungu apone haraka lengo ampe nafasi
Issa.Zikiwa zimesalia wiki tatu ili Glory afikishe miezi miwili,kwenye mgodi
Issa aliokuwa anafanya kazi kulihitajika vijana kumi wa kusafiri kwenda nchini
China,kulikuwa na wachina kwenye ule mgodi waliokuwa wanahitaji vijana kutoka
nchini Tanzania ili kwenda kufanya kazi kwenye migodi iliyokuwa China,vijana
waliokuwa wanahitajika Issa alikuwa miongoni,Issa hakutaka kupoteza ile nafasi.
"Ngoja
nikatafute utajiri huko ili nije niishi vizuri na mpenzi wangu
Glory"alijisemea Issa.Jioni ya siku ile alirudi nyumbani akiwa na
furaha.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Mpenzi wangu
leo nina habari njema kwako"aliongea Issa kwa furaha akimwambia Glory.
"Habari gani
hiyo mme wangu"
"Tulia basi
usiwe na papara,haya ni mambo mazuri hayataki haraka"
"Nambie
basi"
"Nimepata
nafasi ya kusafiri kwenda China"aliongea Issa,hapo Glory alishusha pumzi
kidogo kisha akasema.
"Mme wangu
huko China mnafuata nini?aliuliza Glory.kabla Issa hajajibu Glory alifikiria
kitu.
"Nilijua tu
kuwa watamshawishi mpaka akubali,ona sasa anatafuta sababu za
kunikimbia"aliwaza Glory aliyeonekana kupoa ghafla.
"Glory acha
mawazo mimi naenda China kikazi,usjali kuhusu hera ya kutumia nitakuwa
nakutumia"alijibu Issa kwa sauti ya upole.
"Najua lakini
kama unanikimbia bora uniambie nijue,najua watu wanakwambia mengi kuhusu
mimi,kuliko unitafutie sababu bora uniweke wazi nijue"aliongea Glory.
"Glory hebu
acha kufikiria mengine,mimi huko naenda kikazi,tambua naenda kutafuta pesa kwa
ajili yetu ili tuishi maisha mazuri"aliongea Issa.moyo wa Glory bado
ulikuwa mzito sana,hakukubali Issa aende mbali naye kutokana na kumzoea kwa mda
waliokuwa wote.
"Sasa mimi
hapa nitaishi vipi na huko China utakaa kwa mda gani?aliuliza Glory.
"Nadhani
hawezi kupita miezi minne tutakuwa tumerudi,kikubwa mahitaji ya ndani yote
yasikose,nitahakikisha kila baada ya wiki moja nakutumia pesa ya matumizi hivyo
niruhusu nafanya haya kwa manufaa yetu"aliongea Issa kwa kirefu.
"Hapana mme
wangu siko tayari uende mbali na mimi"aliongea Glory.
"Sawa
nimekuelewa usijali tutakuwa wote"alijibu Issa,upendo aliokuwa nao Issa
ulikuwa mkubwa hakutaka kumkwaza Glory hivyo alikubaliana naye,Glory alijawa na
furaha,hapo ndipo alipodhibitisha kuwa kweli Issa ana upendo wa dhati.Usiku huo
Glory hakupata usingizi kabisa aliwaza maisha yatakuwaje kama Issa akiondoka.
"Lakini
kasema pesa atakuwa ananirushia kwanini nisimuruhusu?aliwaza Glory.
"Lakini ngoja
nimtege kwa hizi siku mbili nione kama atabadirika"aliendelea kuwaza
Glory.Siku mbili zilipita Issa hakugusia tena lile swala,aliendelea na kazi
yake.Ilikuwa siku ya juma tano sikiwa zimebakia siku tatu kabla ya safari Glory
alimuita Issa.
"Mme wangu
najua unanipenda nami nakupenda,kwa moyo mmoja nimekuruhusu kabisa,pia na
baraka zangu kama mke naziweka"aliongea Glory huku akitoa machozi.Issa
alistuka hakutegemea Glory angeliweza kumruhusu.
"Kweli
umekubari kabisa?aliuliza Issa akiwa haamini.
"Ndio ila
najua huko utaenda kuwaona wenye ngozi nyeupe,hivyo kuwa makini sana mme
wangu"aliongea Glory.
"Usjali
kuhusu hilo nadhani upendo wangu utauona nitahakikisha naongea nawe kila
siku"aliongea Issa huku akitoa simu kubwa aliyokuwa ameinunua na kuificha.
"Hii hapa
simu tutakuwa tunawasiliana kwa njia ya kuonana"aliongea Issa huku
akimkabidhi ile simu Glory aliyebaki kuduwaa.Taratibu alianza kumfundisha jinsi
ya kuitumia,alipohakikisha kuwa Glory kaelewa kila kitu alimwambia kuwa.
"Mke wangu
hii ni zawadi yako,hivyo hakikisha kila mda unakuwa hewani,weka bando la
kutosha kwa ajili yangu"aliongea Issa.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Kwa hilo
usijali mme wangu nitahakikisha nafanya kama ulivyonambia"alisema Glory
kwa sauti ya upole.
"Lakini mme
wangu bado sijapona,sasa sijui itakuwaje"aliongea Glory.Alijua kuwa labda
Issa atagusia swala la tendo la ndoa.
"Ondoa
shaka,mimi najua kwahiyo nivumilie mpaka nirudi"aliongea Issa.
"Kweli huyu
ananipenda"alijisemea Glory. Kwingineko Fikiri anapata taarifa kuwa Issa
anasafiri kwenda China,moyoni alijawa na furaha.
"Hii ndo
nafasi sasa"alijisemea Fikiri kwa furaha,alijua Issa akishaenda China
hawezi kumkosa Glory.
Hatimae wiki
waliyokuwa wamepewa wajiandae wale walikuwa wanasafiri kwenda China ilibaki
siku moja,maandalizi yalipamba moto,Glory alihakikisha Issa andaa kila kitu.
"Jamani ntakumis
mme wangu angalia usiniache mimi nakutegemea"yalikuwa maneno ya Glory
akimwambia Issa kabla ya safari.Wale wachina walitoa pesa kwa watu waliokuwa na
familia,Issa alipewa million moja,hiyo yote aliileta kisha akampa Glory
aliyeruka kwa furaha na kumkumbatia Issa.
"Kweli
unanipenda mme wangu"aliongea Glory kwa hisia.
"Usjali
ntahakikisha unakuwa na furaha mda wote,hivyo basi jitahidi simu yako isiishiwe
vocha,kila siku tutakuwa tunawasiliana,pia jitahidi mtoto apate huduma za
kutosha,naamini kila kitu kitaenda saw a,kingine kuwa makini na wanaume nadhani
unawajua walivyo waongo"bado Issa aliendelea kuongea yaliyokuwa moyoni
mwake.
"Sawa
nimekuelewa mme wangu kila kitu kitaenda vizuri"Glory aliongea mpaka mda
huo hakuwa wamekutana kimwili,Glory alikuwa bado hajapona.
"Ngoja
ntamtunzia penzi langu mpaka arudi"alijisemea Glory,kila alipomfikiria
Issa alimuona mwanaume pekee kwenye hii dunia.
"Vijana wa
sasa hakuna anayeweza kufanya hiki kitendo,huyu ndo mwanaume niliyeshushiwa
kutoka kwa mungu,ona Peter kaniacha nikitaabika kanikimbia lakini Issa mpaka
sasa yuko namimi"alijisemea Glory.
Siku ya Juma mosi
kulipambazuka na hali ya hewa safi,vijana walikuwa tayari kwa safari,wale
waliokuwa na wapenzi wao waliambatana nao mpaka kwenye uwanja wa ndege wa
KIA(Kilimanjaro International Airport)uliokuwa Kilimanjaro bado Glory hakuamini
kuwa ndo alikuwa akiagana Issa.
"Ngoja
nimuage kisawa sawa najua huyu sio wa karudi leo wala kesho"alijisemea
Glory huku akimkis Issa mdomoni.
"Mme wangu
naomba utambue kuwa huku umemwacha mtu unayempenda,hivyo
unikumbuke"aliongea Glory akiwa bado amemkumbatia Issa.Ndege aina ya
Quarter airways ilitakiwa kutoka nchini Tanzania kwenda mpaka kwenye mji wa
Guangzhou ulikuwa nchini China ilikuwa tayari,bado Issa alikuwa bado
amekumbatiana na Glory.
"Mme wangu
utarudi kweli?aliuliza Glory.
"Kwa uwezo
wake mungu nitarudi,naomba zingatia yote niliyokwambia"aliongea Issa.
"Usjali mme
wangu ntakuwa makini,safari njema basi mme wangu nakupenda"Glory
alimalizia na busu shavuni kwa Issa.walipungiana mikono hadi Issa anaingia
kwenye ndege alikuwa bado anamuangalia Glory.
"Safari sio
kifo ntarudi"alijisemea Issa baada ya kumchungulia Glory kupitia kwenye
madirisha ya ile ndege.Safari yao ilianza.
"Ngoja
ninunue vocha kabisa ili Mme wangu asikute sipo hewani"alijisemea Glory
huku akinunua vocha kutosha.Baada ya masaa kumi na mbili ndege ilitua kwenye
mji wa China.
"Ngoja nione
kama yuko hewani"alijisemea Issa huku akifungua mtandao wa WhatsApp.
"Yuko hewani
mda wote huyu ngoja nimjulishe kuwa nimefika salama"alijisemea Issa huku
akimpigia Glory,simu haikuita mda mrefu Glory alipokea.
"Nambie mme
wangu"
"Asee vizuri
ndo tumefika hapa"
"Oooh,pole na
safari Mme wangu"
"Asante vipi
Bahati hajambo"
"Huyu yupo tu
naona kalala"
"Akiamuka mpe
simu niongee naye"aliongea Issa kwa utani kidogo.
"Usjali
natamani nije nikukande maana najua umechoka sana"aliongea Glory.
"Tena uwahi
maana sio kwa kuchoka huku"
"Nakuja
jamani Mme wangu"http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Nikutakie
usiku mwema naona tumeitwa hapa hivyo msalimie Bahati,ntakupigia kesho"
"Nawe pia
ulale salama"baada ya maongezi yale Issa alikata simu.Fikiri baada ya
kudhibitisha kuwa Issa kaenda nchini China alifurahi moyoni.
"Hapa haruki
hawa wanawake wanarubunika kwa kitu kidogo tu"alijisemea Fikiri huku
akiwaza jinsi ya kumwingia Glory.Kila siku Glory alijitahidi kufanya
mawasiliano na Issa,ulikuwa upendo mkubwa sana japo kuwa Issa alikuwa mbali.
"Mme
wangu,natamani angalau siku moja nami unipeleke huko nikaangaze
macho"aliongea Glory kwa utani.
Siku
zilisogea,genge alilokuwa analiuza Glory lilikuwa kwa kasi baada ya kuongeza
vitu.Fikiri naye hakutaka papara.Ilikuwa siku ya jumamosi siku hiyo Glory akiwa
gengeni kwake walikuja wasichana watatu,walikuja kununua ndizi,kila msichana
alionekana bize huku macho yake yakiangalia simu ya mkononi.
"Jamani
karibuni"aliwakaribisha Glory.
"Asante,ndizi
shilingi ngapi?aliuliza msichana mmoja.
"Ndizi hizi
miambili hamsini,hizi huku miambili"aliwajibu Glory.
"Ok tunaomba
tatu za mia mbili mia mbili"Glory aliwafungia ndizi lakini bado
walionekana kuwa bize ndipo Glory aliwauliza.
"Mbona
mmeinama hivyo,kwani mnaangalia nini kwenye simu zenu?aliuliza Glory.
"Asee tupo
tunasoma simulizi kwenye makundi ya facebook,asee huyu mkaka sijui anayeitwa
MKAPA JR ana story nzuri sana za kugusia maisha harisi tunayoishi"aliongea
msichana mmoja aliyekuwa anaitwa Lea.
"Huwa napenda
sana kuzisikiliza kwenye radio,vipi namimi mnaweza kuniunganisha au mpaka
mnalipia?aliuliza Glory aliyekuwa hajui lolote kuhusu simu.
"Hapana ni
bure kabisa,kwenye kikundi wapo waandishi wengi na wote hao stori zao nzuri
sana"alisema Lea huku akipokea simu ya Glory.
"Kumbe una
simu nzuri kiasi hiki harafu bado huzipati stori kama hizi?asee pole
sana"alisema Lea.
"Mimi najua
lolote basi?labda najua kuwasiliana na Mme wangu tu"alijibu Glory. Baada
ya kuunganishwa Facebook alipewa maelezo na namna ya kuitumia mpaka apate
makundi ya stori,pia walimuunga na mitandao mingine ya kijamii,hakika Glory
alijiona wa mwisho kwenye hii dunia.
"Kumbe
duniani kuna vitu vizuri kama hivi?sijui nilikuwa wapi siku zote
hizi"alijisemea Glory baada ya kuona vitu mbali mbali kwenye mitandao ya
kijamii,siku hiyo alishinda akisoma stori,nyingi zilimgusa na ziligusa maisha
yake na kuzidi kuipenda zaidi hiyo mitandao hasa Facebook.Ilifikia hatua mpaka
alishindwa kumnyonyesha mtoto wake,mda mwingi alikuwa bize na simu.Fikiri
aliamua kwenda alipokuwa anaishi Glory,lakini bado hakumkuta ndipo alipoulizia
kwa majilani wa karibu.
"Yuko pale
kwenye lile genge ndo kwake"ilikuwa sauti ya mtoto mdogo akimuelekeza kwa
mkono Fikiri aliyekuwa makini kusikiliza,baada ya kuelekezwa alienda moja kwa
moja kwa moja,lakini kabla hajafika mara ghafla simu yake ilipata kuita,aliitoa
mfukoni na kuangalia jina la mpigaji,alipomaliza kuongea aliirudisha mfukoni
kwa wakati huo alikuwa gengeni penyewe.
"Habari yako"alisalimia
Fikiri.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Salama,karibu"aliitikia
Glory huku macho yake yakiwa makini kutazama Simulizi aliyokuwa anaisoma.
ITAENDELEA
.jpg)
0 Comments