STORY YA KUSISIMUA..
**DADA BINAMU**
MSIMULIZI: MEJAH PLAN MAKER.
MAHALI: MBEZI KIMARA.
MTINDO: STRAIGHT FORWARD.
NOTE
kumbuka simulizi hii Ina maudhui ya kikubwa hivyo Isomwe wenye umri kwanzi miaka 18+, tafadhari zingatia hili.
EPISODE O1..
Baada ya uchomvu mwingi niliamua kutulia kibarazani nikifatilia udaku mtandaoni, ghafla nilishtushwa na sauti ya mama ikiita... "Weee masara..
"Mama"
"Ebu njoo uku"
Nilinyanyuka nikiwa nimekunja mdomo maana nilijua sasa ameanza kutuma nilizima data na kuiweka simu yangu mfukoni. Kisha nikavuka sebure kuelekea jikoni.
"Mwanangu sikia nikwambie kit u" aliongea mama kwa utulivu
"Eh mama kuna nini tena" niliamaki kumuona mama akiwa vile
"Tulia basi nikwambie(akijiweka sawa kwenye Kiti) unajua mjomba wako sule Ana biashara nyingi sana unaonaje mwanangu ukienda kwa mjomba wako kuliko kukaa hapa bila shughuli yeyote na Mimi mama yako Kama unavyoniona sina kazi kusema ya maaana ya kukusaidia mwanangu japo ntaji tu ufanye biashara, unaonaje hili mwanangu"
"Ina maana mama umenichoka hivi mpka unataka nitoke hapa nyumbani?? Niliuliza kwa mshangao
"Mmh masara Mimi mama yako nikuchoke kweli jamani usinichumie dhambi ya buree, ninachoangalia kwako mwanangu ni siku za usoni na wewe mtoto wa kiume utahitaji kuwa na familia hapo baadae na mdogo wako faudhia anakuangalia wewe amka mwanangu"
Nilimtazama mama kisha nikiamka na kuondoka zangu nilibamiza mlango kwa hasira nikaongoza njia hadi kwao na kina Jamal
********
"Umeona Atalanta amepewa odds nyingi 2.8 Mimi nampa Atalanta anamuua juve" aliongea Jamal
"Kaka Mimi ninavyouona huu mchezo both timu score Kama uamini utaniambia" niliongea kwa msisitizo
Hayo ndiyo yalikuwa maisha yangu, nikiwa nyumbani naamka saa nne nakuta maandazi na chai nitakunywa chai na kwenda kubet au kujiweni kupiga story mpka muda mwingine wa kula narejea tena nyumbani kula kisha urudi mpirani SAA kumi jioni.
Itaendelea
0 Comments