Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Responsive Advertisement

CHOMBEZO: **DADA BINAMU**

 






SIMULIZI YA KUSISIMUA.


**DADA BINAMU**

MWANDISHI: MEJAH PLAN MAKER.
MTINDO: STRAIGHT FORWARD.
CONTACT: 0620721640.
MAIN CHARACTER: MASARA KURANGWA.

NOTE:
ISOMWE NA WENYE UMRI KWANZIA MIAKA 18+ KUTOKANA NA MAUDHUI YAKE..

EPISODE 02.
Maneno ya mama yaliniiingia akilini nikawazaa "nitaishi hivi mpka lin? Ukizingatia Mimi ni mtoto wa kiume na hatuna baba mama yangu alitelekezwa tukiwa bado wadogo ametulea kwa shida mpka kufikia hapa, acha niende kwa mjomba najua nitapata shida lakini najua ipo siku Mungu ataniangazia nuru yake"

Nilinyanyuka pale nikarejea nyumbani mnamo saa moja jioni nikamkuta mama akipika njee kwenye kuni.
Mimi "mama mbona unapikia kuni Leo"
Mama " mwanangu we acha bajeti ya mkaa Leo sikuwa nayo Ila bahati nimeshaivisha sasa hivi tunaingia ndani tu, vipi kwema utokapo??

Mimi " mmh unauliza kama nimetoka kwenye shughuli yeyote mama nawe"

Mama " lakini si unakumbuka ya wahenga mtembea bure si sawa namkaa bure hata uko utakuwa umepata wazo jipya mwanangu"

Mimi " haswaaaa!! Na kweli nimekaa nimefikiria mama nimeonelea niende tu kwa mjomba maisha haya ya kutazamana asubuhi mpka kuchweo mpka lin?? Ngoja niende nikapambane na maisha uko dad"

Mama " umeamua vizuri mwanangu,, aya mwana kwetu safari yako lini nikuandalie nauli maana safari yaitaji maandalizi uwabebee japo uduvi(aina ya dagaa)"

Tulicheka wote kwa furaha
Mimi "muda wowote nikipata nauli nitakwambia sasa mama wiki ijayo naondoka..

Tuliongea pale mpka alipokuja mdogo wangu faudhia kutoka kujisomea na wenzake huko shule akatukutia pale nje tukiendelea kupiga soga.
Kusema ukweli hali ya maisha ilimlazimu mdogo wangu faudhia kwenda kujisomea na wenzake huko Kutokana na kutokuwa na umeme pale nyumbani.
***************

"Masara changamka watolee wateja mzigo muda huu usilaze dam u" ilisikika sauti ya mjomba

Mimi " umesema cement mifuko tisa na gypsums powder mifuko kumi "

Mjomba "ndio changamka kidogo wateja wanasubiri"

Kipindi cha mwanzo nilipata shida Sana maana sikuwahi Kufanya kazi ngumu namna ile Ila kwakuwa nilidhamiria niliiapia nafsi yangu kuwa nitapambana mpaka tone langu la mwisho sitarudi nyumba na ukizingatia sikuwa na elimu zaidi ya darasa la Saba niliyohitimu shule ya mwenge miaka minane iliyopita.

Mjomba alikuwa na hardware/duka LA ujenzi maeneo ya mbezi na pia alikuwa na biashara mbalimbali alizofungua dar kusema ukweli nilitegemea labda angenipa mradi angalau nikae kwenye duka lake lolote niuze Ila alinipa kazi ngumu kiasi ambacho ukilala usiku utamani kukuche asubuhi kwa uchovu.

Mjomba "sasa wewe tangulia nyumbani tutaonana Mimi kuna sehemu napitia" aliongea mjomba akiwa Ana panda kwenye pikipiki yake

Mimi " sawa hamna shida"

Tuliachana pale nikiwa nimechoka kweli, muda nilikuwa nimeshapokea ujira wangu wa shilingi elfu5 nilimshukuru Mungu kwa hiko pia nilipitia dukani angalau ninunue vocha niweze kumpigia mama.

"Maisha ndivyo yalivyo mwanangu nawe ni mtoto wa kiume pambana masara dume langu usichoke tunakutegemea" ilisikika sauti ya mama ikinitia moyo
*****************

Angela binamu yangu alikuwa anapnda sana kunitia moyo na kunisihi nikipata pesa nijiendeleze kielimu "angela tatizo sio kusoma Ila nataka nimsapoti mdogo wangu fau yeye akimaliza Mimi nitasoma tu"

Angela "lakini masa kumbuka muda si rafiki umesema sasa Una miaka 23 unadhani mpaka fau amalize shule ni Leo jiongeze Ila nimekumbuka nitakupa mbinu"
*********

Baada ya miezi kwenda nakumbuka Siku moja jioni mjomba alirudi kutoka kazinii akapata mashtaka kutoka kwa mkewe kuwa Mimi Nina mahusiano na Angela roho iliniuma Sana nikabaki natokwa na machozi.

"Aunty au ujafurahishwa na ujio wangu hapa?? Niliuliza huku machozi yananitoka

"Masara Mimi nikuchukie wewe kwa liipi kusema ule ukweli tabia zako sijazipenda unaniharibia mtoto na unajua fika anasoma Kama wewe ulifeli shule unataka na mwanangu afeli kama we we?? Baba Angela Mimi masara simuhitaji hapa kwangu kwanza zee zima si akapange? Si anafanya kazi? Hela anapeleka wapi? Akapange tu ataniharibia MTO to" aliongea shangazi kwa jazba

Katika yote Yale sikumsikia ankoo akitia neno hata kidogo alikaa kimya. Niliwaza Sana nikachukua simu yangu nikampigia mika rafiki yangu ambaye ni kinyonzi nikamuomba anipe hifadhi japo mwezi mmoja nikiwa najipanga.

"Usijali mshikaj wangu shida wameumbiwa binadamu wewe njoo utastay/utakaa ghetto mambo yakiwa fresh utaangalia mipango mingine Ila hapo sepa/ondoka" alimaliza mika akakata Sim u

Nilinyanyuka bila nikaaga ndipo nilipomsikia mjomba akiongea "Kama unaondoka kwangu mpe taarifa mama yako asidhani uko kwangu, Ila ni bora ungerudi nyumbani ujipange"

"Mjomba nakushukuru Ila hali ya nyumbani unaijua fika siwez kurudi nyumbani nikawe mzigo kwa mama nitapambana hapahapa tu ipo siku yangu tu" niliongea kishujaa nikaondoka

Nikiwa njiani nilimkuta Angela ananisubiria akiwa Amalia huku mafua yakimtoka "samahani Sana masa nimekusababishia matatizo"

Mimi "Angela hakuna lenye mwanzo lisilo na mwisho ipo siku yatakwisha nipo kwa mika ukiwa na shida utanifata"
*********

Siku zilisonga na maishayaliendelea kila siku Angela alikuwa akiniletea chakula kila jioni nikitoka miangaikoni. Mara zote nilikuwa narudi saa moja jioni nakuta funguo chini ya tofali Kama kawaida siku zikaenda mwezi ukakatika.

Tabia ya mika ilianza kubadilika Mara anaweza akaamka anisalimii au akirudi anisalimii nikajua uenda ameanza kuchoka Ila kibaya zaidi siku moja alifanya kitu cha ajabu Sana....

JE AMEFANYA KITU GANI??????

USIKOSE EPISODE 03

Post a Comment

0 Comments