MTUNZI: Mejah plan maker.
MAHALI: Mbezi (dar-es-salaam)
MTINDO: Straight forward.
Namba: 0620721640.
EPOSODE 03.
Sikuamini macho yangu punde nilipoamka nikalifungua macho yangu na kumuona mwanamke mbele yangu "saa nne hii mika anakuja na mwanamke ana maana gani? Ina maana Mimi nitalala wapi? Mmh(huku navuta pumzi na kushusha) kweli nimeamini akufukuzaye akwambii toka" nilinyanyuka kutoka pale kitandani ili kutoka nje Ila kabla sijafungua mlango nikasikia naitwa. "Masara" niligeuza shingo sababu nilijua aliyeniita alikuwa mika.
Akasema "unajua wewe ni sawa na gunia la misumari"
Nikamtazama kabla sijamjibu kwa mshangao "Mimi Huyu!!!!
Akaongeza "kwani unafikiri naongea na nani? Unadhani naongea na huyu mwanamke?? (Huku anavua T-shirt yake) sioni unachonisaidia zaidi ya mimi kukusaidia wewe, kweli mtoto wa kiume nakupa sehemu ya kulala, nikununulie sabuni ya kuoga, nikuchoteee maji, hata kufua shuka tu uwezi aahaaaa inatosha si ule mwezi mmoja uliosema nikupe hifadhi si umekwisha??
Aliongea kwa kujiamini nikumuangalia yule Dada alikuwa anatikisa kichwa.
"Lala kwa usiku huu Ila kesho tafuta pa kulala Mimi Sasa nataka kuishi na mwanamke nimechoka kuishi kisela sela" alizidi kukandamiza msumari kwenye kidonda kibichi.
Kweli nikimtazama yule mwanamke alikuwa na beg dogo na mfuko wenye viatu Kama si pea tatu basi zaidi ya hapo. Alionekana ni Dada wa mjini haswa alikuwa ni mweusi, mnene, mwenye shepu yake, lakini alikuwa amejipodoa haswa na aliweka kope na kucha za bandia mithili ya kahaba mdangaji.
"Sawa nashukuru rafiki yangu Ila cha kukushauri inavyoonekana huyu mwanamke kwa maisha yako utomuweza, kama umeamua kuoa mika tafuta mwanamke mwenye dini aliye na hofu ya Mungu si kama huyu mika kila kitu hapo ni fake kwanzia nywele(wigi), kope, kucha unadhani ataweza kukufulia huyu?? Ila zaidi uenda amekupndea pesa, Mimi nilidhani baada ya kupata hiyo kazi bandarini ungetulia ujijenge umeamua kuoa!!! Sawa ila (kabla sijamaliza nilisikia sauti ya yule Dada....
"Ishia hapohapo, kaka sikujui unijui naomba unikome kama ulivyokoma kunyonya dole la mkono upo?? Uoni Aibu dume zima unalishwa, kukaa bure, utagongwa fyuuuuuuu" alimaliza kwa tusi na kebehi ya hali ya juu, kitendo kilichoniuma sana nilitamani nimchape makofi Ila nikaamua kuokota beg langu nikaondoka.
*******************
Hali ya hewa ilikuwa ya juu kali lenye kuchoma hasaaa, nikiwa katikati ya mji niliamua kujichanganya na vijana wenzangu kutafuta ridhiki kwenye kubeba mizigo sokoni mpaka jioni nilijikuta Nina kiasi cha shilingi elfu kumi na tano ambayo kwangu ulikuwa mwanzo mzuri maana sikuwahi kuishika kabla. Nilipata mkate na juice ya azam cola ya mia Saba nikajiegesha pembeni ya duka la mpemba nikalala siku Imeisha..
Nikiwa na mawazo mazito juu ya familia yangu na juu ya maisha haya ya dar nikajipa moyo "Ila mgawa riziki ni Mungu ipo siku nuru yake itaniangazia maana Mungu wa matajiri ndio huyo Mungu wa matajiri" nilipitiwa na usingizi mpaka pale niliposikia milango ya maduka ikifunguliwa nikajua sasa kumekucha. Niliamka nikaendelea na shughuli zangu.
Mgosi ambaye ni muuzaji pale kariakoo shimoni alikuwa na rafiki yake anaitwa mwafyale ambaye uchukua mizigo kutoka mikoani na kuuza dar, aliniita na kuniambia jambo "mdogo wangu unaonaje ukatafuta pesa ufanye biashara kwa ninavyo kuona na kazi hizo unaumia sana" aliongea yule kaka
"Natamani Leo kesho niache hii kazi Ila nitafanya biashara gani kaka na pesa ya mtaji sina(niliongea kwa huruma Sana) na kumfanya yule kaka anitazame kwa muda kisha akaniambia
"Usijari wewe ni Kama mdogo wangu nitakusaidia twende mbeya tukirudi utakuwa umepata jibu""
***********************
BAADA YA MIEZI KADHAA..
Niliamka asubuhi nikajitazama kwenye kioo changu cha ukutani nikachukua taulo langu ili nikaoge, ghafla ikaingia meseji "tafadhali naomba nipigie" ilikuwa ni namba ya Angela Dada binamu. Nilitabasamu Sana maana sijapokea simu wala jumbe kutoka kwake takribani miezi minne sasa. Nikachukua simu na kumpigia. Nilizungumza mengi nae huku akisisitiza anatamani kuniona, tuliahidiana kuonana wikiendi nikakata simu na kuendelea na shughuli zangu.
Kweli nimeamini mti wenye matunda ndio unaopigwa mawe. Wakati sina pesa sikuwahi kupendwa na mwanamke japo hata salamu Ila sasa nakamata vihela angalau wanawake hasa wapangaji wenzangu walikuwa wananishobokea Sana.
Nilirejea nyumbani mnamo saa mbili jioni nilimkuta mama mwenye nyumba wangu akiwa amekaa Karibu na mlango wangu nilimsalimu na kuingiza funguo kwnye kitasa changu.
"Samahani baba ninaweza kuongea na wewe hata kidogo?? Aliongea yule mama wa makamo Kama si rika moja sawa na mama
"Nakusikiliza mama" nilimjibu huku namtazama vizuri
"Una ujuzi kidogo wa umeme balbu yangu imeungua nahitaji wa kuniwekea unaweza kunisaidia?? Aliongea
"Hakuna shida ngoja nibadili nguo Mara moja.
******
Nilijikuta nikimtazama yule mama hasa baada ya kuona kanga imefunguka na kudondoka chini..
USIKOSE SEHEMU IJAYO
0 Comments