LATIFA NTANGA
0719618409
Romeo aliogopa sana baada ya kujua wazazi wa Lisa watamuuliza sababu iliyofanya Lisa anywe sumu, na moja kwa moja alijua lazima Lisa atamtaja yeye. Hofu kubwa ilimjaa nakuona sasa maisha yake yapo hatarini. Alimjua Mzee Charles ni baba anayewapenda sana watoto wake, leo hii asikie Lisa umekunywa sumu kisa mapenzi tena kibaya zaidi kwaajili yake. Alijikuta anakosa raha kabisa, alijuta kwa yote aliyofanya tamaa yake ilimponza. Hakujua chakufanya hapo alibakia akitetemeka tu.
Mzee Charles na mkewe walifarijiana hadi wakawa sawa,
"Oh Romeo upo kijana wangu?" Aliuliza Mzee Charles baada ya kumuona Romeo.
"Nipo baba leo nilikuja nyumbani kusalimia ndio nikakutana na majanga ya Lisa" alijikaza Romeo na kuongea.
"Kweli haya ni majanga maana najifikiria sipati jibu imekuaje" Alisema Mzee Charles. Basi siku hiyo walishinda hapo hapo hospitali, jioni Daud na Frank wakaondoka zao pamoja na Romeo na Mzee Charles. Mama Lisa yeye aligoma kuondoka alibakia na mwanae ambaye bado hakuwa amefungua macho. Hadi usiku sana Lisa ndio aliamka na kujishangaa alipokuwepo.
"Mama!" Aliita Lisa na muda huo bi Lucy alikuwa amepitiwa na usingizi mzito kwa sababu alichelewa sana kulala. Lisa aliumia sana moyo wake kuona hajafa yupo hospitali. Moyo wake ulichoma sana kila alipomkumbuka Romeo bado alikuwa anampenda sana. Asubuhi na mapema bi Lucy aliamka na kushangaa kuona mwanae pia ameamka, alimsogelea na kumkumbatia kwa furaha sana.
"Mungu ni mwema mwanangu umerejewa na fahamu zako jamani" Alisema bi Lucy.
"Mama naumia" Alisema Lisa kwa huzuni sana.
"Pole mwanangu tatizo nini kwani?" Aliuliza Bi Lucy. Ila Lisa hakutaka kusema ukweli alimpenda sana Romeo japo kuwa alimkosea ila bado moyoni mwake alimuhitaji. Pia alijua jinsi gani wazazi wake wanavyompenda kusema chanzo cha yeye kunywa sumu ni Romeo basi angeweza kufungwa maisha gerezani kama sio kuuliwa kabisa, Lisa alimjua baba yake jinsi gani anavyompenda na hakutaka apatwe na tatizo lolote hivyo hakuwa tayari kusema Romeo ndio msababishaji aliamua kubaki na siri yake moyoni tu. Mama Lisa alijaribu kumsihi mwanae aseme ila alikaa kimya tu, Ghafla mlango ukafunguliwa na Romeo akaingia akiwa na mfuko mkononi. Moyo wa Lisa ulifarijika sana baada ya kumuona Romeo hakujua nani amempa taarifa ila alijikuta anasahau maumivu yake yote na kufurahia kumuona Romeo hapo hospitali.
"Mama shikamoo!" Alisalimia Romeo.
"Marahaba mwanangu, za tangu jana?" Aliuliza bi Lucy siku ya leo alikuwa vizuri hata tabasamu lilichanua usoni hakuwa mnyonge kabisa.
"Salama mama nashukuru Mungu, pia nimefurahi sana kumuona Lisa ameamka" Alisema Romeo huku akionyesha furaha ya wazi usoni.
"Ni jambo la kumshukuru Mungu sana kwakweli" Alisema Mama Lisa huku akimuangalia mwanae. Romeo akaweka mfuko wake kwenye meza ndogo iliyokuwepo humo ndani, halafu akamsogelea Lisa na kumkumbatia kwa nguvu bila kujali uwepo wa bi Lucy humo ndani akambusu Lisa kwenye paji la uso.
"Lisa am sorry for everything" Alisema Romeo kwa sauti ya chini.
"Romeo nakupenda" Alisema Lisa na kulia, Romeo akambembeleza na kumfariji, kwa utu uzima aliokuwa nao bi Lucy alishagundua hao watu wanauhusiano wa kimapenzi na akahisi moja kwa moja Romeo anahusika ila hakutaka kuingilia alijifanya kama hajaelewa kitu vile.
"Nimekuletea mtori naomba ule mke wangu" Alisema Romeo na kumfanya bi Lucy ashangae mkewe kamuoa lini? ila alikuwa mama mwenye busara zake hakusema lolote alikaa kimya na kuwaangalia tu. Basi Lisa akakubali na Romeo akatoa ndani ya mfuko hotpot na kufungua akachota mtori na kuweka kwenye bakuli kubwa akamsogelea Lisa na kuanza kumlisha. Mama Lisa alikuwa ametulia tuli anaangalia sinema tu inavyoenda. Wakati huo huo Mzee Charles akafika hapo hospitali na kushangaa kuona Lisa ameamka amekaa kitako na analishwa chakula na Romeo.
Itaendelea.
Mwendelezo lipia buku upate vipande 7. 0719618409 lisa ntanga.
0 Comments