Baada ya Daktari kujua ugonjwa wa Mzee Charles haikuwa shida kwao ambapo kumpatia matibabu, na baada ya muda mfupi hali ya Mzee Charles ilikuwa sawa. Alipoamka akajishangaa yupo hospitali hakujua amefika vipi.
"Nani amenileta hapa?" Aliuliza Mzee Charles.
"Vijana wako wawili" Alijibu nesi mmoja.
"Sawa nashukuru naomba mniruhusu niende" Alisema Mzee Charles huku akiinuka.
"Hapana baba, Ungesubiri kidogo hali yako ikae sawa"
"Nashukuru naomba niende" Alisema Mzee Charles na akainuka na kutoka nje huku uso wake ukionyesha jinsi gani anamajonzi. Na alipowaona vijana wake akawaambia wampeleke hospitali akamuone Lisa ambapo Daud na Frank walishangaa sana kusikia Lisa alikunywa sumu na amelazwa hospitali, hapo sasa wakajua kilichosababisha Mzee Charles apandishe presha. Hakukuwa na maongezi tena wote wakaingia kweye gari na safari ya kwenda hospitali kumuona Lisa ikaanza.
**
Baada ya kimya kirefu mlango wa chumba alicholazwa Lisa ukafunguliwa na Daktari pamoja na manesi wakatoka huku wakisukuma kitanda kimoja ambacho alikuwa amelazwa Lisa juu yake. Mama Lisa alipata nguvu na kusimama akawasogelea na kumuangalia mwanae huku machozi yakimtoka.
"Mwanangu anaendeleaje?" Aliuliza mama Lisa.
"Tunashukuru Mungu yupo salama tumefanikiwa kutoa sumu mwilini" Alijibu Daktari.
"Mungu awabariki kwa kuokoa maisha ya mwanangu!"
"Amina mama ngoja tumpeleke chumba cha mapumziko"
Baada ya hapo kitanda kikasukumwa hadi kwenye chumba kingine na Lisa akaingizwa humo. Wakaruhusiwa kuingia na kumuona Lisa alikuwa amefumba macho hajui kinachoendelea duniani.
Ghafla Mzee Charles na yeye akafika na vijana wake na moja kwa moja wakaingia hospitali humo, sababu alijulikana sana haikuwa shida kwake kuonyesha chumba alicholazwa mtoto wake, basi alisogea mlangoni na kufungua akaingia ndani macho yake yakaganda kitandani alipolala binti yake wa pekee!
"Baba!" Ayan alisema na kumkimbilia baba yake akamkumbatia kwa furaha sana.
"Mwanangu!" Alisema Mzee Charles akijizuia machozi yamsimtoke.
"Mume wangu!" Bi Lucy alimsogelea mumewe na kumkumbatia huku machozi yakimtoka.
"Usilie mke wangu, tuombe Mungu Lisa awe mzima" Mzee Charles alijaribu kumpoza mkewe.
"Naumia mume wangu sijui Lisa amepatwa na nini hadi anywe sumu" Aliongea kwa uchungu sana bi Lucy huku machozi yakimtoka kwa wingi.
"Usijali akipona tutamuuliza atuambie sababu ni nini" Alisema Mzee Charles akiwa anamaanisha anachosema, maneno hayo yalisikiwa na Romeo ambaye alianza kutetemeka kwa hofu.
Itaendelea.
Buku vipande 7, lipia sasa nikutumie 0719618409 jina lisa ntanga.
0 Comments