Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Responsive Advertisement

PENZI LA MCHORA TATTOO-42



LATIFA NTANGA
0719618409
Romeo hakutegemea kama Editha angeenda nyumbani kwake, na kuwafumania yeye pamoja na Livia, pia alishindwa hata kujitetea matokeo yake akasababisha wawili hao wapigane haswa hadi kutoana nje na kufanya watu wajae wengi kushuhudia huo ugomvi, Romeo aliona hakufai sasa shughuli kaingia mmasai, alichokifanya alifunga mlango wake na yeye akatoka kwa sababu watu walikuwa makini kuangalia ugomvi ilikuwa rahisi kwake kuondoka bila kuonekana. Nje akapanda kwenye gari lake na kuondoka kabisa eneo hilo. Moja kwa moja alitafuta baa moja sehemu ya mbali kidogo, akaagiza pombe kwanza anywe akili ikae sawa.
"Dah wanawake wengine bana sijui wapoje sasa kuharibiana jina mjini hapa aaah!" Alisema Romeo peke yake nakuendelea kunywa pombe zake.
"Hawa dawa yao ni kuwapiga chini wote kwanza hawana jipya niwa nao nijitie nuksi na mikosi tu nawaacha watajua wenyewe!" Alizidi kuongea Romeo na kufakamia pombe zake. Na baada ya muda mchache alishangaa simu yake inaingia meseji aliposoma ilitoka kwa Livia, hakutaka kumchelewesha hapo hapo akampa makavu yake na kumwambia kuwa hamuhitaji.
Siku hiyo Romeo alikunywa sana mwisho akatafuta gesti karibu na kuchukua chumba akaingia kulala akiwa na amani moyoni wala hakumfikiria mwanamke yoyote kati ya Livia au Editha.
***
Waandishi wa habari walimsogelea karibu Livia na kumuuliza kitu gani kinamliza ambapo Livia hakutaka kuongea kitu kuogopa kuchekwa na watu, akainuka na kuingia kwenye gari lake akalitoa kwa kasi na kuondoka zake huku akiwa analia sana. Baada ya kuona hakuna la maana tena habari zote wanazo watu wakatawayika na waandishi wa habari nao wakaondoka wakiwa na furaha ya kupata habari moto moto mjini.
***
Asubuhi yake ilipofika ilikuwa tafrani mjini, kwenye magazeti yote iliandikwa habari inayowahusu Livia na Editha bahati nzuri picha za Romeo akiwa na Editha walikuwa nazo hivyo ikawa rahisi kumuweka Romeo ukurasa wa mbele na kufanya watu wasiomjua nao wamjue mwanaume aliyewagombanisha hao wasanii ni nani.
"Wanawake akili hawana sasa hiki kitoto wanakipigania cha nini?" Alisikika akisema mwanamke mmoja.
"Wewe hujasikia maneno aliyosema Livia?" Aliuliza mwanamke wa pembeni yake wote wakiwa na magazeti yao mikononi wakisoma.
"Hapana kasemaje kwani maana humu sielewi naona wanaficha mambo"
"Humu magazeti ni sehemu ya wazi kila mtu anasoma hawawezi kuweka wazi vyote, ila shoga ingia Instagram huko kila kitu wazi yani video za kumwaga mwanzo hadi mwisbo wa tukio"
"Wee kumbe.. Ngoja niweke bando mie umbea usinipite"
Habari ikawa hiyo sasa watu walipoona kwenye magazeti hawaelewi kitu wakajaza bando kwenye simu zao na kuingia mitandaoni sasa. Video ya tukio lote mwanzo hadi mwisho watu wakaliona na kuwashangaa hao wasanii kwanini wamgombanie huyo mwanaume. Ila wadangaji nao walipagawa haswa! Kwanza wakaanza kuitafuta account ya Romeo wambea wa Instagram hawashindwi kitu, waliisaka hadi wakampata Romeo baada ya hapo sasa wakaanza kumfollow na wengine wakabeba picha zake, wapo waliofungua account na kuweka picha za Romeo wakijifanya ndio wao, Instagram ilichafuka hakukuwa na kingine ni Romeo tu na wadada nao wakajiapiza lazima waonje utamu wa Romeo.
"Jamani natangaza rasmi Romeo ni wangu, iwe kufa au kupona na nitapigana na ngedere yoyote yule akiingilia nampiga bastola afe huko kwa gharama yoyote lazima niwe na Romeo na atanioa nawaambia!" Ilionekana post moja ya mdada mzuri hatari mtoto wa mjini aitwae Alicia.
"Nyoo malaya wewe nasemaje mwaka huu tutauana ila na mimi Romeo lazima nimpate" ilionekana comment ya mdada akijibu kwenye hiyo post.
Mwendelezo hadi mwisho elfu moja. 0763361677,0719618409 jina lisa ntanga.

Post a Comment

0 Comments