Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Responsive Advertisement

PENZI LA MCHORA TATTOO-50



LATIFA NTANGA
0719618409
"Nisikilize mke wangu, naomba usilie mama yangu!" Alberto alimbembeleza mkewe na kumkumbatia Lisa asilie japo kuwa na yeye aliumia sana kuwa mbali na mke wake.
"Na..u..uu..miaaaa mume wangu!" Lisa kwa kilio cha kwikwi moyoni mwake alisikia maumivu makali sana kuwa mbali na mumewe.
"Najua mke wangu. hata mimi pia naumia sana kuishi mbali na wewe ila haina jinsi walichelewa kukubali maombi yangu ila wamekubali kipindi hiki naumia sana inatakiwa niondoka nikuache na mtoto wangu tumboni" Alisema Alberto kwa masikitiko makubwa sana Lisa alimuona jinsi mume wake alivyokuwa na huzuni, machozi yalimtoka sana kama maji alilia sana kazi ya Alberto ikawa kumbembeleza mke wake na kumfariji sana.
"Lisa mke wangu nyamaza kulia naomba uwe jasiri kwa kipindi hiki kigumu" Alisema Alberto akambusu mkewe.
"Nitajitahidi mume wangu naomba usinisahau" Alisema Lisa.
"Nazani utambua jinsi gani nakupenda mke wangu. Zaidi nampenda mtoto wangu ila nakuahidi lazima nirudi likizo nitakuja kabla haujajifungua lazima nimuone mwanangu mzuri nimbebe mkononi mwangu!" Alisema Alberto akamsogelea Lisa na kumbusu tumboni mwake na kufanya Lisa afarijike sana.
"Hebu inuka twende kwa wazazi nikawaage turudi uniandae mke wangu usilie bwana" Alisema Alberto akasimama na kumuinua mkewe ambaye mimba ilikuwa ndogo bado mwezi mmoja tu wakajiandaa na kutoka pamoja hadi nyumbani kwao na Lisa ambapo waliwakuta wazazi wote wawili wapo waliwasalimia kwa furaha baada ya hapo Alberto akawaaga, na wazazi hawakuwa na pingamizi walimtakia safari njema mkwe wao, baada ya hapo wakaondoka na kwenda nyumbani kwao Alberto na kuwaaga pia ambapo wazazi walishangaa sana safari imefika na Lisa ni mjamzito.
"Jamani lakini si ungewaambia wasubiri kwanza hadi mkeo ajifungue" Alisema mama yake Alberto.
"Mke wangu hujui sheria za kijeshi wewe utafanya mtoto wetu atafutwe na afungwe ataonekana analichezea jeshi ni lazima aende huyu" Alisema baba yake Alberto.
"Ni kweli mama naomba mmuangalie mke wangu mimi nitarudi" Alisema Alberto.
" Lisa ni binti yangu lazima niwe naye karibu kuhusu hilo ondoa shaka" Alisema mama yake Alberto na hawakutaka kukaa sana wakaaga na kuondoka huku Alberto alitakiwa safari njema na wazazi wake.
Baada yakutoka hapo wakapitia sehemu na kuagiza chakula wakala pamoja na kurudi nyumbani kwao, ambapo huko walioga na kuingia kitandani wakapeana haki zao baada ya hapo usingizi mzito ukawapitia na kulala hadi Alfajiri saa kumi na moja wakaamka pamoja na Lisa akamuandaa mumewe kwa kila kitu muhimu baada ya hapo wakatoka na gari lao na kuanza safari hadi Airport kwa sababu ndege ilikuwa inaondoka saa moja kamili asubuhi. Saa moja kasoro iliwakuta Airport tayari wakashuka na hawakuwa na mizigo mingi zaidi kibegi kidogo cha kishkaji alibeba Alberto baada ya hapo akamsogelea mkewe na kumkumbatia kwa nguvu sana. Lisa alilia sana na kumkumbatia mume wake bila kumuachia.
"Nakupenda mume wangu usinisahau baba nina mtoto wako tumboni" Alisema Lisa akiwa analia sana. Machozi yalimtoka kama maji na kumfanya Alberto apate kazi ya kumbembeleza mke wake.
"Nakupenda mke wangu niamini sikusahau mama yangu, trust me ilove you" Alisema Alberto na kumbusu Lisa akainama chini na kulibusu tumbo la mkewe.
"Nakupenda mtoto wangu nitarudi nitakubeba ukizaliwa" Alberto alimwambia mtoto aliyekuwa tumboni, Lisa alikuwa analia kwa kwikwi haswa! Moyo wake ulimuuma hakutegemea kama kuna siku atakuja kutengana na mwanaume aliyekuwa akimpenda sana, alijifikiria ataanzaje maisha ya peke yake bila Alberto hapo kilio kiliongezeka zaidi.
"Nisikilize mke wangu usilie bwana hujui jinsi gani machozi yako yanathamani kubwa sana kwangu nielewe" Alisema Alberto.
"Naumia mume wangu nashindwa kunyamaza" Alisema Lisa. Na Alberto akamkumbatia tena na kumsihi anyamaze muda nao ulikaribia wakasikia tangazo ndege anayotakiwa apande Alberto ipo tayari basi kazi ikawa kumuachia mke wake sasa. Lisa alimganda sana mumewe hakutaka amuache.
"Nisamehe mke wangu lazima niondoke" Alisema kwa masikitiko makubwa sana Alberto moyo wake ulimchoma kama pasi hadi alijuta kwanini alitaka kwenda kusoma jeshi nje ya nchi.
"Usiondoke mume wangu... Usiniache..tafadhali nakuomba baba baki usiende Alberto... Usiendeeeee...." Lisa alilia sana na kumuomba mumewe asiondoke. Huku nako tangazo lilizidi kusikika kwenye maspika humo ndani nakumfanya Alberto haone akichelwa tu ndege itaondoka, akasogeza mdomo wake karibu na wa mkewe akaunyonya kwa hisia kali sana baada ya hapo akajitoa kwa haraka mwili kwa Lisa na kutoka mbio hadi ndani akaingia sehemu ya ukaguzi.
"Mume waaaaanguuuuu....Alberto njooo....usiondoke mume wangu njooooooo....mtoto wako anakuhitaji njoo baba njoo..njoo!" Nguvu zilimuisha Lisa akakaa chini kabisa na kunyoosha miguu huku akilia sana kila aliyemuona hakika alimuhurumia sana wapo ambao walimsogelea wakamuinua na kumuingiza kwenye gari lake maana binadamu wa siku hizi wakiona tu tukio la huzuni hawachelewi kumrekodi na kupost mitandaoni.
Alberto baada ya kumaliza ukaguzi akaingia ndani ya ndege na abiria wenzake, hakika moyo wake ulimuuma sana na hata machozi yalimtoka sana kwa mara ya kwanza alijiona mwenye hatia kubwa kumuacha mkewe nakwenda mbali tena mbaya zaidi ni mwanamke aliyempenda sana, Lisa alikuwa ni kila kitu kwake moyo wake ulimuuma haswa kama mwanaume alishindwa kujizuia alilia sana kwa uchungu.
Hapa ndo mwisho kupost lipia elfu moja tu nikutumie mwendelezo hadi mwisho. 0719618409,0763361677 jina lisa ntanga.

Post a Comment

0 Comments