"Ayan unamaneno wewe!" Alisema Lisa na kucheka.
"Ila kweli mwanangu umezidi kuwa bonge yani umenenepa umekuwa mzuri sana" Alisema bi Lucy.
"Ha-hahaa mama bwana na wewe unamsapot Ayan" Alisema Lisa.
"Ni kweli lakini Lisa umebadirika naona Nairobi ulipapenda sana hata kurudi likizo Tz uligoma" Alisema Mzee Charles.
"Au ulipatwa mkwe uko nini?" Aliuliza kwa utani bi Lucy na kufanya Lisa acheke sana.
"Isije kuwa kweli maana sijasikia hata Romeo akitajwa dada amepata shemeji mwengine" Ayan alisema na kufanya Lisa acheke kwa nguvu zaidi.
"Hapa kuna ukweli na hili swala yani Lisa na Romeo wake nashangaa sijui imekuaje" Bi Lucy na yeye akasema. Lisa alikuwa akicheka tu bila kusema kitu.
"Jamani acheni kumtaja huyo mtu nishamsahau mie" Alisema Lisa.
"Heee makubwa hayo Lisa wa kumsahau Romeo kweli mh" Alishangaa bi Lucy.
"Mama usishangae Dada amepata shemeji mpyaaa oyooo" Alisema Ayan alikuwa muongeaji sana.
"Na kweli kaka yangu we subiri kula pilau la harusi" Alisema Lisa.
"Heeeee makubwa haya jamani yani Lisa ushapata na mume huko!"aliuliza kwa mshangao bi Lucy.
"Mmmmmh mama jamani!" Alisema Lisa na kucheka, Safari iliendelea huku stori mbalimbali wa kiongea na kucheka hadi walipofika kwenye ukumbi mmoja kwa nje magari yakaingizwa ndani na kuwekwa sehemu za parking baada ya hapo kila mmoja akashuka na kuingia ndani.
Walikaa pamoja na kupata chakula pamoja na vinywaji huku stori mbalimbali zikiendelea, siku hiyo walishinda hapo hapo hadi jioni ilipofika sasa ndio sherehe ikaanza rasmi ambapo Lisa alibadilishwa nguo na kuvaa gauni lefu hadi chini zuri lililomkaa vyema mwilini mwake. Alberto na yeye alivaa suti nzuri na kupendeza sana.
Basi sherehe ilianza hapo wageni walikuwa wengi sana kulichangamka haswa! Watu walikula na kunywa kwa furaha wakiwapongeza Lisa na Alberto kwa kumaliza salama masomo yao.
"Ila jamani mimi bado masomo mjue, hapa nasubiri majibu ya maombi yangu kwenye chuo ninachohitaji kwenda kujifunza ujeshi kwahiyo siku yoyote majibu yakitiki nasafiri" Alberto aliwaambia na kufanya watu washangae kumbe Alberto anataka awe mwanajeshi japo kuwa baba yake alikuwa tajiri mwenye pesa sana lakini hilo halikuwa tatizo kwake asiweze kutimiza ndoto zake, hata pale ambapo baba yake alimkataza asiende kwenye mafunzo aligoma na kukazania lazima awe mwanajeshi kwa sababu ndio kitu anachokipenda sana.
Sherehe iliendelea na watu walizidi kumpongeza Alberto kwa kuamua kuwa mwanajeshi na kulitumikia taifa.
Baada ya muda kwenda sana Alberto akaomba maiki na kusogea mbele.
"Mabibi na mabwana, wazazi wangu wote mliokusanyika hapa, ndugu zangu na marafiki zangu pamoja na majirani wote naomba niwajulishe kuna jambo moja la muhimu sana nataka lifanyike leo hii" Alisema Alberto nakufanya watu washangae kuna jambo gani tena hilo.
"Nashukuru siku ya leo kujumuika pamoja hapa najua kwaajili yetu mimi na Lisa ndio maana nyinyi mpo hapa nashukuru sana lakini pia na mimi nina jambo langu la muhimu sana lazima lifanyike leo hii, kwanza Lisa sogea karibu yangu" Alisema Alberto na Lisa akatabasamu na kumsogelea Alberto ambaye alimkumbatia kwa nguvu bila kujali uwepo wa wazazi wao hapo ukumbini. Walikumbatiana sana na bila kujali Alberto alimbusu Lisa mdomoni.
"Tobaaaaaaaaaaaa!" Alishangaa bi Lucy akimuangalia mume wake ambaye alibaki kutoa macho na yeye akishangaa tu.
Hapo hapo bila kuchelewa, Alberto akaingiza mkono mfukoni kwake na kutoa kiboksi chenye Pete akapiga goti moja chini nakumshika mkono Lisa akafungua kiboksi hiko na kutoa Pete nzuri ya dhahabu iliyonakshiwa na madini ya Almas.
"Lisa will you marry me?" Aliuliza Alberto. Lisa hakuweza kujibu machozi yalimtoka sana kwa sababu hakutegemea, Alberto hakujali hapo hapo akamvalisha Pete Lisa na akasimama na kumkumbatia kwa nguvu na kufanya Lisa aangue kilio zaidi.
"Jamani natangaza rasmi Lisa ni mke wangu mtarajiwa" Alberto alisema akiwa amemkumbatia Lisa ambaye hakuweza kujizuia alilia kwa sauti.
"Weweeeeee.....oyoooooo...pa..pap...apaaa!" Ayan alisimama na kushangilia kwa nguvu huku akipiga makofi sana, tena akatoka mbio na kwenda mbele akawakumbatia dada yake na shemeji yake kwa furaha sana.
"Sasa dada unalia nini wakati umepata shemeji jamani?" Aliuliza Ayan na kumfanya Lisa acheke sana na kuacha kulia, wazazi wote wakasogea mbele na kuwakumbatia watoto wao na kuwapongeza sana kwa kitendo kizuri walichoamua kukifanya.
"Nimefurahi sana kuona Lisa amekuwa na mahusinao na Alberto" Alisema Mzee Charles.
"Hataa mimi mume wangu nimefurahi sana kwa sababu Alberto ni msomi anajielewa hawezi kumuumiza Lisa kabisa" Alisema bi Lucy.
"Ni kweli kabisa tuwaombee heri" Alisema mzee Charles.
"Amina"
Waliongea mengi, wazazi wake Alberto na wao walifurahi sana na jambo hilo wakampokea Lisa bila kinyongo walimpenda sana, sherehe iliendelea vizuri siku hiyo hadi usiku sana ikaisha na kila mmoja akaondoka na kurudi kwao. Tangu siku Lisa na Alberto wakawa huru na mapenzi yao kwa sababu pande zote mbili waliujua uhusiano wao, Alberto akaamua kupeleka posa nyumbani kwao Lisa na majibu wakapewa baada ya hapo ikafanyika sherehe ya kumuaga Lisa na siku ya ndoa ikafika sasa.
Ilikuwa siku ya furaha sana si kwa Lisa wala Alberto walikuwa na furaha sana, hatimaye ndoa ikafungwa salama bila kizuizi chochote kile, ilikuwa furaha sana kwao. Baada ya hapo wakapanga fungate yao wakaifanyie kwenye visiwa vya karafuu Zanzibar na kweli baada ya ndoa tu wakapanda boti na safari ya Zanzibar ikaanza, walikaa huko kwa mwezi mzima wakifurahi mapenzi yao baada ya hapo wakarudi nyumbani kwao Lisa akiwa ni mjamzito tayari. Furaha ilitawala sana kwenye ndoa yao, ila wakati wa furaha na Huzuni ipo karibu Alberto alipokea simu ya kupokelewa maombi yake kwenda kusoma nje ya nchi na alitakiwa kesho yake asafiri ilikuwa habari mbaya sana kwao Lisa hakutegemea alilia sana.
0 Comments