LATIFA NTANGA
0719618409
Alberto alilia haswa, hadi pale sauti iliposikika ya mhudumu wa ndege akitangaza abiria wote wajifunge mkanda ndege inataka kuruka alichokifanya Alberto alienda chooni akanawa uso baada ya hapo akarudi kwenye siti yake na kufunga mkanda tayari kwa safari huku moyoni mwake akiwa na majonzi sana. Hatimaye ndege ikaanza kupaa na kuiacha ardhi ya Tanzania. Moyo wa Alberto ulikuwa kwenye maumivu makali sana kila alipomfikiria mke wake aliumia sana moyo wake, safari ilianza na alitakiwa apige moyo konde sababu alikuwa mwanaume na yeye mwenyewe ndio alipenda awe mwanajeshi hakuna mtu aliyemlazimisha hakuwa na budi zaidi ya kukubali matokeo.
Safari ilikuwa ya kuchosha sana walitumia masaa mengi angani huku akili ya Alberto ikiwa haipo sawa kabisa, hatimaye baada ya masaa mengi safari yao ilifika mwisho. Sababu hakuwa na mizigo mingi Alberto alibeba vizuri kibegi chake kidogo na kutoka nje akiwa pamoja na abiria wenzake. Alipotokeza nje tu alimuona mwanaume mmoja amevalia mavazi yakijeshi akiwa na bango dogo limeandikwa jina lake kwa herufi kubwa.
ALBERTO
Alimsogelea yule mwanajeshi akamsalimiana nae kwa uchangamfu mkubwa, baada ya hapo wakatoka nje ya uwanja pamoja na kuingia kwenye gari moja wapo la kijeshi safari ikaanza huku wote wakiwa kimya.
Safari ilikuwa ndefu sana yenye kumchosha Alberto ila hakutaka kuuliza kitu alikaa kimya tu, gari lilizidi kusonga mbele na kupita nyumba nyingi mwisho wakaingia ndani ndani ya mji kama maporini gari lilizidi kusonga mbele tu. Hatimaye wakatokea kwenye jangwa kubwa sana ambapo jua kali linawaka sshemu zote hakuna hata mti mmoja walisonga mbele na kufika katikati ya jangwa. Hapo sasa gari likasimama na yule mwanajeshi akamwambia Alberto ashuke ambapo alikuwa akishangaa tu gari limesimama jangwani hakuna hata nyumba moja. Ila alikaa kimya bila kusema kitu, yule mwanajeshi akawa mbele na Alberto nyuma kama kondoo akimfuata tu. Walitembea umbali mrefu kidogo sehemu moja yule mwanajeshi akasimama na kuinama chini kuna sehemu kama kulikuwa na kitu akakibonyeza hapo hapo hiyo sehemu chini ikafunguka, na ghafla uwazi ukaonekana. Akaanza yule mwanajeshi kuteremka chini ambapo kulikuwa na ngazi akashuka na Alberto hakutaka kusubiria na yeye akashuka wakateremka wote hadi chini kabisa na ule uwazi ukajifunga juu. Ndani kulikuwa giza sana na Alberto alitegemea kuona wameingia chini kwenye shimo ila ilikuwa tofauti. Mwanajeshi alienda kwenye swichi nakuwasha hapo hapo ndani kukawa na mwangaza na kumfanya Alberto ashangae jinsi kulivyo. Ilikuwa ni kama pepo ndogo vile, kulikuwa kuzuri sana humo ndani kuna sehemu umewekwa msitu wa kutengeneza na ndani yake kuna wanyama mbalimbali, pia kulikuwa na kompyuta nyingi sana kila sehemu ambapo ilikuwa kama ofisi, hiyo haitoshi kulikuwa na gym sehemu ya mazoezi ya kisasa sana na trainer alikuwepo mwanaume mtu mzima kiasi amekomaa sana anasura ngumu haswa! Tofauti na hapo kulikuwa na sehemu ya chakula wapishi wengi walikuwepo humo kwenye hiyo restaurant ndogo kiasi lakini nzuri yenye vyakula mbalimbali. Alberto alikuwa akishangaa kila anachokiona. Basi yule mwanajeshi alizidi kusonga ndani na kumpa nafasi Alberto aweze kujionea jinsi humo ndani kulivyo. Hatimaye wakafika kwenye chumba kimoja, yule mwanajeshi akagonga mlango na hapo hapo ukafunguliwa na wakaingia ndani.
Macho yao yalitua kwa mwanaume wa makamo mrefu kiasi mwenye mwili uliojaa vizuri, hapo wote wakapiga saluti kama heshima kwa huyo mwanaume ambaye alikuwa ni mkubwa wao, baada ya hapo yule mwanajeshi akaondoka zake na kumuacha Alberto ambaye alikaribishwa akae kwenye kiti baada ya hapo akaombwa akabidhi kila kitu chake
"Sheria za hapa, ukifika hairuhusiwi kutumia chochote yani humu ndani kila kitu ni cha humu humu hakitoki nje pia mafunzo ni miaka minne hadi umalize hakuna likizo" Alisema huyo mkuu wa jeshi akiwa siriasi hacheki, na kumfanya Alberto kijasho chembamba kimtoke. Na hakukuwa na ushauri wala kusubiria jibu Alberto aliombwa akabizi kila kitu baada ya hapo akapewa jezi maalumu za kuvaa humo ndani pamoja na za mafunzo baada ya hapo akatolewa ofisini kwa mkuu wa jeshi na kupelekwa hadi kwenye vyumba ambavyo wanajeshi wanaishi humo. Mawazo yalimjaa Alberto sheria alizokutana nazo hakuzitegemea kabisa, alitamani japo aongee na mkewe amueleze kama amefika salama safari yake ila hilo halikuwezekana, Alberto aliumia sana moyo wake. Yani haishi miaka minne bila kuonana na familia yake lilikuwa jambo gumu sana.
0 Comments