Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Responsive Advertisement

PENZI LA MCHORA TATTOO-52



LATIFA NTANGA
0719618409
Maisha magumu na ya upweke mkubwa alianza Alberto! Yalikuwa zaidi ya mateso kwake, tofauti na mategemeo yake akifika atawasiliana na mke wake na kumjulisha kama amefika salama pamoja na kumuondoa hofu, ilikuwa tofauti kabisa, alitakiwa akabidhi kila kitu ofisini kwa mkubwa wake wa kazi baada ya hapo alipewa mavazi mengine pamoja na simu ambayo ilikuwa na mawasiliano ya hapo alipokuwepo pekee haikuwezekana kuwasiliana na watu waliokuwa nje ya eneo alilokuwa. Siku ya kwanza ilipita kwa unyonge mkubwa sana, hatimaye siku ya pili ikafika sasa, Alberto akaanza mafunzo yake rasmi akiwa chini ya kiongozi wake aliyekuwa na sura ngumu sana hacheki muda wote yupo siriazi hakuwa na mzaha kabisa! Mafunzo yalikuwa makali na magumu haswa hakuna kuoneana huruma wala kudekezana. Alberto alikoma na kukomaa, alijuta sana kwa kazi aliyoichagua muda mfupi tu alikuwa na alama kibao mwilini mwake, alichubuka kuna sehemu walikimbia msituni alijichoma na miba nakuumia sehemu mbalimbali ule mwili wake mzuri wa mahaba uliharibika haswa na kuwa kama kituko! Aliteseka usiku na mchana kuna muda walikuwa wanashinda asubuhi hadi jioni bila kula kitu huku wakifanya mazoezi magumu sana.
Hatimaye mwaka wa kwanza ukapita Alberto akiwa mafunzoni bila kuwasiliana na wazazi wake wala mke wake. Mwaka wa pili ulipofika sasa Alberto alikuwa ameshazoea mazoezi nakuwa mwepesi sana alijitahidi haswa na kujikuta akipendwa na kiongozi wake kutokana na juhudi zake.
"Uko vizuri sana jitahidi mwaka ujao unarudi nyumbani!" Alisema kiongozi wake Alberto na kumfanya afurahi sana na kujisikia furaha sana moyoni mwake.
***
Lisa alibaki Airport akilia hadi pale alipoona ndege aliyopanda mume wake imeondoka hakuwa na budi zaidi ya kumuombea mume wake safari salama, baada ya hapo akaliondoa gari na kurudi nyumbani kwake akiwa mnyonge sana. Tofauti na mategemeo yake mumewe akifika kambini atamtafuta ilikuwa tofauti kabisa, Alberto hakumtafuta kabisa wala hakumjulisha kama amefika salama safari yake. Lisa aliumia sana siku hiyo alishinda akiwa mnyonge na kulia hadi siku ya pili ilipoingia na kumalizika hakupata simu ya Alberto, Lisa alishindwa kuvumilia akawapigia simu wakwe zake.
"Mama Alberto amewasiliana na nyinyi?" Aliuliza Lisa pale mama mkwe wake alipopokea simu tu bila salamu.
"Hapana mwanangu sijapata simu ya Alberto kuna nini kwani?" Aliuliza huyo mwanamama.
"Mama....naumia!" Alisema Lisa na kushindwa kujizuia akaangua kilio kikubwa kama amefiwa.
"Kuna nini Lisa upo sawa kweli?" Aliuliza huyo mama.
"Hapana mama, Alberto sijui amekumbwa na kitu gani hajanitafuta sijui amefika salama au vipi!" Alisema Lisa na kulia.
"Nyamaza mwanangu, subiri tutafuatilia kesho tujue kipi kimemkuta" Alisema huyo mama na kumbembeleza Lisa hadi alipokuwa sawa wakaagana.
Lisa hakuridhika akampigia simu mama yake.
"Mama...Alberto hajanitafuta hadi leo sijapata hata meseji yake sijui amefika salama au ameku..." Alishindwa kumalizia akaangua kilio kikubwa Lisa na kumshtua mama yake.
"Mwanangu hebu nyamaza kwanza, usilie subiri Lisa nakuja sasa hivi" Alisema huyo mama japo kuwa ulikuwa ni usiku lakini hakujali hilo aliinuka akajiandaa na kutoka na baba yake Lisa hakuwepo alikuwa amesafiri kikazi basi mama Lisa alijiandaa na kutoka hadi nje akaingia kwenye gari na safari ikaanza ya kwenda nyumbani kwa Lisa, alifika salama na kumkuta mwanae amejiinamia akilia sana.
"Nyamaza mwanangu, usilie unajua hali yako hupaswi kulia kabisa" Alisema bi Lucy.
"Mama hujui jinsi gani naumia...mume wangu hata simu kupiga ameshindwa kweli?" Alisema Lisa kwa sauti ya kilio.
"Najua inauma mwanangu wewe nyamaza sawa!"alisema huyo mama.
"Nashindwa mama naumia" Lisa alizidi kulia na kumpa kazi mama yake ambaye alimbembeleza hadi alipokuwa sawa.
"Sasa sikia hapa tunaondoka wote twende tukaishi nyumbani hadi pale mumeo atakaporudi" Alisema bi Lucy na hakutaka mjadala alisaidiana na Lisa wakabeba vitu muhimu baada ya hapo wakapakia kwenye gari na safari ikaanza kurudi nyumbani kwa wazazi wake Lisa. Siku hiyo ilipita na kesho yake mapema wazazi wake Alberto walienda hadi kwenye ofisi na shirika la ndege aliyopanda Alberto walienda kuulizia labda ndege ilipotea angani ila majibu walipata mazuri ndege ilifika salama, swali walilojiuliza ni kwanini Alberto alishindwa kuwapa taarifa nyumbani kwao kama amefika.
"Kwani alienda kufanya nini huko nje ya nchi?" Aliuliza mwanaume mmoja mfupi, mnene anakitambi kikubwa.
"Alienda kambini" Alisema mama yake Alberto.
"Oh kwenye mafunzo ya kijeshi eeeh?" Aliuliza huyo mwanaume mfupi huku akijikuna kidevu chake kilichovimba kama andazi.
"Eeeh ndio" Alijibu huyo mama.
"Sasa mbona jambo jepesi tu mmeshindwaje kujua sasa kule akifika anakabidhi kila kitu ofisini haruhusiwi kutumia chochote kile hadi baada ya miaka minne ndio anarudi nchini kwao akiwa mwanajeshi kamili tena mwanajeshi haswa ambaye haogopi kitu maana mazoezi yao nikienda mimi na kitambi changu hiki wiki nyingi nakuwa na six pack ha-ha-ha-ha"
"Eti Unasemaje?" Aliuliza kwa mshtuko mama yake Alberto.
"Mama kama ulivyosikia huyo hawezi kuwasiliana na nyinyi hadi miaka minne ipite ndio arudi Tanzania" Alisema babu kitambi na kufanya mama yake Alberto apandwe na presha.
Mwendelezo elfu moja. 0763361677,0719618409 lisa ntanga.

Post a Comment

0 Comments