Alipoambiwa hivyo, si akakumbuka kwamba Doreen alimpatia simu ambayo mpaka muda huo hakumuonesha fundi Yassin akajikuta akiachia tabasamu lililoonwa na fundi.
“Vipi naona umefurahi!” fundi Yassin alimwambia.
Kutokana na kauli hiyo, kumzuga fundi wake, Dullah alimwambia alimfurahisha sana alipomwambia atakapoanza kwenda kwenye site nyingine wataenda wote.
“Ndiyo hivyo, siwezi kukutupa mdogo wangu,” fundi Yassin alimwambia Dullah bila kujua mwenzake alifurahi kukumbuka alikuwa kapewa simu ambayo ingemsaidia kuwasiliana na mpenzi wake Doreen.
Wawili hao walipotosheka kwa kinywaji waliondoka na kuelekea nyumbani, walipokaribia Dullah alimwambia fundi wake kwamba anakwenda kumsalimia rafiki yake Ipyana ambaye hakuonana naye kama siku nne hivi.
“Dogo ukiwa na hela hutulii, au unakwenda kuongeza mbili za kulalia nini?” fundi alimwuliza.
“Hapana, naenda tu kumwona mshkaji wangu huenda atanipa mchongo wa kazi maana kuanza kushinda nyumbani bila kazi kwa mtoto wa kiume haipendezi,” Dullah alimwambia.
Kutokana na maneno ya Dullah , fundi alimfagilia na kumweleza alikuwa na mawazo mazuri, akamwambia waonane kesho jioni ili ajue alifikia wapi.
“Poa bro wangu, kanisalimie shemeji yangu,” Dullah alimwambia.
Walipoachana, kijana huyo alikwenda kwenye genge la Chinga akamwambia amkatie tango, Chinga akamtania kwamba mambo yake yalikuwa mazuri maana kila jioni alikuwa akipasha kilaji.
“Hamna bwana, rafiki yangu kanipa tubia tuwili sasa kwenda homu na harufu ni so kwa washua,” Dullah alimwambia wakati huo alikuwa akila ndizi mbivu.
Alipoamliza kula ndizi na tango akaenda nyumbani kwa akina Ipyana na kumkuta akiwa ameketi kwenye moja ya mairi ya gari waliyoyafukia ardhini nyumbani kwao kuzuia magari yasipite.
Marafiki hao walipoona walifurahi sana, katika maongezi yao Dullah alimsimulia kila kitu Ipyana kuhusu kule site na alivyosimamishwa kwenda.
“Da! Wewe kweli balaa, siku mbili tu za kwenda site umempata mtoto wa kishua na kakupa hadi simu, kijana unatisha,” Ipyana alimfagilia Dullah .
“Si ujuaga mambo yangu, mimi huwa sirembi hata siku moja, sasa unafikiri mtoto kajipendekeza mwenyewe mara sijui maziwa, mayai sijui mazagazaga gani, sasa ukimuacha mtoto kama huyo si utapata dhambi za bure kaka!” Dullah alimwambia Ipyana wakaishia kucheka.
Baada ya mazungumzo, Ipyana alimwuliza Dullah kama anaweza kujitoa ufahamu ili siku iliyofuata waongozane kwenda Posta kufanya kazi ya kuosha magari ya wafanyakazi wa serikali, wafanyabiashara na mabosi mbalimbali.
“Kaka kwa hali ilivyo sasa sichagui kazi kinachotakiwa ni kupata fedha tu, wewe unafikiri kama nisingeenda na fundi Yassin kule site ningempaje mtoto wa kishua Doreen aliyenipa hii simu kali?” Dullah alimwambia Ipyana, wakacheka.
“Kama ndiyo hivyo basi poa sana, wewe si unaona jinsi geto langu lilivyo na kila kitu cha maana na ninavyopiga pamba za kishua, kazi ya kuosha magari kaka!” Ipyana alimwambia Dullah .
“Hivi kazi ya kuosha magari inalipa eh?” Dullah alimwuliza.
“Kaka acha, kwa siku mimi kurudi homu na shilingi thelathini mpaka hamsini ni jambo la kawaida, halafu kule dili zipo kibao mfano bosi anaweza kukutuma sehemu ukirudi anakupa teni au zaidi,” Ipyana alimwambia Dullah aliyeishia kushangaa.
“Ipyana bwana si ungeniambia muda mrefu si nami saa hizi si ningekuwa na geto kali kama lako na watoto wakali wangenikoma?” Dullah alimwambia.
Ipyana alicheka sana na kumweleza kwa jinsi alivyokuwa akimuona sharobaro alijua asingeweza kufanya kazi ya kuosha magari ndiyo maana hakumwambia.
“Kaka kama ndiyo hivyo kesho mimi na wewe mguu na njia hadi Posta, kweli jambo usilolijua ni sawa na usiku wa giza, kumbe kila siku unapiga hela ya maana namna hiyo?” Dullah alimwuliza Ipyana.
“Ndiyo hivyo, kikubwa ni kuchakarika tu, wewe kesho twende nikakufundishe kazi,” Ipyana alimwambia.
Baada ya kukubaliana siku iliyofuata kwenda Posta, waliagana ndipo Dullah akaenda kwao na kuwakuta wazazi wake wakiwa wanamalizia kula, walisalimiana kisha akaenda kuoga.
Kwa kuwa valikuwa ameshiba, mama yake alipomwuliza suala la msosi alimwambia kuna sehemu walipitia na fundi Yassin wakala ndipo mama mtu akamwuliza kuhusu kazi.
Aliwaambia ilikuwa nzuri kisha akaenda chumbani kwake akachukua shilingi elfu kumi na tano na kumkabidhi mama yake akamwambia kesho yake anunue mboga.
Wazazi wake walifurahi sana, baba alimsifia na kumwambia kweli alikuwa amekua na kumwuliza aliona faida ya kujishughulisha, akamwambia aliiona.
“Hivyo ndivyo kijana unatakiwa kuwa, wewe unafikiri nisingeshauri utafute kazi ya kufanya leo hii ungempatia mama yako hela ya kukununua mboga, safi sana tena sana,” baba yake Dullah mzee Reli ya Uhuru alimwambia.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Dullah aliwashukuru wazazi wake kisha aliwaaga kwamba alihisi uchovu hivyo anakwenda kulala, wakampa pole na kumtakia usiku mwema akaenda chumbani kwake bila kuwaambia kama fundi Yassin alimwambia asiende site.
“Hawa siwaambii chochote kuhusu ishu ya site, kukicha kesho naenda Posta ila nikitoka huko ndipo nitamwambia mama,” Dullah aliwaza.
Akiwa chumbani, alichukua simu aliyopewa na Doreen, akaweka kadi yake na kuiweka kwenye chaji huku akiwa mwenye furaha kwani hakutegemea kama angepata simu siku za karibuni.
“Tena ikipata chaji kidogo mtu wa kwaza kumpigia atakuwa Doreen, halafu nitampigia Atu na yule demu niliyekutana naye siku ya kwanza wakati tunaenda site,” Dullah aliwaza.
Kijana huyo akiwa kalala chali huku kava bukta pekee, alimlaani sana Zakayo kwa kumchongea kwa fundi Yassin na kusababisha kusimamishwa kufanya kazi kule site.
“Ningekuwa mchawi ningemrogelea mbali Zakayo aanze kuumwa na kurudishwa kijijini kwao, au ningekuwa namiliki bastola ningempiga risasi za kichwa afie mbali kwa roho yake mbaya,” Dullah aliwaza.
Baada ya kutumia dakika kadhaa kumfikiria Zakayo, alipitiwa na usingizi hadi alipokuja kushtuka ilikuwa saa tano, alipoiangalia simu akakuta imejaa chaji fulu akaamua kumbipu Doreen.
Dullah alifurahi sana alipobaini Doreen alikuwa hewani, akiwa katika hali hiyo simu yake ikaanza kuita na mpigaji alikuwa Doreen akapokea.
“Sema mpenzi wangu, nimefurahi kweli ulivyonibip maana tangu nilipopanda kitandani mawazo yangu yote yalikuwa kwako, si unajua tena ulivyouteka moyo wangu kwa muda mfupi?” Doreen alimwambia.
“Hunishindi mimi, yaani kila nikikumbuka joto lako, mahaba yako na hizo embe zako zinazoshika vizuri, nimeshindwa kulala na simu ilipojaa chaji nikaamua kukupigia, yaabu d sijui nikwambieje,” Dullah alimwambia Doreen.
Wawili hao walizungumza kwa muda mrefu kisha Doreen akamwuliza kama simu yake ilikuwa na vocha ya kutosha, Dullah akamwambia alinunua ya mia tano.
“Ngoja nikutumie muda wa maongezi wa kutosha ili tuchati hadi kuna kucha,” Doreen alimwambia.
Kama alivyomuahidi, baada ya kukata simu hazikupita hata sekunde 50 Dullah alisikia mlio wa ujumbe alipofungua akaona ametumiwa muda wa maongezi wa shilingi elfu tano.
“D, asante sana, haya niambie kitu kizuri sana nifutahi usiku huu,” Sharobaro Dullah akamwambia.
“Kitu kizuri ni kwamba nakupenda sana natakamani hata muda huu tungekuwa wote hapa kitandani ukinifanyia mambo yote mazuri ya kunipa raha,” Doreen alimjibu.
“Jamani mpenzi wangu, kwa kuwa uko mbali nami ndiyo hivyo, kama hutajali tukutane hapo kwa njia ya meseji,” Dullah akamwambia Doreen kupitia meseji.
Doreen ambaye alikuwa akipenda sana kuchati alimwambia sawa ndipo sharobaro Dullah akaanza kumvurumishia meseji za kimahaba zilizomchanganya mtoto wa kishua na kujikuta yuko hoi.
Doreen alipomwambia Dullah kwamba alikuwa anajisikia ovyo, kijana huyo akaamua kumpigia wakaanza kuzungumza mambo ya malovee na kuhamasishana hadi Doreen akafikia kilele cha mlima wa Kilimanjaro kupitia simu zao.
Kufuatia Doreen kufika kilele cha mlima, alimfagilia sana Dullah kwa kujua kutumia simu yake maana ilikuwa kama walikuwa wotelaivu, Dullah naye alimshukuru kwa ushirikiano wake, kisha waliagana kwamba wangekutana kesho yake.
Dullah alimwambia poa lakini hakutaka kumweleza kuhusu fundi Yassin kumzuia kwenda site, alipanga kumpigia simu mishale ya saa tatu ya siku iliyofuata kumweleza jambo hilo.
Kutokana na uchovu, msichana huyo akiwa kama alivyozaliwa akapitiwa na usingizi hadi aliposhtuka saa kumi na moja alfajiri, alipojiangalia na kukumbuka kilichojiri baina yake na dullah wakati wakichati akaishia kutabasamu.
Doreen alipoachia tabasamu, akajikuta akijisemea moyoni:
“Mh! Huyu Dullah ni balaa, tukikutana laivu ni moto na kwenye simu pia ni moto zaidi!” Doreen aliwaza.
Msichana huyo aliyekuwa amekolezwa na penzi tamu na sharobaro Dullah aliendelea kumfikiria kijana huyo hadi alipopitiwa tena na usingizi.
Kulipokucha alimsikia Anne akiwa bize kufanya usafi akajiuliza amwambie kuhusu uhusiano wake na Dullah au ampotezee kuhofia huenda naye angelitamani penzi la kijana huyo kutoka Tandale.
“Haina haja, kama atahisi halafu akiniuliza nitamwambia lakini nitampiga mkwara asimzoee na kumtishia siku nikimbamba anajicheketua kwa Dullah ndiyo utakuwa mwisho wa kufanya kazi,” Doreen aliwaza.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Anne alipomaliza kufanya alijiandaa akanywa chai kisha alimuaga Doreen aliyekwishaamka akaelekea chuo, huku nyuma Doreen akawasha runinga na kwenda kukaa sebuleni.
Binti huyo wa kishua alichukua simu yake na kumpigia Dullah kwa lengo la kumjulia hali na kujua muda ule walikuwa wako wapi, cha kusikitisha hakupatikana hewani.
“Huyu atakuwa hajawasha simu yake, ngoja nimsubiri,” Doreen alijisemea moyoni.
Akiwa katika hali hiyo ya kusubiri, akasikia kengele ya getini ikilia akaachia tabasamu, akiwa kava pensi iliyoishia juu ya mapaja yake iliyombana na kuzifanbya hipsi zake zionekane vyema na singilendi iliyozionesha vyema chuchu zake akatoka kwenda kufungua.
Alipofungua akamuona Zakayo, almanusura asonye lakini akapotezea na kumsalimia kisha msaidizi huyo wa fundi akaingia ndani, Doreen akafunga geti na kurudi sebuleni bila kuzungumza zaidi na Zakayo.
“Huyu mtoto jamani kaumbika, sema tu ni haya mambo ya kazi, maana ukijifanya kidume halafu baba yake agundue hakika utalambwa shaba na maiti yako isionekane milele,” Zakayo alijisemea moyoni.
Kule ndani,Doreen alizidi kumuwaza Dullah kwani alitamani sana kumuona ndipo akasikia tena kengele ya getini ikilia, akatoka mbio kwenda kufungua akiwa na imani alikuwa fundi Yassin na Dullah kwani walikuwa na kawaida ya kufika pamoja.
Alipofungua akakutana na Haruni, kama ilivyokuwa awali alitamani kutoa msonyo akajizuia, Doreen akamsalimia ndipo kijana huyo licha ya kumtamani Doreen kwa jinsi alivyokuwa kanona, hakuthubutu kumwangalia mara mbili wala kusema chochote zaidi ya kuelekea eneo la kazi.
Kitendo cha fundi Yassin na Dullah kutowasili, kilimkosesha raha binti huyo wa kishua, hata hivyo hakukata tama kwa kuhisi huenda foleni ilichangia kuchelewa.
Doreen alikwenda mezani akamimina maziwa ya moto kwenye kikombe akachukua na soseji mbili na kurejea sebuleni kusubiri kusikia kengele ya getini ikilia.
Alipokunywa mafunda mawilina nusu soseji, akasikia kengele, aliachia tabasamu pana kwani alikuwa akijua sasa Dullah wake kawasili, akatoka na kwenda kufungua geti, badala ya kumuona Dullah akamuona fundi Yassin.
“Shikamoo fundi!” alimsabahi.
“Marahaba,hujambo Doreen?” fundi Yassin alimsalimia.
“Sijambo!” msichana huyo alimsalimia.
Fundi akiwa ameingia ndani, Doreen alimwuliza Dullah alikuwa wapi akamwambia siku ile asingefika, jibu la fundi lilimnyong’onyesha binti huyo wa kishua aliyemuuliza alikuwa na tatizo gani.
Fundi Yassin hakutaka kumwambia ukweli akamdanganya kwamba alimweleza hakujisikia vizuri nahisi kutokana na uchovu wa kazi, kauli hiyo ilimfanya Doreen kumuonea huruma mpenzi wake.
“Jamani pole yake,” msichana huyo alimwambia fundi Yassin kisha akafunga geti na kuelekea ndani kwao akiwa hana raha.
Akiwa ameketi kwenye sofa alijaribu kumpigia simu Dullah lakini hakupatikana ndipo kwa hasira akaenda chumbani kwake na kujitupa kitandani na kuendelea kumuwa za Dullah .
Wakati Doreen akiwa katika hali hiyo, asubuhi Dullah alikwenda nyumbani kwa rafiki yake Ipyana aliyemkuta akimsubiri na baada ya salamu walikwenda kituoni walikopanda daladala la Posta.
Kama ilivyokuwa kawaida ya sharobaro Dullah kupenda mademu, alikuwa akimtazama kwa matamanio sistaduu mmoja aliyekuwa amesimama naye karibu kwa sababu wote walikosa siti.
Kufuatia kumkazia sana macho, mrembo huyo akawa anaangalia pembeni kwa aibu jambo lililompa nguvu Dullah ya kuendelea kumtazama. Kila mrembo alipomtazama Dullah macho yao yaligongana mwishowe mtoto wa kike akaachia tabasamu.
Gari lilipofika Keko Fenicha, abiria waliokaa siti ya karibu yao waliteremka ndipo Dullah na yule mrembo wakaichangamkia siti hiyo, walipokaa tu Dullah akamsabahi yule dada.
“Mambo vipi mrembo?”
“Poa, ila wewe mkaka ni mchokozi sana, unajua ilibakia kidogo nicheke kwa ulivyokuwa ukinitazama,” yule mrembo alimwambia Dullah .
“Utanisamehe, na wewe si umezidi kuwa mrembo?” Dullah alimfagilia yule mrembo aliyeishia kutabasamu.
“Acha masihara yako, hivi kwa mfano warembo miamoja wakipanga mstari na mimi naweza kuwemo?” yule dada aliyeonekana anapenda sana stori alimwuliza Dullah .
“Siyo mia moja, hata wakiwa kumi wewe lazima uwe wa tatu,” Dullah alimfagilia.
Alipoambiwa hivyo, yule dada alicheka na kumwambia haya bwana kama ni kweli kisha akamwambia akumbuke kama angekuwa mrembo wala asingepanda daladala.
Dullah alicheka na kumfahamisha kila kitu na wakati wake, hivyo awe na subira gari lake lilikuwa njiani kutoka Ulaya.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Da! Wewe kaka una maneno sana, eti gari langu linakuja kutoka Ulaya haya bwana kama maneno yako yawe ya heri,” yule mrembo alimwambia Dullah , wakacheka.
Kwa kuwa asubuhi hiyo hakukuwa na foleni, kufumba na kufumbua wakajikuta wapo Mnazi Mmoja, kama kawaida Dullah aliona atafanya kosa kubwa asipoomba namba ya simu ya yule mrembo.
“Unahitaji namba yangu ya nini?” mrembo alihoji.
“Si gari lako likifika nikupigie uje ulichukue!” Dullah alimwambia.
Mrembo alicheka sana na kufuatia ucheshi wa sharobaro Dullah , akajikuta akimuomba kijana huyo ampatie simu yake ndipo Dullah aliiotoa akaiwasha na kumpatia, akaaindika na kumwambie asevu jina la shangazi.
“Unaitwa shangazi au unapenda niwe nakuita hivyo?” Dullah akamwuliza.
“Ndiyo jina langu, wengi wanapenda kuniita Aunt lakini wewe niite shangazji,” yule mrembo alimwambia Dullah bila kujua asingeweza kumaliza muda mrefu bila kuingia kwenye kumi na nane za kijana huyo mpenda mademu wazuri.
“Sawa, lakini mimi nitakuwa nakuita Aunt,” Dullah alimwambia, wakacheka.
Gari lilipofika Posta, yule wote waliteremka ambapo yule mrembo alisema anakwenda Masaki ndiko alikokuwa akifanya kazi, walipoagana Ipyana akamfagilia Dullah kwa ushapu wake mpaka kuozoeana na yule mrembo kwa muda mfupi.
“We acha tu ndugu yangu tena mpaka namba yake kanipa,” Dullah alimwambia Ipyana.
Ipyana ambaye hakuwa mpenzi sana wa mambo ya wasichana akaishia kucheka, wakati marafiki hao wanaelekea kwenye ofisi za wizara moja ambayo Ipyana alikuwa akifanya ujasiriamali wa kuosha magari, Dullah alikumbuka akuzima simu baada ya kusave namba ya yule mrembo, akaizima.
Alifanya hivyo kuhofia kupigiwa simu na Doreen ambaye hakutaka kabisa kuzungumza naye muda huo, kwa kuwa ofisi hizo za wizara hazikuwa mbali, waliwasili ndipo Dullah akashangazwa na jinsi wafanyakazi wa serikali na madereva walivyomchangamkia Ipyana.
“Dogo vipi hujambo?” dereva mmoja alimsalimia Ipyana.
Si huyo pekee, wafanyakazi mbalimbali walimsalimia kwa furaha ambapo wengine walimwambia atayakuta magari yao sehemu aliyokuwa akioshea hivyo ayaoshe.
Ipyana aliwaambia sawa huku akimtambulisha Dullah kwamba alikuwa ndugu yake, alifanya hivyo mpaka kwa walinzi ambao kwa jinsi walivyomuamini dogo huyo hawakuwa na wasiwasi.
Ipyana na Dullah walipofika eneo la kazi, waliyakuta magari manne ya mabosi ambayo walipaswa kuyaosha, Ipyana alimuelekeza jinsi ya kufanya kazi hiyo Dullah .
Hadi ilipofika saa tatu na nusu walikwishamaliza kuosha magari manne, kwa gharama ya shilingi 4,000 kwa gari moja na tayari walikuwa wana ukakika wa kupata shilingi 16,000.
“Umeona besti, haya magari manne tayari tuna uhakika wa kupata shilingi 16,000,” Ipyana alimwambia Dullah ambaye alimwambia aliamini ile kazi ililipa.
INAENDELEA

0 Comments