Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Responsive Advertisement

Chombezo: Sharobalo wa Tandale sehemu ya nane (08)

 


Wakati wakiwa wanapiga stori wamekaa eneo la kuoshea magari, alikuja dada mmoja wa idara ya uhasibu mwenye shepu matata sana, akawasalimia akina Ipyana.


“Sisi hatujambo da Fatu, vipi kazi?” Ipyana alimsabahi.

Dada huyo ambaye kwa jinsi alivyoumbika na nguo alizovaa kumkaa sawa, Dullah akajikuta anameza tu mafunda ya mate na kujisemea moyoni kwamba wakubwa walikuwa wanafaidi sana.

“Vipi Ipyana, naona leo umetuletea mwenzako, kazi zinakuzidi nini?” Fatu alimwuliza Ipyana kabla hajamweleza shida yake.

“Nimeamua tu kuja na ndugu yangu maana nimeona yupoyupo tu homu,” Ipyana alimwambia.

“Vizuri sana na huo ndiyo urafiki wa kweli, anaitwa nani?” Fatu alimwuliza dada huyo aliyeonekana kuvutiwa na kitu f’lani kwa sharobaro Dullah .

“Abdallah, ila wengi wanapenda kumuita jina lake kwa kifupi yaani Dullah ,” Ipyana akamwambia.

“Oke, karibu sana Dullah , tena kwa kuwa leo ndiyo mara yako ya kwanza kufika hapa nataka gari langu ulioshe wewe, nitakupa shilingi elfu sita kama ofa ya kukukaribisha,” Fatu alimwambia Dullah , kijana huyo ambaye hakuamini alichokisikia akasema asante.

“Leo Ipyana ni zamu ya rafiki yako mgeni, wewe umekula sana hela zangu, sasa gari langu lile pale nataka kuona rafiki yako atakavyoling’arisha,” Fatuma alimwambia Ipyana.

“Dada Fatu bwana kwa visa, haya bwana wewe kaendelee na kazi lakini elewa wadogo zako bado hatujanywa chai,” Ipyana akamtania.

“Kwani mimi ndiye nimewaleta mjini, mtakula jeuri yenu,” Fatu alimtania Ipyana kisha akaingiza mkono kwenye sketi yake iliyombana na kutoa noti ya shilingi 5,000 akampatia Ipyana.

Ipyana na Dullah walimshukuru ndipo dada huyo akaenda kuendelea na kazi, hata hivyo alivutiwa sana na muonekano wa Dullah ambaye alikuwa mrefu wa wastani, maji ya kunde, ana vidiponsi vilivyomfanya anapotabasamu au kucheka vionekane.

“Ukiwa na kijana kama huyo mbona ni raha tupu siyo kama mzee wangu hajiwezi kabisa eneo la kujidai, huyu nitafanya kila njia nimpate,” Fatuma ambaye wengi walipenda kulikatisha jina lake aliwaza.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

“Kaka umeona mambo ya Posta hayo? Mpaka muda huu tayari tuna shilingi 21,000 hata saa tano haijafika, halafu una nyota ya kupendwa, si umemuona dada Fatu alivyokuchangamkia na kutoa hela ya chai?” Ipyana alimwambia Dullah .

“Siyo mchezo kaka, halafu dada yupo bomba mbaya, kweli wakubwa wanafaidi da!” Dullah alimwambia Ipyana.

“Siyo wakubwa, hata wewe ukiamua kujitosa mazima unachukua mzigo, hawa madada wa maofisini huwa wanawapenda sana vijana kama sisi,” Ipyana alimwambia Dullah .

“Acha kunitania Ipyana, dada kama yule mwenye hela zake na alivyo vile anaweza kutoka na vijana kama sisi tusio na mbele wala nyuma?” Dullah alimwuliza rafiki yake.

“Kwani unafikiri wana tofauti gani na mtoto wa kishua aliyekupa hadi simu, mapenzi hayanaga sera hizo ni sawa na kipepeo asiyechagua ua la kutua,” Ipyana alimwambia Dullah .

Dullah alifurahishwa na kauli ya Ipyana na kujikuta akicheka na kumwambia hakujua kama alikuwa na maneno mengi namna ile, rafiki yake huyo alimwambia kauli yake ilikuwa kweli tupu!

Kabla hata hawajaenda lilipokuwa gari la Fatu, alitokea dada mwingine mfupi wa wastani, mweusi wa kung’aa, nyuma ana kiwowowo cha kuleta fujo mjini, miguu ya bia, macho makubwa akikutazama ni kama vile anakukonyeza na midomo f’lani hivi ya mahaba.

Kwa tabia ya kupenda wanawake kuliko hata chakula, Dullah alipomuona tu moyo ukapiga paa.





Dada huyo alimsalimia kwa kumchangamkia Ipyana na kumwuliza kama alikuwa na gari la kuosha muda ule.

“Hapa sista Jully, vipi gari lako chafu nini?” Ipyana alimwuliza.

“Hapana, ila nataka nikutume Mtaa wa Makunganya mara moja,” dada Jully alimwambia Ipyana.

Ipyana alimwambia hakukuwa na tatizo ndipo yule dada akatoa bahasha ya khaki na kumweleza ilikuwa na shilingi laki tatu aende kwenye ofisi za kusajili vizazi na vifo akamuulize dada mmoja aitwaye Milka akimkuta ampe fedha hizo.

Baada ya dada Jully kumwagiza hivyo Ipyana alimwangalia Dullah na kumwuliza Ipyana kama alikuwa ndugu yake, akamjibu ndiyo.

“Naye upo naye hapa?” aliuliza.

Ipyana alimwambia atakuwanaye ndipo dada huyo aliyekuwa kavaa sketi nyekundu na blauzi iliyokuwa na maua ya rangi mchanganyiko, mavazi yaliyompendeza sana akamkaribisha Dullah .

Dullah aliposema asante, dada huyo alimwuliza Ipyana ndugu yake alikuwa anaitwa nani, akamwambia Dullah,

“Haya mdogo wangu karibu sana hapa!” Jully alimwambia Dullah .

“Asante dada yangu, nafurahi kukufahamu,” Dullah alimwambia.

“Mh! Hawa akina dada wa hapa wana mambo balaa yaani kila anayekuona anakushobokea, hongera kaka kwa zali la kupendwa!” Ipyana alimtania Dullah .

Dullah alipoambiwa hivyo kichwa kilivimba kwa sifa akacheka sana, kwa kuwa alikuwa akipenda sana mademu akamwambia rafiki yake lazima atamtafuna mmoja ili kujenga heshima!

Baada ya mazungumzo hayo, vijana hao walikwenda kuosha gari la dada Fatu kwa ushirikiano. Wakati wakiendelea na zoezi hilo Fatu akiwa ofisini akili yake ilikuwa kwa sharobaro Dullah .

Si kwa Fatu tu, hata Jully naye alikuwa kavutiwa na kijana huyo ambaye ndiyo kwanza alimuona siku hiyo, alivutiwa na Dullah kwani alifanana vitu vingi na serengeti boy wake aliyeitwa Peter aliyekwenda kusoma Canada.

“Huyu kijana utafikiria wako pacha na Peter wangu, lazima nifanye kila kitu nimnase kabla hata hajazoeana na wanawake wa hapa maana nawajua kwa kupenda vivulana,” Jully aliwaza bila kujua Fatu naye alimhitaji sana Dullah .

Baada ya kumaliza kuosha gari la Fatu, walikwenda kunywa chai kisha walirudi ndipo Ipyana akamwambia Dullah kwamba amsubiri anakwenda mtaa wa Makunganya alikotumwa.

“Usijali kamanda wangu we nenda, utanikuta,” Dullah alimwambia Ipyana.

Ipyana alipoondoka, Dullah alikumbuka alizima simu muda mrefu akaiwasha, hakukaa hata sekunde mbili Doreen binti wa ushuani aliyekosa raha tangu alfajiri baada ya kumkosa Dullah kisha kuambiwa na fundi Yassin kwamba asingefika site akapiga.

Dullah alipokea simu hiyo, Doreen alipomjulia hali yake alimwuliza alipatwa na masaibu gani yaliyomfanya asifike site, akamwambia ameambiwa asiende.

“Unasemaje d nani kakuzuia?” Doreen alihoji.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Dullah hakuona sababu ya kumficha akamsimulia kila kitu, msichana huyo alisema atafanya kila awezalo Zakayo aondoke pale kama alivyomfanyia mpenzi wake Dullah .

Baada ya kuzungumza kwa muda, msichana huyo alimbusu Dullah na kumuuliza kijana huyo kama alikuwa na nanafasi siku hiyo wakutane sehemu ili wapeane raha.

“Kwa leo haitawezekana mpenzi wangu,nimepata kazi nyingine,” Dullah alimwambia.

Doreen alipoambiwa hivyo alishtuka na kumuuliza alikuwa akifanya kazi gani na wapi, Dullah alimfahamisha kwamba ni kibarua tu huko Posta, msichana huyo akashangaa.

Wakati wapenzi hao wakizungumza Dullah alimuona mama mmoja mtu mzima akija pale walipokuwa wanakaa kusubiri tenda za kuosha magari, mama huyo akamsalimia.

Dullah akiwa ameiacha simu hewani aliitikia salamu ya mama huyo na kumwamkia kisha akamwambia Doreen asubiri atampigia baadaye, msichana huyo aliyesikia wakati Dullah akimwamkia yule mama akasema sawa.

“Ipyana yuko wapi?” mama huyo ambaye licha ya kuwa mtu mzima alionekana alikuwa moto wa kuotembea mbali enzi zake maana aliumbika haswa alimwuliza Dullah .

Dullah alimfahamisha kwamba alitoka kidogo, akamwuliza kama naye alikuwa akishirikiana naye kufanya kazi, Dullah akamwambia ndiyo.

Mama huyo ghafla akatokea kumpenda Dullah kwani ulipita muda mrefu bila kunjunju.

“Ila hujaanza kuja hapa muda mrefu eh?” mama huyo katibu muhtasi aliyefiwa na mumewe miaka minne iliyopita alimwuliza Dullah .

“Nimeanza leo,” Dullah alimfahamisha.

“Oke, akija mwenzako nitarudi nataka munioshee gari langu maana leo ni siku ya tano halijaoshwa,” mama huyo ambaye naye alivutiwa na Dullah alimwambia.

“Hakuna shida mama yangu,” Dullah alimfahamisha.

Mama huyo alipogeuka na kuanza kuelekea ofisini, Dullah aliyagandisha macho yake kwenye wowowo lake tata lililokuwa likitikisika na kuonekana kama lilitaka kudondoka.

“Kudadeki kumbe huku Posta ndivyo kulivyo? Kila demu mpaka akina mama wote wazuri, asante besti yangu Ipyana kwa kunitoa uswahili, maana hawa wanawake wazuri ningewaona wapi?” Dullah aliwaza.

Mama huyo alipotoweka kabisa, Dullah aliyekuwa na namba za mademu wote aliokutana nao tangu siku ya kwanza kwenda site Madale, aliamua kumpigia demu huyo.

“Haloo! Halooo nani mwenzangu?” yule msichana wa kwanza waliyeachana na Dullah kituo cha daladala Mwenge alimwuliza Dullah baada ya kupokea simu.

Dullah alipojitambulisha, yule dada alifurahi kumsikia na kumwuliza habari za tangu walipoachana, Dullah akamwambia zilikuwa poa kisha alimfahamisha ile ilikuwa namba yake na alikuwa hewani.

Pamoja na yote, Dullah alimwomba dada huyo kama atakuwa na nafasi waonane, akamwambia haikuwa na shida na kupanga Jumapili iliyofuata wakutane Temeke Mwisho.

Alipopewa jibu hilo, Dullah alifurahi sana na kujisemea demu huyo siku hiyo asingechomoa lazima atatafunwa kisawasawa kwani kama ni fedha alikuwanazo.

Baada ya kumalizana na demu huyo, alimwendea hewani Atu ambaye tangu walipoachana siku ile walipobilingishana katika gesti ya Keko hawakukutana.

Msichana huyo ambaye hakuwa na namba ya dullah alipomwuliza alikuwa na nani, sharobaro Dullah akajitambulisha, Atu alifurahi na kumwambia kwa nini alikuwa kimya namna ile.

“Jamani si nilikwambia simu yangu iliibiwa,hiyo ndiyo namba yangu halafu naaamu mno ya kukutana na wewe,” Dullah aliyeamua kufungulia mbwa bandani yaani kutaka kuwashughulikia vilivyo viumbe hao alimwambia.

“Ni wewe tu! Mimi hata ukisema leo nipo tayari!” Atu alimwambia Dullah .

Kitendo cha msichana huyo kumwambia Dullah hata sikuile alikuwa na chansi, kijana huyo mpenda mademu wazuri akaona atafanya kosa kubwa sana kumuachia ndege huyo aliyeingia tunduni mwenyewe.

“Oke! Mimi kwa sasa nipo tauni, nikimaliza mambo ya hapa nitakupigia na kukuelekeza sehemu ya kumiti, au iwe pa siku ile?” Dullah alimwambia Atu aliyesema sawa.

Wakati Dullah akiendelea kuzungumza na Atu, Ipyana alirudi ndipo akamuaga Atu na kumfahamisha kuhusu yule mama mtu mzima ambaye alijaaliwa bambataa matata.

“Umesema mnene mfupi kajazia nyuma?” Ipyana alimwuliza Dullah .

“Yeah! Tena akitembea utafikiri mzigo unataka kuanguka wenyewe yaani kaka wanawake wa hapa wazee kwa vijana wote moto kwa kwenda mbele,” Dullah alimwambia Ipyana.

“Mimi naangalia kazi tu, kama ningewaendekeza nisikuwa nimefanya chochote,hivi unajua kama nimenunua uwanja nataka mwakani nianze kujenga?” Ipyana alimwambia Dullah .

Dullah alipoambiwa hivyo alicheka sana na kumwambia kweli hakuutendea haki ujana, badala ya kufurahia maisha eti anafikiria kujenga wakati mshua wake ana nyumba tatu kali na mbili kapangisha.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

“Zile ni za mshua mimi nataka niwe na nyumba yangu,” Ipyana alimwambia Dullah aliyeishia kucheka.

“Ndiyo hivyo, baada ya kumwambia haupo akaniuliza maswali mawili matatu akaniaga na kusema atarudi ukija ngoja tumsubiri,” Dullah akamwambia Ipyana.



“Huyo mama anaitwa mama Maduu alifiwaga na mumewe kitambo tu na siyo bahili wa fedha zake,kwani kuna wakati nikimuoshea gari lake hunipa mpaka shilingi elfu kumi,” Ipyana alimwambia rafiki yake na kuongeza;

“Halafu mama huyo anapenda sana vijana wadogo,” Ipyana alimwambia Dullah ambaye moyo wake ulipiga paa kwa kupata taarifa hiyo.

Wakati wakiendelea na maongezi yao, kumbe mama Maduu ambaye ofisi yake ipo ghorofani aliwaona akatoka na kushuka kwa lifti na kuelekea kwa akina Ipyana.

“Ipyana hujambo?” alimsabahi.

Baada ya salamu alimwambia kwamba alimuona ndugu yake na kumtania kama alikuja kumfundisha kazi ya kuosha magari,” Ipyana akamwambia alikuwa anajua.

Mama huyo alipopewa jibu hilo alimwambia hakuwa na muda mrefu alitaka wamuoshee gari lake na kwamba atafurahi sana kama kazi hiyo nitaifanya mimi, akaahidi liking’aa atanipa zawadi ya kunikaribisha kisha akawa anaelekea ofisini.

“Da! Ukisikia mtu nyota yake inang’aa bila kwenda kwa mganga ndiyo mimi, yaani hata huyu mama inavyoonekana ananitaka, dalili zote zipo wazi,” Abdallah Nzamba aka Dullah aliwaza.

“Kaka si nilikuambia kuhusu wanawake wa hapa, umemsikia alivyokuambia mama?” Ipyana alimwuliza Dullah .

“Kaka sina cha kusema ila ndani ya wiki yule sijui dada Jully, Fatu au huyu mama lazima mmoja nitakupa ripoti kwamba nimeua, wewe subiri kwani siwezi kuwaacha viumbe wenye hela zao wajishaueshaue wakati fyekeo ninalo.

Ipyana alicheka sana na kumwambia awe makini lakini kwa sababu pale wizarani ngoma ilikuwa njenje, Dullah akamwambia hakuna binadamu atakayeishimilele acha ale ujana.

Siku hiyo waliosha magari na kupata shilingi 46,000 achilia shilingi elfu kumi aliyopewa Dullah na yule mama Maduu aliyejifanya kampa ofa ya kumuoshea gari lake vizuri kumbe alikuwa na lake jambo!

Kufuatia urafiki wao, baada ya kumaliza kazi Dullah na Ipyana walioga na kuvaa pamba zao na kuelekea kituo cha daladala cha Posta Mpya kupanda basi la Tandika.

Wakiwa kituoni Dullah ambaye mfukoni alikuwa na shilingi elfu 15 alimwambia Ipyana kwamba akifika Keko atashuka anataka kwenda kumuona mshkaji wake mmoja, Ipyana aliyemshtukia kwamba yalikuwa ni masuala ya mademu akacheka sana.

“Mbona unacheka?” Dullah alimwuliza.

“Wewe si useme unataka kwenda kuonana na mtoto unafikiri sikufahamu Dullah ?” Ipyana akamwambia.

Kama kawaida yake,Dullah alicheka ndipo Ipyana aliyekuwa akipenda sana maendeleo akafungua waleti yake akachomoawekundu wawili wa msimbazi akampatia Dullah aliyeshia kuporomosha tabasamu kwani alijua ishu yake ya kukutana na Atu itakwenda vizuri.

Wakiwa pale kituoni basi la Tandika lilifika wakapanda na kukaa siti moja,

Gari lilipoondoka, akapigiwa simu na Doreen ambaye alimtaka afanye awezavyo kesho yake waonane lakini Dullah alimwambia amsubiri mpaka wikiendi kwani sehemu aliyoanza kazi walikuwa bize sana.

Doreen hakuwa na jinsi zaidi ya kuwa mpole na kumwomba usiku wakutane kwa njia ya meseji ili amkate kiu kwa kutumia usanii wake kama alivyomfanyia siku ile.

“Usijali mpenzi mpenzi wangu,nitafanya hivyo,” Dullah alimwambia Doreen.

Gari lilipofika Keko, Dullah alimuaga Ipyana, Ipyana akaishia kucheka na kumtakia Dullah kazi njema.

Dullah alipoambiwa hivyo huku akishuka kwenye gari akawa anacheka kwani alijua alichokimaanisha Ipyana, gari lilipoondoka akiwa pembeni ya baraba alimpigia simu Atu.

“Niambie mpenzi wangu umeshafika nini hapo?” Atu alimwuliza.

“Yeah! Wewe uko wapi?”

Baada ya kuulizwa hivyo, Dullah alimwambia alikuwa kituo cha daladala ndipo Atu akamwambia kwa kuwa eneo lile watu walikuwa wakimfahamu atangulie katika gesti waliyokutana siku ya kwanza



CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



Sharobaro Dullah alipoambiwa hivyo, aliachia tabasamu kwani alikuwa na uhakika wa asilimia mia moja kwamba siku hiyo angemchinjia mtu baharini.

Alipofika pale gesti hakutaka kusubiri, alichukua rumu kabisa kisha alimwomba mhudumu ampelee bia mbili, akavua shati, suruali na kubaki na boksa pekee akawa anamsubiri Atu.

“Huyu kiumbe akifika tu baada ya salamu jambo la kwanza nikumpatia mkomboti ndiyo mambo mengine yatafuata,nataka mpaka tutakapoachana niwe nimempa mikomboti miwili au mitatu,” Dullah aliwaza.

Hakumaliza hata dakika kumi na tano simu yake iliita alipoangalia mpigaji alikuwa ni Atu akapokea na kumwelekeza amuulize mhudumu amuoneshe namba ya chimbo alilokuwepo.

“Oke mpenzi wangu,” Atu alimwambia Dullah .

Ile kijana huyo mpenda mademu wazuri anaweka glasi iliyokuwa na pombe juu ya meza iliyokuwa mle chumbani akasikia mtu akigonga, akamfungulia na mtoto Atu aliyekuwa kapendeza akaingia.

Atu alipoingia alianza kucheka baada ya kumuona Dullah akiwa na boksa pekee huku mkuu wake wa kaya akiwa kachangamka, akajisemea moyoni; ‘Leo hapa ni kazi tu!”

Dullah hakutaka kusubiri, alimkumbatia na kumpiga mabusu kadhaa ya fasta midomoni, shavuni na masikioni, kufuatia msichana huyo kufanyiwa hivyo na kwa vile alimuona mkuu wa kaya wa Dullah alivyochangamka mwili ukamsisimka si kidogo.

Wawili hao, kwa dakika kadhaa walisahau kabisa shida za dunia wakawa wanakula tu denda a.k.a mua huku wakishikana maeneo mbalimbali ya miili yao hasa yale yenye shoti ya umeme.



ITAENDELEA

Post a Comment

0 Comments