Niliingiwa na roho ya udadisi nikawa nakagua baadhi ya vyumba mle ndani. Nikaingia vingine nilikuta vina madawa ya kulevya. Ila kuna chumba kimoja niliingia huko ndo ilikua kizaazaa. Nilikutana na maiti za watu wengi sana. zingine zilikua zinanuka. Nikataka kujua zaidi zile maiti imekuaje nikaingia ndani kabisa nikawa naangalia huku na kule huku roho ikidunda kwa kasi. Mara ghafla mlango wa kile chumba ukafungwa na taa zikawashwa kisha nikaona............
.......Nikamwona mtu akiinuka katika zile maiti. Kumbe yeye alikua ni mlinzi wa mule ndani. Tena sikuamini kwani ni mtu ambaye sikutarajia kumwona pale. Alikua ni yule jamaa mbabe wa kule jela.
Akaniangalia kisha akasema yafaa kukutana pamoja. Wewe umenifuata hadi huku. Mimi nikamjibu hahaa!! hapana br.. br... broo mimi nilikua nanaa naa. Basi yule jamaa akanikatisha kwa kusema sihitaji ugomvi tena na wewe kikubwa ni kwamba bora maisha ya jela kuliko humu ndani.
Nikamwuliza kwani yeye alifikaje na je! pale ni wapi? akajibu siku nilipomchoma kisu yeye na afande. Wakati wanapelekwa hospitali kwa ajili ya matibabu ndipo walitekwa nyara. Afande aliokolewa sijui yuko wapi. Ila mimi ndio nikajikuta humu ndani. Humu wanasafirisha madawa ya kulevya kupitia hizi maiti. Wanazichana na kuzishona kama magunia. Hivyo mimi nilikabidhiwa ulinzi wa hiki chumba. Ila mimi nimechoka maisha ya humu ndani nahitaji kutoka sasa kwa sababu na wewe ni kamanda tushirikiane.
Nikaona ni wazo jema sana nikakubaliana naye lakini wakati namkumbatia ili kuonyesha kukubaliana naye kwa wazo lake.
Ghafla aliingia mtu mmoja mwenye asili ya kihindi akamimina risasi za kutosha kwa yule jamaa. Pale pale akaaga dunia. Kisha yule jamaa akaondoka bila kunisemesha lolote. Niliogopa sana nikashangaa hivi ni kwanini mle ndani kila anayetoa siri anauawa wanajuaje. Nikaamua moja tu mle ndani ni kuwa mjinga na kufanya kazi maana pakutokea sikupaona. Tangu nilipoingia mle sikuwahi kuona jua wala giza wala mwezi. Ilikua ni mwanga wa taa za umeme tu. Sikujua hata nmekaa muda gani mle ndani.
Ni baada ya kuwa nafuatilia mazingira ya mle ndani kwa ukaribu ndipo nikagundua kila chumba kina kamera. Nikajua kumbe ndio maana watu mle ndani huwa wanauawa. Basi nikazidi kuifanya kazi yangu na muda ukasonga. Ndipo kuna siku niliitwa na jamaa mmoja akidai naitwa na boss. Nikainuka na kumfuata. Akanipeleka hadi chumba fulani ambako nilishtuka sana kumwona mtu mmoja mle.
Alikua ni yule daktari wa kihindi niliyemkuta mhimbili. Nikajiuliza ina maana ndio sababu alikua ananiangalia sana?
Akajisemesha karibu kijana. Nilishikwa na hasira sana kiukweli nikatamani nimrukie hata nimfinyangefinyange. Kisha nimsagesage kwa meno yangu. Lakini jeuri hiyo ningeitoa wapi yusuph mimi? Basi yule mhindi akasema vijana mnipishe. Wote wakaondoka basi yule mhindi akaanza kwa kusema kijana nahitaji kukusaidia. Najua una kesi ila hapa hakuna wa kukushika.
Msaada wangu si wa bure hata chembe. Kwanza nahitaji unisaidie mambo fulani hebu njoo. Kisha akasema nimependa mwonekano wako nahitaji nikuhamishie Afrika ya kusini ukaishi huko maisha ya uhuru na ya amani. Ukatanue huko ila ninachohitaji ni kitu kimoja hebu nifuate. Kwakuwa nilishaingiwa na hofu ya mle ndani nikamfuata. Tukaingia chumba kimoja kilikua kimepambwa vizuri sana ilikua ni chumbani kwa mtu. Kulikua na kitanda na vitu vyote vya chumbani. Basi nikiwa nashangaa yule mhindi akinisogelea.
Kisha akaanza kunishikashika kama vile mi mwanamke. Niliduwa kwa muda kisha nikawa namwangalia nikaona ananivua nguo. Haaa yale yalikua makosa na matusi makubwa kwangu. Nikajisemea moyoni bora kufa kuliko fedheha hii ya kurekodiwa na kamera nikifanya mapenzi na mwanaume mwenzangu. Nikajikuta nimeanza kupandisha hasira yangu taratibu na kuanza kuwa kama mbogo.
Nilimsukuma yule mhindi akaanguka chini kisha nikamrukia kwa gadhabu kuu. Nilimkalia kifuani huku mikono yangu ikimkaba shingoni. Alifurukuta yule mhindi bila msaada wowote. Akajitutumua kiasi kisha akafanikiwa kunisukuma na kuniangushia kwenye meza. Niliinuka na kukaa sawa tayari kwa mpambano. Ghafla mle ndani kukavamiwa na walinzi.
Walininyanyua na kunitupia ukutani. Lakini wakati nashuka chini kuna bomba moja lilikua limepita mle ndani. Lilikua bomba kubwa kweli kweli. Nikaamua kujishikilia kwa kulikumbatia. Walinipiga wale walinzi virungu ngumi na mateke ya kila aina. Lakini sikuachia. Baadae wakaamua kuanza kunivuta walinivuta sana. Taratibu niliona bomba lile linalegea mara ghafla likachomoka haaa!!! .
Ilikua makosa makubwa kwani mle ndani yalianza kuingia maji kwa kasi sana. Yale maji yalikuwa na kasi kubwa yalikuwa yanapita katika lile bomba. Nilmsikia boss yule akisema zima umeme haraka fungua na milango ya kutoa maji. ghafla ikawa giza mle ndani. Maji yalizidi nguvu kisha kuna kitu kikawa kama kimefunguka basi maji kwa kasi yakawa yanaelekea ule mkondo. Nikaona hapa ndo nafasi nikafuata yale maji. Nikasukumwa na nguvu ya maji nikabamizwa huku na kule kisha nikawa napelekwa kama mti mkavu kwenye maji yenye speed.
Nikiwa sijui nini cha kufanya nikajikuta nipo katika maji yaliyotulia sana. Cha ajabu ni kwamba kina kilikuwa kinazidi kuongezeka. Nikaona sasa ndo wakati wa kupiga mbizi. Nikapiga mbizi na kutokeza sehemu fulani ambayo nilijua ni nje ya nyumba ile ya wale mafedhuli. Nikiwa naogelea nikasikia watu wakiambiana kama kashaingia baharini tumemkosa huyu. Nikajiuliza ina maana humu ni baharini? Kwa kuwa nilikua naiona nchi kavu kwa mbali nikaanza kuogelea kuelekea nchi kavu. Mara wakawa kama wameniona wakawa wanakuja wanamulika na tochi kwani ilikua ni usiku.
Kwa mbali nikauona kama mtumbwi hivi wa wavuvi nikaogelea kuufuata. Walipofika eneo ambalo walihisi nipo wakanikosa wakarudi. Nikaudandia ule mtumbwi huku nikiwa nimekunywa maji mengi sana. Nilikua nimechoka sana basi wale wavuvi wakasemezana twendeni pwani tumpe huduma ya kwanza. Basi wakati wakiwa wanaenda nchi kavu nilikua nimezidiwa sana.
Nilizimia nikiwa sijitambui nilishtuka ikiwa kumekucha tulikua ufukweni mwa bahari. Niliinuka na kuangalia pale nikagundua ni ufukwe wa koko. Nikajiuliza wapi nilikua naishi majibu nikakosa ila nikajua tuu kua ni kwa baadhi ya magorofa yaliyo kando na bahari ndo wanaofanya vile. Nikiwa nashangaa huku narudisha kumbukumbu mara nikaona...
Nikajiuliza wapi nilikua naishi majibu nikakosa ila nikajua tuu kua ni kwa baadhi ya magorofa yaliyo kando na bahari ndo wanaofanya vile. Nikiwa nashangaa huku narudisha kumbukumbu mara nikaona.... ENDELEAA
Boti moja inakuja kwa kasi sana usawa ule ambao tulikuwepo. Niliingiwa na woga sana nikaona hapa siyo salama sana kwangu.
Niliamua kuanza mbio wakati naanza kukimbia wale watu walikua wameshafika nchi kavu. Nilikimbia nisijue hata ninakoelekea. Nyuma yangu kulikua na watu kama watano wananikimbiza. Nilitoka mbio sana nikakimbia hadi nikavikuta vichochoro. Pale ikawa ndo pona yangu niliingia kwenye vichochoro vya jiji la dar kisha tukapoteana na wale jamaa.
Baada ya kuhakikisha usalama umerejea nikasimama sehemu na kushusha pumzi nzito. Niliwaza nielekee wapi na kwa umakini kwa sababu nina kesi na pia ni mfungwa. Na zaidi nilikua natafutwa na wale majambazi. Nilijisemea moyoni kazi yangu ni ngumu sana. Nikapata wazo ya kuwa niende Mbeya kwa mama ambaye alikua sasa ni kama mke wangu kwani tayari alikua na mtoto wangu. Shida ikaja sina nauli nikawaza sana nikaona bora nifanye mpango hata wa kuiba pesa. Wazo likanijia niende kariakoo huko ndio kwenye mkusanyiko wa watu.
Basi baada ya kuamua nikatafta sehemu nikakaa na kupumzika. Jioni nikafanya jitihada za kufika kariakoo. Niliona niende jioni kwa sababu sikutaka kuonekana na watu. Ukizingatia nilikua natafutwa na Polisi, Na pia majambazi, hivyo ilikua ni sehemu ya tahadhari. Nikafika kariakoo huku nikiwa makini sana. Macho yakijaribu kuchora hapa na pale ni nani yupo kizembezembe nimlize. Ndipo baada ya mda nikamwona muhindi mmoja akitoka kwenye duka lake akiwa anaelekea sehemu kama kujisaidia. Nikamchora kisha haraka nikaingia na kuchukua simu nne halafu nikakaa nje kumsubiri.
Alipofika nikajitiap kumwuliza bei za simu. Kisha nikaondoka zangu. Njiani nilimwona mama mmoja wakihindi ana mkoba. Kwa kua nilikwishafanyiwa ubaya na wahindi kule kwenye madawa ya kulevya kila mhindi ilikua nikimwona nahisi kumchukia. Nilijikuta nakua na hasira sana na wahindi. Hasa kile kitendo cha kutaka kunifanyisha mapenzi ya jinsia moja. Ni kitu kilinifanya niwaone kama wanyama. Nilijikuta naingiwa na hasira na kuanza kumlia mingo yule mama. Baada ya kuona ameingia kwenye 18 zangu. Nikatoka nanyata na kuukata ule mkoba na kiwembe. Yule mama akabaki na mikanda.
Nilitokomea na mkoba hadi sehemu yenye utulivu. Nikaanza kuukagua mkoba ule. Ulikua na vitu baadhi vya thamani mlikua na hereni za dhahabu, mkufu wa dhahabu. Pia kulikua na simu mbili za gharama kiasi nikazidi kuupekua kisha nikaona na kiasi cha pesa kama elfu sabini za kitanzania. Nikaona nimeweza zoezi la kwanza. Nikautupa ulw mkoba na kuamua kuelekea ubungo. Huko nilitaka nipate gari ya kuelekea Mbeya. Nilifika ubungo usiku sana sababu ilikua ni kutogaka kuonekana.
Baada ya kufika nikatafuta basi la kampuni ya Happy nation. Sababu za kulitafuta basi hilo ni kwasababu ndo basi pekee lilikua linawahi kuingia Mbeya likitokea Dar es salaam. Baada ya kulipata nililala pale stendi ya mabasi ubungo. Huku nikiwa naficha kwa juhudi zote uso wangu. Asubuhi ikafika safari ikaanza. Basi liliacha taratibu ardhi ya jiji la Dar es salaam na kutokomea barabarani. Nilisafiri kwa woga sana hivyo mda mwingi niliutumia kujificha ili nisijulikane.
Mungu mkubwa hatimae nikaingia Mbeya salama salmini. Nikashuka na kuelekea kwa mama yani mke wa boss wangu. Baada ya kufika tuu nilishangaa kupishana na kijana mmoja mrefu na mweupe kiasi. Sura yake haikua ngeni sana nikarejesha kumbukumbu kisha nikakumbuka. Biliwahi kuwaona na mama wakitoka hotelini siku ambayo nilienda kwa yule muhudumu ili anisimulie mabaya ya yule mama. Nakumbuka walikua wanashikana na kuonyesha ni wapenzi. Aaaah kwa kua kichwa changu kilikua kimeshavurugika sikutaka kumfikiria yeye. Nikaamua kuingia ndani ambapo nilimwona mama akiwa ametoka kuoga. Alishtuka sana kuniona mana nadhani ilikua haijapita miaka hata mitano toka niende jela. Alikuja akanikumbatia.
Japo alionyesha kua na woga fulani. Sikujali hilo mimi ilikua ni kuangalia namna ya kurudisha maisha yangu kwenye mstari. Basi akanambia walikuja jela wakiwa wamekata rufaa na wakaambiwa nimetoroka na hivyo natafutwa. Basi mimi nikamsimulia mambo yote yalotokea jela. Nikamweleza pia ni jinsi gani nimefika pale nyumbani. Alinipa pole kisha akanikaribisha sana nyumbani na kumwita mwangu nimsalimie.
Baada ya shamrashamra za hapa napale ghafla mlango uligongwa. Mimi nikaona nijifiche mana sikujua ni nani. Basi alipofungua kumbe walikua ni majirani wakaongea na mama yule mambo yao kisha wakaondoka. Baada ya kutoka sebuleni tuu mlango ukagongwa tena nikatoka na kujificha tena. Safari hii alikua ni happy ametoka kwake kuja kumsalimia mama yake. Basi kuona vile nikatoka japo nilikua najisikia vibaya sana kwa yale maisha.
Basi happy akafurahi sana kuniona hadi akashindwa kujizuia pale akanibusu mfululizo shavuni na mdomoni. Basi mama yake kuona vile akatukalipia kiasi basi tukaacha nadhani mama ilikua ni wivu. Basi tukakaa kimya kwa mda kisha sitori zikaendelea. Mara mlango ukagongwa tena. Mama akauliza nani? Sauti ikasema polisi. Akauliza kuna nini wakajibu fungua mlango. Basi ikabidi nitafutiwe sehemu ya kujificha. Paliangaliwa pale ndani sehemu iliyoonekana ni salama kidogo ilokua ni kwenye Jeneza. Jeneza lile lilikua limenunuliwa kipindi boss kafaa likawa halimtoshi. Hivyo wakaliacha na kununua lingne. Basi nikaingia mle na kufunikwa mle. Mlango ukafunguliwa kisha polisi wakaingia......
Hawakusema lolote zaidi wakaanza kuingia kila chumba na kutoka. Kisha wakasemezana wao kwa wao hayupo itakua siyo kweli. Halafu wakaondoka zao bila kusema lolote kwa mama. Nikainuka toka kwenye Jeneza na kukaa. Basi usiku ule ukaisha kwa usumbufu kama ule.
Asubuhi na mapema nikaamua kwenda kumwona yule mzee aliesema anaishi na mdogo wangu. Nikamfuata na kumkuta tuliongea mambo mengi sana kwa kweli. Nilimwona mdogo wangu alifurahi sana, Wakati natoka kwa yule mzee njiani huku nikiwa natembea kwa kujihami. Nilikutana na dada mmoja ambaye aliniangalia sana. Sikutaka kumjali sana. Nikaendelea na safari yangu. Lakini kabla sijafika nyumbani nikapigiwa simu na yule mzee. Kupokea nilimsikia mdogo wangu akisema kwa Uchungu mkubwa ??wanamuua babu?? kisha simu ikakatika. Kidume kusikia hivyo Nikatoka mbio kurudi.
Wakati nafika nilipishana na mtu akiwa amejifunga na kujitanda mithili ya mwislam wa Saudi arabia. Alikua kavaa juba Jeusi na nikabu. Nikahisi tu huyu atakua ndie muuaji. Basi nikaamua kumsimamisha "dada vipi!!!" akajibu "safi Asalam aleykum." Nikamwuliza vipi wenyewe wapo? Akajibu mi sijui. Sasa kwa kuwa nilishamtilia mashaka nikaamua kumwanzishia noma. Nikamfuata na kumvuta nikabu kwa nguvu. Ilipotoka OMG!!! sikuamini ninachoshuhudia. Nilihisi naota kwa kweli. Alikua ni baba yangu. Nikajikuta naishiwa nguvu na kuuliza Baba!! Yanini kujitesa hadi unavaa mavazi ya kike shida nini?
Wakati nazidi Kuongea Ghafla bin vuuuu baba akachomoa kisu na kunichoma begani, nikiwa naugulia maumivu Yale makali, akachukua nikabu yake na kutokomea. Niliumia sana kiukweli Nikaingia ndani na kukuta maiti za watu wawili wakiwa wameshakufa kwa kukatwa vichwa. Alikua ni yule mzee na mdogo wangu. Basi nililia sana tena sana yani. Nikajiuliza kwanini baba yangu afikie hadi hatua ya kuvaa nikabu na kubadili sauti aonekane wa kike. Dunia ya ajabu sana.
Nilimpigia mama simu na baadhi ya watu kwa ajili ya kutoa taarifa polisi.
Baada ya kukamilisha zoezi ilinibidi nijifiche. Polisi walikuja na kufanya uchunguzi kisha wakaruhusu maiti kuzikwa. Niliumia sana maiti za watu wale niliowapenda kupita maelezo kuzikwa bila uwepo wangu. Ila ningefanyaje nilikua natafutwa na polisi zaidi na majambazi pia.
Basi siku zikaenda baada ya msiba kuisha nilirudi kwa mama yani mke wa marehemu boss wangu. Nilikua najipanga jinsi ya kukabiliana na Jane, na baba yangu, na pia namna ya kumpata dada yangu. Zaidi nilikua nawaza jinsi ya kulitambua moja kati ya ghorofa linalofanya biashara haramu pale kando ya bahari ya hindi. Lengo ilikua nikisha kamilisha hayo yote nijisalimishe mikononi mwa polisi.
Huku nyumbani jimama langu alikua kanimiss sana basi usiku ule tukaamua kuutumia kwa kupunguza mafuta mwilini. Mama alianza kwa kunibusu alionekana alikua na hamu sana na mimi. Kwakua mimi pia nilikua na hamu naye nikamwandaa vya kutosha huku nikimchezea vizuri sehemu za siri. Nilitumia vidole vyangu na ulimi kumpandisha na kumfikisha kileleni. Alilia kwa raha huku akitaja jina langu na kunisifia sana. Nilipoona amekwishafika kileleni kwa mara mbili mfululizo nikaamua kukwea sasa nitumie kifaa halisi. Nilimkuna vizuri mama yule hadi akakojoa kwa mara ya tatu. Safari hii alionekana kuzidiwa nguvu.
Kwani alilia kwa raha akalegea kabisaaa. Kwa kuwa na mimi nilikua nimechoka nikaamua kumwacha. Na usiku ule ukaisha kwa style hiyo.
Siku zilienda huku nikiishi maisha ya kujifichaficha sana. Lakini kingine ni kwamba housegirl nilikua simwoni pale nyumbani tangu nimerudi. Siku moja nikamwuliza mke wangu (jimama), mbona housegurl toka nimerudi simwoni? Akajibu aaah mambo yake ya kijingajinga kama Happy alipata mimba tukamfukuza. Mmmh nilishituka kusikia ujauzito maana naye alikua anapata dozi toka kwangu. Nikajiuli za yawezekana housegirl naye ana mtoto wangu? Nikamwuliza mama kwa mshangao kwa hiyo sasa hivi yuko wapi? Basi mama akasema we na we, achana na huyo mpumbavu!! Basi mi nikaamua kukaa kimya maisha yakaendelea.
Siku moja nikapata wazo yakuwa na mimi niwe navaa nikabu kama sehemu ya kujificha. Niliafikiana na wazo hilo nikaenda dukani na kununua juba jeusi, nikabu na baadhi ya nguo za kike. Nikarudi nyumbani na kujiandaa. Baada ya siku kadhaa nikaona nianze kwanza kumtafuta Baba kisha dada halafu nimalize na Jane. Nikajipanga siku ikafika nikaanza safari ya kuelekea Dar es salaam.
Nilivaa juba langu na kujifunga vizuri hayo ndio yakawa maisha yangu mapya. Niliishi hivyo nikiwa Dar es salaam, Cha ajabu wanaume walikua wakinisumbua sana wakidhani mimi pia ni mwanamke. Nilivumilia kwa kuwa nilijua ni nini nafanya. Kuna siku nikiwa katika pita pita nikamwona Jane akiwa ameongozana na dada yangu. Nilijiuliza nitawaingiaje ili wanielewe? Nikajipanga na kuanza kuwafuatilia. Nikawafuata hadi sehemu fulani. Nikaona wameingia supermaket fulani. Nikajipa moyo kwamba wakitoka nawasimamisha kisha nitamwomba dada kwa pembeni kisha nitaongea naye. Nikiwa nawaza vile nikawaona wanatoka.
Nikawafuata na kuwasimamisha nikawasalimu "Asalam Aleykum kinadada..." Kwa kuwa dada yangu ndie alikua mwislam akaitikia. Lakini Jane akakaa kimya. Nikamwomba kwa kusema dada samahani naomba kuongea na wewe pembeni. Akaniangalia kwa makini huku Jane akionekana kuhisi kitu kisha nikamsikia Jane akisema......
Haaaa we dada kwanini usiongelee hapa hapa na mimi nikisikia? nikajibu ni maongezi ya mimi na yeye tu tafadhali. Basi dada yangu akasema Afande nisubiri pale mbele kidogo nakuja. Jane akaondoka zake na kusonga mbele. Sikushituka sana kuitwa afande kwani ilikua nimemshudia akiitwa hivyo.
Basi baada ya kutupisha nilianza kwa kumwambia dada yangu samahani sana dada mimi nimekuomba usinielewe vibaya dada yangu. Akajibu usijali sema tu. Nikamwambia mimi ni mdogo wako tumezaliwa na baba mmoja na mama mmoja. Akashaangaa kisha akajibu hapana mimi kwetu wa kike niko mwenyewe. Nikadakia kwa kusema dada mi ni Yusuph kisha nikajifunua uso ili anione. Akashituka sana kisha akasema mdogo wangu umefikia huku. Sababu za kuvaa hivi ni nini?? Dada yangu alianza kulia taratibu huku akinisikitikia.
Ilikua ni mshangao mkubwa sana basi akanikumbatia na kusema mdogo wangu nimekutafuta mda mrefu sana. Nashukuru nimekupata. Nina mambo mengi ya kuongea na wewe. Nilimkumbatia dada yangu huku nikihisi uwepo wa joto la dada. Nilifurahi sana. Machozi yalikua yakinitoka kwa furaha. Nikiwa nalia dada yangu naye akawa analia.
Lakini tukiwa tumekumbatiana pale ghafla Jane alirudi. Akanikuta nikiwa nimejifunua uso. Akasema nilijua tu ya kua ni ww mwanaharamu usiyekua na mbele wala nyuma leo nakuua hapa hapa.
Basi akaingiza mkono kwenye koti kisha akatoa bastora na kutuelekezea mimi na dada yangu. Huku akiongea maneno mengi ya kuwa hata dada yangu alikua anamtafuta siku nyingi na sasa ndio mwisho. Basi dada yangu akasema tafadhali niue mimi lakini huyu mdogo wangu mwache tafadhali sana. Jane akasema haa kumbe nyinyi ni ndugu hahahaha sasa naanza na huyo mdogo wako namaliza na wewe kisha akanitarget mimi.
Jane hakuonyesha utani hata kidogo Basi akfyatua risasi ambayo alinilenga kichwani. Cha ajabu dada yangu akanisukuma na kupigwa yeye na ile risasi sehemu za mabega akijeruhiwa vibaya sana.
Jane kuona vile akaamua kuanza kunitarget na mimi lakini kabla hajafyatua risasi kuna maaskari wa jeshi walikua wanakuja pale. Hali hiyo ilimfanya Jane kutoka mbio. Basi wale wanajeshi wakatubeba na kuondoka na sisi kumbe dada yangu alikua na kifaa kilichoashiria yuko hatarini na walivyoangalia eneo alipo wakaja haraka.
Tulifikishwa hospitali na dada yangu kuanza kupata matibabu. Huku mimi nikiwa chini ya ulinzi wa wanajeshi mpaka hapo dada atakapopona. Siku zikaenda na hali ya dada ikawa nzuri. Ni baada ya kuongea na wale maafande wenzie nikaachiwa huru uraiani. nakumbuka siku moja tukiwa nyumbani kwa dada. Nikaanza kumwuliza juu ya baba. Hapo ndipo dada yangu akaanza kulia na kumlaani sana baba yangu. Akasema ya kuwa baba ndie aliyehusika na kifo cha mama na sababu kubwa ilikua ni wewe na mdogo wetu.
Ambapo alidai ya kuwa baba alisalitiwa na mama hivyo mimi na marehemu mdogo wetu si watoto wake. Nikajiuliza inamaana sisi sio watoto wa mzee Ng'ahala. Nikawaza ndio maana alimwua hata mdogo wangu. Kisha nikamwuliza dada yangu kwa hiyo wewe unampango gani na baba. Akajibu mimi baba naongea naye japo tulikuja kukutana huku ukubwani. Maiti ambayo ilizikwa haikua ya baba. Ile ilikua ni ya mtu mwingine. Baba alidai kuwa mtu ambaye alikua akitembea na mama yani baba yenu nyie aliwadhulumu mali yeye pamoja na mama hivyo aliamua kumwua mama japo chanzo kilikua ni mapenzi na wivu.
Dada akazidi kusema mwanzo nilijua muuaji wa familia yetu ni mtu baki. Hivyo niliapa kuja kumwua na yeye na hilo tayari lilitimia. Ila sikujua kama nimemwua mtu mwenye hatia ndogo kabsa. Siyo mbaya mdogo wangu tutafute namna ya kukaa na baba atuelewe ya kuwa sisi ni ndugu kisha akupeleke wewe kwa ndugu zako ambako baba yako alikua akiishi maana nasikia alikua na mke na watoto sasa basi kikubwa ni wewe na mimi kukaa na baba kusahau yaliyopita na kuanza maisha mapya.
Nilimwelewa dada yangu na kuanza mipango. Lakini nikaamua kumwuliza juu ya Jane jinsi walivyojuana naye. Hapo kikatokea kizaazaa kingine ambapo dada yangu akaanza kulia huku akisema. Mdogo wangu wakati naingia jeshini nilipita mapito magumu na ya aibu sana. Hivyo nilipokuja kuajiriwa niliapa kulipa kisasi kwa wote walionitesa. Walikua ni viongozi wakubwa na wafanyabiashara walinibaka na kunidharirisha. Wakati natafuta namna ya kulipa kisasi ndipo hapo nikawaona mabinti watano pale jeshini wakiwa wamepita mapito kama yangu. Na mmoja wao ndie Jane hivyo nikawaomba msaada kwa makubaliano ya kuwalipa.
Nikamkatisha sasa mbona niliwahi kuona Jane amekuweka kwenye orodha ya wanaotakiwa kuuawa? Dada yangu aliniangalia kisha akasema.....
Haaaa kumbe Jane aliniweka kwenye orodha ya wanaotakiwa kuuwawa. Jamani inaonyesha una ukaribu fulani na Jane umemjuaje?
Dada yangu aliniuliza hivyo...!!? Nikamsimulia kila kitu ndipo aliposhtuka sana na kusema mtu ambaye alimtuma akamuue Mbeya ndie aliyedhulumu mali kwa baba. Nikashtuka sana sasa kama ni huyo alimdhulumu baba si ndio huyo alikua na mahusiano na mama? Inamana ndie baba yangu? Nilijikuta chozi la uchungu likinidondoka Dada yangu nae alilia sana akisema sikujua mdogo wangu haya yote nimeyajua wakati nikiwa mkubwa.
Baada ya kujuana na baba na kujua kuwa hakufa. Nililia sana kiukweli mpenzi msomaji. Sasa nikawa najisemea ikiwa aliyeuawa ndie baba yangu inamaana mimi nimefanya mapenzi na mke wa baba yangu.
Haitoshi nimezaa nae. Zaidi nimezaa pia na mtoto wake yaani Happy ambaye ndie dada yangu. Mle ndani kulitawaliwa na vilio kila mmoja akilia kwa uchungu. Nilijihukumu sana nafsi yangu na kuwaza iwapo mke wa marehemu baba atajua ya kuwa mimi ni mtoto wa mumewe itakuaje? Na zaidi siku akijua kuwa yule mtoto wa Happy ni wa kwangu itakuaje? Ina maana nimewachanganya na kuwazalisha mama yangu wa kambo, na dada ninaeshea naye baba...daah!!!
Nikaona siwezi kukubali aibu hiii ni afadhali kufa ili niondokane na aibu ile. Nililia sana huku nafsi ikijutia kwa tamaa zangu za kupenda na kukubali kwa kila aliyenitaka. Nililia sana kwa kweli. Pembeni hivi nikakiona kisu nikaona bora nijichome na kufa. Nikainuka na kukichukua kile kisu. Dada yangu alinyanyuka na kuanza kunibembeleza sana huku akisema hapana yuu mdogo wangu. Makosa tumeumbiwa binadamu kwanini ujiue. Usimkufuru Mwenyezi Mungu aliekuzawadia uhai. Ni wangapi wamekufa.
Maneno ya dada yangu yalikua ni kelele za chura. Bado nilishikilia msimamo wangu wa kujiua. Nikazidi kujiweka sawa huku kisu nimekilekezea tumboni. Dada alilia huku akinisihi sana. Lakini wakati nimeinua mikono ili nishushe kisu kitue tumboni. Ghafla kuna kitu kilipiga kisu changu na kuanguka. Nilishtuka ni nini lakini sikujua. Pale pale dada yangu akasema Jane kaingia hapa na watu wake. Nikamwuliza umejuaje akajibu hicho walichorusha ni chuma fulani ambacho huwa kama nyota na kinanolewa kote. Kikipita mkononi au mguuni kinakukata. Na kikipita shingoni Unakufa hebu njoo huku tuchukue tahadhari.
Nilianza kujihami na kusogea kwa dada yangu. Lakini wakati namfuata kuna chuma kikapita kwa kasi na kumchoma dada yangu tumboni. Kiukweli kilikua kimezama na kupotelea chote tumboni. Nilimwona dada akimwaga damu nyingi sana. Niliamua kumwacha dada pale ili nianze kuwatafuta. Nilinyata kwa kuelekea nje. Ghafla nikakutana na msichana mmoja mrembo akiwa amevalia skin jinsi ya blue na top nyeusi. Huku mkononi akiwa na bunduki aina ya SMG.
Kuniona akaninielekezea bunduki na kunitaka nitulie. Nikainua mikono juu na kugeuka. Lakini ghafla eneo lile likavamiwa na wanajeshi wakawa wanatembeza kichapo lile eneo lote. Hawakuwa wanajali mtu yeyote aliyekua eneo lile alipokea kipigo. Nilishtuka yule mrembo nyuma yangu akianguka. Nilijua tuu atakua kapigwa na wale maafande. Basi mimi nikatoka mbio hadi kwa dada yangu. Kiukweli alikua na hali mbaya sana. Kwa kuwa nilikua na nguvu kiasi nikaamua kumbeba dada yangu ili nimuwahishe hospitali akapate matibabu.
Haikua kazi rahisi sana. Nilitoka baada ya kufika nje nilipata msaada wa Wanajeshi. Wakampakia
kwenye gari hadi Hospitali Ya Amana. Wakati tunafika dada yangu alikua kapoteza fahamu. Nijilaumu sana. Madaktari wakasema anahitaji kuongezewa damu na mimi bila hiyana nikaitoa. Akaongezewa baada ya masaa kadhaa hali yake ikaanza kuwa nzuri nilimshukuru sana Mungu.
Lakini tukiwa hospitali ikumbukwe nilikua natafutwa na na polisi. Ghafla waliingia polisi mle ndani na kuniweka chini ya ulinzi kwa makosa ya kutoroka jela. Nilikua sina Jinsi lakini nafsi yangu sasa ilianza kutulia kwani ukweli nilianza kuujua. Japo inaonyesha kulikua na siri kubwa nyuma ya pazia. Nilikua najiuliza yule niliyekua namwita boss wangu alianzaje kunisaidia? Je alijua mimi ni mwanae? na mbona hakutaka kuniambia kama alikua anajua? Nikasema tena Kwanini asingeniambia kama alijua ona sasa nimezaa na dada yangu yaani Happy.
Niliumia sana kiukweli nikaanza kulia nikiwa kwenye difenda ya polisi. Nilikua nawaza mengi sana nilijikuta uchungu na machozi yanatoka bila kukoma.
Nilifikishwa jela nikapokelewa kwa kipigo kitakatifu na adhabu kali. Bila hata kujua maelezo yangu. Sitaisahau adhabu moja nakumbuka nilizidiwa hadi nilizimia. Walinifunga juu ya meza huku uso wangu ukiangalia juu. Wakanifunga na kitambaa kilichoziba pua na mdomo. Kisha wakawa wananimwagia maji. Kila nikitaka kupumua maji yanaingia puani na mdomoni daaah!!! Asikwambie mtu ile adhabu ni mateso kiukweli na yanaumiza.
Niliteswa sana tena sana huku wengine wakisema tumkomeshe anajifanya mjanja. Nlijikuta nimezidiwa nguvu na kilichoendelea sikumbuki.
Nilikuja kujikuta niko chumba fulani nimefungwa na nyaya kwenye kiti. Nilimwona dada mmoja akichukua prise na kuniambia panua mdomo, nilitii haaa!! nilikua nang'olewa meno bila ganzi. Niliumia sana nilitolewa meno matatu la mbele moja na nyuma mawili. Kiukweli ilikua ni uchungu sana japo sikua na lakufanya. Niliumia sana mpenzi msomaji wa makala hii. Baada ya muda wakaamua ya kuwa nihamishwe Gereza. Na kupelekwa gereza ya jingne. Kwakuwa nilijua kule naenda kukutana na polisi wapya nikaona itakua afadhali kwangu. Basi baada ya siku kadhaa kupita huku nikiwa naugulia kwa maumivu makali. Naikumbuka sana siku niliyokua nasafirishwa mimi na wafungwa wenzangu kutokea Dar es salaam gerezani kuelekea gereza Hilo jingne.
Tukiwa njiani maeneo ya bonde la mto Wami. Ghafla kalandinga yetu na msafara mzima ukavamiwa. Zilisikika risasi zikirindima kuelekea kwetu kisha.......
Wakatokeza wanaume wanne waliojaza miili yao. Walikua na siraha za hatari. Wakazidi kumimina risasi huku wakiua baadhi ya polisi. Lilikua tukio kubwa na la kutisha. Nilitamani kutoka nje ya gari ili nikimbie lakini ningewezaje tulikua tumefungwa pingu kwenye vyuma vya gari.
We una my
Baada ya kuwaua polisi wote huku wao wakiwa salama kabisa wakaja na kuingia ndani ya Karandinga. Wakaangalia kisha mmoja akaipiga kwa bunduki ile pingu yangu. ikalipuka na kufunguka kishaway my m akasema kijana njoo!!! Niliinuka kwa woga na kuwafuata. Walinishika baada ya kutoka nje ya karandinga. Ilikuja gari moja Aina ya Rangerover sport.
Nikachukuliwa na kuingizwa mle ndani nikiwa peke yangu yaani wafungwa wengine wote waliachwa. Basi wakaondoa gari kwa kasi huku wakiwa wamenifunga kitambaa usoni na mikono wakiifunga kwa nyuma. Mdomo wangu wakiubana na soltep. Nilikua natamani japo kusema neno. Ningewezaje yuu mimi nilikua nimewezwa na wajanja. Njiani nilikua nawaza mambo mengi. Huku kubwa likiwa ni juu ya Mke wa marehemu baba yangu nikiwaza akija kujua kuwa mimi ni mtoto wa marehemu mume wake. Na amezaa na mimi. Zaidi akijua kuwa hata mtoto wa Happy ni wangu. Yaani nimezaa na mama na mwana. Akili yangu haikua inawaza wapi napelekwa. Kubwa nilikua nawaza hali ya maisha yangu.
Huku safari ikiwa imepamba moto. Tulifika sehemu wakasimamisha gari na wote wakashuka. Nilihihisi hivyo kwani niliwasikia wakibishana nje. Baada ya muda wakarudi na kunishusha nadhani tulikua tunabadisha gari. Basi baada ya kupanda gari liliwashwa na kuondolewa kwa kasi. Baada ya muda tulifika sehemu wakanishusha na kunipitisha sehemu fulani. Baada kama ya dakika kadhaa wakanifungua kitambaa na kunifunga kwenye nguzo fulani mle ndani na baada ya muda wakaniacha pale huku mdomo wangu umefungwa.
Nilijiinamia pale nisijue la kufanya. Kisha baada ya muda nilisikia mabishano yao na mtu ambae kwa hakika ile sauti niliitambua haraka. Huku wakisema Mtu wako tumeshamuua bwana. Sauti ya Jane ilisikika ikisema mimi sikutaka mumuue nina shida naye. Wenzake wakasema tulizidiwa nguvu tungefanya nini. Jane nikamsikia akifoka kwa sauti kali sana.
Na mara ya kwanza niliwapa dili juu ya mtu huyo mkanambia kuwa mmemuua bahati mbaya. Kumbe alikua akiwasaidia kazi kule koko beach. Na leo hivohivo.
Nilishtuka sana kusikia Jane akiongea vile nikajisemea moyoni inamaana Jane ndio slalichoresha dili ya mimi kukamatwa. Mungu wangu inamana Jane anajuana na mhindi yule alieyetaka kunilawiti...? Haah!!! Ina maana hata leo yeye ndio kahusika kuniteka mbona aniulizia. Lakini. Sikua na la kufanya. Machozi yalinibubujika sana tena sana.
Basi nikamsikia Jane akisema mjue nyinyi madam alisema niwaue kwani ndio mlimpeleka Afrika ya kusini na kuanza kumfanyisha kazi zenu za madawa. Halafu cha kujua ni kwamba huyu na madam ni mtu na mdogo wake. Hivyo akijua kuwa mmemteka mdogo wake patachafuka hapa.
Basi mmoja akasema kwani we utaenda kusema si na wewe atakuandama acha mambo yako ya kisen*e. Basi Jane akasema ninachotaka ni kujua huyu mtu yuko wapi? Wakazidi kusisitiza ya kuwa tumemuua kwa sababu polisi walituzidi nguvu. Jane akasema kama ndo hivyo bora tukose wote mimi nalipua hiii nyumba. Ili kama yumo ndani afe tu tukose wote.
Kusikia vile nilitamani niite hata kwa sauti ya kuwa nipo huku. Lakini ningeongeaje mdomo wangu ulikua umezibwa. Nilibaki kuwasikiliza wakibishana ubishani wa hali ya juu. Baada ya muda nikamsikia Jane akisema Guys mi naondoka ila mjue mimi ndo hua nawafanikishia mipango hivyo kunigeuka kwenu tumekua maadui kisha nikamsikia akiondoka kwa hasira.
Wale jamaa waliobaki wakaanza kusemezana kwa kusema huyu hanaga masihara. Chakufanya ni kumchukua huyu nguruwe tumfikishe kwa boss. Mmoja nikamsikia akisema tungemuua kabisa kwa sababu boss kasema kuna mzigo unatakiwa kusafirishwa kesho na maiti zimeisha. So alisema tukifanikiwa kumkamata huyu tumuue ili asafirishe mzigo kesho kwenda Dubai. Kwa kuwa nilikua nawasikia vizuri nilikua najililia tu ya kuwa siku yangu ya kufa imefika. Mmoja akasema masela kwa hiyo tunammuuaje. Mkumbuke hatakiwi kuwa na jeraha maana maiti zenye majeraha huwa haziwezi kudumu. Mwingine akadakia kwa kusema tumchome sindano ya sumu kisha akikata roho tumpeleke koko beach. Nilikua nawasikia kila wanachopanga nikajisemea moyoni ukisikia kufa huku unajiona ndio leo. Nililia sana.
Nikiwa pale kwa mbali kama wa sentimita kadhaa nilikiona kioo. Basi nikahisi chaweza kuwa msaada huku wao wakizidi kupanga mipango yao. Nikajivuta kidogo nikatumia miguu kupiga ile meza yenye kioo. Mwisho kikadondoka. Baada ya kudondoka nikamsikia mmoja akisema. Hebu kachukue sindano umchome haraka tupotee hapa. Basi mimi nikakivuta kwa miguu kioo kile. nikakibonda mara kadhaa kwa miguu kisha kikapasuka vipandevipande.
Nikavisogeza nyuma ya mikono ili nijaribu kuikata ile kamba. Vioo vile vilinichoma sana mikononi nikiwa na harakati za kujiokoa. Sikujali hilo hata kidogo mbele ya uhai, nikaumia sana lakini nikajikaza kiume.
Nikiwa katika harakati za kuikata kamba ile nilimwona jamaa mmoja kati ya wale waliokua wameniteka. Alikua anakuja ameshika sindano yenye sumu. Alikuja na kunikaribia pale nilipo. Huku akijiamini Akaiinua na kuiangalia kisha akawa anaishusha kama anaielekeza begani kwangu ili kunichoma Kisha taratibu.......
Akawa anaidunga mwilini mangu. Ashukuriwe Mungu ambaye aliwezesha mikono yangu kuikata ile kamba niliyofungwa nayo mikononi. Japo nilikua nimeumizwa sana na vioo vile katika harakati za kutaka kujiokoa. Niliinua mikono kwa taratibu kisha nikakusanya nguvu na kumsukuma kwa nguvu zote yule jamaa.
Alikua ni mnene na mwili wa mazoezi lakini kwa nguvu niliyotumia alifedheheka. Alianguka mithili ya kiroba cha mchele. Niliichomoa sindano mwilini mwangu kwa kuwa alikua bado hajaminya dawa iingie mwilini. Basi nikamfuata na bila huruma nilimchoma nayo shingoni. Nikaminya hadi nikahakikisha dawa yote imeisha. Kwa sababu ya hasira nikahisi sijatosheka nikaichomoa na kuidunga tena. Ile sumu ilikua kali sana asikwambie mtu. Maana pale pale alianza kama kutetemeka kisha akakata roho na kukauka Happ hapo.
Nikajihami na kujifungua ile plasta mdomoni. Mikono yangu ilikua inavuja damu kwa kuwa nilikua nimejiumiza na vioo. Nilijifungua na kuanza kutoka. Nilijihadhari sana nikiwa natoka nilimsikia mmoja akisema huyu mjinga kang'ang'ania huko huko. Hebu nenda kamcheki. Kusikia vile nikacheki pembeni kulikua na nondo.
Nikaichukua na kujibanza mahali. kwa tahadhari niliiweka tayari nondo ile. Baada ya muda nilimwona anakuja nikakaa sawa. Nikainua nondo na kumpiga nayo usoni kwa nguvu zote. Alianguka kwa kishindo nikajua tayari wengine watataharuki. Nikamwinamia na kumpora bastora. Wakati nainuka nilishtuka kuona nimewekwa mtu kati huku nikiambiwa acha silaha chini. Nikiwa nashangaa.
Ghafla waliingia watu mle ndani walikua ni wadada kwa maumbo yao. Walikua wanevalia mavazi yaliziba nyuso zao. Walianza kupiga risasi hovyo. Baada kama ya dakika moja hivi pale ndani pakatulia. Nilishtuka na kuona wale jamaa wote wako chini. Wale wadada wakanitaka nitulie kisha wakanifunga mikono na kunitoa nje. Wakanipakia kwenye gari iliyokua na vioo vyeusi Yaani tinted.
Nilikua bado cjajua niko wapi. Gari ilitolewa kwa kasi sana hadi tukafika sehemu ambayo pia hadi leo sikumbuki ni wapi? Ikasimamishwa na wakanishusha. wakati nashuka nilishtuka sana kumwona dada yangu akiwa mbele yangu. Nikajikuta nalia kwa furaha baada ya kujua kuwa dada yangu kaniokoa. Nikamsogelea dada yangu akanikumbatia na kunibusu.
Basi tukarudi ndani ya lile gari sikutaka hata kuuliza ni wapi pale. kwani moyo wangu ulikua umejaa furaha. Tulifika sehemu ambapo nadhani ilikua ni hotel tukashuka na kuingia dada alichukua vyumba viwili kimoja changu na kingine chake. Usikiu ule tulilala bila kupanga chochote. Asubuhi tuliamka na kuanza mipango ambapo dada akasema kwanza tumtafute baba kisha tuongee naye. Halafu baada ya hapo tumalize biashara ya Jane. Na tukitoka hapo tukaibe file langu mahakamani na kisha ikatwe rufaa ili kwa yale makosa ambayo nina hatia iwe hakuna ushahidi.
Kisha akasema tukimaliza hapo. Turudi Mbeya tukiwa na baba halafu aongee na mke wa boss ili kila kitu tuombane radhi na kusameheana ili yaishe.
Zoezi likaja kuwa gumu kwenye kuiba file na kummaliza Jane. Lakini kwa kuwa dada yangu alikua mwanajeshi nikaingiwa na imani ya kuwa kitu hicho ni rahisi tu. Ni baada ya siku kadhaa Tukaanza safari ya kuelekea Arusha ili tukamtafute baba kwanza. Safari ya Dar es salam to Arusha ilikamilika salama. Tulifika tukatafuta hoteli ya kulala. Huku mimi nikitakiwa kuwa makini sana kwa kuwa nilikua natafutwa. Yani hadi pale nilikua natembea kwa hisani ya dada yangu. Bahati mbaya hata dada yangu hakuwa anajua baba anaishi wapi. Tulichokifanya ni kuanza kumtafuta kwenye kumbi za starehe na sababu kubwa za kumtafuta kwenye kumbi za starehe ilitokana na ukweli kwamba baba yetu alikua akipenda Sana kucheza Kamali.
Hilo lilikua jambo gumu kiasi ambapo tulizunguka kumbi nyingi lakini hatukumwona baba yetu. Basi siku moja naikumbuka wakati tupo ukumbi mmoja Tulimwona baba yetu mle ndani. Baada ya kumfuata Tulishangazwa na majibu yake maana alikana kutujua na kututishia kuwa atatuitia polisi kama hatuelewi.
Kwa kuwa tulikua wote dada akashauri tumwache ila tuulizie ni wapi anaishi ili tumfuate nyumbani. Shughuli ikawa kila tuliyemuuliza akasema hajui ila wanahisi huwa anaishi kwenye hotel kubwa kubwa. Kwa kuwa dada yangu alikua ni askari akaamua kutumia mwamvuli huo ili kupita kila hotel akiiangalia majina ya wageni wanaolala.
Shughuli ile ilikua ngumu kweli kweli ambapo aliniomba msaada wangu. Tulizunguka hoteli nyingi sana. Mafanikio yalikua hakuna. Lakini hatukukata tamaa. Sasa kuna siku tukiwa katika kazi hiyo, Tulifika hoteli moja hivi na kuangalia majina lakini hatukuona chochote. Wakati tunatoka sasa hapo ndipo utata mwingine ukaanza. Tulikutana na mtu ambae hatukutarajia kumwona pale. Cha ajabu mtu aliekua naye. Ilionyesha walikua na mahusiano. Hakua baba bali alikua ni.....
.Mama yaani mke wa baba yangu ambae alikua ni boss wangu. Nilipagawa kiukweli kwani yule mama niliahi ambiwa ya kua ni malaya hadi pale nilikua nimekwisha kuthibitisha. Naye alishtuka sana kisha akaanza kuniuliza vipi mwanangu kuna nini tena huku? na huyo ulie naye ni nani yako?
Aliingiwa na mfululizo wa maswali mengi huku ankijiumauma. Nikajua tuu ni kwasababu ya aibu. Mimi kwakua sikutaka kumwaibisha nikaanza kwa kusema. Mama huyu ni dada yangu kabisa. Nafhani nimewahi kumgusia kidogo katika maongezi fulani mimi na wewe. Kama una kumbukumbu nzuri. Akajibu ndio nakumbuka basi nikamwambia ndo huyu sasa. Akasema sawa mnaelekea wapi?
Baada ya kuona amekua na maswali mengi. Mi nikaamua kumwelekeza mahali tulipofikia ili akija tungee kwa kina. Basi tukatoka na kuzidi kusonga na kazi yetu. Tukiwa njiani tunaenda hotel fulani mi nikapigiwa simu na namba ngeni. Basi nikaipokea na kuisikia sauti ambayo haikua ngeni sana masikioni mwangu. Ilikua ikisema hallow mimi ni muhudumu wa botel fulani mlikija kuna mtu mlikua mnamtafuta sasa kuna kitu nakijua juu ya huyo mtu naombeni tukutane. Nikamwuliza tukutane wapi sasa. Akajibu itakua vema kama hiyo sehemu itakua nje kidogo ya mji huu kwani ana siri kubwa hivyo sitaki matatizo. Mmmh niloguna kisha nikamwukiza kwahiyo we unapendekeza eneo lipi ili sisi tuje.?
Akajibu tukutane Maeneo fulani ya jiji hili la arusha sehemu inaitwa Kikatiti. Mmmh kwanza niliingiwa na woga kwani ile sauti nilihisi naifahamu. Pili nikawa nashangaa kwanini ataje eneo hilo ambalo ni nje ya mji kabsa? Nikamweleza dada yangu ambae alionekana kukurupuka bila kufikiri na kusema twende mara moja.
Nilikubaliana naye lakini akili yangu ilikua hainitumi kabisa. Basi tukafika maramoja sehemu aliyotaka tukutane na kukuta hamna mtu. Wakati natoa simu ili nipige ile namba Ghafla tukamwona dada mmoja akija karibu yetu na ,kutusalimia. Kisha akasema mnaombwa muingie kwenye huu msitu huyo mtu yuko humo anawasubiri. Mmmh nilishtuka kidogo lakini nikaona ngoja twende tuliingia mle msituni kisha tukasimamishwa sehemu. Ghafla kundi la watu kama watano hivi wadada warembo wakatuzingira. Mmh nikajua tayari tumeingia mkenge.
Basi akajitokeza mmoja na kusema sasa ni hivi kuanzia sasa mko chini ya ulinzi. Mko kwenye himaya ya Jane afande na gaidi wa nchi hii. Maneno yale yalinishitua sana. Nikaona tayari Jane atafanikiwa kumwua dada yangu. Nikainua kichwa ili nimwangalie dada yangu nilipigwa na kitu kizito nyuma ya kichwa changu kisha nikaanguka. Nadhani nilipoteza fahamu kwani sikua kilichojiri baada ya pale nikashtuka niko kwenye kochi nimelazwa. Nikainuka ili niangalie ni wapi pale. Nikashtuka sana kumwona Jane na Angel mbele ya uso wangu. Nilifikicha macho na kuhisi ndoto. Lakini ilokua ni ukweli usipingika kia ninachokiona ndicho hicho kilichopo.
Niliingiwa na woga kisha nikawasikia wakisema kidumeeee!!! Leo umewekwa katikati ya wababe wa kike uliokua ukiwatia kwa nyakati tofautitofauti ukijiona wewe ni mjanja kumbe mjinga wa kutupwa. Hatimae adui yetu mkubwa kumbe ni dada yako! Tunamwua mbele yako kwasababu hana tena ujanja na hicho mnakitafuta sijui ndo kibaba yenu tumekiteka hakina ujanja. Tunakiua mbele yako kisha tunakiwinda kile kisokolokwinyo kimalaya chenzio kkmke cha boss wako. Tukiua na hicho kazi yetu itakua imebaki kukumaliza wwe sijui unaonaje mipango yetu? Walikua wanaongea kwa nyodo huku wakipokezana.
Basi mimi nilibaki nawaangalia huku nikiingiwa na hasira nikikereka na vimaneno vyao vya ajabuajabu. Basi Jane akaamuru waletwe mbele yangu baba na dada yangu. Baada ya mda mfupi alibwagwa baba akiwa amechoka chakari.Kisha akaletwa dada yangu akiwa amefungwa vibaya huku akiwa ametapakaa vidonda mwili mzima.
Niliingiwa na hasira sana. Kisha nikamsikia Jane akisema huna ujanja Yuu dada yako ndo alikua ananituma niue watu kwa matatizo yake. Na kwakua alikua akinituma kuufanya dhambi kubwa nikaapa nikija kuwamaliza wote na yeye lazima nimwue. Bahati mbaya au nzuri wewe nimeshakuua kwa UKIMWI. Nilishtuka sana kusikia vile kisha kwa sauti ya uchungu huku nikibubujikwa na machozi nilimwuliza dada yangu je yeye ndie aliekua anamtuma Jane kuua.
Dada yangu akasema ndio mdogo wangu ilikua ni kwasababu niliteswa sana. Niliwahi kudhalilishwa na Afisa mmoja wa Jeshi la polisi wa mkoa fulani. Yeye alinidhalilisha kingono alifanya mapenzi na mimi kisha akanifanyisha mapenzi na mbwa wale wa polisi. Kuna mawazili na wakuu wa majeshi walinifanya wanavotaka hawakuthamini utu wangu hivyo nikaamua kuwaua wote. Wafanyabiashara wote waliowahi kuninyanyasa adhabu ya kifo iliwahusu. Sikutaka kujihusisha moja kwa moja kwasababu mimi nina cheo kikubwa jeshini.
Niliamua kumtumia Jane na kikundi chake kwasababu wao walipitia udhalilishaji kama wangu. Hata mimi nimeathirika mdogo wangu. Maneno ya dada yalikua makali kama maumivu ya mtu anaekata mwili wangu kwa msumeno. Niliumia kisha nikaishia kulia. Mara Jane akasema sasa naanza kuua mmoja baada ya mwingine.kisha akatoa bastora na kuielekeza mara mlio wa risasi ukasikika paaaaaaah!!!!!..........
Mara nikamwona Angel anaanguka chini puu! Nilishtuka sana kisha nikamsikia Jane akisema "sijawahi kua na ndugu wala rafiki nitabaki mwenyewe maisha yangu yote"
kisha nkasikia paaah!! kwa mara nyingine. Huu ulikua mshituko mkubwa kwangu kwani nilimwona baba yangu akianguka.
Niliumia sana nikamsikia baba akisema kwa shida "
"wanaaa waaa wanaang... wana.....naaa...ng....uuuu Mni.... ssss...am..eheee naa naa nasaa.. Muishi. kwaaa kwaa kwaa.. Kupenda..... kupenda...naa."
Mara akakata roho. Ilikua kwa mara ya kwanza nashuhudia dada yangu akilia kwa uchungu sana. Niliingiwa na hasira na gadhabu kali sana.
Ilikua pia kwa mara ya kwanza namsikia baba yetu akisema samahani kwa yote.
Baada ya kutafakari hayo nilijikuta napata ujasiri wa ajabu. Niliinuka na kumfuata Jane kwa kujitutumua nikamvaa mzimamzima na kumbeba juujuu hadi ukutani.
Kisha nikambwaga chini puu!! Nikaokota bastora yake na kumwelekezea Jane ambapo wapambe wake walimwelekezea dada yangu wakinitaka nimwache Jane huru.
Niliona yakua potelea mbali wakimuua dadangu. Na mimi ningemwua Jane bila kujali lolote hata kama mimi pia nitatakiwa kufa ni sawa.
Niliwaangalia nikawalia targeti kiasi kisha nikajifanya kusalimu amri. Nikawa kama nainuka huku kama naweka bastora chini. Kisha niliwafyatulia risasi mfululizo kisha wakaanguka chini wote.
Sasa chumba kikawa kimebaki na Jane mimi na dada yangu na Maiti zile zote. Kwakua nilimwona Jane ameanguka na hajiwezi
nikamfuata dada yangu na kumkumbatia. Haaa ilikua kosa Kumbe Jane alijikongoja na kuokota bastora na kusimams kisha "PAAAAAAAAAAH"
akampiga dada yangu risasi ya bega. Kizuri ni kwamba kila alipojaribu kuongezea kupiga risasi zilikua zimeisha. Hasira na kisasi viliukamata moyo wangu na kuusukuma kwenda kuua kabisaaa.
Ndipo nilijituma kumfuata Jane kisha nikamvuta miguu kwa nguvu.Hali ile ilisababisha aangukie kisogo kwa kishindo sana. Niliinuka na kumshika shingo kisha nikaipindua kwa nguvu na gadhabu kuu. Ilisikika ikilia
"khaaa!!!"
Huo ukawa mwisho wa habari za Jane. Nilikua nalia kwa hasira nikainuka na kwenda kumfuata dada yangu nikamwona akiwa taabani anatapatapa.
Nilimwinua dada yagu na kumweka juu ya bega kumkimbiza hospitalini. Nilimfikisha zahanati fulani akapokelewa ila tayari alikua kapoteza fahamu.
Alihudumiwa pale kwa siku kadhaa mara baada ya hali yake kutengamaaa tuliamua kurudi Mbeya ili tukamalize kazi. Safari hadi Mbeya ilianza Tulifika Mbeya na kumweleza yule mama mambo yote ambapo yeye alikua akilia tuu.
Nikamweleza juu ya mtoto wa happy kua ni wangu.
Pia housegirl kua alikua na mwanangu. Na mwisho Kua mume wake ndie Baba yangu mimi. Alilia sana mke wa boss wangu akajilaani sana kwanini yale yote yametokea.
Mimi pia nilikua nalia sana. Kwani Nilijua kua yale ni fedheha "PENZI LA MKE WA BOSS" Limesababisha aibu kubwa maishani mwangu.
Lakini ikabidi housegirl afuatwe na kuletwa baada ya siku kadhaa. Kisha tulijikusanya wote na kwenda kupima VVU ambapo woote tulikutwa tumeathirika yaani mimi, Mke wa boss, wanangu wote watatu, happy, na pia housegirl.
PENZI LA MKE WA BOSS lilisababisha mimi kuathirika. Limesababisha mimi kujua ukweli wa maisha yangu. Sikutaka kujua mke wa boss ameua wangapi kwani alikua ni malaya sana. Penzi lake kama mke wa boss liliwarubuni vijana wengi hakika alituteketeza wengi sana. Niliumia lakini ilibaki kuomban radhi na kusahau yaliyopita na kuanza maisha mapya.
Basi baada ya kurudi nyumbani tulikua tunapanga namna ya kuweza kuiba file laNgu mahakamani. Lakini siku moja ghafla tulivamiwa na polisi na mimi kukamatwa kwa kesi nyingi mno.
Mauaji niliyofanya kwa Jane na kundi lake yalinihusu. kisha na makosa ya kutoroka Jela yalinihusu pia. Nililia sana. Baada ya kusomewa mashtaka yangu upya na kupatwa na hatia nilihukumiwa kifungo cha miaka 35 Jela na kazi ngumu.
Niliumia sana kuyarudia maisha ya Jela kwa mara nyingine. Nilikaa kwa mda wa miaka mitatu segerea. Ambapo nikatolewa siku ya tarehe 9-12-2013. kwenye msamaha wa Rais ilikua ni sikuku ya uhuru wa taifa letu. Sababu za mimi kutolewa ilikuani kwasababu nilikua nimeathirika kwa UKIMWI na tayari afya yangu ilianza kuzorota nikiwa Jela.
Nilitoka na kurudi Mbeya na kuendelea na maisha ya kawaida. Huku nikiwa kijana mwema. Kwa uchungu namateso yaliyosababishwa na baba yangu. Lakini mateso mengi ilikua ni kutokana na "PENZI LA MKE WA BOSS" Nilianza kuwalea wanangu huku tukiwa wote tunatumia vidonge vya ARVs kwaajili ya kuujenga mwili. Hadi sasa naandika simulizi hii nahtaji wewe baba, Mama, Kaka, Dada, Mdogo wangu, na yeyote ajifunze kupitia makosa niiyoyafanya mimi hadi leo kua hapa nilipo. Funzo kwa yeyote ambaye hatopenda kupitia maisha ambayo Yusuph ameyapitia.
NATUMAI UMEJIFUNZA KITU HAPO NDUGU YANGU
MWISHOOOOOOOO

0 Comments