Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Responsive Advertisement

Chombezo: Mke wa Bosi sehemu ya tisa (09)



Niliogopa sana kusikia maneno yale. Nikawauliza sababu za kunikamata kama mtuhumiwa namba moja. Wakadai kwanza Kitambulisho chako kilipatikana eneo la tukio, pili Ushahidi wa picha unaonyesha kuna mateka mimi niliondoka nae eneo la tukio na kutokomea kusikojulikana. Nilianza kujitetea na kusema

"kuwa yule ni baba yangu na nilikua namwokoa na majambazi". Basi ndipo waliposema "yule ndiye alieleta taarifa ya kuwa ulikua unajaribu kumteka na kumwua hivyo wasamalia wema wamemsaidia.

Na hivyo ndivyo ulivyoingia katika utuhumiwa na jeshi limefanya upelelezi na kujiridhisha kwa ushahidi ilioupata kuweza kukutia nguvuni". "Sasa kazi imebaki kwako ni moja tuu kutusaidia kuwapata wenzako kwa amani kabisa. Ikiwa imeshindikana sema.

SOMA MBINU ZA KUPATA WAFADHIRI WA UJASILIAMALI

Niliwaza na kuwazua nitaanzia wapi na hata jambazi mmoja sikumwona hata kwa sura. Nikiwa nimezubaa pale nikainuliwa na kupelekwa chumba ambacho kiliitwa chumba cha mahojiano. Humo ndani kulikua na...



Vifaa vya ajabu sana, mikasi, shoti za umeme, spoko, misumari,Nyundo na nyaya za ajabu, na sindano, na baadhi ya vifaa vilivyokua vinaharibu kabisa amani ya moyo wangu kwa kweli. Nikapigwa na njemba moja nikakalishwa kwenye kiti kwa ngumi ile Kali sana. Nilifungwa na nyaya pale kwenye kiti kile cha chuma. Askari wote wakatoka. Kisha walikuja wanaume wawili. Hawa walikua wanaume haswaaa. Walikua wameshiba wametuna vifua na miili iliyogawanyika mithili ya matuta.

SOMA MBINU ZA KUPATA WAFADHIRI WA UJASILIAMALI

Niliulizwa "unataja wenzio au hautaji" na mimi nikajibu "siwajui" kwa kwe.... Nilikatishwa na kiwiko kilichotua kifuani na kufanya nikohoe damu. Nikaulizwa tena "unataja au hutaji." Nikajibu tena "siwa...." Ilikua kosa nilishambuliwa na ngumi za wale jamaa wawili baada ya sekunde kama ishirini hivi. pua mdomo, na masikio vilikua vikivuja damu. Nikaulizwa tena "unataja au hutaji?"

"Kweli tena siwajui afande". Nilijibu huku nikitetemeka na damu ikivuja mdomoni. Machozi yalitosha kulowanisha mle ndani.

SOMA MBINU ZA KUPATA WAFADHIRI WA UJASILIAMALI

Basi ikaletwa spoko ya moto ilikua imepashwa kwa nguvu ya umeme. Ndugu yangu polisi hakufai. Nilivuliwa nguo. Bila huruma waliitia spoko ile kwenye uume wangu wakifuata shimo la kukojolea.

Huku wakisema atataja tuu.

SOMA MBINU ZA KUPATA WAFADHIRI WA UJASILIAMALI

Sidhani kama duniani kuna maumivu makali kama yale. Niliumanisha meno kwa uchungu nisiweze kufanya lolote. Kisha wakaiacha spoko ile ndani ikiwa imegusa kibofu cha mkojo. Nilivuja mikojo mle ndani. Baada ya kuichomoa wakanichoma na shoti mgongoni. Kiukweli nilitaabika kwa makosa ambayo sikuyatenda. Niliumia sana tena sana. Nilichomwa na sindano mwili mzima nikawa ni maumivu tele. Sikua na la kufanya machozi yalimiminika, nililia Sana hadi yalikauka yote yakawa haystoki. Uchungu uliandamana nami kama vile kivuli kisivyoniacha. Niliumia sana kiukweli lakini sikua na chakufanya.

SOMA MBINU ZA KUPATA WAFADHIRI WA UJASILIAMALI

Basi baada ya kuona hali yangu ni mbaya sana. Wakasemezana kisha wakanifungua na kuniamuru nisimame. Nilikua siwezi hata kusimama nikaanguka. Kwa kuwa mle ndani vifaa vingi vilikua na mcha kali nilichomwa sana na tuvitu tudogo tudogo kama tumisumali. Maumivu yalizidi maradufu nililia sana. Nikaburutwa hadi mahabusu. Ambapo huko vijana walikua wengi kiasi. Huko nilipokelewa kwa kukanyagwa na maneno ya kejeli na dharau. Kwa kua nilikua na maumivu. Nilizidishiwa mara dufu. Siku iliyofuata niliburutwa na kupakiwa kwenye karandinga. Nikajikuta nashushwa mahakama ya hakimu mkazi.


Cha ajabu ilikua ni mimi kusomewa mashtaka mapema kiasi kile. Nilisomewa mashtaka nakumbuka yalikua matatu hivi.

1.bkula njama na kufanya mauaji.

2. Kumteka mtu na kutaka kumwua kwa makusudi.

3. Kuvamia na kuharibu mali za watu.

Hayo ndo yalikua mashtaka yangu. Niliulizwa kama nina la kujitetea. Baada ya kuulizwa vile nilianguka na kuzimia kweli sijui nini kiliendelea.


Nilishtuka niko mahabusu tena. Nilijiuliza maswali mengi sana kuna kesi nyingi nchi hii zingine huwa zinachukua hata miaka minne hadi mtu kushtakiwa. Iweje kesi yangu iende haraka vile. Nikiwa nawaza mahabusu mmoja akaropoka

" we msen*e kesho unasomewa hukumu yako".

Mwingine akadakia "uyu mtoto mzuri analeta mbwembwe za kikuda hapa. Halafu kesho kabla hujaenda mahakamani ukamwage ma*i aya umesikia we ku** la msen*e".


Sikua na la kujibu zaidi nilikua nalia na kuwaza sana. Asubuhi nikaambiwa nikamwage yale ma*i ndoo ya kuhifadhia ilikua imetoboka toboka hivyo yalikua yakinimwagikia. Sharti ilikua ni inatakiwa nijitwishe. Nilimwagikiwa na kinyesi kile kibichi kibichi kikiwa kinatiririka kuanzia kichwani kushuka chini. Nililia sana kiukweli niliwahi ishi maisha ya mitaani lakini hayakua ya mateso kama yale. Lakini zaidi nilikua naumia kwa sababu haikua kosa langu. Nilimwaga chooni kinyesi kile na kurudi. Nikaambiwa "jifute unahitajika mahakamani sasa hivi". Basi nilitii kisha tukapanda karandinga awoo tunaelekea mahakamani.


Tulifikishwa mahakamani na kuanza kusomewa mashitaka mmoja baada ya mwingine kila mtu na kesi yake na namna ambavyo aliwasilisha ushahidi. Pia utetezi wa mtu ulihusika. Nikiwa nimekaa mahakamani katika kugeukageuka nikamwona mke wa marehemu boss wangu akiwa ndani ya mahakama. Sikujua kafikaje lakini siku hizi usafiri ni mwingi kwa Mbeya-Dar. Nadhani alikuja kwa ndege swali ni je! nani alimpa taarifa za kukamatwa kwangu? Sikujali hilo kwani akili yangu yote ilikua imezama kufikiria hukumu yangu.

SOMA MBINU ZA KUPATA WAFADHIRI WA UJASILIAMALI

Japo nilikua nahukumiwa kwa makosa ambayo sikuyatenda. Nilikaa pale kwa mda mara kuna kikatatasi nikaletewa pale. Baada ya kukifungua na kukisoma nilishtuka sana. Kilikua kimetoka kwa mke wa boss nacho kilisema.

??"Yusuph najua utafungwa na kuniacha mimi na mwanangu wa tumboni peke yetu. Ulikuwa faraja pekee kwangu. Nasikita sana kwa kuwa mdogo wako Happy kafukuzwa shule. Sababu ni kuwa amegundulika ana mimba ya miezi saba....(iliendelea barua ile)???". Nilijikuta nadhindwa kuendelea kukisoma maana Happy tulipima na kukuta hana mimba. sasa kaipata wapi?


Nilikuwa nawaza juu ya ile karatasi. Nikajisemea moyoni je! ikiwa ile mimba ni ya kwangu mama akijua itakuwaje? Na mbona toka tulipoambiwa hospitali Happy hana mimba sikuwahi kukutana naye tena. Je! happy mimba kaipata wapi? Niligeuka kumwangalia mke wa boss nikamwona akibubujikwa na machozi. Hali ile ilinifanya na mimi nishikwe na uchungu mwingi moyoni mwangu na kujikuta namwaga chozi hadharani. Hakika niliumia sana.


Wakati nalia hakimu akagonga meza na kuita jina langu tayari kwa kusomewa hukumu. Nilipandishwa kizimbani. Nikawa na hasira sana machozi yalikua yakinitoka bila kikomo. Nilijiuliza hivi mimi nahukumiwa kwa kosa gani hasa? Na hii kesi yangu haina hata wakili. Anayenishitaki nilishaambiwa nashitakiwa na jamhuri. Hakika ilikua uchungu. Basi Hakimu akaanza kusoma hukumu yangu kama ifuatavyo...




.."Ndugu Yusuph Samson Mkanze unahukumiwa kwa makosa ambayo tayari yametajawa tangu jana.

Je!! una utetezi wowote?"

Kwa kuWa nilikua nimekata tamaa nikajikuta nakaa kimya.

Basi akasema "kwa mujibu wa sheria ya jamhuri ya nchi umekutwa na hatia hivyo unahukumiwa miaka 15 jela. Na viboko 12 siku ya leo unapoingia na 12 siku ya kutoka".

Basi maaskari wakaja wakanitoa kizimbani na kuanza safari ya kuelekea Jela. Niliambiwa napelekwa gereza la Keko. Basi vilio vilitawala kwa baadhi ya watu wanaonifahamu.


Wakati natoka mahakamani nikienda kupanda karandinga mke wa boss wangu ambae kwa wakati ule alikua kama mke wangu halali. Alianguka na kuzimia. Sikua hata na jinsi ya kumbembeleza. Wakati nimepanda karandinga kuna kitu nilikiona sikuamini macho yangu.

SOMA MBINU ZA KUPATA WAFADHIRI WA UJASILIAMALI

Nilihisi nimemwona baba yangu akiwa amesimama na mwanadada mmoja ambaye alikua amenigeuzia kisogo. Nikajiuliza kumbe baba yangu alikuwepo mahakamani ninapohukumiwa. Wakati nazidi kuwaangalia kwa sababu gari lilikua linasubiri wafungwa wengine. Nikapata nafasi ya kumwona yule aliyekua amegeukia mbele akigeuka Mungu wangu alikua ni dada yangu. Nikajiuliza ina mana dadayangu na baba yangu walishapatana? Mbona wamesimama wote pale? Nilihisi kuchanganyikiwa Kwa maswali.

Nilitamani nitoke ndani ya gari ili nikaonane na ndugu zangu yaani baba na dada yangu. Japo baba alionekana kunikana lakini dada yangu nilijua hawezi kunikana. Ila swali likaja inamaana kama alikua mahakamani si angekua ameniona? Nikaona huenda amenisahau maana siku ya uvamizi tulilishwa sumu ya kuvuruga ubongo.


Niliishia kuwatamani ndugu zangu nisiweze hata kuwaaga kwa kuwakumbatia. Wakati gari inawashwa niliona yule mama mke wa boss amezinduka na anatoka nje cha ajabu alisimama kama aliyeduwaa kisha akawa anatembea kwa kasi kuelekea alipo dada na baba yangu. Alipofika akaanza kuonekana akimshangaa sana baba yangu. Alionekana kana kwamba ni mtu asiyeamini kitu fulani. Ghafla nilimsikia mzee wangu akifoka kwa sauti kuu "we mama vipi umenifananisha....?" Gari yetu ikawa taratibu inaondoka hivyo kilichoendelea pale sikujua.


Maswali yakazidi kuongezeka ina maana Mke wa boss anamfahamu baba yangu? Je! kama anamfahamu inamaana sisi hatujuani? Mbona mzee alionekana kasimama na dada lakini yule mama hakuonekana kushughulika na dada inamaana watoto wake hakuwa anatufahamu? Na je! amemfahamia wapi baba yangu?


Hakika nilijiuliza sana lakini sikua na majibu, sikuwa na jibu hata moja. Pengine majibu yangu yangepatikana baada ya miaka 15 baada ya kutoka Keko. Niliumia sana uchingu ulitawala moyoni mwangu. Mwisho tukafika Gerezani. Nilipokelewa vibaya kwa fimbo 12 siyo kama zile za shule zile za jela ni fimbo haswa... Nilikabidhiwa sare zangu na kuingia ndani.


Huko ndani ilikua utata mtupu. Kuna watu wanajiita wababe wa jela. Wakanipokea kwa mbwembwe wakisema vua nguo zote usije ukawa umetujia na mabomu humu. Nilitii kwambinde wakawa wanasema inama, wakaniinamisha nikainuka wakaniinamisha Tena nikainuka wakaniinamisha nikainama kwambinde nikiwa mtupu, Kisha nikasikia haya kohoa. Nikatii. Mmoja akaja akawa anashika shika korodani zangu huku akizibinulia mara kulia mara kushoto. Hakika ulikua ni udhalilishaji wa hali ya juu sana. Ila ningefanya nini wakati ilikua ni mara yangu ya kwanza kuingia jela. Nilibaki naumia moyoni.


Baada ya kumaliza kunidhalilisha wakawa wanapiga makofi huku wakiimba kwa sauti.

"Mke wetu amekujaa!!

Mke wetu amekujaaa!!

mke wetu amekujaaa!!!"

Nikajiuliza ni yupi wanamwimbia hivyo? Majibu yakaja ya kuwa ni mimi. Hilo ilikua makosa makubwa sana kwangu. Nilipatwa na hasira na gadhabu kali sana. Nikakumbuka jinsi nilivyoingia jela. Nikakumbuka jinsi gani nahangaika kumpata baba na dada yangu. Nikajisemea marangapi nimejitoa na kujiruhusu kufa?.


Nikasema hapa naamsha mashetani kama ni kufa wacha nife. Niliinuka kwa hasira na kumfuata yule jamaa aliyekua anaongoza lile kundi.

Jemba alikua ameshiba na mnene kiasi na mwenye mwili wa kutisha. Nikamrukia na kumsukuma kwa nguvu zote hadi akaanguka chini. Nilimtia ngumi mfululizo huku machozi yakinitoka kwa hasira. Wakaja wapambe wake wakanishika niliitolewa pale huku nikilia nikajikunja na kuwasukuma kundi la watu kama sita hivi wakaanguka.

Wakati namfuata tena yule jamaa mbabe wa jela kama yeye alivyojiita. Kuna mtu mmoja nadhani ilikua ni miongoni mwa wapambe wake akanichoma na bisibisi sehemu ya paja ikazama yote.


Hakika ilikua ni maumivu lakini kwa ujasiri uliosababishwa na uchungu nikaichomoa huku chozi likitoka. Kitendo kile kiliwashitua wengi sana. Baada ya kuichomoa nikamfuata yule mbabe nikamchoma na ile bisbis sehemu ya mkono karbu na bega. Hali ile iliwashitua watu nikaona tayari wapambe wameanza kujivuta. Nilikua nalia sana kwa uchungu. Nikainuka na kuwaona wote wananikwepa nikageka na kumwona yule mbabe wa jela akiinuka. Nikataka nimfuate tena nikaona ananyoosha mikono ya kuomba msamaha. Nilikua nimevuja sana damu sehemu niliyochomwa na bisibisi. Nikachukua nguo zangu na kuvaa maana wakati wote nilikua napigana nikiwa uchi.

SOMA MBINU ZA KUPATA WAFADHIRI WA UJASILIAMALI

Nikaanza kutafuta sehemu ya kukaa. Jela ilikua imetulia kimyaa wote wakinishangaa mimi. Nadhani ilikua ni kwa sababu ya kumpiga mbabe wa jela hadi anaomba msamaha. Nikafika sehemu nikakaa kimya bila kumsemesha mtu yeyote huku nikiwa bado nalia kwa hasira na uchungu. Nilikaa pale kwa mda mrefu asiwepo hata mtu mmoja wa kunisemesha. Utulivu wa mle ndani ulitosha kabisa watu wote kusikia kilio changu. Walibaki kunishangaa tu. Mara yule mbabe akawa anaondoka na watu wake ndipo kelele zikaanza kusikika tena. Watu wakiimba

"Amekujaa mume wakooo!!!"

"Utangongwa mpk ukome" "Amekujaa mume wakooo!!!"

" Utangongwa mpk ukome"

"Amekujaaa mume wakooo!!"

"Utangongwa mpk ukome"x2

SOMA MBINU ZA KUPATA WAFADHIRI WA UJASILIAMALI

Muda wote mimi nilikua kimya sana nisieongea wala kufanya chochote. Yule jamaa akapotelea chumba kilichofuata. Mara pale nilipokaa akaja njemba mmoja mweusi wa ngozi alikua amejazia sana. Alikua amejaza kifua mithili ya mpiga mieleka wa siku nyingi. Alionekana si mtu wa mchezo hata kidogo. Mara akasema...

SOMA MBINU ZA KUPATA WAFADHIRI WA UJASILIAMALI

SOMA MBINU ZA KUPATA WAFADHIRI WA UJASILIAMALI

SOMA MBINU ZA KUPATA WAFADHIRI WA UJASILIAMALI

"Kijana hongera kwa kumfundisha adabu yule mjinga mjinga. Naamini sasa nimepata kampani. Akaniinua akanikumbatia".


Basi mazingira ya jela yakaanza kuzoeleka kihivyo huku mimi nikionekana ndie mfungwa pekee nisieongea na watu. Niliamua kuwa mpole mle gerezani ili nisipatwe na makubwa. Siku zilikwenda na miezi ikasonga hatimaye miaka kama miwili ikapita nikiwa jela. Hakuna hata mtu mmoja aliye jaribu hata kuja kuniona. Hatimaye siku moja ikatokeza neema nilikuja nikaitwa na askari nikaambiwa kuna wageni wangu.


Nilipotoka kwenda kuwaona alikua ni Happy na mama yake wote wakiwa na watoto. Waliponiona wote wakaanza kulia hasa mama ndo alikua analia sana. Nikajikuta na mimi machozi yananitoka. Basi baada ya muda tukatulia wote tukasalimiana na kuanza maongezi. Tuliongea mambo mengi sana. Kubwa likiwa la mama kuwa na mtoto hakutaka kulisema pale kuwa yule ni mwanangu kwa sababu bintiye happy alikuwepo pale tulipo.


Nilikua nawaangalia watoto wote wawili haaah hakika wote walikua ni wanangu. Mama akaomba kutoka kidogo ili akachukue vizawadi alivyoniletea ndipo akawa ameniachia upenyo wa kumwuliza Happy. Nilianza kwa kumwuliza

"imekuaje" akajibu "yule ni mwanangu na siku tulivyopima manesi walichanganya majina yale hayakua majibu yangu". Nikamwuliza tena "vipi mbona tulinunua dawa kwa ajili ya wewe kwenda "bleed" na ukanijukisha kuwa umeziona siku zako mimi sikuelewi unajua". Basi happy akasema "zile dawa sikunywa nilikudanganya tu! huyu ni mwanao".

Nikamwuliza " na vipi mama umemwambiaje Happy akajibu

"kuna jamaa nimembamkiza huyu mtoto yeye "nilidate" naye mwezi mmoja baadae. Hivyo kakubali na anamlea". Nikasema "kwahiyo unaishi wapi kwa sasa?" Happy akasema "naishi na huyo mtu maisha ya ndoa ila mimi ukitoka nataka tuoane" kwa kuwa nilikua nimeshachanganyikiwa nikamwambia hayo tuta...


Nilikatishwa na sauti ya mama akiwa anarudi akainiita" yuu mizigo yako hii". akamkabidhi afande mmoja. Kisha akanambia "kuna wakili tumeongea naye tunakata rufaa juu ya kesi yako. Nadhani utatoka siku si nyingi". Nikiwa nataka kuendelea kuuliza afande akasema "we kijana muda umekwisha". Nikatolewa pale na kukabidhiwa vitu nirudi gerezani. Nilipokea vitu vyangu na kuanza kuingia ndani wakati naingia nikakutana na wale wababe wa jela wakiwa wamejikusanya.


Mikononi walikua na bisibisi na wengine visu na viwembe. Nilisimama pale na kuwaangalia basi yule mbabe akatoa bangi iliyokuwa imetiwa kwenye mrija wa sigara Akaiwasha na kuanza kuivuta. Nikajiuliza sasa bangi imeingiaje mle gerezani?

Basi akanisogelea na kuniambia

"hebu nipe ayo mazaga we msen*e". Nikajua anataka zawadi kwa kuwa sikutaka mzozo na nilikua nimeshajizira na maisha ya jela. Nikampa kisha nikaondoka ile napiga hatua ya pili wakanizingira.


Akaanza yule mbabe ambaye walizoea kumwita jina la utani John Cena. "Oya we k**a si ndo umetuzingua siku zile afu ukajikuta mjanja wa mbeleee kumbe fala tuu" Nikamwangalia kisha nikamwambia bro sina ugomvi na wewe naomba nipishe. Akajibu "We unag*ngw* nini unabro hapa jela" Mabro umewaacha kwenu buselesele uko umu ndani we kenge tuu" Alimaliza yule jamaa kisha akaamuru vijana wake wanitie adabu.


Ooh!! Kwa kuwa walijua mimi ni mkorofi walinivamia kwa pamoja na kuanza kunichana na viwembe nilijitutumua lakini wapi! Nilichanwa sana na viwembe mwili ukawa unavuja sana damu. Ghafla akatokea yule jamaa alinifuta siku ya kwanza na kunipongeza. Alipambana nao kidogo na mimi nikapata upenyo baada ya kufanikiwa kupora kisu kimoja. kwa kuwa nilikua najua ya kuwa yule mbabe ndio amri yao nilimfuata na kwa kuwa nilikua na hasira nilimtia kisu tumboni halafu nikachomoa nikatia tena nikachomoa nikamchoma shingoni. Nilikua na hasira sana mara akaanguka chini gafla polisi wakaingia mle ndani.


Kwa kuwa mimi nilikua bado na hasira kuna polisi mmoja alinisogelea vibaya nikamchoma pia kisu cha tumbo. Wakati navuta kisu ili nitoe nikatoka na utumbo. Hali ile iliwafanya polisi wengne waongeze tahadhali. Wakanielekezea mitutu ya bunduki. Mwili wangu wote nilikua navuja damu kwa sababu ya viwembe nilivyochanwachanwa na wale wahuni. Nilikua nalia kwa hasira sikujali mitutu ya bunduki nikawa namfuata askari mmoja.


Mmmh Kuona vile wakaamua kunipiga risasi ya mguu Haaah mguu uliuma sana. Nilikaa chini nikisikilizia maumivu. Kisha polisi wakaja na kuanza kunipiga na vitako vya bunduki huku wakisema mimi jeuri. Nilipigwa sana bila kuangalia kuwa nilikuwa nimeumizwa vibaya sana.

Nao wakaongezea kipigo kikali Uso ulivimba sana wakaniburuta na kuniambia kuanzia sasa utakaa jela ya pekeyako. Nilipelekwa chumba fulani na kufungiwa humo.

Niliugulia maumivu makali sana mle ndani kwani mwili wote ulikua vidonda vidonda vidondaaa...

SOMA MBINU ZA KUPATA WAFADHIRI WA UJASILIAMALI

Lakini zaidi ilikua ni maumivu ya risasi ya mguu na pia kupigwa na mapolisi. Niliishi mle ndani bila huduma za msingi ikiwa ni kama kunikomoa. Chakula nililetewa mara moja kwa siku. Sikuwa na jinsi zaidi ya kuvumilia. Siku zilienda huku hali yangu ikiendelea vizuri kwa kiasi fulani.

SOMA MBINU ZA KUPATA WAFADHIRI WA UJASILIAMALI

Nilikaa mle ndani bila kuongea wala kuonana na watu. Vidonda viliniuma sana. Nilijutia sana kumuchoma kisu afande. Lakini kwa jemba lile lingne nilijisemea kuwa ilikua haki yake.

Niliendelea kuteseka mule bila msaada wowote hakika nilikoma. Jela ilikua ni mahali pachungu kwangu. Nilikumbuka starehe zile niikua napata kwa boss za kuliliwa na wanawake nikajilaumu sana. Kisha nikaapa kuwa lazima Jane nitamwua kwa mikono yangu miwili ili nirudi tena Jela.


Naikumbuka vizuri siku moja asubuhi na mapema. Kuna afande alikuja kwangu na kuniletea barua. Sikujua imetoka wapi. Baada ya kuifungua na kuangalia kwanza sikuamini ilikua barua imetoka kwa baba yangu. Na nilipoanza kuisoma tu iliamsha hisia za uchungu na gadhabu. Barua ilikua na maneno makali sana. Hakika yalikua hayavumiliki. Yalikua yanasomeka hivi...



TULIPOISHIA

Na nilipoanza kuisoma tuu

iliamsha hisia za uchungu na gadhabu. Barua ilikua na maneno makali sana. Hakika yalikua

hayavumiliki. Yalikua yanasomeka hivi...... ENDELEAA ??


"Hallow Yusuph, najua unajua mimi ni baba yako, pia najua unajiuliza nilitokaje kwenye mikono ya majambazi. Usilolijua ni usiku wa giza kiufupi mimi siyo baba yako. Ni kweli niliwahi ishi na wewe kama baba yako lakini mimi siyo baba yako ukitaka kumjua baba yako kamtoe mama yako kaburini umuulize maana mimi ndiye nilimwua mama yako na ndio maana mpaka sasa niko hai. Pole kwa kufungwa jela kwa makosa yasiyo yako. Baba yako angekua hai ungepata mtetezi ila polee naku...".


Nilishindwa kuendelea kuisoma ile barua nikajikuta namwaga machozi. Ina mana baba ndo alimwua mama yetu? Halafu anasema baba yangu angekua hai inamana baba yangu alikufa? sasa kama yeye siyo baba yangu baba yangu yuko wapi sasa? Nilijikuta naumia na kutamka kwa nguvu HAPANAAAAAA!!!!!! Ilikua sauti kubwa iliyoambatana na mwangwi. Nililia sana tena sana kwa kweli. Ndugu msomaji nilijihisi dunia inanitenga na kuniacha peke yangu. Nilijiuliza kosa langu ni nini kwa Mungu? Mbona maisha yangu yanakua ya mateso kila siku.


Nilishtuka polisi wakija na kusema huyu ndo anapiga kelele humu ndani. Basi nikiwa sijapona vidonda nikaanza kupigwa tena. Nilipigwa ambapo nakumbuka kuna afande mmoja akasema. Jamani huenda huyu mtu ana matitizo ya akili. Haiwezekani kila siku anafanya mpya. Wenzie wakasema huenda kweli tufanyaje sasa? Yule afande akasema tumpeleke hospitali akaangaliwe asije akaja kutuua wote akatumaliza bure mi nina mke atii. Alisikika afande akiwatania wenzie.

(Mwanadarubin wetu: oya bro hii ndo nafasi siwajua twazidiana tu kiwango cha ukichaa Sasa fanya kuzidiwa uchizi??)


Basi wakakubalina yakua nipelekwe hospitali. Nilitolewa huku nikiwa na maumivu. Nikapandishwa kwenye difenda 110 ya polisi. Wakashauriana na kusema hospitali ya muhimbili ndo ina kitengo cha magonjwa ya akili. Si kwamba hospital zingine ilikua huduma hiyo haipo ila walihitaji mtu wa uhakika maana shari langu walikua wanalijua. Basi tukatoka huku wakiwa wamenilaza chini na kusimama juu yangu. Sikulaumu wala kuwalaumu polisi ila nilimlaumu baba yangu aliyemwua mama na kunifunga jela mimi. Huenda baba asingemwua mama nisingeishi maisha yale. Nikamlaani sana baba.


Tulifika muhimbili nikapimwa na kuonekana akili yangu iko sawa....(mwanadarubini: Ooh huo ndo ujinga umeahindwa kuigiza?) Lakini daktari akashauri nilazwe ili nipatiwe matibabu ya mwili. Lakini wakati niko chumba cha daktari kuna daktari mmoja mwenye asili ya kihindi alikua ananiangalia sana na kuwasikiliza wale mapolisi maelezo yao. Sikutaka kumtilia maanani basi wakati natafutiwa chumba cha kulazwa. Ghafla kuna uvamizi ulitokea pale hospitalini. Kundi la watu wanne wenye unene wa mazoezi wakavamia pale na kuanza kurushiana risasi na wale polisi niliokuwa nao. Na mimi nikaona huo ndo upenyo wa kukimbia nilitoka mbio. Siku ile nadhani yule ambae huchagua washiriki wa mbio olympic angenichagua. Cha ajabu sasa wale watu wanne wakawa wananifukuzia mimi. Nikashangaa ila sikutaka kusimama. Nilikimbia hadi kufikia sehemu hivi kulikua na fance.

SOMA MBINU ZA KUPATA WAFADHIRI WA UJASILIAMALI

Nilipogeuka tu nikakamatwa na wale jamaa kisha nikakimbizwa kwenye gari moja nyeusi. Ilikua Alteza six silinder. Iliwashwa gari ikakimbia cha ajabu getini ilipita tu! Nikiwa mle ndani mara nikafungwa kitambaa cheusi usoni. Tukafika sehemu wakanishusha na kunipakia kwenye kitu nilichohisi ni helkopta. Baada ya mda nilishushwa na kuanza kupelekwa mahali. Nilifikishwa huko Nikawekwa kati kisha nikafunguliwa kitambaa usoni. Niliangaliwa hawakua wale niliotoka nao kule hospitalini. Nilijiuliza hapa ni wapi? Hawa wanataka nini kwangu? Nikaambiwa aya sasa njoo huku wakaniingiza chumba fulani na kunifungia humo. Sikua najitambua hata kidogo niko wapi.

SOMA MBINU ZA KUPATA WAFADHIRI WA UJASILIAMALI

Kuna muda walikuja wazungu wawili wakanichoma sindano na kuniambia nitulie ile ni tiba. Baadae nikaletewa chakula kizuri sana. Siku zikasonga na kwenda huku nikipata huduma kama mfalme. Cha kushangaza sasa ni kwamba wale watu hawakua wanaongea chochote. Hata pale nilipouliza maswali. Basi siku moja nikatolewa na kuingizwa chumba fulani huko nikaambiwa sasa unaanza kazi leo wenzio wako hapo chumba kifuatacho.


Niliingizwa mle ndani na kuambiwa kazi yangu ni kujaza unga flani hivi kwenye pakti. Sikuelewa ni nini lakini kwa kuwa niliamrishwa nikatii bila matatizo. Niliifanya ile kazi kwa siku kadhaa. Siku moja nikiwa nafanya ile kazi nikamwona mzee mmoja wa makamo kidogo. Kwa kua walinzi walikua hawapo nikamfuata na kuanza kumwuluza pale ni wapi? Mzee akajibu hata yeye hajui. Nikamwuliza na kile tunachojaza kila siku ni nini mzee akasema yale ni madawa ya kulevya. Akazidi kusema hapa tuko mahali hatari sana kwani kuna watu wanauawa kila siku. Akazidi kusema kama mimi niliingia humu nikiwa kijana sijawahi kutoka hadi umri huu. Kila ukijaribu kutoka huoni pakuanzia. Kila kona ni ukuta. Basi wakati tunazidi kuongea akaja mlinzi mmoja akampiga risasi yule mzee na kumwua palepale.Kisha akaniamuru mimi kuendelea na kazi. Niliogopa sana kisha yeye akaondoka zake.

INAENDELEA

Post a Comment

0 Comments