"Tausi kama unauthamini mwili wako na afya yako naomba nifate." aliongea manenop hayo na kutoka. Tausi alitishika na kunyanyuka haraka kumfata Mdoti ambaye alielekea nje ya mgahawa ule.
"Kaka Mdoti! kumbe nawe umekuja huku?" Aliuliza Tausi.
"Yote kwa sababu yako Tausi...sasa twenzetu kabla hatujakutwa hapa. namjua vizuri sana Ndangala na leo nitakwambia kila kitu."
Haraka waliongozana hadi kwenye bajaji. Mdoti alitekenya mafuta na chombo ikaishia eneo lile la Kinondoni pasipo Ndangala kufahamu lolote.
Walipotoka kina Ndangala walikuta patupu pale walipomuacha Tausi.
"Ngoja nikakutoe kabisa uende zako." Alisema Ndangala huku akiwa hana wasiwasi sana kwa kutomkuta Tausi pale alipomuacha akiamini huendaq ameelekea msalani kujisaidia.
Walitoka nje na kuingia kwenye gari ambapo alifungua sehemu moja alipohifadhi pesa za matumizi na kuhesabu noti 35 za elfu kumikumi na kumkabidhi Mc Jaba ambaye toka azaliwe hakuwahi kuzikama noti hizo kwa pamoja. Laki tatu na elfu hamsini.
"Poa kaka." Aliziswekaq kwenye mifuko ya kipensi chake cha jeans kisha kuchomoka garini Jaba huku akichanganya mwendo kana kwamba alikuwa anamkimbia mtu.
Ndangala Ndangala alimtazama Jaba na kucheka mwenyewe huku akiitazama ile pete na kujipongeza moyoni kwa kuichukua kwa pesa ndogo mno kana kwamba aliiokota tu.
"Hapa mjini ha ha haaa dogo laki tatu anajihisi kama kaibeba bank kuu mfukoni kwa alivyopagawa, jee ningempa milioni si angekimbia kabisa huku analia! wa uswazi wa uswazi tu. Mimi ndio Ndangala bwana ndio maana nawaweza naiva nao hawa." alijitapa mwenyewe na kushuka garini kurudi mgahawani ambapo sasa alistuka baada ya kukuta nafasi ziko wazi vilevile hayupo Tausi.
"Magreth! hebu njoo." alimwita mhudumu mmoja aliyepita jirani yake Ndangala.
"Eti huyu binti niliyeingia naye alikuwa amekaa hapa, ameelekea wapi?"
"Anhaa nilimuona akielekea nje muda fulani." Jibu la mhudumu yule lilimfanya Ndngala apige kofi mezani kwa hasira.
"Kweli sokwe ni sokwe tu hata umpambe vipi!" Aling'aka na kuondoka zake.
********
Dakika zilienda huku kina Dudukila wakizidi msubiria mc Jaba pasipo kutokea. Lilikatika lisaa; masaa; hatimaye kulianza kupambazuka kabisa.
"Oyaa! huu ukum** sasa hadi saa hizi?" aling'aka dogo Cholo baada ya kuchoka kusubiri.Watu mmoja baada ya mwengine walitoka kwenye club na mwishowe anga yote ikawa nyeupe huku watu wakipitapita kuanza pilikapilika za siku mpya. Wanafunzi walionekana wakienda shule, huku wengine wakienda maofisini na wengine wakizurura ovyo kama ilivyo kawaida ya jiji la Dar.
"Cholo, twenzetu huenda Jaba alirudishwa na ndinga magetoni." alikata shauri Dudukila na wakaondoka huku mioyoni wakiwa na hasira za kuchomeshwa usiku kucha nje kama walinzi wa Rambo club.
Tunu na Jerida nao walichomoka mida hiyo na kuchukua pikipiki kurudi kwao.
"Eeeh!" Sauti ya Jerida ilisikika pindi walipofika na kuingia ndani.
"Vipi tena?" Tunu alistuka na kuhoji.
"Shoga! angalia ujumbe wa bosi Ndangala"
"Hee!" Tunu naye alishangaa baada ya kuchukua simu ya Jerida na kusoma ujumbe uliokuwa umetumwa na Ndangala.
"Sasa huyu Tausi ana matatizo gani jamani? mbona hatujamkuta hapa kama kweli alimtoroka huko?"
"Mi ndio sitaki hata kumsikia tena! utajua mwenyewe utamfanyaje nduguyo ni heri hata asingekuja kama ulijua tabia zake za uzito wa kuelewa ama usingenambia tumuunganishe kwa Ndangala! tungempeka hata fisi sasa ndio angejua mbivu na mbichi." Aliwaka kwa hasira kiasi Tunu na kurudi chumbani kwake huku Jerida akiwa ameishiwa pozi na kujibwaga kitandani kwa hasira iliyochanganyika na uchovu wa usiku.
Dudukila na dogo Cholo nao walifika magetoni wakiwa hoi na hasira ziliwavaa zaidi walipokuta mlango umefungwa vilevile kama walivyouacha na hata walipochukua funguo ambayo walikuwa wanaificha pembezoni mwa vingazi vya mawe ulipo mlango wa kuingilia chooni, waliingia ndani na kukuta hakuna hata dalili kama Jaba alirudi na kutoka tena.
"Sasa imekuwaje?" Aliuliza kwa hasira zaidi Cholo.
"Sasa unaniwakia mimi we choko nini! mi mwenyewe nimedata na nina unenge wa haja!"
"Sasa tunafanyaje?"
Walitazamana wakiwa hawana jibu lakini mara mlango uligongwa. Walitoka haraka wakiamini ni mc Jaba lakini mbele yao walikutana na uso tofauti kabisa na kujikuta wananyong'onyea miili na uchovu wa akili kutawala vichwani mwao.
******
Saa nne za asubuhi ilitimu. Alikurupuka Tausi kwenye usingizi mzito wa ajabu ambao hakukumbuka jinsi ulivyomvaa. Alitazama kushoto kulia kwa pupa na hofu pale kitandani alipokaa. Maumivu ya kichwa aliyahisi kwa mbali. Akiwa bado anavuta kumbukumbu ni tukio gani lilitokea usiku wake ndipo alihamanika alipojigundua kumbe alikuwa mtupu kabisaaa! kama alivyokuja duniani siku ya kwanza.
"Mungu wanguuuuu!" Alijikuta kilio kinamponyoka na hasira kumvaa.
Mara mlango wa chumba ulifunguliwa na mbele yake alimuona Mdoti akiingia huku akiwa amevalia kitaulo, mkononi ana ndoo ya maji akionesha ametokea bafuni kuoga.
Macho ya Tausi yaliiva na kubadilika rangi ingawaje Mdoti aliingia huku akiwa mwenye tabasamu pana baada ya kumkuta Tausi akiwa yumacho ingawa uso ulitapakaa machozi
Saa nne za asubuhi ilitimu. Alikurupuka Tausi kwenye usingizi mzito wa ajabu ambao hakukumbuka jinsi ulivyomvaa. Alitazama kushoto kulia kwa pupa na hofu pale kitandani alipokaa. Maumivu ya kichwa aliyahisi kwa mbali. Akiwa bado anavuta kumbukumbu ni tukio gani lilitokea usiku wake ndipo alihamanika alipojigundua kumbe alikuwa mtupu kabisaaa! kama alivyokuja duniani siku ya kwanza.
"Mungu wanguuuuu!" Alijikuta kilio kinamponyoka na hasira kumvaa.
Mara mlango wa chumba ulifunguliwa na mbele yake alimuona Mdoti akiingia huku akiwa amevalia kitaulo, mkononi ana ndoo ya maji akionesha ametokea bafuni kuoga.
Macho ya Tausi yaliiva na kubadilika rangi ingawaje Mdoti aliingia huku akiwa mwenye tabasamu pana baada ya kumkuta Tausi akiwa yumacho ingawa uso ulitapakaa machozi.
"Vipi unajisikiaje my Tausi?" Aliuliza Mdoti swali lililomkera Tausi haswa. Kifua kilizidi kujaa pumzi za hasira. Ajabu Mdoti hakuonesha kujali zaidi ya kujifuta maji kwa lile taulo alilojifunga na kubaki na boksa tu. Hali ile ilizidi kumuaminisha Tausi kuwa Mdoti ameshamfanyia unyambisi pasipo hiyari yake. Alijipelekea mkono kwa bibi na kuhisi maumivu ya michubuko kwa ndani. Hii ilitosha kumpa picha jinsi gani Mdoti alijisugua ikuluni mwake kipindi akiwa usingizini. Usingizi ambao hakukumbuka ulivyompitia. Kila alivyovuta picha tukio la mwisho alikumbuka kuna sehemu walisimama na Mdoti kwaajili ya kula huku yeye alikataa kula zaidi alikunywa juice ya matunda tu.
"MDOTI! Umenifanya niniiii?" Aliuliza Tausi kwa hasira huku midomo ikimcheza cheza. Alitazama kushoto kulia kwenye kile chumba alikiona kipande cha nondo. Mawazo yake yalipaa ibilisi akamvaa. Akamtazama Mdoti aliyempa mgongo akivaa. Palepale Tausi alikiwahi kile kipisi cha nondo na kumvaa Mdoti kwa shari huku akimpiga nacho kwanguvu kichwani.
"Mdoti mnyamaaaaaa sanaaa" Aliwaka kwa hasira! Mdoti alitoa ukelele mmoja kabla hajadondoka chini huku mikono akiwa ameishika kichwani. Macho yalimtoka pima. Damu zilianza kumtoka puani huku taswira ya mwanamke mzuri aliyeuvaa moyo wa simba jike ilianza kufifia machoni mwake na kumrudishia kumbukumbu
ITAENDELEA

0 Comments