Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Responsive Advertisement

Chombezo: Singeli Kitaa sehemu ya tano (05)



Wakati huo upande wa nje Mc Jaba akiwa na dudukila pamoja na dogo Cholo walionekana kwa nje wakizoza na mabaunsa waliokuwa wanawazuia kuingia ndani kutokana na kutokuwa na kiingilio.

"Yaani mwanetu hadi sisi wasanii mnatulipisha?" aling'aka Jaba.

"Wasaniii mna usanii gani nyie hebu poteeni bwana." Baunsa aliwatilia ngumu huku akidharau muonekano wao. Wote walikuwa wamevaa vipensi vya jinsi. Ingawa ilikuwa usiku lakini fulana zao hazikumpa mtu shida kubaini kwamba ni chafu.

"Kwahiyo unatukazia mwanetu?"

"Oyaa poteeni "

Ilibidi wawe wapole na kusogea pembeni jiraani ya barabara. Nia yao kuzama ndani ili wakutane na bosi Ndangala ambaye walimshuhudia akiingia muda si mwingi. Kwenye kidosho cha Jaba kulikuwapo ile pete ya almasi na hiko ndicho kilichowafikisha hapo kwa lengo la kuonana na Ndangala waliyeamini angewapa pesa nyingi.

"Jaba mi nilikutonya mwanangu hawa mambwiga waduanzi tu.. ka vipi asubuhi tumuibukie kanjibai town." Dudukila alipendekeza.

"Dudukila unachukulia poa sana, yani uende kwenye maduka ya mjini na bomu hili? likikulipukia? hii ishu ya magumashi tuimalize kimagumashi huyu Ndangala mwenyewe mchizi tu! sasa huko kwa hao wazee si watawaita hata mamwela wakuulize ulipoitoa pete ya aina hii?"

wazo la Jaba liliungwa mkono na wote. Waliamua kutulia pale nje wamvizie bosi Ndangala pindi akitoka. Lakini kwa bahati mida hiyohiyo bajaji ya Mdoti ilitia timu mitaa ya Rambo.

"Ooooiiii Mdotii askari wangu niaje?" alinyanyuka Jaba kwa shangwe pindi alipomuona Mdoti. Walifahamiana vizuri sana na si Jaba tu bali hata kina dudukila walimjua Mdoti.

"Mbona mko nje wanyamwezi? naona nanyie leo mmekuja kuwabeba watoto." Aliongea Mdoti huku akiwapa tano kina Jaba.

"Aaaah! wapi mwanangu hao nyama za sambusa wametuletea mkazo kuzama ndani eti wanataka ngawila...?"

"Dooh! poleni sana unajua hawa wasasa hivi wageni kabisa heri wale wa mwanzo. Lakini sio mbaya mi nina buku mbili hapa kama vipi itawasevu wanangu sina mawe."

"Daah! kweli baharia wetu ila nini safi mwamba."

Walishukuru na ndipo Mdoti alipoelekea kujitoma ndani ya Rambo huku kichwani mwake akiwa na wazo moja tu! wazo lililochochewa na ujumbe wa simu alioupata. Ujumbe aliotumiwa na Tausi jioni hiyo ambao ulimchanganya.

''Kaka, kuna gari imetufata na hapa sina jinsi itabidi niende tu kwa usalama wa kazi ya kina dada...ila naomba ikifika saa sita usiku uje unifate kiwiziwizi nitoroke... heri nionekane nimepotea kuliko kuonekana nikifurahia maisha machoni mwao kumbe moyoni nateketea. Nisaide kunitoa hapa nitapoondoka sitorudi tena! siyapendi maisha haya na sina mtu wa kunisaidia zaidi yako kakangu Mungu atakulipa."

Huo ndio ulikuwa ujumbe wa Tausi alimtumia Mdoti muda mfupi kabla hawajaondoka na kina Tunu kuja pale Rambo baada ya bosi Ndangala kuagiza gari iwapeleke yote hiyo ili tu Tausi asikosekane. Ingawa Mdoti ndiye alikuwa anawapeleka kina Jerida pale na kuwarudisha kwa bajaji yake hata kuwa wateja wake wakubwa, lakini ujio wa Tausi ulianza kubadilisha mambo.

Akilini mwake naye Mdoti alishampenda sana Tausi. Na lengo la msaada wake ni kuhakikisha haangukii kwenye dimbwi la kina Jerida, bali alichofikiria ni kuhakikisha Tausi anaangukia kwenye dimbwi la mahaba yake.

Alilipia mlangoni sasa kuingia club, lakini kabla hajazama ndani ndipo mbele yake uso kwa uso waligonganisha macho na Tausi... Tena Tausi akiwa kashikwa mkono na bosi Ndangala Ndangala na nyuma yao kulikuwa na vipande vya majibaba mawili yaliyokuwa yanachunga usalama.

"Hapana! siwezi kumuacha Tausi aanguke mikononi mwa huyu mshenzi hivi hivwalioangukia kwake wametosha! kwa huyu NO!"

Alisema ndani ya nafsi yake Mdoti.



Alilipia mlangoni sasa kuingia club, lakini kabla hajazama ndani ndipo mbele yake uso kwa uso waligonganisha macho na Tausi... Tena Tausi akiwa kashikwa mkono na bosi Ndangala Ndangala na nyuma yao kulikuwa na vipande vya majibaba mawili yaliyokuwa yanachunga usalama.

"Hapana! siwezi kumuacha Tausi aanguke mikononi mwa huyu mshenzi hivi hivwalioangukia kwake wametosha! kwa huyu NO!"

Alisema ndani ya nafsi yake Mdoti.


Lakini mbali na kupania kote Mdoti alijikuta anashindwa kufanya kitu hadi bosi Ndangala akampita pale mlangoni na kuishia kutazamana baina yake na Tausi. Alijikuta anashindwa hata kuingia ndani ya club yenyewe. Tausi naye alitamani amwambie kitu Mdoti lakini aliishia kumtazama tu kwa muda huo.

"Ooooh bosi kubwa kakaaa...muheshimiwa Ndangala bosiii naomba nisiklize kidogo mdogo wako..." sauti ya Jaba ilisikika huku akiwa amemfata Ndangala aliyekuwa anafungua mlango wa gari yake akiwa sambamba na Tausi. Baunsa mmoja alimzuia Jaba alsilete ghasia kwa bosi wao lakini mara baada ya Ndangala kuingia garini na Tausi, aliwaambia wale mabaunsa wake wa pale club wamuache huyo dogo aseme shida yake.

"Kaka! nina mzigo naamini utakufaa sana."

"Mzigo gani?"

"Ni mzigo mdogo ila ghali sana kwenye ulimwengu. Ni vyema kama tungetulia sehemu nikuoneshe kaka amini nisemacho." aliongea kwa msisitizo Jaba na ndipo kidogo Ndangala alianza kushawishika.

Tabia yake Ndangala ilikuwa kununua vitu vya thamani kwa bei chee kutoka kwa watoto wa uswahilini ambao mara nyiongi vitu hivyo walivipata kwa njia ya wizi.

"Unaweza kunionesha kwanza?" Aliuliza Ndangala na ndipo Jaba alipoichomoa ile pete kutoka kwenye kidosho na kumuonesha Ndngala pasipo kumkabidhi.

Moyo wa Ndangala ulilipuka baada ya kuiona ile pete.

Ingia kwenye gari" alimuamuru Jaba, Jaba nae aliingia haraka huku akiwapa ishara ya utulivu washkaji zake Dudukila na Cholo waliokuwa wamesimama kwa pembeni wakiusoma mchezo.

"Haa! sasa ndio wanaenda wapi tena mbona Jaba anatuacha!?" aliuliza kwa mshangao dogo Cholo.

"Tulia Cholo wanaenda kumalizana chemba si unajua issue yenyewe ya nnya..so haitaki gozi wala ghasia la shazi nyomi. Wee tumsubiri hapa Jaba ayarudi na mafuta tu kesho tutaamka tofauti boy." Alijibu Dudukila kumtoa hofu Cholo ambae ndiye alikuwa mfanya tukio.

Mdoti alirudi kwenye bajaji yake huku jicho likiwa kwenye Prado ya Ndangala.

Ndangala aliagana na mabaunsa wake na kugeuza gari huku ndani yake siti za nyuma akiwa amekaa mc Jaba kimoyo cha shauku kikimpiga akiamini muda si mrefu atakuwa na pesa chafu baada ya biashara ile na Ndangala. Tausi akiwa upande wa mbele siti ya kushoto alimfikiria naye Mdoti akiamini kweli ni kijana pekjeee mstaarabu mwenye moyo wa upendo na huruma kwake hata kumfatilia kwa nia ya kumpa msaada ihali si mtu aliyemfahamu kitambo.

Gari ya Ndangala ilipoondoka tu, bajaji ya Mdoti nayo ikafatia na kuifuata nyuma nyuma huku nia ya Mdoti ikiwa palepale kuhakikisha Ndangala hamchojoi Tausi.


**********


Muda mfupi Ndangala baada ya kuondoka msanii Ronki akiwa na wapambe wake nao walitokaeneo la v.i.p baada ya kumalizana na wahusika waliofanikisha show kisha mdogomdogo walichomoka na kuingia kwenye taxi waliyokodi na kuelekea walipokuwa wanaishi huku wakiifurahia show ya siku hiyo ambayo hawakutaraji mwanzo kuwa ama iivyokuwa.

"Hivi Jose ulirecord video pale ukumbini leo?" Ronki alimuuliza mwenzake ambaye alikuwa na kamera.

"Aaah! niache tena?"

"Kwahiyo yule binti aliyecheza nami huko ulimchukua vizuri nae?"

"Yap, tukifika mjengoni utaiangalia fleshi mwana."

"Hamna noma maana mh! kile kifaa nacho sio powa sijui kimetokea wapi?"

"Hahaha Ronki bwana..na Bernadeta je?"

"Haa! yule mambo mengi pia hakifikii kile kifaa Jose sio poa mi nimekishuhudia kwenye ziro point wee acha tu!"

"Lakini kumbuka Ronki yupo nkazini yule asije kukuua kipindi bado watanzania wanakuhitaji."

"Hamna Jose kama nikimuelewesha ataelewa mi najua shida ndio zinawafanya wapagawe na kuanika nyeti zao lakini kama utamuweka ndani na kumuhudumia vizuri mtoto anatulia yule. Tena anaonesha mgeni kabisa pale si unaona hataalivyovaa?"

"Mmmh!" aliishiua kuguna tu Jose.

Ukweli tayari Ronki naye alipagawa na Tausi. Kwa uzuri wa Tausi naamini hata wewe msomaji ungekutana naye lazima ungepagawa tu na kuhitaji walau umuonje.

Alikuwa kifaa tena kifaa haswa asiyejitambua kama yeye ni mgodi unaotembea.


|||MKWELE PARK|||


Katika bar ya msanii maarufu wa vichekesho hususani katika kipindi cha mizengwe, aliyeitwa Mkwele, usiku huo napo kulikuwa na bonge moja la show lilikuwa linaendelea.

Show ya kucheza ambapo alikuwepo kijana mmoja aliyekuwa na kipaji cha ajabu cha kucheza hususani mziki wa uswahilini.

Kiingilio hapo yalikuwa macho pekee pindi ukinunua kinywaji ama chakula basi unafaidi show ama ukikosa hela ya kinywaji unaweza kusimama hata barabarani. Na ndivyo ilivyokuwa haqkika kijana yule aliwavuta wengi kwa kucheza kwake.

"Haa! huyu Kisingeli nyoko mmh! ona anavyocheza na kujibidua khaaa!"

Alisikika jamaa mmoja aliyekuwa kasimama barabarani na wenzake kipindi show ikiwa inaendelea. Show ya kijana huyo aliyeitwa Kisingeli. Hakika Kisingeli alicheza na alikuwa na 'style' za ajabu hata wanawake waliopinda kwenye kigodoro hawakuwa nazo.

Watu walimshangilia na kumsifia.

"Kisingelii..kisingeliii..kisingeliiiiii" Mc alichombeza kwenye kipaza mara show ilipoisha huku watu wakimtunza.

Baada ya kutoka kwenye show Kisingeli akiwa na mshkaji wake mmoja mara kuna mtu aliwaita. Waligeuka na kuelekea sauti ilipotokea ilikuwa kwenye bajaji ambayo nyuma yake alionekana mtu aliyewaita naye hakuwa mwengine bali ni Kimata.

"Haa! kaka mkubwa nambie!"

"Shwali mdogo wangu naona eeeh! sio poa unakamua ileile he he.." alichombeza Kimata huku akionesha uso wa tabasamu. Tabia yake Kimata alikuwa mcheshi na aliiva na wahuni wote si Tandale tu bali hata Mburahati, Mbagala na sehemu nyenginezo. Na hayo yalichochewa kwa sababu ya shughuli zake za mziki wa kigodoro.

"Nambie kaka Kimata kuna jipya nini?" aliuliza Kisingeli.

"Yah! jipya lipo mdogo wangu. Ni kwamba nimeona bure niwekeze pesa kidogo nilizokuwa nazo kwaajili ya manufaa yetu watu wenye vipaji huku mitaani. Nimeukodi ukumbi ule wa ccm Tandale kwa mkataba wa miaka sita."

"Duuh! enheee! kwa hiyo."

"Sasa kuanzia kesho nishaongea na mafundi wanaanza kuukarabati mule ndani kupaka rangi nyengine tofauti na zile za kichama chao na tutaubadilisha kabisa mtu hatoweza kuukumbuka. Tutajenga bar ya ndani kwa ndani pia jukwaa tutalitengeneza vizuri sana na tutaadnaa show zetu kwa kiingilio maalum. Kila mwisho wa wiki."

Aliongea Kimata na muida wote Kisingeli alisimama akimsikiliza kwa umakini.

"Enhee safi kaka...kwa hiyo show zinakuwaje?"

"Show hatutawachukua wasanii wowote wa bongofleva bali lengo ni kuburudika na mziki wetu halisia wa radha na kiduku wanaoimba kina Jaba. Pia kutakuwa na show za mchiriku, tushaongea na Jagwa wamekubali watakuwepo na bila kusahau show za kucheza ambapo mpaka sasa tushaongea na kina Mandondo wamekubali wale mabinti washawasha wamekubali pia na nikimalizana na wewe ukikubali kesho naenda kukutana na Kanga moko ili baada ya wiki hii ya matengenezo basi wiki ijayo show zianze na tutakuwa tunalipana asubuhi kulingana na kile tulichokipata."

"Daah! kaka Kimata mimi nimekuelewa vizuri na kuhusu hilo ondoa shaka kabisa. Nitakuwepo hapo! Kwa hiyo ukumbi utakuwa unaitwa vilevile ccm au baada ya mabadiliko na jina mtalibadilisha?"

"Hee! tulijadili kuhusu hilo, ukumbi tutauita Manyara Park."

"Safi kaka basi powa!"

"Haina tabu wadogo zangu tufanyeni harakati sana. Hii bajaji itawapeleka. Mwana wa Joo wapeleke."

Alishuka Kimata na kina Kisingeli walipanda bajaji ile iliyoendeesha na kijana aliyeitwa Mwana wa Joo na kutimua eneo lile huku Kimata akizidi kufarijika moyoni mwake kwa kuona vijana wengi anaowashawishi kwenye mpango wake wakikubali bila hiyana wala kinyongo.

"Daah! sasa hapa bado mc Jaba na wenzake." aliwaza huku akiondoka mdogo mdogo kuelekea kwake Kimata ambae sasa alishajivisha upromota kama alivyoshawishiwa na nduguye, tayari kuanzisha harakjati za mziki wa uswahilini ndani ya ukumbi huo wa ccm uliokodiwa na kubatizwa jina la MANYARA PARK.


=> Je, kipi kitatokea kwenye harakati hizo za Kimata kuunyanyua mziki wa uswahilini at?

=> Vipi kuhusu Tausi? Je, Mdoti atafanikiwa lengo lake la kumtoa mikononi mwa Ndangala?




"Daah! kaka Kimata mimi nimekuelewa vizuri na kuhusu hilo ondoa shaka kabisa. Nitakuwepo hapo! Kwa hiyo ukumbi utakuwa unaitwa vilevile ccm au baada ya mabadiliko na jina mtalibadilisha?"

"Hee! tulijadili kuhusu hilo, ukumbi tutauita Manyara Park."

"Safi kaka basi powa!"

"Haina tabu wadogo zangu tufanyeni harakati sana. Hii bajaji itawapeleka. Mwana wa Joo wapeleke."

Alishuka Kimata na kina Kisingeli walipanda bajaji ile iliyoendeesha na kijana aliyeitwa Mwana wa Joo na kutimua eneo lile huku Kimata akizidi kufarijika moyoni mwake kwa kuona vijana wengi anaowashawishi kwenye mpango wake wakikubali bila hiyana wala kinyongo.

"Daah! sasa hapa bado mc Jaba na wenzake." aliwaza huku akiondoka mdogo mdogo kuelekea kwake Kimata ambae sasa alishajivisha upromota kama alivyoshawishiwa na nduguye, tayari kuanzisha harakjati za mziki wa uswahilini ndani ya ukumbi huo wa ccm uliokodiwa na kubatizwa jina la MANYARA PARK.


********


Ndangala alikanyaga mafuta na kuchochea mwendo ambapo safari ilikomea mbele ya mgahawa mmoja mkubwa uliokuwa unafanya kazi masaa 24 maeneo ya Kinondoni ambapo pia ndipo alipokuwa anaishi bosi Ndangala.

Mdoti nae alikuwa nyuma akiwafatilia kwa makini muda wote. Aliwashuhudia wakishuka Ndangala, Tausi sambamba na Jaba. Aliegesha bajaji yake pembeni kidogo na pale ilipoegeshwa gari ya Ndangala kisha naye akazama mgahawani.


"Tausi agiza chochote utachojisikia kula muda huu." Ndangala alimpa nafasi Tausi pindi walipochukua nafasi ya klukaa kisha alimpa ishara Jaba amfate.

Walielekea 'chemba' kidogo upande wa ndani ya mgahawa ule ambapo kulikuwa na utulivu zaidi. Ndangala alionesha ni mwenyeji sana pale pia wafanyakazi wote walimfahamu wala hawakuwa na shaka naye hata walipomuona ameongozana na kijana ambaye machoni tu alionesha sio namba nzuri kabisa. 'dread' chafu kichwani hata nguo alizovaa zilikuwa chafu.

"Enhee hebu kaa hapa tuzungumze hiyo biashara." Ndangala alimwambia Jaba ambaye alikaa pasipo hofu yoyote ingawa ilikuwa mara yake ya kwanza kufika eneo lile.

"Kaka! nina kitu cha almasi hiki hapa." Alisema Jaba huku akiitoa ile pete.

Ndangala hakuamini hata alipoichukua na kuikagua. Aligundua kweli ile pete ina kito cha almasi.

"Enheeheee! mbona hii sio almasi yenyewe kama unavyosema! hii ni 'crystal' ang'avu tu! kwa hiyo ulikuwa unataka shilingi ngapi?" Alicheka huku akionesha kuidharau ile pete kinagaubaga Ndangala na kumrudishia Jaba.

Kwa kuwa Jaba naye hakuwa mtaalamu wa madini alijikuta anaanza kuregea moyoni baada ya kuhisi huenda kweli ile ikawa sio almasi kama alivyowehuka na kina Dudukila punde tu walipoiona mara ya kwanza mikononi mwa dogo Cholo.

"Daah! Bosi Ndangala mbona kitu chenyewe hiki?" aliwekea mkazo laini Jaba ingawa alishaanza kulegezwa moyoni mwake.

"Nimemuacha shemejiyo mwenyewe pale kwaajili ya biashara yako hii lakini biashara yenyewe naona inakuwa ya ajabu 'coz' unanilazimisha kukubali kitu ambacho nishajua sicho. Hii ni 'crystakl' kama nilivyokwambia na sio kwamba nina shida nayo kivileee...ila nataka kukuunga mkono katika harakati zako kijana."

Maneno haya yalimuua kabisa Jaba na kuamua ashushe mzuka kuzungumza na Ndanga ukibiashara zaid.

"Kaka mkubwa basi pawa nipe hata laki tatu." alitamka kiwango hiko Jaba akiona kaongeqa pesa kubwa sana kulingala na pete yenyewe.

"Anhaa! basi sawa nitakupa na elfu hamsini ya taxi. Lete hiyo pete." Aliongea Ndangala huku akitoa simu yake.

"Nikurushie kwa namba ya simu?" aliuliza pasipo hata kusumbua hali iliyomshangaza Jaba na kutamani angeropoka pesa nyingi zaidi ya zile.

"Hapana sina simu nipe tu mkononi."

"Okey sawa basi tuelekee kule kwenye gari."

Walinyanyuka kutoka huku moyo wa Jaba ukienda mbio kwa kujina amefanya ujinga kutamka hela ile.

"Au almasi kweli? Ndangala kanizidi ujanja?!"

Aliwaza pasi kupata jibu.


Kumbe kipindi Ndangala na Jaba wakiingia upande wa pili kuzungumza biashara wakimuacha Tausi mwenyewe pale, Mdoti alishuhudia mchezo mzima.

Alisogea haraka hadi alipokaa Tausi.


INAENDELEA

Post a Comment

0 Comments