Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Responsive Advertisement

Simulizi: Mam'dogo Lisa sahemu ya saba (07)

 


... Baba wewe si ulikwenda mazoezini?.." lilikuwa ni swali la kwanza la Dennis mara tu baada ya kumsogelea baba yake.

:.. ndio si ndo nimetoka kwenye mazoezi yenyewe..." alijibu Mzee Bisu huku akiendelea kumuangalia mwanae machoni kama aliyekuwa anasubiria swali lifuatalo, na kweli lilikuwepo.

💥bofya hapa soma jinsi ya kutengeneza batiki

"... sasa umepita wapi, mbona mimi muda wote nilikuwa hapa sebuleni..." lilikuwa swali la pili la Dennis na alionekana mwenye mashaka sana usoni mwake kwani ni kweli muda wote alikuwepo sebuleni na alipotoka hawenda mbali zaidi ya kusimama nje ya mlango tu.

Mzee Bisu naye alianza kupata wasiwasi akihisi kuwa mwanaye atakuwa kagundua kuwa alitokea chumbani kwa Hasina, lakini akajipa moyo baada ya kujishauri kuwa laiti mwanaye huyo angegundua kuwa alitoka chumbani asingemuuliza maswali yale bali angemuuliza anatoka kufanya nini chumbani kwa Hasina, hivyo akajipa ujasiri na kujibu kwa kujiamini kidogo.

"... sasa wewe ulitaka nipite wapi?.."

"... nauliza hivyo kwa sababu mimi niko hapa muda mrefu..." aliendelea kuongea Dennis,

"... hebu nitolee maswali yako ya kipuuzi,.. mama yako yuko wapi sitaki kuchelewa chelewa tena leo..." aliamua kujifanya mkali ili Dennis asiendelee kumuhoji maswali, maana alishagundua kuwa mwanae huyo aliamua kudadisi ili kujua alikotokea, na kweli, Dennis alikuwa na mashaka lakini hakutambuwa ni wapi alikotokea baba yake, mara mlango wa chumba cha Hasina ukafunguliwa na Hasina akatoka na kuelekea jikoni, Dennis alimuangalia Hasina kisha akamgeukia tena baba yake, akilini mwake alikuwa akijiuliza kama inawezekana kuwa baba yake alitokea chumbani kwa Hasina kweli au?, lakini wazo hilo akalitupilia mbali.

"... we Dennis, mi si nimekuuliza mama yako yuko wapi?.." alikurupushwa kutoka katika lindi la mawazo kwa swali hilo la mzee Bisu.

"... mama yuko chumbani kwake..." alijibu haraka haraka kisha naye akanyoosha na kuingia chumbani kwake.

Mzee Bisu pia aliongoza moja kwa moja chumbani kwake huku moyoni akijisemea "... nimeponea kwenye tundu la sindano... leo kama ningegundulika na mke wangu nilikuwa nimekwisha..." kule jikoni pia Hasina alihema kwa nguvu baada ya kuona maswali ya baba na mwana yamekwisha, maana alipokuwa kule chumbani alikuwa akiyasikia maswali waliyokuwa wakiulizana baba na mwana, na alikuwa tayari na wasiwasi akidhani kuwa Dennis atakuwa kagundua kuwa baba yake katokea chumbani kwake.

Mzee Bisu alinogewa kweli na penzi la Hasina mtoto wa kitanga ambaye ni mfanyakazi wake wa ndani, alishaonja asali akaamua kujenga mzinga kabisa.

💥bofya hapa soma jinsi ya kutengeneza batiki

************************


Hasina alianza kuonekana msicha wa ukweli baada ya kuanza kupendeza kwa nguo alizonunuliwa na Mzee Bisu, alionekana sister duh, ukilinganisha na umbo lake zuri basi alipendeza kwelikweli, jambo ambalo lilizidisha tamaa kwa mzee Bisu,.. lakini pia chembe chembe za tamaa zilianza kutembea mwilini kwa Dennis naye akaanza kupiga mahesabu ya kumnasa Hasina ili aweze kula naye utamu, lakini kwa Bi Pauline yeye alikuwa na maswali lukuki kulingana na mavazi ya Hasina, yamepatikana wapi? na hata kaka kanunua yeye, hela amezipata wapi? maana nguo zenyewe zilionekana ni za bei kubwa ukilinganisha na mshahara wake, hivyo akatamani sana kujua wapi alikopata nguo hizo, hata hivyo akaamua kukaa kimya lakini akilini mwake alishahisi labda Hasina atakuwa na mwanaume ambaye ndo anayempatia pesa za kununulia hizo nguo, akapanga siku amuulize na kama ni kweli ana mwanaume, amrudishe kwao mapema ili asije akaleta mzigo wa mimba pale nyumbani kwake. Alimchukulia Hasina kama motto mdogo kulingana na anavyoelewa yeye, lakini hakujuwa kuwa Hasina alikuwa mdogo wa umri na tu na sio uelewa, Hasina alikuwa mtaalam sana wa mambo ya mahaba tofauti na Bi. Pauline alivyoelewa, hivyo kwake kupata ujauzito ni ndoto.


ilikuwa ni jioni ya saa 10, Dennis alitoka kwenye mizunguuko yake na kurudi nyumbani, alipoingia ndani alikuta sebule ikiwa wazi yaani hakuna mtu, alisimama katikati ya sebule akaangalia huku na kule lakini hakuona mtu, akaongoza moja kwa moja chumbani kwake ambako hakukaa sana akatoka na kurudi kukaa sebuleni na kuwasha tv, Mara mlango wa chumba cha Hasina ukafunguka na Hasina akatokea akiwa katika vazi la kanga moja na huku mkononi akiwa kashikilia sabuni kwa lengo la kwenda bafuni kuoga, mwili wake ulionekana kulowa jasho, alipotokeza sebuleni tu alikutana macho kwa macho na Dennis, alishituka sana kumuona Dennis pale sebuleni hadi Dennis akagundua mshituko wake, hakumchelewesha akamtandika swali.

"... we vipi, mbona umeshituka kuniona?.."

Hasina hakujibu badala yake alianza kurudi nyuma kwa lengo la kurudi chumbani kwake, Dennis akaendelea kumuangalia kwa makini na akagundua kuwa kulikuwa na kitu kama uoga kwenye uso wake.

"... we Hasina, si nimekuuliza?.. mbona umeshituka na mbona uko hivyo?.. aliendelea kuhoji maswali na huku akiwa kamkazia macho.

"... hamna kitu ka... kaka Dennis..." alijibu Hasina huku akiwa tayari kasimama katikati ya mlango

"... sasa mbona umeshituka..."

"... hamna... si... si nilitaka kwenda kuoga..."

"...sasa kuna tatizo gani..."

"... hamna tatizo, lakini si... si nilijua hakuna mtu hapa sebuleni ndo maana nikashituka..." alijitahidi kunyoosha maelezo na huku akiwa tayari kakishika kitasa cha mlango

"... na mbona unatoka jasho hivyo kwani ulikuwa unafanya nini?.."

"... nilikuwa nimelala tu..."

"... sasa mbona umerudi nyuma wakati ulikuwa unaenda kuoga?.."

"... nachukua kanga nyingine..."

Dennis aliangalia huku na kule kisha akamuuliza

"... nani mwingine yuko hapa nyumbani?.."

"... niko mwenyewe... mama toka alivyoondoka ile asubuhi hajarudi mpaka saa hizi..." alijibu Hasina, jibu hilo ni kama lilimfurahisha kidogo Dennis akaamua kumuita

"... hebu njoo kwanza..."

"... ngoja nivae kanga nyingine..."

"...njoo hivyo hivyo..." aliongea Dennis, kuna kitu kilikuwa kinatembea kichwani kwa Dennis au labda niseme kuna kitu ambacho Dennis alishaanza kukitaka toka kwa Hasina.

"... ngoja nivae nguo kaka Dennis..."

Dennis akainuka na akawa kama anamfuta

".. au ngoja nije tuongee kidogo chumbani kwako..."

Hasina alikurupuka pale mlangoni na kumkimbilia Dennis kisha akamzuia

"... haya basi nimekuja tuongee hapa hapa..."

Dennis akapatwa na mashaka, kidogo na akawa kama anajiuliza maswali mwenyewe..." huyu mbona nimezungumzia Habari za kuingia chumbani kwake tu amekurupuka wakati alikuwa hataki kunisogelea eti kwa vile kavaa kanga moja... au kuna kitu anaficha huko chumani nini?.."




💥bofya hapa soma jinsi ya kutengeneza batiki

... Mawazo hayo yalipelekea Dennis kutamani kuingia chumbani kwa Hasina kuhakikisha ni kitu gani ambacho hakutaka kionekane huko chumbani kwake, lakini hakufanikiwa kuingia kwani Hasina alikuwa tayari kasimama mbele yake kwa mtindo wa kama kumzuia asipite, Hata hivyo Dennis hakutaka tena kuongelea kilicho sababisha amuite Hasina, badala yake alipatwa na shauku ya kutaka kujua ni nini ambacho Hasina alikuwa akikificha chumbani kwake.

"... kwani huko chumbani kuna nini we Hasina..." alihoji Dennis akiwa kasimama sambamba na Hasina.

Hasina alijua amekwisha maana Dennis alionesha kweli kuwa na shauku ya kutaka kujua nini kipo chumbani kwake, na yeye hakutaka Dennis aingie au afahamu ni nini kilikuwa chumbani kwake, akaanza kuumiza kichwa kutafuta jinsi ya kumzuia Dennis asiingie katika chumba hicho.

"... kwani kaka Dennis we si uliniita, na nilitaka nikavae nguo vizuri wewe ukaniambia nije hivyohivyo..." alionge Hasina kwa kujiamini.

"... lakini mbona nimeongelea habari za kuingia chumbani kwako ukakurupuka, kwani umeficha nini?.."

akili ya Hasina ilikuwa inafanya kazi kwa haraka na alikuwa akicheza na akili ya Dennis.

"... kaka Dennis sikiliza... mimi nimekuambia kuwa nilikuwa nimelala na ndio maana nimetoka jasho hivi, na hapa nilikuwa nakwenda kuoga... isitoshe kaka Dennis, mimi ni mtoto wa kike na chumba cha mtoto wa kike siku zote yeye ndo anajua ni vipi anaviweka vitu vyake, Kukuzuia kwangu mimi nina maana kuwa kuna vitu vyangu ambavyo nimeviweka vibaya na sio vizuri wewe kuviona ndio maana sipendi uingie chumbani kwangu... kidogo kama maelezo ya Hasina yalianza kumuingia Dennis maana alianza kulainika na kupunguza ukali wa maswali.

"... kwani ni vitu gani ambavyo sitakiwi kuviona?..

"... kaka Dennis... nafikiri unafahamu kuwa sisi wanawake na nyie wanaume tuko tofauti... na sisi wanawake kila mwezi tuna kuwa na..."

"... ahha basi sitaki kusikia habari hizo..." alimkatisha Dennis baada ya kugundua ni nini alitaka kuongea Hasina, akaamua kubadilisha mada, pia alionekana moja kwa moja kukata hata ile taamaa aliyokuwa nayo na iliyosababisha amuite Hasina pale, aliamini kuwa msichana huyo alikuwa katika siku zake kwani kauli yake ilimaanisha hivyo, hivyo hakutaka hata kugusia habari hiyo tena kwani isingewezekana kutokana na Hasina kuwa katika siku zake.

"... haya basi niambie ulichoniitia..." alijifanya kuhoji Hasina baada ya kugundua kuwa tayari alishamaliza mchezo.

"... ah... basi ntaongea na wewe siku nyingine, we nenda kaoge..." aliongea Dennis huku akinyanyuka na kuelekea chumbani kwake, kitendo hicho kilimfurahisha sana Hasina kwani alijua kuwa tayari ameuvuka mtihani uliokuwa mbele yake. Hakuondoka pale sebuleni mpaka alipohakikisha Dennis amezama chumbani kwake na kufunga mlango na ndipo naye akatoka haraka na kurudi chumbani kwake kulitoa tatizo lililokuwa limemkabili. Ni tatizo gani?..

***************

Hasubuhi ya siku hiyo kabla ya mambo hayo ya Hasina na Dennis kutokea, Mzee Bisu aliamka mapema kama kawaida yake kwa ajili ya kufanya mazoezi, lakini siku hiyo pia alikuwa hana lengo hasa la kufanya mazoezi, alitamani sana kuingia tena chumbani kwa Hasina kupata ile Raha aliyoipata jana yake, alipotoka tu sebuleni akiwa na lengo la kufanya mchezo ule ule kama alioufanya jana yake, akakutana na mwanaye Dennis akiwa naye ndo anaingia pale Sebuleni kwa ajili ya kuaanza kufutilia habari mbalimbali katika televisheni, swala hilo lilimchukiza sana kwani alijuwa kuwa itakuwa vigumu kuigia chumbani kwa Hasina wakati Dennis akiwa pale sebuleni, akatamani kumtimua lakini akajiuliza mwenyewe kuwa akimtimuwa mwanaye lazima atamuuliza kwa nini anamtimua, alafu yeye atamjibu nini? akajikuta tu amesimama pale sebuleni akiwa amemkodolea macho mpaka pale alipogutushwa na sauti ya Dennis.

"... Shkamoo Baba..."

"... ah,.. marahaba Dennis... eh.. vipi.. mbona mapema sana..."

alijikuta akimpachika swali bila kutarajia kulingana na msukumo uliokuwa ndani yake wa kutamani kumtimua pale sebuleni.

"... year... nataka tu kufuatilia habari mbalimbali zinazoendelea duniani..." alijibu Dennis huku akiwa tayari anawasha luninga.

"... lakini we huoni kama utajiletea matatizo,.. kila siku unaamka mapema kiasi hiki alafu bado kulala unachelewa?.."

aliendelea kuongea Mzee Bisu katika hali ya kutafuta jinsi gani amtimue Dennis ili apate upenyo wa kuingia chumbani kwa Hasina.

"... matatizo ya nini sasa baba..."alihoji Dennis akiwa tayari ameshakaa kwenye sofa kwa ajili ya kuanza kufuatilia kile kilichomuamsha mapema, swali hilo kama lilikuwa gumu kidogo kwani alipojiuliza ni matatizo gani atakayoyapa kwa kuamka mapema akachemka akajikuta tu ametamka.

"... siku utadondoka ghafla, alafu watu watakushangaa... hebu rudi chumbani kalale tena kama lisaa hivi ndipo uamke..."

Dennis alijikuta akigeuka kumuangalia baba yake kama alikuwa serious au anaongea tu, kwani kauli hiyo ya kumuambia arudi akalale tena kidogo ilimshangaza maana hiyo ni kawaida yake ya siku zote na Baba yake huyo ndo aliwahi kumshauri awe anaamka mapema, sasa inakuwaje leo anamuambia asiamke mapema?.. akatamani amuulize baba yake kama alikuwa sawa, lakini alipomuangalia aligundua kuwa baba yake aliongea kabisa kutoka moyoni, ikabidi tu aikaidi kauli hiyo kwani hakuona sababu ya msingi ya kumrudisha kulala.

"... baba nilishakuambia kuna news za muhimu nataka kuzifuatilia... mi siwezi kulala tena saa hizi..."

Mzee Bisu alitamani amrukie kwa vichwa lakini akasita tena na kujiuliza mwenyewe sasa nikimlazamisha si ataanza kunihoji maswali... na mimi ntamjibu nini?..

akajikuta tu amekaa kimya na kumuangalia mwanaye huyo mpenda habari za asubuhi na mapema kwa jicho kali na la chuki, alikuwa amekoseshwa utamu wa siku hiyo na aliokuwa ameukusudia na kuufikiria kila wakati, akaamua kubadilisha ratiba na kwenda mazoezini, lakini kichwani kwake alikuwa tayari na wazo jipya kwa ajili ya kupata raha zake na mtoto Hasina siku hiyo... Ni gani gani?


💥bofya hapa soma jinsi ya kutengeneza batiki


... Alifanya mazoezi lakini mazoezi yake ya siku hiyo hayakunoga kwani alikuwa na mawazo mengi kichwani, muda wote wa mazoezi yake alikuwa akipanga ni jinsi gani atapata raha siku hiyo kwa mtoto Hasina, siku hiyo hakufanya mazoezi kama kawaida ya siku zote, alifanya kidogo tu kisha akarudi nyumbani, hata Dennis alishangaa kuona Siku hiyo baba'ke anamaliza mazoezi mapema kwani sio kawaida yake, siku zote akienda mazoezini hutumia masaa mawili lakini siku hiyo alitumia nusu saa tu akarudi nyumbani.

Alipoingia ndani alimkuta Dennis akiendelea kufuatilia taarifa ya habari, akampita bila kuongea neno lakini Dennis alipogeuka na kumuona akamuuliza

... baba, mbona leo mazoezi umemaliza mapema?..

... ndio... nataka niwahi ofisini kuna kazi nyingi za kufanya..." aliongea huku akielekea chumbani kwake, lakini kabla hajaingia akageuka na kumuuliza Dennis.

"... kwa leo unaratiba gani Dennis?.."

"... leo mimi sina ratiba yoyote, nitashinda hapa..." alijibu Dennis bila ya kumuangalia baba yake, jibu hilo lilimkera sana mzee huyo kwani alitaka kujua ni muda gani pale patakuwa free ili aweze kurudi na kufanya mambo yake na Hasina, akiwa bado amesimama hapo mlangoni akampachika swali jingine la kizushi.

"... kwa hiyo siku nzima utashinda unaangalia taarifa ya habari..." alihoji mzee Bisu huku akijaribu kuficha Hasira zilizokuwa zinamfukuta moyoni kuhusu mwanaye huyo kutaka kumkosesha alichokikusudia siku hiyo.

Dennis aligeuka na kumuangalia baba yake ambaye naye alikuwa akimuangalia na huku akisubiria jibu.

"... kwani baba kuna sehemu ulitaka twende wote?.." swali hilo lilikuwa gumu kidogo kwa mzee huyo kwani hakutegemea kama ataulizwa swali hilo, akili yake ikafanya kazi haraka na akapata jawabu.

"... hapana,... naona kuwa hii likizo itakubwetesha sana, kushinda unaangalia tv bila kufanya kitu cha msingi naona kuwa itakupotezea vitu vingi sana..." aliongea kwa kirefu ili kumuweka sawa mwanaye huyo asimuhisie kitu, Dennis alijikuta akiwa mpole kwa jibu la mzee huyo, akagundua kuwa kweli hawezi kukaa siku nzima nyumbani akiangalia tu tv, akaamua kuweka wazi ratiba yake ya siku hiyo.

"... ni kweli baba, ukweli ni kwamba sio kuwa siku nzima ntakaa tu hapa naangalia tv, baada ya chakula cha mchana ntakwenda matembezini kidogo, vile vile kuna kitu ntakifuatilia huko kigamboni..."

jibu hilo lilimfurahisha sana mzee Bisu lakini hakupenda kuionesha furaha yake kwani mwanaye angehisi kuna kitu amepanga kukifanya, kabla ya kuingia chumbani akaamua kuuonesha ubaba wake ili kupoteza malengo ya kile ambacho mwanaye huyo angeweza kukihisia.

"... nafikiria nikutafutie college ili uwe unakwenda kuongeza elimu na sio kukaa tu hapo unaangalia tv..." wala hakuwa na mpango huo ila aliamua kusema hivyo tu ili kupoteza maboya ya kutokuonesha furaha yake, akazama chumbani kwake ambako alimkuta mke wake ndo kwanza anaamka, akamsalimia na huku akivua nguo zake za michezo kwa ajili ya kujiandaa kwenda kazini.

INAENDELEA

"... habari za asubuhi..."

"... nzuri... heh,... ina maana umeshamaliza mazoezi?.. kwani saa ngapi saa hizi?.."

"... bado mapema sana ila mimi tu ndo nataka niwahi kuondoka..." aliongea huku akianza kuingia bafuni.

"... basi ngoja nikamuamshe dada aandae chai mapema..." aliongea Bi. Pauline huku akijivutavuta kutoka pale kitandani.

"... hapana, muache apumzike mimi ntakunywa chai cantine..." aliongea na kuzama bafuni ambako haikumchukua mda mrefu sana tofauti na siku zote ambapo akiingia bafuni lazima atumie nusu saa ndio atoke, siku hiyo kila kitu kilikwenda kwa haraka kwani alitaka muda ukimbie ili muda ule alioutaka yeye utimie na afanye kile alichokikusudia, siku hiyo ni dhahiri kuwa alikusudia sana kufanya kitu hicho. haikumchukua muda mrefu kujiandaa, akaaga na kutoka kuelekea ofisini kwake ambako nako kazi zilipigwa fastafasta, lakini pamoja na fastafasta aliyokuwa nayo muda ulikuwa ukitembea kwa mwendo wake wa kawaida kitu ambacho kilionesha kumkera, kwani kila alipokuwa akiitazama saa yake aligundua tu ni dakika tano zimepita toka alipoiangalia tena, akaendelea kuwa mvumilivu hivyohivyo mpaka ikatimia saa saba kamili, akaviweka vitu vyake sawa pale mezani kwake akijiandaa kutoka, lakini baadae akakumbuka kuwa Dennis alimuambia kuwa baada ya chakula cha mchana ndio atatokana kwenda kwenye mizunguuko yake na muda huo wa saa saba ndio muda wa chakula nyumbani kwake, akaamua kuvuta muda tena mpaka ikatimia saa nane kamili. akafunga ofisi yake akatoka na kumuaga secretari wake ambaye naye alishangaa kumuona bosi wake siku hiyo akitoka mapema, kwani huwa hana kawaida ya kutoka hata muda wa lanchi yeye huwa anabaki ofisini.


***************


baada ya kupata chakula cha mchana Dennis hakupenda kupoteza muda, alimuaga mama yake kuwa anatoka na atarudi jioni.

"... hata mimi natoka, nataka niende kwenye mambo yangu..." aliongea Bi. Pauline akiwa anamalizia chakula chake.

"... basi tutakutana jioni..." alijibu Dennis huku akitoka, alipotoka haikuchukuwa muda murefu Bi. Pauline naye akajiandaa, alipokuwa tayari akamuaga Hasina kuwa aangalie nyumba vizuri kisha naye akatoka.

💥bofya hapa soma jinsi ya kutengeneza batiki

INAENDELEA

Post a Comment

0 Comments