kama Hasina asingekuwa makini angegundulika kwani mara tu baada ya kukutanisha macho na Dennis alishituka kwani hakutegemea kama angemkuta Dennis pale akamuwahi na shikamoo.
"... Shikamoo kaka Dennis..."
👉SOMA HAPA MBINU ZA KURIZISHANA KITANDANI
"... marahaba dada, umeamkaje?.."
"... sijambo..." akatembea taratibu akapita nyuma ya Dennis na kuelekea msalani ambako hakuchukuwa muda akarudi na kuingia tena chumbani kwake akimuacha Dennis akiendelea kuangalia Taarifa ya Habari, alimkuta mzee Bisu akiwa kajibanza nyuma ya mlago.
"... ni nani yuko hapo sebuleni?.." alihoji mzee Bisu tu baada ya Hasina kuingia na kuurudisha mlango.
"... ni kaka Dennis..."
"... anafanya nini hapo sebuleni?..."
"... anaangalia taarifa ya habari..."
"... aghrr... huyu mtoto naye mbona anakuwa mjinga sana, anaangalia taarifa ya habari saa hizi ya nini?.." alijikuta akiropoka kwa jazba.
Hasina yeye alibaki kumkodolea macho tu akimshangaa kwa swali lake hilo, alimshangaa kwa kuwa kila siku yeye ndo huwa anamlazimisha mwanaye kuangalia taarifa ya habari ili ajue dunia inakwendaje eti leo anamlaumu kwa kuangalia taarifa ya habari, ama kweli siku ya ndege kufa miti hutereza.
jua lilikuwa likizidi kupanda na muda sio mrefu mke wake angeamka, na kama kawaida yake akiamka tu huwa anakwenda kukaa pale sebuleni kwa muda ndipo aendelee na mambo mengine, sasa kama akiamka mke wake mambo ndo yatazidi kuwa mabaya zaidi.
"... sasa tutafanyaje Hasina maana huyo hatoki hapo mpaka taarifa ya habari iishe..." aliendelea kuhoji Mzee Bisu, Hasina hakuwa na jibu zaidi ya kukaa kimya na kuendelea kutafakari.
👉SOMA HAPA MBINU ZA KURIZISHANA KITANDANI
... hakuna kati yao aliyekuwa akiongea neno wote walizama katika lindi la mawazo na wasijuwe cha kufanya, walikuwa wakitafakari ni jinsi gani watafanya Dennis aweze kutoka pale sebuleni na mzee Bisu apate mwanya wa kuchoropoka mle chumbani kwa Hasina bila kuonwa na mtu yeyote, na ikibidi atoke nje kabisa ili kuwajengea imani kuwa kweli alikuwa mazoezini.
Wakiwa katika kuendelea kutafakari mara walimsikia Dennis akiongea na mtu pale sebuleni, walitega masikio na kusikiliza kwa makini, Hofu iliongezeka baada ya kugundua kuwa aliyejuwa akiongea na Dennis pale sebuleni alikuwa ni mama yake yaani Bi. Pauline mke wa Mzee Bisu.
Mzee Bisu alitamani ardhi ipasuke apite chini kwa chini atokee nje ya geti, kwani alihisi kuwa uwezekano wa yeye kutoka mle chumbani kwa Hasina ulizidi kuwa mdogo sana kwani kitendo cha mke wake kuamka kingesababisha azidi kukaa mle chumbani kwa muda mrefu sana. Alianza kujutia maamuzi yake ya kuingia chumbani kwa Hasina siku hiyo, ni kweli alikuwa amepata raha alizozitaka lakini sasa raha imekuwa karaha, Hakujuwa afanyeje ili kutoka mle chumbani.
Baada ya muda wa kuendelea kutafakari nini wafanye, walisikia mtu akitembea kuelekea mlango wa kile chumba walichokuwemo, jasho lilianza kuwatiririka bila ya kujuwa chanzo cha jasho hilo ilikuwa nini.
Hasina alisogea na kuchungulia mlangoni, aligundua kuwa aliyekuwa akiusogelea mlango ule ni mke wa mzee Bisu, alikurupuka na kumsogelea mzee Bisu na kumuambia kwa sauti ya taratibu.
"... tumekwisha, mama anakuja kugonga mlango wangu..."
mzee Bisu alikurupuka na kukimbilia uvunguni mwa kitanda cha Hasina lakini ikawa vigumu kuweza kuingia kwani ukubwa wa mwili wake ulizidi ukubwa wa uvungu wa kitanda cha Hasina, wakati akihangaika kuingia, mlango uligongwa na sauti ya Bi. Pauline ikasikika.
"... Hasina,.. we Hasina..."
"... Beee..."
Hasina aliitikia huku macho yake yakiwa kwa mzee Bisu aliyekuwa akiendelea kulazimisha kuingia uvunguni bila mafanikio.
"... we bado umelala mpaka saa hizi wakati jua lilishakuchwa?.." aliendelea kuongea Bi. Pauline akiwa palepale mlangoni.
"... hapana mama nilishaamka muda mrefu mama na kuja..."
"... sasa unafanya nini chumbani humo, toka basi..." aliongea Bi. pauline huku akianza kuondoka
"... nakuja mama..."
ni kama walikuwa wanakimbia mbio ndefu kwani walishusha pumzi kwa nguvu tena kwa pamoja na huku sauti ya kuhema ya mzee bisu ikitokea chini ya uvungu, ni baada ya kusikia hatua za Bi. Pauline zikitokomea sebuleni.
Mzee Bisu alikuwa amefanikiwa kuingiza kichwa tu uvunguni wakati kiwiliwili chote kilikuwa nje, alitoka na kuanza kujifuta vumbi. mapigo ya moyo yalikuwa bado yakimuenda mbio na kijijasho kikiwa kinamtoka, akamuangalia Hasina kisha akamwambia.
"... inabidi utoke, maana ukibaki humu mama yako atakuja tena na mara hii ataingia moja kwa moja..."
"... sasa wewe utafanyaje?..." alihoji Hasina
"... wewe nenda mimi ntabaki hata kama ntachelewa kutoka lakini ukishafika nje tafuta ujanja wowote ambao unaweza kuufanya ili na mimi nitoke humu ndani, tofauti na hivyo ntakuwa sitoki humu ndani…"
Hasina alitikisa kichwa kukubaliana na alichokisema mzee Bisu, akafungua mlango na kutoka, hakumkuta Bi. Pauline ila Dennis alikuwa bado kakaa pale pale akiendelea kuangalia tv, alipitiliza moja kwa moja na kuingia jikoni ambapo alianza kupanga kazi za kufanya, haikuchukuwa muda Bi. Pauline naye aliingia jikoni.
"... we Hasina leo unatatizo gani..." alihoji Bi. Pauline mara tu baada ya kuingia jikoni.
"... sina tatizo lolote mama..."
"... we si nilikusikia ukiongea na kaka yako Dennis hapo sebuleni?... sasa mbona ulirudi tena kulala wakati unajua kuwa umechelewa kuamka?.."
"... sijarudi kulala mama nilikuwa na jiandaa..."
"... haya fanya fanya basi haraka, baba'ako saa hivi atakuwa anarudi kutoka mazoezini na yele akifika tu lazima ataanza kuulizia chai si unamjua tena?..."
"... haya mama..." aliitikia Hasina huku moyoni akisema. "ungejua mumeo hajaenda mazoezini yuko chumbani kwangu..."
baada ya kumaliza kilichomleta mle jikoni Bi. Pauline alitoka, Hasina naye hakuendelea na kazi bali alisogea mlangoni kuchungulia ni wapi anaelekea mama huyo, alimshuhudia akipitiliza kwenye korido ya kuelekea chumbani kwake, alipotupa macho pale sebuleni tena alimuona Dennis naye akiinuka na kuanza kutoka nje huku akijinyooshanyoosha, hakufanya kosa alitoka haraka baada ya Dennis kupotelea nje akakimbilia moja kwa moja mlangoni kwake na kunyonga kitasa akaingia bila hata hodi.
kidogo amuue mzee wa watu kwani alishituka sana akijuwa tayari amekutwa na mkewe.
"... utaniua we mtoto, mbona haujabisha hodi..." aliongea mzee Bisu huku akitweta.
Hasina hakujibu wala kupoteza muda wa kuongeaongea tena, akamkurupusha
"... toka, toka haraka wote wameondoka..." aliongea Hasina huku akihema kulingana na zile mbio fupi alizopiga mle ndani.
Mzee Bisu hakupenda kupoteza muda, alichomoka kama mshale na kwenda kusimama katikati ya sebule.
wakati anafunga breki tu akakutanisha macho na mwanaye Dennis ambaye naye alikuwa ndo anaingia kutokea nje, kwanza Dennis alipata mshituko na akabaki akimkodolea macho baba yake bila kuongea neno na huku akiwa kasimama palepale mlangoni akiwa kama kapigwa na soti ya umeme, Mzee Bisu naye alikuwa akimuangalia mwanaye kama kuna kitu alikuwa anasubiria kusikia kutoka kwake…
👉SOMA HAPA MBINU ZA KURIZISHANA KITANDANI
ITAENDELEA

0 Comments