Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Responsive Advertisement

Simulizi: Mam'mdogp Lisa sehemu ya kumi (10) MWISHOOOO

 


.... Alipoingia chumbani kule Hasina alianza kutafuta hicho alichotumwa na bosi wake lakini alikuwa hajakiona, aliendelea kutafuta bila mafanikio, ni dhahiri kwamba Mzee Bisu alimtuma akachukue kitu ambacho hakipo, lakini akiwa anaendelea kutafuta ghafla alishituka kumuona mtu akisimama nyuma yake alipogeuka akakutana uso kwa uso na Mzee bisu, akataka kumwambia kuwa alichomtuma hajakiona lakini kabla hajafanya hivyo Mzee huyo alimrukia na kumkumbatia kisha akamwambia kwa sauti ya chini

“... nilitamani sana kuukumbatia mwili wako mpenzi wangu ndio maana nikakutuma huku...” aliongea hivyo akiwa amemkumbatia kisha akamuachia na kumtazama moja kwa moja machoni.

“... kwani wewe na Dennis mna agenda gani... mbona siwaelewi?..” aliuliza Mzee Bisu.

“... aka... kati yangu na Dennis hakuna chochote kinachoendelea...” alijibu Hasina kwa kuinua mabega juu

“... sasa mbona mko karibu na mnafuatanafuatana, kwani vipi...” aliendelea kuuliza mzee huyo akitaka kufahamu kama ni kweli mwanaye anataka kumuingilia kwenye anga zake au la. lakini kabla hajapata jibu kutoka kwa Hasina wote wawili walishitushwa na muungurumo wa gari likipaki, walibaki kimya kwa muda kisha Hasina akatamka na huku akijinasua kutoka mikononi mwa mzee huyo.

“... mkeo huyo karudi, niache mimi nitoke zangu...” aliongea kwa harakaharaka, lakinbi Mzee Bisu aliendelea kumshikilia

“... subiri Hasina,.. leo usiku usifunge mlango, nitakuja sawa?..” aliongea Mzee Bisu kisha akamuachia Hasina ambaye hakujibu kitu akaanza kutoka, aliuvuta mlango ambao ulikuwa umejirudisha na kutaka kutoka, lakini akasita na kurudi nyumba haraka. ni kwamba alipokuwa akitoka macho yake yalianza kutangulia kule anakoelekea, na hapo ndipo alipomuona Bi. Pauline akipita sebuleni pale kuelekea Jikoni akiwa na mifuko yake mikononi. mzee Bisu naye alishituka na kumuuliza kwa wahka.

“... vipi?..”

“... mkeo,.. amepita kuingia jikoni,,, ngoja niondoke...” alijibu kisha akachungulia tena, hakuona mtu zaidi ya kumuona Dennis akiwa anamkodolea macho. alitoka kwa mwendo wa haraka.

alipoingia jikoni Bi. Pauline aliweka mezani mizigo yake kisha akaanza kutoka tena kurudi sebuleni huku akiongea kwa sauti.

“.. Dennis, kwani huyu Hasina yuko wapi?..”

lakini swali hilo lilimkuta Hasina akiwa tayari amefika pale sebuleni na yeye ndio akalijibu swali badala ya Dennis.

“... niko hapa mama,.. za huko,..” alijibu na huku akitembea kuelekea hukohuko jikoni.

“... ulikuwa wapi mbona sijakuona nilivyoingia,.. alihoji Bi. Pauline.

Hasina aligeuka nyuma kumuangalia Dennis kIsha akageuka na kujibu swali lake kiupole.

“... nilikuwa huko nyuma nilikuwa namalizia kufanya usafi, niliposikia ukipaki gari ndo nikaja...” alijibu kwa kirefu na huku wakati mwingine akigeuka kumtazama Dennis kama ataongea chochote, lakini Dennis alikuwa kimya akiwatazama tu.

“... haya nenda jikoni uanze kuandaa chakula nilishakuletea kila kitu...” aliongea Bi. Pauline na huku akiondoka kuelekea chumbani kwake. Hasina naye aligeuka kwa mara ya mwisho kumtazama Dennis kisha akaondoka kuingia jikoni kwa ajili ya kuandaa chakula.

kabla hajafika chumbani kwake Bi. Pauline alikutana na Mume wake naye akitoka, Mzee Bisu alikuwa na wasiwasi lakini alijaribu kuficha wasiwasi wake kwa kujifanya anamuuliza swali mke wake lisilo na msingi.

“... mbona umewahi kuirudi mama Dennis, umefika sokoni kweli?..” alihoji huku akipishana na mke wake. mkewe naye alimjibu huku akipita.

“... ndio, si nilikwenda na gari langu...” alijibu kisha akaingia chumbani, na kila mtu akaendelea na shughuli zake kama kawaida.

Dennis alitaka kuanza kupata hisia kuwa baba yake atakuwa na mahusiano ya kimapenzi na Hasina lakini alikuwa akijaribu kutafuta pointi ya msingi ya kulithibitisha hilo akaikosa, kwani kuingia chumbani kwa baba yake Hasina alitumwa na kwa vile hakukiona alichotumwa ndio baba yake akamfuata huko kwa hiyo hakuna pointi yakuthibitisha hisia zake hizo. akaamua kuendelea na mpango wake wa kumnasa Hasina, lakini ajabu kwa siku hiyo ilikuwa ngumu kupata hata dakika moja ya kuongea naye kwani kila alipotaka kuwa karibu na Hasina baba yake naye alikuwepo au mama yake. mpaka inafika wakati wa kwenda kulala hakupata nafasi hiyo. akajipa moyo kuwa kesho yake itakuwa ni siku ya jumapili nafasi itakuwa yake kwani wazazi wake wote watakwenda kanisani, hivyo akawa mvumilivu.

*************************

Hadi saa nane za usiku Mzee Bisu alikuwa hajapata hata lepe la usingizi, akili yake yote ilikuwa imehamia kwa Hasina, mwili ulikuwa umemsisimka vibaya na alikuwa anavutavuta muda ili mke wake alale fofofo ili yeye akajilie vyake chumbani kwa Hasina. na ndivyo ilivyo kuwa kwani mida hiyo Bi. Pauline alikuwa anakoroma kama pono. Mzee Bisu alimkagua mara mbilimbili kuhakikisha kuwa amelala kweli.

“... yes... alijisemea mwenye baada ya kugundua kuwa mkewe tayari kalala...” alijishika mdomo kujizuia kutamka neno lingine kwani hata lile yes, lilimtoka tu kulingana na furaha aliyokuwa nayo, alinyanyuka taratibu akavaa bukta lake nataulo akalitupia shingoni akaanza kunyata taratibu, akaufungua mlango wa chumbani kwake taratibu huku akigeuka kumuangalia mkewe japo chumbani kulikuwa na giza. alifanikiwa kuufungua kisha akachungulia sebuleni kwanza kabla hajatoka maana mwanaye Dennis huwa na kawai ya kuangalia tv hadi usiku wa manane. sebuleni kulikuwa shwari, akatembea kwa mwendo wa haraka kidogo, akapita sebuleni na kuusogelea mlango wa chumba cha Hasina, akaangalia huku na huku kuhakikisha kama yuko salama, na kweli hakuona mtu, akakishika kitasa cha mlango wa Hasina na kukizunguusha taratibu, kitasa kikakubali sheria na mlango ukafunguka akageuka tena nyuma kuhakikisha usalama wake Mara macho, yakamtoka pima kama mtu aliyeona jini....



Alipoufungua mlango alikuwa na uhakika kuwa Hasina yuko chumbani na alishajiandaa kwa mpambano wa siku hiyo ambao Mze Bisu aliupania sana, lakini alipogeuza macho kujihakikishia usalama wake kabla ya kuzama chumbani kwa Hasina, alishangaa kumuona Hasina akiwa kasimama nyuma yake akiwa kavaa kanga moja, Mze Bisu akabaki kuduwaa kwanza kabala ya kumuuliza alikokuwa, maana mawazo yake alitaka kuanza kuamini zile hisia zake kuwa Hasina na Denis wanaagenda ya siri hivyo akahisi labda Hasina alikuwa anatokea chumbani kwa Denis kujirusha.

".. unatokea wapi tena saa hizi?..' alihoji akiwa bado na sura ya taharuki.

"... natoka Msalani, mbona umechelewa sana?.." alijibu Hasija na kuunganisha na swali ambalo halikujibiwa badala yake akakutana na swali jingine.

"... sio kama unatoka chumbani kwa Dennis wewe?.." aliendelea kuhoji mzee bisu akiwa kasimama pale pale mlangoni, bila kujali kuwa sauti zao zinaweza kusikiwa na watu wengine mle ndani hasa Denis ambaye chumba chake hakikuwa mbali sana na maeneo yale, ni dhahiri kuwa wivu ulianza kumsumbua mze huyo. lakini hasina hakujibu kitu badala yake alipitiliza na kuingia chumbani bila kujibu jambo, kwani alishaona dalili za kusikiwa na watu wengine kama ataendelea kujibishana na mze huyo wakiwa bado wako nje ya chumba. mze Bisu naye alimfuata nyuma akiwa bado anawasiwasi na alikotoka Hasina, aliufunga mlango nhumba yake baada ya kuingia ndani, lakini hakufunga kwa komeo, kwani alikuwa bado na shauku ya kujua ni wapi alikotoka hasina japo alishajibiwa kuwa alikuwa msalani.

"... nimekuuliza swali mbona hujanijibu?.." alihoji tena mara baada ya kukisogelea kitanda ambapo Hasina alikuwa tayari kajilaza tena kifundifudi huku upande ule wa kanga aliojifuna ukiwa umepanda juu kwa bahati mbaya na kuacha sehemu kubwa na mapaja yake kuondekana.

"... si nimekujibu kuwa natoka msalani?.. au ndo ulishaniona mimi malaya sana ambae ninagawa hovyo kwa kila mtu?.. alijibu Hasina kwa kujiamini kidogo bila kujali kuwa anayemjibu hivyo ni boss wake, yeye anamuheshimu kama boss wanapokuwa nje ya chumba hicho, lakini wakishakuwa chumbani hapo ni mtu mwingine tofauti na boss.

Jibu hilo lilimfanya mze Bisu akae kimya kwani alihisi kuwa Hasina anaweza akachukia kwa maswali hayo, na kama angechukia inamaana ndo asingeweza kupata utamu aliokuwa akiutamani kwa muda mrefu, ikabidi awe mpole tu na kupanda kitandani huku akianza kumpapasa Hasina taratibu akiuzunguusha mkono kutokea kwenye kiuno cha Hasina na kupeleka juu ya makalio yaliyokuwa hayana vishwa kufuli wala chochote zaidi ya ile kanga. aliendelea na zoenzi lile huku maneno ya kumsifia yakianza taratibu.

"... unajua we mtoto ni kama umeniroga, maana nakupenda sana mpaka nakuonea wivu kabisa,.. najua nimekuudhi kwa wivu wangu lakini usikasirike sawa mpenzi?.. wewe ndio friji ya moyo wangu sipendi kukuuzi.." maneno yote hayo yalimtoka huku akiendelea na zoezi la kumpapasa Hasina. maneno na zoenzi hilo vilimfanya Hasina naye aanze mbwembwe taratibutaratibu, alianza kujinyonganyonga kidogokidogo, kisha sauti ya kama kuugulia ikaanza kutoka kwambali vitu ambavyo vilizidi kumpagawisha Mze huyo.

                                                     *****************

Kule chumbani Bi. Pauline alikuwa bado kalala fofo, lakini ghafla alishituka kutoka kama mtu aliyekuwa anakimbizwa na majini usingizini kwani alishituka kwelikweli na kubaki akihema, alimungalia mume wake likolala, lakini hakumuona, akabaki akihema na huku akijaribu kuiweka akili yake sawa katika kuendelea kumsubiri mume wake ili amuadithie aliochokiota, kutomuona pale kitandani mume wake hakukumshitua sana kwani aliamini mumewe atakuwa kaingia msalani. lakini muda ulizidi kukatika bila mume wake kurudi, akajinyanyua pale kitandani na kwenda kufungua mlango wa choo ambacho kimo humo chumbani, akashangaa kweupe hamna mtu, akapatwa na wasiwasi, na kuamua kutoka nje ya chumba.


JE HUU NI MWISHO? UNANGANA NAMI KATIKA SEASON 2

MWISHO

Post a Comment

0 Comments