Mzee Mtata alihisi mapigo ya moyo wake yanaenda mbio sana,kijasho kilimtoka jazba na hasira zilimkaba!
“Umeitupia wapi!!!!?”
“Mtoni!”
“Hivi unajua umenimaliza?dah ivi iviiiii daaah!”
Mtata alikosa neno la kusema,alipatwa na kigugumizi,bora ingekuwa imetupwa hata vichakani angesema wakaitafute ila siyo mtoni!
Wake zake wote walikuwa wanamwaga machozi,lilikuwa ni jambo la aibu kwao kusimama mbele ya mume wake na kusema wana mimba lakini siyo zake!
“Kwanini uliitupa?ilikukera nini?”
Chiku hakusema kitu alilia kwa sauti mpaka kwikwi ikamshika,hakuweza kujibu swali la mumewe!
“Sema kabla sijakugeuza nyau hapaaa!’,alifoka akijua njia pekee ya kumpata mwanamke ni kumtia hofu!
“N..nananananasema babaanguaa nasema!”
Chiku kwa hofu alianza kueleza yote mwanzo mpaka mwisho jinsi ilivyokuwa hakuacha hata punje,na mwisho akamtaja Lukas!
“Lukasiiii!!!!”
Alisimama mzee Mtata akiwa haamini kabisa kama kijana aliyeamua kumtibu bure bila malipo na kumpa kinga dhidi ya uchawi wa aina yoyote ndiye aliyewajaza mimba wake zake!
Tiba ya Lukas ndiyo inamfanya saivi mzimu anamsumbua hataki kurudi kaburini,huku mkewe akiwa ametupa nguvu zake mtoni!
“Unamaanisha Lukas ndiyo kawapa mimba hawa !”
“Siyo hao tu na mimi pia nina mimba!”,alijibu Chiku!
“Niniiiiiiii!
Mtata alianguka presha ilipanda akapoteza fahamu na katika kuanguka kwake aliangukia kile kinu cha kiapo yale maji yakamwagikia miguuni,wake zake wakaanza kulaumiana!
“Unaona sasa tatizo umesema kila kitu!”
“Mlitaka nife acheni ujinga njooni tumbebe tumuingize ndani!’
Walimbeba mume wao wakamuingiza ndani akiwa hajitambui kabisa,hali ya mzee Mtata ilikuwa mbaya sana,kwa vile Chiku anajua baadhi ya amadawa akaanza kumtibia!tatizo alimwagikiwa na maji yale miguuni miguu yake ikapooza!
*********
Mzee Jomo aliamka akiwa hana hili wala lile ,alizunguka nyumba yake akapita zizini huku anapiga miluzi,mkononi kashika mswaki waake wa mti!
Alizunguka na kuridhika na mazingira ya nyumba yake,ndipo akafikiria kwenda kumuamsha Lukas maana alimuahidi kumfundisha baadhi ya madawa!
Taratibu akazipiga hatua zake mpaka kwenye kijumba ambacho Lukas amekuwa akiegesha mbavu zake tangu amkaribishe kijijini!
Alifika akagonga sana mlango akimuita Lukas lakini ukimya ulimpa mashaka sana,hakukuwa na muitikio ndipo akaamua kuingia ndani,alishangaa kukuta kitanda kikiwa kitupu!
“Huyu kijana kashakuwa mwenyeji sasa”
Alijisemea mzee Jomokisha akaendelea na mambo yake,hakuwa na wasiwasi aliaminikama ametoka basi hatokuwa mbali!
Suzy alishtuka baada ya kuamka na kumkosa Selina kitandani,kama kuna watu walikuwa wavivu kuamka mapema ni Selina,alijiuliza inakuwaje leo aamke mapema kiukweli alistaajabu sana!
Aliamua kupotezea akiamini pengine mdogo wake kaamua kubadilika,maana walishapiga kelele mpaka wakachoka!
Aliamka akamkuta baba yake nje akamsalimia kisha akaendelea na shughuli zake kama kawaida,ila kadri muda ulivyozidi kwenda ndivyo wasiwasi ulimjaa!
Mama Zubeda kama kawaida aliingia zizini kukamua maziwa,lakini kuna kitu kilimshangaza siku ile,alijisikia kichefuchefu sana akiwa anakamua maziwa hadi akatapika!
Ilibidi amuite Zubeda aje akamue yeye akashindwa kabisa kuendelea,hali ile ilimshangaza sana mzee Jomo ila akachukulia pengine ni homa za kawaida!
Selina ndiye alikuwa binti anayempenda kuliko mabinti zake wote,alimjua binti yake ni mvivu sana kuamka,hivyo alipoona mabinti zake wote wapo nje ila yeye hajaonekana akajua tu atakuwa amelala!
Alivumilia sana mwisho uvumilivu ukamshinda na muda ule hata Lukas naye alikuwa hajaonekana bado!
“Suzy ebhu kaniamshie huyo Selina analalaje mpaka saivi amekua sasa!”
Kauli ile ilimfanya Suzy aanze kuwaza upya ni wapi mdogo wake alipo,alimsogelea baba yake karibu!
“We sinimekwambia ukamwamshe mdogo wako?”
“Baba misijui hata nisemeje?”
“Usemeje ndiyonini?”
“Baba mimi nimeamka sijamkuta Selina kitandani?”
Mzee alisimama kichwa kilimzunguka,alijiuliza binti yake atakuwa ameenda wapi?Haraka akaiita familia yake yote!
“Nambieni Selina yuko wapi na kaanza lini hii tabia?”
“Mume wangu kwa kweli nayaona haya ni mageni kwa wengine naweza kukubali ila siyo kwa Selina hata mi sielewi!”
“Hayo siyo majibu nayotaka kusikia,nataka kusikia mnaniambia Selina alipo!”
“Baba labda kwa mgeni!”,Suzy alijikuta karopoka!
“Nini?umesema nini wewe?unamaanisha Lukas huyu au mwingine?”
Mzee Jomo kijasho kilimtoka akaanza kuunganisha matukio,Suzy alichafua hali ya hewa!
Haliya hewa ilichafuka,Suzy aliyaibua yaliyojificha na kumfanya Mzee Jomo asimame akiwa amefura kwa hasira!
Suzy baada ya kuona daliliya kutokumuona mdogo wake alijua moja kwa moja atakuwa kwa Lukas,na ukizingatia kuwa jana yake aliwaona waliondoka uwanjani kabla hata shughuliya kuutoa mzimu haijaisha!
“Naomba uniambie kila kitu,unajua nini kuhusu Selina na Lukas?”
“Baba mi niliwafumania siku moja kwenye zizi wanafanya mambo ya ajabu,nikamkanya Selina akasema hatorudia lakini jana tulikuwa kwenye shughuli uwanjani kule,ila waliondoka kabla haijaisha,nikawafutailia wakaingia humo kwa Lukas!”
“Kwanini hukumwambia mamayako?”
“Baba nilitaka nikuambie asubuhi!”
“Baba Suzy muongo Lukas ni mchumba wangu,nilikuwa nakusubiri tu urudi nikuambie?”
“Paaaaa”
Mzee Jomo alishindwa kuvumilia alimtandika kofi zito Zubeda akaangukia pembeni akaanza kulia!
“Mama Zubedaaaa hivi ndivyo unavyolea mabinti zako?”
Mama Zubeda alikuwa analia na mengi,aliwaza mpaka hapo ameshea penzi na binti zake wawili Zubeda na Selina!
“Baba unanipiga bure tu Lukas ni mchumba wangu nampenda!”
“Nyamaza kenge wewe!”,alifoka mzee Jomo akaelekea kwenye kijumba cha Lukas akafanya ukaguzi akagundua Lukas katoka na kavaa nguo alizomletea jana!
Alitoka akiwa na hasira isiyoelezeka alizunguka kama chizi,Selina ni binti ambaye alikuja na neema mapema tu,mpaka hapo alikuwa anategemea mwanae ataolewa na tajiri mkubwa mjini,ambaye alishaonyesha nia ya kumtaka binti yake!
Walishaongea na kukubaliana kabisa ilikuwa mahari tu itoke japo hilo suala hakuwa amemshirikisha hata mkewe!
“Nawaambia kama Lukas kaondoka na Selina na nyie mnaondoka hapa!”
“Baba Zubeda kwani hayupo ndani!”
“Unauliza makofi polisi,watoto mpaka wanapelekwa mazizini eti wapo wanaishi na mama!”
Kilio cha mama Zubeda alilia akiwaza mpaka hapo ana mimba na Lukas kakimbia na mwanaye!
Mzee mtata alichukua baiskeli yake akawahi mpaka katikati ya kijiji huko akaiweka baiskeli kwa mtu akapata gari mpaka Sumbwanga mjini!
Aliangaza huku na kule lakinihakuambulia kitu ni wazi alikuwa amechelewa sana,mgeni kaondoka na mwenyeji wake,kamchukua kampeleka mjini!
Alichoka akatafuta sehemu akakaa kwanza akiwa hana hamu na Lukas,Lukas kampokonya dhahabu yake!
“Lukas nakuua,utakauka kama mti,utateketea kama mkaa,nitakufanya majivu!”,alisema kwa hasira mzee Jomo kisha akaanza safari ya kurudi kijijini!
Huku kila mtu alibaki ana sikitikia moyoni hakuna aliyekuwa nauwezo wakumwambia mwenzake,kila mtu alibaki na aibu yake!
Mama Zubeda alikuwa chumbani akiwaza mengi,kitendo cha kushea bakora na binti zake ilikuwa ni aibu kubwa sana kwake,kibaya zaidi Lukas hakumuacha hivi hivi kamuacha na ujauzito ambao anajua kabisa si wa mumewe!
“Lukas mbona hufananii na matendo yako,ivi kweli we ni wa kunichanganya na binti zangu!”,machozi yaliuosha uso wake siku ile!
Suzy licha ya kusema yale mbele ya baba yake kwa kuona wivu ila moyo ulimuuma sana,hasa alipogundua kuwa licha ya Lukas kufanya mapenzi na yeye na Selina pia alikuwa anatoka na Zubeda!
Aliumia kwa upande mwingine alitamani Selina angemshirikisha katika safari ile wakalifaidi wote penzi tamu la lukas!
“Lukas ivi wewe ni binadamu au mnyama?”,alijisemea akiwa haamini !
Kwa Zubeda yeye kilikuwa ni kilio tu kwa kwenda mbele,kati wanawake waliowahi kumpenda Lukas kupitiliza ni Zubeda,lakini ndiyo ivyo tena moyo Lukas ulikuwa kwa Selina!
Johari yeye hakuumia sana ila alikuwa anajicheka tu! Mpakawakati huo alikuwa hajui kabisa alilalaje na Lukas!
“Huyu kaka jamani au mchawi,yani nikamfuata nikavua nguo mwenyewe mmmmh!hapana hii siyo kawaida!”
Siku hiyo hakuna kazi iliyofanyika,hata chakula hakikulika kabisa,kila mtu alikuwa na majonzi yake!
Mifugo ililia zizini hakukuwa na mchungaji,kama walishindwa kujilisha wao wangewezaje kuwalisha wengine?
Mzee Jomo alirudi akiwa mpole tayari alijua kapoteza,alijuta kumkaribisha Lukas nyumbani kwake,kibaya zaidi hajui anaishi wapi?alimpokea kama msaada tu!
Aliikuta nyumba imekuwa kama imepatwa na msiba,tabasamu lilienda likizo kwa muda na haikujuikana litarudi lini!alitamani kujilaumu lakini hakuona alikosea wapi,anachoamini yeye alitenda wema kama binadamu wengine!
Akatamani kumlaumu mkewe lakini akakumbuka ile siku anampokea yule mgeni muharibifu mkewe alimzuia kabisa,yeye akalazimisha!
“Umeumia Lukas hii ni Sumbawanga,pole sana kijana!”
Siku ile ilipita kesho yake asubuhi na mapema mzee Jomo akapanda baiskeli mpaka kwa swahiba wake wa muda mrefu,naye si mwingine ni mzee Mtata!
Aliuamini uwezo wa Mzee Mtata alijua kwake ni jambo dogo sana,kiufupi alitaka kumfanyia Lukas michezo ya kiswahili ikibidi awe hata kipofu kabisa!
Alifika salama kwa Mzee Mtata lakini alichokutana nacho kilimkatisha tamaa,Mtata alikuwa hoi kitandani anaumwa hawezi kutembea!
“Mzee mwenzangu mbona kitandani?”,aliuliza mzee Jomo!
“Acha tu mzee mwenzangu,ninaumwa umwa ila niko sawa!”
“Kuna kazi nataka unifanyie utaweza kweli?”
“Kazi gani tena?”
Mzee Jomo hakumficha kitu alieleza kila kitu jinsi alivyompokea Lukas na mwisho kaondoka binti yake Selina!
“Umesema Lukas kaondoka na binti yako?”
“Ndiyo!”,mzee Mtata presha ilipanda ghafla hadi Mzee Jomo akashangaa!
“Mzee mwenzangu,mzee mwenzangu vipi tena?”
Mzee Mtata hakuwa yule katili wa kuogopwa tena,alikuwa mdogo kama pilitoni,aliposikia jina la Lukas,hasira ilipanda na presha ikawa juu!
Machozi yalibisha hodi na hata kabla hajayaruhusu yalitoka kwa wingi,Mzee Jomo alimshangaa sana Mzee mwenzie,amemzoea ni mtu mwenye kiburi na majivuno,hakuwahi kufikiria kwamba kuna siku atatokwa na machozi mbele yake!
“Mzee mwenzangu nini tatizo!”
“Acha tu mzee mwenzangu!”
Bila kuficha kitu japo alijihisi aibu lakini aliamua kumueleza kila kitu mzee Jomo,jinsi alivyomkamata na kumleta kwake!Alieleza mengi sana kuhusu Lukas!
“Mzee Mtata kwa hiyo unamaanisha Lukas kawapa mimba wake zako wote?”
“Ndiyo!”
“Dah!hiki kitoto kumbe kishetani hivi!”
“Nakushauri mzee mwenzangu kaipime familia yako yote,yule kijana sidhani kama ametembea na binti zako wawili tu mpime hadi mkeo!”
“Mkewanguuu hapana hapo nakataaa!”
Mzee Mtata alimueleza jinsi mke wake alikuwa anakuja kwake akisema Lukas ni mdogo wake,kwahiyo ana wasiwasi pia na mkewe!
“Kama kamgusa mkewangu namuua namuua mende yule!”
“Humuwezi!”
“Unasema?”,aliuliza Mzee Joma kwa mshangao!
“Nasema humuwezi na hicho ndicho kinachoniuma mimi,yule kijana nilimuamini sana,kwa upendo niliokuwa nao kwake nilimpa kinga kali sana ambayo hata mimi nikitaka kumfanyia ubaya siwezi,muache tu!”
“Haiwezekeni nasema haiwezekani!”,aliondoka kwa hasira mzee Jomo na kumuacha Mtata anamuita bila mafanikio!
Alirudi kwake akachukua ndimu tatu akazikata kisha akachanaganya na madawa aliyoyajua yeye,alipomaliza aliita familia yake yote!
“Huyo mpuuzi kawatia mimba wake wa mzee Mtata wote,navyoongea na nyinyi hapa Mzee Mtata yuko hoi kitandani!”
“Siyo kweli baba siyo kweli Lukas wanamsi…!”
“Kimyaaa!mwanaizaya wewe!”
Zubeda alijaribu kumtetea Lukas lakini baba yake alimnyamazisha!
“Sasa nisikilizeni hapa,ninawapima mimba!”
Mama Zubeda alishtuka sana,kauli ya mume wake ilimfanya apate hofu kubwa sana,aliamua kujitetea mbele ya mume wake!
“Sasa baba Zubeda kwanini usiwapime watoto mimi mambo yao yananihusu nini?”
“Tena unyamaze Mtata kaniambia kila kitu!naomba mchukue ndimu hizo kila mtu alambe!”
Alisema lakini hakuna aliyeshika ndimu kila mtu alibaki kukodoa macho,mzee Jomo akasimama!
“Msinitanie kila mtu achukue ndimu hapo!”
Kwa hofu wote walichukua ndimu wakiwa wanatetemeka baada ya kulamba wakakaa kusubiri,ile ni dawa ambayo imechanganywa ili kama mtu ana mimba akilamba atahisi kichefuchefu na kutapika!
Johari ndiye alikuwa wa kwanza kutapika wote wakamshangaa,mzee Jomo alijiuliza ina maana na Johari ametembea na Lukas!
Wakati anajiuliza swali lile Suzy naye ngoma ikatiki akarudisha chenji wote wakashangaa ,maana yeye anasema aliwafumania Lukas na Selina!
“Wewe si ulisema umewafumania?”
Kabla hajajibu kitu alishangaa kumuona mkewe anarudisha chenji kumaanisha na yeye naye kitu kimetiki!
“Mamaaaaaaaaaaaaaaa!na wewe!”,binti zake waliuliza kwa mshangao!
Mzee Mtata aliingia ndani akatokana panga akasimama akiwaangalia,wote walikuwa wanatetemeka!
Ajabu Zubeda hakuwa na mimba alisubiliwa lakini hakukuwa na matokeo yoyote,jambo lile llimuuma sana akabaki kulia tu!
Mzee Jomo aliwauliza na wote walikiri kuwa mimba ni za Lukas,alitetemeka kwa hasira alihisi kujutia sana!
“LUKASIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIII!!!!”
Alipiga kelele kubwa akiwa haamini kama Lukas ndiye kanmfanyia unyama ule,akiwa katika sintofahamu ghafla alikuja mgeni akiwa ameongozana na binti yake!
Hakuwa mwingine alikuwa ni mama Zahara na Zahara,alipofika tu hakuuliza moja kwa moja akauliza!
“Yuko wapi huyo klidume aliyemtia mimba binti yangui?”
“Kuna nini?”,aliuliza Mzee Jomo!
“Kuna kijana anaishi hapa anaitwa Lukas kamtia mimba binti yangu!”
Kauli ile ilimfanya Zubeda aanguke na kupoteza fahamu,shughuli ikawa imeishia pale!Mzee Jomo hakuwa na namna japo moyoni alisema atamfanya kitu kibaya Lukas!
Siku ile ilipita lakini kesho yake asubuhi walipoamka hawakumkuta Zubeda ,alikuwa ameacha ujumbe kuwa anaenda mjini kumtafuta Lukas!
“Lukas!Lukas!Lukas!”,alilia Mzee Jomo familia yake iligawanyika,mpaka hapo kapoteza binti zake wawili!
Kijiji kiliingia gharika,ule mzimu uliokamatwa na Mzee Mtata na kuwahakikishia kuwa hautorudi,ulirudi kwa kasi sasa ukawa unabaka watu mpaka mchana!
Mzimu ule ulikuja na nguvu kubwa sana,safari hii hii ulikuwa unabaka na kupotea,wanakijiji waliogopa hata kutembea hasa mabinti na wanawake!
Siyo ivyo tu misukule nayo ilionekana mara kwa mara ikikatiza mitaani,walionekana hata watu waliosadikika kufa zamani ambo kumbe walikuwa wamechukuliwa na mzee Mtata!
Kucha zao zilikuwa ndefu na nywele zao pia,kiufupi walikuwa wanatisha sana,hawakuwa wakiongea wengine walikuwa wamekatwa ulimi na wengine walikuwa wana ndimi ila zilikuwa nzito kuongea!
Viongozi walifunga safari mpaka kwa mzee Mtata hili wakamuulize imekuwaje mzimu umerudi na kingine ile misukule imetokea wapi?
Walipofika walishangaa kukuta mazingira ya nyumba yakiwa yamebadilika kila kitu kilikuwa ovyo ovyo tu,ng’ombe walikuwa wamekufa na mbuzi pia,wake wa mzee Mtata hawakuonekana!
Inasemekana walikimbia baada ya kuona misukule imetoka na inaanza kufanya fujo,ule mzimu pia ulianza kuwabaka hata wao!
Mazingira ya nyumba yaliwatisha viongozi lakini walijikaza wakaingia kilingeni ambako hawakuamini walimkuta mzee Mtata kafariki siku nyingi mpaka kaoza,pembeni yake ulikuwaa umekaa ule mzimu ila ulipowaona ukapotea!
Viongozi walitoka mbio baada ya kuona tukio lile,hawakuwa na namna mdaiwa wao alikuwa amekufa!
Hata ng’ombe walizompa walizikuta zimekufa zote na mbuzi,ilibidi wakakae upya kutafakari hatima ya kijiji chao ambacho sasa kila kona ni misukule na ule mzimu ulishika kasi!
Baada ya kutafakari sana walimtafuta mganga nguli kutoka kijiji cha jirani ili aje awasaidie kufanya ile kazi arudishe amani kijijini!
Alikuja nguli kutoka kijiji cha jirani ambaye alipofika tu aliitisha kikao cha wanakijiji wote wakakusanyika!
Alifanya manyanga yake mwisho akaamrisha aitwe mtu anayeitwa mzee Jomo,watu walishangaa sana!
Mzee Jomo alikuwa nyumbani na mawazo yake akafuatwa na sungusungu wa kijiji na kupelekwa mpaka kwenye ule umati!
Hakuwa anajua chochote kuhusu wito ule alibaki kushangaa,Mganga alipomuona tu alisema!
“Matatizo yote yameanzia kwa huyu mzee!”
Wanakijiji walishangaa sana na kubaki kuulizana imekuwaje mzee Jomo anahusikaje na mzimu ule,hata mzee Jomo alibaki kushangaa tu!
“Najua mnashangaa ila huyu mzee kuna mgeni alimkaribisha kwake,mzee uongo kweli?”
Kidogo sasa mzee Jomo akaanza kuelewa alitingisha kichwa kuashiria ni kweli alimkaribisha mgeni ,japo mpaka hapo hajui mgeni yule anahusikaje na ule mzimu!
Alipewa nafasi aelezee kilichotokea mpaka akamakaribisha mgeni nyumbani kwake,alisimama kwa masikitiko makubwa sana!
Kwanza aliwataka radhi wanakijiji kisha akahadithia jinsi alivyokutana na mgeni yule na kumpa hifadhi nyumbani kwake!
Alielezea yote kila kitu mpaka alivyotoroka na mwanaye na kuacha amewatia mimba binti zake wawili,ila hakumtaja mkewe!
Bila kuficha alieleza pia kuwa mgeni aliwatia mimba wake wote wa mzee Mtata hadi kupelekea akapata presha iliyomlaza kitandani na kuuchukua uhai wake!
Wanakijiji walishika kichwa walitamani sana kumjua huyo mgeni shujaa aliyeingia kwa mzee Mtata na kuwajaza mimba wake zake wote!
Waliona ni mtu wa ajabu sana,baada ya kumaliza kuongea aliomba radhi tena huku analia machozi,aliumia kuona kumbe mgeni ndiye amesababisha mambo ya mizimu kuja kijijini!
Mganga alisimama na kuanza kuelezea chanzo sasa rasmi kilichopelekea mzee Mtata autoe mzimu kaburini!
Wanakijiji walishangaa kusikia kuwa mgeni alilala kaburini siku tatu ili aweze kurudi mjini,ila mganga alisema pia mzee Mtata alipoteza nguvu nyingi kumpatia kinga mgeni yule ambayo amekufa akijutia mapa leo!
Kila kilichoongewa kilikuwa kama ndoto au filamu fulani iliyoigizwa na waigizaji mahiri sana duniani!
Baada ya hapo yule mganga alifanya manyanga yake na kuutoa hadharani ule mzimu,wanakijiji walitaka kuushambulia lakini akawazuia!
Baada ya hapo akaongozana na wanakijiji mpaka makaburini huko akafika mpaka kaburini ulipotoka!
Walishangaa kukuta kaburi liko wazi na jeneza liko wazi juu likiwa limechakaa sababu ni la zamani sana!
Mganga alifanya yake mzimu ukakubali kuingia kwenye jeneza na kisha akaurudisha kaburini,kanuri likafukiwa,wanakijiji ili kuhakikisha hautokuja tena kutokea waliufukia kwa mawe na kokoto nyingi sana!
Amani ikarejea kijijini tena mganga yule aliiondoa misukule haikuonekana kabisa amani ilirejea kama zamani!
Ndipo hapo likatolewa tamko kubwa kuhusu wageni kuingia ndani ya kijiji hiko,na hapo ndipo chuki dhidi ya wageni ilianzishwa rasmi!
Wageni hawakukaribishwa tena vizuri katika kijiji kile,ukipata mgeni unaenda kumtambulisha kwa mjumbe kwanza na unaulizwa anakaa siku ngapi?
Mzee Jomo alianza kuhangaika huku na kule akitafuta dawa ya kumfanyia ubaya Lukas,lakini kila alipoenda aliambiwa haiwezekani na wengine wakamtapeli tu!
Aliuza mpaka ng;ombe zake akasafiri mpaka Nigeria lakini hakuambulia kitu,kinga aliyoweka mzee Mtata ilikuwa kiboko!
Hatimaye mkewe alijifungua na binti zake wakajifungua pia,watoto ambao ukiwaona unasema huyu ni Lukas mtupu!
Hali ile ilimchefua zaidi mzee yule ambaye aliongeza juhudi za kutaka kumfanyia ubaya Lukas ambaye zote ziligonga mwamba!
Mzee Jomo hakula kwa amani,alikonda kwa mawazo na huzuni,miaka ikakatika watoto wakawa wanakuwa na kibaya walichukua sura ya baba yao mtupu!
Mawazo hayakumuacha salama Mzee Mtata alifariki miaka mitano baadae, na kumuacha mkewe akiwa analea familia!
Wake wa mzee Mtata waliondoka na kwenda kuishi kijiji cha jirani,ambako wengine walishaolewa huku kila mtu akiwa na chata ya Lukas!
Miaka kumi sasa imepita siyo Lukas,Selina wala Zubeda walioonekana kijijini,hakuna aliyewaona wala kupata tetesi za wapi walipo!
Historia ya mgeni ikawa imeishia hapo,mgeni alikuja mwenyewe kaondoka na watu wawili,hakuja na mtoto lakini kaacha watoto!
Mgeni kamuua shujaa wa kijiji hiki aliyeogopwa mpaka na sisimizi,mgeni kamuua mzee Jomo kabla hata ya siku zake!
Mgeni kafufua mizimu,mgeni kaleta mizimu mgeni kaleta taharuki,ni nani atampenda mgeni tena katika kijiji hiki?Nani atamkaribisha mtu hasiyemjua tena katika kijiji hiki?nani?nani atamuamini tena mgeni katika kijiji hiki!Hakuna hakuna hakuna!
MGENI ALISHUSHA THAMANI YA WAGENI KATIKA KIJIJI CHETU,VIJIJI VINGINE WANAFURAHI WAKIPATA WAGENI LAKINI HAPA MGENI ANATOA KUMBUKUMBU MBOVU SANA ILIYOWAHI KUTOKEA!
**************
“EFUUUUUUUUUUUUHHHHHHH!”
Nilishusha pumzi ndefu sana,hakika ilikuwa ni simulizi yenye kusisimua na kusikitisha sana,hata mimi nilikubali kwa namna ile ni haki wageni tuchukiwe!
“Ndiyo hivyo kaka!”
“Aiseeh poleni sana!”
“Tulishapoa ila ndo ivyo hatupendi wageni!”
“Kwahiyo na mimi unanichukia?”
“Kidogo maana umeonyesha utofauti!”
“lakini hujaniambia mwanzo kabisa ulisema ulimpoteza dada yako kisa mgeni!”
“Zahara alikuwa dada yangu,alifariki akijifungua yeye pamoja na mtoto!”
“Dah pole sana!”
Wakati tukiwa pale tunajadili walipita watoto watatu wanacheza ndipo Regina akanishtua!
“Eeeh unamuona yule mtoto?”
“Ndiyo!”
“Sasa yule mtoto wa Johari yule aliyekuwa anamchukia mgeni basi unaambiwa ndo kaizaa kopi yake yani ukimuona huyo wanasema ni sawa na Lukas kabisa kwa wanaomjua!”
“Ebhu muite!”
“Unataka ufanyeje?”
“We muite tu!”
Regina alimuita yule mtoto alipofika akatusalimia kisha nikachukua simu yangu nikampiga picha kama tatu hivi!
“Sasa mbona umempiga picha?”
“Aaah nimependa tu!”
Kiukweli nilikuwa sina sababu ya kubaki kijijini sababu nilikuwa nimemaliza utafiti wangu kwa asilimia zote,mbali na utafiti wangu lakini pia mbali na utafiti nilipata story nzuri ambayo nina uhakika itapendwa sana na wengi!
Niliomba nipelekwe kwa mama Zubeda wakafanya ivyo,haikuwa rahisi lakini kutokana na kwamba niliwaambia nataka niwasaidie kuwatafuta binti zao yaani Selina na Zubeda walikubali nikaongea nao kisha nikawapiga picha ya pamoja na picha moja moja!
Niliaga nikaondoka kijijini huku Regina akionekana kuhuzunika sana,hata mzee wake aliumia akinisihi nibaki lakini sikukubali!
Niliondoka nikiwaahidi kuwa nitarudi na Selina,Zubeda na pia nitamleta Lukas aje aombe msamaha kwa kijiji ili wageni tupokelewe tena kijijini!
Nilipanda gari asubuhi na mapema na kuanza safari ya kurejea Dar,safari yangu ilitawaliwa na tabasamu pana kwa kupata simulizi nzuri!
Lakini kichwani nilitamani kuyajua maisha ya Lukas baada ya kurudi mjini,je ni kweli wabaya wake walimsamehe au mzee Mtata alimuingiza choo cha kike!
Nilifika nikapumzika wiki nzima kisha nikachukua ile picha ya yule mtoto wa Lukas nikaitoa kisha nikamtafuta mchoraji hodari na maarufu sana kwa jina la Masoud Kipanya!
“Mdogo wangu mambo vipi?”
“Safi kaka shikamoo!”
“Ahh unaniona mzee,nilishakukataza kunizeesha nambie vipi hatuonani?”
“Kaka Masoud nina shida!”
“Ipi tena!”
“Nina picha hapa”,nilimpa ile picha akaiangalia kisha nikamuambia!”
“Kaka nataka iyo picha unichoree lakini huyo mtoto akiwa mtu mzima,yani uvute taswira huyo dogo akiwa mtu mzima atafananaje najua unaelewa cha kufanya we mzoefu!’
Nilimuelezea Masoud kwanini naitaka ile picha akakubali kunifanyia,baada ya wiki moja aliniita na kunikabidhi picha tatu zikiwa tofauti nyingine zina ndevu nyingine hazina!
Nilizichukua zile picha nikarudi nyumbani nikazihifadhi,nilitamani sana kumpata Lukas ili anipe stori yake na Selina mjini!
Bado namtafuta na hakika nikimpata nawaahidi nitawaletea simulizi nyingine ya Lukas kama season ya pili ya hadithi hii!
Bado nina shauku ya kumjua Lukas kiundani,nataka nimjue aliishije baada ya kutoka kijijini?
Nawashukuru sana kwa kuwa pamoja unaweza kutoa maoni yako kuhusu simulizi hii,mwisho wa hadithi hii ni mwanzo wa hadithi nyingine!TUTEGEMEE SEASON TWO KAMA NIKIMPATA NDUGU YETU LUKAS!
MWISHOOOOOOOOO**********
JACK MAMBO THE KING OF STORIES****
0 Comments