Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Responsive Advertisement

Chombezo: Bao tatu za mgeni sehemu ya kumi nne (14)

 


“OYOOOOOOOOOHH!”,wanakijiji walipiga kelele kumshangilia mzee huyu waliyemuona kama mkombozi wao,bila kujua kuwa ndiye mkandarasi wa kila kitu!

Lukas pekee ndiye alikuwa anaujua mchezo ule,alijua ni maigizo tu hakuna chochote pale,pembeni yake alikuwa na Selina

Alimshika mkono Selina akatoka naye pembeni,Selina alimshangaa Lukas kwa kumtoa pale uwanjani!

“Unanipeleka wapi?”,alihoji Selina!

“Nyumbani!”

Hakuwa na jinsi binti yule waliondoka mpaka nyumbani,moja kwa moja akaingia naye kwenye kijumba chake,Selina ilikuwa ni mara yake ya kwanza kuingia mle ndani!

Lukas hakuwa na subira alianza kumpapasa Selina ambaye si muda alilegea na muda mfupi baadaye wakawa watupu tayari kwa kuvunja chaga!

********


Huku kwa mzee Mtata alifanya manyanga yake na mwisho akaufanya ule mzimu ukapotea mbele za macho ya watu!

Ni yeye pekee alijua ulipoenda,wanakijiji walimshangilia na kumpa zawadi mbali mbali huku viongozi wakimkabidhi ng’ombe zake kumi pamoja na mbuzi wake watano!

Ilikuwa ni sherehe kubwa kumuondoa aliyewanyima amani kijijini,waliamini sasa watalala kwa amani!

Mzee Mtata alipomaliza kazi yake aliondoka na kurejea kwake,wake zake walimpokea kishujaa na kumsifia kwa kufanikiwa kuudhibiti mzimu!

Mzee Mtata hakuwa na hofu na ngvu zake kupungua,alijua kila kitu kiko sawa bila kujua dawa yake ambayo iebeba nusu ya nguvu zake imetupwa,na kadri anacvyotumia nguvu alizonanzo sasa zinazidi kupungua!

*********

Lukas na Selina walienda mzunguko mmoja tu wakatulia,hawakuwa na muda sababu muda wowote ule wengine wangerudi kutoka uwanjani!

“Selina mi nataka kuondoka hapa kijijini!”

Kauli ya Lukas ilimshtua sana Selina ambaye alijikuta anaacha kuvaa nguo zake kwanza amsikilize!

“Unasema!!!!?”

“Naondoka!”

“Unaenda wapi?”

“Narudi zangu mjini

“Lukasiiiii!”

Selina aliachia alichokuwa kakishika mikono akaitupia kichwani akiwa haamini alichokisika,alikaa kitandani machozi yalikuwa yanamtoka!

“Sasa unaniacha na nani jamani?”

“Naondoka na wewe!”

“Lukasiiiiiii!”

Alishtuka Selina hakujua Lukas anaondoka naye kivipi?na wataondokaje na nani atawaruhusu?kichwani yalipita maswali mengi!

“Hutaki?”

“Siyo sitaki Lukas,tunaondokaje na nani ataturuhusu!”

“Hatuhitaji ruhusa ya mtu!”

“Lukasiiiii!unamaanisha tutoroke?”

JE NINI KITAENDELEA?SELINA ATAKUBALI ?NA VIPI MZIMU UMEONDOKA?


Chombezo………….BAO TATU ZA MGENI!

Mtunzi……………….Jack Mambo

Whtsp………………..0752761388

Call…………………….0716352102

Umri…………………..18+


Sehemu ya 52


Kila mzazi ana kipenzi chake kati ya wanae wote,atawapenda wote lakini yupo mmoja mzani utaelemea kwake!

Mzee Jomo alikuwa na mapenzi mazito juu ya binti yake wa mwisho ambaye ni Selina,na Lukas naye kajikuta kafanya mapenzi na familia nzima ila kwa Selina ndipo kaweka kituo!patamu hapo!

Selina ilimuwia ngumu kukubaliana na maneno ya Lukas,hakutaka kuamini kwamba ni yeye anataka kutoroka na mwanaume!

“Lukas mi siwezi!”

“Selina utaishi kijijini mpaka lini?mi mjini nina maisha mazuri,utakuwa mkewangu acha huku unanishea na dada yako Suzy!”

“Lukas mi naogopaaa!”,alisema Selina huku akilia!

“Usilie Selina mi nimekupenda na niko tayari kufanya kila kitu kwa ajili yako,tafadhali naomba ukubali kuondoka na mimi!”

Baada ya kubembeleza sana mwisho alikubali kishingo upande kuondoka na Lukas mjini,Lukas alifurahi sana akamuahidi baada ya siku mbili kila kitu kingekuwa tayari!

Baada ya kuachana na Selina alianza kufanya mpango wa nauli,hakuwa na njia nyingine zaidi ya kuuza ng’ombe za mzee Jomo!

Alitafuta mteja wa ng’ombe akampata dalali ambaye alimpa dili,kesho yake akiwa machungani dalali alikuja na mteja akawauzia ng’ombe wawili wakubwa ambao thamani yao ilikuwa zaidi hata ya milioni,lakini aliuza kwa laki tano tu!

Ilikuwa ni ngumu kujua ng’ombe wamepungua sababu zilikuwa ni nyingi sana,akawa tayari amepata nauli ya kwenda mjini!

Baada ya kuirudisha mifugo nyumbani alipumzika akapewa chakula akawa anakula,wakati anakula alishangaa kumuona mzee Jomo anakuja na begi lake!

Alipatwa na mshangao mkubwa sana akashindwa hata kula kabisa,hofu na wasiwasi vilimtawala!

“Babaaaaaaaaa!”,wanae walimpokea kwa furaha kubawa!

Mzee Jomo akaingia nyumbani kwake,akiamini kila kitu kiko sawaa hakujua alimkabidhi fisi bucha,na fisi kaitumia vizuri nafasi ile!

“Lukas!”,alimuita Lukas!

“Naam mzee shikamoo pole na safari!”

“Marahaba!vipi umeenda machungani?”

“Ndo nimefika si muda mrefu napoza njaa hapa karibu!”

“Safi sana!”

Mzee Jomo aliingia ndani na kumuacha Lukas anakula,kwa upande wake Lukas alikuwa na hofu kubwa sana!

Mambo aliyoyafanya yalimfanya ajishtukia na kushindwa kabisa kumtazama mzee Jomo machoni!

Wanasema mwizi akimuona askari huwa anajistukia hata kama askari ana mambo yake tu,anaweza kujikuta anakimbia tu!

Alipopata tu upenyo wa kuongea na Selina alimvutia pembeni akamuambia suala la kuondoka!

“Tunaondoka kesho!”

“Lukas!huoni ni hatari baba karudi!”

“Hatuwezi vuruga ratiba yetu!”

“Lukas tusubiri baba aondoke!”

“Hatuna muda kama huondoki sawa mi kesho hutoniona,kama unaondoka ujue unaamka usiku saa tisa utanikuta nakusubiri!”

Lukas aliondoka na kumuacha Selina kasimama akiwa njia panda,hakujua afanyaje?abaki na ndugu zake au akubali kuondoka na mgeni huyu ambaye ndiye aliyemuingiza kwenye ulimwengu wa mapenzi!


Familia ya mzee Jomo ilikuwa na furaha sana siku ile,kawaida akirudi na zawadi kibao kutoka mjini,aliwapa zawadi zao wakafurahi sana!

Hakumsahau Lukas,alimletea suruali na shati jipya kabisa,hakujua kuwa anayemthamini katembea na familia nzima na kama haitoshi anataka kutoroka na mwanaye kipenzi Selina!

Usiku uliingia wakatawanyika Lukas akaingia kwenye makazi yake,alikuwa na mawazo sana kuhusu Selina!

“Itakuwaje hasipotoka,dah ila itabidi niondoke niliyoyafanya hapa yanatisha,huyu mzee ataniua!”

Usingizi ulimchukua akalala,lakini alikuja kushtuka akipapaswa usiku wa manane,alipoamka alimkuta Zahara ndiyo kamvamia usiku ule!

“Wewe unafanya nini?”,aliuliza Lukas kwa mshangao!

“Unajua nachotaka Lukas acha kujichetua,unataka Zubeda akufaidi peke yake,hujanipa siku nyingi nimeijia utamu wangu!”

“Zahara mi leo sijiskii utakuja kesho!”

“Yani kati ya vitu sitaki kuviskia ni huo upuuzi wako,ukitaka niondoke nipe hutaki nalala hapa Zubeda anikute mpaka asubuhi!”

“We unamuwaza Zubeda tu hujui kwamba mzee Jomo karudi”

“Afadhali tena akiona huyo atanipeleka kwa baba halafu baba atanileta unioe!”

“Unasemaje?”

Lukas alijua kabisa Zahara atamharibia mipango yake ya kuondoka!

JE LUKAS ATAFANYA NINI?ATAFANIKIWA KUONDOKA?


Chombezo………….BAO TATU ZA MGENI!

Mtunzi……………….Jack Mambo

Whtsp………………..0752761388

Call…………………….0716352102

Umri…………………..18+


Sehemu ya 53


Ulikuwa mtihani mkubwa sana kwa Lukas,kwake siku hiyo muda ulikuwa ni kitu muhimu kuliko vyote!

Zahara hakutaka kuelewa kabisa somo siku ile,alichotaka ni penzi la Lukas!licha ya kumkatalia sana lakini hakuelewa somo!

“Lukas we ongea vyote ila penzi utanipa ndiyo niondoke hapa!”

“Lakini nime…!”

Kabla hajamalizia kusema Zahara alimvamia na kuitoa bakora nje,Lukas hakuwa na namna,alichokifanya alimuacha Zahara afanye anachotaka!

“Zahara mi naumwa nakupa bao moja tu hapa kesho uje tutafanya vizuri!”

“Hayo ndiyo mambo sasa siyo nitoke usiku wote huu nirudi bila bao,huo ni ushamba!”

Lukas aliamua kufanya mapenzi na Zahara ili aondoke,alichokifanya ni kutumia staili zilizomchosha haraka Zahara!

Baada ya Zahara kuvunja dafu tatu tu alianza kuomba po!Lukas alipomaliza bao moja tu Zahara akavaa nguo zake!

“Nitarudi kesho umalizie bao zangu!”

Lukas hakuongea neno alimuacha Zahara akiondoka zake,aliona haukuwa muda wa kulala tena,alivaa zile nguo mpya alizoletewa na Mzee Jomo tayari kwa safari!

Kabla hata hajatoka nje alisikia sauti inamuita nje akajua pengine ni Zahara amerudi tena,akaisikiliza tena kwa makini!

“Lukas!Lukaas!”

Hakuamini alipotoka na kumkuta kipenzi chake Selina,ilikuwa bado kidogo tu amfumanie ila bahati ilikuwa upande wake,ni kama shetani alimlinda siku zote.

Kwa furaha ya kumuona Selina alimkumbatia kwa nguvu sana,hakuamini kama kweli Selina ameamua kuacha familia yake na kuongozana naye mjini!

“Selina siamini!”

“Nakupenda Lukas nimekubali kuiacha famili yangu sababu yako!”

“Naahidi nitakupenda daima mpenzi wangu!”

“Tuondoke Lukas baba huwa anatoka nje usiku!”

Hawakuwa na cha kubeba hata Selina alitoka na nguo alizovaa tu,safari ilianza huku Selina akiongoza njia!

Bahati nzuri walipata gari lililokuwa linapeleka mahindi mjini,wakapanda na kuendelea na safari walifika mjini na siku hiyo hiyo wakapata basi la alfajiri la kwenda Dar!

MGENI AKAWA KAONDOKA KIJIJINI!!

********

Mzee Mtata mambo yalikuwa si mambo tena,baada ya kufanikiwa kuwaaaminisha wanakijiji kuwa ameurudisha ule mzimu ulikotoka,alianza kuona mambo yanamwendea kombo!

Ile dawa yake ambayo mkewe mkubwa aliitupa ilimletea matatizo,sababu ilikuwa ni moja ya nguvu yake kubwa ya uchawi!

Ilikuwa inailinda misukule yake na pia iliwafanya hata maadui zake waogope kuingia kwenye ngome yake!

Kumbe siku ile baada ya kuutoa ule mzimu mbele za watu aliupeleka kilingeni kwake akiamini usiku unaofuata ataurudisha kaburini!

Kweli usiku uliingia mzee Mtata akafunga safari mpaka makaburini akafanya manyanga yake kaburi likafunguka na jeneza likatoka kama kawaida!

Tatizo likaja kwenye ule mzimu,aliuita uje lakini haukutokea,hali ile ilimchanganya sana Mzee Mtata!

Alijaribu mara kadhaa lakini hali bado ilikuwa ileile,mzimu haukutokea kabisa alipotaka kulirudisha lile kaburi kwenye hali yake liligoma pia kujifunga!

Mtata alichanganyikiwa kabisa kijasho kilimtoka,kila alichokifanya kaburi lilimzomea tu,muda ulizidi kwenda mpaka kukakaribia kukucha!

Hakuwa na namna alirudi nyumbani kwake na kuliacha kaburi lile wazi,moja kwa moja aliingia kilingeni alipongalia kwenye misukule yake aliuona ule mzimu umekaa umetulia hauna habari!

Aliuangalia kwan hasira lakini hakuwa na cha kuufanya maana ule ni mzimu siyo msukule wake!Alitoka nje kwa hasira akaanza kujiuliza imekuwaje hali ile inatokea?

Baada ya kuwaza sana aliingia ndani kwa mkewe mkubwa akachukua jembe Chiku akabaki kumshangaa!

“Mume wangu wapi na majembe usiku?”

Chiku hakujibiwa kitu,Mtata alitoka moja kwa moja mpaka alipofukia dawa yake ambayo ndiyo inabeba asilimia nyingi ya uchawi wake!

Alifika akachimba lakini kwa jinsi alivyokuwa anachimba aligundua mahari pale pamefukuliwa siku si nyingi,ardhi yake ilikuwa rahisi sana kuchimbika!

Alijipa moyo akaendelea kuchimba lakini hakuona kitu,hakutaka kuamini kuwa dawa yake haipo alichimba shimo refu sana lakini hakuona kitu!

Mtata alichanganyikiwa kabisa hakuamini kama dawa yake haipo,ile peke yake ndiyo ingemuwezesha kuurudisha mzimu kaburini!

Alijiuliza pengine labda alikosea sehemu siyo ile,kila akivuta hisia akili inamrudisha pale pale!

“Hapana ni hapa hapa,sasa imeenda wapi?oooh Maskini ntaadhilika hapa kijijini!”

Mzee mtata alirudi kilingeni akiwa na mawazo,usingizi haukuja alitamani kukuche awaite wake zake na kuwahoji juu ya wapi dawa yake ilipo!

Alikuwa na wasiwasi sana na mkewe mkubwa Chiku,sababu ndiyo msiri wake mkubwa na ndiye peke yake anayejua siri ya dawa ile ya mzee Mtata!

JE NINI KITAENDELEA?MZEE MTATA ATAFANYAJE AKIJUA CHIKU AMEITUPA ILE DAWA?



Chombezo………….BAO TATU ZA MGENI!

Mtunzi……………….Jack Mambo

Whtsp………………..0752761388

Call…………………….0716352102

Umri…………………..18+


Sehemu ya 54


Siku ile Mzee Mtata aliamka mapema akachukua kiti chake na kukaa nje karibu na jikoni kabisa akiwasubiri wake zake waamke!

Kwa alipokaa alikuwa anaona kila mlango wa nyumba za wake zake,katika hali ya kushangaza alimuona mkewe mdogo Vero akitoka mbio mbio ndani na kuanza kutapika kisha akarudi ndani bila kujua mumewe kamuona!

Hali ile ilimshangaza sana mzee Mtata kwa akili ya kikubwa alijua kabisa ile itakuwa mimba tu jambo ambalo hakutaka kuliamini sababu anajua kabisa hana uwezo wa kumpa mimba mwanamke yoyote duniani!

Akiwa kwenye hali ya kujiuliza alishangaa kuona mkewe mwingine ambaye ni Lolenza naye anatoka mbio akatapika na kurudi ndani!

“Hii ni nini?”,alijiuliza Mtata!

Hatimaye wake zake walitoka nje na kushangaa kumkuta mzee yule nje kakaa,mzee Mtata alimuita Chiku!

“Abee mumewangu”

“Naomba waite wenzako wote hapa nina kikao na nyinyi!”

“Sa..sawa mume wangu!”

Sauti ya Mtata ilimtia hofu sana Chiku,hakuongea kama kawaida alionekana ni mtu mwenye hasira sana!

Wake zake walikusanyika kwa pamoja wakakaa kumsikiliza ana nini cha kusema,alionekana amejaa sumu haswa!

“Nauliza hivi nani alichimba dawa yangu pale uwanjani,na aliipeleka wapi?”

Chiku alishtuka sana kusikia vile sababu ni yeye aliitupa ili wapate uhuru wa kufanya mapenzi na Lukas,sababu ile ilikuwa kama inampa machale mume wao!

“Chiku najua ni wewe peke yako unajua niliweka pale ile dawa nambie umeipeleka wapi?”

“Mi..mi…si..si..sjiui mume..!”

“Nyamazaaaa sitaki kusikia upumbavu hapa,nisubirini nije!”

Mzee mtata aliondoka akiwa na hasira akaingia kilingeni kwake,haikujulikana alifuata nini?Huku wake zake wakaanza kutupiana karata!

“Jamani mi simo,Chiku ndiyo uliitupa!”,alisema Vero!

“Hajitoi mtu hapa zilikuwa ni nyege zenu hakuna mtu kujitoa hapa!”,alisema Chiku!

Hakuna aliyejua Mzee Mtata kafuata nini ndani,walikaa kusubiri mpaka alipotoka alikuwa amebeba kinu!

“MUNGU WANGUU!”,Chiku alishtuka baada ya kuona kile kinu sababu alijua maana yake ni nini?

“Nini mbona unashtuka ni nini kwani?”

“Kinu cha kiapo kile tumekwishaaa!”

Mzee Mtata alirudi akiwa na kinu chake akakishusha chini,akamimina maji ndani ya kinu akachanganya na dawa kisha akaongea maneno yake!

Wakati anafanya yake alishangaa sana kumuona mkewe mwingine ambaye ni Tausi akiwa kashika ndimu analamaba muda wote!

Alimezea mate jambo lile akaendelea na jambo lake,alipomaliza kusema maneno yake alikaa huku chungu kikiwa katikati yao!

“Chiku nadhani unajua maana ya hiki kinu,kwa nyie wengine labda niwaambie tu kuwa hiki ni kinu cha kiapo,nitakuuliza kitu unatakiwa useme ukweli,ukitia mikono yako ndani ya hiki chungu kama umedanganya unakauka na kufa hapa hapa!”

“Nadhani mmenielewa,Vero simama ya juu!”

Mzee Mtata alimuamrisha mke wake mdogo asimame akafanya ivyo huku anatetemeka kwa hofu!

“Nadhani umenielewa ukweli wako ndiyo utakuweka hai aya nakuuliza je una mimba?”

Aliuliza swali ambalo lilikuwa nje kabisa na mada aliyokuwa ameianzisha,walibaki wameduwaa,hakuana aliyetegemea swali lile kabisa!

“Nijibu nina mambo mengi ya kufanya,una mimba!”

“Ndiyo!”

“Siyo mimba yangu si ndiyo?”

“Ni..ni…yako mume…!”

“Weka mikono humo usipoteze muda!”

Hapo ndipo palikuwa pagumu,Vero hakutaka kuweka mikono mzee Mtata akamuamsha mkewe Lolenza akasimama!

“Una mimba?”

“Ndiyo mume wangu”

“Kama ni yangu weka mikono kwenye kinu msiniletee mambo ya mzee Nyage na diamond hapa!”

Lole naye alishindwa kuweka mikono akaambiwa akae,akaamshwa Tausi naye alikuwa na mimba lakini hakutia mikono kwenye kinu!

Mpaka hapo ni wazi alijua kuwa wake zake wote wana mimba na siyo mimba zake,sababu hata yeye anajua hana uwezo wa kuzalisha!

Ilifika zamu ya Chiku ambaye aliulizwa swali tofauti na wenzake,Chiku alitetemeka kwan hofu!

“Nambie dawa yangu umeitupa wapi?kama hujaitupa tia mikono kwenye kinu!”

“Mume wangu na…nasema!”

“Ndiyo useme sasa!”

“Nili,,niliitupa!”

“Unasemaje wewe!!!”

INAENDELEA

Post a Comment

0 Comments