“Hapana ngoja nikampe taarifa kama akikuruhusu uingie!”
“sawa!”
Chiku alienda kilingeni aliporudi alimchukua Lukas na kumpeleka kwa Mzee Mtata!
“Karibu kijana,karibu kijana hahahahahaha!”
“Ahsante sana mzee wangu shikamoo!”
“Marahaba kijana wangu!Karibu sana kijana naona umekuja kwenye lile zindiko eeh?”
“Ndiyo mzee wangu!”
“Hii dawa ni ya gharama sana,inagharimu laki tano!”
Kauli ile ilimfanya Lukas apate mawazo ya ghafla,maana alipo hana hata senti,tangu afike kijijini kazi kubwa anayofanya ni kuchunga mifugo tu na halipwi chochote,kiufupi hakuwa na uwezo wa kuipata hiyo pesa kabisa!
“Hahahaha kijana usiwaze,umeishi vizuri na familia yangu,hii dawa nitakufanyia bure kabisa!”
“Ahsante mzee wangu ahsante sana!”
“Usijali mshukuru aliyekufundisha busara,napenda vijana kama wewe,ungekuwa mwanangu ningekurithisha mikoba yangu hahahahaha!”
Tabasamu lilitawala usoni kwa Lukas,kuna muda alijihisi kujuta kwa matukio aliyomfanyia yule mzee,kitendo cha kutembea na wake zake wote kilimuuma sana!
Wanasema hata shetani kuna muda anakuwa mwema,Mzee Mtata aliamua kumtibu bure kabisa bila hata shilingi!
Maskini hakujua nyuma ya pazia Lukas ni mchepuko wa wakeze wote,hawezi kuhisi tena hiyo hali sababu Chiku alishaitoa dawa yake inayomjulisha mambo mengi,ile ilikuwa kama CCTV kwake!
Hakujua kuwa mkewe mkubwa ambaye ndiye msiri wake alishaitoa na kwenda kuitupilia mbali,bila kujali kuwa ile dawa ni ulinzi kwa mumewe anaoutegemea!
Bila kupoteza muda Mzee Mtata alianza kumfanyia dawa anazojua yeye,siku ile Lukas alikula nyungu mpaka akahisi kuchanganyiiwa,ilikuwa ni nyungu na kuoga madawa!
“Sasa kijana hapo kapumzike kwenye kile kibanda chako,usiku ntakufuata twende sehemu tukamalizie dawa!”
Lukas alitoka akiwa anahisi kizunguzungu,nyungu siku nzima haikuwa mchezo,aliingia kwenye kile kijumba akajilalia kwenye kingozi cha ng’ombe akiwa hoi!
Baada ya kupata chakula cha usiku alilala fofofo akisubiri Mzee Mtata aje amchukue waende kumalizia dawa!
Akiwa usingizini alihisi kupapaswa!aliposhtuka hakuamini alikutana na Vero na Lole wakiwa watupu ni wazi walitaka penzi lake,ilikuwa ni hatari sababu muda wowote Mzee Mtata anamfuata!
Kabla hajasema kitu alisikia sauti ya Mzee Mtata kwa nje ikimuita,siyo yeye wala wale wnawake wote walitetemeka!
“Kijana amka kumekucha!”
Sauti ile iliwapa hofu sana,Lukas alijua haukuwa muda wa kulaumiana,maana wale wake zake walikuja bila kujua,kibaya na yeye alisahau kuwaambia kuwa usiku ule atatoka na Mzee Mtata!
“Kijana ina maana umelala?”
Mzee Mtata sasa aliongea huku anaingia ndani akakutana na Lukas aliyetanda mlangoni,Mzee Mtata akawa ameishia hapo!
“Nilijua umelala nikuamshe!”
“Haa…hapana mzee nilikuwa macho!”
“Sawa nifuate!”
Siku ile ngamia alipita kwenye tundu la sindano,Lukas hakuamini kama amenusurika kufumaniwa na Mzee yule anayeogopwa hata na mbwa wa pale kijijini!
Alimshukuru Mungu kwa kumuepusha na msala ule,amfuata yule mzee nyuma bila kujua wanaenda wapi?
Safari ilikuwa ya lisaa lizima mwisho wakatokea makaburini na safari ikawa imeishia hapo,Lukas alibaki ameduwaaa,hakuwaza kama tiba yenyewe ni kupelekana makaburini!
“Kijana ulitaka tiba,sasa utalala kaburini siku tatu,kisha nitakuja kukutoa,kule ulikofanya utakuwa mpya,tutakuwa tumeyazika mambo yako yote na utakuwa mpya!”
Lukas alibaki anatetemeka kwa hofu kubwa,kitendo cha kuambiwa alale kaburini ulikuwa mtihani mkubwa kwake!
“Kwa…kwani hamna tiba nyingine?”
“Uliniambia nikutibu kumbe unaweza kujitibu,jitibu basiii!”
“Haa…hapana mzee tuendelee!”
Mzee Mtata alisogea karibu kaburi moja la zamani sana alipofika alichukua kibuyu ambacho kilikuwa na maji meusi!
Aliulowanisha usinga wake akaanza kuyarusha yale maji huku anaongea kwa lugha ambayo aliielewa mwenyewe!
Baada ya muda lile kaburi lilianza kutoa moshi mweusi,akaendelea kusema lugha zake mpaka ukatoka moshi mwekundu,akaendelea tena mpaka ukaja moshi mweupe!
Moshi mweusi wa kwanza ulimaanisha kuwa maiti iliyozikwa pale alikuwa imekasirika na kama angeacha na kuitoa muda ule ingewadhuru,na ule moshi mwekundu ulimaanisha kuwa sasa haina hasira ila inataka damu,kwahiyo ingetoka muda ule,ingeenda kijijini na kudhuru watu!Lakini ule mweupe wa mwisho ulimaanisha kuwa sasa amani ipo,mzimu hautakuwa na fujo!
Baada ya ule moshi mweupe kutoka mzee Mtata alisita kusema akanyamaza,ghafla kaburi lile likafunguka na jeneza likajileta juu lenyewe!
Mzee Mtata aliendelea kulirushia jeneza maji kwa usinga wake mpaka likafunguka ikaonekana maiti iliyokuwa imefungwa sanda!
Mzee Mtata aliita kwa jina lake ikaanza kuamka mpaka ikasimama na kutoka ndani ya jeneza!
Lukas haja kubwa iligonga hodi achilia mbali mkojo ambao ulikuwa umepita kabisa alikuwa anatetemeka kama katoka kulala ndani ya friji!
“Samahani ninakupa matembezi ya siku tatu,nataka kijana wangu atumie kitanda chako,alale kwenye nyumba yako kwa siku tatu,baada ya hapo utarudi nyumbani kwako tena,ila usidhuru watu sababu sitakuja kukupa matembezi tena!”
Ile mzimu ulikuwa umesimama tu hausemi chochote,Mzee Mtata aliusogelea akaupiga na usinga kichwani akauamrisha ukaondoka taratibu kwa mwendo wa kizombi mpaka ukapotelea kizani!
Akamgeukia Lukas ambaye alikuwa anatetemeka kwa hofu,akaanza kumsogelea alitaka kukimbia lakini alimchapa usinga kichwani akabaki kaduwaa!
Kuanzia hapo ikawa kila anachoambiwa anatii bila shuruti,kiufupi ni kama Mzee Mtata alimchota akili zake na kumfanya zuzu kwa muda!
Mzee mtata alisogea kwenye lile jeneza akalifanyia dawa zake kisha akamgeukia tena Lukas ambaye alikuwa kasimama kama sanamu!
“Ingia humo,usifanye fujo kwenye nyumba ya watu kama king’amuzi kimeisha umnunulie sawa!”
“Sawa mzee!”
Bila uoga Lukas aliingia kwenye jeneza likajifunga kisha taratibu likaanza kuingia kaburini kisha kaburi likajifukia na kuwa kama hamna chochote kilichotokea!
Baada ya kumaliza kufanya yake ,mzee Mtata aliondoka na kumuacha Lukas kaburini,ambaye haikujulikana atatoka mzima au lah!
*******
Mama Zubeda alishangaa kutokumuona Lukas,mwanzo alijua kuwa amelala lakini kadri muda ulivyokwenda ndivyo wasiwasi uliongezeka!
“Selina ebhu kamuangalie Lukas humo ndani!muamshe mbona kalala sana leo!”
“Subiri nikamuamshe mimi”,alidakia Johari mpaka kila mtu akabaki anamshangaa!
“Kulikoni unataka ukamtie makofi mkaka wa watu huko eeh!”,alisema mama Zubeda hakumuamini kabisa Johari sababu anamchukia sana Lukas,bila kujua Lukas alishambadilisha sasa anampenda kufa!
Johari alirudi na majibu kuwa Lukas hakuwepo!walijuliza kaenda wapi?Waliamua wavute subira pengine atarudi lakini mpaka jua linazama Lukas hakutokea!
Siku ikapita Lukas haonekani,ndipo kesho yake Mama Zubeda aliamkia kwa mzee Mtata kujua tatizo ni nini?
Alifika na kumkuta Mzee Mtata kilingeni kajaa tele,alipomuona tu akatabasamu akamkaribisha kwa bashasha!
“Mzee mdogo wangu haonekani,usinambie umemchukua tena!”
“Lakini hukutimiza matakwa yetu,au umesahau mpenzi?”,Mzee Mtata aliamua kutumia fursa!
JE NINI KITAENDELEA?MAMA ZUBEDA ATAKUBALI KUMPA MZEE TIGOPESA?
Chombezo………….BAO TATU ZA MGENI!
Mtunzi……………….Jack Mambo
Whtsp………………..0752761388
Call…………………….0716352102
Umri…………………..18+
Sehemu ya 48
Mzee mtata hakuwa amemchukua Lukas kama kipindi kile,tatizo Lukas hakuwa ameaga nyumbani na alifanya ivyo akiamini angerudi siku ile,hakujua kama atalazwa ndani ya kaburi siku tatu!
Mzee Mtata hakuwa na mpango na ahadi aliyowekeana na mama Zubeda kipindi kile,alikuwa ameshaipotezea,ila alipomuona kaja pale kisa hamuoni Lukas nyumbanui na yeye akaamua kuitumia ile kama fursa!
Akakubali kuwa amemchukua Lukas kimazingara kwa sababu hakutimiza ahadi yao waliyokuwa wamewekeana!
“Kwahiyo unamtesa mtoto wa watu sababu ya hiyo kitu kweli mzee Mtata!”,alihoji mama Zubeda!
“We unaona kidogo icho?”
“Lakini si tufanye kawaida tu kwani lazima mpaka unifanye huko jamani?”
“Usivunje ahadi!”
Mzee yule aliamka bila aya na kuanza kumpapasa Mama Zubeda,hakuwa na haya alitaka kufanya uchafu ule palepale kilingeni bila kujali kama mizimu ingekasirika!
“Mzee Mtata subiri,subiri kwanza naomba nikuahidi kuwa ukimuachia safari hii nakupa unachokitaka!”
“Una uhakika?”
“Ndiyo ila hatutofanyia hapa mi naogopa matunguli yako,tutakutana kule kwenye shamba lako!”
“Sawa nitamrudisha kesho kutwa,atakuwa mzima mwenye afya na nguvu kuliko mwanzoni!”
Walikubaliana ivyo huku ikiwa ni janja ya yule mzee akiamni atamtoa kaburini Lukas baada ya siku tatu!
Mama Zubeda aliondoka huku akijilaumu kwanini hakumpa yule mzee anachotaka mapema,yasingetokea yale,bila kujua Lukas alikuwa anatibiwa ili arudi mjini!
********
Lukas alikuwa kama yupo kwenye ndoto nzito sana,usingizi ulimchukua na kuota ndoto zenye kutisha!
Maisha yake kaburini yalitawaliwa na ndoto zenye kutisha,aliota mara nyingi wale aliowakosea wanamkimbiza na mapanga!
Alikuwa naweweseka sana,jasho lilimtoka lakini cha ajabu alikuwa anapumua vizuri tu ila macho hayakufumbuka!
Zilikuwa ndoto zenye mateso makubwa,kukimbia huku na kule akitetea maisha yake,hayo ndiyo yalikuwa maisha yake ya ndotoni
********
Kijiji kilipata ugeni wa ajabu!ile mzimu uliofukuliwa na mzee Mtata ulianza kuleta ghasia kijijini!ulianza kuvamia nyumba za watu usiku wakiwa wamelala na kufanya mapenzi na mabinti!
Ilifikia hatua kila binti anaamka akiwa amebakwa,ulikuwa unatembea nyumba hata ishiruini na kufanya mapenzi na wanawake hata ishirini kwa usiku mmoja!Ulikuwa na moto Lukas anasubiri!
Wanawake walianza kulalamika juu ya mgeni yule wa ajabu,wengine walianza kukutana na ule mzimu maporini ukiwa unatembea!
Mashtaka yalizidi mzimu ulikuwa unatembeza dozi kama haina akili nzuri,viongozi wa kijiji ilibidi wakae wajadiliane juu ya mgeni yule wa ajabu!
“Jamani hii ni aibu,inauma ila niseme tu jana sijamgusa mkewangu ila asubuhi kaamka ananiuliza kama nimefanya naye mapenzi,acha huyo tu binti zangu wawili nao jana hiyo hiyo wamefanya mapenzi usiku na hicho kiumbe!”,alilalamika mjumbe wa kijiji!
“Jamani mimi kama mwenyekiti naona hili suala limekuwa zito sana!Na haliwezi kutatuliwa kisheria!”
“Sasa tufanyeje?”,aliuliza mjumbe!
“Mimi nina wazo!”
“Wazo gani?”,waliuliza kwa pamoja
“Kwanini tusimfuate mzee Mtata atusaidie kumaliza hili jambo,mnakumbuka zamani kuna kipindi ilishawahi kutokea maiti inatembea akairudisha,japo ile haikuwa kama hii!”;
“Wazo zuri naona twendeni sasa ivi!”
Wazee walijikusanya na kuanza safari kuelekea kwa mzee Mtata ambaye kwa asilimia zote anahusika na usumbufu wa ule mzimu,sababu ndiyo aliifukua na kumlaza Lukas!
Ule mzimu ni kama ulibadilishana makazi na Lukas,baada ya kufanya mizunguko yake yote na kutembeza bakora kijijini ulikuwa inarudi kwenye kijumba cha Lukas unalala!
Hakuna aliyejua sababu ilikuwa inalala chini ya kitanda!Na kingine ilitembeza bakora nyumba zote ila haikugusa nyumba ya mzee Jomo sijui kwanini!
Wazee walifika na kumkuta mzee Jomo kilingeni hana habari anavuta zake kiko,habari za mzimu wala hakuzisikia popote,kiufupi hakuwa na habari!
Ugeni ule ulimshtua sababu viongozi wote waliongozana,aliwakaribisha wakaketi kisha wasalimiana,wote walimuheshimu mzee yule mwenye sifa zake za utata pale kijjini!
“Mzee mwenzangu sijui una habari!”,mwenyekiti alifunguka!”
“Habari gani tena!”
“Kuna kiumbe kinabaka wanawake usiku,yaani kinazunguka kila nyumba na kufanya ufusika sijui utatusaidiaje!
Mzee Mtata alipopata habari zile alijua moja kwa moja ni mzimu aliyoufukua tu ndiyo unayoleta matatizo!
“Mnataka nifanyeje?”
“Kikamatwe na kidhibitiwe ikibidi kirudi kilipotoka!”
“hahahahahahahahahaha!”
JE NINI KITAENDELEA?MZEE MTATA ATAFANYAJE?
Chombezo………….BAO TATU ZA MGENI!
Mtunzi……………….Jack Mambo
Whtsp………………..0752761388
Call…………………….0716352102
Umri…………………..18+
Sehemu ya 49
Habari zile zilimshtua sana Mzee Mtata ila hakutaka kuonyesha hofu mbele ya viongozi wale wanaomwamini,kwa mara ya kwanza alianza kuhisi vitu vya tofauti,haikuwezekana hata kidogo mzimu aliyoufukua ufanye fujo namna ile!
Kuna kitu alianza kuhisi hakipo sawa,aliwaza kuwa atalifanyia kazi baadae!Ila vilevile alitaka kuitumia ile kama fursa!
Mzee Mtata aliwaza mali kwa tatizo alilolitengeneza mwenyewe!alikohoa kidogo kisha akawaangalia wale viongozi!
“Nitawasaidia ila nahitaji ng’ombe kumi na mbuzi watano!”
Wale viongozi waliangaliana malipo aliyotaka yalikuwa makubwa sana,ila hawakuwa na namna baada ya kimya kirefu mwenyekiti alifunguka!
“Kutokana na hili jambo lilipofikia mimi naona tutakupatia unachotaka ila tafadhali fanya mapema sana!”
“Sawa kesho nitaukamata huo mzimu!”
“umejuaje kama ni mzimu?”,mwenyekiti alishtuka kusikia mzee anasema ni mzimu na huku hajauona!
“Mimi ni mganga ujue,na usisahu wananiita mzee mtata!”
“Samahani ivi unamaanisha mkewangu alilala na mzimu na binti zangu pia?”
“Hhahahahahahaha!walibakwa siyo kulala!”,alijibu mzee Mtata!
Yule mjumbe aliinama chini kwa aibu,aliwaza mengi kitendo cha kusikia eti anayetembeza bakora ni maiti kilimchefua sana alihisi kinyaa!
Waliondoka na kumuacha mzee Mtata ambaye aliwataka kesho yake wapige ngoma kijiji kizima wakutane uwanja wa kijiji!
Siku ile ndiyo ilikuwa siku ya kumtoa Lukas aliyetimiza siku tatu kaburini,alijiandaa na kuweka vifaa vyake tayari kwa kazi ile ya usiku wa manane!
Alipanga amtoe Lukas ila maiti auache uendelee kutoa dozi mpaka alipwe ng’ombe kumi na mbuzi watano ndiyo aurudishe!
************
Siku ya tatu ilitimia Lukas akiwa kaburini kwenye usingizi mzito,,kadri siku zilivyokuwa zinasogea ndivyo hali ya ndoto zenye kutisha iliongezeka!
Alikuwa anaweweseka sana,watu aliowakosea walikuwa wanamkimbiza na siraha kali sana kama mapanga marungu,visu,mikuki nk!
Ilifikia sehemu akachoka kabisa ,alikimbizwa akafika sehemu hakuna njia,maadui zake walimfikia wakaanza kumpiga na kumchoma visu,wengine walimkata mapanga wakamchoma mkuki!
Kipigo kilizidi nguvu zikamuishia,alivuja damu kila kona,mwisho kabisa mmoja alikuja na jiwe akalinyanyua akilielekeza kichwani!
“Msiniueee!msiniueeee!”
Kelele zake hazikufua dafu yule aliebeba jiwe aliliachia Lukas akaliona linakuja kichwani alipiga kelele!
“Mamaaaaaaaa!”
Alipiga kelele lakini alishangaa jeneza linafunguka akajikuta yuko nje ya kaburi,alimuona mzee Mtata kasimama na usinga wake mkononi!”
Alianza kujikagua akijiangalia kama ana alama ya vitu,lakini hakuhisi maumivu sehemu yoyote ile!Alikumbuka lile jiwe lililotua kichwani,akajishika kichwa lakini hakikuwa na tatizo!
“SIJAFAAA!”,alishangaa sana Lukas!
“UMEKUFA MIOYONI MWAO!”,alijibu mzee Mtata!
“Unamaanisha nini?”,aliuliza Lukas huku anatoka ndani ya lile jeneza!
“Wamekuua kwenye mioyo yao,sasa utakuwa huru kwani ulishaona kuna mtu anaidai maiti?”
“Hapana!”
Mzee Mtata alilirudisha kaburi lilivyokuwa,jambo lile lilimshtua sana Lukas,maana alijua kabisa alitakiwa akitoka yeye kaburini ile mzimu urudi!
“Mzee ile maiti iko wapi?”
“Nina kazi nayo ila iwe siri yako kwa chochote kitakachotokea!”
“Sawa!”
Lukas hakujua mzimu umeliamsha dude kijijini untembeza bakora kama ukwaju wa bakhresa!
“Tuondoke!”
Safari yao iliishia nyumbani kwa mzee Mtata,waliingia kilingeni mzee akaanza upya kufanya mambo yake!
“Kijana!”
“Naam!”
“Sasa nataka nikupe kinga,kinga ambayo itakukinga na uchawi wa aina zote hata majini watakuogopa,hakuna atakayeweza kukuloga hata mimi pia!Sijawahi kumpa mtu hii kinga ila kwa kuwa nimekuona ni kijana mzuri basi nakupa hii kijana,ila usiitumie kuwadhuru watu!”
Machozi yalimtoka Lukas,yule mzee alionekana kuwa mwema sana kwake,alijuta kwanini alitembea na wake zake!
Baada ya kumpatia ile kinga alimruhusu akamwambia akalale kwenye kile kijumba,lakini Lukas alisema anaondoka nyumbani!
Hakutaka kulala pale sababu aliwahofia wake wa mzee Mtata wanaweza kumvamia,njiani wakati anarudi alishangaa baada ya kupishana na ile mzimu ukiwa na sanda!
Kwa ujasiri aklianza kuifuatilia kwa nyuma mpaka ikaingia kwenye nyumba moja hivi,liashangaa baada ya kuchungulia na kuiona inamvua nguo mdada mmoja kisha nayo ikatoa bakora tayari kwa kumuingilia,Lukas hakukubaliana na lile jambo akataka apambane na ile mzimu!
JE NINI KITAENDELEA?MASU ATAWEZA KUPAMABNANA NA ILE MAITI?
Chombezo………….BAO TATU ZA MGENI!
Mtunzi……………….Jack Mambo
Whtsp………………..0752761388
Call…………………….0716352102
Umri…………………..18+
Sehemu ya 50
Maneno ya Mzee Mtata yalimjia kichwani kuhusu kinga aliyopewa,akajiona ni kama anaweza kupambana na ule mzimu!
Alimuonea huruma yule binti aliyekua kalala hajitambui huku mzimu ukifanya naye mapenzi,Lukas alishikwa na huruma pia wivu ulimkaba maana alikuwa anakula binti mrembo hatari!
Aliujua ule mzimu ni ule uliyofukuliwa ili yeye apate tiba,akakumbuka jibu alilopewa na Mzee Mtata kuhusu ule mzimu!
Mzee alisema ana kazi nao Lukas aliwaza labda ile ndiyo kazi yenyewe ile,alikumbuka pia aliambiwa afiche siri!
Nguvu zilimuishia akajikuta kaganda kama sanamu akishuhudia jinsi ule mzimu inavyosukuma kiuno chake kwa pupa!
Baada ya muda kama dakika ishirini ilimalizana na yule binti ikarudisha bakora yake kisha ikaondoka,cha ajabu ulimuona kabisa Lukas lakini haukuwa na muda naye,ni kama ulikuwa unamfahamu!
Lukas aliufuatilia tena ukazama kwenye nyumba nyingine kutoa dozi,aliufuatilia mpaka akachoka maana ulikuwa unatembeza dozi balaa!
Lukas alichoka akaamua kwenda zake nyumbani,alifika akaingia kwenye kijumba chake akaanza kutafakari!
Alikumbuka sana maisha ya mjini,akakumbuka vitu alivyoacha na kukimbilia kijijini kisa wanafunzi na wake za watu!
“Ivi sitakamatwa kweli?”
Alijiwazia bado hakuamini sana kauli ya mganga,hakutaka kuyaamini maneno ya mganga moja kwa moja!
Usingizi ulimchukua mpaka aliposhtuka baada ya kusikia kama kuna mtu mle ndani,hakuamini baada ya kuuona ule mzimu,wazo lililokuja ni kuwa mzimu unataka kumuambaruti!
“We vipi humu hakuna mwanamke!”
“Ina maana hunisikii?nimesema humu hamna mwanamke!”
Mzimu haukuwa na mpango naye uliingia chini ya uvungu ikalala zake,akabaki Lukas ana wasiwasi mkubwa!
Usiku ulikuwa mrefu sana kwake,aliogopa kulala akiamini mzimu utamfanyia mchezo mbaya!
Usigizi ulikuja ukamchukua akalala,alikuja kushtuka asubuhi kumekucha,kitu cha kwanza aliinama akaangalia uvunguni hakuona chochote!
Ule mzimu ulikuwa umeshaondoka,haraka akajishika ili ajue kama mzimu ulimfanyia mchezo mchafu,lakini alijikuta mzima malinda yalikuwa salama!
“Eeeefuuuuuuuuuuh!”
Aliivuta pumzi ndefu akazishusha,aliinuka akatoka nje akamkuta mama Zubeda anaandaa vifaa vyake aingie kukamua maziwa!
“Wow Lukas umerudi!”
Mama Zubeda alishindwa kujizuia akaweka chini vitu vyake akamkumbatia kwa furaha,bahati ilikuwa kwao sababu wanae walikuwa bado wamelala!
“Hey watatuona!”
Alisema Lukas akajitoa kwenye mikono ya Mama Zubeda,mama Zubeda akaona isiwe tabu alimshika mkono akamrudisha kwenye kijumba chake,humo akaanza kumpiga mabusu mfululizo!
Mama Zubeda alishindwa kuvumilia alijikuta anataka penzi asubuhi ile jambo ambalo Lukas hakutaka kukubaliana nalo!
“No!siyo saivi tutakutwa!”
“Nipe kidogo bhanaaaa!”
“Hapanaaa!”
Mama Zubeda aliambulia manyoya kwa Lukas,alimkazia akiamini si muda sahihi wa kufanya vile,kwa mara ya kwanza Lukas akajifunza uchoyo!
Mama Zubeda alitoka kishingo upande mpaka zizini akaanza kukamua ng’ombe,akili yake ilikuwa mbali sana!
Alijua kurudi kwa Lukas kunamaanisha nini?Aliikumbuka ahadi yake na Mzee Mtata anayeyataka malinda yake ili Lukas awe salama!
“Huyu mzee jamani,hivi kweli anataka kuniambaruti jamani kisa Lukas,Lukas mwenyewe ananipa kwa masharti wakati malinda yangu yako hatarini hapa!”
Familia nzima iliamka na wote walifurahi uwepo wa Lukas,sasa hata Johari alikuwa anampenda Lukas,alibadilika mpaka wenzake wakawa wanamshangaa!
Lukas alifurahi sana kumuona Selina,maana kati ya wote pale mahaba yake yalikuwa kwa Selina!
Alikuwa ameshaanza kuwaza kuondoka kijijini arudi zake mjini,maana alikuwa na uhakika kabisa kwa tiba aliyopewa na Mzee Mtata hakuna atakayemgusa mjini!
Kutokana na mahaba aliyokuwa nayo kwa Selina aliwaza akiondoka aondoke naye,tatizo lilikuwa je atakubali?
********
Ngoma ilipigwa kijijini ikiwataka wanakijiji wote waende kwenye uwanja wa kijiji kumshuhudia mzee Mtata akimkamata anayebaka wanawake usiku!
Zilikuwa ni habari njema sana kwao,wote walikusanyika uwanjani kumshuhudia huyo anayebaka watu usiku!
Mzee Mtata tayari alikuwa uwanjani na vifaa vyake,tayari kumtoa huyo anayesumbua kijini,Lukas naye alikuwa uwanjani tayari!
Lukas alijua kabisa ile ni janja ya mzee Mtata ambaye ndiye aliyeufufua ile mzimu ili kumtibu yeye,lakini sasa anautumia ili kupata mali,ilimbidi kukaa kimya kuitunza siri ile!
Mzee Mtata alianza kufanya yake,aliongea lugha zake huku watu wanasubiria maajabu!
INAENDELEA
Shauku ilikuwa kubwa sana kwa wanakijiji,kuna waliobakiwa wake zao pia binti zao!kijiji kilikuwa na hasira sana!
Mzee Mtata alisimama kabla hajamleta hadharani alitaka kutoa onyo kwa wanakijiji wale ambo walionyesha hasira za waziwazi!
“Jamani mnataka nimtoee?”
“Ndiyooooo!”,waliitikia kwa pamoja!
“Mnata mumuone mchumba wenuuuu?”,alitania lakini hapo wanakijiji walikaa kimya!
“Hahahahahhaha!natania jamani!sasa nisikilizeni namtoa hadharani anayesumbua kijiji hiki,lakini chonde msimguse wala kumpiga,atakayemgusa ajue atakuwa anatembelewa kila siku na huyu mgeni awe mwanaume au mwanamke!”
Mzee Mtata ilibidi awatishe maana walikuwa na hasira za wazi wazi kabisa,baada ya kusikia vile wanakijiji waliogopa sana!
“Jamani tumeelewanaaaa!”
“Ndiyooooo!”
“Hamtamgusaaaaa?”
“Ndiyooooo!”
“Shauri yake atakayemgusa sitamtibia!”
Baada ya kutoa vitisho Mzee Mtata alichora duara kubwa kwa majivu kisha akaweka dawa zake akachukua kibuyu chake akaweka maji mdomoni na kuanza kuyapuliza juu!
Alipomaliza alianza kuuita ule mzimu ambao ghafla ulitokea kwenye lile duara huku unatetemeka na kuzunguka ndani ya ile duara!
Wanakijiji walipigwa na butwaa,kilikuwa kiumbe kinachotisha sana,wanawake waliokuwa wamehisi kufanya mapenzi na kile kiumbe walipatwa kichefuchefu wengine hadi wakatapika!
“Mmemuona eeh,ndiyo huyuuu!sasa namrudisha alipotoka hamtamuona tena kijijini,mimi ndiyo mzee Mtataaa!”,alisema huku anajipiga kifuani!
0 Comments