Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Responsive Advertisement

Chombezo:Bao tatu z mgeni sehemu ya pili (02)

 “Hivi Regina!”

“Rabeka!”

“Kuna kitu nataka nikuulize!”

“Kitu gani kaka halafu hujaniambia unaitwa nani?”

“Naitwa Jack Mambo!”

“Mmh aya unataka uniulize nini?”

“Oooh!nataka kujua kuna nini kwenye hiki kijiji mpaka wageni hawapokelewi vizuri?”

Swali lile lilimfanya Regina ainame chini na uso wake ukabadilika,ghafla akainuka akaacha kula na kuondoka!

Nilibaki njia panda yule mzee kasikia wageni kainuka akaondoka,Regina naye hataki kusema chochote,kuna nini katika kijiji hiki?wageni walikosea wapi?


Safari yangu ilikuwa ni kufanya utafiti wa kitabu changu lakini sasa shauku kubwa niliyonayo ni kujua siri iliyopo kati ya wageni na hiki kijiji!Nilitaka kujua kwanini wageni hawapokelewi vizuri katika kijiji hiki?Kwanini wageni wanachukiwa hapa!

Baada ya Regina kuacha kula na kungia ndani kisa nimemuuliza kuhusu mgeni,nilimfuata ndani nikamkuta kakaa kitandani kainama analia kwa sauti kubwa mpaka nikaogopa!

“Regina una nini?mbona unalia?”

“Dada yanguJack,pengine hasingekuja mgeni hapa ningekuwa na dada mimi!”

Kauli yake ilianza kunipa picha kidogo kuhusu mgeni,japo sijajua mgeni alikuwa muuwaji au alikuwaje!

“Kwani Regina kuna nini?mbona sielewi?”

“huwezi kuelewa niache Jck siko sawa!”

Nilimuacha Regina nikatoka zangu nje,nikiendelea kuangalia mazingira mazuri ya Sumbawanga,hakukuwa na joto kubwa kama la Dar,hali ya hewa iliruhusu kabisa kuujaza ulimwengu!

Nilichukua kiti nikakaa nikiwa na mawazo yangu kichwani,kwenye ule mji kuna njia ya watu kupita kwenda kisimani,nilidhani nimeshaona wanawake wazuri kumbe nilikosea aiseeh!

Kuna mabinti walipita wanaenda kisimani aiseeh!nilijiuliza sana kile kijiji kina nini?mbona kina warembo namna hii,mabinti wale walipita huku wakionyesha kunishangaa sana!

Regina alitoka ndani akanikuta nimekaa pale,akanisogelea akaniambia…..

“Kaka Jack usipende kukaa nje wageni wanachukiwa kwenye hiki kijiji,wanaweza wakakufanyia kitu kibaya!

“Kwani kuna nini Regina mbona unanitisha sasa!”

“Sikutishi nakuambia ukweli chukua tahadhali,wageni waliacha vita kwenye hiki kijiji ,wageni ni maadui wa hiki kijiji!”

Kauli yake ilinifanya nisimame ili niulize maswali kadhaa kuhusu uadui wa kile kijiji na wageni!

“Unasema wageni ni maadui?kivipi?”

“Ni historia Jack!”

“nisimulie tafadhali!”

“Ntakusimulia kesho maana tukianza asubuhi tutamaliza jioni au kesho yake asubuhi!”

“mmh!”

Niliishia kuguna Regina akaendelea na mambo mengine,niliingia ndani nikakaa maana tayari Regina alishanitisha kuhusu kile kijiji!

Niliingia mitandaoni nikaanza kukagua stori zangu nikipitia huku na kule kusoma komenti za wadau mwisho nikaposti stori nikatoka!

Mtandao ulikuwa chnini sana hivyo sikuweza kukaa sana mtandaoni,usingizi ulinichukua nikalala mpaka Regina alipokuja kuniamsha mchana kula!

Niliamka nikala nikarudi ndani tena,jioni alikuja Mzee wa ukoko akatukuta tumekaa nje tunaota moto!

Tulisalimiana kisha Regina akaingia ndani na kutuacha wawili,mimi na mzee wa ukoko!

“Kijana!”

“Naam!”

“Unatokea wapi?”

“nimetokea Dar!”

“Unaonekana mstaarabu sana kijana!”

“Kwanini mzee wangu?”

“Hhahahahah!kijana mimi ni mtu mzima najua kutofautisha maziwa na chokaa!”

Tuliendelea kupiga stori za hapa na pale huku akinipa majibu ya maswali yangu kuhusu kile

kijiji,japo sikumuuliza tena suala la wageni sababu nilihofia kumkwaza!

Yule mzee alikuwa mcheshi sana alitaka kuzivunja mbavu zangu,stori zake hasa za ujana ziliniacha hoi kwa kicheko!

Regina alileta chakula tukala,kisha mzee akaniambia kauli ile ile ya jana hapo nikachoka zaidi!

“Kijana utalala na binti yangu leo pia,kumbuka masharti ni yaleyale usimguse mimi nalala na mama yenu leo!”

Niliinama chini nikashika kichwa bado sikujua kwanini yule mzee ananifanyia vile,niliwaza pengine ananitega aniue!

“Huyu mzee anataka nikosee masharti aniloge huyu siyo bure kabisa!”

Niliinuka nikaenda kwenye kijumba cha Regina nikiwa nimenyong’onyea hadi akanishtukia.

“Vipi kuna nini?”

“Hivi Regina kwanini baba yako ananilaza huku ananitakia nini?”

“Kwani unaogopa!?”

“hivi we unaona kawaida?ujue wewe mwanamke mimi ni mwanaume itakuwaje?”

“Usiwaze Jack wewe lala kama jana tu,baba ana kidemu chake siku hizi kinakuja usiku tuu kwahiyo usiwaze!”

“Ikitokea nimeshindwa kuvumilia Regina itakuwaje?”

Swali lile lilimfanya Regina aangalie chini kwa aibu muda huo na mimi hisia zimenikaba,bakora ikasimama,mpaka hapo nilihisi nafeli kabisa maana kwa jinsi tulivyokuwa karibu nilijikuta natamani kumkumbatia Regina!”

“Jack usiwaze ujinga lala kesho nikupe stori unayoitaka,maana najua hiki sicho unachotaka kwangu!

Ni kama masikio yaliziba nikamsogelea karibu zaidi Regina,mpaka nikagusana naye,bakora yangu liyokuwa imesimama ikamgusa huku chini akashtuka!

“Jack ni nini hiyo?”




Regina alishtuka baada ya bakora yangu kumgusa huku chini,aliruka pembeni akaangalia usawa wa zipu yangu!

“Jack nini hiyo,ayaaaa umedindisha!”

Nilitoka nje haraka maana nilihisi kuna kitu kibaya kitatokea ambacho kinaweza kuniweka matatizoni!

Nilichukua kiti nikakaa nje nikisubiri hisia zitulie ndiyo niingie ndani,wakati niko pale nilimuona Mzee wa ukoko akiingia kwenye kijumba chake na mwanamke ambaye sikumuona vizuri kutokana na giza lililokuwepo,japo nilifanikiwa kuona kwa nyuma alikuwa amejaliwa haswa!

Nilitamani kwenda kupiga chabo ila nilipokumbuka kule ni Sumbawanga niliishiwa pozi,nisije nikapofuka macho bure!

Nilijizoa zoa mpaka ndani nikamkuta Regina ameshalala muda huo na mimi bakora imetulia nikalala bila tabu,huku nikijitahidi kuyazuia mawazo mabaya!


Kulikucha asubuhi siku hiyo niliamka mapema nikamuacha Regina amelala,hata mzee wa ukoko alikuwa bado amelala!

Niliwasha moto nikaanza kuota ndipo mzee wa ukoko akatoka akijinyoosha,alishangaa sana kunikuta nje muda ule!

“Hahahahaha kijana wa mjini mbona mapema sana leo!”

“Sina usingizi mzee shikamoo!”

“Marahaba kijana,au umemkimbia binti yangu kijana?”

“Hahahahah hapana mzee yule ni dada yangu!”

“hahahaha kijana unanichekesha sana hahahaha ngoja nifuate viazi tuchome!”


Mzee wa ukoko alizunguka nyuma ya nyumba akarudi na viazi tukaanza kuchoma huku tunapiga stori za hapa na pale!

Alipomaliza alinichukua mpaka kwa mwenyekiti wa kijiji kuitambulishwa,cha kushangazwa niluliza nakaa siku ngapi?

Swali lile lilinishangaza sana yani kama niko marekani jamani hiki kijiji kiboko,niliwaambia siku tatu tu,yule mzee alinichukua tukarudi nyumbani!

Mwisho aliondoka zake akaniacha pale,Regina aliamka akanikuta nipo natafuna viazi vya kuchoma!

“Mbona hujaniamsha jamani?”

“Usimuamshe aliyelala utalala wewe!mbona hata wewe jana hukuniamsha”

“Ulipaswa kuniamsha mapema nichemshe uji tunywe nikusimulie simulizi ya mgeni!”

“Kuna viazi nimechoma vingi uji siyo lazima kaa hapa unisimulie!”

Regina alikaa pembeni akachukua kiazi akaanza kula huku ananiangalia sana machoni mpaka nikajiuliza kulikoni?

“Vipi mbona unanitazama kiasi hicho?”

“Jack!”

“Naam!”

“Unataka stori ya mgeni?”

“Ndiyo!”

“Nambie kwanza jana ulinigusa na nini huku chini!”

“Regina ebhu acha hizo stori ujue niko Sumbawanga hapa,nasikia na Gamboshi iko huku usije ukaniponza!”

“Hhahahahahah!unaogopa kuwa msukule!”

“Usicheke Regina tuache hizo stori!”

“Sawa aya nianzie wapi kusimulia?”

“Anzia mwanzo kabisa!”

“Sawa ila hii simulizi ya mgeni hii ina tabu kweli ujue!”

“tabu gani?”

“Unaweza ukanibaka hapa?”

“Siwezi bhana siyo rahisi kiasi icho!”

“Unasema tu mi mwenyewe wakati nasimuliwa hii stori nilijikuta natoa mwenyewe,na ndiyo siku niliyopoteza bikra yangu!”

“Ulitaka bhana huwezi toa bikra kisa stori!”

“Nilikuwa mbishi kama wewe,ila kabla stori haijaisha nilivua nguo mwenyewe nikachanua miguu msimuliaji akachukua akaweka waaah!”

“Hhahahaahhaahaha!unanichekesha ujue iyo si nyimbo ya Diamond hiyo?”

“Ndo nakuambia sasa alichukua akaweka waah!nilishtuka bakora iko ndani navuja damu maumivu kama yote!”

“Aya niahidi hutonibaka!”

“Unazingua ujue mi sikubaki bhana nisimulie usijali!”

“Sawa,ila ujue hata msimuliaji anaweza kubaka pia!”

“Regina nihadithie bhana achana na hayo mambo!”

Regina alianza kula kiazi chake akashushia na maji,kisha akakohoa kurekebisha koo ili anisimulie,ni kama aliweka utani mwingi maana alinyanyuka akakaa kama anataka kupiga push up!

“Sasa ndiyo nini ivyo Regina!”

“Weee! Unadhani simulizi ya mgeni ya mchezo ngoja nipashe misuli nikupe hadithi we mkaka wa mjini!”

“Dah!sasa hadithi mpaka uipigie push up kweli jamani?”

“Unataka hadithi hutaki?”

“Nataka!”

“Aya kaa kwa kutulia!”





Waasema mtaka cha uvunguni sharti ainame,ndicho kilichotokea kangu,stori ya mgeni aliyeleta utata kijijini niliitaka sana,ivyo ilinibidi niwe mpole!

Regina alifanya upuuzi wake akamaliza akaketi kisha akaniangalia usoni akasema

“Sasa nakupa hadithi ya mgeni,ila chonde usinibake maana tupo wawili tu hapa bora baba angekuwepo!”

“Regina bhana nilishakutana na kina chausiku sikuwabaka kina kidawa na mwisho Lisa sembuse huyo mgeni?Nipe stori mimi acha uoga!”

“Sawa napenda watu wanaojiamini kama wewe!”

“Leta mambo!”


*********


Miaka kumi iliyopita kijiji chetu kilimpokea mgeni,mgeni ambaye aliacha majonzi makubwa kijijini,mgeni ambaye ameziba kabisa milango ya wageni kupokelewa katika kijiji chetu!

Ilikuwa usiku kama saa mbili siku hiyo ilikuwa inanyesha mvua kubwa sana,wenye nyumba za bati walikuwa bize wakikinga maji safi ya mvua,maana kama unavyoona kijiji chetu tunatumia maji ya kisimani!

Mzee mmoja maarufu kama mzee Jomo alikuwa ndani na familia yake,wao maji ya mvua yaliwapita sababu hakuwa ameezeka nyumba yake kwa bati!

“Unaona sasa mume wangu tungekuwa na bati tungekuwa tunafaidi maji ya mvua hapa!”,alisema mke wa mzee Jomo!

“Mkewangu wewe subiri yani safari hii nikiuza mpunga wangu najenga nyumba kubwa sana hapa naezeka na vigae kabisa sitaki bati mimi!”

“Baba muogope Mungu na huku ukiuza tu unaoa hapa nyumbani huonekani pesa zote kwenye pombe!”,alisema binti mkubwa kati ya mabinti zake wanne alionao,Mzee Jomo mpaka alipofikia hajabahatika kupata mtoto wa kiume,alishawahi kujaribu kuchepuka akampa mimba mwanamke mwingine lakini napo akapata mtoto wa kike!

“Mwambieni baba yenu!Mi nishamaliza maneno yote na safari hii akiuza mpunga akakimbia hasirudi hapa anakuta nami nimeolewa!”

“Haahhahahahahah mamaaa acaha kutuchekesha!”

Mabinti wa mzee Jomo walicheka kwa pamoja,kauli ya mama yao iliwachekesha sana,Mzee Jomo hakuwa mkali sana kwa familia yake kiasi kwamba hata mabinti zake hawakuwa wanamuogopa kiivyo!

“Mnacheka kwa hiyo mnasapoti upuuzi wa mama yenu ebhu nendeni mkalale!”

Alisema Mzee Jomo mabinti zake wakainuka ila kabla hawajaingia chumbani mlango uligongwa,wote walistaajabu maana haikuwa kawaida kugongewa mlango usiku kama ule!

Wale mabinti walisimama wakamuangalia baba yao,mzee Jomo baada ya kuona macho yote yapo kwake akasimama kwenda kufungua mlango huku analalamika!

“Unaona sasa saivi mnanitolea macho mimi,angekuwepo kijana wa kiume hapa mngeniangalia hivi kweli!”

“Kwa mtoto wa kiume labda subiri wajukuu nadhani hata wewe unaona limeshindikana hili!”,alidakia mke wa mzee Jomo!

“Nani?”,aliuliza Mzee Jomo!

“Nifungulie nahitaji msaada!”

“Wewe ni nani?tatzo sizo kufungua tatizo namfungulia nani?”

“Mi…mi…ni mgeni hapa!”

Mzee Jomo aligeuka akaiangalia familia yake,wote walijiuliza ni mgeni gani wa usiku kama ule!

“Zubeda ebhu niletee panga langu chini ya uvungu!”

Alimuagiza binti yake mkubwa ambaye aliingia chumbani punde akarudi na panga na kumkabidhi baba yake!

Mzee Jomo alifungua mlango huku kashika panga lake mkononi,alikutana na sura ya kijana ambaye alikuwa mgeni kabisa machoni mwake!

Alipomuangalia hakumuona na kitu chochote chenye kudhuru,hakuwa na begi wala kitu chochote!

Alimuonea huruma kutokana na mvua kubwa iliyokuwa inanyesha,akaamua kumkaribisha ndani,aliingia ndani wakampa kiti akakaa!

“Karibu kijana!”

“A…a…asa…nte!”

Aliitikia yule kijana huku anatetemeka kutokana na kunyeshewa na mvua ile kubwa kwa muda mrefu!

Wote walimshangaa alikuwa mgeni kabisa kwao,kijiji kile si kikubwa sana kwahiyo kama ni mgeni unajulikana haraka!

“Wewe ni mgeni hapa?”

“Ndi…o!”

“Umetokea wapi?”

“Ni…ni…mepotea!”

Yule mgeni aliongea kwa tabu kutokana na kupigwa na baridi la muda mrefu,Mzee Jomo alielewa hawataweza kuelewana katika mazingira kama yale!

Aliwaagiza wampe chakula wakampa wali na maharage uliokuwa umebaki,yule mgeni akala kwa pupa nkama mtu ambaye hajala muda mrefu sana,inaonekana alikuwa na njaa kali sana,alipomaliza alishukuru kisha Mzee Jomo akamchukua na kutoka naye nje muda huo tayari mvua ilikuwa imepungua!

UNAHISI MZEE JOMO ANAMPELEKA WAPI MGENI YULE WA AJABU?




Mzee Jomo alimshika mkono mgeni yule na kutoka nje,safari iliishia kwenye kijumba kimoja cha udongo kilichoezekwa kwa nyasi pia!

Alifika akaingia naye mpaka ndani kulikuwa na godoro la pamba na kitanda cha chuma,hakikuwa na vitu vingi kama vyumba vya mjini!

“Kijana naona kwa hali yako hatuwezi kuongea kabisa,sasa utalala hapa nadhani tutaongea kesho!”

“Sawa Mzee nashukuru!”

“Hiki ni chumba cha mdogo wangu,usije kujaribu kuiba kitu humu,nimekuamini japo sikujui ila usisahau pia hii ni SUMBAWANGA!”

Yule mgeni alitabasamu sababu hakuona kitu cha kuibika mle ndani,kwake ni kama kilikuwa chumba chenye hadhi ya chini kuliko vyote alivyowahi kulalia!

“Sawa Mzee mi nashukuru sana!”

Mzee Jomo aliondoka na kumuacha yule kijana mle ndani,alifika akaikuta familia yake inamsubiri!

“Umempeleka wapi?”,mke wake alimpokea kwa swali!

“Kwenye nyumba ya Mashaka!”

“Wewe akibeba kigodoro cha watu akaondoka nacho?”

“Wacha abebe Mashaka mwenyewe tangu aondoke hapa kwenda mjini hataki kurudi kijijini!”

Walitawanyika Mzee Jomo akaingia chumbani na mkewake na watoto wake wakaingia chumbani kwao!

“Mume wangu vipi sasa?”

“Kuhusu nini?”

“Haki yangu mume wangu,leo wiki ya pili hujanigusa!”

“Mkewangu lazima uelewe sasa tumekuwa watu wazima,hatuwezi kucheza mechi kama vijana wa miaka ishirini!”

“Hata kama Jomo yani ndiyo mwezi upite jamani?”

“Umeniitaje?yani unaniita Jomo kweli,umeshindwa kuniita mume wangu si uniite hata baba Zubeda,baba Suzi,baba Johari au baba Selina?”

Mzee Jomo alilalamika huku anataja majina ya binti zake,ni kama alipata sababu ya kumkwepa mkewake siku ile!”

“Samahani mume wangu basi nipe!”

“Hapo jipange kesho tena,umeniuzi sana adabu yako imepungua siku hizi!”

“Umepata tu sababu ya kunikwepa na kesho nataka hali yangu mimi!”

Alisema Mke wa Mzee Jomo kisha akajifunika shuka akaanza kuutafuta usingizi,baridi la siku ile lilishawishi kabisa kufanya tendo,lakini mume wake hakuwa tayari!Hakujua sababu ni uzee au kuna chanzo kingine,maana hii tabia imeanza miezi mitatu iliyopita!


*********


Upande wa mgeni yeye alivua nguo zake akazianika,maana hakuwa na nguo kabisa za kubadili,alikuwa yeye kama yeye!

Alijifunika shuka akaanza kufikiria maisha yalivyombadilikia ghafla,kuna kitu alionyesha kukijutia ila haikujulikana ni kitu gani!

Alionyesha kushukuru sana kwa hifadhi aliyoipata,aliwaza amwambie nini yule mzee aliyempokea ili akubali kuishi naye pale,maana kuliko kurudi alipotoka ni mara mia abaki hapo,alale kwenye kigodoro cha pamba lakini awe na amani!

Usingizi ulimchukua akalala japo alionekana kuweweseka sana ndotoni,ni wazi kuna jambo kubwa lilikuwa linamkabili!


********


Mzee jomo ni kama alikuwa na wasiwasi sana na yule mgeni wa usiku usiku,alihofia kuibiwa kigodoro cha mdogo wake,ambaye aliondoka kwenda mjini kutafuta maisha miezi mitano iliyopita!

Alikuwa anaamka mara kwa mara kwenda kumchungulia mgeni kama yupo au lah!aliamka kama mara tatu kila akienda kumchungulia anamkuta kalala!

Kulipokucha tu akaamka na kwenda kumgongea mlango mgeni akafungua akiwa amejistiri na shuka tu sababu nguo zake zilikuwa bado hazijakauka!

“Oooh kijana umeamkaje!”

“Niko salama mzee wangu shikamoo!”

“Marahaba!”

Mzee Jomo alimuangalia yule kijana ambaye kisura alionekana mpole na mkarimu sana!

“Angalia kuna mavazi ya mdogo wangu uvae naona kama mnaendana mwili!”

Mgeni alirudi ndani akaangalia hayo mavazi aliyoambiwa,yalikuwa mavazi ambayo hakuwahi kufikiria kama kuna siku angevaa nguo za namna ile!

Moyoni aklikiri kweli shilingi imepinduka,hakuwa na jinsi alivaa zile nguo kisha akatoka akamkuta Mzee Jomo kakaa kwenye kijua cha asubuhi anapata vitamini D!Pembeni kulikuiwa na kiti akakaa!

“Kijana unaitwa nani?”,aliuliza Mzee Jomo!

“Naitwa Lukas!”

“Oooh unaweza kuniambia jana ulikuwa unatokea wapi?na umefikaje kwenye kijiji chetu?”

“Ni stori ndefu mzee wangu,kiufupi mi nina matatizo,nimekimbia Daresalam sababu kuna majambazi wananitafuta waniue,wameshamuua baba na mama yangu sasa wananitaka na mimi na yote ni sababu ya mali ya mzee wangu!”

“Bado hujanijibu swali umefikaje hapa!”

Lukas alijua kabisa anachoongea ni uongo na alishajipanga kudanganya ili mradi tu apate nafasi ya kuishi kwa mzee yule aliyempokea!




Mzee Jomo alitaka maelezo yaliyoshiba sababu kumpokea mtu kijijini bila kumfikisha kwa mjumbe au mwenyekiti ni kosa kubwa,mfano angefanya ubaya wowote ni wazi angewajibika yeye.Ndiyo maana alitaka maelezo ya kutosha kabisa ili ajiridhishe kuwa yupo na mtu salama!

“kijana jieleze vizuri bwana!”

Lukas alikohoa kidogo kurekesha koo kisha akajipanga kunyoosha maelezo ambayo hayakuwa na ukweli ndani yake,alichotaka ni kupata hifadhi ya muda mrefu ili aliyoyafanya mjini yasahaulike!



“Mzee wangu kama nilivyokwambia natafutwa na majambazi wanaotaka kuniua kisa mali za baba yangu,juzi nilivamiwa ndani kwangu bahati nzuri nikafanikiwa kutoroka,na kama unavyoniona sikubeba chochotye hata simu yangu niliiacha ndani,nilikimbia na nguo zangu tu nilizokuwa nimevaa!”

“Kwanini hukwenda polisi kutoa taarifa?”

“Mpaka sasa kifo cha wazazi wangu hakuna kilichotokea kabisa,tunazungushwa tu dana dana za kila siku na wauaji wanajulikana,ndiyo maana nilipovamiwa tu nikajua maisha yangu yako hatarini,nilikimbia mwisho nikaenda stendi nikapanda basi ambalo hata sikujua linaenda wapi?sikuwa hata na nauli nikashushwa porini na kujikuta nimefika kwenye hiki kijiji,naomba nafasi baba ninusuru roho yangu wataniua,walau nipotee kwa muda wanisahau!”


Aliongea Lukas kwa hisia na kumfanya Mzee Jomo amuamini aliyamwaga machozi kama mtoto,Lukas alilia kama mtoto!

Mzee Jomo alimuangalia bado hakuonyesha kama amekubali au lah!bila kusema neno aliinuka akaingia ndani na kumuacha Lukas akiwa na maswali mengi,hakuelewa kama amekubalika au lah!

Alichofanya ni kuendelea kuyavuta machozi kwa nguvu na kulia kwa hisia kali yote ni kuonyesha huruma ili ahurumiwe!

Mzee Jomo aliingia ndani aliporudi alitoka akiwa na familia yake yote,yeye mke wake na bintize wanne!

Alipofika aliketi kitako akakohoa kidogo kisha akamuangalia Lukas ambaye alikuwa kama mfungwa anayesubiri hukumu ya mwisho!

“Lukas!”

“Naa..m!”

“Naitwa Mzee Jomo huyu ni mkewangu na hawa ni binti zangu,historia yako imenigusa na nimeamua kukufanya mmoja kati ya familia yangu,utaishi hapa mpaka pale utakapohisi hali imekuwa shwari utaondoka!”

“Ahsante baba sijui nikushukuru vipi?”

Alisema Lukas akionyesha kufurahia kiasi akataka kupiga magoti kabisa kushukuru kupokelewa katika familia ile!

“Usijali kijana huna haja ya kunishukuru hivyo cha msingi ni kuzingatia heshima kuniheshimu na kuwaheshimu dada zako basi,pia usisahau hii ni SUMBAWANGA!”

Baada ya utambulisho ule Lukas aliingia kwenye kile kijumba alichopewa kuishi,alifika akaanza kurukaruka,alifurahi sana kuruhusiwa kukaa pale!

“Ooh!afadhali nijifiche kwanza huku maana moto niliowasha mjini hauzimiki leo,ila nitulie sasa Lukas dah,funga zipu Lukas!’”

Alijisemea Lukas kisha akajitupa kwenye kigodoro cha pamba akalala chali akaanza kuwaza namna alivyonusurika!

“Wanafunzi watatu wote wana mimba,kwa hiyo kila mwanafunzi miaka thelathini kwahiyo jela miaka tisini,bado yule mke wa mjeda ana mimba yangu yule mjeda anagenifuata jela aniambarruti bila mafuta yule,na yule mke wa jirani daaaah Lukas funga zipu sasa,ila ntaweza kweli maana mzee ana pisi kali tupu mmh Lukas tamaa itaniponza!”


*********


“Hivi mume wangu unamkubaliaje kirahisi ivyo je kama anadanganya?”

“Hapana machozi hayadanganyi mkewangu yule kijana ana shida ila kama anadanganya shauri yake hii ni Sumbawanga,itamfundisha kusema ukweli!

Mke wa Mzee Jomo alionyesha wasiwasi juu ya Lukas lakini mzee Jomo alimtetea,machozi ya Lukas yalimfanya amuamini moja kwa moja kabisa!


*********

INAENDELEA

Post a Comment

0 Comments