IMEANDIKWA NA : JACK MAMBO
*********************************************************************************
Ngurumo na radi vilitawala,huku wingu zito likitanda,ilikuwa ni dalili kuwa muda wowote mvua itanyesha,tena siyo ya rasharasha ilikuwa ya uhakika!
Muda huo ndiyo nilikuwa nimeshuka kwenye basi lililonileta mpaka Sumbawanga,ilikuwa safari ndefu sana lakini nashukuru nilifika salama!
Kulikuwa na pilika pilika za hapa na pale lakini,lakini zilikuwa za kawaida si kama Dar jiji lenye pilika zake!
Rafudhi za watu wa pale haikunipa tabu kujua kuwa sasa nimeingia Sumbawanga!
Uchovu ulikuwa mkubwa sana ilibidi nitafute sehemu nipumzike kabla sijaunganisha safari kuelekea katika vijiji nilivyovikusudia!
Hali ya hewa ilikuwa tofauti kabisa na Dar hiyo ilinifanya nifungue begi langu lenye nguo chache tu nikatoa sweta nikavaa,sikuja na nguo nyingi sababu niliamini sina siku nyingi huku!
Sikuona sababu ya kuunganisha safari siku ile,niliulizia sehemu ambayo naweza kupata nyumba za wageni!
Nilipata chumba nikalipia kwa usiku mmoja tu sababu kesho yake ilikuwa ni lazima niendelee na safari yangu!
Safari yangu ilikuwa ni kufanya utafiti wa mazingira ya Sumbawanga na vijiji vyake,sababu niko mbioni kuandika kitabu changu kitakachohusisha sana mazingira na tamaduni za watu wa Sumbawanga!
Wakati nikiwa kwenye mawazo nikiwaza kitabu changu kitakuaje mlango wangu uligongwa,nikaufungua mlango nikakutana na dada mmoja mweupe ana umbo zuri sana kasimama mlangoni!
“Vipi dada!”
Nilimuongelesha baada ya kuona simuelewi kasimama ananiangalia kwa macho yaliyolegea legea!
“Safi kaka nili nilikuwa nakuuliza kama hupendi kulala peke yako si unaona baridi!”
Nilishtuka sana kusikia vile ni jambo ambalo sikulitegemea kabisa,tayari nilishamuelewa ila sikutaka kuonyesha nilihitaji afafanue zaidi,mambo kama yale nilijua yako dar tu kumbe mpaka mikoani!
“Samahani sijaelewa unamaanisha nini?”
“Jamani kaka mbona naeleweka au unaninaje?”
Alisema yule dada huku akianza kulivuta juu vazi lake na kuanza kuyaacha mapaja yake wazi,nilishtuka sikutegemea kama tungefika kule!
“Basi!basi!basi!”
Nilimzuia yule dada hasinionyesha maungo yake ila wala hakuwa na habari,ndiyo kwanza alizidi kuipandisha juu mpaka nikaanza kuona kabisa dalili ya kukiona kitumbua chake!
Yule dada macho yake yalitua kwenye zipu yangu na kuona tayari bakora yangu imesimama!
“Wow!jamani niishike basi!”
Alisema yule dada huku ananisogelea ghafla akaleta mkono na kunishika usawa wa zipu yangu,ilinibidi nifanye maamuzi magumu maana niliona naenda kuvunja masharti niliyojiwekea ya kujiepusha na mapenzi ninapokuwa katika harakati zangu za kazi!
Niliufunga mlango ghafla nikamuacha yule dada anashangaa shangaa tu hasiamini kama nimevuka salama kwenye mitego yake!
Nilijitupa kitandani nikavuta pumzi ndefu kisha nikaitoa,muda huo bakora yangu nayo ikaanza kutulia na kurudi katika hali yake ya kawaida!
“Duh nilijua haya mambo yapo Dar tu kumbe mpaka huku daaah!”
Usingizi ulinichukua hata sikujua nimelala sangapi?Nilikuja kushtuka asubuhi na jua tayari limeshatoka!
Nilikurupuka nikakimbilia bafuni japo kulikuwa n baridi kali ila nilijitahidi nikaoga ili kurudisha mwili katika hali yake ya kawaida!
Nilichukua begi langu nikatoka,sikuwa na muda wa kupoteza,nilikuwa na siku tatu tu kule nirudi Dar kuanza kuandika kitabu changu ambacho nilipanga kitawaliwe na mkoa wa Sumbawanga!
Wakati natoka nilikutana na yule dada naye anatoka kwenye chumba cha pembeni yangu kumaanisha kwamba aliponikosa mimi alienda kutega kwingine!
Aliponiona aliona aibu akainama chini nikampita bila kumsalimia,moja kwa moja nikachukua boda boda mpaka kijiji cha Mponda!
Nilipokelewa vizuri japo sikuwa na mwenyeji,niliwaeleza ujio wangu pale wakanipa ushirikiano mkubwa sana!
Nililala pale kisha kesho yake nikaelekea kwenye kijiji cha cha Kisumba ambako ndiko nilikopata hii stori ninayokuletea leo!
Kwanza kilichonishangaza ni mapokezi niliyopewa,nilishawahi kufanya tafiti mbali mbali katika vijiji vingi ila nikiri hiki ni kiboko!
Kwanza hakuna mtu aliyenijali wala kunipokea kama mgeni nilijitahidi kujitambulisha na kuwachangamkia wenyeji lakini hawakunichangamkia kabisa!
Mpaka inafika jioni sikuwa nimeambulia chochote na hata sikuwa nimepata mwenyeji maana kila niliyemfuata alinisikiliza na kunipuuza!
Njaa ilikuwa kali sana muda huo tayari giza lilishaanza kuingia,bahati nzuri niliona sehemu inayouza chakula!
Nilijisogeza nikaagiza chakula nikahudumiwa,niliagiza ugali na maziwa mtindi nikala sana kutokana na njaa kali niliyokuwa nayo!
Baada ya kumaliza tatito la njaa sasa swali likabaki kuwa nalala wapi?nilipowaza kurudi kwenye kijiji nilichotoka umbali wake na usafiri ni wa shida!
Nilihisi kuchanganyikiwa nikikumbuka na stori nazosikia kuhusu Sumbawanga nilichoka kabisa aiseeh!Hakuna gesti wala sehemu ya kulala maeneo yale!
Nilijitahidi japo nizoeane na mwenyeji lakini ilishindikana kabisa,kwenye kile kihotel napo walianza kufunga hapo ndipo nikazidi kuchanganyikiwa!
Ngurumo za radi zilisikika ishara ya kwamba mvua kubwa itanyesha muda si mrefu,mpaka wakati huo anilikuwa sijapata sehemu ya kulala!
Walianza kufunga hoteli huku wakiwa wanaongea lugha ambayo sikuielewa,ila kabla hawajafunga kabisa kuna mzee alikuja kutafuta chakula!
“Vipi huo ukoko haujaungua kama wa jana?”
“Leo uko vizuri babu!”
“Niletee si bei yetu ile?”
“Ndiyo babu!”
Yule mzee ilionekana ndiyo kawaida yake kuja kula ukoko kila siku wale wadada wakimaliza kuuza chakula!
Alikabidhiwa lile sufuria akaanza kulifakamia jungu lilikuwa na makoko mengi sana!
“Kijana karibu!”
“Ahsante mzee mimi tayari!”
Ulipita ukimywa kilichosikika ni sauti ya yule mzee akitafuna tu ukoko wake,baada ya nusu saa jungu lilikuwa jeupe kabisa!
Wale wadada walikuwa wamemaliza kuosha vyombo na kufunga,wakati yule mzee amemaliza akalipa anataka kuondoka mi bado nilikuwa pale,kitendo kile kiliwachanganya wale wadada ambao walianza kunifikiria labda nataka kuwatongoza,ila kilichowapa maswali ni begi nililokuwa nimebeba!
“Kaka si tunataka kufunga!”
Kauli ile ilikuwa kama msumari iliuchoma moyo wangu na kunipa mawazo mengi sana,ilibidi niseme ukweli kuliko kulala nje bora wanipe ruhusa nilale mle kwenye kile kibanda!
“Jamani mimi ni mgeni hapa!”
“MGENIIII?”
Walishtuka hadi yule mzee wa ukoko naye akageuka na kuniangalia kwa makini,bado sikujua kwanini watu wa kijiji hiki wanashtuka sana wakisikia neno “MGENI”.
“Ndiyo mi ni mgeni nimekuja hapa kufanya utafiti kuhusu tamaduni na maisha ya hapa,ni muandishi wa vitabu,naitwa Jack Mambo!
“Wewe kaka hiki kijiji hakipokei wageni kama nyie,tupishe tufunge sisi!”
Wale wadada walisema wakionekana kuwa hawana masikhara,nilijitetea lakini hakuna aliyenisikiliza kabisa,sikuwa na jinsi mpaka muda huo yule mzee wa ukoko alikuwa kimya hajasema kitu!
Nilijizoazoa taratibu na kibegi changu nikakiweka mgongoni,taratibu nkazipiga hatua zangu nikatoka nje!
Sikuwa najua pa kuelekea,sijui mtaa wowote sina mwenyeji wala mtu ninayemfahamu,nilishawahi kufanya tafiti mbali mbali ila kwa hii stori duh!
Nilianza kutembea nikiwa sijui naelekea wapi,wakati huo giza limeshaingia na mvua imeanza kunyesha taratibu!
Nilitamani kulia ila nilijikaza nikiamini ni changamoto ,japo kilichonipa hofu ni zile stori nilizosikia kuhusu Sumbawanga!
Nikiwa kwenye kuwaza ghafla nilishikwa mkono begani nikastuka sana,niligeuka nikakutana na yule mzee wa ukoko!
“Kijana unaenda wapi?”
“Sijui mzee wangu!”
“Nifuate!”
Alisema yule mzee kisha akaanza kuondoka,nilibaki nimesimama nikiwa na hofu kubwa lakini niliona hakuna jinsi!
Taratibu nilianza kuzivuta hatua zangu kumfuata yule mzee wa ukoko,haikuwa safari ndogo wala ndefu sana!
Mwisho tulifika sehemu ambayo kulikuwa na nyumba nyingi huku chache zikiwa zimeezekwa kwa bati!nyingi ziliezekwa kwa nyasi huku zingine zikiwa zimejengwa kwa nyasi kuanzia chini mpaka juu!
Safari ilitupeleka mpaka kwenye vijumba viwili vya udongo vilivyoezekwa kwa nyasi na vyote vilikuwa sehemu moja!
“Karibu kijana!”
“Ahsante sana mzee!”
“Ngoja nimgongee binti yangu atupe chakula!’
Nilishtuka kusikia yule mzee anataka chakula na huku ametoka kupakia jungu la ukoko tena mwingi tu!
Sikutaka kumuonyesha kuwa nimeshangaa nilitaka kiletwe hicho chakula nione yule mzee atakulaje na makoko aliyoyajaza tumboni!
Yule mzee alienda kwernye moja ya vile vijumba akagonga mlango,alitoka binti mmoja ambaye mwanga wa mbalamwezi ulisaidia kunionyesha urembo wa binti yule!
Alikuwa ni mrembo haswa!nakiri ni mmoja wa wanawake warembo niliyowahi kuwaona maishani!
Alifika akamsalimia ule mzee kwa kilugha chao kisha akanisalimia mimi pia kwa kilugha chao nikabakli nimeduwaa!
“Shikamoo!”
“Marahaba!”
Alipoona tu simuitikii akanisalimia kiswahili,kisha yule mzee akampa maelekezo akarudi kwenye kile kijumba chake!
Yule mzee alinichukua mpaka kwenye kile kijumba kingine,akawasha chemli,punde yule binti alikuja na chakula ambacho kilikuwa ni ugali na nyama!Nilikula kidogo tu nikawa nimeshiba,ila yule mzee alikula kama hajala ukoko nikabaki namshangaa tu,nikajiuliza au wako wawili!
Baada ya kumaliza kula ndipo akatoa kauli ambayo iliniacha kwenye wakati mgumu sana!
“Kijana mimi leo nalala na mama yako hapa,wewe kalale na binti yangu ila usimguse,kati ya vitu sitaki ukosee ni kufanya mapenzi na binti yangu!”
Kauli ile ilinishtua sana,kama ni mtihani ni ule,nilijiuliza nawezaje kulala na binti yule alivyo mrembo na nisimguse?
“Laikini mzee…!”
“Hakuna lakini kama huwezi nikurudishe nilipokutoa,nimekupa msaada sasa unataka nilale na mwanamke wangu na wewe humu ndani!?”
Mwisho niliamka na kuelekea kwenye kile kijumba cha yule binti nikagonga akanifungulia huku ananitazama kwa mshangao!
“Ni…ni….nimeambiwa nilale hu…huku!”
“Karibu!”
Nilishafanya mitihani mingi hasa ya shule nikamaliza,sikujua kama ntakuja kukutana na mtihani mwingine kama huu!
Nilijiuliza nitawezaje kulala chumba kimoja na binti mrembo kaa yule nma nisiwaze kumgusa!
Baada ya kumwambia vile kuwa nimeambiwa nilale naye mle ndani,yule binti alinikaribisha ndani huku akionyesha kutokuwa na wasiwasi wowote jambo lililozidi kunitia wasiwasiw!
Yule binti alitandika chini kisha akataka mi nilale kwenye kile kitanda cha chuma chenye kigodoro cha pamba!
“Hapana wewe lala hapo juu mi ntalala chini!”
“hapana kaka wewe lala kitandani tu,wewe ni mgeni!”
Tulibishana sana ila sikukubali kulala kitandani,mwisho yule binti ambaye nilisikia yule mzee anamuita Regina akakubali kulala kitandani!
Nililala pale chini baridi lilikuwa kali kiasi cha kushawishi kumkumbatia yule dada tupeane joto!Ila nilipowaza kauli ya yule mzee kuwa nisifanye naye chochote nilituliza nyege zangu!
“Huku kutafutana ubaya tu,huyu mzee ananitafutia sababu tu aniroge anipeleke Gamboshi huyu!Anawezaje kumlaza Simba kwenye banda la swala?Ila hanipati kudadeki!”
Nilijisemea japo hisia zilikuwa kali,shetani alikuwa kazini anafanya kazi yake,usingizi ulikuwa mgumu sana siku ile!
Sijui nililala sangapi nilikuja kushtuka asubuhi jogoo anawika,nilifumbua macho nikaangalia kitandani sikumuona yule binti,nikajua tu alishaamka zamani,mabinti wa kijijini huamka mapema siyo kama wale wa mjini wanaokesha whatsap na insta!
Nilikurupuka nikajinyoosha,kwa mbali nilihisi mbavu zinauma sababu ya kulala chini,ila nilishukuru sababu nililala ndani kuliko kulala nje,halafu sehemu yenyewe ni Sumbawanga sasa!
Nilitoka nje nikamkuta yule mzee amewasha moto halafu amekaa pembeni yake,nilisogea pale sababu kulikuwa na baridi sana!
Nilichukua kigoda nikakaa pembeni ya yule mzee ambaye niligundua kwenye ule moto alikuwa anachoma viazi vitamu!
“Karibu kijana!”
“Ahsante sana shkamoo mzee wangu!”
“Marahaba kijana!”
Bado nilikuwa sijiamini amini,nilikuwa nawaza itakuwaje yule mzee akisema nimefanaya mapenzi na binti yake?
Ukimya ulitawala kati yetu muda huo yule mzee akatoa kiazi kimoja kwenye ule moto akanipatia!
Nilikipokea nikakiweka chini maana kilikuwa cha moto hatari,sijui hata yule mzee aliwezaje kukishika!
Muda huo yule binti alikuja akiwa amebeba maji,nikajua tu anatoka kisimani,nilipata muda sasa wa kumuona vizuri mrembo yule!
Dah!nilijisifu sana kuushinda mtihani ule,moyoni nilikiri nimekuwa sasa maana siyo kwa mtihani ule duh!
Nilipogeuza shingo kumuangalia yule mzee,nilikuta ananiangalia nikainama chini kwa aibu maana kaniona nilivyokuwa namtathimini binti yake!
“Hahahahahahah kijana!”
Alicheka yule mzee nisijue anacheka nini?nilikuwa mtu wa mashaka mashaka tu bado sikujiamini kabisa!
“Hongera kijana wewe ni mwanaume,uanaume siyo kufungua zipu tu hata ukijifunza kuifunga ni uanaume tena uanaume wa kweli!”
“Unamaanisha nini mzee wangu?”
“Namaanisha usiwe kama mbwa kila mgeni unambwekea tu ukiamni ni mtu mbaya!unaonekana utakuwa mgeni wa tofauti kuliko wageni wengine,kwa ajili yako naweza kuwaza kukishauri kijiji changu kianze kupokea wageni tena!”
“Wageni!!!!”
Niliuliza kwa mshangao cha ajabu yule mzee akaondoka zake huku anacheka,nilianza kuwaza namna nilivyopokelewa na wanakijiji wa pale,nilipounganisha na maneno ya yule mzee nilishindwa kuelewa,nikabaki na maswali mengi kichwani!
“WAGENI WANA NINI KWENYE HIKI KIJIJI?”
Licha ya kilichonileta nilitamani pia nifanye uchunguzi nijue kuna siri gani ya kile kijiji na wageni!
Yule binti alimaliza kuchota maji akachemsha uji na viazi tukanywa,muda ule yule mzee hakuwepo,alikuwa ameshaondoka zake!
Nilianza utafiti wangu kwa ajili ya kitabu changu kwa kumuuliza mambo mbali mbali yule binti ambaye alinipa ushirikiano wa kutosha kabisa!
Baada ya kumuuliza maswali yangu karibu yote ndipo nikaamua kumuuliza hili duku duku langu kuhusu wageni!
SOMA HAPA DALILI ZA MWANAMKE ANAYETAKA KUKOJOA
INAENDELEA
0 Comments