Taratibu za kumsaka Ernest popote pale alipo zilianza mara moja usiku huo huo na kuanza kupata baadhi ya sehemu ambazo anapendelea kufika. Hata walipofika nyumbani kwao waliweza kufahamishwa kuwa hakuna mtu kwenye nyuma ni mara baada ya kutokea kwa mauaji ndani ya familia hiyo. Na mtu pekee aliyebahatika kuwa hai ni Ernest ambaye siku hiyo ya tukio la mauaji hakuweza kulala kwao.Taarifa hizo walipo zipata ikabidi wamtaarifu mkubwa wao Mr.Alex ambaye japo hilo lilimshtua na kuhisi huenda kuna jambo lengine linaendelea. Hakutaka kulifikiria hilo aliwaamuru wazidi kuchunguza zaidi na zaidi.
Kesho yake asubuhi na mapema kabla ya kuelekea kwenye usaili Ernest aliweza kuwasiliana na rafiki yake Oscar ambaye ndiye anafanya naye utundu wakiwa mjini Dar es Salaam. Hadi kupata wazo la kutafuta nafasi katika kampuni ya MOLEN, kisha akafanikiwa kumtambua Mwalimu Otieno ambaye waliweza kujua uwezo wake ni Oscar ndiye aliyetoa mawazo hayo na Ernest akayapokea na kuamua kuyafanyia kazi lengo likiwa ni kuhakikisha ndugu yake Albert anatoka gerezani.
"Vipi kila kitu kinaenda sawa huko?"aliuliza Oscer akiongea na swahiba wake Ernest kwa njia ya mtandao wa IMO.
"Huku fresh tu hapa ndio najianda midamida tunaelekea kwenye usaili, So anytime be online i need your help ( Hivyo muda wote uwe hewani nahitaji msaada wako)." alisema Ernest.
"Usijali man tuko pamoja mwanzo mwisho, usisahau tena kuweka kinasa sauti kwenye miwani karibu na sikio ili nisikie unachoulizwa nikusaidie ukikwama."alisema Oscar na kumfanta Ernest apate imani ya kufanikisha zoeezi hilo.
Baada ya mazungumzo yao waliagana na Ernest akajiandaa huku Mwl.Otieno akimuandalia baadhi ya vitabu aonekane kweli yupo siriasi na kuhitaji nafasi. Alimsaidia kumuandaa na baada ya zoezi hilo kukamilia alijitazama kwenye kioo na kujiona vile alivyo. Hata yeye alitabasamu baada ya kujiona amekuwa tofauti kabisa, alinyanyua begi lake na kulivaa mgongoni.
"FairView Hotel ndipo wanapofanyia usaili huo hivyo muhimu ni kujiamini kwa kile unachoulizwa na usijibu kwa mkato jibu kwa ufanisi na ufasaha zaidi mimi naamini utachaguliwa tu, Nami najiandaa nitafika hapo baadae."alisema Mwl.Otieno na kumfanya Ernest atii alichoambiwa. Walipeana mkono wa baraka kisha Ernest akageuka na kuondoka zake kuelekea huko kwenye sehemu husika.
1-40 FEEE
STORI INA VIPANDE 91 LIPIA 1500 UTUMIWE YOTE.
0716469242
SEHEMU YA 06
Upande wa pili gerezani, askari mmoja alitumwa kwenda kuwaita kundibla DEVIL MOOB ambao wote kwa pamoja walinyanyuka walipokuwa wamepumzika na kuanza kuongozana na askari huyo. Simon na wenzake waliweza kuwaona kundi hilo wakielea na askari yule.
"Ukiona wanaongozana na askari juwa kuwa kuna tukio siku za karibuni litatokea. Nimekuwa nikifuatilia hivyo nyuma kuna mauaji ya wafungwa watatu waliuawa tofauti na chanzo nikihisi ni hawa mashetani."alisema Simon akiwa amekaa na wenzie.
"Sasa hili gereza limekuwa lao mbona wanafanya mambo ya kipuuzi hivyo na wachuliwi hatua.?"aliuliza Albert.
"Wale wanakula pamoja na mkuu wa jela Albert na ndio maana wanajiamini kupindukia."alisema Johnson, Mrusi aliyeipenda lugha ya kiswahili akajifunza na kuielewa.
"Na ndio maana watu wengi wanawaogopa kutokana na kuwa na jina kubwa na kujulikana kwa mkubwa wa gereza pia."alisema Simon na kumfanya Albert awaelewe hasa DEVIL MOOD.
Safari ya kundi hilo iliishia ofisini kwa mkuu wa jela na walipoingia mlango ukafungwa wakawa wanaongea mambo yao kwa siri.
*"There's a job i'm supposed to give you within three days must be finished, there's something that the prisoner number 417 has,so you have to punish him until he says where he has put it* ( Kuna kazi nahitaja kuwapa muifanye ndani ya siku tatu iwe imekamilika, kuna kitu yule mfungwa namba 417 anacho hivyo mnatakiwa mumuadhibu mpaka aseme wapi ameweka.)"alisema mkuu wa jela akiwaambia DEVIL MOB ambao baada ya kupokea taarifa hizo walitii na kukubali kazi hiyo kuifanya.
Nchini Kenya usaili ulikuwa ukiendelea kwenye Hoteli ya FairView. Vijana wengi wenye ujuzi wa IT walijitokeza siku hiyo kujaribu bahati yao kama wataweza kupata nafasi ya kuchaguliwa na kampuni hiyo ya MOLEN ambayo ilipendelea kuchukua vijana kumi watakao kidhi vigezo katika usaili huo.
Kila kijana aliyefika pale alielekea kujiandikisha na kuchukua fomu kusubiria muda na wakati atakaoitwa kuanza interview.
Ernest alikuwa ametulia sehemu moja ametulia tu ,alitazama kila kona na kuona wenzake wakiwa wameweka makundi makundi wakipiga stori za hapa na pale.Alitoa miwani yake aliyoiandaa kisha akaseti kinasa sauti kabisana kuivaa akianza kujaribu kuwasiliana na swahiba wake Oscar.
"Yes Oscar unanipata?"aliongea Ernest .
"Nipo online muda wote best nakupata vizuri."aliongea Oscar akiwa chumbani kwake Dar es salaam akionekana kuseti mitambo ambayo ilinasa sauti kutoka kule alipo Ernest.
"Okay powa naona watu wameanza kuitwa mmoja mmoja ndani so tunaskilizia hapa."alisema Ernest na gafpa akashangaa kumuona msichana mmoja akisogea pale alipo na kukaa. Alishusha begi lake na kuanza kujipepea. Ernest alimtazama usoni na kushuhudia jinsi Mungu akivyoshusha neema ya uzuri kwa mrembo yule.
"Wewe usijali ondoa hofu na safari hii tutafanikiwa tu naamini."ilisikika sauti ya Oscar akimpa moyo Ernest.
"Subiri kidogo."alisema Erne akimwambia Oscar huku akiwa anamtazama dada yule.
"Wewe namba ngapi kuingia?"aliuliza yule msichana akionesha tabasamu usoni mwake huku akimtazama Ernest.
"Oh sorry hadi na forget kutoa salamu. Habari vipi uko good?"alisema mrembo yule na kumfanya Erne aachie tabasamu.
"Mimi ni mzima tu sijui hali yako, pole kwa kukimbia sana."alisema Erne huku akimtazama msichana yule akiwa anajipepea jasho likimtoka.
"Hahaha thanks. Nilihisi nachelewa usaili na sikuweza kupata pesa ya nauli kunifikisha hapa but God bless me nimewahi na nikaona nije karibu yako kupunga upepo maana nakuona alone."alisema dada huyo aliyekuwa akiongea lafudhi ya kikenya.
"Ah nilipenda tu kukaa hapa alone kwakuwa sina hobi na groups ndio maana, mimi ni namba 27 kwenye usaili."alisema Ernest akiigiza lafudhi ya Kenya.
"Wooh kumbe ni doto kwako. Mimi ni 28,so utakapohitajika wewe kwenda mimi na jiprepare (najiandaa) huku nje. Naitwa Jenifer, natokea Kisumu hadi kufika hapa Nairobi lengo ni kupata nafasi ya kuwa miongoni mwa watu watao chaguliwa na kampuni ya MOLEN, unajua ukiweka nia na jambo moja basi moyo unaridhika na hata God ana bless jambo hilo. Mimi naamani nitapita tu japo wingi wa watu ukiwemo wewe hainizuii kupigania nafasi yangu. Tumuombe God yeye ndiye everything for this day."alisema mrembo Jenifer ambaye maneno yake yakamtanya Ernest atabasamu tu kwa mengi. Kwanza nafsi yake tu imejikuta ikimuona mrembo huyo kwa hisia za karibu sana. Isitoshe uongeaji wake ni dhahiri kuwa anaongea sana na maneno yake yakamfanya Ernest atambue msichana huyo hana woga na ni mtu mwenye kujiamini sana.
"Ernest nani huyo anaongea sana kama mtanzania?"aliuliza Oscar akiwa amesikiliza maongezi ya wawili hao. Ernest alishindwa kumjibu muda ule akaendelea na mazungumzo yao.
"Unachokisema ni kweli Jenifer, Mungu ndiye wa kumtanguliza sana siku ya leo, naamini ukijiamini pia itasaidia."alisema Ernest na kumfanya Jenifer atabasamu.
Maongezi mengine yalendelea na muda mfupi baadae namba 27 ikaitwa kuingia ndani ya chumba cha interview. Ernest alinyanyuka na kuagana na Jenifer kisha akazama ndani.
Walionekana wanaume wawili wa kiafrika pamoja na mwanamke mmoja wa kizungu wakiwa wamekaa huku meza zao zikiwa na baadhi ya vifaa. Ernest alipoingia tu na kuona vile vitu alivifahamu mapema kwakuwa ni mzoefu wa vitu hivyo. Alikaribishwa na kukaa kwenye kiti kilichokuwa mbele hatua kama tatu na walipo watu hao.
*"Okay we need to prove your name,just introduce so as to know your talent* (Haya tunahitaji kuhakikisha jina lako, jitambulishe na tujue uwezo wako)" alisema yule mwanama mzungu huku akifunuafunua makaratasi yaliyo mezani.
*"My name is Ernest Gama from Mombasa, I'm here for interviewing so I can get in touch with the company MOLEN. I think through this company I will be able to lift myself somewhat through my IT profession. I have experience in doing some work as connecting to a certain part and finding it for a frequency that wept very well. I also have my creative ability to design some of the devices that can identify a certain part there is a problem or any bad thing. For example on the table ...* ( Niko hapa kwaajili ya kufanyiwa interview ili nipate nafasi ya kujiunga na kampuni ya MOLEN. Nadhani kupitia kampuni hii nitaweza kuinyanyua kiasi fulani kupitia taaluma yangu ya IT. Nina uzoefu wangu wa kufanya baadhi ya kazi kama kuunganisha mawasiliano sehemu fulani na kuyapata kwa frequence iliyo tulia na nizuri sana. Pia nina ubunifu wangu wa kutengeneza baadhi ya vifaa vinavyoweza kutambua sehemu fulani kuna tatizo au jambo lolote baya. Kwamfano hapo mezani...)"alisema Ernest na kunyanyuka pale kwenye kiti na kusogea pale mezani.
*"Among these things at the table I'm just aware of that only three devices are related to Information Technology like this ... which is in the case of Mobile Technology, which is also online conferencing issues and this last is about SQL server. All of this is not in line with the thing we brought here though I can also explain it if I'm going to be given time to explain.*( Kati ya hivi vifaa mezani nikiangali tu nafahamu kuwa ni vifaa vitatu tu ndio vinahusiana na masuala ya Information Technology kama hiki...ambacho kipo kwenye masuala ya Mobile Technology, hiki pia ni masuala ya Online conferencing na hiki cha mwisho ni kuhusu SQL server. Hivi vengine vyoooote haviendani na jambo lililotuleta hapa ingawa naweza kuvielezea pia kama nitapewa muda wa kueleza.)"alisema Ernest na kuwatazama watu wale.
"Baba hapo umeua kila kitu yaani hawakupingi.. wakichomoa hapo basi tena!"ilisikika sauti ya Oscar masikioni mwa Ernest na kubaki akitabasamu tu kuona wako pamoja na rafiki yake.
Watu wale wakabaki kuangaliana tu maana kile kilicho ongelewa pale ni vilevile. Na kizuri zaidi ni kwamba amechambua kila kitu hadi maswali ambayo walitala kumuuliza. Yule mama mzungu alishindwa kujizuia kusimama na kuanza kumpigia makofi Ernest.
*"You are GENIUS. I like you...take his name*( Unaakili sana, nimekupenda... chukueni jina lake huyu.)"alisema mama yule na kauli ile ikamfanya Ernest atabasamu na kushukuru sana kwa kuambiwa vile. Hakukuwa na lengine la kuendelea na muda uleule wakachukua namba ya Ernest na kumweleza watampigia jioni ili kesho waweze kukutana pamoja na wenzake waliochaguliwa. Ernest alitoka mule ndani akiwa na furaha sana lakini furaha yake hakuweza kuionesha usoni mwake.
Alipotoka tu nje alisikia namba 28 akiitwa kuingia akajua ni Jenifer ndiye zamu yake. Haraka akamsogelea na kuvua ile miwani yake.
"Oscar msaidie huyu dada huko ndani pindi akikwama nampa miwani avae hii namuhitaji huyu."alisema Ernest.
"Haa Erne unafanya mambo gani tena?"aliuliza Oscer alishangaa kuona mwenzake anaingiza kazi myengine.
"Nina maana kubwa, we msave tu nakuomba sana."alisema Ernest na kumsogelea Jenifer pale alipo akijiandaa kuingia ndani.
"Naona umetoka tayari."alisema Jenifer.
"Yah nimetoka hakuna kigumu sana ni kujiamini."alisema Ernest.
"Okay sawa wacha nami niingie, baadae basi."alisema Jenifer na kupiga hatua mbele kuondoka Ernest akamshika mkono. Jenifer akageuka na kubaki kutazamana na Ernest ambaye alisogea karibu yake wakabaki kuangaliana. Kwa aibu na kuhisi utofauti Jenifer akatazama chini lakini Ernest akaunyanyua uso ule uliojaa aibu kisha akamvalisha ile miwani.
"Kuwa makini uingiapo huko ndani."alisema Ernest na kujenga tabasamu usoni kisha akageuka na kuondoka zake. Jenifer akabaki kumtazama tu asijue anamaana gani kusema vile.
Jenifer aliongoza njia na kuelekea zake ndani apo kama ilivyoada alipofika alikaa kwenye kiti baada ya kusalimia.
Walimtazama vile alivyo muonekano wake, uzuri na tabasamu lake usoni lilidhihirisha wazi ni msicha anaye jielewa.
"mambo yako"alisalimia yule mwanamama mzungu huku akiwa mwenye tabasamu baada ya kusalimia kwa Kiswahili
"mambo poa"alijibu Jenifer.
"okay the way ulivyo ningependa kujua undani wako hasa jina na lengo hasa la kuja hapa."alisema mmoja wa wale wanaume waliokuwa sambambana yule mama mzungu.
"ok asante kwa kunipa nafasi hii na ingependeza nikaanza kwa majina yangu. Naitwa Jenifer Franco from Kisumu."
*"Wooh from Kisumu to Nairobo is so far.* ( eh kutoka Kisumu hadi hapa Nairobi ni mbali.)"alisema yule mwanamama.
*"yah its so far but if you're intending to do something then the distance you see is just the same* ( ndio ni mbali lakini ukiweka nia ya kufanya kitu basi ule umbali unaona ni kawaida tu)"alisema Jenifer kwa kujiamini.
"safi sana,ukiwa na nia ni moja ya kitu kizuri. Hebu tueleze sababu hasa ya kuja hapa siku ya leo."
"sababu kuu hasa kufika hapa ni kutimiza lengo langu."
"kama nitafanikiwa kuchaguliwa basi tutaweza kuinyanyua juu kampuni ya MOLEN tukishiriana kwa pamoja katika suala zima la Tecnology."sauti ilipenya masikioni mwa Jenifer ambaye aliposikia akashangaa lakini kwa kujiongeza akafahamu huenda ni ile miwani aliyovalishwa na Ernest.
"kama nitafanikiwa kuchaguliwa katila usaili huu basi naamini kwa kushirikiana na jopo la wenzangu tutaweza kuinyanyua MOLEN kutoka pale ilipo na kuzidi kupiga hatua mbele zaidi katika suala zima la Technology."alisema Jenifer huku akiwa makini kwa kile alichoongea.
Aliulizwa maswali mengi sana ya kumjaribu kama anafaa lakini aliiweza kuyajibu kwa ufasaha zaidi akiwa anajiamini baada ya kuona kuna msaada anaupata kupitia ile miwani aliyovaa.
Baada ya muda Ernest akiwa zake nje kule aliwasili Mwalimu Otieno na kuungana naye.
"nimefanikiwa kupata nafasi, jioni ya leo watanipigia simu kunijuza kesho muda wa kukutana."alisema Ernest.
"taarifa nzuri, nahisi ni mwanzo mzuri wa safari yetu, kazo ni kubwa hapo mbele hivyo unatakiwa kuwa makini sana."alisema Mwalimu.
"ila kuna mtu nataka tuongozane naye katika hii safari, naamini atakuwa na mchango mkubwa sana hapo mbele."alisema Ernest na kitazama kule walipotoka watu kwenyw usaili.
*"whom one* (nani huyo?)"aliuliza Mwalimu Otieno na kimya kikatawala kama sekunde kadhaa.
Mlango ulifunguliwa na kutoka ndani Jenifer akiwa mwenye tabasamu moja kwa moja akaelekea mahala alipo Ernest ambaye muda wote alikuwa akimtazama hadi alipofika pale.
Alivua miwani ile Jenifer na kumpatia mwenyewe.
"awali nilikuwa sijaelewa ulikuwa na maana gani kusema niwe makini, ila nilipofika nikaelewa. Nashkuru sana Ernest, nimeweza kupass my interview kwa msaada wako, asante sana"alisema Jenifer na kumfaya Ernest atabasamu kuona mambo yameenda sawiya.
"usijali maisha ni kusaidiana Jenifer."alisema Ernest.
"okay wacha nikutambulishe, huyu ni anko wangu anaitwa Otieno, anko huyu ni Jenifer she is my friend."aliwatambulisha pale wakashikana mikono kama salamu.Waliongea mawili matatu kisha Ernest akatoka noti mbili na kumpa Jenifer kama nauli ya kurejea kwao maana alikuja kwa miguu hapo awali. Baada ya maongezi hayo wakaagana na Jenifer akaondoka zake.Mwalimu Otieno akawa anamtazama tu binti huyo hadi alipotokomea.
"nadhani atatusaidia hapo mbele Jenifer, ni msichana anaye jiamini sana."alisema Ernest kumfanya Mwalimu amtazame.
"ulimueleza chochote kuhusu kinachoendelea.?"
"atafahamu tu hapo baadae, turudi tukapange mikakati mengine"alisema Ernest na kuongoza njia kuondoka kisha Mwalimu akafuata.
Dar es Salaam, wale watu waliendelea kusaka kuhakijisha wanampata Ernest popote pale.Hii ni kutokana na kuhisi huenda akawa anajua mambo ya kaka yake Albert kuhusu zile password za faili la CSE.Kwa juhudi walizo zitumia na kuuliza uliza sehemu mbalimbali waliweza kufanikiwa kujua mtaa ambao anapatikana Ernest hivyo walielekea mtaani hapo na kuendelea kudadisi.
Walimsimamisha kijana mmoja kutaka kumuuliza.
"mambo vipi,"
"ah salama tu"
"aisee kuna kijana tunamuulizia, anaitwa Ernest ni mtaalamu sana wa mambo ya mitandao na teknolojia sijui unampata?"aliuliza mtu mmoja akiwa na wenzake watatu wakiwa makini kutazama huku na kule.Yule kijana kwa kuwatazama tu akajua si wema kwa jinsi walivyo tu.
"mh aisee mimi bado sijazoeana na watu hapa mtaani si mwenyeji sana, ila vijana wa maswala hayo ya mitandao wanapatikanaga mitaa ile kule mbele.Huenda mkienda kuwaulizia kule wanaweza kuwafahamisha."alisema yule kijana.
"dah poa kijana tunashkuru kwa kutuelekeza, zuia hii "alisema yule jamaa na kumpa yule kijana noti ya elfu Tano kisha akaondoka na wenzake kuelekea kule walipoelekezwa.
Yule kijana alibaki akiwatazama tu wanapoenda kisha akageuza kurudi nyuma na kuanza kukimbia.Ni Oscar ambaye muda mfupi alikuwa akiongea na watu wale na kuzawadiwa elfu Tano.Alifahamu kuwa hawakuja kwa heri hivyo aliamua kuwapoteza njia kwa makusudi .
Dakika kadhaa alifika chumbani kwake na kianza kuchukua kila kitu muhimu cha kubeba na kuweka kwenye begi lake la mgongoni haraka haraka kisha akachomoa chomoa nyaya za baadhi ya vifaa na kuviangusha kusudi isijulikane kulikuwa na mpango gani unao endelea. Alipohakikisha ametenda hayo aliondoka zake na kutokomea mbali na mtaa huo. Hata alipofika mbele aliweza kumtumia ujumbe Ernest kuwa huku kuna watu wanamtafuta amekimbia pale wanapoishi.
Huku nyuma wale watu waliweza kuelekezwa anapoishi Ernest hivyo walipiga hatua hadi walipofika kwenye chumba kile wakabisha hodi zaidi ya mara tano bila kujibiwa.Walitazama na kuona bora wauvunje tu na dakika chache wakafanikiwa kuvunja kwa kupiga mateke kitasa kikaachia.Walipofika ndani walishangaa kuona vitu vipo shagala bagala mule ndani.Wakaanza kupekua pekua kutafuta chochote ambacho kinaweza kuwasaidia.Mmoja wao alisogea kwenye zile nyaya pale na kutambua kuwa zilikuwa ni nyaya za mawasiliano ya kuunganisha.
Walizidi kupekua pekua na kukuta kuna ramani za nchi ya Kenya huku ikiwa imechorwa baadhi ya sehemu na kuwekewa alama.Wakaanza kuhisi kuna jambo huenda lilikuwa linaendelea.
"oya hii picha si ya yule dogo tuliyo muuliza muda ule?"aliuliza mwenzao mmoja baada ya kupekua na kufanikiwa kuiona picha ya Oscar.
Wenzake walipoitazama ile picha walishangaa na kuona kumbe walimuuliza mtu ambaye ndiye angewaambia wapi alipo Ernest.Walikasirika sana na kuamua kutoka kuondoka haraka kujaribu kama wataweza kumuwahi Oscer huku wakiwana ile ramani ya Kenya waliyoikuta mule ndani.
Ndani ya gereza la Oregon,harakati za kumtia mikononi Arbert ili waweze kumpa kipigo kundi la DEVIL MOB ziliendelea.Kama walivyopewa oda hiyo na mkuu wa jela hivyo hakuna yeyote wa kumzuia.
Siku hiyo askari alimchukua Albert na kumpangia kufanya usafi maeneo ya chooni.Bila mwenyewe kuelewa kuwa kuna njama za yeye kuwekwa kati na kundi la DEVIL MOB zinaenelea. Alianza kusafisha kule chooni lakini alishangaa sekunde chache tu wanaingia watu mule chooni wakawa wamemzunguka kumuweka kati iwa ameshika ufagio wake akiwa kwenye usafi.
Ilimbidi asimame kwanza na kuwatazama watu wale na kukutana na sura ngeni ambazo ndio kwa mara ya kwanza anaziona tangu aingie gerezani pale.
*"who are you ?* (nyie ni nani?" aliuliza Albert na kuwafanya watu wale waliokuwa watano watabasamu na kuanza kucheka.
Watatu kati yao wakaanza kuvua nguo zao na kuonesha tupu zao kumaaisha wanataka wamuingilie kimwili Albert.Taratibu waaanza kumsogelea hadi pale na mmoja wao akamshika bega kutaka kumvuta lakini aliona ngumi nzito ikitua kidevuni kwake na kumfanya adondoke zake chini huku damu mdomoni zikimtoka.Wenzake walipoona vile hasira zikawapanda wakaanza kumfuata Albert kwa pupa, aliona ngoja awafundishe adabu siku hiyo wazungu hao ambao wamekuwa wakizoea kuona mtu mweusi wakimdharau na kuona ni kama yule James ambaye ni mwanaume aliyezoea michezo hiyo.Dakika kadhaa tu kila mtu kwenye kundi lile aliweza kutoka ngeu kwenye mwili wake na kuona njia rahisi kunusuru miili yao kuzidi kuumizwa wakatoka mbio na kumuacha Albert pale akiwa anawatazama.
"was....e nyie wazungu mnakimbia nini njoeni sasa mnaona kila mtu shoga!"aliongea kwa hasira sana Albert baada ya kuwashikisha adabu vijana wale.
Alikamata ufagio wake na kuendelea na kazi yake ya usafi lakini gafla tu akaona kuna watu tena wanasogea kwake.Aliponyanyua uso wake akipata kuona sura za kundi la DEVIL MOB wakiwa wamesimama nao wakimtazama huku sura zao zikiwa zimenuna.
Taratibu wakaanza kumsogelea hadi pale aliposimama waiongozwa na mkubwa wao aliyeonekana kutoboa pua na kuweka kipini.
*" here are two you need to choose from these settings.. just tell us the CSE password we will leave you or play a blow when you say in mandatory.* (hapa kuna mawili unatakiwa kuchagua moja kati ya haya.. utuambie tu password za CSE tutakuacha au uchezee kipigo huku ukisema kwa lazima.)" alisema mkuu wa kundi ajiwa amemsogelea kabisa kwa ukaribu Albert ambaye alikiwa ameshikilia tu fagio. Kitendo cha kuambiwa tu vile akajua hili swa tayari limeshakuwa kubwa hadi makundi haya yanafahu na kupewa kazi ya kumbana yeye.Kwa jinsi swala hilo lilivyo na maana kubwa akajua hawa wamekuja kwkujiandaa kikamilifu siku hiyo.
Alitupa macho pembeni na kuwatazama wengine ambao walikuwa wakijiandaa wakinyoosha mikono yao vyema kwaajili ya kumfanya mtu kitu kibaya. Hakuwa na hofu nao hata kidogo na kila akimtazama yule mkubwa waona kuiona ile tatoo iliyo shingoni ikimkumbusha tukio la nyuma, ilibidi baye amsogelee kabisa usoni yule baunsa wa DEVIL MOB.
*" I need more detailed information to ask for your fellow stupid guys who have the tattoo where they are located.* (Nahitaji maelezo ya kina zaidi unitajie malaya wenzako wenye hiyo tatoo wanapatikana wapi.)"alisema Albert kwa kujiamini saa ha yule jaa akashangaa. Ilimbidi ageuke nyuma kuwatqzama wenzake na kuanza kucheka kwa dharau.Hawakuwahi kudharauliwa kiasi hicho na mfungwa yeyote mule gerezani hivyo matusi anayopoka Akbert kwao ilikuwa ni fedheha kubwa sana.
*"let show you who we are* (ngoja tukuoneshe sisi ni nani)"alisema yule na kurusha ngumi nzito kueleakea usoni mwa Albert mbaye kwa wepesi wa aina yake aliikwepa na kusimama sawiya.Wale mabaunsa wakqqnza kuja sasa kumchangia Albert ambaye alikuwa fiti akitumia mti wa ufagio kuwasurubu kama watoto. Hawakuwa wenye lujua kupambana kwa ngumi au mateke wao walikuwa waitumia staili mieleka kumzoa mtu na kumtupia mbali lakini kwa akili za Albert aliweza kuwamudu kuwakwepa kwepa na kila aliyesogea alichezea fimbo kadhaa za uso na mbavuni. Hadi mwenyewe akabaki kusikitika na kuona kumbe watu waawaigopa kwa miili tu waliyonayo lakini hawana kitu.
Hasira ziliwapanda na kuona ni dharau kubw kwao kupigwa vile, wakaanza kutumia silaha zao wakatoa visu kwa kujihami. Albert kuona vile akajua sasa awe makini nao maana waweza kumbana wakamuua kweli.
Walikuja na nguvu mpya ya kushambua wakawa wanaenda wawili wawili wakimchanganya Albert kwa staili yao na kufanikiwa kumchana mkononi.Maumivu aliyo yasikia muda ule yalimfaya aanze kuzuia mashambulizi kwa kuweka umakini wa hali ya juu. Gafla akatokea Simon akiwameshika biblia yake.
*"hey guys what's going on?* (oya kuna nini kinaendelea hapa?)"aliema Simon na kusogea pale.Alipomkaribia Albert amkuta ana jeraha mkononi mwake.
"Albert.. uko salama?"aliuliza Simon bila kupata jibu kamili.Albert alikuwa akihema kwa purukushani za mpambano.
Simon aliwageukia wale DEVIL MOB na kujenga tabasamu.
*" It's enough now to stop, the battle is not good for us and we need to live by lov...*( inatosha sasa muacheni, kupigana sio kuzuri kwetu na yatupasa tuishi kwa upe...)" hakumaliza sentensi yake alishangaa anapelekewa kisu shingoni naye haraka akakwepa na kurikia pembeni.Hawaitaka kuikiliza mahubili yoyote maana kipigo walichopata kutoka kwa Albert kimewafanya wajione kudharauliwa sana. Hawakifikiria tena swala la kumpiga wambane aongee kuhusu zile password bali kwa sasa walitaka kummaliza kabisa Albert.Naye japo aliumia mkono kwa kukatwa lakini hakuwa haba kwenye kujibu msshambulizi na kuzidi kuwaa wakati mgumu kundi hilo.
Simon akibaki kutaza tu na kuona jinsi kundi lile linavyozidi kumuandama mwenzake.
" Baba uliye mbinguni, nakuomba nisiikaribie hii zambi tena nilitubu kwako kutoendelea kuyatenda haya, Eimen."alisema hayo Simon na kuibusu biblia yake huku kelele za mpambao ule ukiendelea kundi like likizidi kumuandama Apbert ambaye taratibu alianza kupunguza kasi ya mashambulizi akawaaruhusu baadhi ya visu kumchana.Akawa anawachenga na kuwakwepa sasa ili kuwachosha lakini wanaume wale walizidi kusogea.
Hali ile hata Simon aliiona na kujua wanazidi kumuandama mwenzake.Akajikuta anashindwa kuvumilia toba yake na kuamua kuingilia kati akasimama mbeke ya Albert kama kumkinga asiendeee kufuatwa.Walipomuona amesimama mbele ya mtu wao wakajua naye anataka kumtetea, walimsogelea Simon na kutaka kumsumia huko lakini haikuwa rahisi.Alirusha teke mo na kumfanya adondoke chini yule baunsa mmoja aliyemsogelea. Wenzake kuona vile wakajua kumbe wapo pamoja wacha wawape kipigo wakaanza kuwavamia kwa silaha zao mikononi ambazo zikufua dafu kwa Simon ambaye alikuwa mwepesi zaidi ya maelezo na kufanikiwa kumkwapua mmoja wapi kisu akakishika yeye mkononi huku akiwa amesimama.
Waliangaliana na kuona wana kazi ya kupambana na mchungaji huyo.Walitoka wote kwa pamoja na kumvamia kwa nguvu zote wakamtupa huko Simon aliyedondokea kwenye maji machafu huku kisu alichokuwa ameshika kikitupwa mbali.Alinyanyuka haraka ja kuona wanakuja tena, Albert kuona vile akanyanyua ufagio mmoja na kumrushia Simon ambaye alupoupata tu akaanza kuutumia kuwapa kipigo wabaya wae.Albert naye akapata nguvu ya kuendelea na pambano hilo wakawa wanawashikisha adabu kundi lile jama robo saa. Walipoona hali inazidi kuwa ngumu kwao kundi la DEVIL MOB wakaona bora wakimbie tu maana wameingia sehemu siyo.Albert alibaki kuwatazama tu wakiondoka huku waiwa wanachechemea kwa kipigo walicho kipata.
BONYEZA MAANDISHI HAYA KUSOMA MAKALA ZA AFYA
INAENDELEA
0 Comments