Walitoka chumbani mule na kuanza kutembea kweye korido ndefu kuelekea chini ili waelekee huko walipoambiwa.Mmoja wao akamshika mkono Ernest wakiwa wanatembea kusudi isijulikane kama wamemteka. Wakiwa wanatembea Ernest alishangaa kumuona mwalimu Otieno akiwa mbele kabisa anakuja hivyo lazima watapishana pindi wakipita. Na mtu pekee ambaye alihisi ndio atakuwa msaada kwake ni mwalimu huyo maqna jinsi alivyoshikwa hakufikiria kama swala lake la kuwakimbia watu hao litafanikiwa.
Walikuwa wakitembea tu bila kumfahamu mwalimu huyo ambaye alipowakaribia akaanza kuwattazama na kusimama.
"ooh Ernest vipi mbona una jeraha kwa noise?"aliuliza Mwalimu Otieno akamshika mkono Ernest na kumbinya kidogo. Wale watu hawakutaka kufanya lolote wakamtaiti Ernest kwanyuma asiongee lolote lililo tokea, walisubiri mtu huyo aongee na mtu wao kisha waendelee na safari yao.
"ah tunaelekea kwa hospital nimepata accident hivyo naenda kupata huduma."alisema Ernest na kumfanya mwalimu aamini kijana huyo hayupo kwenye mikono salama.
Aliwatazama wale watu kwa makini wakionekana hawana habari wamesimama sawa na Ernest akajua namna ya kufaya na gafla akiwa na wepesi wa hali ya juu akarusha teke moja na kumuangusha mmoja wa wale watu kisha akamuwahi pale chini juipiga teke bastola aliyokuwa nayo yule mtu na kusimama wakawa wanaangaliana. Ernest kuona hivyo naye akageuka kwa weledi mkubwa na na kumtia kifuti cha tumbo yule aliyekuwa amemshika na kuanza kupambana naye kwa mkono.
Ilikuwa ni piga nikupige kwa watu hao wanne kila mtu akipambana na mwenzake.Mwalimu Otieno alikuwa fiti amekamilika kilq idara hivyo hakusumbuliwa hata kidogo dhidi ya yule mtu aliyekuwa akipambana naye ambaye aliishia kichezea kichapo kikali bila huruma.Alijitahidi kujibu mashambulizi lakini haikusaidia kitu na mwishowe alikamatwa kikamilifu na kutiwa mikononi mwa mwalimu ambaye hakutaka kupoteza muda akamnyonga bila huruma na kumfanya adondoke chini kama mzigo.Aligeuka kumtazama Ernest ambaye akionekana kupambana na yule mtu..Hakika alikuwa mwepesi sana kwenye kurusha mateke ki iliyomfanya adui yake ashindwe kumudi kuzuia baadhi ya mapigo. Mwalimu Otieno hakutaka kupoteza muda naye akiingilia kati pambano hilo wakawa wanamchangia yule mtu ambaye aliona ni wazi anazidiwa lakini alishachelewa kuchukua uamuzi wa kuyaokoa maisha yake maana alisikia ngumi nzito ikitua jichoni hadi akaenda chini na kuanza kuugulia maumivu. Ernest raka akamuwahi pale chini na kumkwida amueleze ukweli wametumwa na nani.Akiwa kwenye tukio hilo mwalimu alisogea na kumnyonga yule mtu haraka.
"tuondoke haraka hapa kuepuka kesi hii."alisema Mwalimu ns haraka Ernest arejea chumbani kwake kuchukua vitu vyake wakaondoka mule Hotelini na kuelekea Hotel aliyopanga Mwalimu Otieno. Hadi wanafi hakuna aliyefungua mdomo wake kuongea huku Ernest ajimtazama tu mwalimu yule maana hakutegemea kama anauwezo wa kupambana kiasi kile. Walipofika waliingia zao ndani na huko ndipo Ernest akashangaa pindi alipoingia na kukutana na vifaa kadhaa ambayo alikuwa ajivitumia kumtazama mwalimu huyu pindi akiwa kwenye chumba chake.Akajua kuwa kumbe hata yeye alikuwa akitazamwa.
"ulijuaje kama nilikuwa nimevamiwa maana sikutegemea kama nitapata msaada wako mahala pale."aliuliza Ernest huku mwalimu yule akichungulia dirishani kuuangalia chini maana wapo juu gorofani.
"kila siku nimekuwa nikikuchunguza tu tangu siku ya kwanza uliponipoka vitabu vvyangu. Hata leo nilihisikuna watu wanatufuatilia nyuma pindi tulipokuwa tunatoka darasani hadi kufika huku,niliwaona wakifunga mapazia ya dirisha lako nikajua kuna jambo linaendelea ndio maaana ukaniona nimefika pale."alisem yule mwalimu na kugeuka kumtazama Ernest aliyekuwa naye akimuangalia mwalimu.
Mwalimu Otieno akatoa bastola na kuielekezea kwa Ernest.
"wewe sio mkenya hebu niambie, wewe ni nani? na umekuja Kenya kufanya nini?"aliuliza mwalimu Otieno huku akimuweka chini ya ulinzi kijana Erne ambaye kuona hali ile ilimbidi tu afunguke.
"ni kweli mimi ni mtanzania, Ernest Gama ndio jina langu, nimekuja Kenya kwaajili yako lengo ni kutaka msaada kutoka kwako Otieno.Nilikifahamu toka awali kuwa wewe ulikuwa mfungwa ndani yq gereza la Oregon nchini Marekani na details zako zote nazifahamu hivyo nikaona utakuwa ndio msaada mkubwa kwangu kufanikisha zi yangu."alisema Ernest kijana mwenye umri wa miaka 23.
"yote hayo kuhusu mimi uliyajuaje? na kazi gani unayotaka wewe ukinihusisha mimi?"alisema Mwalimu Otieno na kumfanya Ernest akae kwenye kiti angali ameoneshewa bastola, alishusha pumzi kidogo na kuendelea.
"nina kazi mbili mbele yangu nahitaji kuzikamilisha, kuhusu kukufahamu wewe ni jambo la kawaida tu maana nipo na mwenzangu kwenye hili na tunashirikiana kikamilifu kuyamudu haya yote.Sisi tuna taaluma ya kucheza na kompyuta kutafuta data na documents za watu mbalimbali na ndio maana tukakutafuta wewe na kujua ulifungwa gerezani Oregon miakq 15 na mwaka juzi ndio umetoka hivyo nikahisi una mambo mengi unayajua kuhusu gereza hilo.Ndai ya gereza hilo yupo ka yangu amehukumiwa miaka 15 jela tena kwa kosa ambalo sio lake, hakutenda yeye. Pointi yetu ni kutaka kumtoa kaka yangu ndani ya gereza hilo maana kuna japo ambalo yeye anakifahamu na inahitajika mapema sana kufanyika alifanye."alisema Ernest akionesha kuwa siriasi.
Mwalimu Otieno alimtazama kijana huyo na maneno aliyoongea akaona ni tofauti hamuamini.
"usifikirie kutoka gerezani ni kazi rahisi tu kama unavyodhani wewe . Kule ni sawa ja kujitolea kufa yaani ukikamatwa unatoroka basi kifungo chako kina double."
"usiongelee swala la kufeli Mr.Otieno.. hakuna anayeombea hayo shida sisi ni broo aweze ku escape ndani ya gereza lile. Yeyw akitoka ndio kila kitu kinaenda sawiya naamini hata wewe utakapo kubali kushirikiana nami kuna fungu noni utalibeba baada ya kazi hii. Naomba ukubaliane nami kufanikisha hili nakuhakikishia kukupa utajiri."alisema Erneat akiongea kwa kujiamini sana.
Mwalimu alipomtazama jinsi kijana anavyoongea kidogo akaanza kumuamini, aliteremsha bastola yake na kuiweka kweye kiti baada ya kujiridhisha kuwa kijana huyo si mtu mbaya.Akashuka na kukaa naye kwenye kiti.
"hili swala nila kujitoa kimasomaso maana ni zaidi ya hatari.Nilishaamua kutulia na kuendela na kazi yangu ya ualimu na naendelea vyema hadi kuwaajiri wenzangu tunasaidiana. Unishaniwishi kufanya hayo lakini hadi nipate uhakika wa malipo yanakuwaje."
"hilo ondoka shaka."alisema Ernest na kusogeza begi lake akafungua zipu na kutia kitita cha noti za dola za kimarekani na kumpatia mwalimu. Alipozipokea akaamini sasa swala hili lipo siriasi kweli, alinyanyua macho yake na kumtazama Ernest.
"sawa tutakuwa pamoja"alisema Mwalimu Otieno na kumfanya Ernest atabasamu baada ya kusikia hivyo.
Upande wa pili ndani ya gereza Albert alikuwa sambambana wenzake kila sehemu wanayo kwenda. Siku hiyo wakiwa kwenye kazi ndani ya gereza hilo wakipangiwa kupasua magogo ya kuni pamoja na wafungwa wengine wengi.Miongoni mwa hao walikuwemo kundi la DEVIL MOB ambao wao waijitenga na kufanya kazi kivyao huku askari zaidi ya kumi wakiwa wana wasimami wafungwa kwenye kazi hiyo.
"Yaani wale majamaa hawataki kabisa kushirikiana na wenzao kwenye kazi wanajiona ndio wafalme ndani ya gereza hili."alisema mrusi Johnson akiwa amelowa jasho kwa kazi ya kupasua magogo makubwa.
"na wakichoka wao wanaacha hawaguswi na mtu wale, tazama askari wote wanatusimamia sisi lakini wale wapo free."alisema Simon wakimweleza hali halisi Albert ambaye alikuwa akishuhudia hayo huku akiendelea kukata kuni.
Huku muda mwingine akiendelea kusoma ramani tu ya gereza lile na jinsi ulinzi unavyoendelea kila wakati.
Baada ya masaa kadhaa walimaliza kazi na kuelekea kupumzika kidogo. Johnson na Albert wakaelekea zao maliwato kujisaidia baada ya kutoka kufanya kazi ngumu.
"kwahiyo sasa Albert mpango wako upoje sasa wa ku escape humu.. una ramani kamili ya kutoka humu maaa huo mpango hata mimi umenigusa kwa kweli.. *i miss my family* (nimeikumbuka familia yangu."alisema Johnson kwa sauti ya chini wakiwa kule chooni.
"usijali Joh mambo yakiwa sawa nitakushtua."alisema Albert akimpa moyo mrusi.
Kwa mbali wakasikia mtu akiugumia kama bata, walistuka kidogo na kuamua kutoka kule chooni wakaanza kuusogea kusikia sauti hiyo inapotokea.Kila wanapozidi kupiga hatua ndio kelele zile zinapozidi hadi walipofika eneo husika Albert alishangaa kuona tukio lile ambalo hakutegemea kabisa.
"*fuc... bitch* kumbe ni huyo malaya wa kume, tuondoke Albert."alisema Johnson na kugeuka kuongoza njia kuondoka.Albert alibaki kushanga tu haamini kumuona kijana mwenye asili ya kiafrika akifanywa kinyume na maumbile kwenye korido ya vyoo. Hakutaka kuendelea kuangalia aligeuka ja kuondoka zake akiongozanaja Johnson.
"anaitwa James ila mwenyewe anapenda kuitwa Jamie.. ni shoga mzoefu humu gerezani kila mwenye hamu ya kufanya mapenzi anamfuata yeye. Anawatukanisha sana waafrika wenzake humu gerezani na kuonekana wote ndio tabia zao.Mshenzi sana yule."alionhea Johnson akimueleza Albert kuhusu yule sho waliomkuta kule chooni.
"dah unajua naonaga tu kwenye muvi kumbe haya mambo yapo aisee."alisema Albert akiwa haamini.
"ndio hivyo kama ulivyoona, akimaliza pale anapewa hela kidogo au atapeliwe,kashazoea"alisema Johnson na kumfanya Albert azidi kusikitika wakielekea zao kwenye sero yao na kumkuta Simon akiwa ameshika biblia akijisomea. Hawutaka kumsumbua wakamuacha na wao wakapanda vitandani kupumzika.
Dakika chache mbele kupita alikuuja askari mmoja kwenye sero yao na kugonga kirungu chake kwenye nondo za sero ile kuwashtua.
"*prisoner no.417 hurry up get out and follow me* (mfungwa namba 417 toka nje haraka na unifuate)"alisema askari yule na wote wakamtqzama Albert ambaye ndiye mwenye namba hiyo kwenyw sare yake.
Bila kuchelewa alishukq kitandani na kuwaaga wenzake akaongozana na yule askari kuelekea asikopajua.
Walienda moja kwa moja kwenye ofisi ya mkuu wa gereza na alipofik tu akamuona Mkuu huyo akiongea na simu, ikabidi asimame kumsubiri akiongea na sekunde kadhaa mkuu yule aakampatia simu ile Albert ikiwa hewani.
"*talking to this person* (ongea na huyu mtu)"alisema yule mkuu wa jela Albert akaipokea ile simu ja kuiweka sikioni bila kusema lolote.
"hellow Mr.Albert.. Mambo vipi, ni mimi Mr.Alexa naongea hapa nadhani jina hili sio geni kwako."ilisikika sauti ile iliyopenya sikioni mwa Albert ambaye baada ya kusikia jina hilo alishangaa sana.
Ikambidi ashike simu vizuri baada ya kuitambua sauti ile.
"Naona upo ndani ya suti mpya ya miaka kadhaa ambayo huwezi kuivua ipite siku. Haya yote uliyataka wewe mwenyewe kujifanya mjanja wa kutupatia password feki ambazo sio tulizo hitaji. Jueri yako ndio hiyo miaka 15 ya Oregon ni sawa na kifo tu maana mambo utakayoyapata humu ni zaidi ya unavyodhani." alisema Mr.Alex kwa kujiamini sana.
"Mr.Alex... ni muda sana sijaisikia sauti yako, kitendo cha kuisikia tu nimejichafua kwa jinsi ilivyo nisisimua."alisema Albert kwa dharau kumtusi kimafumbo Mr.Alex ambaye alicheka tu kwa dharau.
"Okay nadhani bado hujakaribishwa ndio maana, nimekupigia ili uniambie zile Password kwa mara nyengine ili tufanye mpango wa wewe kukutoa humo gerezani. Ila kama bado utakuwa jeuri sawa endelea na miaka yako 15 ya kutumikia gerezani."
"Labda nikwambie tu Mr.Alex. Sahau kuhusu password hizo kamwe hamtazipata. * You have killed my girlfriend you think I'll leave you alive?* ( Mmemuua mpenzi wangu unafikiri nitawaacha muishi?). Hapana sitavumilia haya."alisema Albert kwa uchungu sana.
"Hahaha hahahaha usinichekeshe bwana mdogo. Hivi nani kakwambia unatoka humo leo au kesho? Eti ulidhani ni mchezo wa kuigiza kukaa humo, yaani wewe kaa uhesabu kuwa hayo ndio maisha yako hadi ukamilishe kifungo chako lini sijui, by the way kaa fikiria ukiona msoto ndani Oregon unazidi usisite kumfuata mkuu hapo uongee na mimi tupeane makubaliano ili utolewe, nikutakie siku njema."alisema Mr.Alex na kukata simu. Albert akashusha simu ile na kuiweka mezani kisha akageuka kutaka kuondoka Mkuu wa jela akamshika mkono.
"*Think twice about what you were told, otherwise you will die in Origon* ( Fikiria mara mbili juu ya kile ulichoambiwa, laa sivyo utakufa humu Origon.)"alisema Mkuu huyo na kumfany Albert amkate jicho la aina yake.Aliutoa mkono wake na kuondoka zake akisindikizwa na askari baada ya kuona wanamchanganya tu.
Hata alipofika sero kwa wenzake alijitupa kitandani na kutafakari maongezi yale waliokuwa wakiongea na Mr.Alex. Hali ile ilimpelekea kukumbuka tukio la nyuma siku ambayo alimpoteza mchumba wake baada ya kuvamiwa na watu ambao alipata kufahamu kuwa walitumwa na Mr.Alex. Alijawa na hasira sana kila akifikira kuwa yupo jela kwa kusingiziwa kuwa amemuua Angela kipenzi chake hali ya kuwa waliofanya jambo hilo wapo uraiani na bado wanamuqndama kutaka awatimizie jambo lao. Alikumbuka siku ile jinsi alikubali kuwaonyesha zile password za faili la CSE ambalo linasadikika kuwa na mambo muhimu sana na badala yake aliwapa Password ambazo ziliweka kuingiza data zengine ndani ya lile file baada ya lisaa kupita hivyo walipompiga Albert usiku ule akazimia wakaanza kumtengenezea kesi ya mauaji kisha wakapiga simu Polisi waje na wao wakaondoka eneo ya tukio baada ya kumshikisha bastola iliyotumika kufanya mauaji ya mrembo Angela. Walijua wamefanikiwa kupata zile password hivyo walipoondoka eneo lile na kwenda kumuonesha boss wao ambaye ndiye Mr.Michael hali ilibadilika baada ya kufika na kufungua faili hilo kukuta kuna data za biashara ya midoli hali iliyomfanya Mr.Alex apaniki.
Yote hayo alikuwa akijenga picha Albert na kuhisi huenda ndivyo walivyomfanyia hadi kuja kupata kesi hiyo ya mauaji japokuwa amewapatia kwenye kuwalaghai kuhusu password. Aliingiza mkono mfukoni na kutoa flash iliyokuwa na neno CIE. Aliitazama kwa muda na kushusha pumzi kidogo kisha akairudisha kwenye mfuko wa suruali aliyovaa.
"Wamekuitia nini hawa watu?"aliuliza Simon akiwa juu kitandani amejilaza.
"Kuna fala mmoja alipiga simu, ni mtu ambaye amenifanya niwe hapa saahizi."alisema Albert.
"Ah sasa bado anataka nini kutoka kwako angali amekufanya unateseka gerezani?"
"Na bado wataendelea kunifuatilia sana, kuna kitu wanakitaka kutoka kwangu hivyo sidhani kama wataacha kunifuatilia."alisema Albert na kumfanya hata Johnson akae vizuri.
"Albert huoni ni danger kwako kukufuatilia hivyo, they can kill you (wanaweza kukuua)."alisema Johnson.
"I dont think that they can.( Sifikirii kama wataweza). Maana wakiniua hawatapata wanachokita, na naapa hawataweza kukipata hicho wanachokitaka abadani."alisema Albert ajiwamwe kujiamini sana, wenzake wakabaki kuangaliana tu hawajui ni kipi hasa kinacho takiwa na hao watu.
Nchini Kenya Mwalimu Otieno alikuwa na kijana Erne wakiwa chumbani wametandika ramani ya jengo la kapuni ya M O L E N pamoja na ramani ya gereza la Oregon.
"Kesho usaili wa kuwatafuta vijana wa kujiunga na kampuni ya MOLEN unaanza asubuhi. Hivyo njia peke ya kufika America kwa urahisi hadi kuingia kwenye gereza hili ni kufaulu kwenye interview hiyo ya kesho ukifanikisha hili basi kazi itakuwa simple ya kumalizia mambo mengine na Albert aweze kutoka gerezani. Lakini endapo tukifeli ukakosa nafasi ya kuchaguliwa basi tutaanza kazi hii mwanzo kabisa hadi kuandaa mbinu upya za kuingia kwenye gereza hilo."alisema Mw.Otieono akimpa maelezo Ernest jinsi mambo yanavyokuwa.
"Hadi nimekuja huku Kenya njia ilikuwa ni kupata nafasi ya kuchaguliwa na kampuni hii. Nawafahu fika jinsi wanavyopata tenda mbalimbali kutoka kweny gereza la Oregon hivyo naamini kupitia kampuni hii nitaweza kuingia Oregon nikafanya kitu mule kumsaidia bro."alisema Erne na kumfanya Otieno atabasamu.
"Napenda unavyo jiamini, kweli wewe ni Mbongo."alisema Mwalimu huyo na kumfya hata Erne atabasamu.
Basi jioni ya siku wakawa wanapena njama na namna ya kulimaliza swala la kesho huku Ernest ajiwa makini kusikiliza masa Mwalimu huyo ni mtaalamu wa mambo mengi sana.
Usiku huo upande wa pili Mr.Michael akiwa kwenye kampuni yake ya CSE alikuwa akisimamia wafanyazi wake ambao muda wote walikuwa kwenye mashine na kompyuta zao wakihaha kutafuta na kujaribu Password ambazo zitaweza kufungua faili la CSE. Faili ambalo lina mambo mengi ya siri na haijulikani imekuwaje Password hizi anazijua mtu mmoja tu ambaye ni Albert.
Wafanyakazi walizidi kupekuwapekua kila sehemu hadi kuamua kumtafuta Albert na kujua maisha yake kwa undani zaidi.Wakapata kufahamu kuwa ni Mtanzania na ni raia pia wa Marekani kwakuwa alikuwa akiishi na mrembo Angela ambaye alimtafutia uraia huo mpenzi wake Albert. Katika kutafuta familia yake wakapata kuona kujua mtu huyo ana pacha wake anayeitwa Ernest ambaye yupo Tanzania na ni mtu wa masuala ya IT ( Information Technology) . Walipofahamu wakajua kuwa kwa namna yeyote ile Ernest atakuwa anaelewa kitu kinachoendelea juu ya kaka yake hivyo Mr.Alex akaanza kuwasiliana na watu wake nchini Tanzania waanze kumsaka kijana huyo wajue alipo wamkamate na kumbinya kisawasawa aongee ukweli.
FANYA HIVI KUFANIKIWA KWENYE BIASHARA
INAENDELEA
0 Comments