MEANDIKWA NA : HEMED MAYUGU
*********************************************************************************
Kama uliwahi kusoma na kutazama Tamthilia za Kifalme ambazo ziliisha bado ukitamani kuendelea basi hii siyo ya kuacha. Ni liwaya ambayo ilitungwa na Mtunzi mashuhuri kwa Jina anaitwa James Velvedo kutoka katika Taifa la Ujerumani.
Hii ni Liwaya nzuri iliyobeba mafundisho katika jamii. Liwaya hii inahusu utawala wa Kifalme.
Iyumbwi ni falme ambayo ilikuwa na nguvu sana miaka 100 nyuma, ni Ufalme ambao Watu wake waliishi kwa amani huku wakiamini kuwa Mungu alikuwa pamoja nao. Ufalme wa Iyumbwi ulikuwa umegawanyika katika Vijiji vingi. Upande wa Mashariki Ufalme wa Iyumbwi ulikuwa imepakana na inchi nyingine tena ya Kifalme ambayo ilijulikana kama Nghumbi. Halafu upande wa Kaskazini ilikuwa imepakana na Mto mkubwa wa Chibaya, Mto ambao ulikuwa kama mpaka uliokuwa unatenganisha falme ya Iyumbwi na Falme ya Chutema. Inasadikika kuwa katika Falme zote ambazo ziliwahi kutokea katika Uso wa Dunia, Falme ya Iyumbwi ndiyo Falme pekee ambayo ilikuwa na Jeshi kubwa na lenye nguvu hasa. Falme za Jirani ziliamini kuwa Falme ile ilikuwa imeteuliwa na Mungu, Kwasababu ilikuwa imebalikiwa kuwa na kila kitu kilichohitajika. Watu wa Taifa lile teule la kifalme hawakuwahi kukumbwa na majanga yoyote Hapo Kabla lakini walikuwa mahasimu wakubwa sana wa Falme ya Jilani ya Ngh'umbi.
Kama ujuavyo mabadiliko huwa yanatokea kila wakati. Kama hivyo, kuna mambo mbali mbali yalianza kujitokeza katika Falme ya Iyumbwi na kusababisha Falme ile kufa kabisa na kutengeneza Taifa moja kubwa ambalo liliziunganisha Falme za Nghumbi pamoja na Falme ya Iyumbwi na kuiita Falme ile kwa jina moja la Ng'umbwi. Falme ile ilikuwa chini ya Mfalme CLEOPA pamoja na Malkia aliyejulikana kwa Jina la Sophia.....unataka kujua ni nini kilisababisha Taifa kubwa la Kifalme la Iyumbwi kufa? King CLEOPA alifanikiwa vipi kuziunganisha Falme mbili zilizokuwa mahasimu. CLEOPA alikuwa nani na changamoto zipi alikutana nazo katika zoezi hilo zito la kuunganisha Falme? Kwanini iliitwa Notification from the Dream?
Fuatilia kisa hiki cha kusisimua.
SONGA NAYO
Ilikuwa ni katika kikao, Zayoni Mfalme wa Taifa la Iyumbwi, ambaye wakati huo alikuwa katika wakati wa Mwisho kabisa wa kulitawala Taifa lake, alikuwa amelikusanya baraza lake la Mawaziri pamoja na Makatibu mbali mbali katika Falme yake. Kikao hiki kilikuwa cha muhimu sana kwake. Alikuwa ni Mfalme aliyependwa sana na watu wake, na walimuhusudu sana.
"Jamani hiki ni kikao changu cha mwisho kwenu Mimi nikiwa kama Mfalme. Ufalme huu nitauacha kwa Mwanangu wa pekee Prince Yolam!"
Mfalme aliitamka jina la kijana wake ambaye mpaka wakati huo alikuwa kaisha tangazwa na kuvishwa taji la Crown prince (mfalme mtarajiwa)
Katika kikao hicho Prince au Mwana wa mfalme naye likuwepo akisikiliza.
"Mimi kesho natakiwa niondoke hapa kwenda kuiaga miungu ili Kesho kutwa tuwe na Sherehe za kumsimika Mfalme mwingine wa Taifa letu Prince Yolam"
Mfalme alisema. Ilikuwa ni Taarifa ngeni kabisa kwa kila aliyekuwepo pale. Kila Mmoja alishituka kabisa kabisa.
Walijaribu kumshauri lakini hakubadili maamuzi yake ya kuondoka siku ya kesho.
Walizungumza mengi ya kumshauri ili ahairishe safari yake kwa siku aliyokuwa ameipanga, lakini mfalme hakuelewa Mwisho kabisa mwa Kikao Mfalme alisema.
"Tumezoea wafalme wote kuwa wanaenda kuongea na Miungu huko katika Milima ya Mbagilwa Wakiwa na wanajeshi watatu au wanne wa kuwalinda lakini Mimi nitakuwa peke yangu pamoja na Lady divine!"
Alichokitamka tena kiliwashitua Mara mbili ya hawali kwani Ilikuwa imezoeleka toka enzi za Mababu zao, wafalme waliopita walikuwa wakienda huko wakiwa na ulinzi wa maaskari zaidi ya wawili, halafu wakiwa wameambatana na Lady divine kama alivyotaka yeye.
"Lakini Mfalme huoni kama kuna Hatari huko uwendako unaweza kushambuliwa na kuuliwa!"
Waziri mkuu katika utawala wake alisema.
"Hapana Waziri Mkuu, najiamini na nazani hata wewe mwenyewe unanijua....... Hata hivyo Taifa letu halina tatizo kila sehemu wanamtambua Mfalme na watamlinda mfalme. Hakuna ambaye anaweza kunidhuru Mimi, naombeni muondoa Shaka!"
"Lakini Baba mimi sijapendezwa na Swala hili, kwanini usiende hata na Askari mmoja ili kama ukipata Tatizo huko, aje atoe taarifa ili tuwahi kukusaidia. Kumbuka kuwa unavuka Mto kwanza ndio unaifikia hiyo milima ya Mbagilwa, ambako ndiko kuna mapango ya kuongea na Miungu!"
"Usijali Prince Yolam Nitafika na nitarejea nikiwa salama!"
Mfalme alisema. Hakutaka kukubaliana na ushauri kwasababu alikuwa kaisha amua kabisa kuwa akienda lazima atafika akiwa salama na atarejea lakini hatokuwa peke yake Bali ataongozana na Mwanamke Mtumishi wa Mungu ambaye ni kawaida kuongozana na Mfalme kwenda katika milima ya Mbagilwa, Milima ambayo wao waliamini kuwa ndiko miungu yao ilikuwa ikiishi huko.
Baada ya mjadala mfupi ambao uliwachanganya karibu watu wote waliodhulia Kikao kilifungwa.
Taarifa ya Jambo ambalo lilitamkwa na Mfalme zilimfikia Malkia, mwanamke yule hakuamini kabisa ambacho alipewa kama ni taarifa ambayo ilisemwa na mumewe ndani ya kikao. Moja kwa moja aliamua kumfuata mumewe na kumuomba, lakini mumewe alikataa na kumtoa wasiwasi mkewe mtukufu Malkia. Walizungumza sana na mkewe lakini bado mfalme hakubadili maamuzi yake ya watu wawili tu kutoka katika Ufalme na kwenda katika milima ya Mbagilwa kwa ajili kwenda kuongea na Miungu tena ilikuwa ni siku moja tu ambayo ilikuwa inangojwa kuche Mfalme aende katika milima hiyo ya Mbagilwa.
*******
Akiwa katika Chumba chake ambacho Mara zote alikuwa akifanya maombi yake, Mwanamama Mcha mungu, Mtumishi teule ambaye alikuwa ameteuliwa kuwa Mtumishi wa Miungu, mwenye maono, Lady divine Alifikishiwa taarifa zile zile alizozitamka mfalme katika kikao chake na Mawaziri. Baada ya kuzipokea taarifa hizo Lady divine alishituka sana, hakuamini kabisa kama kweli Mfalme kaamua maamuzi ya Ajabu kiasi hicho. Ilibidi aombe kukutana na Mfalme labda angeweza Kumshawishi ayabadili maamuzi yake.
"Kwanini umeamua maamuzi ya Ajabu kiasi hicho?"
Mwanamke yule Bikra alisema baada ya kuingia katika nyumba ya Mfalme.
"Naomba usiwe na Shaka, tutafika na tutarejea!"
Mfalme alimjibu Lady Divine.
"Lakini kumbuka kuwa tunakoenda ni mbali!"
"Tutafika, amini tutafika. Kwani hii itakuwa mara ya Kwanza kwangu? hii itakuwa mara ya tatu, nawe pia hii siyo ya Kwanza kwako ni ya pili. Kwahio ondoa Shaka!"
Mfalme alisema. Msimamo wake ulibaki kuwa ule ule kuwa watafika na watarudi.
Mwanamama yule Mtumishi wa mungu au Lady divine alishindwa kumshawishi Mfalme.
Lady Divine katika Ufalme ni mwanamke ambaye alikuwa anamtumikia mungu na aliyekuwa anatoa utabili wa mambo ambayo yalikuwa yanatokea katika Dunia. Alikuwa akiheshimika sana katika Ufalme wa Iyumbwi na alikuwa tegemezi sana, kwanza alikuwa kama Dakitali. Huyu na wanafunzi wake ndio walikuwa akimtibu Mfalme. Mwanamke huyo alikuwa akilindwa na Jeshi lake maalumu ambao pia walikuwa ni Mabinti Mabikira.
"Sikutarajia kabisa kama Mfalme bado anaubishi wake ule ule wa kitoto!"
Lady Divine alisema baada ya kufika Chumbani kwake, huku akiwa amezungukwa na wanafunzi wake aliokuwa akiwafundisha kuwa wanawake wa Miungo ya kwao.
"Kwani kasemaje Lady Divine?"
Mmoja wa Wanafunzi wake aliuliza.
"Hajakubali kuacha kwenda huko Kesho tujipange kwanza ili twende siku nyingine na pia kakataa kabisa kuandamana na Ulinzi!"
"Kwa maana hiyo wewe na yeye wawili tu ndio mtaondoka?"
"Ndio maana yake!"
"Mmh! Mtafika na Kurudi kweli, maana mpaka muuvuke Mto Chibaya, na ni mbali eti mpaka kufika huko!"
"Basi kwasababu tunaenda kwa ajili ya Kazi ya Mungu tutafika tu!"
Mwanamke Lady Divine alisema.
Kiujumla mchana kutwa katika Jumba la Utawala katika Ufalme wa Iyumbwi, kulikuwa ni Majadiliano Juu ya Jambo la Kumwacha Mfalme aende peke yake katika milima ya Mbagilwa.
"Lakini Waziri huwezi kumshawishi Baba akaacha kwenda kesho, au hata kama anaenda kwanini asiandamane na Ulinzi ambao utamsaidia katika Safari yake?"
Mwana wa Mfalme ambaye alikuwa ndiye anatarajiwa kuja kuwa Mfalme alisema. Wakati huu alikuwa akiongea na Waziri mkuu.
"Nimeongea sana, nimejitahidi kumbembeleza lakini kakataa katakata...... Ila nimepata Wazo moja!"
"Wazo gani hilo?"
"Wakati anaondoka hapa, nyuma tutatuma maaskari wawe wanawafuatilia ili wakipatwa na tatizo huko, wawe karibu yao kuutoa msaada!"
Waziri mkuu alisema.
"Mmmh! Ili kweli ni Wazo Zuri sana, nimelipenda na lazima tulifanyie kazi!"
Prince Yolam alisema.
Baada ya mazungumzo hayo walitawanyika kila Mmoja akarudi katika sehemu yake ya Kujipumzisha katika Jumba kubwa la Utawala wa Kifalme katika ufalme ule wa Iyumbwi.
Kesho yake mapema kabisa nyakati za Saa mbili Mfalme. Pamoja na Lady Divine walipanda Farasi zao na safari ya kutoka katika Ufalme kuelekea katika milima ya Mbagilwa kwa ajili ya kuongea na Miungu kama ilivyokuwa tamaduni katika Falme yao ikaanza.
Wakati Mfalme na Mwanamama Lady Divine wakiwa wanaongoza njia kutoka katika Ufalme tayari waziri mkuu na Prince yolam walikuwa washaandaa maaskari wanne ambao walikuwa wanamfuatilia Mfalme alikokuwa anaelekea katika milima ya Bagilwa. Safari yao ilikuwa ndefu sana, urefu ambao uliwachukua masaa mawili kabisa kuufikia Mto Chibaya, Mto mkubwa ambao ndio ulikuwa umesimama kama Mpaka baina ya Falme yake na Falme ya Chutema. Mpaka kuufikia Mto huo walikuwa washavuka vijiji zaidi ya vitano ambavyo vilikuwa vinaiunda Falme ile ya Iyumbwi. Nyuma Askari waliokuwa wametumwa wakiwa kwenye farasi walizidi kumfuatilia Mfalme wao. Askari wale walikuwa waangalifu sana, kwani hawakutaka Mfalme wao awaone.
Mpaka wanafika katika Mto huo wa Chibaya hakukuwa na Matatizo ambayo yaliwakuta, walipanda mtumbwi uliokuwa pale kwa ajili ya kuwavusha kuwapeleka katika Milima Ya Mbagilwa ambayo ilikuwa si mbali kutoka kivukoni, kwa mtumbwi ilikuwa kama Dakika kumi tu wanafika katika milima hiyo. Kundi la Maaskari lilopofika kivukoni pale lilisimama hapo hapo kwanza Mfalme afike halafu wao ndio wavuke waelekee huko huko ili kumlinda Mfalme wao.
*******
Akiwa amekaa Chumbani kwake pekee Malkia alikuwa anawaza sana, kichwani Mwake alikuwa hawazi kuwa Mfalme atarudi Salama, hapana alikuwa na kitu alikuwa anakikumbuka, kitu hicho kilimuumiza kichwa.
"Lakini hapana Prince Zayoni, mimi sitakiwi kufanya mapenzi nahitajika kuwa Lady Divine!"
"Hapana Amana, kumbuka kuwa nakupenda, tumetoka mbali Mimi na wewe, umekulia katika Ufalme wetu kwahio lazima wewe uwe Mke wangu...............!"
"Hapana Prince Zayoni, nishakwambia haiwezekani Mimi kuolewa au kujihusisha na Mapenzi na Mwanadamu yoyote, Mimi nishakuwa mwanamke wa kuitumikia Miungu,....halafu kwanini usimpende Lady sayuni mwanamke mzuri ambaye umechaguliwa kumuoa!"
"Simpendi basi tu, ni kwasababu Baba alikuwa Hajui kuwa simpendi na nimekubali kwasababu ya kuilinda heshima ya Ufalme kama Prince ambaye natarajia kuwa Mfalme katika Falme hii ya Iyumbwi......lakini kwanini usikubali kuwa mwanamke wa moyo wangu uwachane na huo U lady Divine!"
"Hapana Prince zayoni. Nitaharibu utaratibu!"
Akiwa mwenye mawazo Malkia aliyakumbuka hayo. Watu wale ambao alikuwa akiwakumbuka ndiye mumewe Mfalme pamoja na Lady divine ambaye ndiye wameambatana kwa pamoja kuelekea katika milima ya Mbagilwa kwa ajili ya kuongea na miungu. Kwa jinsi ambavyo Mfalme ameondoka Malkia hakuwa na Amani kabisa moyoni mwake.
"Kwanini kakataa kuondoka na Jeshi?"
Kwanini kaachia utawala mapema wakati bado umri unaruhusu?"
Hayo ni maswali mazito kabisa Malkia alikuwa anajiuliza pekee ndani ya chumba chake.
Kumbukumbu yake ilimrudisha tena nyuma, wakati wa majibizano ya Prince Zayoni pamoja na Lady Divine wa sasa. Baada ya kuongea sana kwa Muda mrefu Prince alimkumbatia Lady Divine huku lady divine akiwa ametulia tu kifuani kwa Prince Zayoni ambaye ndiye Mfalme sasa. Malkia hakuchoka kuangalia ingawa yeye ndiye alikuwa kaisha tangazwa kuwa Mke mtarajiwa wa Prince zayoni ambaye wakati huo alikuwa anangojwa kuwa Mfalme. Alikumbuka kuwa Zayoni na Lady Divine au Amana kwa jina, walikumbatiana kwa muda mrefu sana, hii ilionesha kuwa Prince zayoni na Amana kabla ya kuperekwa katika Utumishi wa Mungu kama Lady divine walikuwa kama wachumba au wapenzi ambao walikuwa na matarajio ya kuona, ila familia zao zilikuwa hazijui kabisa kuhusu swala hilo. Hata mwanzo wakati Amana anasimikwa kuwa Lady Divine, Zayoni ambaye alikuwa Kaisha pandikizwa kuwa Mfalme alisikitika sana, karibu wiki nzima hakuwa na amani.... Baada ya kumbukumbu hizo, Malkia Aliwaza kuwa Bila Shaka Mfalme Zayoni na Amana au Lady Divine walikuwa na Lao Jambo. kwasababu mfalme anaenda kuachia Ufalme kwahio watafanya mapenzi na Amana lazima Atauwachia U ledy divine na kuwa mtu wa kawaida.
Kabla sijaimaliza hadithi hii nikukumbishe kuwa mcha mungu.
Kama alivyokuwa anawaza Malkia Sayuni, mke mfalme.
Baada ya tu ya kuuvuka Mto Chibaya na kuifikia milima ya Mbagilwa, Mfalme alimvuta Lady Divine moja kwa moja na kusogea naye pembeni kabisa taofauti na yalipokuwa mapango ya Miungu.
"Mbona umenileta huku Mfalme?"
Lady Divine aliuliza baada ya kufikishwa sehemu nyingine ambayo hakuiwaza.
"Nitabaki huku, nitafia huku kama hutonisikiliza!"
Mfalme alisema huku akimwangalia Lady Divine usoni kwa macho ya huruma.
"Unamaanisha nini?"
"Usijisahurishe kuwa Mimi na wewe tuliwahi kuahidiana kuwa wapenzi.......Maisha yangu yote tangu kuwa mfalme sikuwahi kabisa kuwa na furaha kila nilipokuwa nakuona Amana. Wewe ni Mwanamke wa pekee ambaye ulipaswa uwe faraja yangu, tafadhali naomba ukubali kile ambacho nakihitaji kutoka kwako!"
"Unamaanisha nini......na kwanini unasema hivyo, inamaana umejisahau kuwa wewe ni..ni Mfalme na Mimi ni Lady Divine, sihitajiki kabisa kuwa Mke wa Mtu katika kipindi hiki Chote?"
Amana(Lady divine) alisema. Alishangazwa na Maneno ya Mfalme.
"Sihitaji kugombana na wewe, kama unataka nifie huku huku ondoka zako!"
Mfalme alitamka tena huku akimwangalia Lady Divine kisha akageuza shingo yake na kuangalia upande mwingine, wakati huo huo aligeuka mwili mzima, na kuanza kuzipiga hatua kusogea sehemu nyingine ambayo ilikuwa ni hatari kwa Maisha yake.
"Sikutarajia kama Bado una utoto Zayoni, kumbe ndio maana umekataa kuandamana na Ulinzi kwasababu ulikuwa unawaza kufanya mapenzi na Mimi!"
Lady Divine(Amana, jina lake) alisema kwa msisitizo.
Mfalme hata hakugeuka wala hakusimama aliendelea na kutembea. Karibu kabisa kulikuwa na jiwe ambalo alisimama na kutazama upande wa pill wa Mlima huo. Kulikuwa ni mbali sana, yaani kwamba mtu akianguka pale lazima uyapoteze maisha yake, huku kila kiungo kikiwa kimetupwa upande wake.
"Zayoni!.... Usifanye hivyo niko tayari kwa unachokihitaji!"
Lady Divine alisema. Lakini bado Mfalme aligoma kabisa kumsikiliza. Muda huo huo Lady Divine aliamua kutoka alipokuwa amesimama mbio kumuwahi Mfalme wake, lakini wakati anakimbia alipata wazo moja tu kuwa akizivua kabisa nguo zake inaweza kuwa kishawishi kikubwa kwa Zayoni au Mfalme kuacha kujirusha. Mwanamke Yule mchamungu katika Ufalme wa Iyumbwi aliyavua mavazi yake ambayo yalikuwa Meupe na kuyapaki pembeni yeye akabaki mtupu kabisa.
"Tayari Zayoni?"
Lady divine alisema.
Mfalme aligeuka kuangalia na kumkuta mwanamke Yule akiwa mtupu kabisa akimwangalia kwa aibu huku machozi yakimtoka. Mfalme hakuwa na Jambo la kusubili alimsogelea kisha akamlaza pale pale juu ya mlima na kuanza kumuingilia mwanamke Yule mteule wa Miungu ya Iyumbwi.
******
Askari walikuwa wametumwa Bado walibaki sehemu ya kuvukia huku wakiwa wanajiuliza wataweza vipi kujificha Mfalme asiwaone kwani angewaona angeweza kuwapa adhabu kari sana.
"Tubaki hapa hapa!"
Mmoja wa Maaskari alisema.
"Hata Mimi naona tukibaki hapa itakuwa bora zaidi!"
"Sawa tukubaliane kubaki hapa hapa!"
Maaskari wote kwa pamoja walikubaliana nakubaki kando ya Mto wakimngoja Mfalme atoke lakini pia hawakutaka waonekane, walikuwa sehemu ambayo ilikuwa imejificha.
Nusu saa wakiwa maeneo hayo walimuona Mfalme wao pamoja na Lady Divine wakiupanda mtumbwi kuuvuka mto Chibaya kutoka katika milima ya Mbagilwa.
"Mbona Mfalme kawahi sana kutoka huko?"
Mmoja wa maaskari aliuliza.
"Sijui huwenda wamefanya haraka sana!"
Askari walisemezana huku bado wakiwa wamejificha ili Mfalme asiwaone.
Dakika kumi za kuwavusha zilikatika nao tayari walikuwa washauvuka Mto Chibaya wako wanazipanda farasi zao tayari kwa kurudi katika Ufalme.
Njiani Lady Divine alikuwa anawaza sana, mawazo yake yalikuwa yanachanganikana na Machozi huku akiwa Juu ya Farasi, alijiona kafanya kosa kubwa sana, kosa ambalo hakupaswa kabisa hata kulikaribia. Aliaminiwa na Kila Mtu wa Taifa katika ufalme kuwa ni Mwanamke wa Miungu yao, mwanamke ambaye alikuwa na Maono makubwa kweli kweli lakini alifanya mapenzi na wakati hakutakiwa kabisa kufanya .
"Moyo wangu unahisi kuwa naadhibiwa Adhabu kubwa ambayo haipimiki kwa uzito wake!"
SOMA HAPA NAMNA YA KUANZISHA BIASHARA
INAENDELEA...
0 Comments