Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Responsive Advertisement

Simulizi: Ujumbe Kutoka Ndotoni (Notification From the Dream) Sehemu Ya Pili (02)



Lady Divine alijiwazia mwenyewe akiwa juu ya Mgongo wa Farasi.

Wakati huo Mfalme alikuwa nyuma ya Lady Divine wakiongozana. Mfalme yeye hakuwa na Wasiwasi kabisa kwasababu kitu cha pekee ambacho alikuwa akikitamani Kabla hata hajawa Mfalme alikipata. Wakati huo huo Lady Divine Aliishiwa nguvu kabisa, akajikuta anajilaza juu ya Mgongo wa Farasi aliyokuwa ameipanda, kitendo hicho kilimshitua sana Mfalme Zayoni. Aliongeza mbio za farasi wake ili kuwahi kumsimamisha Farasi aliyekuwa amekaliwa na Lady Divine, Amana. Kila hatua Lady divine alikuwa anaelekea kuanguka kutoka juu ya mgongo wa farasi mpaka chini. Wakati huo Farasi wake alikuwa mbio kweli kweli. Mfalme alijitahidi sana kuwahi lakini alimchelewa alifika tayari Lady divine akiwa kaisha anguka chini. Alimsimamisha farasi wake, na kuwahi kumwangalia Lady divine kama ni mzima. Alimkuta ni mzima lakini alikuwa amepoteza fahamu. Alianza kumnyanyua ili kumuweka juu ya Farasi.

"Mfalme umepatwa na nini?"

Sauti hiyo ilimshitua King Zayoni na kugeuka haraka nyuma kuangalia. Macho yake yalipigwa na bumbuwazi baada ya kukuta ni kikundi cha Askari kutoka katika Ufalme wake.

"Hakuna tatizo ila inaonekana Lady divine kapatwa na mshituko akaanguka chini!"

"Basi tunaomba tumbebe tumuwaishe akatibiwe!"

Mmoja wa maaskari wale waliokuwa wanne alisema.

"Sawa ila naomba twende katika kijiji hiki cha Chifoome, kwasababu kipo karibu nitapumzikia hapo kwa kiongozi wa kijiji hiki huku Lady divine akipewa huduma, halafu akipata nafuu tutaondoka kurudi katika Ufalme!"

"Sawa Mfalme!"

Maskari walikubaliana na mfalme wao moja kwa moja, hakukuwepo na maswali zaidi ya hayo. Mmoja wa maaskari wale alimbeba Lady divine kwenye farasi yake, huku mwingine akiongozana na Farasi ya Lady divine Amana. Askari wengine walibaki kama walinzi.

Waliongoza safari yao mpaka kwa kiongozi wa kijiji cha Chifoome. Walipofika walipokelewa vizuri, Lady divine aliperekwa katika chumba cha matibabu kwa ajili ya kufanyiwa huduma.

Akiwa tayari kakaa Mfalme alimwagiza Mmoja wa maaskari wale wanne akimbize taarifa katika Ufalme kuwa kapatwa na Tatizo, kwahio anaweza isirudi siku hio mpaka kesho Asubuhi atalala kijijini pale.

Askari aliyeagizwa alitoka mbio kuwahisha taarifa katika Jumba la kifalme la Iyumbwi. Askari yule alipozifikisha taarifa katika ufalme, kila Mmoja aliyezipokea alishituka na kuamini kuwa huwenda Mfalme kakutwa na matatizo makubwa. Wakati huo huo Prince Yolam aliamua kuagiza kikundi cha maaskari wengine zaidi ya ishirini wakiwa kabisa na mkokoteni wa kufunga nyuma ya farasi kwa ajili ya kumbeba Lady divine ili aje akafanyiwe matibabu katika ufalme. Jeshi aliloliagiza alikuchelewa, lilijikusanya haraka kisha safari ya kutoka ikuru Iyumbwi kuelekea kijiji cha Chifoome ikaanza. Walitumia zaidi ya dakika 35 wakawa wamekifikia kijiji hicho. Walipofika walimpa mfalme maelekezo ambayo walipewa na Mtoto wake, Prince yolam. Maelekezo yalikuwa yanamuomba Mfalme Arudi katika Ufalme ili Lady divine akafanyiwe huko Matibabu. Mfalme hakukataa kwasababu usafiri wa kumbeba Lady divine walikuwa wamefika nao. Kwahio Mfalme alilazimika kubadili maamuzi yake ya kupumzika katika Kijiji hicho cha Chifoome na kuianza safari ya kurudi makao makuu ya Ufalme Iyumbwi. Lady divine alibebwa katika mkokoteni na safari ikaanza kurudi katika Ufalme. Mkokoteni ulikuwa umefungwa kwenye farasi, halafu kwa juu umefunikwa vizuri kama kijumba kidogo na kukiwa na Godoro ndani yake, yeye alikuwa amelazwa katika godoro hilo.


Saa Saba machana ndio wakati ambao walikuwa wanafika katika Ufalme. Walipokelewa kwa haraka sana kisha Lady divine akawaishwa katika Chumba chake kwa ajili ya matibabu. Matibabu yake yalifanywa na wanafunzi wake, alikuwepo Mmoja ambaye alikuwa kaisha onesha kabisa kuwa ni Mwenye nguvu na ndiye alikuwa akipewa kipaumbele cha kuwa Lady divine baada ya Amana. Huyu ndiye alikuwa akifanya kazi ya Miungu badala ya Lady Amana, wakati mwingine alikuwa na maono makubwa kuliko Hata Lady divine amana. Baada ya kumpokea Lady divine, Binti yule aliyekuwa anajulikana kwa jina la Eunike aliendelea kumfanyia matibabu vilivyo mkuu wao.

Mpaka inafika saa moja za jioni Lady divine alikuwa hajaamka wala kuonesha dalili za kuamka kitandani.


Mfalme akiwa katika chumba chake alikuwa kila mara akiagiza watu wakaulizie hali ya Amana kama kaisha pata nafuu, majibu aliyokuwa anaeletewa ndiyo yalikuwa yanamtisha na kumzidishia wasiwasi.

"Samahani mtukufu mfalme Malkia anahitaji kukuona?"

Wakati mfalme akiwa katika dimbwi la mawazo sauti ya mlinzi wa Kiume aliyekuwa karibu sana na Mfalme ilisikika ikimsemesha.

"Mruhusu aingie!"

Mfalme alisema. Wakati huo huo Malkia aliingia katika chumba cha mfalme.

"Mfalme Mbona unaonekana mwenye mawazo kiasi hiki?"

Malkia aliuliza baada ya kuona mumewe akiwa katika hali ambayo hakumzoea kumuona nayo.

"Hapana, ila nafikiria kinachomsumbua lady Amana!"

"Kwani ni kitu gani ambacho kimemkuta mpaka kupoteza fahamu!"

"Wakati tukiwa njiani kurudi, nilishangaa tu anaanguka chini kutoka juu ya mgongo wa farasi. Ndipo kuwahi kumwangalia nikakuta akiwa kapoteza fahamu!"

Mfalme alimjibu malkia.

"Wakati naenda kumbeba Lady divine mmoja wa watu wa pale alisikika akisema kuwa Lady divine alikuwa amepatakaa damu katika mapaja yake!"

Wakati mfalme anazungumza Malkia aliyakumbuka maneno ambayo aliambiwa na Mmoja wa maaskari waliokuwa wametumwa kwenda kumchukua Lady divine pamoja na Mfalme katika kijiji cha chifoome. Askari huyo alikuwa amechomekwa na Malkia mwenyewe kwa lengo la kufanya uchunguzi.

Baada ya kuyakumbuka hayo malkia alimwangalia sana Mfalme kama sekunde 30 bila kusema chochote, lakini moyoni mwake alikuwa kaisha jua kabisa kuwa mfalme na Lady divine wamefanya mapenzi.

"Sherehe za kumuapisha Prince yolam zitakuwa lini?"

Malkia aliuliza swali lingine tena.

"Naona tusubili mpaka Lady divine apate nafuu ndio tuzifanye kwasababu yeye ndiye atamuapisha na kumuombea kwa miungu"

Mfalme alisema.

"Asipoamka tutafanya nini?"

"Itabidi tumtumie mmoja wa wanafunzi wake!"

"Kwanini tusimsimamishe Eunike kuwa Lady divine badala ya Amana ambaye kaamua kuisaliti kazi yake?"

Malkia alitamka maneno hayo huku akimwangalia mfalme.

Mfalme alishituka sana.



Kitendo cha kuyasikia maneno Yale mfalme alishituka sana, akabaki ameganda kama sekunde kumi macho yake yakiwa yameishia katika uso wa Malkia.

"Unamaanisha nini kusema hivyo Sayuni?"

Mfalme alimuuliza mkewe.

"Hapana, kwani ujui kama Lady Amana kaisaliti miungu na ndio maana kazimia!"

Malkia alizungumza tena, alikuwa anamtafuta mfalme kwa makusudi kabisa. Maneno yake yalimfanya Mfalme aendelea kumwangalia asijue nini cha kusema.

"Kwani wewe sahivi ni Mfalme, nazani wewe siyo tena Mfalme, ila umekaa kupoteza wakati na kuficha kinachoendelea!"

Malkia alisema tena. Hapo ndipo alimaliza nguvu Mfalme, mpaka mikono ilimtetemeka. Akajikuta anapata hasira ghafura. Hapo hapo akaipereka mikono yake na kumshika Malkia kwa nguvu shingoni"

Malikia alipiga kelele ambazo zilisikika inje ya Chumba cha mfalme. Mlangoni Askari waliokuwepo walizisikia wakaufungua mlango haraka kuangalia ili kama kuna hitajika msaada wautoe. Walipoufungua mlango tu walimkuta Mfalme kamshikilia Malkia shingoni mwake.

"Mfalme!"

Askari wote waliita. Walikuwa ni wawili.

Mfalme Alishituka sana, huku ameyatoa macho yake. Alimwachia Malkia taratibu na kukaa kwenye kiti chake, lakini hakuweza kukaa alianguka chini na kupoteza Fahamu.

"Mfalme!"

Malkia aliita huku akinyanyuka kwenye kiti kumwangalia Mumewe.

"Mfalme amka tafadhali!"

Malkia alisema tena.

"Kapoteza Fahamu!"

Mlinzi Mmoja alisema baada ya kumchunguza Mfalme.

"Basi mmoja akamuite Eunike awahi haraka akamwangalie Mfalme!"

Malkia alisema.

Wakati huo huo Askari Mmoja alitoka mbio kwenda kumuita Eunike katika chumba cha Lady Divine. Wakati Eunike anangojwa, Malkia na Mlinzi aliyebaki walisaidizana kumnyanyua Mfalme kimsogeza kitandani kwake.

Dakika saba Eunike alifika kumwangalia Mfalme.

"Mfalme tayari Kaisha Fariki!"

Eunike alilitoa jawabu hilo baada tu ya kumwangalia Mfalme.

"Mh!"

Malkia aliitikia kama vile hakusikia.

"Mfalme kaisha fariki!"

Eunike alirudia tena kwa msisitizo. Alikuwa ni Binti Mdogo tu, Umri wake ulikuwa upungui miaka kumi na miwili.

Mallkia alishituka akakisogelea kitanda cha mfalme huku akiwa kapiga magoti chini mikono yake ikiwa imeishia usoni mwa Mfalme, machozi tu ndio yalikuwa yakimmwagika vilivyo huku kilio kikiwa kimemtawala.


Ndani ya muda mfupi taarifa za Kifo cha Mfalme Zayoni zilisambaa Ikuru nzima ya Ufalme wa Iyumbwi. Ndani ya Chumba cha Mfalme Prince yolam alifika haraka sana kuhakikisha kama kweli Baba yake kafariki. Ukweli ulibaki kuwa ukweli kuwa Mfalme kafariki.


Masaa mawili baadaye takaribani Mitaa na vijiji vyote vilivyokuwa vinaiunda Falme kubwa ya iyumbwi vilipata taarifa juu ya Kifo cha Mfalme Zayoni. Watu karibu wote katika Ufalme wa Iyumbwi hawakuamini kabisa kuwa Mfalme kipenzi katika Falme yao ndiye kafariki.

Kwakuwa masaa yalikuwa yashaenda sana, geti la Ikuru lilifungwa na matangazo yakapita kuwa mazishi ya Mfalme yatafanyika siku tatu baadaye.


Kama ilivyokuwa imepangwa siku tatu ziliisha. Siku hiyo ya Mazishi mwili wa mfalme ulitolewa ndani ya jengo kubwa la Utawala wa Kifalme na kuwekwa katika uwanja mkubwa ambao ulikuwa inje ya Utawala. Watu walikusanyika kutoka sehemu mbali mbali katika ufalme kwa ajili ya kumuaga mfalme wao. Sababu iliyomuua ilikuwa ishajulikana kuwa alikufa kwa mshituko tu. Kwakuwa Zayoni alikuwa mfalme hata wafalme na wawakilishi wa Wafalme pamoja na viongozi wengine kutoka katika Falme za Jirani, akiwemo muwakilishi wa Mfalme kutoka inchi ya Jirani na maasimu wakubwa, falme ya Nghumbi naye alikuwepo ili kumuaga Mfalme Zayoni.

Kawaida katika falme hizi walikuwa wakizika majivu ya Viongozi wao. Kwanza walikuwa wakiiweka maiti juu ya kuni kisha wanawasha kuni moto na kumuunguza mfalme. Zoezi hilo lilikuwa chache tu, mpaka kufika nyakati za jioni hakukua na kitu ambacho kilikuwa kimesalia katika mwili wa Mfalme zayoni, waliyachukua majivu yake na kwenda kuyazika katika makaburi ya wafalme wengine ambao walikuwa kabla yake, na habari za Mfalme Zayoni ziliishia hapo na kubaki kama kumbukumbu.


Ndani ya Ufalme tangu kupoteza fahamu bado Lady divine aliendelea kuwa vile vile, na hakukuwa na Dalilia kabisa kuwa ataamka lini, kwani mpaka hapo matumaini ya kuamka kwake yalikuwa hayapo tena. Kilichokua kimesalia vichwani na vinywani mwa Watu katika Ufalme wa Iyumbwi ni kujiuliza na kuulizana maswali ni Sababu gani iliyoperekea Lady divine kupoteza fahamu? Wakati huo huo walikuwa wakihusanisha na kifo cha Mfalme, kwani matukio yote mawili yalitokea siku moja. Cha ajabu ni kwamba ilikuwa siku hiyo hiyo ambayo Mfalme Zayoni alikwenda na Lady Amana, huko katika milima ya mbagilwa. kwahio kila mmoja katika Ufalme alikuwa anajiuliza sana. Kwa wakati huu Lady divine Amana akiwa kitandani. Eunike alikuwa anayasimamia maswala yote yaliyokuwa yanahusu maombi katika ufalme.


Siku mbili baada ya mazishi ya Mfalme zayoni, Tangazo lilipita kuwa Mtoto pekee wa Mfalme, Prince Yolam ataapishwa kuwa mfalme siku mbili zijazo toka siku hiyo. Tangazo hili muhimu lilisambazwa katika ufalme wote wa Iyumbwi kila Mtu akazipokea.


Siku Moja baada ya Tangazo Kupita kuwa Prince yolam ataapishwa kuwa Mfalme, Ikuru ya iyumbwi alikuja Mgeni. Mgeni huyo alikuwa ni mmoja wa wenyeji katika Falme hiyo kubwa. Mtu yule alikuwa na Shida ya kumuona Prince Yolam.

Alichukuliwa moja kwa Moja na kuperekwa kwa Prince yolam ili kumwambia ni kitu gani kilikuwa kimempereka ikuru ya mfalme.

"Nambie shida yako?"

Prince Yolam alimuuliza Mtu yule ambaye alionekana mtu mzima wa makamo.

"Ni kwamba naupenda Ufalme huu uwendelee kudumu milele. Ila leo wakati naelekea sokoni katika Mambo yangu nikakutana na Kijana Mmoja akiwa anasema maneno haya.

"Mfalme Zayoni kaondoka lakini kamwachia Mfalme atakaye kuwepo Mtihani. Nasema hivyo kwasababu Ufalme ushakuwa laana. Ila katika hiyo laana atatoka Mfalme ambaye atakaye iunganisha Falme ya Iyumbwi na Falme ya Nghumbi, si mbali sana hayo yatatokea lakini Mimi nimesema kama mtu tu napita zangu. Mfalme huyo atatokea katika Ufalme wa Iyumbwi lakini ataishi katika Ufalme wa Nghumbi na ndio utabili wa kweli utafanyika. Haya sio maneno yangu Bali ni maneno yaliyokuwepo toka enzi za mababu zetu na yameandikwa katika vitabu kama hadithi, hadithi ya kitabu hicho aliisoma babu yangu na kilikuwa ni kimoja tu, na kipo katika Falme ya Nghumbi. Babu yangu alinisimulia mengi sana kuhusu huyo Mfalme lakini kila kukicha huwa nasahau kimoja kimoja lakini Leo nimeamua kuusema ukweli huu kwenu ninyi ndugu zangu wa iyumbwi nawapenda. Narudia tena kuwa, nami nasema kwasababu napita tu, lakini si ya kujitungia ila kwakuwa nimeyatamka siku moja yanaweza kujidhihirisha wazi kabisa. Ila vita kubwa itafanyika wakati wa tukio hilo la pekee katika uso wa Dunia hii!"

"Hayo ndio maneno ya kijana huyo, nikijana mdogo tu, na Babu yake huyo anayemsema ni marehemu tangu zamani, huyo Kijana huwa anafanya shughuri za kubeba mizigo za watu sokoni!"

Mtu Yule alimaliza kumsimulia Prince Yolam kisa ambacho alikisikia sokoni kutoka kwa Kijana mdogo tu mbeba mizigo sokoni. Wakati huo Prince Yolam alikuwa amenyamaza kama anawaza jambo.

"Huyo Kijana anapatikana sokoni mara zote, hata sasa nikiwatuma maaskari wanaweza kwenda kumchukua na kumleta?"

"Ndiyo tena ni maarufu sana, anajulikana kwa jina la Semwali, ni kijana mchafu mchafu tu hivi"

"Sawa, nashukuru ila naomba utaongozana na Maaskari wakamkamate kijana huyo aje"

"Sawa Prince Yolam!"

Baada ya maongezi hayo Prince Yolam aliwaomba Maaskari watatu waongozane na Mtu Yule aliyeleta Taarifa kwakwe kuhusu Utabili wa Falme kubwa ya Iyumbwi kufa na kuungana na Falme ya Nghumbi na kuunda Falme moja ambayo hata jina lake bado lilikuwa halijafahamika.


Baada ya kuwagiza maaskari kwenda kumkamata kijana huyo ili kumleta katika Ufalme, yeye alikwenda moja kwa Moja kwa Malkia au Mama yake Mzazi queen Sayuni.

"Mama nahitaji kujua jambo ambalo limejificha nyuma kuhusu kifo cha Baba yangu, kwani mpaka sasa sina hakika kama ni mshituko tu ndio sababu ya Kifo chake. Askari wake nao hawataki kuusema ukweli au nao uliwakataza wasiseme Jambo lolote?"

Prince Yolam alisema. Uso wake ulionesha dhaili kuwa alihitaji kuujua kabisa ukweli.

Baada ya kuyasikiliza maneno ya Mwanaye mama alibaki kimya kidogo, wakati huo huo alikumbuka kabisa kuwa aliwakataza walinzi wa mfalme wasiuseme ukweli wa tukio Jinsi walivyomkuta Mfalme kamkaba yeye kisha akaanguka chini na kuperekea kifo chake, tena kwa wakati huo huo alikumbuka juu ya taarifa alizopewa siku ambayo Mfalme alikwenda katika milima ya Mbagilwa kwa Miungu, kumbe hakwenda kwa nia ambayo wao walikuwa wanaikusudia bali alikwenda kwa nia ya kwenda kufanya mapenzi na Lady Divine Amana.

"Mama!"

Prince Yolam aliita baada ya kumuona Mama yake amezubaa.

"Abee!"

Mama aliitika.

"Mbona umezubaa, nambie mama maana nahisi Ufalme unaelekea katika Mashaka, nahitaji niupambanie!"

Prince Yolam alisema tena, hapo Mama alishituka na kuwiinua uso wake, macho yake yakaishia katika uso wa Mwanaye.


Kabla sijaimaliza Hadithi hii nakukumbusha kuwa mcha Mungu.




"Unamaanisha nini Yolam?"

Mama alimuuliza mwanaye.

"Mama hata wewe unashindwa kutambua. tazama Baba kafariki ghafra, halafu Lady Divine amepoteza fahamu wiki sasa!"

"Mwanangu Yolam. Hakuna Jambo ambalo linaweza kukuletea Shaka, halafu kuhusu Swala la kifo cha Baba yako hakuna jambo geni ni hivyo hivyo unavyo jua!"

Malkia alisema. Prince Yolam alibaki kimya kwanza. Kisha akasema.

"Mama kumbuka kuwa kesho naapishwa kuwa mfalme kama kuna Jambo unanificha basi tambua kuwa wewe ndio utakuwa umeniweka Mimi katika wakati mgumu!"

Alipoyasema maneno hayo alisimama na kutoka ndani ya Chumba cha Mama yake, na kuzipiga hatua kuelekea chumbani kwake.

Jumba la ufalme wa Iyumbwi lilikuwa ni Jumba kubwa, jumba ambalo lilikuwa limegawanyika katika vyumba mbali mbali kulingana na aina ya watu, na vyumba hivyo vilikuwa vikubwa navyo pia viikiwa vimejigawa kama nyumba kamili, yaani sebule na vyumba vya kulala na maswala mengine. Kulikuwa na Sehemu ya Waziri mkuu, na Sehemu ya Mfalme na sehemu ya Malkia na Sehemu ya Lady Divine na Sehehemu ya Mwana wa Mfalme, pia na Sehemu ya Kamanda Mkuu wa Jeshi la Maaskari katika Ufalme. Jumba lile lilikuwa ni Kubwa sana.


"Tafadhali Prince tunaweza kuingia ndani!"

Akiwa amekaa ametulia kwenye kiti chake huku akiyatafakari maneno aliyo ambiwa kuhusu Ufalme wa Iyumbwi kufa na kuungana na Falme nyingine ya Nghumbu na kuunda Taifa moja. Mlangoni prince Yolam aligongewa hodi ya kuingia.

"Unaweza kuingia.

Wakati huo huo aliingia Mlinzi wake ambaye alikuwa akimwamini sana.

"Yule Kijana kaisha letwa!"

Badala ya kuagiza aingizwe ndani Prince Yolam mwenyewe alisimama na kutoka inje kumwangalia kijana ambaye Ilikuwa anatawangazia watu sokoni kuhusu Ufalme wa Iyumbwi kutoweka.

"Naombeni mumlete huku!"

Prince Yolam aliwaomba Askari wamfuate alipokua anaelekea.

Waliingia katika moja ya Chumba ambacho kilionekana ni cha kutunzia Makorokoro katika Ufalme. Prince Yolam hakutaka kabisa kulifanya jambo lile akiwa anaonekana katika? Macho ya Mtu mwingine katika Ufalme. Askari nao aliwapa Onyo wasiseme kwa watu wengine.

"Tafadhali naomba unambie kitu ambacho ulikuwa unakisema kwa Watu kuhusu Ufalme wa Iyumbwi na Nghumbi kuungana?"

Prince yolam alimuuliza Yule Kijana.

"Kama ambavyo umeambiwa au kusikia watu wengine wakisema!"

"We umejuaje kuwa watu wanazisamabaza Habari hizi?"

"Kwasababu ndizo zimetapakaa kila sehemu na Watu wengi wanazisema huku wakiwa hawaamini kuwa huo ni Utabili uliokuwepo toka Zamani!"

"We umejuaje kama itakuwa hivyo?"

"Nilisimuliwa na Babu yangu, kuwa hapo hawali Ufalme wa Nghumbi na Iyumbwi zilikuwa ni Taifa Moja kubwa lanye nguvu lakini walitokea Maprince wawili ambao hawakuelewana ndio wakaigawa Falme hiyo ambayo jina lake nimelisahau kwasababu ni muda sana tangu Babu anisimulie. Leo nimeamua niisimulie kwa watu ili waujue ukweli nisije kusahau kabisa, ili hata ikitokea kweli wajue ni utabili uliokuwepo ndio umetimia kuwa; Taifa la Nghumbi pamoja na Taifa la Iyumbwi vitaungana na kuwa Taifa moja!"

"Imeandikwa wapi?"

"Babu yangu alinambia kuwa imeandikwa katika kitabu, na kitabu hicho kiko katika Falme ya Nghumbi. Kitabu hicho kiliandikwa na mtu mmoja aliyekuwa anatafasili ndoto za watu katika Ufalme huo mkubwa. Inasemekenana kuwa kuna Mtu aliota ndoto ya mambo mengi sana kuhusu ufalme wa Iyumbwi na Nghumbi. Baada ya kuiota ndoto hiyo alikwenda kwa huyu mtafasili ndoto akatafasili hiyo ndoto yake na Kisha kuiandika katika Kitabu"

"Kwahiyo unajua kuhusu utabili huo?"

"Nakumbuka machache sana, mengine yashanitoka lakini Babu yangu ambaye ni marehemu mpaka sasa alinisimulia mengi sana!"

Yule kijana aliendelea kuwa muwazi kwa Prince Yolam.

"Ebu nambie hayo Machache"

Prince Yolam naye aliendelea kuuliza ilia aambiwe japo kwa uchache.

"Ni kwamba; itafikia kipindi atatokea Mfalme ambaye ataligawa taifa baada ya kuzaa Mtoto inje ya Ufalme, Mtoto huyo atakulia katika Ufalme wa Nghumbi na hatojulikana kwa Watu kabisa mpaka anakuwa mkubwa. Mtoto huyo ndiye atakuwa Mfalme ambaye atayaunganisha Mataifa haya mawili na ndiye atakuwa Mfalme"

"Kwahio unataka kusema kuwa huyo Mtoto atakuwa Prince katika Ufalme wa Iyumbwi lakini atakulia katika inchi au ufalme wa Nghumbi?"

"Hujakosea na ndivyo ilivyo!"

"Umesema kuwa yote hayo yamo katika kitabu, na hicho kitabu kipo katika maktaba ya Nghumbi?"

"Ndiyo, na kinajina Kabisa la huyo Mfalme! Lakini jina lake nimelisahau!"

"Huwezi kukumbuka?"

"Kweli kabisa nimelisahau labda chakusaidia utume watu katika Maktaba hiyo ya Nghumbi wakakitafute hicho Kitabu, kimetunzwa kama hadithi na watu huwa wanakisoma kama hadithi tu, kwani hata kilivyo andikwa kimeandikwa kama Hadithi ili kuwaficha watu ukweli kuwa huyo Mfalme atakuja!"

"Kwahio hata wao huwa hawakielewi?"

"Ndiyo, ni kama hivyo hivyo kwasababu kilivyoandikwa ni kama tukio ambalo linasimulika kuwa alitokea mfalme akayaunganisha Mataifa mawili makubwa ya kifalme. Na hata majina ya hizo Falme hayajatajwa ndani ya hicho kitabu... Ila babu yangu alinambia kuwa kilichokusudiwa ndani ya Kitabu hicho ni kile kinachokuja!"

"Asante kwa kunambia ukweli huu. Unaitwa nani?"

"Naitwa Semwali!"

"Naomba utabaki katika Ufalme na nitakuunganisha na Jeshi la Ufalme!"

Prince Yolam alisema kisha wakatoka ndani ya Chumba hicho.

"Naombeni mkamkabizi Mavazi ya Jeshi awe miongoni kwa wanajeshi na afundishwe taratibu za Kijeshi kuanzia Leo!"

Prince Yolam alisema. Wakati huo huo Askari wake walitekeleza walichoambiwa.


Baada ya kuupata uhakika wa kile alichokuwa anakitaka. Prince Yolam alirudi ndani kwake na kukaa kwenye kiti huku akitafakari sana.

""Ni kwamba; itafikia kipindi atatokea Mfalme ambaye ataligawa taifa baada ya kuzaa Mtoto inje ya Ufalme, Mtoto huyo atakulia katika Ufalme wa Nghumbi lakini Asili yake ni Iyumbwi. Lakini pia hatojulikana kwa Watu kabisa mpaka anakuwa mkubwa. Mtoto huyo ndiye atakuwa Mfalme ambaye atayaunganisha Mataifa haya mawili na ndiye atakuwa Mfalme""

Akiwa katika wimbi zito la Mawazo aliyakumbuka tena maneno aliyoambiwa na Semwali

"Kwahio hatojulikana kwa watu, nitamjuaje sasa.......kama ni hivyo lazima nifanye mpango wa kuweka mazoea mapema na Ufalme wa Nghumbi ili nikichukue hicho kitabu halafu nikisome nimjue huyo Mfalme........ Nikisha mjua lazima nitamuua Mapema kabisa!"

Prince Yolam Aliwaza mwenyewe akiwa Ndani ya Chumba chake. Mawazo yalikuwa mengi sana, alijisahau kabisa kuwa alichokuwa anapanga ni Utabili ambao ulikuwepo toka enzi za Mababu zake na ni kwamba ni kazi kuutengua japo kuwa anaweza, lakini lazima atumie nguvu sana kuutengua Utabili ambao ushaandikwa kupitia ndoto.


"Tafadhali Prince Yolam naweza kuingia!"

Akiwa katika wimbi zito la mawazo aliisikia sauti ya Waziri Mkuu akimgongea kuingia.

"Pita tu!"

Prince Yolam alimruhusu waziri mkuu aingie.

"Mbona unaonekana unawaza kiasi hicho?"

Waziri Mkuu alimsemesha Prince Yolam.

"Hapana ila nawaza kwasababu kesho ndio siku ya kuapishwa kwangu Kuwa Mfalme. Kwahio nawaza Jinsi gani nitaweza kuliongoza Taifa kubwa lenye zaidi ya watu milion kadhaa"

"Usijali jukum hilo halitokuwa lako pekee, mimi na mawaziri wengine pamoja na Makatibu tutakusaidia na tutashirikiana na wewe kwa kila jambo, kila hatua. Taifa hili ni kubwa na lina historia ndefu, nitaifa ambalo lilitengenzwa na Prince ambaye aliitwa Yolam kama wewe. Baada ya kufauru kulipigania aliapishwa na kuwa Mfalme. Ufalme huu katika historia ya Nyuma ni kwamba lilikuwa Taifa Moja kubwa ambalo lilijulikana kama Ng'umbwi lilikuwa limejumuhisha Falme kubwa ya Nghumbi na Hii Falme yetu, lakini ulitokea Mgogoro Mkubwa ambao ndio ulitengenisha Falme hizi.

Ni Miaka 200 iliyopita tangu sasa. Alikuwepo Mfalme aliyeitwa Zilizayoni, Mfalme huyu alikuwa na Mtoto Mmoja wa Kiume aliyemzaa kifalme katika Ufalme wa Ng'umbwi, lakini kumbe alizaa Mtoto mwingie pembeni. Mtoto huyu alikuwa ni Mtoto wa inje ya ndoa aliyemzaa na Binti ambaye alimuokoa Vitani. na ndiye aliyekuwa Mtoto Mkubwa, lakini Mtoto huyo alikuwa ajulikani kama Prince kwani Mfalme aliifanya siri. Umri wa Mfalme ulikwenda mpaka ikafika wakati wa kuachia madaraka ndipo alipomtangaza yule kijana wake ambaye alijulikana kwa Jina la Cleopa kuwa ni Mwanaye. Kweli alikuwa anafanana kabisa na Mfalme. Kama nilivyokwambia Prince Cleopa ndiye alikuwa mkubwa na alikuwa Hodari sana katika mapigano, alikuwa anapambana sana. Mpaka kuperekea kumtungia jina moja la Mfalme wa vita. Kitendo cha kumtangaza Cleopa kuwa ni Mwanaye kilileta mtafaruku mkubwa sana katika Ufalme, nani atakuwa Mfalme? Lakini watu wote walipendekeza Mfalme awe Yolam kwasababu ndiye alikuwa anatambulika kama Prince na ndiye alikuwa Tumaini na Matarajio ya kila Mmoja kuwa ndiye atakuwa Mfalme wa Taifa. Ingawa Mfalme wa Vita alipendwa sana hasa na wanajeshi lakini hakupewa nafasi ya kuwa Mfalme baada ya Baba yao Zilizayoni.

Kwa swala la Prince Yolam kuwa Mfalme, Mfalme Zilizayoni alikubali, lakini Cleopa ambaye alikuwa ni Mkubwa hakufurahishwa na Maamuzi yale, ndipo alipoamua kuichukua Familia yake na kwenda kuishi katika Kijiji cha Nghumbi mbali kidogo kutoka hapa na kuanzisha makazi yake. Aliondoka na Jeshi kubwa sana na Imara, alipofika huko alijitangaza kuwa Mfalme katika eneo hilo kisha akaanza kuwashawishi viongozi wa Vijiji vilivyokuwa vimepakana Nghumbi kuungana naye, hata walipokuwa wanakataa alikuwa akivamia na kuwaweka chini yake. Vipo vijiji vingi alivisogeza katika Falme yake. Mambo hayo yalimuuzi sana Baba yake, pamoja na Prince Yolama. Baada ya kuona sasa Cleopa anazidi kuyateka maeneo mengi na ya Muhimu, ndipo Prince Yolam naye alipomuomba Baba yake amuachie Jeshi kwa ajili ya kupambana na Kaka yake. Jeshi lake lilikuwa kubwa sana, jeshi hilo lilianza kushambuliana na King Cleopa, mwisho akafanikiwa kuvirudisha baadhi ya Vijiji katika Ufalme wa Iyumbwi. Vita ilikuwa kubwa sana, watu wengi waliuwawa sana.

Vita yao iliisha baada ya kifo cha Baba yao Mfalme Zilizayona, ndipo wote walikutana wakakubaliana kuwa kila Mmoja ashike eneo lake ambalo analitawala ili wasiendelee kuua watu. Kwahio mambo yaliisha hivyo. Na hiyo ndio historia ya Mataifa makubwa mawili ya Iyumbwi na Nghumbi. Lakini Iyumbwi bado ilibaki Taifa la Pekee, ambalo heshima yake haikushuka. Hata baadhi ya watu waliweza kutoroka kutoka katika Falme ya Nghumbi na kuhamia huku. Taifa hili, chini ya Uongozi Wa King Yolam, mambo yalikuwa mazuuri na yaliendelea kuwa mazuri mpaka sasa. Mpaka sasa ninavyongea na Wewe, kila Mmoja anafurahi kuwa Ufalme utabaki kuwa pale pale na Watu wataishi kwa Amani kabisa kama ilivyokuwa kwa King Yolam wa kwanza"

"Kwanini umesema hivyo waziri mkuu?"

"Kwasababu jina lako ni la Mfalme mkubwa, Mfalme ambaye alipendwa na watu wengi na alidumu sana katika uongozi wake na ndiye muhasisi wa Falme hii ya Iyumbwi!"

"Mbona Mimi siijui historia hii?"

Prince Yolam aliuliza tena.

"Kwasababu hukuwahi kuifuatilia Historia ya Taifa hili, lakini kitabu chake kimo maktaba ya Mfalme. Kwahio hata wewe utakisoma usijali!"

Waziri Mkuu alisema.

Waliiendelea kuongea mengi ya kutiana moyo lakini Mwisho Waziri mkuu alimuacha Prince Yolam pekee na kurudi zake.


Waziri mkuu akiwa anaamini kuwa alichomsimulia Prince Yolam kitamfanya kufurahi, lakini kumbe ilikuwa kinyume, historia hiyo ndio ilimuongezea Prince Yolam mawazo, kwani aliyaunganisha maneno aliyoambiwa na Semwali muda mfupi, akapata Jawabu moja kwa moja kuwa ukweli wa kile alichoambiwa Upo na akiupuzia atashindwa kulizuia swala hilo.




Masaa yaliendelea kukatika, Prince Yolam aliendelea kuwaza kuhusu alichoambiwa na Hadithi aliyosimuliwa. Mpaka inafika husiku anaenda kulala bado Prince hakuwa na Moyo wa amani, hata alipoulizwa na Mpenzi wake aliuficha ukweli na kusema kuwa anaiwaza kesho ya kutawazwa kuwa Mfalme wa Falme kubwa ya Iyumbwi.

*******

Mpaka masaa hayo, bado hali ya Lady divine iliendelea kuwachanganya wanafunzi wake, hasa Eunike ambaye alikuwa akimpenda kuliko wanafunzi wake wote.

Eunike alikuwa anawaza na kuomba sana ili Lady Amana apate kuamka, wakati mwingine alikuwa ali kabisa kwasababu ya kuyasimamisha maombi kwa ajili ya Lady Amana kuamka ili aweze kulisimamia zoezi la kumsimika Mfalme mpya wa Falme yao ya Iyumbwi. Kiumri yeye bado alikuwa ndogo aliona kuwa Jukum ambalo anapewa lilikuwa zito sana kulifanya.

"Eunike naomba tumuombee kwa Mara nyingine huwenda akaamka usiku huu ili kesho akalisimamie zoezi la kumuapisha Prince Yolam kuwa Mfalme, kumbuka kuwa sisi hatuna uzoefu kiasi cha kulifanya zoezi hilo zito!"

"Uko sahihi, lakini nishajitahidi sana, na hata wewe mwenyewe ni shuhuda, sijui alifanya kosa gani mpaka hali hii kumkuta?"

Eunike alisema na wenzake. Hali ya Lady Amana iliwasikitisha sana, walikuwa wakijiuliza maswali kila Mara lakini hawakupata majawabu kabisa.

"Malikia anataka kuingia ndani!"

Wakiwa katika majadiliano Mara sauti ya mlinzi wa nje ilisikikia ikiwaomba ruhusa.

"Mruhusu apite!"

Eunike alisema. Na udogo wake lakini wenzake walimuheshimu sana. Kiumri na umbo pia yeye ndiye alikuwa mdogo kupita wote.

"Sasa naombeni wengine wote mnipishe kwanza niongee na Eunike"

Malkia alisema baada ya kufika ndani na kukaa.

Haraka wanafunzi wengine waliokuwemo katika chumba hicho walitoka inje.

"Eunike?"

"Abee Mtukufu Malkia!"

"Hali ya Lady Amana inaendeleaje?"

"Kwakweli hata Mimi bado inanitisha, kiujumla hatuna matumaini kabisa!"

"Hhiiiiihhhaa!.....vipi ushafanya hata maombi kwa miungu?"

Malkia aliisusha pumzi kwanza kisha akauliza.

"Ndiyo Mtukufu Malkia, nishafanya maombi kwa kushirikiana na Wenzangu lakini hakuna mabadiliko hata!"

Eunike alijibu. Alikuwa anaongea katika hali ya udhuni sana.

"Naomba usiudhunike, mwalimu wako atapona tu Usjilali!.......lakini Eunike Amjagundua kitu chochote katika mwili wa Lady Amana?"

Malkia aliuliza. Swali ambalo alimuuliza Binti yule mdogo lilimshitua kwanza.

"Hapana hatujagundua kitu!"

"Kweli Eunike?!"

"Ndiyo Mtukufu Malkia!"

"Haya usijali. lakini kesho utalazimika wewe ndiyo ulifanye Jukum la kumsimika Mfalme kwasababu wewe unaaminika katika Ufalme na wakati wowote unaweza kutangazwa kuwa Lady divine. Kwahio nakuomba ujiandaye, nakuamini sana na naomba kesho usiniangushe!"

INAENDELEA

Post a Comment

0 Comments