Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Responsive Advertisement

Simulizi: Ujumbe Kutoka Ndotoni (Notification From The Dream) Sehemu ya Saba (07)



 "Unaweza kutembea sahivi?"

Malkia aliuliza tena.

"Ndiyo nguvu ninazo za kuniwezesha kutembea!"

"Basi simama ukaoge kwanza!"

Malkia alisema. Wakati huo huo Maji ya kuoga yaliandaliwa na Tamali akaenda kuoga. Alitumia dakika kama saba akawa amemaliza kuoga, na kurudi ndani Chumbani.

Baada ya kufika Malkia alichukua sanduku dogo dogo la mbao, na kurudi kitandani na kulifungua. Ndani yake kulikuwa na Vazi nzuri pamoja na mapambo ya dhahabu. Vazi lile lilikuwa la kimalkia kabisa.

"Hili ni vazi ambalo nimelitengeza mimi kwa ajili yako. Vazi hili linanikumbusha mbali sana wakati nikiwa Binti kama wewe, Baba na Mama yangu walinambia natakiwa kujifunza kutengeneza mavazi ya Heshima ambayo yatanifanya nieshimike katika Ufalme. Nilianza kujifunza mwisho nilitengeza Vazi zuri ambalo lilipendwa na Malkia aliyekuwepo. Huyo alikuwa ni Mama mzazi wa Mfalme Joktan, nimelazimika kukutengezea Vazi hili kwani wewe ni Princess ndani ya Ufalme huu Tangu sasa"

Malkia Velian alisema, kisha akaanza kumpamba Tamali. Alimpaka manukato mazuri, na kumvisha Vazi lile, akaongezea na Mapambo Mengine. Mtazamo wa Tamali ulibadilika ghafra, akaonekana bomba kupita kiasi.

Malkia Velian alimsogeza Tamali kwenye kioo ili naye apate kujitazama Jinsi alivyo pendeza.

Kwa Jinsi ambavyo alijikuta amebadilika, Tamali hakuamini kabisa. Machozi yalimdondoka pale pale, akageuka tena kumwangalia Malkia Velian ambaye alikuwa akiangalia pia kwenye kioo.

"Usilie Tamali, sasa wewe inapaswa uizoee hali hii. Kwani utaishi kama hivi kuanzia sasa!"

Malkia Velian alisema. Tamali hakumjibu alimkumbatia Mama yule, Malkia katika Ufalme wa Nghumbi.

Alitumia kama dakika tatu kumkumbatia tu mama yule huku moyoni akiwa anajisemea.

"Mungu akupe Maisha marefu, kwani nilikuwa nishakata tamaa kabisa ya Kuishi, nilikuwa nishajiona Laana kama nilivyoambiwa. Enyi miungu ya Ardhi hii dumisheni Mapenzi haya mpaka kifo changu!"

Kwa upande wa Malkia Velian naye alikuwa anawaza pia.

"Hakika Moyo wangu sasa umepata ujasiri na nitaishi kwa kujiamini kuanzia sasa. Wewe utakuwa mwanangu na nitakulinda kama nilivyo kuahidi. Nakupenda sana Tamali!"

Baada ya kuwaza hivyo wote kwa pamoja waliachana.

Tamali alikuwa sahihi kulia kwani Maisha yake ya nyuma yalikuwa yamejaa manyanyaso, hakuwahi kuvaa na kupambwa kama ilivyokuwa siku hiyo. Hayo ndiyo yalimfanya kulia.

"Naomba nikupereke kwa Mfalme akuone, kisha nikutembeze eneo hili la Ufalme ujionee maadhari ya Hapa!"

Malkia Velian alisema. Kama alivyosema walitoka Chumbani na kuanza kutembea katika Valanda kubwa la Jumba la Kifalme katika Ufalme huo wa Nghumbi. Kituo cha kwanza ilikuwa ni katika chumba cha Mfalme katika Jumba lile Kubwa. Mfalme alipomuona Tamali naye alistahajabu sana.

"Wewe ni Princess kutoka Falme ipi umekuja kunitembelea Mapema hivi?"

Mfalme Joktan aliuliza baada ya kusalimiana na Tamali pamoja na mkewe Malkia Velian.

"Huyu si Princess kutoka katika Falme ya Mbali ila ni Princess Tamali wa Falme ya Nghumbi. Mwanao wa pekee!"

Malkia Velian alisema. Maneno yalimfanya Mfalme kutabasamu kwani alimjua mke wake kwa utani.

"Kama vile namjua,....si ndiye yule Binti tuliyemkuta kule porini siku nne kabla tukiwa tunatoka Iyumbwi kwenye sherehe ya Mwana wa Mfalme?"

"Haswaa! Ujakosea Mfalme, huyu ndiye!"

"Kabadilika sana. Kumbe ni Binti mzuri kiasi hiki!"

Mfalme alisema. Huku akimwamgalia Tamali.

"Huyu ndiye Mwanetu kuanzia sasa. Na aliyeko tumboni mwake ni Mtoto katika Ufalme, naimani atakuwa mwanaume kwahio atakuwa Prince katika Ufalme wetu!"

Malkia Velian alisema maneno hayo kwa mumewe.

"Nashukuru sana Mke wangu, Hatimaye Miungu ya Nghumbi imekisikia kilio chetu. Tumempata mwana!"

Mfalme Joktan alitamka, maneno yake yalimfanya mkewe kufarijika, hata Tamali alijikuta anajiona kama vile ni Mwana wa Mfalme.

"Ahsante Mfalme wa Ardhi hii, na nakuombea kwa Miungu Ufalme wako Udumu milele!"

Tamali alisema.

"Ahsante Sana Princess. Lakini jina lako bado sijalijua!"

"Mimi ninaitwa Tamali!"

"Tamali!....jina lako ni zuri kweli, nimelipenda. Na kuanzia leo utaitwa Princess Tamali"

Mfalme alisema. Baada ya kuzungumza maneno hayo yenye furaha, Mfalme Joktan alitaka kumjua Tamali zaidi. Hawali alikuwa akiishi wapi na kwanini walimkuta porini?

Alisimuliwa kila kitu, hakuacha hata kimoja.

"Pole sana, na nakuomba uondoe Shaka, utaishi hapa Maisha yako yote na hutokutana na Jambo la kukuumiza. Kuanzia Leo utaitwa Princess!"

Mfalme Joktan alisema. Kama hivyo alikuwa ni mwenye Busara nyingi na hakutaka kabisa kumfanya Mkewe Aishi katika Upweke, alimpenda Mkewe Aishi kwa Raha siku zote. Kitendo chakumpata Tamali kilimfanya kuamini kuwa Mke wake ataishi kwa Furaha kuanzia wakati huo.

Toka siku hiyo Tamali Aliayaanza Maisha yake katika Ufalme wa Iyumbwi kama Princess ndani ya Ufalme, hakukuwepo na Mtu ambaye. Alipata ujasiri wa kupingana wala kuuliza kuhusu habari zake. Kwakuwa Mfalme na Malkia ndio waliujua ukweli wa Maisha yake, hata hawakuthubutu kuusema ukweli huo kwa Mtu yeyote katika Falme hiyo, hata Tamali naye alikatazwa kabisa kuwa akiulizwa aseme kuwa ni Mtoto wa Mfalme Joktan asiuseme ukweli wa Maisha yake kwani ingekuwa Hatari kwasababu taarifa zingeweza kusambaa mwisho zikafika kwa Mfalme wa Iyumbwi King Yolam kuwa Mtoto wa Lady Amana yupo anaishi.


ILIKUWAJE MTOTO WA LADY AMANA AKAENDELEA KUISHI.

Huu ndio ukweli jinsi mambo yalivyokuwa. Baada ya Malkia kuagiza Askari amchukue Mtoto wa Lady Amana akamtupe, Askari yule alimchukua Mtoto lakini hakumtupa ila ilikuwa hivi

Baada ya kumchukua mtoto, Askali yule alipanda juu ya farasi wake na mtoto kisha akaelekea porini kumtupa mtoto, Alipofika porini alishuka kwenye farasi na mtoto, kisha akaangalia huku na kule, hakuweza kugundua kuwa kulikuwa na Mtu ambaye alikuwa anamwangalia. Ndipo aliposogea sehemu ya kichaka kikubwa na kutaka kumtupa mule mtoto yule, lakini kabla hajafanya hivyo, alishituka, kisha akainama na kumwangalia Mtoto yule. Alikuwa Bado amelala tu, lakini alikuwa anahema askari yule huruma ilianza kumungia ghafura, akajikuta anapata Mgogoro nafisini mwake.

"Nimtupe tu kwani sina jinsi ya kumsaidia na nitamjibu vipi Malkia endapo nisipomtupa?..... Lakini ni Mtoto mdogo Masikini, hajitambui, kwanini Nimtupe wakati yeye hana dhambi?"

Askari yule alijisema mwenyewe kimoyo moyo ndani ya pori. Baada ya kuwaza sana, nafisi ya kumtupa mtoto ilimshinda. Akasogea kwenye kichaka na kumuweka Mtoto yule chini, hakutaka tena kumtupa, alimuweka Taratibu kabisa. Baada ya zoezi hilo alisimama na kumwangali Mtoto Yule, bado tu alikuwa amelala, alipomwangalia sana, alitamani ainame amchukue tena lakini pia alishindwa, hapo aligeuka na kurudi kwenye farasi wake. Wakati anapanda Juu ya Mgongo wa Farasi sauti ya Mtoto ilisikika akilia kuashiria kuwa anahitaji msaada. Askari yule alishindwa kumruhusu farasi aianze safari yake, aliendelea kusimama huku ikiwaza kuhusu Mtoto yule.

"Hata nikimsaidia nitampereka wapi?"

Askari yule alijisemea mwenyewe. Wakati huo sauti ya kilio cha Mtoto nayo ilizidi kumpagawisha. Alishindwa ikambidi ashuke tena Juu ya Farasi na kwenda kumchukua Mtoto Yule, baada ya kufika tu hivi Mtoto yule alinyamaza kulia na Kutabasamu kabisa. Ingawa alikuwa mchanga lakini kwa kitendo hicho askari yule alishangaa sana. Yule Mtoto alijuaje kama alikuwepo Mtu karibu yake wakati alikuwa bado hajaona. Basi Askari yule ilimbidi kumbeba tena Mtoto yule na kumpereka kwa ndugu yake aliyekuwa anaishi katika kijiji cha pili kutoka katika Ufalme wa Iyumbwi.

Hivyo ndivyo ilikuwa na ndiyo pona pona ya Mwana wa Lady Amana, ambaye kwasasa anajulikana kama Tamali. Mama yake alifariki miaka kumi na Saba iliyopita.



Kabla hujaendelea, Tafadhali naomba kushare ndugu zangu wasomaji. Unajua inatia uchovu sana kama nikuomba Kushare halafu Amsambazi.

Haya endelea.


Maisha ya Tamali katika Ufalme wa Nghumbi yalikuwa ya Furaha, aliheshimika sana kama Princess.

Kama ujuavyo masaa huwa yanakatika mwisho siku inaisha, na kuzidi kusogea mbele mpaka wiki hatimaye Mwezi unafuata. Mieze tisa ya mjamzito ilitimia, sasa ikabaki siku kwa ajili ya kumpokea Mtoto Mpya katika Falme ya Nghumbi. Mfalme na Malkia Velian walikuwa macho sana, na walikuwa wanaomba Princess Tamali Ajifungue Mtoto wa kiume ambaye baadaye atakuja kuwa Mfalme katika Ufalme ule wa Nghumbi.


Hatimaye siku ambayo ilikuwa inangojwa kwa hamu ilitimia, Hii ilikuwa siku ya jumanne, nyakati za Asubuhi kabisa Princess Tamali alianza kujisikia vibaya huku akidai anasikia Maumivu Makari hasa Tumboni. Madai yake yalitosha kuwapa Watu majawabu ya kuwa Alikuwa katika wakati wa Kujifungua Mtoto. Malkia Velian alijumuika na Wakunga katika Ufalme kwa ajili ya Kusaidia Jukum la kuhakikisha kuwa Princess Tamali anajifungua Salama.


Masaa matano tu Tangu hali hiyo imkute, alijifungua Mtoto. Kila mmoja alikuwa makini kuangalia ni Mtoto wa Kiume au wa kike. Malkia Velian ndiye alikuwa wa kwanza kuangalia kupata uhakika, alikuwa ni Mtoto kama aliyekuwa anamuwaza, kwani hata ndotoni alikuwa kaisha pata taarifa kuwa Ndani ya Nyumba yake kuna Mfalme. Alijisikia Raha sana Malkia Velian baada ya Mtoto wa Kiume kuzaliwa. Walihakikisha wanamfanyia Usafi haraka na Taarifa zikafika kwa Mfalme kuwa Mtoto kaisha zaliwa na ni Wakiume. Kitendo cha kuzipokea Taarifa hizo Mfalme alijikuta anacheka sana, furaha ilikuwa ni nyingi sana moyoni mwake. Taarifa hizo zilisababisha Mfalme Joktan kushindwa kukaa kusubili aletewe Mjuu kumuona, moja kwa Moja alitoka ndani mwake na kuelekea ndani Kwa Princess Tamali kushuhudia mwenyewe kwa Macho yake.

"Mfalme yupo nje anahitaji kuingia!"

Sauti kutoka nje ilisikika ndani Kwa princess Tamali ikimuombea Mfalme kuingia. Kwakuwa kila kitu kilikuwa kisha kuwa sawa Mfalme Aliruhusiwa kuingia.

"Tafadhali nahitaji kumuona Prince wa Falme ya Nghumbi!"

Hiyo ndiyo ilikuwa Kama salam kutoka kwa Mfalme. Aliletewa Kichanga mikononi mwake naye akakipokea vizuri. Alikiangalia sana Kichanga kile kisha akasema.

"Jina lako utaitwa CLEOPA, Jina lako litatukuzwa kila mahali, Utaeshimika na Kila Mmoja, utakuwa rafiki Mwema kwa Watu wako, Ufalme wako utaimalika kila sehemu, Utawala wako utakuwa ni wa Pekee na Utadumu Maisha marefu ewe Mfalme Mtukufu!"

King Joktan kwa Ujasiri kabisa alijikuta anayatamka maneno hayo Utafikiri alikuwa anamuapisha Mtoto aliyezaliwa kuwa Mfalme. Maneno yake yaliwashangaza watu karibu wote hasa Jina alilompatia Mtoto. Jina la Cleopa lilikuwa ni Jina la Muhasisi wa Kwanza wa Falme hiyo Ya Nghumbi yaani King Cleopa. King Cleopa wa Kwanza alikuwa na Nguvu kweli kweli na Alijua kutumia nguvu zake vilivyo katika Mapambano ya Vita, kitendo kilichoperekea Mpaka wakamuita Jina la Mfalme wa Vita.

"Hongera sana Mwanangu Princess Tamali kwa kinipatia Mtoto Atakaye Kuja kuwa Mfalme!"

Mfalme alisema tena kwa Mara nyingine kumpongeza Tamali, kisha akageuka na kutoka Inje.

Ndani watu walibaki wakijiuliza Mwaswali kwanini Mfalme Joktan aliyanena maneno yale. Mkewe Malkia Velian Aliwaza kuwa Labda Mfalme anakaribia kufariki ndiyo Maana.

Waliendelea kuyatafakari lakini hawakupata Jawabu.


Baada ya Mfalme kutoka ndani mwa Princess Tamali, alienda kutoa Taarifa za kuitisha kikao cha Dharula katika Ufalme. Aliwaita Mawaziri na Makatibu wake, pamoja na

watu wengine muhimu katika Ufalme.

Ndani ya Kikao Kabla Mfalme hajaanza kuzungumza swala ambalo alikuwa amewaitia Mawaziri na Makatibu wake, Mfalme alimuita Askari wake Mmoja na Kumnong'oneza. Kitendo hicho kilichukua sekunde kadhaa kisha Askari aliondoka ndani ya Kikao hicho na kumwacha Mfalme na Baraza lake.

"Sina maneno mengi ya kuzungumza na Ninyi ila nina Jambo moja tu kubwa. Jambo hili ni kwamba Ufalme wetu kupitia Princess Tamali umepata Prince!"

Mfalme alisema. Watu wote waligeukiana kuangaliana, muda huo huo wakapiga makofi na kupiga kelele za kumpokea Prince katika Ufalme.

Muda huo huo ndani ya Kikao waliingia Malkia Velian pamoja na Tamali huku Lady Divine wa Falme hiyo akiwa mbele yao kama kuwaongoza.

"Nilichokuwa nakiongea nazani ndicho hichi mbele yenu!"

Mfalme Joktan alisema tena baada ya kumchukua Mtoto mikononi mwake na kumuinua Juu kuwaoneshea Viongozi wake aliokua anasaidizana nao katika Jukum la Kuliongoza Taifa lake la Kifalme. Watu wote waliokuwemo kwenye hicho kikao waliinamisha vichwa vyao chini kuitoa Heshima kwa Prince katika Ufalme wa Iyumbwi.

"Jina lake ataitwa CLEOPA, kwahio kuanzia sasa tutamuita Prince Cleopa. Huyu ndiye Mfalme wa Siku zijazo, na wala sitarajia Mfalme mwingine Tofauti na huyu. Kwa maana hiyo natarajia ushirikiano wenu wa Kutosha kwa Mwana wa Kifalme Prince Cleopa. Nahitaji kila Mmoja awe Mlinzi wake kila atakapokuwa. Asanteni!"

Mfalme Alisema tena. Watu wote waliinamisha chini vichwa na kusema.

"Ndiyo Mfalme, Tunamuombea Prince Maisha Marefu!"

Baada ya kusema hivyo hakuna Jambo geni ambalo liliendelea pale kikao kilifungwa.


Siku hiyo katika Ufalme wa Nghumbi ilikuwa ni sikukuu ya kipekee, watu walikuwa wenye Furaha sana. Waliarika ngoma za Asiri na watu wakacheza kuifurahia siku ya Kumpokea Prince katika Ufalme wao.

Mfalme Joktan alikuwa mwenye Furaha wakati wote, Mkewe Malkia Velian ndiye Usiseme. Ingawa hakuwa na Mtoto lakini alijiona kuwa Yeye ndiye kamzaa Mtoto yule.


Toka siku hiyo maisha ya Malkia Velian yalikuwa Machangamfu wakati wote, alijisikia Furaha sana. Kila Asubuhi alikuwa anakwenda katika Chumba cha Princess Tamali kumwangalia Prince Cleopa, vile vile kwa Mfalme. Hawakuthubutu kuacha hata Mara moja kwenda kumwangali Mtoto yule. Siku moja Malkia alipoingia ndani kumuona Prince alisema.

"Bila Shaka Princess Sophia kaisha zipata Taarifa kuwa Prince wake kaisha zaliwa!"

Maneno yake yalimshangaza sana Tamali kisha akauliza.

"Unamaanisha nini Mama?"

Tamali aliuliza, alipenda kumuita Queen Velian Mama kwani ndilo jina ambalo aliona linathamani kubwa kwa Malkia Velian kuliko kumuita Malkia.

"Namaanisha kuwa Malkia wa Ufalme huu wa Baadaye Kaisha zipata taarifa kuwa Mfalme wake kaisha zaliwa. Malkia huyo anatoka katika Ardhi ya Iyumbwi. Huyu Malkia jina lake anaitwa Sophia, jina hilo Mimi ndiye nilimpatia. Ni mwanamke mzuuri mwenye mvuto kama wewe!"

Malkia Velian aliamwambia Tamali. Kwa mbaali Tamali alijikuta napata wasiwasi. Hali hiyo Malkia aliiona na kuuliza.

"Mbona unaonekana kuwa mwenye wasiwasi?"

"Hapana Mama niko sawa tu!"

"Najua unawasiwasi kwasababu Ufalme wa Iyumbwi ni Maadui wako, lakini usiwe na Shaka hawatojua kamwe na nazani mapenzi ya Prince Cleopa na Princess Sophia hayatoweza kuzuilika kwani ishaandikwa. Labda niseme kuwa wao wenyewe ndani ya nyoyo zao washakubaliana tayari!"

Malkia Velian alisema. Wakati anayasema hayo Prince Cleopa bado alikuwa ni Mchanga, Princess Sophia kwa wakati huo alikuwa kaisha timiza miezi minne tayari.

"Sawa Mama nimekuelewa!"

tamali alikubali tu, lakini ni kwasababu alikuwa anamwamini sana Malkia Velian. Princess Tamali alikumbuka kuwa Wakati akiwa Mjamzito Malkia alisema kuwa ndani ya Nyumba kuna Mfalme na Aliwahi kutamka kuwa Mfalme huyo ndiye atamuoa Sophia. Hicho ndicho kilimpa matuamini naye akaamini kama Malkia alivyokuwa anaamini kuwa Mapenzi ya Cleopa na Sophia yameandikwa.


Taarifa za kuzaliwa kwa Prince Cleopa ndani ya Falme ya Nghumbi zilifika pia Iyumbwi. Katika Falme ya Iyumbwi taarifa hizo zilifika mapema sana kwa Ishara kupitia Mtoto wao Sophia, wakati huo yeye alikuwa akilia wakati wote, mpaka siku taarifa inafika rasimi katika Ufalme ule kuwa Ndani ya Falme ya Nghumbi kazaliwa Prince ndio siku ambayo Sophia alianyamaza na Kucheka. Tena siku nzima kwa Mtoto yule ilikuwa ni Furaha ya kupindukia, hakulia kabisa siku hiyo, hata pale alipoisi njaa hakulia badala yake alikuwa anakula vidore vyake ndipo walipogundua kuwa anaisi njaa.

"Ni nani ambaye kajifungua Mtoto huko Nghumbi wakati tunajua kabisa kuwa Mke wa Mfalme hana uwezo wa Kuzaa?"

Ni swali ambalo watu wa Falme ya Iyumbwi akiwemo Mfalme wao King Yolam walikuwa wanaulizana.

"Mimi nimesikia kuwa Mfalme Joktan alikuwa na Mtoto wa kike ambaye alimzaa na Mwanamke Mwingine inje ya Ufalme, kwahio huyo Binti mfalme ndiye Kajifungua Mtoto wa Kiume!"

Waziri Mkuu wa Iyumbwi alisema. Wakati huo alikuwa amekaa yeye na Mfalme wake wakizungumzia taarifa za Prince Cleopa wa Nghumbi.

"Kwahio hata Malkia Velian amekubaliana na swala hilo?"

"Bila shaka, isingekuwa amekubali asingekubali huyo Mtoto aitwe Prince na kutangazwa kwa kiasi hicho ndani ya Ufalme. Tazama Leo ni wiki tu Tangu kuzaliwa kwa huyo Mtoto!"

"Ni kweli kabisa Waziri mkuu. Lakini..........basi sawa!"

Mfalme Yolam alitamka hivyo, alikuwa anahitaji kuzungumza Jambo lakini akalimezea, hakutaka kulitamka kwa Waziri mkuu wake. Hivyo ndivyo taarifa za kuzaliwa kwa Prince Cleopa zilipokelewa katika Ufalme wa Iyumbwi.


Hatimaye Mwezi na Siku kumi za Kuzaliwa kwa Prince Cleopa zilifika. Mfalme wa Iyumbwi King yolam alikuwepo katika kuazimisha siku Arobaini zakuzaliwa kwa Prince Cleopa. Yeye alifika peke yake pamoja na Ulinzi, Mkewe Malkia Eda alibaki Iyumbwi. Licha ya Hivyo sherehe zile zilienda vizuri kupita maelzo. Ilikuwa tamu kuliko hata aliyofanyiwa Princess Sophia wa Iyumbwi. Mpaka Mwisho wa shereh hizo kila Mmoja alifurahi vya Kutosha, hakuwa King Yolam wala Mtu yoyote ambaye hakufurahia Tukio hilo. Kitu cha pekee ambacho akikugundulika Mpaka Mfalme Yolam anatoka katika Ardhi ya Nghumbi kurudi katika Ufalme wake wa Iyumbwi ni kuhusu Tamali, hakujua kabisa kuwa Tamali ndiye Mtoto wa Aliyekuwa Lady Divine katika Ardhi ya Iyumbwi, Lady Amana.

Hivyo ndivyo sherehe zile za aina yake zilikuwa.


MIAKA SABA BAADAYE.

Akiwa na Umri wa Miaka saba tu Cleopa alianza kujifunza jinsi ya kupigana, kurusha mishare, pamoja na Kupigana kwa kutumia Upanga. Hali hiyo alikuwa akiwashangaza sana watu wote katika Ufalme wa Iyumbwi. Alipokuwa anazuiliwa alikataa na kulia akidai kuwa lazima awe hodali. Lakini kila alipokuwa anamaliza kujifunza ndani ya Jumba la Ufalme alipenda kwenda kutembea Inje ya Jengo la Ufalme kwa Watoto wenzake ili kucheza nao. Hakutaka kabisa Ulinzi wa kumlinda, alikuwa anasema kuwa Marafiki zake ndio walinzi wake.

Hali hiyo haikuwa kwa Cleopa tu hata kwa Sophia pia, ingawa alikuwa ni msichana lakini alipenda kujifunza kupigana kwa kutumia Upanga, kurusha mishare pamoja na kupigana Kwa mikono mitupu. Pia hivyo hivyo kama ilivyokuwa kwa Cleopa naye alipenda sana kutoka inje ya Ufalme, ila kwake alikuwa akizuiliwa kutoka mara kwa mara, mara chache sana Mfalme alikuwa akimruhusu yeye na Ndugu zake pamoja na Ulinzi wanatoka kutembea inje ya Jengo la Ufalme.


Huko Nghumbi Prince Cleopa aliwazoea Sana Watoto wenzake wa Mitaani, alikuwa anawaperekea Zawadi mbali mbali kutoka katika Jumba la Ufalme. Wototo wenzake walimpenda sana, walimpenda kuliko hata kawaida. Mpaka wakati mwingine walikuwa wanaapa na kuvirudia viapo vyao kwake kuwa watamlinda kwa namna yoyote ile asidhurike. Na si hivyo tu wakati mwingine walikuwa wanamuita Mfalme wao. Kutokana na Mapenzi hayo Makubwa kwa Wenzake, Prince Cleopa aliwashauri wenzake waanze kujifunza pia jinsi ya kujilinda na kumlinda yeye, alifanya hivyo kwasababu yeye alipenda sana kujifunza. Swala hilo lilipokelewa vizuri sana na wenzake, kisha kwa pamoja walianza kujifunza mapigano walipokuwa Majumbani mwao. Wazazi wa watoto wale walipokuwa wanajaribu kuwazuia watoto wao kujifunza Mapigano, Watoto walilia na kudai kuwa wanafanya hivyo ili wawe walinzi wazuri wa Prince au Mfalme wao Cleopa, kwahio walilazimika kuwaacha. Wakati mwingine walipokuwa pamoja na Cleopa alikuwa anawafundisha namna ya kupambana pia. Kwa hali hiyo walijikuta urafiki wao unazidi kudumu na kukuwa zaidi na zaidi, na walikuwa wanazidi kuimalika hata kimwili katika nyanja ya mapigano. hata wazazi wa watoto marafiki wa Cleopa walilazimika kuwafundisha Watoto wao kupambana na wengine kuwatafutia watoto wao Walimu wa kuwafundisha.


Siku moja kama ilivyokuwa imezoeleka kwa Cleopa kutoka na kwenda kucheza na Wenzake, alimkuta Mmoja aliyekuwa anajuliakana kwa jina la Manase, akiwa amevaa mavazi ambayo yalifanana na Mavazi ya Jeshi la kifalme, kitendo cha kuona vile Cleopa alishangazwa na kumuuliza.

"Manase mbona leo umavalia nguo hizo za Jeshi huoni kama unalivunjia jeshi heshima?"

"Hapana Cleopa, ni kwamba nimeota ndoto nikiwa kiongozi wa Jeshi la Kifalme ndio maana niameamua kuvaa hivi!"

"Unasema umeota ndoto?!"

Cleopa aliuliza kwa Mshangao kwani hakujua Ndoto ni nini.


Kabla sijaimaliza hadithi hii soma hapa ni muhimu pia.

Swali aliloulizwa lilikuwa ni rahisi kujibiwa lakini Cardin Solomon alishindwa kujibu. Kweli alichokizungumza yule Binti kilikuwa cha kweli, kabisa, na kilichokuwa kinamfanya Cardin Solomon asijibu swali kwa wakati ni yule Askari, yeye alikuwa amekaa pembeni ya yule Binti.

"Sina la kusema kwasababu familia yangu ishaangamizwa!"

Cardin Solomon alisema.



"Ndiyo, nimeota ndoto nikiwa mkuu wa Jeshi la Kifalme na Nilikuwa nikipigana vita!"

Manase alisema tena. Bado alimshangaza sana Cleopa.

"Ndoto ni nini?"

Cleopa aliwauliza wenzake. Wote waligeukiana kisha wakacheka. Hali hiyo ilimfanya ajione mnyonge sana.

"Usiudhunike Prince tutakwambia maana ya ndoto nini!"

Manase alisema. Wenazake nao pia wakamuunga mkono kumliwaza Prince wao.

"Basi nambieni hiyo ndoto inakuwaje na Mimi nikaote siku nakuwa Mfalme!"

Cleopa alisema, kisha wenzake wakaanza kumsimulia ndoto zao. Walikuwa wakimwambia kuwa huwa tukilala tunaota ndoto.

"Kwahio ukilala tu ndio unaota ndoto?"

Cleopa aliuliza tena. Alitamani kujua sana kuhusu ndoto.

"Ndiyo, kwani wewe ukuwahi kuota ndoto?"

Mmoja wa watoto wale aliuliza huyu alikuwa anaitwa Yona.

"Ndiyo Yona, sikuwahi kabisa kuota ndoto ndio maana nawauliza ninyi mnambie jinsi hiyo ndoto inavyokuwa.

"Daah! pole sana, Mimi nishaota ndoto nyingi, ambazo Mara zote zinanifurahisha zingine zinanitisha. Kila nikiota huwa namuuliza mama, Mama huwa ananiambia kuwa ni kawaida tu!"

Mtoto mwingine tena alisema. Huyu alikuwa anaitwa Mdogwa.

Karibu watoto wote walisema mambo kuhusu ndoto. Tena walianza kumsimulia ndoto ambazo washawahi kuziota. Zingine alizipenda sana, kwani zilimfurahisha sana Prince Cleopa. Zingine zilimtisha lakini alivumilia sana kuzisikia. Alijisikia furaha sana siku hio, kwani ndoto karibu zote alizosimuliwa zilikuwa nzuri.

Muda ambao alikuwa amezoea kurudi katika Ufalme alipowadia alirudi, watoto wenzake walipenda kumsindikiza Mara nyingi mpaka karibu kabisa na geti la Jumba la Kifalme ndio wanarudi.

Baada ya kuingia ndani jambo la Kwanza alifikia kwa Mama yake.

"Mama naomba unisimulie kuhusu ndoto ambayo ushaiota, kwani Marafiki zangu Leo wamenisimulia ndoto zao!"

Maneno ya Mwanaye yalimfanya kutabasamu kwanza.

"Cleopa mwanangu, unapenda kusimuliwa ndoto?"

"ndiyo Mama, napenda ndoto kwani ni Nzuri zinafurahisha!"

"Haya Usijali nitakusimulia ndoto nzuri ambayo Mimi niliiota!"

Mama alisema kisha akaanza kumsimulia Cleopa kisa kizuri.

INAENDELEA....

Post a Comment

0 Comments