Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Responsive Advertisement

Simulizi: Ujumbe Kutoka Ndotoni (Notification From The Dream) Sehemu ya Sita (06)



Kundi kubwa la Maaskari likiwa lishaingia Mtaani kuwasaka, Lady Amana na Foibe ndio walikuwa wanatoka nje ya njia ya siri na kuanza kupandisha mlimani ili watokezee upande wa pili kulikokuwa na Kijiji kingine kwa ajili ya kutafuta msaada wa usafiri kuwakimbiza kijiji cha pili kutoka katika Ufalme, huko ndiko alikuwa anaishi Mjomba wake na Foibe. Na ndiko Foibe alikuwa anampereka Lady amana akaishi huko. Walijitahidi kutembea kwa haraka kuupandisha mlima huo na kuuteremka mlima huo. Kweli walifanikiwa kufika katika kijiji hicho bila kukutwa na kundi la Maaskari waliokuwa wametumwa na Mfalme. Walipofika hapo walikutana na wafanya biashara wa masafa. Wafanya Biashara hao walikuwa ni kikundi na walikuwa wanaume tu. Kikundi hicho pia kilikuwa na farasi wao, Farasi wengine walikuwa wamebeba mizigo na wengine walikuwa ni kwa ajili ya kubeba watu katika Msafara huo.

Bahati nzuri huo msafara wa wafanyabiashara alikuwepo Mtu Mmoja aliyekuwa anamjua Lady Amana. Lady amana naye alipomuona alimuomba msaada amsaidie ili haweze kufika alikokuwa anaelekea.

"Usijali na kwa bahati nzuri Mimi ndiye Mkuu wa msafara huu, naomba upande Juu ya farasi yangu hii na ujifunge vizuri mavazi yako, najua hawatoweza kukuona hata wakifika, na wakiuliza Mimi nitawambia kuwa huyu ni Mke wangu!"

Kama alivyoelekezwa, kwa haraka Lady Amana alivishwa vazi la kufunika kichwa chote na kuacha sehemu ndogo sana ya Uso wake, kwa jinsi ambavyo alikuwa amefungwa, ilikuwa si rahisi mtu kuona na kugundua kuwa ni yeye, kwa kuwa Farasi walikuwa wa kutosha katika msafara ule, hata Foibe naye aliombwa avae kama Lady Amana kisha akapanda Juu ya Farasi na Msafara ukaanza kuongoza njia kuelekea katika kijiji cha mbele kutoka katika Ufalme wa Iyumbwi.


Nyuma askari nao waliendelea kuwasaka kwa juudi zote. Lady Amana na kundi lile la wafanya biashara wakiwa wanatembea taratibu mara kundi lingine la askari wa Jeshi la Iyumbwi walitokea mbele yao.

"Tunaomba msimame ili tuwakague!"

"Kwanini?"

"kuna watu wetu wametoroka ndio tunawatafuta!"

"Watu wanafanana je?"

"Wanawake wawili"

"Lakini hatujawaona huku watu wa namna hiyo!"

Basi subili tufanye uhakiki wetu ili tuthibitishe haya unayo yasema"

Askari mmoja aliuliza.

Nao walisimamisha lakini Lady Amana pamoja na Foibe walikonyezwa wasishuke juu ya Farasi waendelee kukaa.

Kweli Askari walianza upekuzi wao kwenye mizigo ya wafanya Biashara wale. Walijitahidi sana, huku umakini ukiwa umewatawala.

Wakati zoezi linaendelea, Askari Mmoja alikuwa anamuangalia sana Lady Amana, Askari huyo alikuwa akimtilia wasiwasi sana Lady Amana, alikuwa anamfananisha ila alikuwa hana hakika kama ni yeye.

"Na Mwanamke huyu ni nani?"

Hatimaye Askari yule aliuliza baada ya kukosa Hujasiri!!

"Huyu ni Mke wangu, na huyu ni mfanya kazi wangu!"

Mwanaume aliyekuwa Mkuu wa msafara alisema. Jawabu lake lilitosha kabisa kwa askari Yule kunyamaza, kwani lilimrizisha na bahati mbaya zaidi kwa maaskari wale ni kwamba hata Mfanya Biashara huyo walikuwa wanamjua kwahio ilikuwa lazima wakiamini kile walicho jibiwa.

Baada ya kufanya ukaguzi wao bila mafanikio hatimaye Askari waliuruhusu msafara wa wafanya Biashara uwendelee na safari yao kuelekea katika Kijiji cha Pili kilichokuwa kinajulikana kwa Jina la KIJIJI CHA MILAKANI


Kwa kusaidiwa na Wafanya Biashara hatimaye walifika katika Kijiji hicho, Foibe alimpereka Lady Amana kwa Mjomba wake ili kumuifadhi. Mjomba alimpokea vizuri na kuahidi kumlinda kwa namna yoyote ile. Mazingira ya nyumba ya mjomba yalikuwa hayana Mashaka.

"Utakaa hapa na sitaruhusu wewe utoke inje hovyo hovyo, utakuwa unakaa ndani wakati wote ili kujilinda na Jeshi la Mfalme maana linaweza kufika sehemu hii!"

"Nashukuru sana kwa mapokezi yako!"

Lady Amana alisema, machozi yalikuwa yanamtoka kabisa.

"Usilie Lady Amana hapa upo sehemu Salama, nitakulinda, na hii itabaki kuwa siri yangu, Foibe pamoja na wewe.

Mimi mwenyewe kama unavyoniona Sina mke, nakaa peke yangu. Mke wangu alifariki miaka miwili iliyopita. Tangu hapo niliishi peke yangu. Foibe ni Mjomba wangu!"

Mjomba wa Foibe alisema. Hata yeye pia Machozi yalianza kumtoka, alimkumbuka Mke wake aliyekuwa anampenda.

"Pole!"

Lady Amana alisema, wakati huo huo alilishika vazi lake, na kuupeleka mkono wake wa kulia mpaka kwenye Uso wa Mwanaume Yule na Kumfuta Machozi yake. Kitendo hicho cha pekee kilifanya wote kwa pamoja kubaki wanaangaliana.

"Jamani Chakula tayari, naombeni mkaribie"

Wakati Bado wakiwa wanaangaliana sauti ya Foibe ilisikika ikiwasemesha kwa ajili ya Chakula.

Wote kwa pamoja walishituka. Kisha mjomba akasogea na kukaa kwa ajili ya chakula, hivyo hivyo kwa Lady Amana.

Tangu siku hiyo Maisha ya Lady Amana yaliendelea kuwa pale na hata Askari wa Kifalme walijitahidi sana kumtafuta bila Mfanikio. Malkia Sayuni na Mwanaye Mfalme Yolam hawakukata tamaa ya Kumtafuta, waliendelea kumtamfuta kwa Umakini kila sehemu ndani ya Vijiji karibu Vyote vilivyokuwa vinaunda Falme ya Iyumbwi, pamoja na Vijiji vilivyokuwa vinaiunda Falme ya Nghumbi. Ingawa tayari makubaliano ya ushirikiano yalikuwa yashasainishwa, ila Askari wa Kijeshi kutoka Iyumbwi waliingia Nghumbi kiwizi na walikuwa wamevaa mavazi ya kawaida ili kuepuka migogoro. Sababu kubwa ilikuwa ni kumtafuta Lady Amana kiusiri bila kugundulika kuwa waliingia kinyemela. Hata hivyo kwa kibali wasinge ruhusiwa kwa misingi ya kuilinda Amani.

*********

Baada ya Miezi Sita tangu kutoka katika Ufalme wa Iyumbwi Lady Amana alijifungua Mtoto wa kike, alijisikia faraja sana. Alikuwa anawaza na kuomba sana mwanaye awe mtoto wa kike, kwani kwa wakati huo angekamatwa angeuliwa pamoja na Mwanaye endapo angekuwa wa kiume. Hivyo ndivyo alikuwa anawaza. Hata hivyo aliambiwa na Malkia Sayuni kuwa endapo mwanaye akiwa wa kiume lazima auawe lakini akiwa wa Kike itakuwa pona pona yake. Kwahali hiyo Lady Amana alijikuta anafurahi sana huku akijisemea kuwa hata akikamatwa basi hatouawa kwasababu amejifungua mtoto wa kike.


Siku tatu baada ya kujifungua hata kabla hajampa mwanaye jina, Jeshi la Mfalme Yolam lilifika sehemu ambayo Lady Amana alikuwa akiishi pamoja na Mjomba wake Foibe na Foibe Mwenyewe.

Walimkamata Lady Amana na kumrudisha katika Ufalme kwa Mfalme Yolam. Kabla hajafikishwa katika Ufalme njiani alifungwa kamba ndefu mikononi na kuiunganisha moja kwa moja na Farasi aliyekuwa amekaliwa na Kamanda wa kikosi kile. Ingawa walikuwa hawakimbii lakini walifika katika Jumba kubwa la Utawala wa Iyumbwi, masikini Lady Amana akiwa hoi kabisa, kwani hata huko njiani alipokuwa anashindwa kutembea walikuwa wanamtandika bakora ambazo zilimfanya kulazimika kusimama na kuanza kutembea. Mwanaye walimbeba maaskari wenyewe na alikuwa amelala kabisa njia nzima. Safari yao kutoka katika kijiji cha Milakani ilikuwa ni ndefu sana, kwani iliwachukua lisaa na dakika kadhaa.


Kitendo cha kufikishwa pale katika Ufalme, kilileta Mshangao sana kwa Watu ndani ya Ufalme. Kilichokuwa kinawashangaza ni Kitendo cha Lady Amana kuzaa Mtoto. Mwanzo watu walizipata Taarifa kuwa Lady Amana ametoroka katika Ufalme, lakini wengi wao walikuwa hawajui ni Sababu ipi ambayo ilimtorosha. Lakini siku hiyo watu wengi walijua ni sababu gani ilimfanya kutoroka katika Jengo la Ufalme wakati wao waliamini kuwa alikuwa ni Mwanamke Bikira na mchamungu.


Baada ya kumfikisha katika utawala moja kwa moja aliperekwa kwa Mfalme Yolam na wakati huo huo Lady Sayuni alifikishiwa taarifa kuwa Lady Amana kakamatwa na Kaisha jifungua Mtoto wa Kike, Mwanamke Yule alitoka haraka ndani mwake na Kuelekea katika Chumba cha Mfalme Yolam ambaye alikuwa mwanaye wa Kuzaa.


Wakati Malkia Sayuni anaelekea katika Chumba cha Mfalme, Mfalme naye alikuwa anaendelea kuongea na Lady Amana.

"Lady Amana, najua kabisa ulikimbia kwasababu ya kujikomboa, na hukutaka mwanao hadhurike, lakini hamna Jinsi kwasababu inapaswa mwanao Afariki japo ni wa kike lakini pia hata wewe!"

Mfalme Yolam alisema.




Wakati huu Malkia alikuwa amekaa ndani mwake ametulia Mara mlangoni aligongewa ili Lady Divine aingie ndani.

"Mbona unaonekana una Mashaka kiasi hicho Eunike!"

Malkia aliuliza baada ya kusalimiana na Eunike. Ilikuwa ni asubuhi nyakati za saa mbili.

"Nina Jambo nahitaji kukwambia Eee mtukufu Malkia!"

"Jambo gani hilo Eunike?"

"Usiku wa leo nimeona maono kupitia ndoto!"

"Maono gani Eunike?"

Malkia aliuliza haraka, alijikuta anapata wenge la kuhitaji kujua haraka kile ambacho Eunike alitaka kumwambia.

"Nimeona Ndoto kama ile ile, ambayo niliiona siku za nyuma!"

"Unasema?!"

Malkia aliuliza kwa mshangao sana, hakutarajia kabisa kusikia kitu kama hicho. Maono ya Lady Divine yaliaminika na kila Mmoja katika Ufalme ule.

Lady divine alirudia tena kusema maneno hayo. Malkia hakutaka tena kuendelea kuzungumza na Lady Divine Eunike, alimuomba urudi amwache yeye atafakari kwanza. Kwa utaratibu kabisa Lady Divine Eunike alitoka katika chumba cha malkia na kurudi sehemu yake.


Baada ya kuyatafakari maneno aliyo ambiwa, Malkia Sayuni aliamua kwenda kwa Mwanaye kujadili kuhusu maono hayo.

"Mama Unataka kunambia kuwa hatujafanya la Maana kumuua Lady Amana?"

Mfalme alisema baada ya kufikishiwa taarifa za maono ya Lady Divine Eunike.

"Ndio maana yake!"

"Hapana Mama, lazima kuna kitu!"

"Kitu gani Yolam, hapa cha kufanya ni kumtafuta huyo Mwanamke Mwema mwingine, aliyezaa au Mtoto yoyote ambaye katoka katika kizazi cha Mwanamke mwema. Hivyo tu ndio itakuwa njia ya kulimaliza tatizo hili. Na labda kitu cha Msingi nikuombe swala hili lifanyike kwa usiri sana, lisijulikane kwa watu na nitamzuia Lady Divine Eunike asiliseme swala hili kwa Mtu yoyote hata kama ni Waziri mkuu. Tutafanya sisi wenyewe na tutakamilisha!"

Malkia sayuni alisema. Mwanaye Mfalme Yolam hakubishana na kauli ya Mama yake. Mazungumzo yao yalichukua muda sana, huku wakipanga mbinu za kumtafuta mwanamke ambaye ni Mwema halafu anamtoto, huyo Mtoto wamuue, au Kama mwanamke huyo atakuwa mjamzito auliwe. Mipango yao ilikuwa mizuri na hatimaye walikubaliana kuwa Mfalme na Malkia Sayuni wataanza kutembelea kijiji mpaka Kijiji kwa ajili ya kuwatafuta wanawake wema wenye watoto. Walipanga kuwa watakuwa wanatoa taarifa kuwa Wanawake Wote wenye watoto wadogo kuanzia mwezi Mmoja mpaka miaka miwili walitakiwa kufika na Watoto wao sehemu husika kwasababu mfalme alihitaji kuwapa zawadi.

Mpango wao huo ulikuwa maridadi sana.


Kama walivyokuwa wamepanga. Baada ya wiki moja Malkia Sayuni Pamoja na Mfalme Yolam Waliamua kuanza kuvitembelea vijiji vilivyokuwa vinaunda Falme ya Iyumbwi.

Kila kijiji ambacho walikuwa wanafika waliwaita wanawake Wote katika nyumba za viongozi wa Vijiji hivyo, kulikuwa na zawadi ya vikuku vya Dhahabu ndivyo walikuwa wanawapa wanawake wale.

Kwanza walikuwa wanawauliza mwaswali kama ifuatavyo.

1. Wewe ni nani?

2. Uliwahi kuwa nani?

3. Wazazi wako walikuwa akina nani katika Ufalme wa Iyumbwi?

Maswali hayo matatu ndiyo yaliwapa wanawake zawadi ya Vikuku vya dhahabu kama sehemu ya mapambo katika mihili yao.

Wanawake wengi walijitokeza katika swala hilo. Zoezi lao liliwapa matumaini makubwa sana, kwani walifanikiwa kuwapata wanawake zaidi ya watano ambao wengine Mama zao waliwahi kuwa Miongoni mwa Mabikira katika Ufalme wa Iyumbwi na wengine katika yao waliwahi kuwa Mabikira. Si kwamba walifanikiwa kuchaguliwa kuwa Ma lady Divine hapana ila walikuwa miongoni mwao kwa maana hiyo pia walikuwa na upako wa wanawake wema.

Baada ya kuwapata wanawake hao, Mfalme Yolam na Malkia Sayuni hawakuangaika, kila Kijiji ambacho alipatikana mwanamke wa Namna hiyo waliwatuma Askari usiku huku wakia wamevalia mavazi ya kawaida kwa lengo la kuangamiza. Kweli walifanikiwa kuwaua wanawake Wote pamoja na watoto zao. Askari wale walipokuwa wanaua walizichukua maiti na kwenda kuzitupa mashimoni kabisa ili isilete utata kwa watu katika vijiji.


Zoezi lao hilo liliwachukua siku chache sana, kisha wakarudi katika Ufalme. Baada ya kufika pia walipokelewa kwa furaha sana na Watu katika Ufalme, wengi waliamini kuwa alichokuwa anakigawa kwa wanawake wale ndio ilikuwa dhamila iliyomtoa katika Ufalme, kumbe yeye alikuwa na Dhamila nyingine kabisa. Toka hapo Lady Divine hakupata kuona tena maono ya Kuhusu Ufalme wa Iyumbwi kuungana na Falme ya Nghumbi. Falme ya Iyumbwi uliendelea kuwa safi kabisa.

Baada ya Mwaka Mmoja tangu matukio Yale kutokea, Mfalme Yolam alifanikiwa kupata watoto wawili Mapacha wa kiume kutoka kwa Mke wake Queen Eda.

Mtoto wa kwanza alimuita Zayoni, akimaanisha Baba yake, na Mtoto wa Pili alimpa Jina lililokaribia kufanana na la kwenye kitabu cha Hadithi ya Kweli, alimuita mwanaye jina la Ziliopa elufi moja tu tofauti na jina la Zileopa, na alifanya hivyo ili kuibainisha ahadi yake kwa Mfalme Joktan wa Nghumbi. Hakuogopa kabisa kwasababu ilikuwa imeandikwa kuwa King zileopa atatoka katika Kizazi cha Mke Mwema.


Mwezi Tangu Mke wa Mfalme apate watoto wawili Mapacha Mama Mfalme, Malkia Sayuni alifariki Dunia. Kifo chake, kiliacha Simanzi na maumivu kwa Watu Wote katika Ufalme wa Iyumbwi. Walimfanyia mazishi ya Heshima ya Hali ya Juu kabisa. Ingawa Mama yake alifariki akiwa bado anamuhitaji, Prince Yolam alijisikia Faraja kwasababu Mama alifariki akiwa amewaona Watoto wake.

Mwezi tena baada ya Kufariki kwa Malkia Sayuni, Lady Divine Eunike aliota tena ndoto nyingine na kwenda kumwambia Mfalme Yolam pamoja na Mkewe Malkia Eda.

"Nimeona maono kupitia ndoto kuwa; Malkia Eda Atazaa watoto wengi sana, wakike na wa kiume, lakini wa Mwisho atakuwa wa Kike na Ataolewa na Prince katika Falme ya Nghumbi"



Taarifa hizo zilimshitua sana Mfalme Yolam na Mkewe Malkia Eda.

"Lakini hakuna Tatizo kwasababu Nghumbi ni Marafiki na ikiwa hivyo nitaweza kumtumia huyo Mwanangu kuifanya Falme ya Nghumbi kuwa sehemu ya Taifa la Iyumbwi"

Mfalme Yolam Alisema. Huku akimwangalia mkewe Malkia Eda.

"Nakupenda sana ewe Malkia wa Ardhi hii ya Iyumbwi!"

Baada ya kumwangalia mkewe, King Yolam Alisema.

"Nami pia Nakupenda Ewe Mfalme wa Ardhi hii ya Iyumbwi"

Malkia naye alimrudishia Mumewe Mfalme neno hilo Zuri. King yolam hakuishia maneno alisogeza kichwa na kumchum Malkia wake kwenye paji la Uso.

Hapo kila Mmoja alitabasamu, wakati huo watoto wao walikuwa kitandani wamelala, na Lady Divine Eunike alikuwa akiwatazama.

"Nashukuru Lady Divine, mwanamke mtukufu katika ufalme kwa Taarifa hizi nzuri, nakutegemea na kukwamini kwa ajili ya Ufalme!"

"Ahsante na nami nakuombea uzidi kuwa Mfalme mwema na Ufalme wako Udumu milele!"

Lady divine Eunike alisema kisha akaondoka katika nyumba ya Mfalme.


BAADA YA MIAKA KUMI NA SITA.


Maisha ya Falme zote za Iyumbwi na Nghumbi ziliendelea kuwa katika amani, Watu wa Sehemu hizi waliishi kwa usawa. Kama ambavyo Mfalme Yolam na King Joktan walivyokuwa wameongea na kuweka mikataba ya Ushirikiano. Kwa hali hiyo Falme Hizi ziliendelea kushirikiana kwa kila namna.

Ilikuwa ni Siku ya Ijumaa, hii ilikuwa ni siku muhimu sana kwa Mfalme wa Taifa la Iyumbwi King Yolam. Alikuwa anasherehekea kupata Mtoto wa nane katika kizazi chake na Malkia Eda. Mtoto huyu alikuwa wa Kike na alikuwa ni mtoto wa tano katika watoto wa Kike ambao Mfalme Yolam na Mkewe Malkia Eda walijaliwa kuwapata. Watoto wa Kiume walikuwepo Watatu, wawili wakiwa ni Mapacha Zayoni na Ziliopa.

Kwa Kuona kuwa Sherehe hiyo ilikuwa ya Muhimu King Yolam alimwalika King Joktan wa Nghumbi na Mkewe Queen VELIAN

Masikini Mpaka wakati huo Mfalme Joktan na Mkewe Malkia Velian walikuwa hawajajaliwa kabisa kupata Mtoto. Walikuwa washaiomba Miungu ya Ardhi ya kwao ya Nghumbi iwapatie Mtoto hata Mmoja wa Kujifariji naye, lakini maombi yao hayakufua dafu kwa muda huo wote. Mapema kabisa nyakati za saa mbili Mfalme Joktan na mkewe walifika katika Ufalme wa Iyumbwi kwa ajili ya kujumuika kwenye sherehe ya Mtoto wa Mfalme Yolam kutimiza siku Arobaini.


Nyakati za Saa nne siku hiyo Ya Ijumaa ndio Sherehe zilianza. Mtoto wa Mfalme Mchanga alitolewa Inje na kuwekwa sehemu maalum aliyokuwa ameandaliwa kuwekwa, lakini ilikuwa ni mbele ya Wafalme wote wawili, yaani King Yolam na King Joktam pamoja na Wake zao Queen Eda na Queen Velian. Mfalme Yolam alikuwa mwenye Furaha sana wakati wote, hata King Joktan naye Alijiona kawaida sana Ingawa alikuwa hakuwahi kupata Mtoto toka kumuoa mkewe Malkia Velian. Kwa Upande wa Velian Mambo kidogo yalikuwa tofauti sana, Machozi yalianza kumtoka kwasababu aliumia, Alijiona kama Mwanamke ambaye hajakamilika kwasababu hakuwahi kumzalia Mumewe Mtoto. Alikuwa anajitahidi kuyafuta Machozi yake ili asigundulike lakini hakuweza kabisa kuyazuia, kwani kila alipokuwa anawaona Watoto wa Mfalme Yolam ndivyo uvumilivu ulizidi kumshinda.

"Sasa nawaomba watoto wa Mfalme waweze kuja hapa mbele yetu, kisha kila mmoja atainama na kumbusu Mdogo wake kwenye paji la Uso ili kuonesha mapenzi kwa ndugu yao!"

Mtu aliyekuwa ameteuliwa kama Mshereheshaji wa Tukio lile alisema. Haraka sana watoto wengine wa mfalme Yolam kwa Tofauti yao ya Umri wote walisimama na Kusogea mbele huku wamepanga mstari mbele ya Wafalme wawili, King Joktan na Baba Yao King Yolam.

Baada ya kusimama na Kuwasalimia Wafalme, Mprince na Maprincess katika Ufalme wa Iyumbwi walilifanya zoezi lililokuwa lianafuata la Kumchum mdogo wao kwenye paji la Uso.

Yote hayo yakiwa wanafanyika watu wengine walikuwa wakishuudia na kuyafurahia kwani waliyaona ya Pekee, hiyo ni kwasababu hapo hawali tukio kama hilo lilikuwa halijawahi kutokea katika Falme hizo. Mtihani uliendelea kuwa kwa Malkia Velian. Yeye alishindwa kabisa kukaa kwenye kiti alichokuwa amekikalia. Alisimama na kutoka sehemu ile na kwenda pembeni akafika kuchuchumaa na kuendelea kulia. Machozi yalikuwa ni Mengi sana, masikini alishindwa kujizuia kabisa.

"Malkia Umekuwaje?"

Mfanya kazi wake wa kike alifika sehemu hiyo na kumuuliza.

Malkia Velian hakujibu Chochote aliendelea kulia kilio cha kwikwi.

Huku kwenye Sherehe Mfalme Joktan alimnong'oneza Maneno Mfalme Yolam Kisha naye akasimama na Kumfuata Mkewe kule alipokuwa. Cha kwanza kabisa baada ya kufika, alimgusa mkewe kwenye mabega ili ainue uso wake kwani alikuwa ameinamisha chini kichwa. Malkia aliinua kichwa na kumwangalia mumewe. King Joktan hakuishia hivyo tu, alimpa mkono mkewe aushike ili asimame. Kwa taratibu kabisa Malkia aliupoke mkono wa Mfalme na Kusimama. Bado King Joktan hakuishia kumsimamisha Mkewe, Alimkumbatia kisha akasema.

"Usilie Mkewe wangu, chukulia kuwa ni Maisha ya kawaida, ndio maana Mimi nimeridhika, najua miungu ina maana kubwa kutuacha sisi katika Hali hii!"

Mfalme alisema.

Maneno yake yalipenya moja kwa Moja katika Masikio ya Mkewe Malkia Velian kisha yakapita katika ubongo, Ubongo nao ukayaratibu kama kawaida yake, Kisha yakaenda mpaka kwenye moyo, sehemu ya pekee katika mwili wa mwanadamu inayojua kubeba faraja ya mwili, Moyo baada ya kuyapokea ukafarijika sana. Mzunguko huo wa maneno ya Mfalme katika mwili wa Malkia, yalimfanya Malkia Velian kumwangalia mumewe Mfalme Joktan usoni kwa tabasamu la machozi. King Jokta naye hakujali akainua mikono yake na kumfuta machozi mkewe, halafu sasa akampiga bufu la kwenye paji la Uso, busu pekee lenye maana kubwa katika mapenzi. Busu hilo liliongeza faraja ya moyo wa Queen Velian.

"Naomba twenda tukajumuike na Wengine!"

King Joktan alimwambia mkewe, huku akiwa kamshikilia Mkono wake, walisogea mpaka sehemu husika kwenye meza kuu na kukaa tena. Wakati huu Queen Velian alionekana mwenye Tabasamu pana sana, alikuwa akimwangalia mumewe Mumewe naye alimuoneshea Tabasamu, alijikuta anafurahi na kuizoea hali iliyokuwa pale.

Kiujumla Mfalme Joktan alikuwa akimpenda sana Mkewe Malkia Velian, Mfalme Yule ambaye Kiumri alikuwa kaisha fikisha Umri zaidi ya Miaka 45, hakuwa na Wasiwasi kabisa na swala la kupata mtoto yeye aliamini kuwa Kumpata Mtoto ni Mipango ya Miungu ya Ardhi ya kwao. king Joktan alikuwa ni Mfalme ambaye alipendwa sana katika Ufalme wake kuliko kitu chochote, alikuwa ni Mfalme mwenye maamuzi sahihi siku zote na alikuwa na Busara za pekee katika maamuzi. Watu wengi walipenda kumtembelea katika Ufalme wake na Kumpa zawadi nyingi, huku wakimuombea Maisha marefu. Huyu ndiye alikuwa Mfalme wa Nghumbi, Falme Ambayo hapo hawali ilikuwa ni asimu mkubwa wa Falme ya Iyumbwi, kwasababu Falme hizo zote zilitokana na Falme Moja kubwa ya Ng'umbwi.

Sherehe ziliendelea na zilikuwa za aina yake, watu katika Jumba la Mfalme walikuwa na Furaha isiyokuwa na Kifani, hasa Watoto wa Mfalme Yolam, hawa walikuwa na Furaha kupita kiasi siku hiyo.


Sherehe ziliendelea kupamba moto toka saa nne mpaka saa nane wakati ambao ulikuwa ni wakati wa Chakula, kabla ya kutawanyika kwenda kupata Chakula, Mfalme Yolam alisimama ili apate kuzungumza maneno machache na watu waliokuwepo .

"Kwanza kabisa napenda nimshukuru Mgeni wetu, Mfalme wa Iyumbwi, Kaka yangu Mfalme Joktan pamoja na Malkia Velian, pia nimshukuru Mke wangu kipenzi Malkia Eda, kisha niwashukuru wengine wote akiwemo Waziri Mkuu pamoja na Lady Divine Kipenzi Eunike. Jambo ambalo napenda kulizungumza kwenu ni kwamba nimefarijika sana kwa uwepo wenu hapa katika siku hii Maalumu. Lakini pia kitu cha pekee ambacho nilikuwa ninakingoja kwa hamu nahitaji mwanangu huyu mchanga apewe Jina, tangu kuzaliwa kwake hatukuwahi kumpatia Jina. kiujumla nimekosa kabisa Jina la Kumpa. Kwa maana hiyo ningependa mwanangu apewe Jina na Malkia Velian!"

Hayo ndiyo yalikuwa maneno ya Mfalme Yolam baada ya kusimama kuzungumza. Alichokisema kiliwashitua watu wote, lakini walipiga makofi kuunga mkono swala hilo.

Baada ya kusema hivyo Mtoto Mchanga ambaye alikuwa ni Msichana aliletwa tena na kuperekwa meza kuu waliyokuwa wamekaa wafalme wa Falme zote mbili Iyumbwi na Nghumbi, wa kwanza kumpokea alikuwa ni King Joktan wa Nghumbi, alimbeba na kumwangalia Mtoto Yule kisha akasema.

"Ni Mtoto mzuri kweli, Natamani awe Malkia katika Ufalme wa Nghumbi!"

Mfalme Joktani alisema. Maneno yake yalikuwa ya pekee, yalimfanya Malkia Eda pamoja na Mumewe King Yolam kutabasamu. Lakini pale pale walikumbuka maneno ambayo waliambiwa na Lady Divine Eunike kuwa.

"Nimeona maono kupitia ndoto kuwa; Malkia Eda Atazaa Watoto wengi sana, wakike na wa kiume, lakini wa Mwisho atakuwa wa Kike na Ataolewa na Prince katika Falme ya Nghumbi"

Baada ya kuyakumbuka maneno hayo Mfalme Yolam naye alisema.

"Tuiombe miungu ilitimize hilo!"

Hayo ndiyo maneno ya King yolam.

Mtoto aliendelea kusafiri, aliitoka mikono ya King Joktan sasa alikabidhiwa muhusika wa jina Malkia Velian. Malkia Yule alimwangalia sana yule Mtoto, alivutiwa naye, machozi yakamtoka na kudondoka kwenye midomo wa Mtoto Yule, hakuweza kuyafuta machozi Yale, yakaingia mpaka ndani ya kinywa cha Mtoto ikawa kama anayamung'unya kuyameza.

"Sophia!"



Alijikuta analitamka Jina hilo Malkia Velian. Jina hilo lilisikika moja kwa Moja Masikion mwa King Yolam. Pale pale akasimama na Kusema

"Mwanangu ataitwa Jina la Sophia kuanzia Leo. Kwahio ataitwa Princess Sophia"

Baada ya Mfalme kutamka hivyo, kila Mtu alisimama na kupiga makofi kulishangilia Jina Zuri alilopewa mwana wa Mfalme, Princess Sophia.

Baada ya zoezi lile fupi watu walitawanyika na kwenda kupata chakula. Mfalme Yolam na Mfalme Joktan pamoja na wake Zao. Malkia Eda na Malkia Velian walikaa meza Moja ya Chakula katika Nyumba ya kifalme, wakati huo Mtoto mchanga wa Mfalme Princess Sophia, kama alivyopewa Jina na Queen Velian alikuwa amelazwa pembeni karibu na meza ya Chakula huku akiwa aanaangaliwa na Mfanya kazi wa Malkia.

Wakati wanakula Queen Velian alikuwa anamuwaza Mtoto aliyempa Jina, wakati mwingine alikuwa akibaki ameganda tu kwasababu ya kumtafakari Mtoto yule wa Mfalme Yolam.

Mfalme Joktan alimuona mkewe katika hali ile lakini alishindwa kumsemesha kwasababu isingependeza.

"Anaonekana atakuwa Mtoto mzuri mwenye akili nyingi!"

Masikini akiwa katika wimbi la mawazo Malkia Velian alijikuta anaropoka, maneno hayo yalisikika kwa watu wote wanne.

"Queen Velian, kula tafadhali usiwaze hayo tena!"

Queen Eda alimsemesha mwenzake baada ya kuona amezidi kuzubaa.

"Samahani!"

Queen Velian alisema kisha akaendelea kula. Alikuwa anakula ilimradi tu ionekane anakula lakini moyo wake ulikuwa hujafungamana na kula, alikuwa anawaza mbali sana mwanamama yule. Mtoto alimuuma sana, miaka zaidi ya ishirini na mitano(25) tangu kuwa na mumewe Mfalme Joktan hawakuwahi kupata Mtoto.

Chakula kilimshinda Malkia Velian akaomba kunawa. Mfanya kazi ndani ya Ufalme alifika na kumnawisha. Muda huo huo alisimama kutoka kwenye kiti alichokuwa amekalia na kuelekea alipokuwa Mtoto Sophia kalazwa. Wakati huo Mfalme Yolam na Mumewe King Joktan walikuwa watazamaji tu. Malkia yule aliyekuwa na Umri wa miaka isiyopungua Arobaini, alikuwa ni Mpole msitaharabu kuliko kawaida, labda ndio maana hakuwa na Mtoto Mpaka wakati huo. Baada ya kufika alipokuwa Mtoto aliinama na kumbeba Princess Sophia. Alikuwa ni Binti wa Kupendeza kweli kweli ingawa bado alikuwa mchanga, lakini kwa mtazamo tu, alikuwa ni Mtoto mwenye mvuto hasa. Baada ya kubebwa na Malkia Velian mtoto yule alicheka. Fizi zake za meno ndizo zililionesha Tabasamu lake.

"Natamani ukuwe uje uwe Malkia katika Ufalme wa Nghumbi, hakika kizazi chako kitakuwa cha pekee na Chenye akili nyingi. Princess Sophia, Miungu ikulinde na ikupe Umri mrefu!"

Malkia Velian alisema kisha akamrudisha Mtoto Sophia alipokuwa amewekwa.

Baada ya kumaliza alikaa kungoja wengine wamalize kula kwa ajili ya Ratiba Nyingine.

*******

Kwasababu ya kuwa ilikuwa sherehe ya Mwana wa Mfalme katika Falme yao ya Jilani au Ndugu zao wa Iyumbwi Mfalme Joktan alilazimika kulala pale kwa siku moja. Siku iliyofuata asaubuhi nyakati za saa mbili yeye na Msafara wake aliaga na kuondoka katika Ufalme ule kurudi katika Falme yake ya Nghumbi. Ilikuwa ni Mbali kama masaa manne akiwa njiani kwa mwendo wa Taratibu. Jeshi alilokua ameongozana nalo kulinda usalama wake lilikuwa la kutosha na lilikuwa Imara sana. Wakati yuko njiani, umbali mdogo kabisa ukiwa amesalia, kuingia katika Vijiji vya Mwanzo vilivyokuwa vinaiunda Falme yake, mbele yao walimuona Binti Ambaye alioneka kuchoka sana, halafu Binti huyo Alikuwa Mjamzito. Kimtazamo Binti Yule alikuwa anatembea amechoka sana. Mfalme aliusimamisha msafara wake kwanza na kuangali kwa Umakini. Akiwa anaangalia Ghafura Yule Binti alianguka chini kabisa, Hapo hapo Malkia Velian kwa haraka alishuka kwenye Farasi wake na kukimbia kumuwahi msichana yule kwa ajili ya kumpa msaada.

Masikini alimkuta msichana yule amepoteza Fahamu tayari. Malkia aliagiza Kundi la Askari kwa kushirikiana na Wafanya kazi wambebe na kumuweka kwenye Mkokoteni wa Kifalme, Mkokoteni ambao yeye mwenyewe alikuwa amebebewa wakati wa Kwenda Iyumbwi, ila wakati wa Kurudi katika Ardhi yake alikataa kuutumia huo Mkokoteni. Ni Mkokoteni wenye mataiili ambao ufungwa kwenye farasi na kuvutwa, lakini huu wa Kifalme huwa umefunikwa kwa Juu kama nyumba.

Baada ya Zoezi hilo lililowachukua dakika Tano tu Msafara uliendelea. Wakati huu hata Mwendo uliongezeka ili kumuwaisha yule Binti katika Ufalme kwa ajili ya Matibabu.

Nusu saa baadaye waliingia katika Jumba kubwa la Utawala wa Nghumbi. Mapokezi ambayo Mfalme wao alikutana nayo yalikuwa ya aina yake, walimpokea kwa shangwe sana Mfalme Joktan na Malkia wake Velian. Binti waliyemuokota Njiani walimuingiza ndani ya Haraka na Kumuita Dkt kwa ajili ya Kumuhudumia. Dkt aliyekuwa mwanamke alifika Haraka sana kumfanyia matibabu, huyu Hakuwa Lady Divine ingawa hata katika Ufalme wa Nghumbi pia Lady Divine alikuwepo kama kawaida. Daktali yule alimfanyia matibabu kwa haraka yule Binti akaanza kuyafungua macho yake, lakini bado aliendelea kuonekana dhaifu, Daktali aliagiza wamletee uji Binti yule, haraka Uji ulikorogwa na kumperekea yule Binti. Malkia Velian mwenyewe aliingia na kuomba amnyweshe Uji msichana yule, kwakuwa Uji ulikuwa ishapozwa, yule binti alinyweshwa bakuli zima akamaliza. Baada ya zoezi hilo msichana yule aliendelea kulala lakini Malkia Velian hakutoka tena mule ndani ya Chumba, aliendelea kukaa jilani na Kitanda alichokuwa amelazwa Yule Binti. Mpaka hapo moyoni mwa Malkia kulikuwa kushakuwa na Mapenzi ya kweli kwa Binti Yule, kwakweli alijikuta anampenda sana Binti yule, halafu sasa alimuhurumia sana Binti yule, majeraha aliyokuwa nayo ndiyo yalimuumiza Malkia Velian.

Siku hiyo Yule Msichana hakupata nguvu kabisa za kumuwezesha kuamka kitandani.

Siku tatu tangu afikishwe pale katika Ufalme ndio alipata kuyafumbua macho yake vizuri na Kukaa kitandani, wakati anaamka Malkia Velian alikuwa akimkanda kanda usoni. Kwanza alishangaa sana kumuona Binti yule anaamka, alikuwa ni Binti Mzuuri sana.

"Unajisikiaje?"

Malkia Velian ndiye alikuwa wa kwanza kumuuliza Binti Yule swali. Swali la Malkia hakulijibu kwani yeye alikuwa anamshangaa Malkia Velian na Maeneo ambayo alikuwepo kwa wakati huo.

"Hapa ni wapi?"

Akiwa anaangalia angalia Binti yule alimuuliza Malkia Velian.

"Hapa upo katika Ufalme wa Nghumbi!"

Baada ya kuambiwa hivyo Yule Binti alishituka sana.

"Mbona umeshituka...hii ni sehemu salama hata usiwaze, lakini ujanambia unajisikiaje?"

"Najisikia vizuri tu, lakini naomba kujua nimefikaje hapa?"

Binti Yule aliuliza tena.

Malkia Velian hakusita kumsimulia Binti Yule Jinsi alivyo fika katika Ufalme wa Nghumbi.

Baada ya kusimuliwa Binti Yule alianza kulia.

"Usilie, hapa upo sehemu salama!"

Malkia Velian alisema huku akimkumbatia Yule Binti, alitumia dakika kama Kumi hivi kumbimbeleza Binti yule na kumtuliza kabisa kabisa.

"Kwani ulikutwa na nini mpaka kufika sehemu tuliokukuta?"

Malkia Velian alimuuliza Binti Yule.

Binti Yule Masikini aliinamisha uso wake, akaliangalia Tumbo lake ambalo lilikuwa na Mtoto ndani yake, kisha akaususha mkono wake wa kulia na kulishika tumbo lake, Mara akaanza kukumbuka alikotoka na kuanza kumsimulia Malkia Velian.

"Jina langu ni Tamali, nimezaliwa na kukulia katika Falme ya Iyumbwi. Mpaka kufika hapa nilikuwa naishi na Baba ambaye aliniokota na kunilea Mimi kama mwanaye, lakini baada ya kufikisha umri wa Miaka kumi na Tano alianza kunilazimisha ili niwe mkewe, nilijitahidi kumkatalia sana, kwasababu nilimuona kama Baba yangu. Swala hilo yeye hakulielewa kabisa ila alitaka nifanye naye mapenzi. Siku moja usiku alinifuata chumbani kwangu, akiwa na kisu huku akidai kuwa nisipokubali kufanya naye mapenzi ataniua halafu kisha naye atajiua. Baada ya kunambia hivyo niliogopa, ilibidi nikubali kufanya naye mapenzi, hiyo ndio ilikuwa Mara yangu ya kwanza kujihusisha na jambo hilo. Baada ya wiki kupita tangu kufanya hivyo, alianza kunifanya kama mke wake, ikawa mazoea mwisho ndivyo kama hivi akanipa mjamzito. Mwanzo nilikaa naye kwa Amani sana huku akidai kuwa atanilea kama mkewe. Miezi sita baadaye alianza kubadilika, akawa anakuja nyumbani masaa yashaenda huku kalewa kabisa. Nilipokuwa namwambia kuhusu swala hilo alinipiga vibao halafu akidai kuwa sitakiwi kuonekana katika Ardhi ya Iyumbwi la sivyo nitauawa. Mara nyingi alikuwa akija ananipiga halafu ananiambia hivyo. Hatimaye nilishindwa ikanibidi nimuulize kwanini alikuwa ananiambia kuwa nitauawa. Baada ya kumuuliza hivyo alinambia kuwa.

"Wewe uliletwa kwangu ukiwa mdogo kabisa, yaani hata ukiwa ujitambui kabisa. Hapa kwangu uliletwa na Askari wa Falme ya Iyumbwi akanambia kuwa nikulee, wakati huo nilikuwa na mke wangu nazani unamjua amekufa wewe ukiwa na umri wa miaka sita. Nilipomuuliza kuwa amekutoa wapi alinambia kuwa ataniambia ila wakati ulikuwa hujafika. Kwakuwa ulikuwa bado mchanga, Tulipata Shida sana kukuelea, kwani Chakula chako wakati huo mara nyingi kilikuwa Maziwa ya wanyama na uji kwa uchache sana. Pindi ukiwa na umri wa miaka miwili Yule Kaka yangu alikuja akanambia siri ya Maisha yako kuwa wewe ni Mtoto wa Lady Divine aliyeitwa Amana na kaisha fariki, Baba yako ni marehemu pia ila alikuwa ni Mfalme katika Falme hiyo ya Iyumbwi, huyo Mfalme ndiye Baba yake na Mfalme Yolam wa Leo, Baba yako huyo alikuwa anaitwa Zayoni. Wewe inasadikika kuwa ni Laana. Kwasababu hiyo Malkia katika Falme ya Iyumbwi aliagiza ukatupwe shimoni, lakini Kaka yangu aliona uchungu kumtupa mtoto mchanga ambaye hukuwa na kosa lolote, ndipo alipokuficha na kukuleta kwangu. Hivyo ndivyo historia yako ilivyo.

kwahio unasitahili kufa. Labda cha kukusaidia nitakupiga nikuchoshe halafu nikubebe kwenye farasi kisha nikakutupe mbali utajua utakapo kwenda, kama si hivyo hapa hutoweza kuishi na ukigoma nakupereka kwa Mfalme Yolam akakuuwe kwa mikono yake mwenyewe!"

Hivyo ndivyo ilivyokuwa Mama! Baada ya kunambia kuwa atanipereka kwa Mfalme Yolam, nilimuomba afanye chochote lakini asiniue halafu mwisho aniachie niende popote. Nilipomwambia hivyo alianza kunishushia kipigo, kisha akanifunga nguo vizuri ili watu wakiona wasigundue kuwa kanipiga, kisha akanibeba kwenye farasi na kunipereka porini mbali kabisa, na ni huko mliko nikuta""

Binti yule aliyejitambulisha kwa Jina la Tamali aliusema ukweli kuhusu maisha yake na hiyo ndiyo ilikuwa historian fupi ya Maisha yake.

Nazani ushajua ni nani?



Kabla hujaendelea, Tafadhali naomba kushare ndugu zangu wasomaji. Unajua inatia uchovu sana kama nikuomba Kushare halafu Amsambazi.

Haya endelea.


Wakati anasimulia kisa cha Maisha yake, machozi yalikuwa yanamtoka kwa wingi, kisa chake kilimuumiza sana, kwani Mtu ambaye awali alimueshimu kama Baba yake ndiye alimlazimisha kufanya naye mapenzi na kuperekea mjamzito, wakati huo huo yakaanza manyanyaso huku akumtishia kumuua.

Kwakweli inaumiza sana. Malikia Velian naye hakuachwa hivi hivi, naye pia machozi yalimdondoka.

"Hhhhaaaahh! Pole sana Tamali, ndivyo Maisha yalivyo. Kawaida maisha huwa yanamisukosuko ya kila aina. Ingawa si kwa Watu wote ambao hukutana na misukosuko mibaya ya kuumiza lakini pia kila mwanadamu huwa na Changamoto zake za Maisha. Kikubwa ni uzima tu!"

Malkia Velian alisema. Wakati huo huo alianza kumfuta Tamali Machozi yaliyokuwa yanamtoka.

Maneno yake yalimuingia sana Tamali.

"Asante kwa moyo wako ulionioneshea. Najisikia faraja sana sasa. Nahisi kama vile niko sehemu salama!"

Tamali alisema.

"Usijali na wala usiwe na wasiwasi kabisa Tamali. Wewe sasa utaishi hapa, na Kuanzia sasa utaishi kama Mwanangu, na utakuwa Princess ndani ya Ufalme huu. Nitakulinda kwa kila hali, na Mtoto wako atakuwa Prince katika Ufalme huu, na kisha atamuoa mwanamke mzuuri kutoka katika Falme ya Iyumbwi. Atamuoa Malkia Sofia. Mapenzi yao yatakuwa ya aina yake. Kwa mtazamo wangu Naona kama vile mapenzi yao yameandikwa katika kitabu ila kitabu hicho kizuri kimo ndani ya moyo wangu pekee!"

Malkia Velian alisema. Alizungumza maneno mageni kabisa, maneno ambayo Tamali hakuwa na taarifa nayo kabisa. Ingawa alikuwa katika hali ya udhuni alijikuta anatamani kujua Malkia Velian alikuwa anamaanisha nini.

"Unamaanisha nini kusema hivyo"

Tamali aliuliza.

"Najua kuwa unatamani kujua kile ambacho nimekisema!"

Malkia Velian alisema huku akimwangalia Tamali usoni. Tamali naye alibaki akimwangali tu.

"Usijali, nitakwambia kwanini Nimesema hivyo....... Siku ya kwanza kukuona wewe, kichwani wazo liliniajia kuwa wewe ni mtu wa pekee sana. Lakini cha kushangaza zaidi usiku wa siku hiyo nikiwa nimelala kitandani kwangu, Ndoto ilinijia usingizini. Ndoto hiyo ilikuwa hivi; siku moja nilikua niko katika mapango ya kuabudia miungu ya Ardhi yetu. Ghafura nilitokewa na Mfalme wa Kwanza wa Falme hii. KING CLEOPA. Mfalme huyo alinambia maneno machache tu kuwa.

"Ndani ya Nyumba yako kaingia Mfalme, kwahio toka Leo usilie hiyo ndiyo itakuwa faraja yako!"

Baada ya ndoto hiyo sikuendelea kulala, nilikaa nikitafakari sana, lakini ni nani huyo Mfalme? Nilijiuliza swali hilo haraka sana nikagundua kuwa ndani ya Tumbo lako ndimo yumo huyo Mfalme!"

Malkia Velian alisema. Maneno yake yalifanya Tamali kutabasamu na kukosa la kuzungumza.

"Nambie unajisikiaje Mwanangu Tamali?"

Baada ya kumsemesha kwa maneno mazuri Malkia Velian alimuuliza Tamali. Tabasamu lilikuwa limemjaa mwanamke yule kweli kweli.

"Najisikia vizuri tu!"

"Kwahio sasa unajiona mwenye furaha?"

"Ndiyo!"

"Usiudhunike tena tangu sasa, na utaishi kwa furaha kama nilivyokuahidi!"

"Asante!"

"Unaweza kuniita Mama au Dada ukipenda!"

Malkia Velian alisema. Maneno yake yalimshitua kidogo Tamali. Kisha akasema.

"Hapana wewe ni Mama yangu, wewe ni Mama ambaye miungu imenileta kwako. Hata mimi pia nitakuheshimu na nitakuwa mnyenyekevu kwako!"

Tamali alisema wakati huo huo machozi yalianza kumdondoka.

"Usijali Tamali, ni kweli Mimi nitakuwa Mama yako!"

Malkia Velian alisema.

SOMA HAPA VITABU VYA MAFANIKIO

ITAENDELEA

Post a Comment

0 Comments