Lengo kuu la Amina kufunga safari yake kutoka Mombasa Mpaka Dar ni kwenda kumtafuta Ansbert ambaye amepotea kwa kipindi kirefu tofauti na makubaliano yao.
Gari hii ya TAHMEED ilikuwa inayakata mapori vilivyo hadi wakaingia kwenye mji unaitwa LUNGALUNGA ikiwa ni tayari saa tatu Asubuhi, ndani ya dakika za kuhesabu tayari walikuwa kwenye mji mdogo unaitwa JUAKALI hapo ilimaanisha kuwa wanakaribia kuingia HOROHORO ambapo ndio iliko Boarder Post.
Gmina alishuka mpaka wa Horohoro kwa upande wa Kenya akalipa shilingi 285 za kenya ambazo ni sawa na takribani shilingi elfu sita za Tanzania kisha akagongewa kibali chake mhuri na hatimaye wakavuka kuingia upande wa Tanzania ambapo walionyesha vibali vyao na safari ikaendelea.
Safari iliendelea hadi wakafika sehemu inaitwa Amboni ambayo ni karibia sana na Kuingia Tanga Jiji.
Gari yao ilipigwa mkono na kusimama pembeni kushoto huku askari wa kikosi cha usalama barabarani wakiifwata.
Mabishano yalionekana dhahiri kati ya wale askari na wafanyakazi wa hili gari ambapo hatimaye abiria walikuwa wakiwatazama jinsi walivyokuwa wanaingia kwenye gari.
"Abiria wote poleni na safari na habari zenu"
"Nzuri" (Abiria hawa waliitikia salamu hii ambayo ilitolewa na maaskari)
"Tunaomba samahani kwa usumbufu lakini tunamtaka kila abiria ashuke chini na achukue mizigo yake asimame nayo"
Huku wakinung'unika walishuka chini na kila mmoja akachukua mizigo yake na kusimama nayo.
Askari wale walianza kusachi kila mzigo hadi wakamaliza, walipomaliza waliingia ndani ya gari na kutafuta kona zote kama vile kuna kitu waliambiwa kimo.
Walipomaliza waliingia kwenye buti kisha wakatoka na kiroba kilichoonekana kujazwa kitu kama mahindi hivi.
Kiliposhushwa chini walianza kuuliza mzigo ni wa nani lakini hakuna aliyeonekana kuukubali.
Walipoona watu wote wako kimya waliufungua ule mfuko ambao ulikuwa na karafuu, waliupekua vyema na hatimaye wakakuta mfuko mweusi wa Rambo ndani ya zile karafuu ambapo walipoufungua walikutana na miraa ( Mirungi) iliyopangwa vizuri kwenye vifungu.
Hapa kila mmoja alishtuka na hata wale wafanyakazi wa lile gari pia....
"Kondakta wa hili gari aje hapa twende ofisini mpaka akaeleze huu mzigo ni wa nani na anaupeleka wapi"
"Afande mimi sitaki kwenda mbali, HUU mzigo ni wa huyu kaka, alinidanganya kuwa ni karafuu tu zilizopo huko ndani ndio maana nikaupakia"
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Amina alishtuka kwani kaka aliyeonyeshwa ni yule aliyekaa nae siti moja.
Askari walichukua Pingu yule kijana akavishwa mikononi kisha akaingizwa kwenye gari ndogo ya Polisi pamoja na mizgo yake kisha safari ikaendelea ambapo Lile basi nalo likaondoka pale.
Ndani ya Basi Amina alitamani ashuke ili akamtetee Yule kaka mpaka mwisho lakini aliyapuuza mawazo yake na kuendelea na safari.
............................................
Rozina kwa kiwewe alichokuwa nacho alijikuta akilia kwa sauti kubwa huku akijipigiza hapo chini, Oscar aliamua kuchukua maamuzi ya kumuondoa Rozina pale kuhofia sauti zake kusikika kwa watu.
alimbeba juujuu mpaka kwenye gari kisha akaliwasha kwa kasi na kumrudisha Rozina nyumbani na kumfungia ndani.
Alipomaliza alichukua gari kwa haraka na kuligeuza kurudi kule shambani, lengo lake kuu ilikuwa ni kwenda kufuta ushahidi.
alilikimbiza gari kama vile ameliiba, Ndani ya dakika 45 tayari alikuwa ameshafika ambapo alianza kusafisha lile eneo kwa kudeki ili kuondoa damu.
Alichukua michanga na kufukia damu zilizokuwa zimetapakaa nje, alipohakikisha kuwa kumekuwa safi aliuchukua mwili wa Ansbert kwa ajili ya kuupeleka kichakani achimbe shimo auzike.
Aliubeba kwa tahadhari kubwa kisha akaupeleka kwenye kichaka kilichopo mpakani na shamba kisha akauweka hapo.
Alirudi pale kibandani kwa ajili ya kuchukua Majembe na chepe lakini akasikia simu yake ikiita akaitoa mfukoni na kuona jina la mkewe Michelle.
Aliikata simu kisha akaizima na kuitumbukiza mfukoni, kicwhwani kwake akili ilikuwa imevurukika kabisa na mambo yalikuwa yakipita kwa kupandiana.
Alipoinua macho yake kutazama mbele ili apige hatua alikutana na Mdomo wa SMG ukiwa umemuelekea huku nyuma yake kukiwa na askari wawili waliovalia kiraia.
Oscar alipagawa vilivyo lakini akajiapiza ndani ya Moyo wake kuwa hakubali kwenda jela.
Alinyoosha mikono yake juu ishara ya kusarenda kisha wale askari wakaanza kumfwaata kwa lengo la kumkamata huku wakiwa na pingu mkononi.
Kama mshale Oscar alitia mkono wake mfukoni na kutoa Bastola yake lakini kabla ya kuifyatua alishtukia Risasi mbili zikiusambaratisha mkono wake ulioshika Bastola kitu kilichompelekea kudondoka chini lakini hata hibvyo alishafyatua Risasi ambayo alicharaza sikio la Yule Askari.
Kwa kasi ya umeme wale maaskari walimfwata Oscar ili wamchukue wampeleke Hospitali lakini waligundua kuwa kwa bahati mbaya Risasi moja ililenga upande wa Moyo wa Oscar na tayari alikuwa ameshafariki Dunia.
....................................
Ukweli ni kuwa Oscar alikuwa amefariki dunia kwa kushambuliwa na polisi ambaye alikuwa anajihami na hakuna kingine kilichoendelea zaidi ya askari wale kuchukua hatua zote za kukamilisha taratibu za kuripoti tukio.
Walipiga picha na kuchukua mwili wa Ansbert pamoja na ule wa Oscar.
.......................
Wakati Oscar na Ansbert wakiwa wanazozana ndani ya kile kibanda pale shambani alikuja Ally, Huyu ally alikuwa ni kijana ambaye alishawahi kufanya kazi kwenye hili shamba kwa kuajiriwa na Ansbert japo baadae walishindwana kwa kuwa Ally alikuwa sio mwaminifu hivyo akafukuzwa.
Aliamua kurudi kwao Rufiji lakini kule maisha yakkkampiga sana akaamua kurudi kwa bosi wake angalau aombe msamaha na kurejea kazini.
aliamua kwanza apite shambani ili akifika pale atazame kama kuna mfanyakazi mwingine ama lah!
Wakati akielekea huko bahati ilikuwa yake kwani aliona gari la bosi wake likielekea maeneo hayo na kuamua kulifwata, kilichomshangaza baada ya kufika pale nje ya kibanda alisikia mzozo na hatimaye milio ya risasi kitu kilichomfanya aogope sana na kuamua kwenda kutoa taarifa Polisi.
.......................
Gari Mbili aina ya Difender zilikuwa nje ya Nyumba ya Ansbert huku askari wenye vyeo wapatao sita wakishuka na kuingia ndani. Walipofika walikutana na Sura ya Rozina aliyekuwa amechoka kwa mawazo huku wasiwasi ukiwa umemjaa.
"Habari yake Mama"
"nzuri tu, Karibuni na niwasaidie nini"
Laiti kama askari hawa wangejua wangemhusisha sana Rozina na lile tukio kwani alikuwa akitetemeka sana ila wao walidhani labda anatetemeka kwa kuwa huenda hajazoea kuona Polisi lakini ukwe ni kwamba Rozina alikuwa anahofia Jela.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Samahani sana Hivi mumeo yuko wapi?"
"Aliniaga kuwa anasafiri kikazi na atakaa siku nne au wiki"
(Rozina aliamua kudanganya)
"Ok samahani tuna taarifa mbaya kidogo, Mumeo ameuawa na Majambazi huko Kwenye shamba lenu lililoko Mkuranga"
"Mnasemaje? uuuuuuuuuuuuuuuuuuuwiiiiiiiiiiiiiii, jamani Mume wangu!"
kilichofwatia hapo ni Kishindo kikuu cha Rozina kudondoka chini na Kuzimia.
Ukweli ni kwamba Rozina alikuwa kwenye maigizo kwani hili tukio alilijua vizuri na alishiriki kinagaubaga katika kile kilichomtokea Mme wake.
Kujiangusha chini ilikuwa ni mBinu ya kumfanya asishtukiwe, japo maumivu aliyokuwa nayo ndani ya Moyo yalikuwa ni makubwa na yalikuwa maumivu ya Hatia, Naam ... hatia ya kumuua mme wake.
Kazi ilikuwa kwa wale askari wa Kike ambao ilibidi waanze kumfunikwa Rozina vizuri kwani KANGA aliyoivaa ilikuwa imefunuka juu kabisa na kuacha nguo ya ndani ionekane.
Hakuna kitu kilichoowatoa udenda wale maaskari wa Kiume kama kuona mapaja ya Rozina, walibaki wakikodoa macho huku denda ziikiwatoka, hakuna hata mwanamme mmoja aliyekamilika ambaye angeweza kujinasua kwenye maumbile ya Rozina kwa urembo aliokuwa nao.
kila mmoja kwa wakati wake alijiapiza kuwa baada ya kila kitu lazima wamchukue Rozina awe mke wao bila kujua kuwa wanaaenda kuanzisha vita nyingine.
.......................
Hakuna mtu aliyelia kwenye siku hii ya kuwaaga vigogo hawa wa serikali (Oscar na Ansbert) kama Amina, Maro na Michelle.
Michelle alilia mpaka sauti ikamkauka, Maro alikuwa amekuwa kama kichaa na marakwa mara alikuwa akilala juu ya Jeneza la baba yake.
Amina japo aliishi kwa Muda mfupi lakini alikuwa amempenda Ansbert kiasi ambacho alitamamani afe azikwe nae siku ile.
Alijiuliza Mtoto aliye nae Tumboni atamlea vipi wakati Baba yake hayupo.
Walikatishwa na sauti ya Ving'ora vilivyokuwa vinaimgia pale kushirira kuwa Rais wa Nchi alikuwa amewadia.
Wstu wote walisimama na baada ya taratibu zote Rais aliagaa miili ile na kuanza kuhutubia, moja ya senetensi za kwenye hotuba ni kuwa atahakikisha watoto na wake za marehemu wote wanapata stahiki zao kamili huku akiahidi kuwasomesha wale watoto mpaka level yao ya mwisho hata nje ya nchi.
Alilitaka Jeshi la polisi na Vyombo vya Usalama kuhakikisha kuwa wahusika waa tukio hilo wanakamatwa haraka sana na hatimaye kuchukuliwa hatua stahiki.
...........................
"Naongea na Rozina"
"Ndio mimi, samahani wewe nani maana hii namba ngeni"
"Najua, Mimi ni Afisa Upelelezi wa Jeshi la Polisi na ninahitaji kufanya mahijiano na wewe"
"Mahojiano kuhusu nini? kwani uko wapi"(Rozina alianza kuogopa mno kwani alijua labda ameshtukiwa)
"Njoo hapa ofisini kituo cha kati"
"Jamani mbona mimi sipajui"
"Wewe uko wapi kwani"
"Niko nyumbani"
"Kama nikiwatuma vijana kuja kukuchukua utalipia gharama za usafiri"
"Nitalipa Afande"
Ndani ya dakika tano gari ilikuwa inapiga honi nje ya geti la nyumba ya Marehemu Ansbert, geti lilifunguliwa na hatimaye mzee mmoja wa umri wa miaka hamsini aliingia na kuelekea sebuleni kwa Rozina.
walisalimiana na hatimaye wakaanza mahojianao
"Rozina taarifa tulizo nazo zinaonyesha kuwa kabla mme wako hajauawa wewe ulionekana na Muuaji mkienda eneo lile zaidi ya mara tatu tena usiku wa manane,, unaweza kunieleza kwanini ulienda kule na mlikuwa mmebeba nini?"
Rozina alishindwa kujibu swali na kujikuta akitetemeka na kujiuma uma tu, kila kitu kilirekodiwa na hatimaye Rozina akaulizwa swali lingine.
"Taarifa tulizo nazo ni kwamba wewe ulikuwa unaonana na Muuaji hoteliini mara kwa mara na inasemekana pia kuwa alikuwa ni mpenzi wako wa nje na hii ndio ikawa sababu ya Kisasi, unalizungumziaje hili?"
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Kwa maswali Rozina aliyoulizwa alijikuta akikosa majibu na kuanza kulia kwa kwikwi.
Afande Rocky alichokifanya baada ya mtego wake kuonekana kunasa aliamka kwenye kiti chake na kumfwata Rozina kisha akampigapiga begani huku akimwambia...
"Ukiwa mjanja nitakusaidia, ukiwa mbishi utaozea jela"
Rozina alishtushwa na kauli ile kisha akanyamaza kulia na kumtazama yule askari kwa jicho la Mshangao.
"Unamaanisha nini Afande?"
Afande Rocky hakujibu kwa maneno ila alijibu kwa kumshika Rozina ziwa llake la kulia.
mpaka hapo Rozina alishaelewa ni nini kinahitajika ili awe huru aepuke jela.
Rozina kwa woga wa Jela alianza manjonjo yake huku akianza kufunua Kanga na kuacha mapaja wazi, kkwa uchu aliokuwa nao Afande huyu hakulaza damu, alimpeleka Rozina chumbani wakavuana nguo kisha wakafanya Ngono.
Afande Roccky alinogewa na Penzi la Mrembo Rozina ambapo waliahidiana kuwa wapenzi huku Afande akimuahidi kumsaidia kwenye kesi yake endapo atakuwa wake peke yake.
Mchezo wa Rozina ukawa ni Ngono kila wakati na Afande Rocky, kilichotokea ni kwamba kila askari aliyelijua swala la Rozina alitumia mda wake wa pekee kumrubuni Rozina na kisha kupata penzi lake.
Ndani ya MWEZI Mmoja Rozina alikuwa ametembea na Askari kumi na mbaya zaidi walishaanza kujuana.
..........................
Amina alijua kuwa hajulikani kwenye ukoo wa akina Ansbert hivyo kwenye Mirathi hatahusika na wala mwanae hatatambulika mbele ya Rozina, alichoamua ni kurudi Mombasa, alimshukuru Mungu kwani Miradi aliyoachiwa endapo ataisimamia vizuri atakuwa Tajiri maisha yake yote.
Aipanda kwenye basi kwa ajili ya kurejea Mombasa, wakati akiwa njiani alimkumbuka kaka aliyeketi nae kwenye gari hatimaye akakamatwa na Polisi kwa kusafirisha Mirungi.
Moyo wake ulilipuka na kujikuta akiamua Kushuka Tanga na kumtafuta yule kaka kwenye vituo vya Polisi. Bahati ilikuwa yake kwani aliweza kumpata na hatimaye akafanikiwa kuhonga shilingi laki sita zilizomuacha yule kaka awe Nje.
Yule kaka hakuamini kwani ilikuwa imebaki masaa tayari Kesi yake iende mahakamani, alimshukuru sana yule dada ambaye hata hivyo alishamsahau lakini baadae kumbukumbu zake zilirudi na kugundua kuwa walionana kwenye gari.
"Samahani dada, hivi unanifahamu zaidi ya tulivyoonana kwenye gari?"
"Hapana kwakweli"
"Sasa imekuwaje mpaka ukaamua kunisaidia"
"Yani sijui ila nimejikuta tu nikikupenda alafu unafanana sana na Mwanaume wangu aliyenipa ujauzito huu japo amefariki"
Amina alianza kumwaga machozi kitendo kilichomfanya yule kaka amchukue kisha wakaenda kwenye mgahawa wakaketi na kuanza kutambulishana vizuri.
Wakati wanatambulishana yule kaka ambaye alisema anaitwa Godlove alianza kulia kwa kwikwi kitendo kilichomshtua sana Amina.
Ukweli ulikuwa umejulikana kuwa Godlove ni mdogo wa mwisho wa Ansbert Maro ambaye alizamia nchini Afrika Kusini na kulowea kwenye uuzaji wa madawa ya kulevya hadi pale alipoingia tenna kenya na kuuza Mirungi.
wakati wote huo ndugu zake walishatafuta na kukata tamaa wakidhani amekufa kumbe alikuwa hai. Haya yalikuwa maajabu lakini kweli.
Amina alikuwa na raha sana kwani aliamini kuwa Mungu kamkutanisha na mtu sahihi sana, mapenzi yalichipuka na hatimaye Godlove alimrithi Amina na kuendesha bishara alizoacha kaka yake kwa mafanikio makubwa sana.
Utajiri wao ulikua mara dufu hadi kufikia hatua ya kumiliki mmagari, mahoteli na majumba mengi Mombasa Tanga, Dar es salaam Na Moshi.
Wazazi wa Ansbert waliumizwa sana na kifo cha Ansbert lakini walijikuta wana furaha Mpya kumpata Godlove.
........................
Zogo lilikuwa kubwa sana ndani ya baa ya Mrombo iliyoko Sinza Afrikasana ambapo askari wa kituo cha kati walikuwa wanagombea mwanamke.
kilichosikika baada ya hapo ni milio ya Risasi ambapo askari hawa wawili waliuana huku bbaadhi ya Risasi zikimpata Rozina na kufa pamoja na Askari hao.
....................................................CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Michelle hakurudi Ghana, aliamua kubakia Tanzania ili aendeleze Mali za Oscar akishirikiana na familia ya Oscar, Tayari alikuwa na watoto mapacha mmoja wakike na mmoja wa kiume.
Alijitahidi kwa Nguvu zote kuendesha miradi ambayo ilimfanya awe tajiri Mkubwa mno na kushikilia nafasi ya kwanza kwa wanawake matajiri Tanzania.
Mali zote aliziandika majina ya watoto wake ambao walikuwa wanasoma nchini Marekani.
MWISHO
0 Comments