“Hivi baba Careen,
unajua mimi sikuelewi kabisa siku hizi?”.
“Kwa nini
hunielewi?”. Nilimjibu mama Careen.
“Eti eeeeh!
Unajifanya huelewi”. Mama Careen aliongea huku sasa akiwa amekishika kiuno
chake kwa mikono yote na kunitolea macho pima.
“Hapana naelewa”.
Nilijibu kwa kifupi.
“Unaelewa nini?”.
Mama Careen alibandika swali jingine.
“Ninaelewa kwamba
hunielewi siku hizi?”. Nilimjibu kwa nyodo.
CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Haya bwana, wewe
jifanye una misemo kama waswahili wa pwani”. Mama Careen alinichambua.
“We mwanamke hebu
acha kuniharibia siku. Yaani ndiyo kwanza kunakucha lakini ushaanza kuupepeta
mdomo pe pe pe peeee! Mithili ya chiriku”. Nami nilimzodoa mama Careen kwa
maneno ya dharau na kashifa.
“Sawa bwana
mshindi wewe. Lakini mi nakwambia mbio za sakafuni huishia ukingoni”. Mama
Careen aliniasa.
“Acha maneno yako
bwana. Hayo ni maneno ya kuku tu wala hayamtishi mwewe”. Nilimjibu mke wangu
kwa dharau huku sasa mikono nikiwa nimeiweka mfukoni na mguu mmoja nikiusugua
chini.
Mama Careen
hakujibu kitu bali alimnyanyua Careen ambaye alikuwa hajui ambacho kinaendelea
kutokana na umri wake na kuelekea ndani chumbani.
Mimi nikampuuza
mwanamke huyu ambaye niko naye katika ndoa mwaka wa kumi sasa. Nilimwona ni
mwanamke wa kawaida ambaye hakuwa na jipya zaidi ya maneno mengi kila uchao.
Nilitoka nje ya
sebule na kuanza kufanya utaratibu wa kuelekea kazini. Mwanamke huyu kwa kweli
alikuwa amenichafua kabisa asubuhi hii ya leo. Roho yangu ilikuwa nyeusi na
sikuelewa nitaimalizaje siku.
Nilitamani
nighairishe kuelekea kazini lakini nikaona huo utakuwa si uamuzi wa busara hata
kidogo. Haikutakiwa mafarakano ya nyumbani yaharibu utaratibu mzima wa kazi.
Nilijua namna nzuri ya kumdhibiti mwanamke huyu.
****************
Ilikuwa ni majira
ya jioni wakati mimi nikitoka kazini kuelekea nyumbani kwangu. Nilikuwa sipendi
kabisa kurejea nyumbani kutokana na maneno ya kero ya mke wangu. Ndiyo kwangu
mimi yalikuwa ni maneno ya kero ingawa ilikuwa ni haki yake kuongea kutokana na
kusikia tetesi za kwamba nilikuwa nikitoka nje ya ndoa.
CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Unajua Juma mimi
nina tatizo moja kubwa sana ambalo linanikera sana”. Nilimwambia Juma rafiki
yangu ambaye tulikuwa tukifanya kazi katika ofisi moja.
“Tatizo gani bwana
Mayanja?”. Juma aliniuliza huku akinitazama usoni na wakati huohuo tukitembea
kuelekea majumbani kwetu.
“Unajua huyu
shemeji yako amekuwa kero sana siku hizi”. Nilimweleza bwana Juma.
“Ki vipi bwana
Mayanja?”. Aliniuliza bwana Juma.
“Yaani siku hizi
amekuwa akiupepeta mdomo kama wale wanawake wa uswahilini. Yaani yeye muda wote
ni manenomaneno tu”. Nilimwambia Juma huku uso wangu nikiwa nimeukunja.
“Ha ha ha ha ha
haaaaaaaa!”. Juma aliangua kicheko kikubwa sana kitendo ambacho kilinishangaza
sana.
“Yaani Juma mimi
nina matatizo makubwa nyumbani halafu wewe unanicheka. Ina maana unanidharau?”.
Nilimwuliza Juma kwa ghadhabu sana.
“Siyo kwamba
nakudharau rafiki yangu ila unanifurahisha sana Mayanja”. Juma aliongea.
“Sasa ni nini
ambacho kinakufurahisha hapa?”. Nilimwuliza Juma huku nikiwa dhahiri
nimestaajabu.
“Mwanamke hawezi
kukusumbua hata kidogo. Mwanamke hatakiwi kukuendesha hata siku moja bwana
Mayanja”. Juma aliongea.
“Lakini yule ni
mke wangu Juma”. Niliongea.
“Hata kama!
Unatakiwa utende kiume!”. Juma aliongea huku akinipigapiga mgongoni.
“Sasa nifanyaje
Juma?”. Nilimwuliza Juma.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Sasa hilo ndilo
swali bwana Mayanja”. Juma aliongea huku akiniangalia usoni.
“Ndiyo unijibu
haraka sasa, maana mimi nimechoka kabisa”. Nilimwambia bwana Juma nikiwa nina
munkari wa kutaka kujua suluhu ya tatizo hili ambalo lilikuwa likinikabili.
“Tulia bwana
Mayanja, mambo yako yatakuwa safi kabisa”. Juma aliendelea kunipooza moyo wangu
ambao kwa sasa ulikuwa ukichemka sana.
“Kwa hiyo
tunafanyaje sasa rafiki yangu?”. Nilimwuliza bwana Juma.
“Mwanamke hatakiwi
kukuendesha hata kidogo. Jambo la kufanya ni wewe kwenda kuondoa stress”. Juma
aliongea.
“Sasa hizo stress
nitaziondoa wapi na nitaziondoa vipi”. Nilimwuliza bwana Juma kwani maelezo
yake sikuyaelewa hata kidogo na yalizidi kunichanganya.
“Wewe subiri wala
usiwe na mchecheto. Mimi ndiye kamanda wako katika hili na nitakuelekeza kila
kitu na mambo yako yatakuwa fresh kabisa.
Maongezi yetu
yalitupeleka mpaka kituo cha daladala. Tulipanda ndani ya daladala ambayo
ilitupeleka mpaka katika mtaa wa Mbazi ambako ndiko yalikuwa makazi ya bwana
Juma.
Juma
alinikaribisha katika nyumba anayoishi kisha yeye akaingia chumbani. Sikufahamu
alienda kufanya nini kule chumbani lakini baada ya muda wa kama sekunde
thelathini alirejea pale sebuleni. Alinikuta nikiwa nimejipumzisha katika sofa
mojawapo pale sebuleni. Naye akaketi katika sofa mkabala na mimi.
“Bwana Mayanja,
kama nilivyokueleza hapo awali, ni kwamba tatizo lako leo litakwisha kabisa na
utairejelea furaha yako kama hapo zamani”. Juma aliongea huku akichukua rimoti
na kuwasha Tv iliyokuwa pale sebuleni.
“Lakini bwana Juma
wewe unaonekana una maneno mengi kama chiriku”. Nilimwambia Juma.
CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Kwa nini wasema
hivyo Mayanja?”. Juma aliniuliza huku akinitazama usoni.
“Una maneno mengi
lakini vitendo hakuna. Sasa toka umeanza kuniambia kwamba tatizo langu leo
litafika suluhu ni muda mrefu sasa lakini sioni vitendo”. Nilimwambia Juma.
“Tulia bwana
Mayanja kwani mazuri hayataki haraka. Muda bado haujafika. Kuwa na subira
kidogo na baadaye utafurahi mwenyewe na roho yako”. Juma aliongea.
Huyu Juma mimi
namfahamu vizuri kwani amekuwa ni rafiki yangu kwa muda mrefu sana. Tatizo la
huyu jamaa ana maneno mengi utafikiri mwanasiasa lakini vitendo mara nyingi
huwa ni sifuri.
Ni mwaka wa saba
sasa Juma amekuwa ni rafiki yangu mkubwa. Tumekuwa tukishirikiana katika mambo
mengi sana ya huzuni nay ale ya furaha. Katika kipindi hicho chote cha urafiki
wetu kuna jambo moja limekuwa likinishangaza juu ya Juma.
Mpaka sasa hivi Juma
ni kijana ambaye anaishi maisha ya ubachela ingawa umri na uwezo wa kuoa anao.
Kila ninapomuhoji juu ya hili basi amekuwa ni mtu wa kupiga danadana za hapa na
pale.
************
Ilikuwa ni majira
ya saa mbili usiku, mimi na Juma tulikuwa tumetinga katika mtaa wa Pinto. Mtaa
huu ulikuwa ni mtaa maarufu sana jijini Kano. Ulikuwa ni moja ya mitaa ambayo
imechangamka sana. Muda wote iwe mchana au usiku watu walikuwa wakishughulika
utadhani hawalali.
Jambo ambalo
liliufanya mtaa huu uwe maarufu sana ni biashara ya ufuska. Biashara hii
ilikuwa maarufu sana hasa nyakati za usiku katika mtaa huu. Akina dada wengi
walikuwa wakionekana wakiinadi miili yao kwa lengo la kuwavutia wanaume ambao
wangekwenda kulala nao na kuwapatia pesa.
“Sasa bwana
Mayanja hapa ndio penye suluhu la matatizo yote yanayokukabilia katika ndoa
yako”> Juma aliniambia huku akinyoosha kidole kunionyesha jengo la Grand
Cassino.
“Mbona sikuelewi
bwana Juma? Yaani kunizungusha kwote kule umeamua kuja kunileta huku ambako
kumejaa laana na ushetani wa kila aina!”. Niliongea huku nikimshangaa bwana
Juma.
CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Ushetani?
Ushetani uko wapi?”. Juma aliniuliza huku akinitazama usoni.
“Ina maana wewe
huna macho? Angalia wanawake wale makahaba, yaani wako uchi kabisa”.
Nilimwambia Juma huku nikimwonyesha wanawake ambao walikuwa wakijiuza nje ya
Grand Cassino.
“Kweli wewe bwana
Mayanja naona umeanza kuchanganyikiwa. Ile ndiyo tiba halisi ya matatizo ya
ndoa yako ambayo unasema kila kukicha inakuchanganya kichwa chako”. Juma
aliongea maneno ambayo yalinishangaza sana.
“Una maana gani
Juma?”.
“Nina maana ya
kwamba, inakupasa uende ukachague mrembo mmoja wa nguvu ambaye atakuondoa
mawazo na huzuni ulizonazo na kukufanya uwe bwana Mayanja kamili”. Juma
aliongea.
“Juma rafiki yangu
sasa naona umeamua kunipotosha kabisa”.
“Sasa nakupotosha
nini Mayanja?”.
“Hivi wewe huoni
badala ya kupunguza matatizo ndiyo nitakuwa nayaongeza matatizo kwa kumsaliti
mke wangu?”. Nilimwuliza Juma.
“Mimi siwezi
kukupotosha hata kidogo rafiki yangu. Wanawake wa hapa hawana stress.
Unamchukua unalala naye na kisha unamlipa ujira wake kidogo halafu mnaachana.
Mimi miaka yote ndipo mahali ambapo huwa najivinjari na mwenyewe waniona sina
presha kabisa katika mambo ya mapenzi”. Juma aliongea.
Kwa mbali nilianza
kuona kama maneno ya Juma yalikuwa na ukweli ndani yake. Kwa nini nimbembeleze
mwanamke ambaye habembelezeki? Mimi siyo mtumwa wake kabisa. Yaani namlisha,
namvisha, akiugua namtibu nab ado nimbembeleze? Aaaaaaah! Haiwezekani hata
kidogo.
“Ok, sasa ndiyo
nafanyaje?”. Niliamua kumwuliza Juma maana mimi nilikuwa mgeni kabisa katika
mambo haya.
“Kwanza shika hizi
kondomu. Pili unaenda pale na kumchagua unayemtaka baada ya hapo mnaenda gesti
na kumalizana. Gesti haziko mbali. Utaniangalia mimi ninavyofanya”. Juma
aliongea huku akinikabidhi mipira ya kiume.
CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Baada ya hapo
tukaondoka kuelekea nje ya Grand Cassino ambako kulikuwa kumejaa wanawake wengi
warembo makahaba.
“juma nenda na
mimi. Cheki ninavyolipa”. Mwanamke mmoja alimwambia Juma huku akiyatikisa
makalio yake.
Kumbe Juma alikuwa
maarufu sana katika maeneo haya. Kila mwanamke kahaba alikuwa akimfahamu. Ama
kweli waswahili walisema tembea uyaone.
Macho yangu
yalitua kwa mwanamke mmoja mrembo ambaye alikuwa akija kwangu kwa mwendo wa
maringo sana. Alikuwa na uzuri ambao ulikuwa ni ngumu sana kumithilika na uzuri
wowote duniani. Moyo wangu uliingiwa na ganzi na mdomo wangu ulishikwa na
kigugumizi. Nikatokea kumpenda ghafla kwa mahaba mazito.
“Twende zetu”.
Mwanamke yule mrembo aliniambia huku akinishika mkono.
Nami mithili ya
mwanakondoo aliyekuwa akielekea machinjoni nilimfuata yule mrembo. Nilikuwa
nimeshikwa na wehu wa ghafla.
Tulipata gesti na
kisha nikachukua chumba. Tukaingia ndani huku nikiongozwa na yule mwanamke
ambaye alionekana ni mwenyeji sana maeneo yale.
“Vipi mbona
unaonekana mwoga sana?”. Yule mrembo kahaba alinihoji kwa sauti moja tamu sana.
“Mh! Hapana. Niko
safi kabisa”. Nilimjibu kwa sauti iliyokuwa imejaa kigugumizi.
“Ok, umebeba
kondomu?”. Aliniuliza.
“Yes! Ninazo”.
Nilimjibu huku nikizitoa zile kondomu na kuziweka juu ya meza ambayo ilikuwa
mle ndani.
“Sawa. Fastafasta
ni shilingi elfu tano, saa moja ni shilingi elfu kumi na tano na mpaka asubuhi
ni shilingi elfu thelathini. Sijui wewe ungependelea huduma ipi kati ya hizo?”.
Yule mrembo kahaba aliniuliza.
“Saa moja”.
Nilimjibu yule mrembo.
CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Yule mrembo
alianza kutoa sketi yake fupi na laini na kubaki na tight ambayo ilizionesha
vyema hips zake. Akaitoa blauzi yake na kubaki na sidiria ambayo iliyabeba
matiti makubwa kiasi yenye mvuto sana.
Baada ya zoezi
hilo kuisha alikuja na kunikumbatia kisha akanipa busu moja mwanana katika
sikio langu. Busu lilile lilinifanya nisisimkwe na mwili na kuirekebisha vyema
akili yangu ambayo ilikuwa mbali sana. Mjomba naye alisisimka na kuanza
kujitutumua ndani ya suruali yangu mithili ya chatu aliyemwona mwanambuzi.
Yule mrembo
alinichukua na kunikalisha taratibu juu ya kitanda na kisha akanikalia katika
mapaja yangu na kuanza kufungua vifungo vya shati langu huku macho yake ya huba
yakinitazama.
Baada ya sekunde
kadhaa akafanikiwa kunifungua shati langu na kulitupia mbali. Baadaye sasa
akaja katika suruali yangu ambapo aliutoa mkanda wa suruali na kisha kuifungua
zipu ya suruali taratibu na wakati huo wote mjomba aliendelea kututumka mle
ndani ya mkwego utadhani amelishwa hamira.
************
ITAENDELEA

0 Comments