“Mnakwenda wapi?” Dereva
aliniuliza.
Sikuwa na pa kwenda.
Nilichohitaji ni kuondoka eneo hilo kuelekea popote. Sikuwa tayari kuwaona wale
vijana wa Kimasai tena. Kwani kama wasingeniua mimi ningewaua wao au mmoja wao.
Pia sikuwa tayari
kutazamana na akina Leakey macho kwa macho, iwapo wangerejea ghafla kutokana na
hasara niliyowatia.
“Wapi?” Dereva
alihimiza.
“Kwani nyie mnakwenda
wapi?”
“Singida, kupitia
Babati,” Sikuhitaji kumjibu. Niliparamia gari lake. Msichana alifanya
hivyohivyo. Tukaondoka. Tulipumzika kwa muda. Nilitumia mapumziko hayo kumvuta
kando na kumtaka abakie hapo na kuwatafuta ndugu zake wengine. Alikataa
katakata kwa maelezo kuwa toka alipokataa tohara tayari amekataa ndugu wote
hivyo hana mahala pa kwenda.
“Kwan nini usikubali
kupata tohara?” Nilimhoji. “Naogopa.” Lilikuwa jibu lake.
“Unaogopa?”
“Kufa. Mwenzangu alikufa
jusi tu.” Alisisitiza.
“Lakini mimi sina pa kukupeleka.
Mwenyewe sijui nitakwenda wapi, nitalala wapi. Huoni kuwa unanipa mzigo juu ya
mzigo?” Nilijaribu kumshawishi. Badala ya kunielewa aliangua kilio. Kwa mara
nyingine ushujaa ulinitoka, ubinadamu ukachukua mkondo wake.
Kwa bahati nzuri
nilikuwa na tabia ya kutembea na akiba yangu yote ya fedha mfukoni, isipokuwa
zile zilizokuwa benki peke yake. Hivyo, mkasa huo ulinikuta nikiwa na vijisenti
ambavyo vingeweza kuniweka hai kwa wiki mbili tatu kabla ya kuanza kutaabika
kwa njaa. Nilitumia sehemu ya senti hizo kulipia nauli na kula chakula cha
mchana kabla ya kuanza tena safari ya Singinda.
Mzee mmoja tuliyekuwa
naye safarini humo. Nadhani alisoma sura yangu iliyojaa mashaka na ule uso wa
Kimasai uliolowa machozi. Aliniuliza kulikoni. Nilihitaji sana ushauri hivyo
sikusita kumsimulia kila kitu, toka mwanzo hadi mwisho wa mkasa. Kwa mshangao
wangu nilimwona akiangua kicheko baada ya kunipa pole.
“Sioni kama kuna jambo
la kuchekesha hapo,” nilimwambia kwa sauti ndogo iliyoficha hasira zangu dhidi
ya kitendo chake hicho.
Mzee alinishika bega
kabla ya kuninong’oneza ili msichana yule asisikie. “Nacheka kwa kuwa
unasumbuliwa na jambo dogo sana,” alinieleza.
Sikumwelewa. “Dogo
kivipi? Mtoto wa watu hana pa kwenda kwa sababu ya uzembe wangu. Mimi mwenyewe
sina pa kwenda kwa sababu ya uzembe uleule. Unaliita jambo dogo?” nilimwuliza.
“Dogo sana.” Alisema.
“Nitakusaidia mara tutakapofika Singida. Naitwa Kingu. Halfan Kingu. Kwa hilo
ondoa wasiwasi mwanangu.”
Nilishusha pumzi. Kwa
muda nilisahau matatizo yangu na kuifurahia safari kwa kuyaruhusu macho yangu
kuburudishwa na mandhari mbalimbali za mazingira kando mwa barabara hiyo. Mbuga
pana zilizojaa ndege na wanyama ainaaina zilitulaki, majabali yaliyosimama
katika maumbile ya kusisimua yalitushangaza, majangwa yasiyo na msitu wala
nyasi nayo yalikuwa sehemu ya mazingira hayo.
Tulifika Singida jioni
sana. Wakati huo tayari roho yangu ikiimba tenzi na mashahiri juu ya Singida
niliyoifahamu kupitia simulizi za kihistoria na maandishi ya vitabuni.
Kwa mfano, nilipata
kusoma juu ya reli iliyojengwa enzi za vita kuu inayounganisha mji huo na reli
ya kati kupitia Manyoni. Leo nilikuwa nimepata fursa ya kuiona kwa macho yangu
mwenyewe reli hiyo.
Singida, nchi ya
mwanamke pekee shujaa katika historia ya mapambano ya Watanganyika dhidi ya
ujio wa wakoloni. Mwanamke huyu Leti Kidanka, kati ya mwaka 1903
hadi 1907 aliongoza
majeshi ya Wanyaturu kupambana na yale ya Wajerumani hata wakaelekea kusalimu
amri. Kama isingekuwa kwa ajili ya silaha zao kali na nyingi Wajerumani wale
wasingefanikiwa kumkamata, wakamchinja na kuondoka na kichwa chake kama
walivyofanya kwa Mkwawa.
Niliweza kuyaona majengo
ya kale, boma la kilimatinde walilojenga Wajerumani hao kati ya mwaka 1880 na
1890 na lile la mkoloni lililojengwa 1900 hadi 1911. Boma ambalo lilikuwa makao
makuu, ofisi, gereza, makazi ya maafisa wao na eneo la kunyongea watu.
Nilishangaa kuona mti uliokuwa ukitumika kunyongea watu toka enzi zile ukiwa
hai hadi leo.
Mzee Kingu ambaye
tulifuatana naye katika safari hiyo ya mjini baada ya kuhusika kwenye gari
alitabasamu kila aliponiona nikivutiwa na hiki au kile.
“Laiti ungefika Iramba,”
alisema na kuongeza “Kuna vivutio tele ambavyo kwa udadisi wako vingekusisimua
sana. Kuna mapango kama yale ya Kondoa Irangi na majabali yaliyoumbwa kwa namna
ya binadamu,” alisema.
“Unaifahamu Sodoma na
Gomora?” Aliniuliza ghafla. “Naam. Imesimuliwa katika Biblia na Koran,”
nilimjibu. “Unafahamu chochote juu ya mwanamke aliyegeuka
mwamba wa chumvi baada
ya kugeuka nyuma kuutazama mji wa Sodoma ukiteketea kinyume cha maelekezo
waliyopewa?”
Hili pia nililifahamu,
“Mke wa Lutu sio?”
Mzee Kingu alitikisa
kichwa kuafikiana nami. “Kwa taarifa yako sanamu ya mwanamke yule aliyeganda na
kugeuka nguzo ya chumvi iko huku kwetu. Ukienda Iramba, uingie maporini
utaikuta. Na chumvi inapatikana hadi leo kama ilivyoandikwa,” aliongeza.
“Wewe ulipata kuiona?”
Nilimuuliza.
“Sijapata lakini wazazi
wangu walinihakikishia. Wao walikuwa wakienda huko katika safari zao za
uwindaji.”
Sikuweza kumkubalia wala
kumkatalia. Tulikuwa tukitembea mjini. Yeye mbele, mimi kati, msichana wa
Kimasai nyuma. Ilikuwa safari iliyobuniwa na mzee huyo kwa maelekezo kuwa ni ya
kunisaidia. Hata hivyo, alikuwa hajaniambia tunakwenda wapi.
Vivutio vya mji wa
Singida havikuwa na mwisho. Maziwa yaliyojikita katikati ya mji, Singidani na
Kindai ni miongoni mwa mambo ambayo yasingekosa kumvutia mgeni yeyote. Sehemu
fulani tuliwaona wavuzi wakitafuta riziki zao katika maziwa hayo, huku ndege
kama bata maji na yangeyange nao wakijishughulisha na yao.
Safari yetu iliishia
mbele ya jengo moja lililokuwa na maandishi yaliyosomeka EVANGELICAL LUTHERAN
AUGUSTANA SYNOD. Kingu aliniambia kuwa hiki kilikuwa kitengo cha kanisa ambacho
kilijishughulisha na kusomesha watoto yatima na wale wasiojiweza. Aliniambia
kuwa wasingesita kumpokea msichana huyo na kumlea, hasa baada ya kuonyesha
msimamo wake wa kupingana na mila potofu za jamii yake.
Nilimweleza hivyo
msichana yule. Nilishukuru kuona akiipokea habari hiyo kwa utulivu.
Tulikaribishwa ndani. Mtumishi aliyetupokea hakushangazwa na maelezo yetu hata
kidogo. Alimshika msichana yule mkono kwa dalili zote za upendo kabla ya
kumwuliza umri wake.
Hakujua ana miaka
mingapi. Kwa kukadiria kwangu hakuzidi miaka kumi na miwili. Mchungaji wao
hakuwepo. Hivyo alitutaka mimi na Kingu kuondoka kwa maelezo kuwa msichana huyo
alikuwa katika mikono salama.
Tuliinuka. Nilishangaa
kuona msichana huyo naye akiinuka na kunifuata. Nilimtazama kwa macho makali
yenye maswali mia moja na moja. Hata hivyo, nilipumua pale nilipomuona
akitabasamu na kisha kusema kwa kiswahili chake kibovu, “Taka kushukuru.
Yenyewe imeokoa maisha yangu.”
Alinikumbatia. Machozi
yakimlengalenga machoni.
Kitendo chake kiligusa
ile sehemu laini katika moyo wangu. Mie pia nilihisi machozi yakinilengalenga.
“Hapana ni wewe uliyeokoa maisha yangu,” nilimwambia. Ulikuwa ukweli toka
katikati ya moyo wangu.
“Hapana kweli… mimi
haribu maisha yako,” alijitetea.
Sikutaka kuendelea na
mjadala huo. Hivyo nilijikwanyua taratibu toka katika mikono yake na kuanza
kuondoka, huku nikijitahidi kuyaepuka macho yake.
Hutaki kujua hata jina
langu? Nilihisi swali hili katika macho yake. Nikajikuta nikitokwa na swali
hilo.
“Mimi naitwa Nashifa,”
alisema.
“Vizuri sana Nashifa.
Mimi naitwa Petro. Petro Kionambali,”
* * *
Kuutua ‘mzigo’ ilikuwa
mwisho wa tatizo moja. Tatizo la pili, langu binafsi lilikuwa palepale. Sikujua
usiku huo na siku zinazofuata ningekitua wapi kichwa changu wakati nikianza
upya kufikiria hatma ya maisha yangu, baada ya miaka kadhaa ya kuzungukwa na
akina Leakey katika Bonde la Ufa na miji au vijiji vya jirani.
Nadhani kwa mara
nyingine Kingu aliweza kuusoma moyo wangu. Ni pale nilipomsikia akianza
kujinadi ghafa
kwamba anatoka katika
ukoo unaoheshimika na usio na njaa. “Wanyaturu wote wananifahamu. Natoka katika
ukoo wa Machifu. Huyu unayemsikia Chifu Said Gwao mdogo wangu upande wa baba.
Kwangu utalala, utakula bila wasiwasi wowote.”
Nikashtuka. “Hayo
yametokea wapi tena?” nilimwuliza.
“Naona unasumbua kichwa
chako kufikiri leo utalala wapi,” alinijibu. “Hilo achana nalo kabisa mwanangu.
Fikiria mengine.”
Nilimtumbulia macho ya
mshangao uliochanganyika na aibu. “Nisingependa kukusumbua zaidi. Tayari
umenisaidia sana. Kunipatia makazi ya yule msichana lilikuwa tatizo langu
kubwa. Mengine sioni kama yatanisumbua,” nilimweleza.
“Huwezi kulala nje.
Huwezi kutupa pesa katika vyumba vya wageni kwa ajili ya kulala tu. Utakuwa
mgeni wangu. Leo, kesho na keshokutwa. Utakaa hadi hapo utakapoamua
vinginevyo.”
Sauti yake iliashiria
kufunga mjadala. Akiwa mtu mwenye umri mkubwa, bila shaka zaidi ya baba yangu,
ingawa hakumpata babu, nililazimika kumsikiliza. Tukaongozana kuelekea kwake.
Yeye mbele mimi nyuma.
Mzee Kingu alikuwa
akiishi nje kidogo ya mji. Kauli yake kuwa hakuwa mtu mwenye njaa ilidhihirika
mara tulipofika nyumbani kwake. Kwa kweli haikuwa nyumba bali majumba. Alikuwa
na kijiji! Nyumba kama nane hivi, zikiwa katikati ya shamba la ekari zipatazo
tano au zaidi, za matama na alizeti. Tatu zilikuwa nyumba za wake zake, nne za
wanawe na moja niliyoambiwa kuwa ilikuwa maalumu kwa ajili ya wageni. Pembeni
alikuwa na zizi kubwa la mifugo. Milio ya ng’ombe na mbuzi ilisikika.
Tofauti na alivyokuwa
safarini, mcheshi na mzungumzaji sana, hapa nyumbani alikuwa mtu mwingine
kabisa. Tulifika yapata saa mbili za usiku. Mji huo ulikuwa umechangamka kwa
kelele za watoto, sauti za redio na pilikapilika za akina mama. Hali ambayo
ilibadilika mara mzee alipotia mguu katika himaya hiyo. Wajukuu walipunguza
kelele, kila mmoja akirejea kwa mama yake. Watoto walimfuata na kumsalimu,
lakini katika hali ambayo haikuwa tofauti sana na salamu za askari na afande
wake. Walibadilishana maneno mawili matatu, ya juujuu, kabla ya watoto hao
kuteleza kila mtu akienda anakokufahamu. Hali haikuwa tofauti sana na wake zake
wadogo. Ni mke mkubwa pekee ambaye baada ya kumsalimu aliketi na kumwuliza
habari za safari. Hata hivyo, baada ya dakika moja tu yeye pia alijikuta hana
cha kuzungumza. Aliketi pale kwa utulivu kama anayesubiri amri, ambazo zilianza
kumiminika mara moja.
“Huyu ni mgeni wangu.
Chumba chake kimeandaliwa?” “Wale ng’ombe wawili wagonjwa wamepatiwa dawa?”
“Nina mashaka kama mmekumbuka kurekebisha lile
ghala linalovuja…”
Mkewe ambaye tayari
alikuwa mama wa makamo alijibu kila swali kwa ufupi na umakini mkubwa kama
mwanafunzi kwa mwalimu wake.
Muda mfupi baadaye
chakula kililetwa. Hakikuwa chakula cha watu wawili wala watatu. Ulikuwa mlo
ambao watu sita wangeweza kula na kusaza. Ulikuwepo mguu wa mbuzi wa kuchoma,
kuku wawili waliopikwa, sinia kubwa la wali na bakuli la matunda. Wakati mimi
niliishia kula mapaja mawili ya kuku na wali kidogo mzee Kingu aliteketeza robo
tatu ya chakula kile. Alikula nusu ya matunda na kushushia kwa birika zima la
maji.
“Endelea kula.”
Alinihimiza “Mimi nimechoka. Unajua utu uzima tena! Watakuonyesha sehemu ya
kulala,” alisema akiondoka bila kusubiri shukrani zangu.
Mie pia uchovu ulikuwa
umenishika. Hivyo, mara alipoondoka nilinawa mikono, nikamshukuru bi mkubwa
ambaye muda wote alikuwa pale. Kisha niliomba nielekezwe yalipo malazi yangu.
Mvulana mmoja alinipeleka kwenye nyumba ya wageni. kiasi ilijitenga na nyumba
nyingine na hivyo kutoa uhuru wa kutosha kwa wageni. Taa ya chemli ilikuwa
ikiwaka chumbani, kando ya kitanda kilichotandikwa kwa blanketi na shuka mbili
safi. Mara tu kijana huyo alipotoka nilivua nguo zangu na nikafunga mlango na
kisha kujibwaga kitandani.
Mkesha wa siku hiyo,
uchovu wa safari ya miguu na gari pamoja na purukushani za siku nzima vilifanya
usingizi unichukue mara tu nilipokitua kichwa changu juu ya mto. Ulikuwa
usingizi wa pono. Nililala hadi saa tisa au kumi za alfajiri nilipoamshwa na
kitu fulani. Sikufahamu ni kitu gani lakini hisia zilifanya nishuku jambo. Sina
tabia ya kukoroma, bado niliamini kuwa nilijisikia kama nakoroma usingizini.
Nilitulia kimya nikijaribu kufikiri kitu gani kiliniamsha. Sikuelewa. Wakati
usingizi ukianza tena kunichukua hisia zilezile za kukoroma zilinireja. Hapa,
hazikuwa hisia. Ilikuwa sauti halisi ya kukoroma tena ikitoka chini ya kitanda.
Nilishuka toka
kitandani, nikapandisha mwanga wa taa na kuchungulia uvunguni. Nilishangaa
kuona kitu kama tochi mbili zikinimulika toka chumbani humo. Tukio ambalo
lilifuatiwa na mguno mzito kama ule wa mbwa anayehisi kuhatarishiwa uhai wake.
“Fisi!”
Niliropoka baada ya
kutazama vizuri. Fisi mkubwa kabisa alikuwa amelala uvunguni humo, chini ya
kitanda changu! Nilitetemeka. Nikaruka kuendea nguo zangu ambazo nilivaa
harakaharaka na kutoka mbio.
Mbio ambazo ziliishia
mbele ya nyumba ambamo nilimuona mzee Kingu akiingia kulala. Kabla hata
sijagonga niliona mlango ukifunguliwa, mzee akiwa amevaa kikoi, kifua wazi.
Alitoka. “Kuna nini?” alihoji kwa sauti kali kidogo.
“Fisi yuko chumbani
kwangu.” Nilimjibu.
Mzee akaangua kicheko.
“Hilo tu?” alinihoji baadaye. “Yule pale hana neno. Zaidi anakulinda kama
anavyoulinda mji huu.”
Sikumwelewa. “Hana
madhara! Kwa hiyo nikalale na
fisi?”
Mzee alicheka tena.
Kisha akasema, “Kumbe wewe bado
mtoto mdogo sana sio?
Unadhani himaya hii utailinda vipi bila kuwa na vitu kama vile? Yule amefugwa.
Anatii amri zangu zote na hafanyi jambo lolote bila maagizo yangu. Isitoshe ni
mtumishi mzuri anayebeba mzigo na hata kunibeba mimi mwenyewe katika safari
zangu za usiku.”
Nilizidi
kuchanganyikiwa. Nazungumza na binadamu au shetani? Anazungumzia kufuga fisi
kama kufuga mbwa!
“Binadamu anawezaje
kumfuga mnyama kama yule?” nilimwuliza bila kutarajia.
Na bila kutarajia
vilevile alinijibu. “Ujuzi tu mdogo wangu. Nyie mnaita uchawi lakini ni ujuzi.
Ukipata jino la fisi unaweza kumfuga fisi. Ukipata la mamba unaweza kummiliki
mamba. Vivo hivyo kwa simba, chui na hata nyoka. Watu wanawafuga binadamu
wenzao washindwe kumfuga mnyama?” alisema. Sasa nilikuwa na hakika kuwa
sizungumzi na binadamu
wa kawaida. Sikuona kama
nilihitaji kuendelea kumsikiliza. Alizisoma hisia zangu. “Nenda
kalale,”akaniamuru.
Nikageuka kuondoka. Mara
akaniita tena, “Kijana,” alisema. “Kitu kimoja kinanisumbua. Umekula nini
wewe?”
“Nimekula nini? Una
maana gani?” sikumwelewa.
Maana wenzako wote
hulala na fisi wangu hata kwa
mwezi bila kumwona wala
kumsikia. Wewe umetafuna nini?”
Sikumjibu. Niliondoka.
Wala sikurudi kwenye banda lake la kuchangia na fisi. Nilipitiliza kuifuata
njia iliyonifikisha katika mji huo. Nilitembea taratibu hadi mjini. Alfajiri
ilinikuta nikipitapita katika mitaa ya mji huo. Jua lilipochomoza lilinikuta
nimeketi kando ya ziwa Singidani nikitazama pilikapilika za wavuvi.
Sikuwa na wazo jingine
zaidi ya kutafuta gari litakalonipeleka kokote kwenye usalama. Sikuwa tena na
hamu ya kuendelea kuivinjari Singida.
Niliuliza mahala
wanapopandia magari ya kwenda mikoani, nikaonyeshwa. Sikusita kulipia nauli ya
kwenda Kilimanjaro na kuianza safari mara moja.
?
17
Ben R. Mtobwa
SURA YA KUMI NA SABA?
Kilimanjaro, Paa la
N
ilikuwa nimesikia mengi
ju ya Kilimanjaro, mlima mrefu kuliko wote barani Afrika. Hali kadhalika,
nilisoma mengi na kutazama picha nyingi
zilizoonyesha mlima huo.
Lakini katika yote hayo niliyosikia au kuona kwenye picha hakukuwepo lolote
lililoniacha nisiweze kupigwa na butwaa huku nikiwa siyaamini macho yangu pale
nilipoutia machoni mlima huu. Kwa kweli, ni mlima ambao lazima uuone, kusimuliwa
pekee kulikuwa hakutoshi.
Ilikuwa ndio kwanza
nashuka toka katika basi lililonileta mjini hapo, macho yangu yalipopokelewa na
utukufu ule. Ujio wangu Kilimanjaro ukiwa umefanyika bila matarajio baada ya
yale mapokezi ya kutisha niliyoyapata Singida. Mapokezi ya kulazwa chumba
kimoja na fisi.
Ni mawazo hayo
yaliyofanya Singida kama nuksi nyingine iliyokuwa ikinisubiri. Hali
iliyopelekea baada ya siku mbili tatu za kuzurula mjini hapo nipande basi
lililonileta Kilimanjaro, kwa matarajio ya kupata kazi au biashara yoyote
ambayo ingeniwezesha kupata chochote ili nitimize azma yangu ya kurudi
nyumbani. Azma ambayo umuhimu wake uliongezeka siku baada ya siku.
Mlima ulisimama pale kwa
kiburi na fahari zote. Ulikuwa?
peke yake, ukiwa umechomoza
hadi juu ya mawingu, kiasi cha kujionyesha vizuri popote uliposimama katika
eneo la miji kama Moshi, arusha na vitongoji vyake. Ukiwa umepambwa kwa
theluthi iliyokuwa ikimeremeta kileleni, Kilimanjaro ulisimama pale, peke yake,
kama mfalme aliyevalia taji lake ambaye hakuwa na mpinzani. Hapana, alionekana
zaidi kama malkia mwenye majivuno, aliyevalia mapambo yake yote, ambaye
hakupenda kujichanganya na watu wengine. Sijui ningeukodolea macho kwa muda
gani mlima huo kama nisingehisi kushikwa bega huku sauti ya mtu mmoja ikisema,
“Angalia, yasije yakakukuta yaliyomkuta Rebmen kwa kuushangaa mlima huo.”
Nikazinduka. Nikayaondoa
macho yangu toka kileleni na kumtazama msemaji. Alikuwa mpita njia tu, mvulana
aliyevaa mavazi ya shule, mfuko wa madaftari yake ukiwa kwapani. Alikuwa
akitabasamu.
“Rebmen gani?”
nilimuuliza.
“John Rebmen. Yule
Mjerumani aliyekuwa Mzungu wa kwanza kuutia machoni mlima huu,” alifafanua.
Nikalikumbuka jina hilo.
Nikakumbuka pia tarehe na mwaka ambao Rebmen aliuona mlima huo kwa mara ya
kwanza. Ilikuwa Mei 11, 1848.
“Rebmen alifanya nini?”
niliuliza.
“Hukumbuki?” mwanafunzi
huyo alinihoji. “Hukumbuki yaliyompata? Hukumbuki kuwa aliibiwa mfuko wake
uliokuwa na fedha zake, nyaraka zake na kumbukumbu zote za safari yake?
Ulivyokuwa umeduwaa pale wewe pia ungeweza kuporwa huo mfuko wako bila kujijua”
Nikacheka. Nilikumbuka
kusoma tukio hilo kwenye kitabu cha mwandishi mmoja. Nadhani alikuwa Rebmen
mwenyewe aliyeandika.
Kwamba akiwa Kilimanjaro, maeneo ya kibosh, aliibiwa mfuko wake uliokuwa na
fedha zake zote na nyaraka zake zote muhimu. Siku hizi watani wa Wachaga, hasa
Wapare, hulitumia tukio hilo kuwadhihaki Wachaga kuwa kwa ajili ya tukio lile
Rebmen aliyekuwa mmisionari aliwalaani hata wakawa watu wa kupenda na kuabudu
sana pesa kuliko utu. ‘Mchaga mzuri ni aliyekufa tu,’ ni moja ya kauli
zinazoendana na utani huo.
Ingawa sikumbuki kama
kweli Rebmen aliibiwa wakati akiushangaa mlima lakini bado nisingeweza
kumlaumu. Kwa mtu kama yeye, aliyetoka mbali sana na ambaye hakupata kusikia
wala kuona picha ya mlima huo kama mimi, kuduwaa kiasi cha kuibiwa begi lake
kamwe lisingekuwa jambo la ajabu. Kitendo cha ardhi kuchomoza hadi meta 5894
juu usawa wa bahari, huku ukiwa umesimama peke yako siyo jambo la kawaida.
Aidha, ile theluji kileleni na historia ya milipuko ya volkano katika vilele
vyake vitatu vya Kibo, Mawenzi na Shira ni sababu nyingine za kihistoria ambazo
zitamfanya mtazamaji aukodolee macho hata kuweza kuporwa begi lake.
Hata hivyo, kauli ya
mtoto yule wa shule ilinifanya nianze tena kutembea mitaani, begi mkononi,
macho yakiwa hayakomi kurudi kwenye kilele cha mlima mara kwa mara.
Mji huu wa Moshi, ulio
mbali kwa kilomita 580 toka Dar es Salaam na 76 toka Arusha, uko kilomita 890
toka usawa wa bahari. Hesabu ya watu wa mwaka 1948 ilionyesha kuwa mkoa mzima
wa Kilimanjaro ulikuwa na idadi ya watu wapatao 267,700.
Hiyo ilikuwa sehemu ya
akiba yangu ya kumbukumbu juu ya Kilimanjaro. Sehemu nyingine ilikuwa juu mkazi
mkuu wa mkoa huo, Mchaga. Wakati watu wengi walifahamu
kuwa Wachaga ni kabila
moja, linaloongea lugha moja, mimi nilikuwa na taarifa tofauti. Wakiishi kusini
mwa mlima Kilimanjaro Wachaga ni mkusanyiko wa makabila mbalimbali,
wanaozungumza lugha mbalimbali wakiwa wametoka katika maeneo mbalimbali kwa
nyakati mbalimbali. Watu hawa, ambao kwa bahati wote ni wabantu, baadhi yao
wanafananishwa na Wakamba wa Kenya kwa siha na lafudhi. Wengine wanafaninishwa
na wataveta na hata watu wa Niger na Kongo. Wataalamu wanahisi watu hawa
walivutwa na hali ya hewa, mbali na utajiri wa misitu kwenye mteremko wa mlima
tangu karne ya kumi na saba. Hali iliyowawezesha kuwa wakulima wakubwa wa
mibuni kama zao la biashara na migomba kwa ajili ya chakula.
Miongoni mwa makabila
yanayounda Wachaga ni pamoja na Warombo, Wamachame, Wavunjo na Wamarangu.
Inaaminika kuwa katika zama zile za kuhamia Kilimanjaro makabila haya, ambayo
yalikuwa na falme tofauti kama zilivyo lugha na tamaduni zao walipigana vita
mara kwa mara. Kabila jingine maarufu Kilimanjaro, Wapare, lilitumia fursa hiyo
kwa manufaa yao kiuchumi. Inaaminika Wapare walikuwa wafua vyuma mashuhuri
ambao koo mbalimbali za Wachaga ziliwategemea kuundiwa silaha mbalimbali kama
mikuki mishale na mapanga kwa minajili ya kujipatia ushindi dhidi ya koo
nyingine.
Nilijikumbusha hayo wakati
nikitembea taratibu toka kituoni hapo nikifuata barabara ambayo sikuifahamu,
wala sikuwa na haraka ya kuifahamu. Nilikuwa nimejikumbusha nguo zangu za kazi,
kaptula na shati la kaki murua ya Marekani, viatu vizito vya dhoruba na soksi
nyeusi. Nywele zangu, kama kawaida, zilikuwa fupi zilizochongwa vizuri. Nadhani
nilionekana mrefu kuliko
watu wengi eneo hilo. Nadhani pia ngozi yangu ya maji ya kunde, usafi wa mwili
wangu na utulivu wangu wakati nikivuta hatua moja baada ya nyingine kutoka
kituoni hapo ni miongoni mwa vitu vilivyovutia macho ya wapita njia dhidi
yangu. Niliona nikitazamwatazamwa kuliko kawaida, baadhi ya watu
walinong’onezana huku vidole vikielekezwa kwangu.
Halafu likatokea jambo
ambalo halikupata kutembelea fikra zangu. Kundi kubwa la kinamama liliibuka
toka mahala fulani kituoni hapo na kunifuata mbio. Waliponifikia walianza
kuimba huku wakipiga makofi na vigelegele.
Babaaa baba huyoo….
Babaa baba huyo…. Baba…
Sikuelewa. Nilisimama na
kugeuka huku na huko nikitazama nani anapokelewa na kushangiliwa kiasi hicho.
Hakuwa mwingine zaidi
yangu. Walikuwa tayari wamenizingira, mfuko wangu ukapokonywa na mama mmoja
kuamua kuubebea yeye. Waliendelea kuimba.
“Karibu sana baba,”
mmoja wao alisema huku akinikumbatia.
Nilizidi
kuchanganyikiwa. Ama wana wazimu ama mimi napata wazimu! Niliwaza nikijaribu
kujibabadua toka katika mikono ya mama huyo.
“Vipi… kuna nini?”
nilijaribu kuuliza. Sikusikika. Kelele zilikuwa nyingi. Yule aliyenikumbatia
kwanza aliwageukia wenzake na kuwaambia, “Mnaona? Niliwaambia ni mtu mwenye
haya sana.” Akawageukia vijana wa kiume waliokuwa kando na kuwauliza, “Mbona
hamchangamki? Mpokeeni kishujaa shujaa wetu.”
Kauli hiyo ilifuatiwa na
vijana hao wa kiume kunivamia,
wawili kati yao
wakaniinua na kunibeba juu wakiniongoza njia kunipeleka walikokujua. Katika
maongezi yao nilisikia mmoja akisemea, “Nilidhani Nyerere ni jitu kubwa,
linalotisha na kuwatetemesha wakoloni. Kumbe ni mtu wa kawaida…”
Ndipo nikaeleka. Walikuwa
wamenifananisha na Nyerere!
Wakati huo vuguvugu la
kudai uhuru likiwa linazidi kupamba moto majina ya akina Julius Nyerere, Oscara
Kambona, Bibi Titi Mohamed na wengineo yalikuwa yametawala sana katika vyombo
vya habari. Nyerere, ambaye wakati huo alikuwa mwalimu wa shule moja ya
sekondari kule Tabora alifahamika zaidi kutokana na maandishi yake katika
vyombo vya habari hasa magazeti akiwa msomi aliyefika hadi Makerere, Uganda.
Nyerere aliwaandaa Watanganyika kujitawala. Alisema na alisikika sana.
Sikupata kufikiria kama
ingetokea siku mimi, Kiguu na Njia nikapokelewa kwa heshima kiasi hicho. Hivyo,
lazima nikiri kuwa kwa kiasi fulani nilifurahia nafasi hiyo ya kubebwa. Lakini
pia, kwa ajili ya kelele na imani yao kuwa nina haya nilijua wasingeamini chochote
ambacho ningewaambia. Nikaamua kutulia tuli juu ya mabega yao nikicheka
kimoyomoyo.
Msafara huo uliishia
katika nyumba moja ya wageni, mtaa wa tatu kutoka katika kituo hicho.
Nilipelekwa moja kwa moja katika chumba maalum kilichoandaliwa kwa ajili
‘yangu’. Kilikuwa na bafu na choo chumbani humo. Mfuko wangu wa safari tayari
uliwekwa juu ya meza, salama salimini. Yule mama aliyejipa uenyeji zaidi yangu
alisema, “Baba, oga upumzike kidogo. Bibi Titi alifika jana. Nitamwarifu juu ya
ujio wako, pengine mtapenda kuteta kidogo kabla ya kuanza safari ya Machame.
Chifu Abdieli Shangai atakuwa tayari
amewasubiri.”
“Lakini mimi sio
Nyerere,” nilimwonya. “Naitwa…” hakusubiri hata nitaje jina langu. Badala yake
aliangua kicheko, akipuuza alichokichukulia kama mzaha wangu. Akatoka huku
akiufunga mlango nyuma yake.
Sikuwa na jinsi.
Nikaoga. Nikapaka mafuta na kuvuta zile nguo zangu za safari. Nikavaa suruali
na shati safi. Nikatia tai na koti juu. Nilifanya hayo kwa uangalifu mkubwa
bila kuchafua bafu wala kuvuruga kitanda ili mweye chumba chake halisi
atakapotokea akikute kikiwa kisafi.
Wakati nikijiandaa
kutoka, nikiwa na dhati ya kuwahakikishia kuwa mimi sikuwa Nyerere, mlango
uligongwa nikaufungua. Bibi Titi Mohamed alikuwa pale. Sikuhitaji kutambulishwa.
Alikuwa mwanamke mfupi, mnene, mwenye macho maangavu.
“Julius, umeruka kwa
ndege? Nilidhani ungefika hapa jioni,” alisema kwa sauti yenye mamlaka. Sauti
hiyo ilififia ghafla aliponitazama usoni na kubaini kuwa mimi sikuwa Julius
Nyerere waliyekuwa wakimtegemea.
“Nimejitahidi sana
kuwaambia mimi sio Nyerere, hawakukubali,” nilijitetea. “Ni kama nimetekwa
nyara na kuletwa hapa,” niliongeza.
Bibi Titi aliangua
kicheko. Aligeuka kuwatazama wenyeji wetu waliosimama nyuma yake kunisubiri.
Kicheko chake kilizungumza kila kitu. Akageuka tena kunitazama, “Pole sana
bwana. Ni kweli umefanana sana na mwalimu. Kwa mtu asiyemfahamu vizuri
kuwafananisha si ajabu.”
Sikumjibu. Sikuwa na la
kujibu zaidi ya kutabasamu.
“Ulikuwa ufikie wapi?”
aliniuliza.
“Nilikuwa natafuta
mahali pa kupanga.”
“Basi unaweza kulala
hapa,” aliniambia. “Malaika wako amekwishakukuongoza hadi chumbani humu, huna
sababu ya kupingana naye. Pumzika, baadaye tutakaa tuzungumze. Si ajabu mola
kakuleta mikononi mwetu kwa sababu maalum.”
Sikuwa na sababu ya
kukataa.
* * *?
Kwa mujibu wa maelezo
niliyoyapata baadaye, vuguvugu la wagombea uhuru nchini, chama cha TANU ambacho
kilikuwa kimeanzishwa kutokana na TAA kulikuwa na matatizo katika kanda hiyo ya
mashariki, hasa Kilimanjaro. Kwa mujibu wa maelezo hayo, matatizo hayo hayakuhusiana
na chama kukubalika au kutokukubalika eneo hilo bali yalitokana na mvutano
ndani ya Wachaga wenyewe.
Baada ya ule mvutano na
mapigano ya makabila mbalimbali yanayounda Uchaga ulifika wakati pamoja na
kukubaliana kuwa kitu kimoja. Uamuzi huo ulifuatiliwa na kumteua Mangi mkuu
kama msimamizi na msemaji rasmi wa masuala ya Wachaga. Mangi mkuu huyu
aliyekuwa na makao yake huko Marangu aliwekwa juu ya viongozi wengine wote wa
kikabila.
Hata hivyo, ule mzimu wa
chuki na kutokutamaniana miongoni mwao, ingawa ulizikwa, bado haukufa. Ni kama
ulizikwa hai. Ujio wa Mjerumani, ambaye alifuata nyayo za mpelelezi wao Rebmen,
ulifanyika Kilimanjaro iwe chaguo lao la awali, wakati machifu wengine wakisita
kuwapokea. Mangi Sina wa Kibisho, miaka ya 1890 akiwa amejizatiti kiuchumi kwa
kilimo na ufugaji, alikuwa pia ameimarisha jeshi lake ambalo lilikuwa kero
kubwa kwa utawala wa wajerumani. Awali ya hapo Wajerumani hao, chini ya uongozi
wa Karl
Peters, waliendesha
utawala wa kinyama na ukatili mkubwa Kilimanjaro, hali iliyopelekea April 25,
1897 gavana huyo katili afukuzwe kazi na serikali yake.
Lakini miaka mitatu
baadaye, Machi 2, 1890 Wajerumani hao waliwanyonga hadharani, mjini Moshi, viongozi
tisa wa kikabila. Viongozi mashuhuri kati ya waliopoteza maisha siku hiyo
wakiwa Mollelia wa Kibosho, Ngalami na Meli wa Moshi. Madai ya Wajerumani kwa
kitendo hicho yakiwa kwamba viongozi hao walikuwa wakiwavurugia jitihada za
uongozi wao Kilimanjaro.
Hivyo, mkataba ambao
Mangi Rindi wa Chaga aliingia na Mjerumani miaka mitano kabla ya kitendo hicho
cha kikatili, na kuufanya mji wa Moshi kuwa kituo kikubwa cha biashara ya ndovu
na watumwa kati yake na Zanzibar, lilikuwa pigo jingine katika jitihada za
kuifanya Kilimanjaro kuwa na sauti moja.
Ujio wa vuguvugu la
kupigania uhuru kukawa kama msumari wa mwisho kwenye jeneza la jitihada hizo.
Wakati huo tayari yakiwepo malumbano makubwa ya iwapo kulikuwa na uhalali na
haja ya Mangi mkuu kuendelea kutoka katika ukoo na kabila moja na cheo hicho
kiende kwa kupokezana au la. Mangi mkuu, wakati huo Chifu, Thomas Mareale na
kambi yake walishikilia msimamo wao. Kwa upande mwingine, machifu kama Abdiel
Shangali walilipinga hilo kwa vitendo. Wasomi wengi wakiwa nyuma yake, Shangali
alitumia fursa hiyo ya mparanganyiko kuunga mkono TANU na kuwekeza kimsimamo
mikononi mwa mkewe Solomon Eliofoo, aliyekuwa ametokea masomoni Uingereza na
Marekani na kurudi na kuazishwa tawi la TANU Machame.
Lilikuwa tatizo zito kwa
Chifu Mareale. Jitihada zake za kuwekeza kwa Petro Njau hazikuzaa matunda
yaliyotarajiwa, hali iliyopelekea uhusiano wake na TANU ulegelege. Ingawa yeye
binafsi aliwasiliana sana na Nyerere na wakati fulani kumtaka aje Kilimanjaro
kuzungumza na Machifu wote bado alionekana kama mtu aliyekuwa njia panda. Hali
ambayo baadaye ilishusha umaarufu wake, lakini hadhi yake na nafasi yake katika
historia kamwe haikupata kufutika.
Kwa upande mwingine,
Kilimanjaro haikuwa na njaa sana ya uhuru kama zilivyokuwa sehemu nyingine za
Tanganyika. Kiuchumi alikuwa mbali zaidi. Kilimo cha mibuni kilikuwa
kimeanzishwa katika eneo hilo tangu mwaka 1919 na kushika kasi 1930 na
kuendelea. Hali hiyo iliambatana na kuanzishwa kwa vyama vya ushirika, ikiwa
nchi ya Kwanza Afrika kuwa na mfumo huo. Hali ya hewa na ujio wa mapema wa
wakoloni katika maeneo hayo pia ilikuwa neema nyingine kwao. Walipata shule
nyingi na bora zaidi mapema.
Huduma za matibabu,
barabara na maji pia walizijua
kabla ya maeneo mengi ya
nchi kufikiriwa.
Hivyo, inaweza kueleweka
pale ‘Mshumbue’ Mangi mkuu Thomas Lenana Mlanga Mareale II aliponukuliwa
akishuku kuwa Nyerere ‘alikuwa akinikwepa,’ na kwamba alimsahau katika harakati
za uhuru. Hata hivyo, Mangi mkuu huyu aliendesha harakati mbalimbali za kisiasa
ndani na nje, ikiwa pamoja na kumlipa wakili ambaye alimtetea Kenyatta wa Kenya
hadi akaachiwa toka kifungoni wakati akituhumiwa kujihusisha na Mau Mau.
“Hivyo, ni sehemu fupi
ya historia ya uchagani kaka yangu,” Bibi Titi Mohamed alisema baada ya maelezo
hayo ambayo niliyaunganisha na kujaribu kuyaweka katika mtiririko
mmoja baada ya huyu
kusema hili, huyu lile nikijumuisha na yale yaliyokuwa katika kumbukumbu zangu.
Tulikuwa katika ukumbi
wa hoteli hiyo. Watu wapatao wanane, wakiwemo wanawake watano, Bibi Titi na
wawili wengine kati ya wale walionipokea pale kituo cha mabasi. Nilionekana
kama muujiza. Nadhani hata kama angekuwa Nyerere mwenyewe hangepata idadi kubwa
ya watu waliokuwa wakiingia na kutoka kwa nia ya kumwona ‘mtu aliyefanana na
Nyerere’. Wingi wa watu hao wakiwa kina mama ambao walicheka na kujicheka sana
kwa kosa la kunichanganya na kijana huyo aliyekuwa akitajwatajwa sana. Nadhani
kwa namna fulani walidhibitiwa, kwani baadaye tuliketi na kuingia katika maongezi
marefu, yaliyoongozwa zaidi na Bibi Titi, mwanamama msemaji sana, mwingi wa
vichekesho huku akiwa pia msikilizaji mzuri.
“Wachaga wana historia
tofauti na sehemu nyingi za nchi,” Bibi Titi aliongeza. “Sisi watu wa Pwani
tuna historia inayotofautiana kwa kiasi kikubwa na wao. Nadhani wageni wengi
waliotembelea makwetu toka enzi za enzi waliacha athari nyingi miongoni mwetu
zaidi ya Uchagani ambako ni mbali kutokea Pwani.”
“Nadhani,” niliunga
mkono. “Maana toka Waarabu, Wareno, Wajerumani na baadaye Waingereza wenyeji
wao wa awali ni nyie tu.”
“Bibi Titi alitabasamu.
“Tuyaache hayo,” alisema. “Hebu na wewe tuambie yako tukusikie. Ilikuwaje
ukafananishwa na bwana Julius?” alinihoji.
“Kwa kweli sijui. Simjui
Julius wala sijapata kumtia machoni labda imetokea tu tukafanana maana duniani
wawili wawili,” nilimjibu.
“Huna udugu naye?” “Hata
kidogo.” “Wewe ni Mzanaki?” “Wala.”
“Kumbe nini basi.”
“Mie Muha. Natokea kigoma.”
Hufanani na Waha.
Utakuwa Mmanyema.” Bibi Titi alidai. “Lakini hilo halina haja kwa sasa,”
aliongeza. “Kama hutajali, tuambie wewe ni nani, unatokea wapi na unaelekea
wapi.”
Nikawatajia jina langu.
Nilitaja pia kazi niliyowahi kufanya ambayo sasa sikuwa nayo. Walivutiwa na
taarifa ya safari za hapa na pale katika miji na vijiji mbalimbali vya Bonde la
Ufa pamoja na mbuga za wanyama.
“Hujapata kufikiria
kujiunga na harakati za kupigania uhuru?” Bibi Titi aliuliza. Akaongeza, “Maana
wewe unaonekana ni mtu wa watu. Halafu, unatembea sana. Lakini la muhimu zaidi
ni kwamba tungependa kupata mtu wa kwenda kuhamasisha harakati hizi huko kwenu.
Ndiyo kuna watu tayari, lakini hawatoshi. Kumg’oa mkoloni siyo mchezo.
Inahitajika kila silaha na kila askari.”
Wazo hilo halikupata
kunitembelea akilini. Sikuwa na hakika kama mimi ni mtu wa kupanda jukwaani,
mbele ya kadamnasi na kuanza kujinadi kuwa mimi ni bora zaidi ya wengine, au
kumnadi mtu mwingine kwamba anafaa kuliko mwingine. Kwa ujumla sikupata kuwa na
ndoto ya kuwa mwanasiasa maishani mwangu.
Bibi Titi alisoma hayo
katika macho yangu. Akatabasamu. “Ni jambo linalohitaji kulifikiria.” Alinena.
“Harakati zetu bado ni changa. Hakuna fedha za kulipa mtu wala kulipwa. Kwa
ujumla tunajitolea.
Tunachopigania ni uhuru. Ukipatikana kila mtu atakula matunda ya uhuru.”
Alisita, akaitazama saa
yake. “Nadhani basi alilopanda Mwalimu linakaribia kufika. Nisingependa akina
mama wakampokee mtu mwingine wa watu na watu. Naenda mwenyewe kumpokea.
Atafikia hoteli hiihii. Nitakukutanisha naye, pamoja na Kambona, ili uzungumze
nao. Nadhani utakuwa tayari umefanya uamuzi.”
Akainuka na kuondoka,
alifuatana na wale kina mama wengine na wanaume wawili.
Nilibakia na watu wawili
mmoja alikuwa mtu mfupi, mweupe, ambaye kama si kwa ajili ya mvi mbili tatu
kichwani ungeweza kumfikiria kuwa ni mtoto mdogo, ingawa umri wake ulizidi
wangu kwa mbali sana. Hakuonekana kuwa Mchaga. Na hakuchelewa kunithibitishia
hilo pale alipozungumza na mara moja nikabaini lafudhi yake kuwa ya Kipare
zaidi.
“Nikweli
miminiMpare,”alijibu swalilangu.“Nimeungana hawa watani wangu wajanjawajanja,
katika harakati hizi za kupigania uhuru. Tatizo ni hapo utakapopatikana huo
uhuru. Mchaga atapenda kuuteka nyara uwe wake, maana Mchanga mzuri ni yule
aliyekufa tu.” Alisema akimtazama Mchaga.
Yule Mchaga akacheka.
Yeye pia alinizidi umri. Alikuwa amevaa suti ya kijivu, tai shingoni na
alishikilia mkoba wa nyaraka mkononi. Uso wake uliojaza ulipambwa na miwani.
Hali iliyompa sura ya usomi.
“Achana na wajukuu wetu
hao,” aliniambia. “Hao wameshindikana kabisa. Mpare anapata kesi ya kuku, ama
kwa kuiba au kuibiwa. Atauza hata ng’ombe ili ashinde kesi hiyo. Kuna mtu
hapo?”
Mie pia nililazimika
kucheka.
soda.
Waliagiza vinywaji. Wao
walikunywa bia mimi nilikunywa
“Bia?” alihoji mmojawao.
“Sinywi.”
“Kwa nini? Unaumwa?”
“Hapana. Sijawahi kunywa
toka nizaliwe.” Walinitazama kwa mshangao kana kwamba
nimewaambia jambo la
ajabu kuliko yote waliyopata kuyasikia. “Kwa umri huo?” Yule Mchaga aliuliza,
“Huo ni umri wa
kunywa vitu vya kiutu
uzima.” Aliongeza.
“Tatizo ni kwamba
sijapata kuitamani wala kuifiria.
Halafu bei yake kubwa
mara tatu kuliko soda.” Nilijitetea. “Acha ubahili wa Kipare,” Mchaga alisema
akicheka.
Mpare alicheka pia.
Lakini alihamisha maongezi na kunitaka nimsimulie juu ya safari zangu za
maporini. “Huko ulikokwenda kuna wanyama?”
“Wengi tu.” Nilimjibu
“Unaweza kukutana na kundi la nyati wengi kama Ng’ombe wanaofugwa, kundi la
twiga utadhani wako kwenye maonyesho na pundamilia kana kwamba wana sherehe.”
“Tembo?”
“Wengi kupita kiasi”
“Vifaru?”
“Wengi tu.”
“Umepata kuwaona kwa
macho yako?” “Mara nyingi tu.” Nilimjibu.
Mchaga alijaribu
kuingilia kati, lakini Mpare alimkatisha kwa maswali yake juu ya wanyama na
maeneo tuliyotembelea. Nilipomtajia kuyafahamu kwangu vyema maeneo ya Manyara,
Ngorongoro na Tarangire alionekana kuvutiwa zaidi. Nilihisi
kuona dalili za udenda
zikielekea kudondoka toka mdomoni mwake. Sikuwa na hakika kama niliona vizuri.
“Itabidi tuzungumze kama
wanaume baadaye,” aliniambia. “Unatarajia kuondoka lini?”
“Sina haraka,”
nilimjibu. “Nitapenda kufika Arusha pia
kabla ya kurejea
maporini,” niliongeza.
“Nitakupeleka.”
Alidakia. “Mimi ni mwenyeji Arusha kuliko hapa Moshi. Hutohitaji kulala au kula
hotelini.”
Mchaga aliangua kicheko
cha dhihaka, kicheko kilichofuatiwa na “Ndugu yangu umekwisha. Mpare ajitolee
kukupeleka Arusha, akupe malazi na chakula! Kuna jambo hapo,” alisema.
“Atakwisha yeye,”
nilijibu, “Maana siye Wamanyema tuna historia ya kula watu. Nitamla mzimamzima
kabla yeye hajanila,” kauli ambayo iliniangusha kicheko kirefu.
“Lakini Wapare unawajua
vizuri? Wana maradhi yasiyo na dawa ya uchoyo. Wewe na yeye mtakufa njaa hata
kabla hujafikiria kumla, huku mkiwa na fedha mfukoni,” aliongeza na hivyo
kuongeza kicheko. Sikujua mengi juu ya Wapare zaidi ya ukweli kuwa ni kabila
jingine kubwa la Kilimanjaro, wanaishi katika miteremko ya milima ambayo ni
sehemu ya mlima Kilimanjaro, na kwamba wao pia wamegawanyika katika sehemu kuu
mbili, Wapare wanaozungumza Kingweno, wanaoishi kaskazini na Wachasu waishio
Usangi, Kusini. Lugha zao zina aina fulani ya kulandana na zile za Wataveta na
Asu wa Kenya.
Enzi za kale Wapare
walisifika kwa uganga wa mvua na uhunzi. Uhakika kuwa kabila hili ni la kale ni
pale nilipowahi kuona kitabu kitakatifu cha Biblia iliyoandikwa kwa lugha ya
Kipare, kilichochapishwa mwaka 1910. Pamoja na ujio huo
wa dini za kisasa Wapare
waliendelea na tiba mbalimbali za asili kama maziwa ya Konda badala ya mama
kumtibu mtoto mwenye wintu, maradhi ya sangasi yaliyoharibu vinywa vya watoto,
majani yaliyoitwa more yaliyotibu ‘Kirumu,’ ‘kiruti’ au ‘kinyoka’, maradhi ya
macho kwa watoto wadogo.
Historia ya dini za
kigeni Upareni inaanza na mmisheni Jakob Janssen Dannholz, Mjerumani wa
madhehebu ya kiluteri ambaye mwaka 1908 alianzisha ‘kazi ya bwana’ huko Mbaga,
Upare ya kusini. Aliishi hapo hadi mwaka 1907 alipokamatwa na kuchukuliwa na
Waingereza kama mfungwa wa kivita hadi katika kambi yao ya Misri ambako
alifariki mwaka mmoja baadaye. Alifariki na umri wa miaka arobaini lakini kazi
aliyoianzisha iliishi, ikakua na inaendelea kukua hadi leo.
Kinyume na makabila
mengi nchini, wanawake wa Kipare walikuwa mstari wa mbele, pengine kuliko
wanaume zao, katika harakati za kupigania uhuru na haki zao. Kumbukumbu zangu
toka vitabuni zilinikumbusha mwaka 1946, kule Usangi, pale maelfu ya akina mama
walipoibuka na kuanzisha vurumai kubwa wakipinga kulipa kodi. Tukio hilo
liliibuka pale Chifu mmoja alipotembelewa na mkuu wa wilaya kwa ajili ya
majadiliano. Umati wa wanawake wapatao mia tano waliizingira nyumba hiyo kutaka
ufafanuzi juu ya utaratibu wa kodi ambao hawakuafikiana nao. Mkuu huyo
alipojaribu kuondoka bila kuwapa ufafanuzi walipandwa na hasira, walianzisha
nyimbo huku wengine wakiipiga mawe nyumba hiyo ya Chifu. Tukio hilo lilifuatiwa
na maelfu ya wanawake kujiunga katika vuguvugu hilo ambalo lilitikisa serikali
ya mkoloni.
Kama Wachaga, Wapare pia
walikuwa katika mstari wa
mbele katika kuiunga
mkono TAA na baadaye TANU katika mapambano ya kudai kujitawala. Hali hiyo
inachukuliwa kuwa ilisaidia kuondoka wazo la kuibuka kwa chama cha kikabila
ambacho kingeweza kuwa chini ya ‘PARE UNISI’ ambayo ilikuwa na nguvu nyingi
kutokana na mchango wa kiuchumi iliyotokana na kilimo cha mibuni, katani na
chai.
“Unasemaje?”
Mpare alinizindua.
Nikamtazama.
“Naona uko mbali sana,”
aliongeza. “Nilikuuliza unadhani tuondoke lini kwenda Arusha?”
“Nilikuambia sina
haraka, kwani hatuonani tena baada ya leo?” nikamuuliza.
“Tutaonana. Bila shaka
yoyote.”
Mara akina mama
walikwenda stendi kumpokea mwalimu wakaanza kurudi, mmoja baada ya mwingine.
Hawakuwa na furaha kama ile waliyoonyesha wakati wakinipokea mimi.
Hatukuchelewa kuelewa sababu.
Mwalimu Nyerere
hakutokea.
Mchaga aliyekuwa kimya
muda mwingi, akishughulikia kinywaji chake alitabasamu kidogo akinitazama.
Kisha akasema, “Maadam Nyerere hakuja, na wewe umefanana naye, tutaendelea
kukuita Nyerere. Unasemaje?”
Sikumbuki kama
nilimjibu.
SURA YA KUMI NANE?
Za Moshi?
oshi na Arusha ni miji
jirani sana, ikiwa imetenganishwa kwa umbali wa kilometa 75 tu na hivyo kufanya
safari toka mji huu hadi
ule iwe takriban dakika
sitini kwa gari lisilo na matatizo.
Safari ya Arusha na
Moshi ni burudani tupu. Japo barabara haikuwa nzuri sana, lakini kule kupita
katikati ya mashamba makubwa ya mibuni na migomba, vijiji vichache vikichomoza
hapa na pale ilikuwa burudani ya macho. Ilikuwa alfajiri moja tulivu na angavu
sana. Anga lilitakata pasi ya wingu lolote. Jua lililokuwa likichomoza
Mashariki liliufanya mlima Kilimanjaro ambao tuliupa kisogo usimame pale, taji
lake jeupe kichwani, juu ya kiwiliwili chake cha kijani, ukiwa umetuinamia kama
mzimu au malaika aliyekuwa akitutakia heri katika safari yetu. Sikuchoka
kugeuka mara kwa mara kuutazama uzuri huo wa pekee.
Hata kabla Kilimanjaro
haujatokomea nyuma yetu, ulijitokeza mlima mwingine mbele yetu. Kama
Kilimanjaro, ulisimama kando ya mji wa Arusha, kwa maringo na utukufu wa aina
yake. Japo mbele ya Kilimanjaro mlima huu ulikuwa kama mtu na mdogo wake, bado
utukufu wake ulikuwa palepale. Sikuhitaji kuambiwa kuwa huu ulikuwa mlima
Meru, fahari nyingine ya
Tanzania. Ukiwa umepanda juu ya usawa wa bahari kwa mita 4565 mlima huu
ulimwaga hewa safi yenye ubaridi mwanana uliopenya katika miili ya wakazi wa
Arusha na vitongoji vyake hadi kuitikisa mifupa ya wageni wa mandhari hiyo.
“Naona tayari umeanza
kumsahau mrembo mmoja umeanza kumtamani mrembo mwingine. Vipi, unafikiria
kumpanda?”
Nikazinduka na kumtazama
msemaji. Alikuwa rafiki yangu mpya, yule Mpare, ambaye toka tukio lile la mimi
kufananishwa na Nyerere na kumsimulia kwa ufupi maisha yangu ya maporini
aliniganda kama kupe. Siku zote tatu nilizokaa mjini Moshi alikuwa nami kama
kuku na vifaranga vyake. Sikupata kujiuliza nani alikuwa kuku nani kifaranga
kati yetu. Lakini ile tabia yake ya kuwa nami bega kwa bega, tukiachana wakati
wa kulala, nikiamka tayari ananisubiri, nilianza kupata hisia pamoja na yeye
kujifanya kuku ilielekea kuwa yeye ni kifaranga asiyetaka kumpoteza mama yake.
“Mrembo gani?....
Kumpanda nani?” nilimuuliza kwa mshangao.
“Mrembo Kilimanjaro,
dada mtu. Mara tu ulipomwona mdogo wake, Meru, tayari umehamishia mapenzi yako
kwake. Hilo liko wazi katika macho yako. Ukipenda tunaweza kufanya mipango
tuupande. Sio mrefu kama Kilimanjaro,” alijibu.
Niliyatafakari maneno
yake kwa muda. “Kama ningepata fursa hiyo ningeitumia kupanda mama wa milima
yote Afrika, mwenye sifa zote za pekee duniani, Kilimanjaro; ili nipate kitu
cha kuwasimulia wajukuu zangu pale nitakapozeeka,” nilimweleza.
“Wajukuu! Uliniambia
hujaoa.”
“Iko siku nitaoa.
Nitapata watoto na baadaye wajukuu,” nilimjibu, jibu ambalo lilifanya mada hiyo
iishie hapo.
* * *?
Arusha ilinisisimua kwa
mengi. Mji mdogo ndiyo, lakini ulikuwa na pilikapilika nyingi, wageni wengi.
Ukiwa mji wa mpakani, ukiwa umetenganishwa na Nairobi kwa kijiji mashuhuri cha
Namanga. Wageni wengi walioitembelea Arusha walikuwa wafanyabiashara, watalii
na wataalamu mbalimbali wakiwa katika pilikapilika hii na ile. Wahindi wachache
walikuwa na biashara zao lakini sehemu kubwa ya biashara ilishikwa na wenyeji,
Wachaga, Wapare na Waarusha wachache.
Wamasai walinisisimua
pia. Ingawa kiasili wao ndio wenyeji hasa wa mji huu lakini kama wanavyoishi
mbungani ndivyo walivyokuwa wakiishi hapa. Siku zote walionekana wageni wa mji,
wakifanya kazi yao nje kabisa ya mji ambako wao na ng’ombe wao walijiona huru
zaidi. Hata ujio wao mjini kwa mahitaji muhimu kama chumvi na vipande vya nguo
walivyozowea kuvaa, bado vaa yao, upande mmoja wa mwili ukiwa wazi, sime
kiunoni kana kwamba muda wote wako vitani huku kiswalhili na lugha nyingine
zinazotumiwa na wengi kikiwapiga chenga. Kuwepo kwao mjini kulifanya waonekane
kama watu waliopotea njia.
Mpare, wakati fulani
aliponiona ninavyowashangaa, alinisimulia kisa kimoja cha kuchekesha juu ya
Wamasai. Kwamba katika jitihada za kuwalazimisha kuvaa nguo za kisasa serikali
ilipata kutoa amri ya wauzaji wote wa maduka kutomuuzia kitu Mmasai ambaye
hakuvaa ama suruali ama kaptula ndani ya shuka lake.
Hatua hiyo iliwaudhi
sana Wamasai. Hata hivyo, ili wapate huduma hizo kijiji kilibuni mbinu ya
kununua kaptula moja ambayo kila aliyekuwa na shida mjini aliiazima. Kwa aibu,
kaptula hiyo ilivaliwa nje kabisa ya kijiji. Na baada ya manunuzi anaporejea
nyumbani Mmasai aliivua kaptula hiyo nje ya kijiji kabla ya kuirejesha.
Sikushangazwa kabisa na
habari hiyo, kwa jinsi nilivyowafahamu Wamasai.
Kama ilivyokuwa Moshi,
Mpare hakuwa Mpare wa kawaida Arusha vilevile. Hatukulala hotelini. Alinipeleka
kwa ndugu zake, maeneo ya Kaloleni ambako alinitambulisha kama rafiki yake
‘mpenzi.’
Alinitembeza maeneo
mbalimbali ya mji, Oljoro, Kijenge, Mianzini na kwingineko. Alinifikisha hadi
Namanga, Mpakani, ambako alijaribu kuomba ili turuhusiwe kuvuka mpaka na
kuikanyaga ardhi ya Kenya walau kwa dakika kumi, tukakataliwa. Wakati
tukirejea, kwa hasira zake za kukataliwa kuvuka mpaka aliamua kubadili uelekeo
wa safari yetu. “Twende zetu Ngurdoto, tuburudishe macho yetu,” alisema.
sana katika mbuga,
misitu mito na ziwani. Nimeona wanyama na ndege wengi sana. Lakini sikupata
kuona wanyama wa kuvutia kama tumbili weupe, lino wekundu, mbega na ndege wengi
kama niliowaona Ngurdoto. Niliwaona kereng’ende, kibeti, aina mbalimbali za
vibisi, kicheleko na wengine wengi ambao waliifanya Ngurdoto kuwa mahala pa
kusisimua.
Mandhari ya eneo hilo
pia ni kitu kingine cha kuvutia. Ikiwa karibu kabisa na mji wa Arusha, katikati
ya milima mikubwa maarufu ya Kilimanjaro na Meru Ngurdoto ilikuwa zawadi
nyingine ya asili kwa nchi na vizazi vyake.
Tulirejea mjini jioni
sana. Kwa ushauri wake tulikula chakula cha usiku hotelini. Tukashushia kwa
vinywaji. Yeye bia za moto, mie fanta mbili za baridi. Kama ilivyokuwa katika
mambo mengine, alisisitiza kulipia vinywaji na chakula hicho peke yake. Nikakataa
katakata na kulipia. Kisha nilimwambia, “Nadhani umefika muda wa kuzungumza ana
kwa ana kama wanaume wawili. Umekuwa mwema kwangu kwa muda mrefu. Umelazimisha
urafiki na udugu hadi nikaukubali. Niambie, unahitaji nini sasa kutoka kwangu?”
Mpare alitazama huko na
huko kuona kama tulikuwa katika faragha. Hakuridhika. Akanishauri tuhamie
katika kona ya baa hiyo iliyokuwa na meza mbili tatu zisizo na watu. Tukahama.
“Nataka tuwe marafiki,” alisema baada ya kuketi.
“Nadhani tumeshakuwa.”
“Nataka tuwe ndugu,” aliongeza.
“Nadhani tumeshakuwa,”
nilimjibu tena.
Alisita kwa muda kabla
hajasema, “Nataka tuwe wasiri. Kwa mwanamume udugu na urafiki havitoshi. Tuwe
kitu kimoja. Langu liwe lako, lako liwe langu. Tuafikiane hilo kwanza, kisha
tuchukue hatua ya pili.”
Nilimtazama kwa mshangao
uliochanganyika na mashaka. Alikuwa akizungumza kwa makini na msisitizo kuliko
ilivyokuwa kawaida yake.
“Hatua ya pili ni ipi?”
Nilimuuliza.
“Nataka tutafute pesa.
Nataka tuwe matajiri. Mimi nawewe,” alijibu mara moja.
“Kwani hatutafuti?”
Nilimuuliza.
Swali hilo lilimfanya
aangue kicheko. “Tunatafuta ndiyo. Lakini tunazotafuta ni fedha za kula tu,
fedha za kubadili mboga na mashati. Mwanamume anahitaji fedha zilizotakata.
Unaona maghorofa yake
yanayopanda?” aliuliza akinielekeza nje ya dirisha ambako jengo la ghorofa nne
lilikuwa likijengwa. “Lile linajengwa na binadamu kama mimi na wewe.?
Nataka miaka miwili
ijayo tuwe na majengo kama yale. Tuwe na magari ya maana. Tuweze hata kununua
ndege.”
Nikacheka.
“Usicheke. Hii sio
ndoto. Nyota yangu na yako zinafanana. Naona waziwazi mimi na wewe tukiogelea
katika bahari ya pesa. Tunajenga… tunalimisha mashamba makubwa… tunakwenda
kutembea Ulaya…”
Alizungumza huku
akitazama angani, macho kayakodoa kama anayekiona hicho anachozungumza.
Nilitamani kucheka tena, lakini kitu fuani kilinizuia. Kitu ambacho sikuweza
kukipambanua kati ya hofu na mashaka juu ya rafiki yangu huyo.
“Nitakusimulia hadithi
moja,” alisema ghafla. “Sio hadithi ya kupendeza sana, lakini itakufanya uelewe
kwa nini nahitaji fedha za maana. Yuko bwana mmoja,” alianza hadithi yake.
“Alizaliwa katika familia moja masikini sana. Kwa bahati mbaya sana, familia
hiyo ilizungukwa na familia yenye kipato kikubwa, familia ambazo zilisomesha
watoto wao nje ya nchi, zilijenga nyumba za maana na kushindana katika kubadili
magari na mavazi. Masikini na huyu na ndugu zake wote waliishia kuajiriwa
katika mashamba ya majirani hao ambao waliwanyanyasa na hata kuwapiga makofi hadharani.
Hali hiyo ilimfanya jamaa huyu asononeke na kukosa raha.”
“Siku moja bwana huyu
masikini alikuta baba yake akiwa amepiga magoti mbele ya mtoto wa tajiri yao
mmoja, huku akisihi na kubembeleza. Kisa? Masikini baba yake alikuwa amefukuzwa
kazi kwa kushindwa kufika kazini
jana yake kutokana na
maumivu ya mgongo. Baba alikuwa akijaribu kumsihi mtoto huyo wa tajiri abadili
uamuzi wake na kumruhusu kuendelea na kazi ya shamba. Kijana huyo hakukubali,
badala yake alimtukana kwa kila neno chafu alilolifahamu hata masikini mzee
akawa akitokwa na machozi.” “Ilikuwa picha ya kusikitisha sana kwa yule
kijana.?
Alimfuata baba yake na
kumwinua huku akimwambia, “Kufukuzwa kazi sio mwisho wa dunia. Nenda nyumbani
kapumzike,” kauli ambayo yule mtoto wa tajiri aliisikia.
Akageuka na kumwambia,
“Na wewe pia umefukuzwa kazi. Toka leo msikanyage katika mashamba yetu.”
“Masikini kijana yule
maisha yakawa magumu sana. Alikuwa ndio kwanza ameoa na kupata watoto wawili
mapacha. Alishindwa kuwalisha. Watoto wakapata utapiamlo na kufa mmoja baada ya
mwingine. Mama wa watoto alishindwa kuvumilia. Alilia kwa wiki mbili. Asubuhi
moja ya wiki ya tatu mama huyo alikutwa akining’inia kwenye paa la nyumba yao.
Alijinyonga kwa kamba ya katani.”
“Uchungu, aibu na hasira
vilimfanya baba huyo aondoke nyumbani na kwenda mjini kutafuta kazi. Hakuwa na
elimu ya kutosha, hakuwa na ndugu mwenye madaraka, hivyo suala la kazi likawa
ndoto. Masikini aliishia kuambulia vibarua vya hapa na pale, ambavyo
havikumsaidia sana. Wakati akihangaika huko mjini alipokea habari mbaya moja
baada ya nyingine. Mama yake alikuwa amefariki kwa malaria. Hakwenda, kwa aibu
ya kwenda mikono mitupu. Baba yake naye akafa. Hakwenda, kwa sababu zilezile.
Familia yao sasa ilibakiwa na watu watatu tu, bibi mzaa baba, kikongwe ambaye
kila usiku ulipoingia waliamini kuwa kesho asingeamka kutokana na malalamiko ya
maumivu ya miguu na mgongo
yaliyokuwa yakimsumbua.
Wengine walikuwa wadogo zake wawili, msichana aliyekuwa kiwete na mvulana
ambaye ndiye aliyekuwa akichangia kuleta walao vibaba vya unga vilivyowawezesha
kuvuta siku.”
“Yule bwana, masikini,
hadi leo anahangaika mijini akijaribu kushika ama hiki ama kile bila
mafanikio,” alimaliza hadithi yake na kunikazia macho.
“Hii ni hadithi ya
kweli,” baadaye alisema. “Na wahusika wake ni wa kweli. Mhusika mkuu ni mmi.”
“Wewe?” Niliuliza kwa
mshangao.
“Naam, mimi mwenyewe.
Na, kwa kweli, hicho ulichokisikia ni moja ya kumi tu ya mateso na aibu
zitokanazo na umasikini ambazo nimepata kukutana nayo. Kinachoitesa roho yangu
sana ni huyo bibi na wajukuu zake ambao wanaishi kwa kudra ya mwenyezi mungu.
Tatizo lolote linalohusiana na pesa linaweza kumfanya yeyote kati yao au wote
wapoteze maisha kama mende au kunguni mikononi mwa binadamu.”
Sikupata kujua kama
nilikuwa na huruma. Lakini nilipohisi machozi yakinilengalenga kwa simulizi
hiyo nilijua kuwa nimeshikwa na huruma. Akili ikahama na kunifanya niifikirie
familia yangu huko Buha. Pengine ina hali kama hiyo. Pengine haipo tena, wote
wamekufa kwa shida hii au ile! Chozi moja liliteleza ghafla na kulifikia shavu
langu. Nililifuta mara moja kwa kiwiko cha mkono na kisha kutoa leso yangu
ambayo haikutoka mkononi mwangu kwa muda mrefu.
Tulipigwa na kimya cha
muda mrefu, kimya ambacho Mpare alikiondoa pale aliposema baadaye, “Ninaposema
nimejaribu kila kitu maana yake ni kila kitu. Nimejaribu biashara lakini bila
mtaji ni biashara gani utafanya? Nimejaribu kutafuta kazi. Bila elimu utapata
kazi gani ya maana? Lilipokuja
vuguvugu la siasa na
kupigania uhuru nilikuwa mstari wa mbele kujiunga, kwa matarajio kuwa nitakuwa
mmoja wa wachache watakaowahi kula matunda ya uhuru. Lakini humo pia nimekata
tamaa. Elimu yangu ya ngumbaru, niliyoipata kwa taabu haikufua dafu mbele ya wenzangu
ambao tayari wamejipanga vizuri. Hata pale unapokuwa na wazo la maana bila
elimu au pesa kamwe hutasikia wala kusikilizwa.” Alisita kwa muda.
Alipozungumza tena ilikuwa kama aliyenisahau, na kuzungumza peke yake.
“Nimepoteza watoto niliowapenda. Nimempoteza mke niliyempenda. Nimepoteza
wazazi. Siwezi kupoteza tena nafasi ya kutajirika.”
Akanigeukia ghafla na
kusema, “Nitakuwa tajiri. Nitafuta aibu zangu zote. Wewe utanisaidia. Tutapaa
kama mlima Kilimanjaro. Wote waliokuwa wakitupuuza watainua nyuso zao
kutushuhudia.”
“Ulisema juu ya tatizo
la mtaji. Umeshaupata?” nilimuuliza.
Kwa mara ya kwanza
katika kipindi kirefu nilimwona akitabasamu. “Naam, mtaji ninao tayari,”
alijibu baadaye.
“Uko wapi?”
“Wewe ni mtaji.”
Alijibu.
“Mimi! Nilishangaa
“Unajua sijakuelewa?”
Akatabasamu tena kabla
hajasema, “Utanielewa. Ni rahisi sana. Kwa ujuzi wako wa mambo ya porini, kwa
uzoefu wako wa masuala ya mbugani na msimamo ambao nauona katika macho yako,
naamini tukishikana ni mtaji tosha.”
Bado sikumwelewa.
Akafafanua, “Tunahitaji
bunduki moja tu na risasi tano. Risasi moja ikilenga shabaha tayari
tumetajirika. Bunduki ninayo, risasi ninazo. Kitu gani kitanizuia?”
Bado sikuwa nimemwelewa.
Nikamtumbulia macho ya kumtaka ufafanuzi.
“Nadhani nizungumze kwa tuo.
Nisikilize kwa makini, tafadhali,” alisema akijiweka vizuri juu ya kiti na
kukivuta karibu yangu zaidi.
* * *?
Niliwapenda wanyama wa
porini. Niliwapenda sana. Kukuru, kakara, tumbili na nyani wakicheza juu ya
miti, mara waruke toka tawi hadi tawi au toka mti hadi mti, kwangu ilikuwa
burudani safi sana. Niliwahusudu chui, ngozi zao za madoa yanayopendeza na
mwendo wao wa maringo porini, pasi ya kishindo, kana kwamba wao ni malkia wa
nyika ni mambo ambayo yalinisisimua sana. Nilivutiwa na simba, wafalme wa
mwituni, kwa ubabe na jeuri yao hasa wale wa Serengeti ambao hupanda miti na
kupumzika juu yake kama chui. Niliwapenda twiga na shingo zao ndefu,
niliwapenda hata fisi wala mizoga. Kwa ujumla, niliwapenda wanyama wote.
Niliwapenda pia ndege,
tai mvumilivu ambaye anaweza kumfuata mnyama na hata binadamu mgonjwa kwa siku
kadhaa hadi atakapozidiwa na kukata roho ndipo humvamia na kumla, njiwa ambao
huburudisha kwa sauti zao nzuri, korongo na jamii zake zote, korongo mfuko
shingoni, korongo uso mwekundu na wengineo. Nilimpenda pia bundi na hadithi
zake zenye mapokeo anuwai.
Samaki wa majini, wadudu
wa ardhini pia ni viumbe niliowapenda. Kila mmoja ambaye ungemtazama kwa makini
na kufuatilia nyendo zake, kama unazo fikra usingekosa kujifunza jambo toka
kwao. Nyuki na malkia wao, ambao kwa umoja wao hujengwa himaya kubwa na
kutuwezesha kupata
asali. Mchwa ambao
pamoja na udogo wao hujenga vichunguu, kinyonga mwenye uwezo wa kubadili rangi
ya mwili wake kama anavyojisikia, jongoo menye miguu elfu moja na moja lakini
asiyeweza kukimbia, nyoka asiye na mguu hata mmoja, mwepesi wa kuteleza
maporini kama mshale.
Zaidi ya wanyama
niliyapenda mazingira yanayowawezesha kuishi: misitu murua yenye mimea na
vivuli wanavyohitaji, mito na mabwawa yanayowapatia maji na hifadhi kwa wale
waishio majini, mawe, milima na mabonde ambayo ni sehemu ya maisha yao na
kadhalika. Licha ya mazingira haya hifadhi ya wanyama bado ni kivutio muhimu
cha watalii, ambao kutembelea kwao nchini kuna maana ya kuleta pesa. Aidha,
mazingira ni urithi wa watoto na wajukuu wetu ambao wana haki ya kufaidi kama
tunavyofaidi sasa.
Niliwaza yote hayo
nikiwa chali kitandani, usingizi ukiwa umenikimbia usiku kucha. Ilikuwa baada
ya Mpare, ambaye jina lake halisi lillikuwa Daniel Mbonea.
Alikuwa ameibuka na wazo
la mradi wa hatari, unaoshawishi na kutisha pamoja, mpango wa kunitaka
tushirikiane katika uwindaji wa wanyama pori na kujipatia nyara ambazo
zingetupatia utajiri wa harakaharaka.
“Kila kitu katika
wanyama ni pesa,” alikuwa amesisitiza. “Ukimwua tembo pembe zake ni pesa.
Ukimwua chui na hata mamba ngozi zao ni pesa. Lakini tunayemtaka zaidi ni
kifaru. Ukiwaua wawili tu, umasikini kwa heri. Wako wengi huko mbungani. Lazima
tuwatafute.”
Wazo hilo sikupata
kulifikiria. Kwa kila namna lilinitisha, nikijua kuwa si kazi ya hatari kwa
maisha yetu tu, bali kwa vyovyote vile ni kinyume na sheria. Nilimkumbusha
hilo. Lakini Mpare alicheka tu, kisha akaniuliza, “Hivi unafahamu
hawa waliotajirika
wamefanya kazi gani?” Nikamjibu kuwa sijui.
“Huwezi kujua. Hutapata
kujua. Na wao hawatajua utajiri wetu umetoka wapi. Mwanamume anahitaji
kuthubutu. Hii ni nafasi yetu ya pekee.”
Nilikuwa na mengi ya
kufikiri. Awali ya yote lilikuwa lile pendekezo la akina Bibi Titi Mohamed la
kunitaka nirudi nyumbani nikaanzishe tawi la TANU ili kujiandaa kwa uhuru ambao
alisisitiza kuwa ‘umenukia.’ Kimsingi nilikuwa tayari nimeafikiana naye. Si kwa
ajili ya kwenda kufanya siasa pekee. Nia yangu kubwa ilikuwa kufika nyumbani
kwetu kuwajulia hali wazazi wangu. Akiba yangu ya pesa haikuwa ndogo. Ningeweza
kabisa kuwajengea nyumba bora zaidi, kuwanunulia mavazi mapya na kumpatia baba
baiskeli. Nilimwambia hivyo Mpare. Lakini alinicheka tena kabla ya kuniuliza,
“Baada ya kujenga hiyo nyumba?”
Sikumjibu haraka.
Akaamua kujibu kwa niaba yangu. “Baada ya nyumba utarudia kwenye umasikini
wako. Hutakuwa na kitu tena. Kwa maana hiyo ni kwamba huna kitu. Lazima
tutafute pesa zilizotakata. Achana na vijisenti ambavyo havitabadili maisha
yako.”
Ndipo nikamwomba aache
nilifikirie wazo lake hadi kesho, fikra ambazo zilifanya nipoteze usingizi wangu
kucha na kubakia nikitapatapa kitandani kuubembeleza.
Nilishawishika.
* * *?
Kuwinda sio lelemama.
Sio kuingia porini, kuona mnyama, kuelekeza bunduki na kuifyatua peke yake. Ni
zaidi ya hapo. Kuwinda kuna miiko na maadili yake. Mimi sikuwa
mwindaji. Lakini sehemu
kubwa ya maisha yangu nikiwa nimeitumia maporini nilikuwa nimeona mengi na
nimejifunza mengi, mengi tosha kunipa ujanja na maadili ya porini.
Kwa mfano, usiku mmoja
tukiwa katika barabara moja mbovu, ya mkato katika maeneo ya Makuyuni,
nilishangaa kuona njia imeziba ghafla. Nikasimamisha gari na kumuuliza mmoja wa
abiria wangu kuna nini mbele yetu. Aliangalia mara moja tu na kuniambia
“Tembo.”
Kumbe tembo mkubwa
alikuwa amesimama katikati ya njia akitutazama. Baada ya muda alianza
kutusogelea taratibu. Nikaweka gia ya kurudi nyuma na kuanza kurudisha gari taratibu.
Tembo alizidi kutusogelea. Kwa wasiwasi nilijikuta nimerudisha gari vibaya na
kuingia shimoni. Tembo aliendelea kuja taratibu. Mara nikamsikia abiria wangu
mwingine akiuliza kama kulikuwa na mtu mwenye kiberiti. Nilikuwa nacho.
Nikampa. Kwa mshangao wangu alishuka nje ya gari na kuwasha sigara. Moshi na
harufu ya sigara ulipeperushwa na upepo kuelekea aliko tembo, tulimwona
akisita. Kisha tembo yule aligeuka na kuondoka zake taratibu kama alivyokuwa
akija.
Tembo hapendi harufu ya
sigara.
Katika tukio jingine
niliwahi kulala ndani ya hema langu mapumzikoni, huko Ngorongoro. Nyakati za
alfajiri nilipata hisia kuwa mambo si shwari. Nikafungua macho kutazama nje.
Pazia la hema langu lilikuwa limefunguka. Simba wawili, dume na jike waliketi
pale mlangoni wakinitazama. Walipoyaona macho yangu waliinuka na kuondoka zao
polepole. Niliwatazama hadi walipotokomea porini.
Wanyamawanajuabinadamunidhaifu,hawamshambulii
bila sababu.
Nilimsimulia hayo
Mbonea. Hayo na mengine mengi. Nilimwambia kimaadili ni mwiko kumuua mnyama
mwenye mtoto au watoto.
“Hutakuwa umeua mnyama
mmoja tu, bali wengi. Baadhi ya wanyama wachanga huweza kutembea dakika tatu tu
baada ya kuzaliwa. Wanamhitaji mama kwa maziwa na ulinzi. Ukimwua mama umewaua
wao pia,” nilimfafanulia.
“Binadamu tunamwogopa
sana simba, pengine na chui,” nilimweleza. “Lakini wanyama wote ni hatari.
Nyati, kwa mfano, ni mnyama mwenye hasira na hila nyingi. Ukimpiga risasi
ukamwona ameanguka usije ukamsogela. Wakati mwingine hata ukiwa umemkosa au
kumjeruhi atajiangusha chali na kujifanya kafa. Ukimsogelea unakufa wewe. Kifo
cha nyati ni mpaka pale utakapoona amejikojolea.”
“Mkojo huo wa nyati
akiwa hai ni silaha kali sana.” Niliongeza. “Kama utakuwa umepambana na nyati
halafu unamkimbia na kupanda juu ya mti atakachofanya ni kuukojolea mkia wake
na kisha kurushia mkojo huko aliko. Mkojo wake unawasha sana. Ukikupata kwa
vyovyote utaachia mti na kuanguka chini, ambako utamkuta akikusubiri.
Atakusagasaga kwa miguu na pembe zake hadi ahakikishe umekufa.
Mpare Mbonea alishangaa.
Ilikuwa dhahiri kuwa hilo hakulijua.
“Tembo hata kama
hujampiga risasi, ukimwona kaanguka usimwogope. Tembo akianguka haamki, huwa
ndio mwisho wa maisha yake. Ndiyo maana tembo hata akilala hulala wima, ama kwa
kujiegemeza kwenye mti au kwa tembo wawili kuegemeana.”
Hilo pia Mbone
hakulijibu. Alizidi kuduwaa.
“Huyu tunayemwinda ni
mkali zaidi na wa hatari zaidi,” niliongeza. “Kwa bahati hana akili nyingi.
Kifaru ana nguvu nyingi sana na kasi ya ajabu. Akikuona unatishia maisha yake
atainama na kukujia kwa kasi, macho kayafumba, kwa lengo la kukuchoma lile pembe
lake. Ukiona hivyo ondoka haraka sana eneo hilo. Wawindaji wajanja hulipata
pembe lake kirahisi sana kwa njia hiyo. Wao husimama mbele ya mti mkubwa. Faru
anapokuja huondoka mara moja kwa hasira zake na hujikuta amechomeka pembe lake
katika shina la mti huo na kulididimiza. Katika jitihada za kuitoa mara nyingi
pembe hiyo hung’oka, kifaru hutokwa na damu nyingi na baadaye kukata roho.
Mwindaji hujipatia
hitaji lake kwa urahisi kabisa.” Mbonea alinisikiliza kwa makini sana, kana
kwamba nilikuwa nikimfundisha namna ya kuingia katika ufalme wa mbinguni.
Alinisikiliza. Lakini sina hakika kama alikuwa akinisikia, kwani mara alipopata
nafasi ya kwanza aliivunja kanuni ya kwanza kabisa ya uwindaji. Kitendo hicho
kiliniua kwa mara ya pili katika maisha yangu.
SURA YA KUMI NA TISA?
Pembe Za Faru?
W
anasema ‘za mwizi
arobaini’. Sisi hatukuzihitaji arobaini hizo. Siku ya tatu tu, toka tulipoanza
shughuli hizo, ilitosha kabisa
kututia hatiani.
Tukio hilo lilianza
hivi;
Baada ya kufika na
Mbonea, aliniacha Arusha na kwenda Kilimanjaro. Aliporejea jioni hiyohiyo,
akiwa na ‘vifaa’ vyake; viatu aina ya safari, suruali na shati la kaki, mfuko
wa ngozi na zaidi ya yote silaha. Alikuwa na bunduki kuukuu ambayo aliielezea
kama hazina yake pekee itakayomtoa katika lindi la umasikini. “Hii ndio baba,
ndio mama. Nina hakika haitaniangusha,” alisema wakati akiitoa katika mfuko
wake na kunikabidhi ili niikague.
Alfajiri ya siku
iliyofuata tuliuacha mji wa Arusha, tukiifuata barabara ya Dodoma. Tulivipita
vitongoji vya Ngarenaro, Sombetini na Majengo. Tukafika Kisongo na kuiacha njia
ya Monduli kulia hadi tulipofika Makuyuni. Hao tungeweza kuelekea kulia
vilevile na kufika Mto wa Mbu, Karatu na hatimaye Ngorongoro ambako nilitarajia
tuanzie shughuli zetu. Tulipita kwa chini na kuliona ziwa Manyara kwa mbali
kabla ya kuingia Magugu na hatimaye Babati.
Mbonea alisisitiza sana
juu ya kuwatafuta vifaru kabla ya wanyama wengine. “Pembe zao ni almasi!”
“Zinatafutwa sehemu mbalimbali za dunia.” Tukiipata walao moja tu….”
Nilitamani kucheka.
Kwangu mimi kifaru ni mnyama mwenye sura mbaya na umbile lisilovutia kuliko
wanyama wengine wote. Alivyokuwa na bahati mbaya zaidi pembe zake hizo kubwa na
ndogo, zinazodaiwa kuwa za thamani zimeota juu ya pua, katikati ya uso wake.
Wataalamu wanasema pembe hiyo ni mkusanyiko wa aina fulani ya nywele, zinazoota
toka kwenye fuvu lake la kichwa jambo ambalo hupelekea kupoteza pembe hizo
apoteze pia uhai wake.
Mbonea alinisikiliza kwa
shahuku. Lakini nilihisi shahuku yake kubwa ilikuwa ni kumwona kifaru na
kumpiga risasi, si vinginevyo.
* * *?
Kifaru anaweza kuishi kati
ya miaka 35 hadi 40, umri ambao humwezesha kufikia uzito wa tani moja na nusu
hadi mbili. Pamoja na uzito huo anaposhambuliwa hukimbia kwa kasi kati ya
kilomita arobaini na tano au hamsini kwa saa. Kifaru hana makuu. Pamoja na
machachari yake yote chakula chake pekee ni majani, hata yale yenye miiba. Si
msumbufu, kwani muda mwingi wa mchana hupenda kujipumzisha kando ya mito au
mabwawa. Hali hiyo hufanya kazi ya kumwinda isiwe ngumu kama inavyotarajiwa.
Imani ya muda mrefu juu
ya pembe zake hizo, kuwa hutengeneza dawa fulanifulani muhimu kwa binadamu
pamoja na mapambo murua ni sababu iliyofanya aanze kuadimika sana duniani.
Ukweli huo niliufahamu fika kupitia matangazo ya watetezi wa wanyama katika
vyombo vya habari. Na hivyo
ikawa sababu mojawapo
iliyonifanya kushiriki katika jukumu hili huku roho ikinisuta.
Lakini pindi maji
ukishayavulia nguo huna budi kuyaoga. Sikuona kama ingekuwa uugwana kubadili
uamuzi, hasa nikiwa tayari humo porini. Nilimwelekeza Mbonea maeneo yote ambayo
yalikuwa na sifa za kuishi vifaru. Nilimkumbusha mara kwa mara kuwa makini.
“Macho ya kifaru ni dhaifu kidogo kuona mchana. Lakini pua zake ni makini sana.
Akipata harufu yako kabla hujamwona na akishuku kuwa una nia mbaya ujue kuwa
utakufa wewe badala yake,” nilimwambia.
Nikaongeza, “Lakini
kifaru si wa kuogopa zaidi. Yupo askari wake. Huyu ni ndege ambaye muda wote
hukaa juu ya miili ya vifaru akidonoa wadudu wanaomsumbua. Wakati mwingine hata
pale kifaru anapokuwa na jeraha ndege hawa huliongeza kwa kulidonoadonoa.
Kifaru humvumilia. Pengine analazimika kumvumilia kwa kuwa hana la kufanya.
Ndege huyo huona mbali sana na humshtua kifaru kwa mlio wake mara anapohisi
dalili za hatari kwa bosi wake.”
Wataalamu wanakubaliana
kuwa Ngorongoro ni moja ya miujiza kadhaa ya dunia. Wanaikadiria kuwa ni
mwujiza wa nane duniani. Miujiza mingine ikiwa pamoja na ile ya yale majengo
yaliyopo Misri. Piramidi, ambayo yalijengwa miaka ipatayo 4700 iliyopita lakini
yangali hai hadi leo. Mojawapo ambayo yametumia mawe na miamba yenye uzio wa
tani moja hadi mbili kila moja na kupaa juu urefu wa meta 140. Ikizingatiwa
kuwa wakati huo hakukuwa na vifaa maalumu vya ujenzi kama leo, majengo hayo
yaliyoandaliwa kama hifadhi ya miili ya farao yanamshangaza kila mtu
anayeyaona. Sanamu ya mmoja wa miungu ya wagiriki, Zeus, akiwa amekaa juu ya
kiti chake cha enzi, chenye ukubwa wa meta 12, ikiwa
imeundwa kwa meno ya
tembo na kupambwa aina mbalimbali za madini ni mwujiza mwingine wa dunia.
Muujiza wa Ngorongoro
unatokana na maumbile yake. Wakati eneo hili ambalo limo katika Bonde la Ufa
linakadiriwa kuwa na ukubwa wa kilometa za mraba 8,300 zenye wanyama pori
wapatao 300,0000 ndani ya eneo hilo kuna kilometa za mraba zipatazo 250 za
kushangaza ziadi. Eneo hili, katika mabadiliko mbalimbali ya maumbile ya dunia
lilididimia kwa kiasi cha meta 600 toka usawa wa ardhi. Humo ni shamba pekee la
wanyama. Zaidi ya wanyama wapatao 20,000 wakiwemo vifaru weusi, nyati ,
pundamilia, tembo, fisi na wanyama wengine tele. Wamo pia ndege anuai na
wadudu.
Ikiwa kama bustani ya
aina yake, eneo hilo lenye maji tele, lishe ya kutosha na mazingira ya kuvutia
limefanywa na wanyama hao kama makazi yao ya kudumu ingawa wanao uwezo wa
kutoka na kuingia.
Kama ambavyo eneo hili
humshangaza kila binadamu anayeliona kwa mara ya kwanza ndivyo lilivyomshangaza
rafiki yangu Mbonea. Nilihisi kuona kitu kama machozi yakimlengalenga katika
macho yake na dalili za udenda kumtoka pale tulipoingia na kuwaona wanyama
mbalimbali wakiendelea na shughuli zao bila ya kututilia maanani. Twiga mmoja
aliyekuwa akinyonyesha aligeuka kutuangalia kidogo kisha akaendelea kula juu ya
kilele cha mti. Swala mmoja alikurupuka toka kichakani na kukimbia hatua kadhaa
kabla hajasimama, kututazama kwa muda kabla na kisha kutokomea tena vichakani.
Kwa mbali sana, tuliweza kuona kundi kubwa la nyati likipunga upepo huku vitoto
yao vikiruka huku na huko katika michezo yao ya kawaida.
Mbonea alizidi
kushangaa. Alishindwa kustahimili,
chozi likamdondoka.
Alijaribu kulifuta harakaharaka, lakini haikuwa kabla ya kuliona, jambo
lililofanya niangue kicheko. “Tunawatafuta faru,” nilimkubusha. “Sio kitoweo.
Kwa hiyo, punguza papara.”
Tulizurura maporini humo
kwa siku nzima. Tulipita katika mito ya layara, oljiro na Mungo. Tulipita
kandokando mwa ziwa Makkat na katika bwawa la Mandus. Tuliingia hata katika
msitu wa Lerai. Tuliwaona wanyama wengi sana isipokuwa yule tuliyemwitaji,
kifaru. Ilikuwa siku mbaya.
Siku ya pili ilianza kwa
namna ya pekee. Ilikuwa angavu sana na hata hali ya hewa haikuwa ya ubaridi
mkali. Tulifuata barabara ya Lemaka iliyotupeleka tena kwenye ziwa Makkat
ambako tulikuwa tumeona dalili za wanyama hao vikiwemo kinyesi na nyayo. Wakati
tukiwa umbali wa kilometa moja toka ziwani hapa nilisikia milio ya ndege,
askari wa vifaru ikitokea vichakani. Kisha niliwaona ndege hao wakiruka angani
na kutokomea.
“Wapo,” nilimwambia
Mbonea. “Kwa bahati mbaya, wameshapata hisia za hatari. Lazima tuwe waangalifu
sana,” nilimsisitizia. Hata hivyo, nilikuwa na mshangao kidogo. Ndege hao
walikuwa wametuona sisi kweli au hatari nyingine? Maana tulikuwa mbali na pale
walipotokea.
Tulitembea kwa hadhari
kuelekea huko, mitutu ya bunduki zetu ikiwa imeelekezwa mbele, tayari
kufyatuliwa iwapo lingetokea lolote lile. Tulipofika pwani ya ziwa tuliambaa
nayo kuelekea upande wa kulia walikorukia ndege. Hata kabla hatujapiga hatua
ishirini tulimwona kifaru mmoja akiwa amesimama katika hali ya tahadhari
akiangalia tunakotokea. Alikuwa na mtoto, kifaru mdogo ambaye alisimama
katikati ya miguu ya mtoto wake.
Mara nikamwona Mbonea
akipiga goti chini na kulenga shabaha. “Usimwue… ananyonyesha…” nilijaribu
kumwambia. Sauti yangu ikimezwa na mlio mkubwa wa ghafla kutoka kwenye bunduki
yake. Alikuwa na shabaha ya pekee. Risasi ilipenya katika paji la uso la kifaru
huyo bila kuharibu pembe zake. Kifaru alitapatapa kwa muda akipigania roho yake
kabla hajaanguka chini. Risasi ya pili, iliyomwingia tumboni ilimfanya akate
roho palepale.
“Umefanya nini?”
nilimuuliza kwa ukali. “Nilikuonya mapema kuwa mnyama anayenyonyesha! Kinda
yule atafanya nini peke yake katika mazingira haya?”
Mbonea alikuwa
akitabasamu, tabasamu pana ambalo sikupata kuliona huko mbeleni katika uso
wake. Badala ya kunijibu nilimsikia akisema, “Mmoja tayari! Bado wawili tu
tumekuwa matajiri!”
Nilikuwa nimekasirika
kiasi kwamba nilitamani kumlenga bunduki yangu na kuifyatua. Majuzi tu alikuwa
akilalamika watoto wake pacha waliopoteza maisha kwa utapiamlo leo anaacha
mtoto wa faru apoteze maisha kwa njaa, baridi au kukosa kiongozi wa kumsaidia
mbinu za kuishi porini.
Mbonea alijua
nimekasirika. Hakujua kama alinikasirisha zaidi pale aliposema “Toto la kifaru
litakufaa nini rafiki yangu. Hata pembe halina. Achana nalo, tushughulikie mali
yetu.”
Wakati huo ‘toto’ hilo
la kifaru lilikuwa limehisi kuwepo kwa jambo baya lililomtokea mama yake.
Lilionyesha kushangazwa na damu. Likamzunguka mama yake mara tatu na kujaribu
kumtikisa kabla halijaanza kulia kwa sauti yake mbaya, sauti ambayo masikioni
mwangu ilitia huzuni kubwa.
Sijui nini ambacho
kingefuata baina yangu na rafiki yangu Mpare kama jambo jingine, kubwa zaidi,
lisingetokea. Tulijikuta ghafla tumezingirwa na kundi la askari wa wanyama pori
wasiopungua sita, kila mmoja akiwa na bunduki mkononi. Na kila bunduki ikiwa
imetuelekea.
“Tueni bunduki zenu
chini na muweke mikono yenu juu mara moja!” mmoja wao alitoa amri.
Tulitazamana na Mbonea
kwa mshangao. Hatukuwa na namna yoyote ya kupambana nao wala kukimbia.
Tukaziangusha bunduki na kuweka mikono yetu juu ya vichwa.
“Washenzi wakubwa nyie,”
askari yule aliendelea kufoka. “Tumemlinda kifaru huyu kwa miaka nyie mnamuua
kama mchezo. Mtakuwa mfano mzuri sana kwa jamii. Kama hamjafungwa maisha, miaka
ishirini kwa kila mmoja wenu haitamkosa.”
Walizichukua bunduki
zetu. Wakatutia pingu za mikono kisha tukaanza kusukumwa kuelekea walikoificha
gari yao. Tukatupwa ndani ya gari, ikatiwa moto na kuelekezwa mjini Ngorongoro
ambako tulifungiwa katika kijichumba kidogo kwa siku tatu kabla ya kupelekwa
Arusha. Tulifunguliwa mashataka.
* * *?
Kabla ya kesi yetu
kuanza kusikilizwa tulikaa rumande kwa wiki tatu nzima, tukiwa tumewekwa katika
chumba cha watu hatari sana. Chumba hicho kilijumuisha watu watatu wa kesi za
mauaji, watu watano wanaotuhumiwa kwa kujaribu kuvunja benki kwa nia ya kuiba,
mmoja aliyekamatwa akimnajisi ng’ombe na wengine tele wenye tuhuma hii au ile.
Mmoja kati ya watuhumiwa
hao nadhani alikuwa kichaa. Siku zote , wakati wote, alikuwa mtu wa kupiga
kelele. Na kauli yake ilikuwa moja tu; ‘Nitaua mtu. Kama si leo kesho!’ Kauli
hiyo ilinitisha sana kwani sikujua alikusudia kumwua nani. Hakimu anayesikiliza
kesi yake, askari aliyemkamata au yeyote kati yetu mahabusu wenzake. Macho yake
yalikuwa yanatisha, sura yake ikitangaza shari kama shetani mwenyewe. Kwa kweli
alininyima raha na kufanya nijitahidi kila ilivyowezekana kumkalia mbali.
Hiyo ndiyo jumuiya mpya
niliyojiunga nayo, jumuiya ya wahalifu, jumuiya ya waasi wa sheria. Mimi, Petro
Mtukwao Kionambali Kalimanzira tayari nilikuwa mmoja wao. Machoni mwa jamii
nilikuwa mtu duni, asiyefaa kuishi uraiani bali gerezani kusubiri hukumu
kamili.
Ilinisikitisha zaidi
pale watuhumiwa hao walipotupokea kwa furaha kana kwamba sisi ni mashujaa.
“Jengo hili limejengwa kwa ajili ya wanaume kama nyie,” mmoja wao alisema.
“Bila nyie, polisi na mahakimu wangekufa njaa, kwani hakuna mtu ambaye
angekubali kuwalipa mishahara bure!”
Sikumwelewa.
Wala hakunijali.
Aliendelea na mawaidha yake ya kishetani, “Wanaletwa hapa watu kwa makosa ya
kitoto kabisa. Eti jitu zima limepiga hadi kumwua mkewe au mwanawe. Eti jitu na
akili zake limeiba kuku wa jirani. Nyie wanaume bwana! Kuingia msituni,
kupambana na wanyama hatari kama faru ili mpate zile pembe zake ni uanaume.
Kukamatwa kwenu ni ajali kazini tu. Kama msingeshikwa mngekuwa matajiri wakubwa
kutoka nchi hii.”
Hiyo ndiyo jela! Hakuna
siri! Toka siku ya kwanza tulipoingia tayari tulikuwa gumzo. Kila mmoja
alionyesha dalili
ya kutupongeza! Laiti
wangejua nilivyokuwa najisikia moyoni! Nilikuwa taabani kwa aibu na kukosa
raha. Sikutegemea kamwe maishani nifanye kitendo chochote, ama kwa makusudi ama
kwa bahati mbaya, ambacho kingeniweka upande wa pili wa sheria. Nilikuwa na
nilitegemea kuwa mtu mwaminifu na mwadilifu katika uhai wangu wote. Nilijuta
kukutana na Mbonea. Nilijuta zaidi kumsikiliza. Nilitamani kumchukia maisha
yangu yote. Nilitamani kumwambia hayo.
Hata hivyo, Mbonea
hakuwa katika hali ya kuambiwa hayo. Toka tulipokamatwa muda wote alikuwa mtu
wa kutokwa machozi. Mara nyingi, kwa sauti inayotetemeka, nilimsikia
akinong’ona, “Bibi yangu kikongwe atafanya nini jamani… dada yangu kiwete
ataishi vipi…” alisema huku akifuta machozi. Kwa muda huo mfupi Mbonea tayari
alikuwa amekonda na kupungua uzito kwa zaidi ya kilo kumi. Hakupata usingizi.
Alikula kwa shida baada ya ushawishi mwingi. Ndiyo, ni yeye aliyeniingiza
katika mkasa huo. Lakini kwa jinsi alivyokuwa akitia huruma nilijikuta
nikimhurumia kuliko hata nilivyojihurumia mimi.
Mbonea alikuwa na ndugu
wengi. Alitembelewa na watu mara kwa mara na kujadiliana nao hili na lile.
Nilishangaa alivyokuwa haonyeshi nia ya kunishirikisha katika maongezi hayo,
ambayo nilitarajia yangelenga katika kutafuta ufumbuzi wa tatizo letu. Sikuwa
na la kufanya. Nikabakia na uyatima wangu nikiyaweka yote mikononi mwa Muumba.
Kabla ya kupelekwa
mahakamani, tulihojiwa na watu mbalimbali, polisi, wanasheria na hata
watuhumiwa wenzetu. Kila mmoja alikuwa na ushauri wake kwetu. Polisi na
wanasheria wa serikali walinishauri kukiri kosa ili kupunguza uzito wa adhabu.
Wanasheria wengine walinishauri kukataa
katakata kuhusika na
suala hilo. Watuhumiwa na wenye uzoefu wa masuala ya kesi pia walinionya juu ya
athari za kukubali kosa kubwa kama lile. Hali iliyofanya nijione kuwa
nachangwanywa akili.
Tatizo jingine lilikuwa
mshitakiwa mwenzangu. Kila nilipomtaka tukae na kuweka mkakati wa pamoja
alikuwa akiishia kulia tu. Hatukupata hata mara moja kukaa na kuzungumza lolote
kwa tuo. Mbaya zaidi ni pale ambapo tulikuwa tukihojiwa na hata kuandika
maelezo kila mmoja kwa wakati wake. Sikujua amejieleza vipi na kuandikisha
lipi, kama ambavyo niliamini yeye hakujua nilichoeleza.
Hatimaye, siku ya siku
ikafika. Tulichukuliwa na lori la polisi toka gereza la Kilimwanga,
tulilokuwemo na kupelekwa mahakamani mjini Arusha. “Pilato” alikuwa mzungu, mtu
mfupi; mwembamba mwenye sura ya kitoto. Isipokuwa kwa miwani mizito na joho
alilovaa isingekuwa rahisi kumfananisha na hakimu. Nilikuwa nimepata sifa
nyingi za hakimu huko gerezani. Nusu ya wafungwa wote ni yeye aliyewahukumu.
Nilikwishaambiwa mapema kuwa kama tungemkuta hakimu huyo, ambaye gerezani
walimwita “Fisi maji” kwa ukali wake, gereza lisingeweza kutuepuka. Ajabu ni
kwamba kwa sura hakuonekana katili kama alivyoelezewa.
Siku hiyo mahakama
ilikuwa na kesi nyingi, kubwa na ndogo. Lakini nadhani kesi yetu ndiyo
iliyomvutia zaidi maana niliona kesi nyingi akiziendesha harakaharaka. Zingine
alizihairisha na nyingi alizitolea hukumu bila umakini mkubwa, huku mara kwa
mara akitupa jicho upande wetu kama anayetusubiri kwa hamu.
Saa na hatimaye dakika
ikawadia. Tukiitwa kwa majina, mmoja baada ya mwingine na kusimamishwa
kizimbani. Mimi
nikitetemeka kidogo,
mwenzangu akitetemeka na kupepesuka kama jani la mwembe.
Hakimu alivua miwani na
kututazama kwa takribani dakika nzima, kabla hajaivaa tena na kusoma jalada la
tuhuma zetu lililokuwa mbele yetu. “Petro Mtukwao Kionambali… Daniel Mbonea
mnashtakiwa kwa kuingia katika hifadhi ya taifa ya Ngorongoro kwa makusudi ya
kufanya vitendo vya uharamia. Kosa la pili, kwa makusudi vilevile mlimuua
mnyama aitwaye kifaru kwa kumpiga huku mkijua fika kuwa kifaru huyo ni mmoja wa
wale wanaolindwa na serikali kwa gharama kubwa ili kuifadhi viumbe hao walio
hatarini kutoweka. Aidha, kosa lenu la tatu ni kumwua kifaru huyo huku mkijua
na kuona wazi kuwa alikuwa na mtoto mchanga ambaye alimtegemea. Kwa maana hiyo
mmehatarisha maisha ya kichanga huyo pia.” Hakimu alivua tena miwani yake na
kunikazia macho,?
“Petro Mtukwao
Kionambali… ni kweli au si kweli?”
Nikageuka kumtazama
mwenzangu. Alikuwa akinitazama pia, ingawa macho yake yalijaa machozi. Kwa
namna fulani alikuwa kama anayenisihi jambo fulani. Sikujua ni jambo lipi.
Nikainuka na kumtazama hakimu. “Ni kweli Mheshimiwa,” nilijibu.
Nilipata hisia kuwa kila
mtu katika chumba hicho cha mahakama, ikiwa pamoja na hakimu mwenyewe, alipigwa
na butwaa. Hakimu aliinama, akaandika jambo katika faili lake, kisha akainua
tena miwani na kumkazia macho Mbonea. “Daniel Mbonea, mashtaka haya ni kweli au
si kweli?”
“Sio kweli, Mheshimiwa,”
Mbonea alijibu kwa sauti iliyokuwa na uhakika kinyume na hali yake.
Hakimu aliandika jambo.
Akainua tena uso wake na kututazama kwa zamu kabla hajauliza, “Nataka kufahamu
kitu kimoja. Kati yenu
nani aliyefyatua bunduki, ambayo risasi yake ilimuua kifaru yule?”
Tulitazamana tena na
Mbonea. Alikuwa amebadilika tena. Anatetemeka na anapepesuka nusura aanguke
chini. Macho yake yalijaa huruma na simanzi. Niliweza kuyasoma mawazo yake
katika macho yake hayo; bibi yangu kikongwe atafanya nini jamani… dada yangu
kiwete ataishi vipi… ujumbe ambao ulinifikia bila sauti. Ukanitia huruma. Bila
kujua nilifanyalo, niliinua tena mkono wangu na kumjibu hakimu, “Ni mimi
Mheshimiwa.”
Nilisikia sauti za kitu
kama, “Ah!” zikiwatoka watu wawili watatu chumbani humo. Wengi wao walinikazia
macho ya mshangao na kutoyaamini masikio yao. Hata hakimu alionekana kutoamini
kile alichokisikia. Akaandika alichokuwa akikiandika. Kisha aliahirisha kesi
kwa kupanga tarehe ya hukumu.
Tukarudishwa mahabusu.
Huko nilikuwa gumzo kubwa. Kila mtu aliyesikia kilichotokea mahakamani alitaka
kuniona kwa macho na kuisikia sauti yangu.
“Pole sana, mdogo
wangu,” mzee mmoja aliyekaa rumande kwa miaka tisa sasa aliniambia. “Hivi
hujaambiwa kuwa hata kukubali kosa ni kosa? Maana yake ni kwamba ulifanya kosa
huku ukijua kuwa unafanya kosa. Adhabu yake ni kubwa sana. Humu, wewe anza
kutafuta kona yako ambapo utalala kwa miaka ishirini. Halafu huonekani kama mtu
wa kumudu chawa, kunguni na chakula cha ajabu kinachotolewa.” Nadhani nilikuwa
nimechanganyikiwa kwani haikuniingia akilini uzito wa mkasa uliokuwa mbele
yangu hadi siku ya hukumu. Hakimu, akiwa mkali kama pilipili, alitumia zaidi ya
dakika arobaini kuelezea athari za ujangili?
kwa wanyamapori hasa
wale adimu kama faru. Alitoa mifano ya nchi mbalimbali za dunia ambazo zimeweka
sheria kwa ajili ya kuwalinda wanyama ambao wanazidi kutoweka siku baada ya
siku.
“Tumeirithi nchi hii
ikiwa na mazingira murua, wanyama na ndege tele. Tumerithi hayo kwa kuwa babu
zetu hawakuwa waharibifu wala katili kwa wanyama. Tunahitaji watoto na wajukuu
zetu nao warithi hali ile tuliyoikuta. Kwa bahati mbaya baadhi yetu wametia pamba
masikioni mwao. Wanapuuza jitihada zote za serikali na dunia kwa matarajio ya
maslahi yao binafsi. Hawa lazima wawe mfano kwa wengine kwa kupewa adhabu
kali,” hakimu alisema.
“Kesi iliyo mbele yangu
inamhusu Petro Mtukwao Kionambali na Daniel Mbonea. Hawa walikamatwa na askari
wa wanyamapori waliokuwa wakitelekeza jukumu lao la kumlinda kifaru huyu mwenye
mtoto. Kwa ukatili mkubwa walimpiga risasi na kumwua.”
“Katika maelezo yao hapa
mahakamani na hata yale ya awali, Mbonea alikataa kuhusika na mauji haya.
Anasema kuwa alimtembelea rafiki yake huyo mbugani baada ya kufahamiana naye
mjini Moshi na Arusha bila kujua kuwa kazi yake ni uwindaji wa vifaru. Kuwa
kifaru yule mwenye mtoto alipotokea alimwona akiandaa bunduki na kutaka kumwua.
Alimtahadharisha lakini Kionambali hakumsikiliza. Alifyatua risasi na kumwua
kifaru yule. Kwa upande wake Kionambali mwenyewe katika maandishi na maelezo ya
ana kwa ana mahakamani amekiri yote yaliyotokea. Hivyo, mahakama inamwachia
huru Daniel Mbonea. Aidha, inamuhukumu Petro Mtukwao kifungo cha kwenda jela
miaka ishirini na kazi ngumu na viboko kumi, ili awe mfano kwa wengine.”
Sikuelewa. Nilimwona
Mbonea akibebwa juujuu na ndugu zake huku wakishangilia. Mimi nilitiwa pingu,
nikasukumwa kuelekea kwenye gari la magereza ambako nilipandishwa na kurejeshwa
Kilimanga ambako nilivuliwa mavazi ya uraiani na kuvishwa yale ya gereza yenye
namba na tarehe yangu ya kufunguliwa. Niliondolewa katika chumba cha mahabusu
na kuelekezwa katika selo nyingine ambayo ingekuwa makazi yangu hadi mwisho wa
kifungo changu. Kama ile ya mahabusu hii pia haikuwa na kitanda wala godoro.
Nilipewa blanketi kuukuu na kuelekezwa mahala pa kulala. Juu ya sakafu ngumu.
Kona moja ilikuwa na kijichumba kidogo chenye harufu kali ambacho kilitumiwa
kama choo na bafu. Mlikuwa na bomba lakini halikupata kutoa walao tone moja la
maji!
Nilitoka nje na kuketi
mahala fulani nikiwa nimejiinamia. “Pole sana,” nilisikia sauti ikiniambia.
Nikatazama. Alikuwa yule mzee wa miaka tisa mahabusu. “Nilikuuliza kama
unamwamini mshtakiwa mwenzako hukupata kunijibu,” alisema na kuendelea, “Yule
kakuuza rafiki yangu. Kesi yenu ilikuwa mbaya sana. Ilikuwa lazima mtu afungwe.
Amekuchezea akili umefungwa wewe, yeye ametoka.”
“Kwa vipi?” niliuliza
“Mbona mtu mwenyewe alikuwa mtu wa kulialia muda wote?”
“Kulia!” mzee alisema
akicheka. “Kama alikuwa analia kweli basi yalikuwa machozi ya mamba. Alikuwa
akikuchota akili huku akikucheka. Kwa bahati mbaya, wewe ulishiriki
kumrahisishia azma yake kwa kukiri hili na lile. Hilo limemfanya atoke haraka
kuliko alivyotegemea.”
Machozi ya mamba!
Niliwaza kwa mshangao.
?
20
Ben R. Mtobwa
SURA ISHIRINI?
miaka ishirini
M
fikiriemtotomdogosanawakiume,
aliyeondoka kwao zamani sana kuiokoa roho yake, mtoto ambaye alifuatana na babu
yake, wakavuka
misitu na nyika, milima
na mabonde, mito na mabwawa hadi nchi ya mbali. Huko mtoto aliona nuru mpya
elimu. Akaanza kusoma huku akiwa na matumaini.
Mtoto huyu, ambaye kwa
miaka nenda miaka rudi alikuwa hajazitia machoni sura za wazazi wake wapenzi,
wala kuonana na babu yake kipenzi, majuzi tu alikwishafikia uamuzi wa kurejea
nyumbani. Na alitarajia kupokelewa kishujaa kwani akiba yake benki ilikuwa ya
kuridhisha. Angeweza kujenga nyumba ya kisasa na kutoa zawadi nyingine tele
ambazo zingefanya ukoo mzima umshangilie. Lakini, kwa mara nyingine tena
likatokea jambo jingine, kubwa kuliko yote yaliyopata kutokea. Na sasa yuko
kifungoni. Hategemei kutoka kabla ya miaka ishirini! Hategemei kuwakuta wazazi
wake wakiwa hai! Yeye mwenyewe hategemei kutoka akiwa hai!
Mtoto huyo ni mimi,
Petro Mtukwao Kionambali. Tayari miezi miwili ilikuwa imepita toka nianze
kutumikia kifungo. Miezi miwili! Ilibakia miezi isiyopungua mia mbili
thelathini na nane, nikiwa ndani ya chumba hiki kinachonuka, nikilala juu
ya sakafu hili gumu na
kula chakula chao kisikolika! Mara kwa mara wafungwa wenzangu walinishauri
nijitahidi kuyazoea maisha ya jela, lakini yalikuwa hayazoeleki. Binadamu gani
atazoea kula mlo mmoja, tena usioridhisha, kwa siku? Binadamu gani atazoea kula
saa kumi na moja jioni, katika chumba kisicho na madirisha na kutoipata tena
hewa ya nje hadi kesho yake?
Niliteseka sana
kialikili zaidi ya kimwili. Nilitafakari kwa nguvu zangu zote na kushindwa
kabisa kutambua kitu gani kinafanya siku zote niwe kondoo wa kafara. Sikuweza
kuelewa kwa nini nilikwenda Kilimanjaro na kukutana na ‘Mpare’ Daniel Mbonea.
Sikuweza kuelewa kwa nini nilikubali kushawishika hata nikafuata ushauri wake
na kuahirisha dhamira yangu ya kurejea nyumbani Buha na badala yake kuingia
naye porini kuwinda nyara za serikali. Zaidi sikuweza kuelewa kabisa sababu
iliyofanya nijisikie kumhurumia kiasi cha kumlinda kwa kujitoa kuwa ni mimi
niliyefyatua risasi ya kumwua kifaru kutokana na madai yake ya kutegemewa na
bibi kizee na dada kiwete? Mie pia si nilikuwa na babu kizee na ndugu vilema
wengi tu ambao walinitegemea. Machozi yake ya mara kwa mara? Mie pia ningeweza
kutokwa na machozi siku nzima kama ningependa. Kwa kweli sikuweza kabisa
kuelewa sababu.
Hisia za siku nyingi,
ambazo nilianza kuzisahau zilinirejea. Hirizi iliyopotea! Nilianza kueleka
kuamini kuwa chanzo cha balaa na mikosi yangu ni kuipoteza hirizi ile ambayo
babu alinihusia kuitunza. Una alama… alama ya shari... Niliyakumbuka tena
maneno niliyoambiwa kule Sumbawanga na Mbeya. Pengine ni kweli? Pengine alama
hii ndiyo iliyomvuta Mbonea? Iwe kweli iwe uongo, niliwaza,
kwa vyovyote vile
ilihusiana na hirizi yangu iliyopotea. Kama ningekuwa nayo, niliendelea kuwaza,
mtu yeyote mwenye nia mbaya nami asingenisogelea. Kamwe nisingewekwa alama!
Majuto ni mjukuu!
Niliwaza. Nilikuwa na miaka isiyopungua ishirini ya kuishi katika gereza hilo
huku nikiwaza hayo. Mawazo ambayo yangeweza kunitia kichaa. Lazima nijifunze
kuachana nayo. Lazima nipate jambo jipya la kuwaza badala ya kukodolea macho
kalenda nikiitafuta siku ambayo ingechapishwa baada ya miaka ishirini.
Nilijitahidi pia
kumfukuza Mbonea katika fikra zangu. Bwana huyu alikuwa mtu wa ajabu sana.
Alikuwa mnafiki asiye na haya kuliko binadamu wote niliopata kuwafahamu. Siku
tatu tu baada ya yeye kupata uhuru wake na mimi kuanza kutumikia kifungo
alikuja gerezani kuniona. Niliarifiwa kuwa nilikuwa na mgeni, sikuambiwa mgeni
huyo alikuwa nani. Pengine nisingekwenda. Nikamkuta kakaa kitako akinisubiri.
Alikuwa anang’ara mwili na mavazi, hali iliyofanya nijishuku kuwa nanuka jasho
na uchafu wa nguo zangu.
Nilimwona akitafuta
chozi la kunionyesha uchungu aliokuwa nao kwangu. Halikotoka. Sikuwa tena mgeni
wa machozi yake ya mamba. Nilitamani kucheka. Hakunipa nafasi hiyo. Aliinuka na
kunikumbatia bila ridhaa, kisha akanipa mkono wake wa kulia ambao muda wote
alikuwa ameufumba. Nikaupokea na kubaini kuwa katika kunipa mkono huo alinipa
kitu fulani kilichokuwa kiganjani. Nikaufungua mkono kutazama. Alikuwa amenipa
kipande cha aina fulani ya jani.
“Nini hiki?” Nilimuuliza
“Jani.”
“Jani la nini?”
“Jani la isale,”
alinijibu.
Nililifahamu jani hilo.
Isale ni majani uhimu sana kwa Wachaga. Hutumiwa kupanda katika mipaka ya
mashamba, kuepusha migongano. Lakini jani hilo pia hutumiwa kwa upatanishi.
Mchaga anapomfuata mwenzie kwa suala zito kama kuombana radhi, kudaiana na hata
ndoa huweka jani hilo mkononi na kumshikisha mwenzi huyo kabla ya mazungumzo ya
siri. Mara nyingi baada ya kitendo hicho mazungumzo huwa ya amani na mafanikio
kwa pande zote mbili.
“Unanipa isale ya nini?”
nilimuuliza.
“Nataka kukuomba radhi
kwa yote yaliyotokea,” alisema. “Nataka tuendelee kuwa ndugu. Ndiyo, uko ndani
niko nje. Nitautumia uhuru wangu huko nje kuhakikisha hukai ndani zaidi ya
miezi mitatu. Nitahakikisha…”
“Umenipa isale ya nini?”
nilimkatiza kwa ukali kidogo. “Mimi sio Mchaga na wewe sio Mchaga pia, kama
ulikuwa ukisema ukweli.”
Mbonea alikohoa kidogo
kabla hajanijibu akisema, “Ni kweli mimi sio Mchaga. Lakini sisi Wapare wa
Ugweno tuna tamaduni nyingi zinazofanana na Wachaga. Moja ni jani hili.
Tunalitumia katika upatanishi na mengineyo.”
Nilimtazama kwa makini
mtu huyu. Alikuwa Mbonea yuleyule mwenye sumu ya nyoka na hila za kinyonga.
Sikuona sababu za kuendelea kumsikiliza. Nikamwambia, “Sikiliza Mbonea. Mimi
sio malaika. Mimi sio Yesu Kristo ambaye aliwaelekeza wanafunzi wake wakipigwa
shavu moja wakinge na la pili. Mimi ni binadamu kama wewe. Naomba uondoke.
Naomba usikanyage tena hapa kwa niaba yangu.”
Nadhaini hakunielewa.
Nilimwona kaduwaa, hajui lipi zaidi aseme. Nilimwacha katika hali hiyo na
kurudi katika ‘utumwa’ wangu wa miaka ishirini.
Siku mbili tatu baadaye
nilipata ugeni mwingine. Huyu alikuwa mwanamke. Alikuwa mnene, maji ya kunde.
Sura yake nzuri haikuwa na dalili zozote za dhiki wala misukosuko ya maisha.
Alifuatana na watoto wawili wa miaka saba au minane, mapacha.
“Mgeni wangu?”
Nilimuuliza. “Ndiyo. Wewe si Petro Kionambali?” “Ndiye.”
Basi mimi ni mgeni wako.
Nimetumwa na rafiki yako Daniel Mbonea nikuletee chakula. Ameniagiza
nikutembelee mara mbili kila wiki na kukuletea mahitaji yako yote muhimu.
“Mbonea!” Nikaropoka.
“Wewe ni nani kwake?” “Mimi ni mkewe.”
Sikuyaamini masikio
yangu, “Mkewe?” Nikauliza kuhakikisha. “Mke wa ngapi?”
“Kwani alikuambia anao
wake wangapi?” “Ninachofahamu ni kwamba hana mke. Mkewe alifariki
zamani kwa kujinyonga.”
Ikawa zamu ya mama huyo kushangaa.
“Mkewe alijinyonga?”
Kisha akaangua kicheko.
“Bila shaka alikuwa akikutania. Tumeoana toka tukiwa vijana, sasa tunaelekea
uzeeni. Hana mke mwingine, hana mke aliyepata kujinyonga.”?
Niliduwaa kwa muda. “Na
hawa watoto? Unataka kuniambia kuwa ni wake?”
“Ndiyo. Ni watoto wetu.
Alikuambia hana watoto?” Nilishindwa kumwambia kuwa kwa mujibu wa
Mbonea mwenyewe watoto
wake pacha walikufa zamani kwa utapiamlo. Nilishindwa kuuliza juu ya bibi kizee
na dada yake kiwete wanaomtegemea. Sikuhitaji kuhakikishiwa kuwa yote
aliyosema ulikuwa uongo,
uongo mtupu, uongo uliokusudiwa kunitia huruma ili nishawishike kushirikiana
naye katika dhamira yake chafu ya kutafuta utajiri.
“Mama, nashukuru sana,”
nilimwambia. “Naomba umrudishie chakula chake. Halafu, tafadhali mwambie,
sihitaji msaada wake wa aina yoyote si leo si kesho wala keshokutwa.”
Nikageuka na kuondoka
zangu.
Nilimwacha mama huyo
kaduwaa, haelewi kinachoendelea. Laiti angejua kuwa aliolewa na nyoka…
* * *
Gerezani kuna kiu.
Kwangu kiu hiyo haikuwa ya vinywaji baridi au vinywaji laini. La, hasha!
Ilikuwa kiu ya habari. Gerezani kuna njaa. Lakini njaa yangu mimi haikuwa ile
ya chakula chao kibovu, ilikuwa ya kuona na kusikia kile kinachoendelea nje ya
ukuta huo imara wa gereza la Kilimoanga. Kwangu hiyo ilikuwa adhabu kubwa zaidi
na inayonitesa zaidi. Kwa nia ya kukidhi adha hiyo nilijenga urafiki na mfungwa
mmoja kwa namna ya ajabu. Alikuwa na redio ndogo.
Kwa bahati mbaya, bwana
huyu alipenda sana kusikiliza muziki. Mara kwa mara alitafuta stesheni
zinazopiga muziki wa kina Mbaraka Mwinshehe na Salumu Abdallah. Nyimbo za
‘malaika’, ‘wanawake wa tanzania’, ‘mwanameka!’ ‘shida na Marijani Shabani’
zilikuwa mdomoni mwake kila dakika kufuatia mipigo redioni. Ilikuwa kazi ngumu
kumshawishi mara chache aniruhusu kusikiliza taarifa za habari na vipindi
vingine makini zaidi.
Ni kwa kupitia redio
yake hiyo nilipofahamu kuwa Zanzibar, nchi ambayo ilitawaliwa na waarabu kwa
muda mrefu, nayo ilikuwa ikiwaka moto kwa vuguvugu la kudai kujitawala.
Chama kilichoitwa Afro
Shiraz kilikuwa kimeanzishwa na kuwapa taabu kubwa watawala.
Aidha, nilibaini kuwa
hesabu ya watu ilifanywa mwaka 1957chini Tanganyika ilionyesha kuwa tulikuwa
9,087,6000 kati ya hao 364,072 au asilimia 4 tu wakiishi mijini.
Mwaka wa 1958 zikasikika
habari za Julius Nyerere kushtakiwa mahakamani kwa kuandika katika gazeti la
TANU, sauti ya TANU. Habari ambazo magavana wawili wa wilaya walidai kuwa
ziliwadhalilisha. Nyerere alishinda shitaka moja na kutiwa hatiani kwa shitaka
la pili. Adhabu yake ilikuwa kifungo cha miaka sita jela au faini ya shilingi
3,000/= alilipa faini. Kama asingelipa uenda tungejumuika naye gerezani humo.
Tukio hilo lilikuwa kama
chachu ya matukio tele ya kisiasa yaliyoendelea kutumbuiza maisha yetu gerezani
humo. Zilisikika habari za TANU kuchachamaa katika kudai uhuru. Zikasikika
habari za chama kipya, ANC, kilichoongozwa na Zuberi Mwinyishehe Mtemvu, pia
kiliomba ridhaa ya wananchi kuongoza serikali. Hatimaye, ikaja ile siku ya
siku, desemba 9, 1961 tulikesha tukisikiliza redio, sauti ya Dar es salaam
iliyokuwa ikitangazwa na bwana mmoja, Hamza Kasongo, kusheherekea uhuru.
Ilipotimia saa sita za usiku tulisikiliza taarifa za bendera ya malkia wa
Uingereza ikishushwa na ile ya Tanganyika ikipandishwa, Julius Nyerere akiwa
Waziri Mkuu wa kwanza.
Pilikapilika hizo
hazikuwa Tanganyika pekee. Kenya na Uganda pia kulikuwa kukiwaka moto. Lakini
tukio lililonigusa ni lile la visiwa vya Zanzibar, Unguja na Pemba. Huko nako
kulikuwa na purukushani kali za kisiasa. Mtu mmoja aliyeitwa Abeid Aman Karume
na chama chake cha Afro Shiraz alikuwa
akusuguana na vyama vya
ZPPP na ZNP. Uchaguzi uliojaa hila ulifanyika na kutoa madaraka kwa vyama vile
vilivyokuwa na ushawishi mkubwa wa Waarabu dhidi ya Afro Shiraz iliyoshindwa
kwa asilimia 54.3 januari 12, 1964 visiwa hivyo vililipuka, Waarabu wakatimuliwa,
Karume na chama chake wakachukua uongozi.
Aril 21, 1964, pamoja na
kuwa mfungwa nililala nikiwa Mtanganyika, kesho yake nikaamka nikiwa Mtanzania.
Hiyo ilifuatia Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ambao uliambatana na kubuniwa
kwa jina jipya la nchi.
Nikiwa mfungwa kutokana
na tuhuma za kuharibu maliasili na urithi wa taifa masikio yangu hayakuwa wazi
kwa habari za kisiasa pekee. Nilitegemea siku hiyo habari zote zilizohusiana na
mazingira, misitu na viumbe wake, maziwa na vyote vilivyomo na hata hali ya
hewa. Kila nilipofanikiwa kupata gazeti nilifurahi zaidi na kulisoma lote,
ikiwa pamoja na mashairi na kujaribu kujaza mafumbo.
Kupitia gazeti moja zile
jitihada zilizobuniwa mwaka 1954, za kupandikiza aina mpya ya samaki katika
ziwa Nyanza, ambalo sasa liliitwa Victoria, lilikuwa limetiliwa mkazo zaidi
mwaka 1960 na kwamba jaribio hilo lilianza kutoa matunda. Hata hivyo, kulikuwa
na malalamiko mengi toka kwa wana mazingira mbalimbali duniani kuwa samaki hao
ambao ni wakubwa zaidi walikuwa wakiwateketeza samaki wa asili kwa kuwala. Hali
ambayo ilielezewa kuwa iliashiria kuwa aina zipatazo hamsini za samaki wa ziwa
hilo zilikuwa hatarini kutoweka.
Kwa upande mwingine
nilijifunza kuwa serikali ilikuwa imeongeza jitihada za kuwalinda wanyama, miti
na misitu asilia. Pamoja na Serengeti maeneo kama Ngorongoro, Ziwa Manyara,
Tarangire, Mikumi,
Rubondo, Udzungwa na mengineyo tayari yalisajiliwa kama hifadhi maalumu za
taifa. Maeneo mengine yalikuwa pamoja na Selow, Kilimanjaro, Gombe, Mahele na
Katavi.
Hali kadhalika, mapori
na misitu kadhaa ilihifadhiwa kwa ajili ya urithi. Selow yenye ukubwa wa
takriban kilomita za mraba 50,000 ikiwa na maana kuwa inazishinda nchi kama
Switzerland au Denmark kwa ukubwa lilikuwa eneo mojawapo. Ikiwa haina mtu
anayeishi huko wala shughuli zozote za kibinadamu zinazofanyika, Selow
inakadiriwa kuwa na tembo wapatao 60,000, nyati 160,000, viboko 40,000 na simba
5000. Pamoja na wanyama wengine anuai Selow inakisiwa kuwa na aina 440 za
ndege. Ziwa Tagalala mto Rufiji, miti ya miombo na migunga pamoja na misitu
inayoambaa na mito ni baadhi ya vivutio vinavyotajwa katika hifadhi hiyo.
Mapori mengine
yaliyoifadhiwa yalikuwa pamoja na Moyowosi, Bugiri, Rungwa, Maswa, Kisiwa cha
Saa Nane, Mkomazi na Ugala. Pia Usangu, Mpanga, Rukwa, Swaga, Ikorongo ni
miongoni mwa mapori hayo.
Huko Zanzibar pia jithada
tele zilikuwa zikifanyika kulinda mazingira ya nchi kavu na bahari. Pomboo,
viumbe wa majini ambao wataalam hawapendi kuwaita samaki kwa kuwa wananyonyesha
watoto wao, walikuwa wakitafutiwa namna ya kuwalinda. Vifo vya mara kwa mara
vya viumbe hao, ambao ni wahamajihamaji vilikuwa vikisumbua sana vichwa vya
wana mazingira. Viumbe hao, ambao wanafundishwa kwa urahisi hasa pale
wanapochupa toka majini kama golikipa anayedaka mpira wanaweza kuwa kivutio
kikubwa cha watalii.
* * *?
Pamoja na ‘alama’, kama
kweli nilikuwa nayo nyota yangu ya kupendwa na watu bado ilikuwa iking’ara,
hali ambayo naamini ilichangia kufanya niweze kuyamudu maisha ya gerezani humo
hadi mwisho wa kifungo. Wakati wenzangu wengi walipigwa kama ng’ombe, baadhi
wakifa kwa kutiliwa maanani wanapougua, mimi hali ilikuwa tofauti. Nilipendwa
na mkuu wa gereza. Nilipendwa na maafisa wake pia. Nadhani kale ka usomi kangu
kalisaidia. Mara kwa mara nilipewa kazi ya ukarani, kujaza fomu, kurekodi
matumizi au mahitaji, kuandaa taarifa za wafungwa wenzangu na kadhalika. Kazi
hizo zilipokuwa finyu nilipewa udobi wa kunyoosha nguo za askari magereza. Mara
nyingine nilipewa kazi ya kutunza bustani ya mkuu wa gereza ambazo ziliambatana
na kudokolewa chakula cha binadamu toka jikoni mwake.
Sherehe za uhuru na zile
zilizofuatana mara kwa mara ziliambatana na kuachiwa kwa baadhi ya wafungwa
wenye makosa madogomadogo au ambao tarehe zao za kufunguliwa zilikaribia.
Bahati hiyo mimi haikunipitia. Uzito wa kosa langu haukuruhusu kunijadili
katika kundi hilo. Kama ungeruhusu naamini nisingekuwa na sababu ya kusubiri
tarehe iliyobandikwa kifuani pangu.
Uhuru wenyewe ulianza
kunitia mashaka kabla sijauonja. Tulitarajia uhuru ulikuwa mwisho wa kero zote
za Mtanganyika, ambaye sasa aliitwa Mtanzania. Tulidhani uhuru ungekuwa mwanzo
wa neema na faraja kubwa nchini. Haikuwa hivyo. Nyimbo za hali ngumu ya maisha
toka huko uraiani zilitushangaza sana wafungwa. Tulishangaa zaidi pale kasi ya
watuhumiwa waliokuwa wakiletwa gerezani ilipoongezeka badala ya kupungua, wengi
wakiwa watu wenye makosa ya ovyoovyo yaliyoashiria jambo moja kubwa ‘njaa!’
huyu kampiga mke wake
hadi kumwua kwa kupoteza shilingi mia! Yule kafungwa kwa kuiba kuku wa jirani.
Na Yule? Yeye alitupa kitoto kichanga jalalani!
Kasi hiyo, ilifanya selo
zifurike, tuanze kulala ‘mzungu wa nne’. Huyu aliweka kichwa huku yule kule.
Chakula kiliongezeka ubaya, hata hewa katika selo ilibadilika na kuwa nzito
kutokana na kutumiwa na watu wengi kuliko ilivyokusudiwa.
Nadhani ni hali hiyo
iliyoibua tatizo jingine zito zaidi, ‘maradhi.’ Zamani kidogo ugonjwa mkubwa
gerezani ulikuwa malaria. Mara yaliingia maradhi mapya ya kipindupindu. Ugonjwa
hatari wa kuharisha ambao ulimchukua binadamu siku mbili tu kupoteza maisha.
Wafungwa wengi
walipoteza maisha, kutwa watu sita au zaidi hadi ulipodhibitiwa kwa vidonge vya
kufunga tumbo. Tuliambiwa ugonjwa huu hatari chanzo chake kilikuwa uchafu.
Lakini kutokana na shida ya maji gerezani humo, naamin tuliobakia hai ilikuwa
kwa kudra za Mwenyezi Mungu zaidi ya jitihada kujikinga.
Habari za kipindupindu
humo nje ya gereza pia zilivuma sana. Dar es salaam, Dodoma, Singida na
kwingineko kipindupindu kiliteketeza maisha ya watu kama watu wa kusini
wanavyoshambulia ‘dagaa nchanga’ au Wahaya wanavyowaonea ‘nsenene’. Sikuelewa
hata kidogo kila nilipofikiria hilo. Watanzania tuteketee kwa uchafu kwa ajili
ya uhaba wa maji! Nchi ambayo imezungukwa na maji kila upande, ikajaliwa mito,
maziwa, mabwawa na chemchemi tele! Kwa kweli sikuweza kuelewa.
Wakati bado natafakari
hilo, likaja jingine la kutisha zaidi, UKIMWI. Ugonjwa ambao wataalamu walidai
kuwa
ulitokana na wadudu
wanaoitwa HIV ambao hushambulia chembechembe nyeupe ambazo ni kinga ya mwili wa
binadamu na kumwacha wazi kwa ugonjwa wowote kumtia mweleka wa mwisho.
Niliwaona baadhi ya wafungwa wenye UKIMWI. Wanatisha kuliko chochote kile
ulichopata kukiona. Nywele zao zilinyonyoka, mwili kuota mapele huku tumbo
likiwa halina uwezo wa kuhifadhi chochote kutokana na kuharisha. Kama
kipindupindu kiliogopwa kwa kuua haraka UKIMWI uliogopwa zaidi kwa kuchelewesha
sana kumwua mteja wake huku ukimpa kila aina ya mateso.
Wajuzi wa masuala ya
tiba walitueleza kuwa njia kubwa zaidi ya maambukizi ya UKIMWI ni katika
kujamiiana bila kutumia kinga. Jambo ambalo mtu yeyote angeweza kulielewa mara
moja na kujiepusha nalo. Lakini taarifa ya tatizo hilo huko nje lilikuwa kubwa
na la kutisha kupita kiasi. Haikupita siku mbili bila kumsikia mfungwa mmoja
wapo akiangua kilio. Kisa? Kafiwa na mdogo wake, mtoto wake, mke wake au rafiki
yake. Taarifa za wasichana kujiuza katika majumba ya starehe, akina baba wenye
pesa kuwarubuni wanafunzi, kuzagaa kwa mabaa na sehemu za starehe mitaani na
vishawishi tele vya anasa ziliendelea kutufikia gerezani humo kwa kiwango
kilekile cha kukua kwa kasi ya UKIMWI. Hali iliyoashiria kitu kimoja tu, hali
ngumu maisha. Kwa lugha nyepesi; njaa!
Wakati huo tarehe yangu
ya kumaliza kifungo ilizidi kukaribia. Siyo siri kwamba nilianza kuyaogopa
maisha ya huko uraiani zaidi ya gerezani. Kama mazingira ya gerezani humo
yangeweza kuboreshwa kidogo tu siyo siri, ningefikiria suala la kubaki gerezani
humo wa makini zaidi.
?
21
Ben R. Mtobwa
YA ISHIRINI NA MOJA?
Mfungwa Mikono Musoma
W
anahistoria
wanatukumbusha kuwa adhabu ya kifungo, ambayo mimi na wenzangu gerezani humu
tulikuwa tukiitumikia,
ilianzishwa huko Ulaya
yapata miaka 300 iliyopita.
Awali ya hapo mhalifu,
au mtuhumiwa aliyepatikana na hatia ama alinyongwa ama alitoswa baharini au
kuachwa katika visiwa vya mbali visivyo na watu.
Hapa Afrika pia tulikuwa
na adhabu zetu mbalimbali. Mhalifu alilazimishwa kutoa baadhi ya mali zake kama
adhabu, kutengwa na jamii yake hata kufukuzwa kijijini. Wakati mwingine
alitungiwa nyimbo za mafumbo ambazo ziliimbwa katika sherehe na hivyo
kumdhalilisha sana mbele ya jamii. Hali hiyo ilipunguza sana tabia ya uhalifu.
Hivyo, wageni
walipoingia na kutushawishi kufuata dini na tamaduni zao kwa upande mmoja,
upande wa pili walitushurutisha kutii sheria na adhabu zao. Moja ya adhabu hizo
ni hili la gereza. Unakamatwa na mtu anayeitwa polisi, unapelekwa kwa mtu
anayeitwa hakimu, kufumba na kufumbua uko mikononi mwa bwana magereza; ukifanya
kazi ambazo hulipwi na kupewa chakula ambacho hushibi.
Ni katika hali hiyo
tuliposhangazwa siku moja alipoletwa?
huyu kampiga mke wake
hadi kumwua kwa kupoteza shilingi mia! Yule kafungwa kwa kuiba kuku wa jirani.
Na Yule? Yeye alitupa kitoto kichanga jalalani!
Kasi hiyo, ilifanya selo
zifurike, tuanze kulala ‘mzungu wa nne’. Huyu aliweka kichwa huku yule kule.
Chakula kiliongezeka ubaya, hata hewa katika selo ilibadilika na kuwa nzito
kutokana na kutumiwa na watu wengi kuliko ilivyokusudiwa.
Nadhani ni hali hiyo
iliyoibua tatizo jingine zito zaidi, ‘maradhi.’ Zamani kidogo ugonjwa mkubwa
gerezani ulikuwa malaria. Mara yaliingia maradhi mapya ya kipindupindu. Ugonjwa
hatari wa kuharisha ambao ulimchukua binadamu siku mbili tu kupoteza maisha.
Wafungwa wengi walipoteza
maisha, kutwa watu sita au zaidi hadi ulipodhibitiwa kwa vidonge vya kufunga
tumbo. Tuliambiwa ugonjwa huu hatari chanzo chake kilikuwa uchafu. Lakini
kutokana na shida ya maji gerezani humo, naamin tuliobakia hai ilikuwa kwa
kudra za Mwenyezi Mungu zaidi ya jitihada kujikinga.
Habari za kipindupindu
humo nje ya gereza pia zilivuma sana. Dar es salaam, Dodoma, Singida na
kwingineko kipindupindu kiliteketeza maisha ya watu kama watu wa kusini
wanavyoshambulia ‘dagaa nchanga’ au Wahaya wanavyowaonea ‘nsenene’. Sikuelewa
hata kidogo kila nilipofikiria hilo. Watanzania tuteketee kwa uchafu kwa ajili
ya uhaba wa maji! Nchi ambayo imezungukwa na maji kila upande, ikajaliwa mito,
maziwa, mabwawa na chemchemi tele! Kwa kweli sikuweza kuelewa.
Wakati bado natafakari
hilo, likaja jingine la kutisha zaidi, UKIMWI. Ugonjwa ambao wataalamu walidai
kuwa
ulitokana na wadudu
wanaoitwa HIV ambao hushambulia chembechembe nyeupe ambazo ni kinga ya mwili wa
binadamu na kumwacha wazi kwa ugonjwa wowote kumtia mweleka wa mwisho.
Niliwaona baadhi ya wafungwa wenye UKIMWI. Wanatisha kuliko chochote kile
ulichopata kukiona. Nywele zao zilinyonyoka, mwili kuota mapele huku tumbo
likiwa halina uwezo wa kuhifadhi chochote kutokana na kuharisha. Kama kipindupindu
kiliogopwa kwa kuua haraka UKIMWI uliogopwa zaidi kwa kuchelewesha sana kumwua
mteja wake huku ukimpa kila aina ya mateso.
Wajuzi wa masuala ya
tiba walitueleza kuwa njia kubwa zaidi ya maambukizi ya UKIMWI ni katika
kujamiiana bila kutumia kinga. Jambo ambalo mtu yeyote angeweza kulielewa mara
moja na kujiepusha nalo. Lakini taarifa ya tatizo hilo huko nje lilikuwa kubwa
na la kutisha kupita kiasi. Haikupita siku mbili bila kumsikia mfungwa mmoja
wapo akiangua kilio. Kisa? Kafiwa na mdogo wake, mtoto wake, mke wake au rafiki
yake. Taarifa za wasichana kujiuza katika majumba ya starehe, akina baba wenye
pesa kuwarubuni wanafunzi, kuzagaa kwa mabaa na sehemu za starehe mitaani na
vishawishi tele vya anasa ziliendelea kutufikia gerezani humo kwa kiwango kilekile
cha kukua kwa kasi ya UKIMWI. Hali iliyoashiria kitu kimoja tu, hali ngumu
maisha. Kwa lugha nyepesi; njaa!
Wakati huo tarehe yangu
ya kumaliza kifungo ilizidi kukaribia. Siyo siri kwamba nilianza kuyaogopa
maisha ya huko uraiani zaidi ya gerezani. Kama mazingira ya gerezani humo
yangeweza kuboreshwa kidogo tu siyo siri, ningefikiria suala la kubaki gerezani
humo wa makini zaidi.
?
21
Ben R. Mtobwa
YA ISHIRINI NA MOJA?
Mfungwa Mikono Musoma
W
anahistoria
wanatukumbusha kuwa adhabu ya kifungo, ambayo mimi na wenzangu gerezani humu
tulikuwa tukiitumikia,
ilianzishwa huko Ulaya
yapata miaka 300 iliyopita.
Awali ya hapo mhalifu,
au mtuhumiwa aliyepatikana na hatia ama alinyongwa ama alitoswa baharini au
kuachwa katika visiwa vya mbali visivyo na watu.
Hapa Afrika pia tulikuwa
na adhabu zetu mbalimbali. Mhalifu alilazimishwa kutoa baadhi ya mali zake kama
adhabu, kutengwa na jamii yake hata kufukuzwa kijijini. Wakati mwingine
alitungiwa nyimbo za mafumbo ambazo ziliimbwa katika sherehe na hivyo
kumdhalilisha sana mbele ya jamii. Hali hiyo ilipunguza sana tabia ya uhalifu.
Hivyo, wageni
walipoingia na kutushawishi kufuata dini na tamaduni zao kwa upande mmoja,
upande wa pili walitushurutisha kutii sheria na adhabu zao. Moja ya adhabu hizo
ni hili la gereza. Unakamatwa na mtu anayeitwa polisi, unapelekwa kwa mtu
anayeitwa hakimu, kufumba na kufumbua uko mikononi mwa bwana magereza; ukifanya
kazi ambazo hulipwi na kupewa chakula ambacho hushibi.
Ni katika hali hiyo
tuliposhangazwa siku moja alipoletwa?
Nikasema, “Itabidi
tutafute muda tukae na kusimuliana masaibu yetu kwa kituo.”
“Kuna ubaya gani?”
Butiku alijibu.
* * *?
Mkoa wa Mara unapakana
na nchi ya Kenya kwa upande wa kaskazini. Mkoa huo ambao unachangia neema ya
ziwa Victoria na mikoa ya Mwanza na Kagera, Mashariki umepakana na mkoa wa
Serengeti. Mji wa Tarime, alikozaliwa Matayo Butiku, au ‘Umsolopogaas’ kama anavyopenda
kujiita, uko mpakani na Kenya. Mji huu ni maarufu kwa pilikapilika nyingi kama
ilivyo miji mingine ya mipakani kama Namanga, na Tunduma uko katika wilaya ya
Tarime, kando kidogo ya mpakani, Sirari.
Mkoa huo una sifa zote
ambazo nchi hii imejaliwa; mvua za kutosha, ziwa lililojaa samaki, ardhi
iliyojaa rutuba na mbuga za wanyama kama Ikorongo, Nata na baba lao; Serengeti.
Mara una makabila mengi
ya asili na wahamiaji. Ya asili ni Wakurya, Wazanaki, Wajita na Wajaluo ambao
pia, kama Wamasai, wana mizizi yao nchini Kenya. Wahamiaji ni pamoja na
wahindi, Wanyarwanda, Warundi, Wahangaza na wengineo. Pamoja na sifa tele za
neema katika nchi yao, watu wa?
Mara, hasa Wakurya
wamerithi maradhi ambayo hadi leo tiba yake haijapata kupatikana; Ubabe. Mauaji
na vita vinavyoitwa vya kikabila, ambavyo kwa kweli ni vita baina ya koo ndani
ya kabila moja, vimekuwa vikitawala macho na masikio kupitia katika vyombo vya
habari. Vijiji, kama Kubitarere, ni miongoni mwa vile ambavyo vimeathirika mara
kwa mara na ubabe wa baadhi ya wanajamii wa ama Waachari ama Walyanchoka.
Kisa? Ama hawa
wameshukiwa kuiba ng’ombe wa hawa, ama wamevamia shamba la hawa. Vita vitazuka,
watu wanapoteza maisha, mashamba yanachomwa, nyumba zinabomolewa na uharibifu
mwingine tele usio na kifani. Mara nyingi serikali, kupitia vyombo vyake vya
usalama pekee ambayo huingilia vita hivyo na kuituliza. Lakini si kwa muda
mrefu.
Ni mirathi hiyo ya
hatari ambayo ilimgharimu rafiki yangu Matayo Butiku mikono yake yote miwili na
kumpa kilema cha maisha.
Ilikuwaje?
Zilikuwa zimepita siku
mbili toka nilipomtia machoni kwa mara ya kwanza akiwa katika hali ile.
Tulipata wasaa wa kuzungumza, mimi nikifyeka majani yeye, aliyepangiwa kufyeka
pia akipita hapa na pale huku akimwaga gumzo na vichekesho ambavyo nilibaini
baadaye kuwa vilimsaidia sana kupatiwa huduma mbalimbali, ikiwa pamoja na
kulishwa chakula.
“Tulipoachana pale
shuleni mimi niliendelea kwa miaka miwili kabla sijaacha masomo na kurudi
nyumbani ambako nilijiunga na shughuli za uvuvi katika ziwa Victoria. Baadaye
niliacha kuvua na kuanza biashara ya kupeleka samaki Nairobi na Kampala.
“Unajua sangara hawaishi
kuliwa tu?” aliniuliza ghafla. Sikumwelewa. Akafafanua, “Siku hizi sangara ni
mali katika kila kiungo chake. Ngozi yake siku hizi ni mali ghafi
inayotengeneza pochi murua za akina mama matajiri. Mifupa yake ni malighafi kwa
viwanda vya mbolea na madawa. Siku si nyingi hata ile harufu yake itageuzwa
manukato ya aina yake. Sangara ni almasi za ziwani.
“Nilipata fedha nyingi
sana. Kwa viwango vya pale kijijini
nilikuwa tajiri.
Nikajenga nyumba safi na shamba kubwa la miwa. Toka hapo ndipo mambo yalianza
kwenda mrama.” Alisita kidogo.
Nikaitumia fursa hiyo
kutumbukiza swali, “Ulikuwa hujabahatika kuoa?”
“Nini? Kuoa?” aliuliza
huku akiangua kicheko. “Toka niko darasa la nne, wakati tukilala wote pale
bwenini, mimi tayari nilikuwa na mke,” alisema.
Nikapigwa na butwaa.
“Ulikuawa na mke!” “Naam.”
“Ulioa lini?”
“Sikuoa, niliozeshwa na
ukoo wangu. Nilikuwa mtoto pekee wa kiume katika familia yangu. Dada zangu
walikuwa kumi na mmoja. Walianza kuolewa. Tulipata ng’ombe wengi sana lakini
wazazi hawakuridhika. Walihitaji mjukuu ili awe mrithi wa mali hizo na awapatie
watoto wa kiume.”
“Uliwapata?” “Watu
gani?”
“Watoto wa kiume.”
Nikamwona Matayo, kwa
mara ya kwanza, akipoteza tabasamu na kuonyesha dalili za masikitiko. Nusu
dakika tu, mara alirudia sura yake ya kawaida na kunijibu akisema, “Kuoa ni
khiari, kuzaa ni majaliwa. Leo hii nina wake watano, hata mmoja hajanipatia
mtoto wa kiume!”
Wake watano! Hata hivyo,
sikushangaa sana. Matayo alikuwa mtu wa vituko na miujiza siku zote, muujiza wa
kwanza ulikuwa ule wa kujiunga na shule akiwa ametuzidi umri wote darasani.
Mwujiza wa pili ukiwa ule wa kuja shule na silaha zake zote. Sasa huu wa kwamba
wakati wote alikuwa na mke!
“Hilo linakushangaza?”
aliuliza baada ya kuyasoma mawazo yangu. “Kwa hiyo, utashangaa zaidi
nikikwambia kuwa hata wakati tuko shule, kila likizo niliingia kwenye vita na
kuwashikisha adabu adui zetu?”
Muujiza mwingine!
“Nilipigana sana. Na
nilipata sifa tele za ushujaa. Adui zetu waliniogopa kuliko simba kwa njinsi
nilivyokuwa hodari wa kupanga mashambulizi na kukwepa mishale na mikuki yao.
Kwa kweli, jina la yule mzee wa Kizulu lilinistahili sana. Hadi leo sina mikono
bado wananiogopa sana na kila vita niko mstari wa mbele nikiongoza mapambano.
Kama nisingekamatwa na kushitakiwa wangenikoma.
“Ilikuwaje?” “Nini?”
“Ilitokea nini
Umsolopogaas akaishiwa ujanja na kukatwa mikono?” nilifafanua.
Akacheka. Kisha akasema,
“ Naweza kusema ndege mjanja hunaswa na tundu bovu. Nilifanya kosa la kumdharau
adui yangu. Mtoto mdogo sana, tena ambaye alikuwa hajapigana vita yoyote.
Tulivamia kijiji chao, tukateka mifugo yote. Watu wazima wote walikimbia, mtoto
huyu, wa miaka kumi na moja au mbili aliachwa nyuma akilia. Mkononi alikuwa na
sime.
“Nilikatazama katoto
kale. Ka kiume! Ningeweza kukaua, ningeweza kukavunja shingo. Lakini
nikakahurumia. Kwangu mtoto wa kiume alikuwa lulu. Nikakaacha na kugeuka ili
niondoke zangu. Mara waa! Mkono wangu wa kulia uliokuwa na sime ukaanguka
chini. Maumivu makali yakanishika, lakini hayakunishinda hasira niliyoipata.
Nikageuka kwa kasi. Waa! Nilikutana na pigo la pili ambalo lilidondosha mkono
wangu
wa pili. Maumivu
hayakuwa na kifani. Bila khiari nilianguka na kupoteza fahamu. Nilipozinduka
nilijikuta niko hospitali, mikono yangu tayari imekuwa vibutu.
Na nilipopata nafuu
nilishtakiwa kwa mauaji na uporaji na kupewa adhabu hii ninayoitumikia.
Ilikuwa taarifa ya
kusikitisha sana. Nilimhurumia, sikuwa na uwezo wa kumsaidia. Nikaishia kumpa
pole tena. Nadhani nilimhurumia. Lakini kutokana na vitendo vyake mwenyewe na
msimamo wake hata baada ya kupoteza mikono nilishindwa kuamini kama kweli
ninamhurumia au la.
“Haya na wewe niambie
kulikoni hadi ukafika hapa,” alisema. “Si walisema ukijua kupokea ujue na
kutoa? Ama ukiwa mroho usiwe mchoyo?” aliongeza.
Yangu yanaelezeka kweli?
Nilijiuliza.
M
Kiguu n2a Njia
2
YA ISHIRINI NA MBILI?
Hadi?
fungwa hana kauli.
Mfungwa hana hiari. Mara tu ukishahukumiwa wewe si wewe tena, ni mali ya mtu
mwingine. Utafuata matakwa
na hiari yake hadi
mwisho wa kifungo chako.
Kwa mtu aliyekuwa na
kifungo kirefu kama mimi, mfumo huo wa kanuni za mfungwa uliniathiri mara kwa
mara, ingawa wakati mwingine athari hizo zilikuwa faraja kwangu kwa namna moja
au nyingine.
Moja ya faraja hizo ni
pale nilipobahatika kuwemo katika kundi la wafungwa walioteuliwa kwenda
Zanzibar kusaidia kazi ya kuvuna karafuu. Kwa mujibu wa mkuu wa gereza karafuu
zilipamba sana na zilikuwa zikielekea kuharibika. Vijana wa jeshi la kujenga
uchumi wa huko walikuwa tayari wamepelekwa lakini hawakukidhi mahitaji.
ITAENDELEA

0 Comments