Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Responsive Advertisement

PENZI LA MCHORA TATTOO-13



LATIFA NTANGA
0719618409
Romeo alicheka sana na kujiona bonge la mshindi kwa kuweza kumfikisha kileleni Mwanakombo. Basi alichukua taulo dogo na kuingia bafuni humo humo ndani, hiyo nyumba ilikuwa nzuri na ya kisasa kila chumba kina choo na bafu ndani japo kuwa nje pia kulikuwa na bafu la jumuiya, Basi Romeo akajimwagia maji na kujisugua mwilini huku akitabasamu sana. Baada ya kumaliza alitoka na kumkuta Mwanakombo akijigeuza tu.
"Mamii amka mie nataka kuondoka" Romeo alimwamsha Mwanakombo.
"Si...wezi.." Alijibu Mwanakombo kwa sauti ya chini sana.
"Nini? hebu amka huko bwana" alisema Romeo na kumshika Mwanakombo akamsaidia hadi akainuka na kukaa kitako.
"Hebu inuka uoge kwanza upate nguvu!" Romeo alimwambia na akamsaidia kusimama akampeleka hadi bafuni na huko akafungulia maji hakutaka kumuacha alimsaidia Mwanakombo akaoga na kutoka wakakaa kwenye sofa la humo ndani. Romeo akatoa maji na kumpa Mwanakombo anywe ambapo alikunywa mengi sana.
"Opsssss..wewe mwanaume shikamoo!" Alisema Mwanakombo kwa sauti ya uchovu. Romeo alicheka sana tena kwa nguvu.
"Hongera baba umejua kunikomesha daaah siamini!" Mwanakombo alizidi kusema.
"Hahaaha jamani kwani nimefanyaje mie?" Aliuliza Romeo.
"Mh baba wewe ni kiboko yani hatari tupu, hivi unajua leo ndio mara ya kwanza nakojozwa yani sikuwahi kabisa mara zote nakuwaga mshindi kwa kumpagawisha mwanaume ila mimi sijawahi kabisa" alisema Mwanakombo.
"Oh pole sana, unajua wanaume wengi hawajali hisia za wapenzi wao yani mwanaume anajali hisia zake yeye tu wala hafikirii kama mwanamke wake amefika kileleni au bado yeye anachojali akojoe basi mwanamke aridhike au asiridhike hilo hajui" alisema Romeo.
"Hilo ni kweli na wanawake wengi waliokuwa kwenye ndoa au hata wasioolewa hawajui kukojoa kupoje wala kileleni hawajawahi kufika" alisema Mwanakombo.
"Ni kweli kabisa"
"Romeo nakuomba usiniache" alisema Mwanakombo.
"Lakini unajua nina mpenzi"
"Najua Romeo nitavumilia tu naomba usiniache uwe na mimi pia"
"Sawa usijali mtoto mzuri"
"Nakupenda sana"
"Nakupenda pia mamy, nipe tena basi"
"Mmh hapana nitakufa bure sitaki"
"Hahhaa acha uoga haufi jamani"
"Hapana Romeo siwezi tena hapa mwili wote unauma mwenzio sina nguvu nimeishiwa kabisa"
"Dah sawa ninyime tu"
"Hapana sikunyimi ila sijiwezi"
"Poa hamna shida acha niondoke"
"Jamani si ubaki tupige stori tu"
"Hapana nitaumia tu acha niende"
"Basi naomba namba yako"
Wakabadilishana mawasiliano yao baada ya hapo Romeo akaondoka na kurudi chumbani kwake.
**
Uhusinao mpya ukaanza juu ya Romeo na Mwanakombo ikawa mara kwa mara wanakutana na kufanya yao. Mwanakombo alijitoa sana kwa Romeo na kumuona ni kama mpenzi wake, na kipindi hiko Lisa alikuwa bize sana na masomo hivyo waliishia kuwasiliana kwenye simu na Romeo bila kwenda nyumbani kwake, kwa Mwanakombo ulikuwa muda wake wa kujidai na Romeo ambapo asubuhi na mapema alikuwa akimuandalia chai ya nguvu na kumpelekea kwake au hata alikuwa akienda kimya chumbani kwake, na siku ambazo alikuwa akishinda nyumbani haendi kazini basi walikuwa wakishinda pamoja huku mahaba niue yakitawala kwao.
"Mume chakula tayari amka tule" alisema Mwanakombo kwa mahaba yote kama vile Romeo tayari amemuoa. Mahaba yalikolea kwao kiasi kwamba Mwanakombo akajiona amefika haswa kwa Romeo. Alikuwa na wivu sana juu ya Romeo hadi kumfanya Romeo aanze kuchukia na kujuta kwanini amekuwa na uhusiano nae.
"Uko wapi, hadi sasa hujarudi nyumbani?" Alikuwa akiulizwa maswali na Mwanakombo ambaye alikuwa na wivu sana. Na hata pale walipokuwa pamoja na Lisa akapiga simu Mwanakombo alikuwa anachukia sana.
"Ukiwa na mimi naomba simu yako zima" alisema Mwanakombo kwa hasira na wivu wa wazi kabisa.
"Lakini unajua huyu ni mpenzi wangu kwanini unachukia nikiongea nae"
"Bwana sitaki maneno mimi pia nina moyo kwanini uongee na malaya wako mbele yangu"
"Mwanakombo tafadhari usitake kuniona nikichukia nakuwaje tena naomba umuheshimu Lisa sana"
"Naanzaje Romeo siwezi, naumia na mimi pia nina roho jamani najua kupenda na maumivu nayasikia"
"Sawa ila kabla tangu mwanzo unajua Lisa ni mpenzi wangu hivyo lazima umuheshimu"
"Sawa bwana yaishe" ilibidi Mwanakombo awe mpole japo kuwa alikuwa anaumia sana na kuona wivu Romeo akiongea na Lisa. Basi waliendelea na mahusiano yao wakijiachia sana, Romeo alijua bado Lisa yupo bize na masomo hivyo Mwanakombo alikuwa akienda chumbani kwake wanalala pika pakua kama mume na mke.
Siku moja asubuhi wakiwa wamelala pamoja usiku kucha, na waliamka wakaingia bafuni kuoga walipotoka Mwanakombo alikuwa akiandaa kifungua kinywa na Romeo amekaa akiperuzi mitandaoni, ghafla mlango ukagongwa.
"Mh atakuwa nani huyo?" Aliuliza Romeo kwa wasiwasi.
"Sijui labda majirani nenda kafungue" alisema Mwanakombo. Na Romeo akainuka na kwenda kufungua mlango ambapo alipigwa na butwaa baada ya kumuona Lisa amesimama mlangoni.
Itaendelea.
Lipa sasa buku upate vipande 7. Ukilipa jero vipande vitatu. Ukilipa elfu2 vipande 14. 0719618409 lisa ntanga.

Post a Comment

0 Comments