Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Responsive Advertisement

PENZI LA MCHORA TATTOO-14



LATIFA NTANGA
0719618409
Ilikuwa siku ya jumamosi ambapo Lisa aliamka mapema akajiandaa na kutoka nyumbani kwao, alijua siku hiyo lazima Romeo atakuwa nyumbani kwa sababu alikuwa akifahamu ratiba za mpenzi wake huyo. Na ulipita mwezi mzima bila kuonana yote kwaajili yakuwa busy sana na masomo, Lisa alikuwa na hamu sana akutane na mpenzi wake zaidi wafurahie mapenzi yao ndio maana siku hiyo mapema asubuhi aliondoka bila hata kuwaaga wazazi wake. Safari yake iliishia nyumbani kwa Romeo akapaki gari lake nje na kwenda hadi mlangoni na kuanza kugonga mlango. Alifurahi sana baada ya kumuona mpenzi wake ameenda kufungua mlango.
"Waooo my husband, nimekumisi sana jamani!" Alisema Lisa kwa furaha na kumsogelea Romeo akamkumbatia kwa bashasha. Ila alishangaa kumuona Romeo hayupo sawa ni kama anahofu flani hivi.
"Baby what's wrong with you?" Aliuliza Lisa akitaka kujua Romeo anatatizo gani.
"Aaam..hakuna Lisa" alijibu kwa kubabaika Romeo.
"Mh au hujapenda mimi kuja kwako?" Aliuliza Lisa.
"Hapana" Alisema Romeo.
"Ok nipishe niingie ndani" Lisa alisema lakini Romeo alikuwa mgumu kumpisha Lisa aingie ndani kwake.
"Kuna nini kwani mbona sikuelewi?" Aliuliza Lisa huku kengere ya hatari ikianza kulia kichwani kwake. Mwanakombo ndani alishangaa Romeo anaongea na nani bila kurudi ndani, kwa sababu alikuwa tayari amemaliza kuandaa kifungua kinywa basi akainuka na kwenda hadi mlangoniLisa akamkumbatia Romeo kwa nyuma.
"Mume wangu chai tayari" alisema Mwanakombo kwa mahaba na sauti yake ikasikiwa na Lisa.
"Whaaaaaat! Romeo unamwanamke ndani na anakuita mume mbele yangu mimi?" Aliuliza Lisa akiwa haamini anachokiona.
"Noo Lisa..listen to me my wife" alisema Romeo na kujitoa kwa Mwanakombo akamsogelea Lisa.
"Romeo...umekosa nini kwangu? Kwanini unanifanyia hivi?" Lisa aliuliza na kuanza kulia.
"Heee Romeo sikia hata mimi ni mwanamke pia usinifanye mie kama roboti nina moyo ujue" Mwanakombo alisema.
"Please Mwanakombo naomba usiniharibie kwa mke wangu tangu mwanzo nilikwambia kuhusu Lisa"
"Nani akuharibie kwani nina kasoro gani mimi? Huyo mwanamke na mimi mwanamke pia tena nimemzidi kila kitu hadi dhambi" Mwanakombo alisema.
"Romeo nashukuru sana baba Mungu akubariki" alisema Lisa na kukimbia akatoka hadi nje na kuingia kwenye gari lake. Romeo alimtazama kwa hasira Mwanakombo akatoka nje na yeye na kumuwahi Lisa.
"Mkewangu nisikie ni shetani tu nakuomba nisamehe Lisa" Romeo alifika akafungua mlango wa gari na kuingia ndani akamkuta Lisa akilia sana kwa uchungu.
"Nimekosa nini Romeo kwanini hauridhiki na mimi kwanini?"
"Lisa nielewe mama yangu nisamehe na kuomba mke wangu nielewe mama nimekosa sana"
"Romeo nimechoka niache endelea na wanawake zako, yani kitanda ninacholalia mimi na wanawake wengine wanakilalia kweli Romeo?"
"Nisamehe mama tafadhari"
"Romeo siwezi nasema toka kwenye gari nenda kamfuate mwanamke wako"
"Lisa nisamehe nakupenda"
"Romeo shuka kwenye gari langu nitakuitia mwizi"
"Punguza hasira mke wangu nakuomba tushuke wote twende ndani tukaongee"
"Uende ndani na nani malaya wewe yani nikaingie kwenye chumba alichokuwa malaya mwenzako tena bora ungetafuta mwanamke mwenye akili zake unaokota makahaba huko yule msichana anaonyesha tu ni kahaba hata aibu usoni haoni Romeo wazazi wangu bado wananihitaji usije ukaniua kwa magonjwa!"
"Lisa nimekosa nisamehe mke wangu mzuri nakuomba nimepitiwa"
"Sikusamehi yani kuanzia leo sahau kuhusu mimi, toka kwenye gari tokaaa tokaaa nasema nitakuitia mwizi"
"Hapana usifanye hivyo nakuomba"
"Nasema tokaaa..mwiii.."
"Basi basi mke wangu natoka dah" Romeo alihuzunika sana.
"Toka nenda kwa malaya wako huko"
"Lisa kweli unanifanyia hivi?"
"Bwana toka huko" Alisema Lisa na Romeo akatoka kwa unyonge Lisa akawasha gari lake na kuliondoa kwa kasi sana.
Romeo alirudi ndani akiwa na hasira sana, akamkuta Mwanakombo amelala chali mtupu bila nguo na mwili wake wote ukiwa wazi.
"Karibu mpenzi wangu" Alisema Mwanakombo kwa sauti ya puani na kufanya hasira za Romeo zipungue.
Itaendelea.
Lipia buku upate vipande saba. 0719618409 jina Lisa Ntanga.

Post a Comment

0 Comments